Jumapili, 7 Februari 2016

MUHAMAD NA YESU KRISTO MKUBWA NANI?


Hapo juu tulikuwa na swali upi ni muongozo wa Mungu wa kweli Quran au Biblia? Swali lile lilikuwa tamu maana tuliona jinsi qurani inavyokiri yenyewe kuwa Biblia ni Muongozo wa kweli,swali hilo halina tofauti na hili tunalojiuliza sasa isipokuwa tu hili la sasa ni gumu zaidi lakini ni muhimu likajibiwa tena mapema kwani kizazi hiki ni kizazi chenye utafiti mkubwa na kinachotatizwa sana na ukweli uko wapi?Kati ya viongozi hawa wakubwa ambao wameanzisha dini na hatimaye wamefanikiwa sana na wana wafuasi wengi sana duniani je katika hawa mkubwa nani? nani anastahili heshima na kuaminiwa?tutaangalia mambo ya msingi ya maisha yao.

   Ufahamu kuhusu kuzaliwa kwa Muhamad na kuzaliwa kwa Yesu.
Katika somo nyeti kamahili ni vema tukaanza kuchambua maisha ya viongozi hawa polepole na taratibu kiasi cha kumsaidia kila mmoja aweze kuelewa yampasayo kuelewa Muhamad alizaliwa akiwa na Baba na mama kama mtu wakawaida,babae aliitwa Abdallah na mamae aliitwa Amina hivyo Muhamad alikuwa mtu wa kawaida,hatuambiwi kuwa alitabiriwa na manabii,alitangazwa na malaika au neno la Mungu hapana!Tena wazazi wake waliabudu sanamu nayeye mwenyewe wakati wa utoto wake aliabudu sanamu zilizokuwepo pale al-kaaba(soma maisha ya Muhamad uk 5kifungu cha mwisho).
     Yesu hakuzaliwa kwa njia ya kawaida kama watu wengine alizaliwa kwa uwezo wa Roho mtakatifu wa Mungu,alichukuliwa mimba na bikira Mariam tendo hili pekee linamfanya Yesu asiwe wa kawaida yeye ni Roho iliyotoka kwa Mungu hivi ndivyo Quran isemavyo (an – nisaa 4;171) Yesu ni muujiza kwa ulimwengu (al-anbiyaa 21;91)Yesu ni roho inayotokana na Mungu (tahryym 66;12) Malaika alimtangazia Mariam habari njema kutoka kwa mungu kuwa yeye angemzaa Yesu (al-imran 3:45),alizaliwa mtakatifu bila dhambi (Maryam 19;19)Kwa hivyo quran inatupa ushahidi kuwa Yesu hakuwa mwanadamu wa kawaida alipozaliwa alipelekwa hekaluni na wazazi wake walikuwa wacha Mungu.

  Ufahamu kuhusu heshima ya Muhamad na Heshima ya Yesu
Katika quran Tunasoma moja ya heshima aliyopewa Yesu masihi hata kabla hajazaliwa katika (al-Imran 3;45)Tunaona kuwa Yesu ana heshima huko Mbinguni na Duniani na kuwa Yu karibu na Mungu,pia anaitwa Neno (au Tamko)la Mungu(al-Imran3;45 na nisaa4;171)Manabii wote walipewa au kuamriwa kuusema neno la Mungu,Lakini yesu sio kuwa alisikia au kuamriwa bali yeye Mwenyewe alikuwa Neno la Mungu maana yake ndani yake kulikuwa na Mamlaka kamili ya neno la mungu lenye nguvu ya kuumba, kuhuisha, kusamehe kufariji na kutia Nguvu mpya (Yohana 1;1-3,14). Quran haituambii popote kuwa Muhamad alikuwa ni neno la Mungu, lakini alikuwa tu akipokea aya (wahy) kupitia malaika na kuzikariri kwa wasikilizaji wake, mama yake hajapata kujulishwa juu ya kuzaliwa kwake, Wala hakujazwaRoho mtakatifu kama ilivyokuwa kwa Mariam ambae quran inasema alitukuzwa kuliko wanawake woote soma (al-imran 3;42).
    Jina Mariam limetajwa mara 34 katika Quran ambapo jina la mama wa Muhamad halikutajwa hata mara moja, tunaambiwa muhamad alipomuombea mama yake aliyekuwa ameshakufa mungu alimkatalia ombi lake jambo lililomfanya alie kwa uchungu sana

