Nataka kusimulia haya
yaliyonikuta kwani nimeona ni heri niyaseme ili nipate ahuheni kuliko kuendelea
kuyaweka moyoni na kuendelea kunitesa, Ni baada ya kumaliza elimu yangu ya
sdekondari nilijiuynga na chuo cha uhazili, Tabora kwa mafunzo ya ukatibu
muhtasi, Nilipata ajira kwenye shirika Fulani hapa nchini, baada ya masomo
yangu nilifanya kazi muda mfupi kabla yakupata mchumba na kuolewa, Mume huyu
alikuwa ni bosi kwenye kampuni Fulani, nilikuwa siwapendi watu wenye fedha au wenye uwezo mkubwa kwani wengi wao ni wanyanyasaji
ama kwa wake zao au kwa walalahoi, lakini ilikuwa ni tofauti sana kwa bwana
huyu hakuwa na tabia za dharau na manyanyaso kama walivyo wengi wenye kipato
kikubwa.
wakati wewe unacheka wako wengine wanalia, wakati wewe unalimbuka na Utajiri wako Masikini
Habari zilifika nyumbani kwetu
kuwa nimeolewa na kizito mmoja na kuwa tayari nina mtoto ambaye nilimpata kwa
njia ya upasuaji, mama yangu alishitushwa na habari hizo kiasi kwamba alikosa
usingizi. Ukweli ni kwamba tuliishi maisha magumu sana na familia yangu kwani
baba alifariki nikiwa darasa la kwanza, ilibidi marta nyingi nikatishwe masomo
yangu na mama yangu ili kumsaidia kulea wadogo zangu, wakati mama alipokuwa
akifanya vibarua mbalimbali, ila waalimu wangu walinipenda sana kwa sababu
nmilikuwa najitahidi darasani hivyo walinitia moyo na hata nilipofaulu kwenda
shule ya sekondari ya Songea gils kijiji kizima walinichangia,Mume niliye naye
tulifgahamiana nikiwa Tabota chuoni, tulikuwa marafiki – wachumba na hatimaye kuoana, alinisaidia sana kunipa
mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na pesa wakati nikiwa chuoni. Kosa kubwa
nililolifanya kwenye uhusiano wetu ambalo naomba wengine wasilifanye kama mimi ni kuwa nilumueleza kuwa sikuwa na
wazazi, ndugu waka jamaa, wote walikufa na mimi nililel;ewa na uongozi wa
kanisa tu, kwa vile huyu bwana alinipenda na alikuwa na nia ya kweli ya kunioa
alinishauri twende kwa mkuuu wa wilaya tukafunge ndoa kisheria.
Kumbe duniani hakuna siri wadaku
walipeleka taarifa kuhusu ndoa yangu na kujifungua kwangu mtoto ilibidi mama
akope nauli na alisafiri kutoka nyumbani mpaka Dar tulikuwa tunaishi Masaki na
mpambe alimleta mama mpaka getini.Nilisikia mbwa wanabweka walibweka sana na
kutoa ishara kwamba kuna mtu getini au mgeni, Nilimtuma msichana wangu wa kazi
aangalie kuna nani mlangoni jibu ni kuwa
kuna bibi mmoja mchafu,chafu aliyevaa nguo zilizoraruka raruka vipende vipande
na aliukuwa amechukua mzigo uliokuwa umefungwa na kaniki na alikuwa na kidonda
mguuni, nilishituka sana na kuhisi kuwa ni mama yangu kwani alikuwa na kidonda
ndugu, Yule msichana akaniuliza nimfungulie mlango, nilimzuia nikimwambia
asubiri kwanza . Wakati nikiwa najishauri kwenda kumuangalia huyo mgeni wa
ajabu mara mume wangu alipigfa honi na haraka msichana wangu wa kazi akaenda
kufungua geti, Tulishangaa baada ya kuingia na kusimamisha gari alimsalimia
Yule mgeni na kumshika mkono na mkno mwingine akashika ule mzigo uliofungwa kwa
kaniki akamleta hata sebuleni.
Kumbe bwana alikuwa ni mama yangu
mzazi kweli, Mume wangu alifungua kabati langu la nguo na kutoa vitenge, khanga
na gaunilangu akampa mama ingawa vilikuwa havimtoshi, alimuongoza mama bafuni,
Yuel mgeni baada ya kuoga mume wangu alimsafisha kidonda na kumfunga kasha
alikaa naye mezani na kula naye chakula. Wakati hayo yote yanafanyika mimi
nilikuwa nimejiinamia kwa fedheha huku nikijilaumu kwa nini nilificha upande
wangu wa pili na nilimlaumu mama kwa kuja kwake pale kwangu, Nilisubiri baada
ya kumaliza kula ndipo nikapata nguvu ya kumsalimia, lakini aliniitikia bila ya
uchangamfu.
Kesho yake mume wangu alimwambia
msichana wangu wa kazi amwandaye mama ili ampeleke hospitali ya kazini kwake.
Baada ya vipimo akamridisha nyumbani, kwa ujumla suala la mawasiliano lilkatika
kwani sikuulizwa lolote na mume wangu na alionyesha uungwana na kumpenda sana
mama yangu, Baada ya wiki moja mama alimshukuru mkwewe kwa yote mazuri
aliyomfanyia na alimuombea kila la kheri awe na Baraka katika maisha yake na
alimuomba amruhusu arudi nyumbani ingawa mume wangu alimuomba asubiri majibu ya
hospitali,ili kujua kwamba kidonda chake kinaweza kikawa kansa , lakini mama
alikataa na kung’ang’ania kurudi nyumbani. Baadaye aliruhusiwa na tulimkatia tiketi
kurudi nyumbani.
Baada ya mama kuondoka looh!
Mbona nilikoma, nilichambuliwa kama karanga, siku zote tulizokaa na Yule bwana
sikujua kama alikuwa na maneno ya nyodo kiasi kile,kwa kweli niliyataka
mwenyewe kwani sikuwa mkweli toka mwanzo na pia nilishindwa kukubali hali yangu
ya umasikini iliyonikuza hadi kukutana naye na akanipenda siwezi kumlaumu sana mumwe wangu ila
najilaumu mwenyewe kwani nlijitakia unafikiri ataniamini tena? Kama unafikiri
hivyo sizani kama akili zako ziko sawasawa lakini kuna kusameheana na
kuchukuliana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni