Jumapili, 31 Januari 2016

MKONO WANGU UKASOGEA HADI KWENYE MATITI!



Kila mtu anamikasa yake ambayo amewahi kukutana nayo na mingine inaweza kukufedhehesha, mimi nimeshawahi kufedheheka mara nyingi lakini zilikuwa fedheha ndogondogo, lakini hii ya mwaka juzi ilikuwa sio fedheha bali ni jifehdeha unajua ilikuwaje? Nilikuwa ndiyo nimehitimu kwenye chuo cha ustawi wa jamii huko Tengeru Arusha. Nilitoka Arusha na kurejea Dar ambapo ndipo wazazi wangu waliko, Nilipofika Dar nilibahatika kupata kibarua kwenye taasisi moja ya watoto.

Nilianza kazi pale kama mtu wa kujitolea ili kupata uzoefu kama wenyewe walivyoniambia, ningeweza kupata ajira pia baadaye kama ningeonyesha uwezo mkubwa na Ufahamu wa shughuli za kuishi na watoto yatima, Hapo kwenye kituo kulikuwa na na mama ambaye ndiye aliyekuwa naibu mkuu wa kituo, mama huyu alikuwa mcheshi na mwelewa sana, alikuwa na upendo wa kweli kabisa ambao mtu angeweza kuuhisi hata kutokea mbali sana.

 samahani kwa Picha hii kama itakusumbua Masomo haya yanawalenga jamii mbalimbali hasa vijana kwa kusudi la kuwajenga hivyo usifadhaishwe

Mimi kama kijana ambaye sikuzoea upendo mwingine ila ule wa ngono tu, nilianza kuutafasiri vibaya upendo ule wa ngono, nilijua kuwa Yule mama alikuwa ananitaka, nilijua anataka vijana, Nilijiambia kuwa hiyo ni kweli kwani hata wakati ninafanyiwa usaili alionekana kunitetea sana , nilijua nikimpata tu na ajira nimepata, Lakini pia alikuwa anatamanisha! Niliamua kumfanyia kampeni ili kumnasa nilianza harakati hizo kwa kumzoea na kumtania kidogo, kwa utani niliona bila shaka asingepata ujumbe maana alikuwa mtu wa utani na kila mtu , mtu mcheshi na mwenye kuelewana na kila mtu, Basi siku hiyo asubuhi kwenye saa tatu nikampatia nafasi, nilimkuta yuko kwenye chumba  kimoja akiwa peke yake, nilimsalimia na kumwambia kwamba nina ujumbe wake, aliniuliza kimzaha ni ujumbe gani asubihi ile , ule mzaha ulinifanya niamini kwamba ameshaelewa na amefurahia ninachotaka kusema, Nilituma  ombi langu ni kiwa na matumaini ya dhati kubwa sana. Alistuka lakini alijikaza na kusema huo siyo utani mzuri sana, wakati huu tayari ibilisi Alisha nipanda  hivyo nilimwambia sikutanii niko siriasi ninakupenda tangu siku ile ya kwanza, usione aibu usijisikie vibaya kwa sababu unanizidi kidogo umri najua wewe una ….’

Yule mama alinikatisha kwa kunipungia mkono, Nilishusha maruhani yangu, sikiliza najua kama binadamu unaweza kweli kunipenda  kwa njia hiyo, lakini huoni kuna hatari, mimi ni mke wa mtu tunatarajia kufanya kazi pamoja  na umri wako ni mdogo kwangu haipendezi sana 