Ufahamu kuhusu maisha ya dhambi kati ya Muhamad na Yesu masihi
Inasimuliwa katika hadithi kwamba siku moja wakati wa utoto wa Muhamad,Malaika wawili walifika wakamchukua kando na wakampasua kifua na kusafisha moyo wake kwa maji ya zamzam,Wanazuoni wa kiislamu kwa kuzingatia kifungu hiki katika Quran (surat alm-Nashrah 94;2-5). Baada ya kuondolewa Dhambi (mizigo mizitomizito) ndipo akaambiwa ajipendekeze kwa Mola wake (aya ya 8).
     Kwa upande wa Yesu masihi  alikuwa mtakatifu tangu kuzaliwa (Maryam 19;19)Maulaamaa na wanazuoni wa kiislamu wanakubali kuwa neno Mtakatifu sana linalotumika katika aya hiyo hapo juu maana yake ni kutokuwa na waa lolote au dosari au dhambi,Yesu alimpendeza Mngu na wanadamu (Luka 2;52),wanazuoni hao wa kiislamu ni pamoja na  al-Tabari,al-Baidan na al-Zamakhshari.Quran imeshuhudia kuwa manabii mbalimbali walitenda dhambi isipokuwa Yesu peke yake,Muhamad alikiri wazi mara tatu katika Quran kwamba alilazimika  kuomba msamaa kwa Mungu allah(al-Muumin 40;55.Muhamad 47;19,al-Fat’h 48;1-2.)
     Hivyo tunahitimisha kifungu hiki tukiwa na uhakika wazi kuwa Muhamad alikuwa wa kawaida kama wanadamu wengine wowote,aliishi maisha ya kawaida kama mwanadamu mwengine wowote,alikuwa mwenye dhambi na alitenda dhambi na ndio maana aliomba asamehewe,Bali Masihi alizaliwa kwa uwezo wa Roho mtakatifu,alikuwa ni Neno la Mungu .alizaliwa pasipo kufanya dhambi,aliishi maisha matakatifu bila kufanya dhambi jiridhishe kwa kusoma (Yohana 8;46,2Korithian 5;21,Ebrania 4;15,1Petro2;22,1Yoh 3;5)

