Jumapili, 31 Januari 2016

MKONO WANGU UKASOGEA HADI KWENYE MATITI!



Kila mtu anamikasa yake ambayo amewahi kukutana nayo na mingine inaweza kukufedhehesha, mimi nimeshawahi kufedheheka mara nyingi lakini zilikuwa fedheha ndogondogo, lakini hii ya mwaka juzi ilikuwa sio fedheha bali ni jifehdeha unajua ilikuwaje? Nilikuwa ndiyo nimehitimu kwenye chuo cha ustawi wa jamii huko Tengeru Arusha. Nilitoka Arusha na kurejea Dar ambapo ndipo wazazi wangu waliko, Nilipofika Dar nilibahatika kupata kibarua kwenye taasisi moja ya watoto.

Nilianza kazi pale kama mtu wa kujitolea ili kupata uzoefu kama wenyewe walivyoniambia, ningeweza kupata ajira pia baadaye kama ningeonyesha uwezo mkubwa na Ufahamu wa shughuli za kuishi na watoto yatima, Hapo kwenye kituo kulikuwa na na mama ambaye ndiye aliyekuwa naibu mkuu wa kituo, mama huyu alikuwa mcheshi na mwelewa sana, alikuwa na upendo wa kweli kabisa ambao mtu angeweza kuuhisi hata kutokea mbali sana.

 samahani kwa Picha hii kama itakusumbua Masomo haya yanawalenga jamii mbalimbali hasa vijana kwa kusudi la kuwajenga hivyo usifadhaishwe

Mimi kama kijana ambaye sikuzoea upendo mwingine ila ule wa ngono tu, nilianza kuutafasiri vibaya upendo ule wa ngono, nilijua kuwa Yule mama alikuwa ananitaka, nilijua anataka vijana, Nilijiambia kuwa hiyo ni kweli kwani hata wakati ninafanyiwa usaili alionekana kunitetea sana , nilijua nikimpata tu na ajira nimepata, Lakini pia alikuwa anatamanisha! Niliamua kumfanyia kampeni ili kumnasa nilianza harakati hizo kwa kumzoea na kumtania kidogo, kwa utani niliona bila shaka asingepata ujumbe maana alikuwa mtu wa utani na kila mtu , mtu mcheshi na mwenye kuelewana na kila mtu, Basi siku hiyo asubuhi kwenye saa tatu nikampatia nafasi, nilimkuta yuko kwenye chumba  kimoja akiwa peke yake, nilimsalimia na kumwambia kwamba nina ujumbe wake, aliniuliza kimzaha ni ujumbe gani asubihi ile , ule mzaha ulinifanya niamini kwamba ameshaelewa na amefurahia ninachotaka kusema, Nilituma  ombi langu ni kiwa na matumaini ya dhati kubwa sana. Alistuka lakini alijikaza na kusema huo siyo utani mzuri sana, wakati huu tayari ibilisi Alisha nipanda  hivyo nilimwambia sikutanii niko siriasi ninakupenda tangu siku ile ya kwanza, usione aibu usijisikie vibaya kwa sababu unanizidi kidogo umri najua wewe una ….’

Yule mama alinikatisha kwa kunipungia mkono, Nilishusha maruhani yangu, sikiliza najua kama binadamu unaweza kweli kunipenda  kwa njia hiyo, lakini huoni kuna hatari, mimi ni mke wa mtu tunatarajia kufanya kazi pamoja  na umri wako ni mdogo kwangu haipendezi sana 

Ulikuwa ni ukweli mtupu, lakini kufikiri vibaya ambapo huwa tuna kuita ibilisi, kulikuwa kumejenga kibanda akilini mwangu, sikuliona hilo, hivyo niliendelea kubwabwanya, Najua ni kweli lakini ninavyokupenda huwezi kuniambia kitu nikubali kwa kweli nihurumie nakuomba…’ Nilimfuata polepole pale alipokuwa amekaa na kupeleka mkono wangu shavuni mwake alinyamaza akiniangalia, nadhani kwakuwa hakuamini kuwa ninafanya upumbavu ule, mimi mawazoni mwangu niliona kwamba kumbe ni rahisi Nilijithibitishia kwamba alikuwa akinipenda sana, nilishusha mkono wangu na kuufikisha shingoni na ibilisi wa kujipachika aliupeleka mkono wangu hadi kwenye matiti, Yule mama alisimama na kutimua mbio hadi nje na dakika kumi baadaye nikiwa najaribu kujiuliza nimekosea wapi wakati kila kitu kilikuwa kinaenda vizuri niliona walinzi wawili wa kituo wakiingia mle ndani, waliniomba niende nao ofisini nilianza kubabaika kwa kuwauliza kulikoni, walisema hakuna jambo isipokuwa wameambiwa wanipeleke ofisini kwa mkuu wa kituo, nilijua labda yangekuwa ni maswala ya kazi.