Ulikuwa ni ukweli mtupu, lakini kufikiri vibaya ambapo huwa tuna kuita ibilisi, kulikuwa kumejenga kibanda akilini mwangu, sikuliona hilo, hivyo niliendelea kubwabwanya, Najua ni kweli lakini ninavyokupenda huwezi kuniambia kitu nikubali kwa kweli nihurumie nakuomba…’ Nilimfuata polepole pale alipokuwa amekaa na kupeleka mkono wangu shavuni mwake alinyamaza akiniangalia, nadhani kwakuwa hakuamini kuwa ninafanya upumbavu ule, mimi mawazoni mwangu niliona kwamba kumbe ni rahisi Nilijithibitishia kwamba alikuwa akinipenda sana, nilishusha mkono wangu na kuufikisha shingoni na ibilisi wa kujipachika aliupeleka mkono wangu hadi kwenye matiti, Yule mama alisimama na kutimua mbio hadi nje na dakika kumi baadaye nikiwa najaribu kujiuliza nimekosea wapi wakati kila kitu kilikuwa kinaenda vizuri niliona walinzi wawili wa kituo wakiingia mle ndani, waliniomba niende nao ofisini nilianza kubabaika kwa kuwauliza kulikoni, walisema hakuna jambo isipokuwa wameambiwa wanipeleke ofisini kwa mkuu wa kituo, nilijua labda yangekuwa ni maswala ya kazi.

Nilipoingia ofisini nilishangaa kukuta wafanya kazi wote wa kituo pamoja na Yule mama, bado nilikuwa najua yalikuwa ni maswala ya kikazi, au kuna dharula Fulani ofisini , ukiendekeza mwili kweli unakuwa bwege sana niliwasalimia wale wafanyakazi na wengi hawakuniitikia. Mkuu wa kituo hakuzungumza sana kwani baada ya kusalimia tu alisema ni jambo la kuhuzunisha sana kukutana asubuhi ile kujadilisuala ambalo halina maana sana Alisema kuna mwenzetu mmoja asubuhi hii ameonyesha utovu wa nidhamu ambao haujawahi kuonyeshwa na mtumishi yeyote hapa kituoni, mwenzetu huyu amemtongoza mama na kujaribu hata kumbaka, napengine sio kujaribu bali kwa sheria za inchi hivi sasa tunaweza kusema kuwa alimbaka, watumishi wote walisema ayahaa! Si unajua upambe tena Nilijua kabisa kuwa nilikuwa muhanga, nilijaribu kujipa moyo kwamba labda angekuwa ni mtumishi mwengine lakini kutajwa jina Yule mama kulinifanya niache kuendelea kujidanganya.

Mama amewahi kutoa taarifa hii na tulikuwa tunafikiri kulifikisha Polisi jambo hili lakini tumeona tutaharibu sifa ya kituo hivyo tunamwomba (alitaja jina langu) amwombe radhi mama … kwa kile kilichotokea asubuhi ya leo, nilikuwa natetemeka na mimacho ya watumishi wote ilikuwa kwangu, nilitamani kukanusha, kutukana, na kusema ondoeni upuuzi wenu lakini nilishindwa  nilijikuta nasema naomba radhi Mama… kwa yote niliyoyatenda Halafu nilinyamaza. Tunashukuru kwa hilo kuanzia hivi sasa hutakiwi kuonekana katika maeneo haya na ukionekana itakuwa ni kwa hasara yako mkuu wa kituo alisema.

Unataka kujua mambo yaliendaje baada ya pale? Nenda kawaulize pale kituoni na uwaambie wewe ndiye Yule mwakilishi mkuu wa wambeya wa jimbo lenu.

NIKAMSANIFU MTU MFUPI MWEUSI.



Mwaka 1997 nilipokuwa nimemaliza masomo yangu ya shahada ya kwanza pale chuo kikuu cha Dar es Salaam, nilikuwa nimefanyiwa mpango wa ajira na jamaa yangu mmoja kwenye kampuni moja jijini Dar na nikawa nimefanikiwa, Baada ya mipango ya hapa na pale  na kunifagilia sana kama wanavyosema watu wa mjini nilifanikiwa kupata barua ya ajira  kama afisa uhusiano kwenye kampuni moja ambayo haikuwa kubwa  sana wakati ule ingawa sasa hivi imeshakuwa, Nilipata barua iliyonitaka kuanza kazi wiki inayofuata kwa kweli nilifurahi sana , lakini kitu kibaya kwangu ni kuwa sikuwa na adabu na kile kiburi cha watoto wa kidato cha pili  siyo cha mtu aliyemaliza chuo kikuu  bado kilikuwa kinayawala kwangu.