 Ufahamu kuhusu Ishara na miujiza Aliyotenda Muhamad na aliyotenda Yesu Kristo.
     Bado tunaendelea na utafiti wetu kutaka kujua Muhamad na Yesu mkubwa nani, tukimpata huyo tutakuwa tunamsikiliza zaidi kama Tulivyopata kitabu ambacho ni muongozo wa kweli wa Mungu sasa Tunatafuta Nabii ambae tutamuamini na kumsiliza zaidi.
   Wasomi na waalimu wa Kiislamu wanadai kwamba miujiza pekee ambayo Mungu alimpa Muhamad imejidhihirisha kwenye aya zaQuran, Hii ina maana ishara na mijiza ya Muhamad ilikuwa ni maneno tu na sio vitendo!
  Kama hivyo ndivyo mimi sioni ajabu kwani manabii wengi walipewa vitabu na aya hata wanafunzi wa Yesu kama Yohana alipewa kitabu cha ufunuo namna wanavyopokea aya hizo ni vilevile
  Lakini Quran Inamshuhudia Kristo kwamba alikuwa na uwezo wa pekee wa kuponya wagonjwa,hakulaani,wala kuhukumu,alikuwa na huruma na upendo na rehema,Uweza wa kimungu ulidhihirika kwake kwaIshara na miujiza mingi ambayo aliifanya waziwazi, Quran inasema aliwezesha vipofu kuona bila dawa na aliponya kwa kutamka maneno yake yenye uweza na nguvu kuu Maryam 19;31,Mungu alimfanya mbarikiwa popote alipo yeye ni chemchem ya uzima na Baraka kwa watu woote wa vizazi vyoote (al-Imran 3;49 na al-Maida 5;110) aliwaponya wenye ukoma,Alifufua wafu,aliumba ndege na yule ndege akawa hai al Imran 3;49,alilisha watu kwa mikate al-Maida 5;112-115,Yesu alijua siri za Mungu huku Muhamad alikiri kuwa hajui siri za ndani za Mungu isipokuwa yale yale ambayo alidai kwamba amefunuliwa na Mungu al- Imran 6;50,Lakini Kristo yeye ni tofauti Muhamad mwenyewe ameshuhudia kuwa Kristo alijua siri al-Imran 3;49 Aidha quran inatuambia kwamba Kristo alileta sheria iliyojaa neema na hekima,aliwaruhusu watu wake kula vyakula vilivyokatazwa katika sheria ya Musa sawa na Mathayo 15;19 Qurani inathibitisha kuwa Kristo alikuwa na mamlaka ya pekee na kukiri kwamba hakuwa na sababu ya Kuwa chini ya sheria bali alikuwa juu ya sheria na mkamilishaji wa sheria ( Imran 3;50)Muhamad alishauriwa kuwa kama anaona shaka  juu ya hayoaliyoteremshiwa basi awaulize  wakristo na wayahudi yaani waliopewa kitabu  kabla yake soma Yunusi 10;94; Kristo hakuhitaji kutafuta waalimu kuhusu ufafanuzi wa sheria kwani yeye mwenyewe alikuwa ni neno la Mungu Hivyo anapaswa kufuatwa na Watu kumtii Al-Imran 3;50.
Kristo haelekezi wale wanao mfuata Mungu tu Bali anaamuru wamfuate na kuzishika amri zake, qurani inasisitiza na kuwapa majina ya pekee wafuasi wa kristo na kuwaita wasidizi wa Mungu.
 Wale wanaomfuata Yesu quran inasema wamewekewa Upole na Rehema katika mioyo yao Al-Hadyd (Chuma) 57; 27.quran pia imeahidi kuwa Yesu na wale wanaomfuata watawekwa juu ya wale wanaokufuru al-Imran 3;55
     Aidha quran inathibitisha kuwa wanaomfuata Yesu ni wa tofauti na wapekee kati ya wanadamu ni wapole hawaqjivuni wala hawajitakii makuu ona hayo katika Al-maida 5;82,Hii ni sawa kwani Kristo ni mnyenyekevu wa moyo hivyo wamfuatao pia ni wanyenyekevu.  
            
Ufahamu kuhusu Kifo cha Muhamadi na Kristo
 Ibn Hishim ametueleaza kwamba kifo cha Muhamadi kilitokana na homa kali,inasemekana kwamba muhamad alipokaribia kufa alisema kwamba sumu alivyolishwa na Myahudi ndiyo iliyovunja moyo wake,Hii ilitokana na kwamba mjakazi wa kiyahudi (Mtumwa wa kike ambaye Muhamad alitaka kumuoa baada ya kutekwa vitani alikataa) hivyo siku moja alitia sumu kwenye chakula cha Muhamad ambacho alikuwa amemwandalia Mgeni wake ambae alipokula alikufa palepale,Muhamad alipokionja alikitema upesi na baadae inasemekana ndio ilipelekea kifo chake.
     Hata hivyo Kifo cha Yesu Kristo kilitabiriwa wazi kabisa katika quran kwamba  ni kwaajili ya kutimiza mpango wa Mungu wa kuwa baraka  kwa wanadamu wote Surat Al-Imran 3;55 “Nitakufisha Kisha Nitakuinua Kwangu” Ingawa maneno hayo hayaonekani katika Biblia hata hivyo yanathibitisha  kwamba Kristo hakufa  kama wanadamu wa kawaida bali alikufa kwa kusudi na mpango kamili wa Mungu kwa ajili ya amani ya wanadamu (surat Maryam 19;33). Baada ya vifo vyao ni wazi kuwa Muhamad alizikwa Madina na kaburi lake liko pale hadi leo na waislamu wanaamini kuwa roho yake iko mahali pa wafu (yaani Barzakh) ikingoja siku ya hukumu na waislamu woote wanahimizwa kumuombea mtume wao ili kwamba Mungu amrehemu. Bali tunasoma kwamba Mungu alimpaisha Kristo kama alivyomuahidi na anakaa huko mbinguni soma surat al-Imran 3;35 na inathibitishwa ahadi hii katika an-Nisaa 4;158Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwake”. Kaburi la Yesu liko wazi kwa sababu hayuko kaburini Amefufuka kama alivyosema kabla hajakamatwa na wayahudi na kuuawa.