Nilipoingia ofisini nilishangaa kukuta wafanya kazi wote wa kituo pamoja na Yule mama, bado nilikuwa najua yalikuwa ni maswala ya kikazi, au kuna dharula Fulani ofisini , ukiendekeza mwili kweli unakuwa bwege sana niliwasalimia wale wafanyakazi na wengi hawakuniitikia. Mkuu wa kituo hakuzungumza sana kwani baada ya kusalimia tu alisema ni jambo la kuhuzunisha sana kukutana asubuhi ile kujadilisuala ambalo halina maana sana Alisema kuna mwenzetu mmoja asubuhi hii ameonyesha utovu wa nidhamu ambao haujawahi kuonyeshwa na mtumishi yeyote hapa kituoni, mwenzetu huyu amemtongoza mama na kujaribu hata kumbaka, napengine sio kujaribu bali kwa sheria za inchi hivi sasa tunaweza kusema kuwa alimbaka, watumishi wote walisema ayahaa! Si unajua upambe tena Nilijua kabisa kuwa nilikuwa muhanga, nilijaribu kujipa moyo kwamba labda angekuwa ni mtumishi mwengine lakini kutajwa jina Yule mama kulinifanya niache kuendelea kujidanganya.

Mama amewahi kutoa taarifa hii na tulikuwa tunafikiri kulifikisha Polisi jambo hili lakini tumeona tutaharibu sifa ya kituo hivyo tunamwomba (alitaja jina langu) amwombe radhi mama … kwa kile kilichotokea asubuhi ya leo, nilikuwa natetemeka na mimacho ya watumishi wote ilikuwa kwangu, nilitamani kukanusha, kutukana, na kusema ondoeni upuuzi wenu lakini nilishindwa  nilijikuta nasema naomba radhi Mama… kwa yote niliyoyatenda Halafu nilinyamaza. Tunashukuru kwa hilo kuanzia hivi sasa hutakiwi kuonekana katika maeneo haya na ukionekana itakuwa ni kwa hasara yako mkuu wa kituo alisema.

Unataka kujua mambo yaliendaje baada ya pale? Nenda kawaulize pale kituoni na uwaambie wewe ndiye Yule mwakilishi mkuu wa wambeya wa jimbo lenu.

Maoni 3 :

Gerd Ulrich alisema ...

Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma,

Kwaheri Gerd Ulrich

Bila jina alisema ...
Chapisho hili limeondolewa na msimamizi wa blogu.
Bila jina alisema ...

Nilikuwa na uzoefu mgumu na wa kutisha katika mahusiano yangu ya awali na nilisubiri sana hadi nilipokutana na mume wangu na baada ya kukutana, tulipendana na kuoana. Baada ya miaka miwili ya muungano, alibadilika na kuanza tabia za ajabu na hatimaye kuniacha mimi na mtoto wetu. Nilifanya kila niwezalo kumrudisha lakini yote yalikuwa bure. Nilipata maoni mengi na kila mtu alikuwa akisema juu ya Dk Dawn. Niliwasiliana naye na alinijibu na kunipa juhudi zake zote na msaada ili kuifanya ndoa yangu ifanye kazi tena. Yeye ndiye aliyenijulisha kuwa mume wangu alichukuliwa kutoka kwangu na mwanamke mwingine na akafanya uchawi wa kuungana tena ambao uliturudisha pamoja na kurudi nyumbani kwangu na kijana wangu. Hakika, hakuna mtu huko alidanganya kuhusu Dk Dawn na matendo yake mema. Mume wangu alirudi nyumbani saa 73 baada ya kufanya kazi kama alivyoahidi. Wasiliana naye sasa na uwe na uhakika kwamba atakusaidia kuunganisha tena ndoa/uhusiano wako.
Atakusaidia kushinda kesi mahakamani au kulipiza kisasi dhidi ya adui zako.
Atakusaidia kuponya ugumba na kila aina ya magonjwa/magonjwa.
Ana suluhisho la shida yako.
Wasiliana na Whatsapp yake: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com