Usimdharau Mtu awaye yote kwa sababu ya Mtazamo wa nje tu Mungu huangalia kwa namna tofauti


Siku ya kuripoti kazini iliwadia ambapo niliamka mapema sana na kujiandaa. Nilikuwa naishi mabibo External kwa wazazi wangu wakati huo, Niliondoka nyumbani saa 12 asubuhi nikiwa na uhakika kuwa nitafika mjini Posta  kabla ya saa mbili asubuhi muda wa kuripoti ofisini, Nilipanda basi hadi  ambapo nilipanda basi linguine , tulisafiri hadi pale Shekilango ambapo gari Fulani ilipoteza muelekeo likataka kuivaa daladala niliyokuwemo, ilibidi mwenye gari lile linguine kusimama na daladala yetu pia ilisimama, Abiria wa daladala walishuka na wa lile gari linguine aina ya Prado nao walishuka , mimi nikawa wa kwanza, kuwaendea wale wenye gari nyingine ambao walikuwa watatu, mmoja wao mwembamba kiasi na mwenginemfupi mweusi sana aliyekuwa ndiye msemaji, Hakuwa anasema chochote zaidi ya kuomba radhi kwa unyenyekevu kuwa gari lao lilikuwa limepata tatizo la usukani. Mimi nilipandisha  sana huku nikitumia maneno ya kingereza kuwaambia kwamba hawajastaarabika , nilimwambia Yule aliyekuwa msemaji wao kwamba ndio maana  amekuwa mweusi na kafupi sana kwa sababu ya ujeuri, Yule jamaa alisema ni sawa ninavyonena, hata hivyo dereva wa daladala yetu alikuwa mstaarabu aliwaunga mkono jamaa wale  akisema anaelewa aina hozo za tatizo na akaomba abiria tupande garini  na kuondoka  niliwageukia wale jamaa na kuwaambia “You are just luck guys” nikimaanisha kwamba wana bahati sana

Ndani ya basi nikazidi kusema kama kinanda , baadhi ya abiria wenye tabia kama mimi wakaniunga mkno , abiria wengine hawakuniunga mkno, ingawa hawakusema  hivyo, bali ile tazama yao  niliijua tu sikujali. Nilifika Posta mapema na kwenda moja kwa moja kwenye ofisi ambayo nilitakiwa kuanza kazi, iliandikwa kwenye barua kwamba nimuone mkurugenzi mkuu kabla sijaenda kwa menenja  kupangiwa majukumu yangu ya awali. Ilipotimu saa mbili niliomba kuingia kwa mkurugenzi ambapo niliruhusiwa, niliingia nikijua kuwa nitapokea zinga la sifa kwa kuchaguliwa kwangu kujiunga na kampuni ile , haikuwa hivyo ndugu yangu, pale mbele ya kiti alikuweko bwana mmoja unaweza kuhisi ni nani ? alikuwa ni mtu mfupi mweusi sana. Sikuwa na akili ya samli kwani nilimtambua mara moja kuwa , Naye hakuwa boga kwani aliponitazama tu alitabasamu Halafu alisema karibu afisa uhusiano kasha alinyoosha mkono wake  kutaka tusalimiane, nilikuwa natetemeka naye alijua dhahiri, karibu kaa alisema bila shaka unajua shughuli za kampuni yetu, kila saa na kila siku utakuwa unapambana na wateja wakorofi unadhani utaweza kuwavumilia? Aliuliza nilijua alikuwa ananisanifu tu nilisema ndiyo nitaweza 

Halafu aliniuliza je ukiwa kazini akatokea mtu mwenye gari alafu akjataka kukugonga kwa bahatri mbaya.. no tuseme ukiwa kwenye daladala likatokea gari linguine likataka kuigonga ile daladala utafanyaje? Nilinyamaza kwa muda kisha Nitamwacha dereva azungumze na mwenzake wajue watakavyomalizana wenyewe’ kwa nini hiyo ilikushinda leo asubuhi? Badala ya kuwa abiria ukawa dereva?