Ijumaa, 5 Februari 2016

Vijana na Nguvu za Mungu !



Somo la kumi na nne

Vijana na Nguvu za Mungu

Hakuna jambo linalompendeza Mungu kama kijana kutembea na nguvu za Mungu,kila Upande ungependa kuwatumia vijana, Shetani hupenda sana vijana na Mungu hitaji sana vijana,n.k.Biblia inaonyesha jinsi ambavyo  wakati wa ujana  ndio wakati mzuri na unaofaa sana kwa kujitoa kumtumikia Mungu, Hii haimaanishi kuwa mungu hawapendi wazee au makundi mengine la hasha  ana wapenda lakini anataka uzee uwe matokeo ya kutembea na Mungu (Muhubiri 12;1-7) Kumkumbuka muumba wetu humaanisha kurudi katika kusudi la Mungu la kutuumba, shetani hakutuumba; Mungu ndiye aliyetuumba hivyo ni lazima tuishi kwa kutimiza kusudi lake,Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo;-

  • Kulitumikia shauri la Mungu.
  • Vijana na Nguvu za Mungu.
  • Vijana na kanisa la Mungu
Kulitumikia shauri la Mungu.
(Matendo 13; 36)Ni muhimu kwetu sisi vijana kuwa makini kuangalia Mungu anataka nini na kutimiza kile anachokitaka;Roho mtakatifu aliangalia kazi iliyofanywa na kizazi kilichofuata baada ya Adamu, lakini mambo waliyoyatimiza yalikuwa ni kuongeza idadi ya watu duniani tu kwa kuzaa, lakini wengi wao hawakufanya zaidi ya hayo wengi hawakutembea na Mungu (Mwanzo 5;6-21) ni Mtu mmoja tu Henoko yeye alifanya kitu cha ziada yeye alitembea na Mungu alienda na Mungu (Mwanzo 5;22-24)Mungu anataka watu ambao hawataishi duniani na kuzaa na kuongezeka tu, bali anataka  watu ambao  wanaliangalia shauri la Mungu na kulitumikia, Daudi siku zote alitaka kujua kua Mungu anataka nini na kufanya, Yeye aliitwa akiwa kijana lakini alitembea na Mungu kwa uhodari, ni lazima tumtumikie Mungu wetu tukiwa tungali vijana Yeremia,Yoshua,Yesu,nk. walitumika wakiwa vijana tu

Vijana na nguvu za Mungu
Ni muhimu kufahamu kuwa hatuwezi kulitumikia kusudi la Mungu Bila nguvu za Mungu, ili tuweze kufanikiwa kutembea katika utumishi kwa Mungu kila kijana ni lazima azingatie mambo muhimu yafuatayo ambayo yatachochea nguvu za Mungu maishani mwake kwa nini kwa sababu tunachangamoto nyingi zinazotuzunguka sisi vijana na Bila nguvu za Roho Mtakatifu ni vigumu kwetu kukabiliana nazo bila Roho. wake mambo ya muhimu ya kuyazingatia sisi vijana ni pamoja na;-
  1. Lazima tusome neno la Mungu.
Biblia inasema neno la Mungu na likae kwa wingi ndani yenu ni neno linaloweza kutusaidia katika wakati huu wa changamoto ngumu za kidunia (zaburi 119;9,Yoshua 1;7-8,!Falme 2;1-3).
  1. .Lazima Tupende kuomba kuabudu na kuishi maisha ya kumtumainia Mungu. Daniel, shedrak, Meshak na Abdnego waliweza kukabiliana na changamoto zilizowakabili kwa sababu walijaa Roho na walipenda kuomba Tumuombe Mungu atujaze kwa Roho wake kila siku.
  2. Lazima tujifunze kumfanya Mungu kuwa wa kwanza katika kila jambo (Mathayo6;33)
  3. Usijidharau wala kujiona kuwa u mtoto Mungu yu aweza kukutumia (Yeremia 1;4-7 1Timotheo 4;12-16)
  4. Jizoeze kufunga na kuomba na kufanya maombi ya alifajiri au meditations Mungu awe nawe.