Nilitamani kuona jambo Fulani linatokea ili mahojiano yale yaishe ni kweli jambo lile lilitokea  Yule mkurugenzi ambaye ni Yule bwana niliyemkashifu pale shekilango aliniomba ile barua ya ajira, aliichukua na kuichanachana, halafgu aliniambia  potea nisikuone hapa ofisini hata mara moja, nilitaka kufanya jambo Fulani kama kupambana naye ili nimfunze adabu  jamaa naona alijua aliinua simu kuita mlinzi nilitoka kwa haraka  nikiwa nimeshukwa uso,”kweli aushikaye upanga ataangamia kwa upanga” leo hii ndio nasema habari hizi kwani hata ndugu zangu sikuwaambia sababu za kukosa kibarua kile

BIBI MWENYE KIDONDA NDUGU AKAJA KWANGU!



Nataka kusimulia haya yaliyonikuta kwani nimeona ni heri niyaseme ili nipate ahuheni kuliko kuendelea kuyaweka moyoni na kuendelea kunitesa, Ni baada ya kumaliza elimu yangu ya sdekondari nilijiuynga na chuo cha uhazili, Tabora kwa mafunzo ya ukatibu muhtasi, Nilipata ajira kwenye shirika Fulani hapa nchini, baada ya masomo yangu nilifanya kazi muda mfupi kabla yakupata mchumba na kuolewa, Mume huyu alikuwa ni bosi kwenye kampuni Fulani, nilikuwa siwapendi watu wenye fedha  au wenye uwezo mkubwa kwani wengi wao ni wanyanyasaji ama kwa wake zao au kwa walalahoi, lakini ilikuwa ni tofauti sana kwa bwana huyu hakuwa na tabia za dharau na manyanyaso kama walivyo wengi wenye kipato kikubwa.

 wakati wewe unacheka wako wengine wanalia, wakati wewe unalimbuka na Utajiri wako Masikini

Habari zilifika nyumbani kwetu kuwa nimeolewa na kizito mmoja na kuwa tayari nina mtoto ambaye nilimpata kwa njia ya upasuaji, mama yangu alishitushwa na habari hizo kiasi kwamba alikosa usingizi. Ukweli ni kwamba tuliishi maisha magumu sana na familia yangu kwani baba alifariki nikiwa darasa la kwanza, ilibidi marta nyingi nikatishwe masomo yangu na mama yangu ili kumsaidia kulea wadogo zangu, wakati mama alipokuwa akifanya vibarua mbalimbali, ila waalimu wangu walinipenda sana kwa sababu nmilikuwa najitahidi darasani hivyo walinitia moyo na hata nilipofaulu kwenda shule ya sekondari ya Songea gils kijiji kizima walinichangia,Mume niliye naye tulifgahamiana nikiwa Tabota chuoni, tulikuwa marafiki – wachumba  na hatimaye kuoana, alinisaidia sana kunipa mahitaji muhimu  ikiwa ni pamoja na pesa  wakati nikiwa chuoni. Kosa kubwa nililolifanya kwenye uhusiano wetu ambalo naomba wengine wasilifanye  kama mimi ni kuwa nilumueleza kuwa sikuwa na wazazi, ndugu waka jamaa, wote walikufa na mimi nililel;ewa na uongozi wa kanisa tu, kwa vile huyu bwana alinipenda  na alikuwa na nia ya kweli ya kunioa alinishauri twende kwa mkuuu wa wilaya tukafunge ndoa kisheria.

Kumbe duniani hakuna siri wadaku walipeleka taarifa kuhusu ndoa yangu na kujifungua kwangu mtoto ilibidi mama akope nauli na alisafiri kutoka nyumbani mpaka Dar tulikuwa tunaishi Masaki na mpambe alimleta mama mpaka getini.Nilisikia mbwa wanabweka walibweka sana na kutoa ishara kwamba kuna mtu getini au mgeni, Nilimtuma msichana wangu wa kazi aangalie kuna nani mlangoni  jibu ni kuwa kuna bibi mmoja mchafu,chafu aliyevaa nguo zilizoraruka raruka vipende vipande na aliukuwa amechukua mzigo uliokuwa umefungwa na kaniki na alikuwa na kidonda mguuni, nilishituka sana na kuhisi kuwa ni mama yangu kwani alikuwa na kidonda ndugu, Yule msichana akaniuliza nimfungulie mlango, nilimzuia nikimwambia asubiri kwanza . Wakati nikiwa najishauri kwenda kumuangalia huyo mgeni wa ajabu mara mume wangu alipigfa honi na haraka msichana wangu wa kazi akaenda kufungua geti, Tulishangaa baada ya kuingia na kusimamisha gari alimsalimia Yule mgeni na kumshika mkono na mkno mwingine akashika ule mzigo uliofungwa kwa kaniki akamleta hata sebuleni.

Kumbe bwana alikuwa ni mama yangu mzazi kweli, Mume wangu alifungua kabati langu la nguo na kutoa vitenge, khanga na gaunilangu akampa mama ingawa vilikuwa havimtoshi, alimuongoza mama bafuni, Yuel mgeni baada ya kuoga mume wangu alimsafisha kidonda na kumfunga kasha alikaa naye mezani na kula naye chakula. Wakati hayo yote yanafanyika mimi nilikuwa nimejiinamia kwa fedheha huku nikijilaumu kwa nini nilificha upande wangu wa pili na nilimlaumu mama kwa kuja kwake pale kwangu, Nilisubiri baada ya kumaliza kula ndipo nikapata nguvu ya kumsalimia, lakini aliniitikia bila ya uchangamfu.

Kesho yake mume wangu alimwambia msichana wangu wa kazi amwandaye mama ili ampeleke hospitali ya kazini kwake. Baada ya vipimo akamridisha nyumbani, kwa ujumla suala la mawasiliano lilkatika kwani sikuulizwa lolote na mume wangu na alionyesha uungwana na kumpenda sana mama yangu, Baada ya wiki moja mama alimshukuru mkwewe kwa yote mazuri aliyomfanyia na alimuombea kila la kheri awe na Baraka katika maisha yake na alimuomba amruhusu arudi nyumbani ingawa mume wangu alimuomba asubiri majibu ya hospitali,ili kujua kwamba kidonda chake kinaweza kikawa kansa , lakini mama alikataa na kung’ang’ania kurudi nyumbani. Baadaye aliruhusiwa na tulimkatia tiketi kurudi nyumbani.

Baada ya mama kuondoka looh! Mbona nilikoma, nilichambuliwa kama karanga, siku zote tulizokaa na Yule bwana sikujua kama alikuwa na maneno ya nyodo kiasi kile,kwa kweli niliyataka mwenyewe kwani sikuwa mkweli toka mwanzo na pia nilishindwa kukubali hali yangu ya umasikini iliyonikuza hadi kukutana naye na akanipenda  siwezi kumlaumu sana mumwe wangu ila najilaumu mwenyewe kwani nlijitakia unafikiri ataniamini tena? Kama unafikiri hivyo sizani kama akili zako ziko sawasawa lakini kuna kusameheana na kuchukuliana.

MZEE NIKAMWAGA SERA!



Ilikuwa ni mwaka 1998 nikiwa kidato cha pili jijini Dare es salaam, Nakumbuka nilikuwa napedna  sana kucheza soka na vijana wenzangu mtaani, katika mtaa tuliokuwa tukiishi kulikuwa na kiwanja  hakijajengwa nyumba bado, kiwanja hiki ndicho tuilichokuwa tunakitumia kwa michezo , kwemye timu niliyokuwa niiichezea nilikuwa na rafiki ambaye hatukuwa tunasoma shule moja  lakini wakati wa kujisomea nilikuwa nikienda kwao tukisoma pamoja  na kusaidiana  kimasomo,kwani yeye alinizidi kidato kwa kuwa mama yake alikuwa mwalimu alipenda kutusisitiza kimasomo.

                                                       Nkrumah Hall Chuo kikuu cha Dar es Salaam


Rafiki yangu alikuwa na wadogo watatu, wawili wakiwa ni wasichana na mmoja ni mvulana, lakini huyo msichana huyo msichana alikuwa kidato cha tatu kama kaka yake kwa kweli dada wa rafiki yangu aluikuwa ameumbika ajabu, Katika kipindi chote  nilipokuwa nikifika pale kwa rafiki yangu kujisomea  nilikuwa nimevutiwa sana na huyu dada yake,nilijikuta namtamani hali ambayo tumezoea kuiita kupenda, wakati wa kujisome ukifika tulikuwa tukisoma pamoja  sebuleni lakini ikifika saa mbili yuel rafiki yangu alikuwa akitumwa kwenda kununua mayai kwani ni biashara amboyo mama yake alikuwa akiifanya basi hapo ndipo ilikuwa nafasi  ya kupata muda wa kuongea na yule dada wa rafiki yangu.