Mkumbuke Muumba wako siku za Ujana wako Muhubiri 12:1-8 

Vijana na Kanisa la Mungu.
   Kanisani ndilo eneo lako la kujikuzia na kuchochea vipawa,Mtumikie Mungu kwa uaminifu kwenye kanisa lenu na chini ya Mchungaji wako waheshimu na kujionyesha kuwa wewe huna moyo wa kutaka kumuasi Mungu isibitishie jamii kuwa Mungu anaokoa vijana na anatembea nao na anawatumia hii itaondoa ile dhana ya watumishi wengi wa mungu kufikiri kuwa vijana wengi ni watenda dhambi huku wakisahau kuwa dhambi haina cha mzee wala cha kijana,kuwa karibu na watumishi wa Mungu jifinze kutoka kwao iige imani yao washirikishe mambo yako Heshimu wazazi wako, muheshimu kila mtu, simama barabara wakati wa majaribu. Mungu na akubariki sana nakutakia ujana mwema na ujazwe nguvu za mungu na uwe kiongozi bora katika taifa letu Niombee na mimi kwa kazi hii ngumu ya kutoa muelekeo kwa jamii ili niwe msaada kwa watu wengi Mungu atulinde hata tuonane,

Vijana na athari ya Utandawazi !



Somo la kumi na tatu

Vijana na athari za Utandawazi

Utandawazi Globolaization ni mwingiliano mkubwa wa maendeleo ya kisayansi, kiteknolojia, kiuchumi, kihabari na hata kitamaduni ni mkaribiano wa mataifa makubwa yaliyoendelea na mataifa ya dunia ya tatu yanayoendelea ambapo zamani ule upande wa pili tulikua tunausikia kama mbinguni lakini kwa sasa kwa sababu tumeungwa katika utandawazi dunia imekuwa kama kijiji yaani yanayotokea upande wa pili sasa kwa sekunde tu yanakuwa  yameenea dunia nzima na lolote utakalo kulijua unalijua bila kipingamizi kupitia teknolojia kutokana na mwingiliano huu kuna athari za kitabia kimaadili na kitamaduni zinazojitokeza kwa sababu ya utandawazi.
Tutaliangalia somo hili fupi kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatyavyo;-

  • Athari za utandawazi kitamaduni.
  • Tofauti ya tamaduni za mashariki ,Afrika na Tamaduni za kimagharibi.
  • Mambo ya kuyazingatia.
Athari za utandawazi kitamaduni.
 Kwa kawaida watu amabao hawajawafahamu sana wazungu hupenda kuwaiga tabia zao lakini kumbuka kuwa si mambo yoote ya wazungu ni mazuri au yanafaa na hasa mataifa na tamaduni za kimagharibi,kihistoria woote tunajua kuwa ustaarabu na uungwana uko mashariki zaidi kuliko magharibi,aidha ni muhimu kufahamu kuwa kama kuna watu ambao wangeeathiriwa sana kitamaduni ni watu wa Afrika ya kusini maana wamekaa na wazungu kwa muda wa karne nyingi sana lakini kwa sababu ya tabia mbaya ya kibaguzi na unyanyasaji waliyonayo wazungu kwa watu weusi jamii ya watu wa Afrika ya kusini walitunza tamaduni zao na hata leo tunaziona bila kuathiriwa na wazungu

Tofauti ya tamaduni za mashariki Afrika na Tamaduni za kimagharibi.
  Kuna tofauti kubwa kati ya utamaduni wa Afrika na tamaduni za kimagharibi,Sisi tunathamini jamii wao wanathamini uthamani wa mtu binafsi,utambuzi wa kijamii utambuzi wa mtu binafsi,kuishi kwa umoja kuishi kibinafsi,Muingiliano wa familia kubwa familia peke yao,umuhimu kwenye matukio,umuhimu kwenye Ratiba,Maisha halisi maisha ya kanuni,kiroho,kisayansi,mazungumzo maandishi,Heshima kwa wakubwa heshima kutokana na elimu,kurithishana madaraka,kupigiana kura,Hizi ni baadhi tu ya tofauti za kiafrika na kimagharibi yapi ni maisha bora nay a kuiga na ya kibiblia ni haya tunayoishi wa afrika kwa msingi huu basi hatupaswi kufikiri tu kuwa kila kilichochema ni cha wazungu tu.