Ilikuwa ni ngumu kunielewa awali kwani hakutegemea wala kuamini kuwa ningeweza kumtamkia maneno kama yale, lakini siku zilivyozidi kwenda niliendelea kumsumbua, ni afadhali angenipa jibu la ndiyo au hapana, badala yake aliamua kujifanya nataka – sitaki. Mimi matumaini yangu yakaongezeka siku zikapita kwa kasi huku nikizidi kumsomea mtoto sera zangu za upendo wa dhati.
Siku moja kama kawaida yangu nilipofika pale nyumbani kwaajili ya kujisomea nilimkuta dada Yule wa rafiki yangu akiwa peke yake mezani, kidume nikaanza kujitutumua mzee nikwamwaga sera ! huku Yule dada akiwa bize akipekua kurasa za daftari baada ya kumaliza kusema hovyo kwangu aliniuliza umemaliza? Mimi nikamjibu ndio, mara nikasikia akimuita kaka yake atoke chumbani kwake kwani chumba kilikuwa karibu na sebule, mara akatoka Yule rafiki yangu sura amaikunja na kuniuliza kama kile ndicho kilichonileta pale kwao. Nilikuwa kama nimeloweshwa maji,

Bila kuuliza huku nikiwa natetemeka nilichukua kila kitu kilicho changu na bila ya kuaga mtu hadi leo sijakanyaga nyumba ile nasikia Yule dada yuko chuo kikuu kwani walikuja kuhama mtaa ule nilioishi kwa kweli anastahili kwenda chuo kikuu. Unagoja nini sasa we huoni kuwa ni fedheha hii?.misikio mipana kama tembo

NIKAPATA SIMU KUITWA KITUO CHA POLISI


Naamini ya kuwa kisa hiki kilichonifundisha mimi somo muhimu kitakufundisha na wewe hususani kijana mwenzangu, Naitwa Didas Kibonye mkazi wa Yombo mjini Dar es Salaam, ilikuwa mwaka 2000 wakati huo ndio nikiwa nimeanza kujitegemea , nikiwa ninaishi nyumbani kwa mama yangu pamoja na dada zangu wawili  ambao walikuwa wanafanya kazi pia. 

Tamaa ya Maisha na kutokujikubali huwaponza wengi


Nilikuwa wakati huo nahaha sana na wanawake yaani mpenda wana wake sana , wakati huo nilikutana na msichana mmoja matata sana , Nikisema matata nina maana zote tu, alikuwa ni msichana mzuri kwa sura , mtanashatisana aliyependa kulka vizuri na pia kupenda vitu vizuri, kwa ufupi alikuwa ni wasichana ambao huitwa sista du, Hta hivyo kwa upande wangu mimi nilikuwa ni brazameni kwa hiyo nikisema Brazameni na sista du nina maana ya watu wanaopenda kujionyesha  kwa nje kwamba wana hali nzuri sana na mafanikio  makubwa sana  katika mambo mbalimbali wakati hali halisio siyo kweli, ni watu ambao wako tayari kuazima gari wakaonekane nalo mahali, au waazime simu ya bei mbaya sana wakaonekane nayo mahali mradi tu waonekane kwamba wanaweza kumiliki  vitu hivyo vya thamani kwa kifupi ni watu wasiojiamini kabisa , kwa hiyo mimi na huyu sista tulikuwa wa kada hiyo.

Tulianza uhusiano wetu kwa fujo na mkwara mzito sana  kwa kuwa nilikuwa nakula na kuoga na kupiga mswaki nyumbani basi kamshahara kangu kalikuwa hakana kazi kwa hiyo mtoto alijua kabisa kwamba amefika kwa mwenye mali name sikutaka kujivunjia heshima au kujishusha  kwa hiyo nilijitahidi kutoa. Tuliendelea kwa miezi kama mine hivi kabla binti hajkaanza kudai apate mkufu wa dhahabu nzito kidogo kwani ule wake ulikuwa ni wa gramu tano tu, kama ningepata walau wa gramu 15 ingekuwa nafuu sana Nilimwambia atulie tu atapata mkufu, nilijua mkufu aliokuwa anautaka kwa wakati ule ungegharimu kiasi cha shilingi 150,000, kwa kuwa nilikuwa na uhakika kuwa nisingeweza kuupoata hadi baada ya miezi saba labda baada ya kudunduliza, niliona labda niombe mkopo pale ofisini, lakini kumbe kutokana na muda wangu kazini sikuwa naruhusiwa kukopa, siku moja wakati niko nyumbani, dada yangu mkubwa alisahahu mkufu wake sebuleni, ulikuwa mkiufu wa nguvu hasa kama gramu ishirini au zaidi, Niliona Mungu akikupa hakugusi, bali hukuonyesha kinamna, Niliuchukua mkufu ule na kutokomea nao gizani.Dada alilalamika sana  alipobaini kuwa ameibiwa mkufu. Mkono wa lawama na tuhuma ulimwelekea hausigeli na mtoto wa mjomba wangu tuliyekuwa tukiishi naye pale nyumbani, nilijua nimeokoka, kwakweli mkufu ule ulifanya msichana wa kazi kupoteza kibarua chake.

Siku zilipita huku Yule hawara yangu akiamini kwamba simba au Dume lake limemnunulia mkufu ule na ilipita miezi sita. Siku hiyo nikiwa ofisini nikapigiwa simu kwamba niende kituo cha polisiMsimbazi, nilipouliza kulikoni niliambiwa kuwa Dada yangu mkubwa ana tatizo niliomba ruhusa ofisini  na kwenda kwenye tukio.Kufika nilimkuta dada pale kaunta na Yule hawara yangu, huku hawara yangu akilia , Nilipoona hiyo hali kumbukumbu za mkufu ilinijia haraka , kabla sijauliza ,dada aliniuliza  ulimpa huyu mwanamke mkufu wowote? Nilikuwa natetemeka, Maafande kadhaa na raia waliokuweko kaunta walinikodolea macho, kwani vipi mbona sielewi nasikia mkufu, wengine wanalia kuna kitu gani? Nlijifanya mtoto wa mjini afande mmoja aliingil;ia kati jibu swali bwana tuna kazi nyingine za maana , Nilinywea na kusema ndio kwani vipi! 

Dada yangu aliulizia uliutoa wapi mkufu huo? Niliona sina njia kama ninataka kutokuyakuza mambo Si ule mkufu wako ushasahau sista vipi? Dada yangu alikuwa na busara na alikuwa ananijia Pengine kwa kumtazama tu Yule msichana alijua kuwa nilikuwa naendeshwa puta, Afande naomba nipewe mkufu wangu tukayamalize nyumbani, Bila shaka afande Yule alikuwa anamfahamu dada kwani alimtaja kwa jina  na kumwambia sawa hakikisheni mnayamaliza yasirudi hapa,Halafu alicheka . Tulitoka kituoni kufika pale nje tu nilipokea matusi ya kumwaga kutoka kwa Yule hawara yangu matusi ya nguoni, kwenye kaptura, kwenye gagulo yangu ya mama na baba na ukoo mzima kwa ujumla. Kumbe mkufu ule ulikuwa na alama maalumu ya dada ambayo mgeni nao asingeweza kuijua, alimfuma Yule msichana akiwa saluni ndipo walipochukuana Polisi baada ya msichana Yule kuleta nyodo alipokuwa akihojiwa, wiki ileile ilibidi nihame kutoka nyumbani kutokana na aibu, ingawa hakuna aliyekuwa akinizonga, yake macho yao tu  yalivyokuwa yakinitazama ilikuwa kama vile wanapiga kamera kila kiungo changu cha mwili huko ndani, Watanzania bwana najua umekodoa mimacho ukitaka kujua tulimalizana vipi na Yule hawara yangu hiyo hainihusu mimi tena utajijua mwenyewe!