Mambo ya kuyazingatia.
  Tunaweza kuiga na kujifunza mambo ya msingi ya maendeleo kama ya kiteknolojia lakini tusiruhusu utandawazi kutuharibia tamaduni zetu wakati umefika wa sisi nasi kuwa na mambo ambayo wazungu watayaiga kutoka kwetu

Vijana na Ufahamu wa Uwezekano wa Kutokuolewa !



Somo la kumi na mbili
Vijana na ufahamu wa uwezekano wa kutokuolewa
  Kuna ongezeko kubwa la wanawake wasioolewa hasa hapa kwetu Afrika na makanisani,Tatizo hili la kukaa bila kuolewa linaweza kuwa kubwa na linaweza kuleta athari kwa kina dada kujihisi kuwa hawawezi wao wenyewe na kujifikiri kuwa labda hawavutii wanaweza kujichukia na kujiona kuwa wamekosa jambo la msingi na la muhimu katika maisha wengi tunajua wazi kuwa future ya mwanamke Barani Afrika ni kuolewa kwamaana ya kuwa maisha kwa mwanamke ni kuolewa Hivyo anap[olikosa jambo hilin humfanya ajione kuwa amepungukiwa sana ,Hili linaweza kumfanya ajione amekataliwa na jamii na kuwa labda yeye ana tofauti wengine hujiingiza katika ukahaba hivyo ni muhimu nkufikiri kwa upana kuhusu mabinti wasioolewa na kuwahudumia lazima tulione hili kuwa ni tatizo la kulishughulikia na tutalijadili hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo

  • Wajibu wa kanisa kwa maandalizi ya mabinti.
  • Biblia inasema nini kuhusu kutokuolewa
  • Faida za kutokuolewa
Wajibu wa kanisa kwa maandalizi ya mabinti.
  Kanisa lina wajibu mkubwa katika kuliandaa kanisa na mabinti pia ili wajitambue kuwa wako katika nafasi gani ya maisha na jamii si vema kuwapandikizia watu hasa mabinti mawazo ya kuwa wataolewa tu na kufikiri kuwa kuolewa ndio kilele cha ubara wa maisha lazima Tufikiri kwa upana kama kuolewa ni kilele cha ubora katika maisha Kwa nini Kristo hakuoa au baadhi ya Mitume ni wazi kuwa kam Yesu hakuoa basi maisha yana maana pana zaidi ya kuoa au kuolewa Ni lazima basi kweli hii izaamishwe ndani katika maisha ya vijana wa kike waanze kufikiri kwa upana zaidi kuolewa ni kuzuri lakini kama hakujatokea je Tufanyeje?Kanisa linawajibu wa kufundisha kwa ukamilifu Imani na pande zake kuu mbili ili zieleweke vema kwa waamini wetu ni mara nyingi tumefundisha juu ya Imani ya kutoka katika shida na matatizo lakini hatujawahi kufundisha kuwa hata kufia katika tatizo ni imani mwandishi wa kitabu cha waebrania alifundisha hilo (Webrania 11;32-37) ni lazima kanisa lielewe kuwa mungu wetu ni mwokozi na ni mwenyekutia nguvu (He is a Serviour and Sustainer) huwa anaokoa katika majaribu ,lakini huwa anatia nguvu katika majaribu. Kanisa linawajibika pia kuwaajiri wanawake wasioolewa ili wasikae bila shughuli, waamini watoe kazi kwa mabint waioolewa badala ya kuwatelekeza na kuwaona wamepungukiwa eti kwa sababu hawana waume.

Biblia inasema nini kuhusu kutokuolewa
 Watu wengi wanafikiri kutokuolewa au kutokuoa ni balaa, lakini ni muhimu kuangalia nbiblia inasema nini? Yesu mwenyewe hakuoa! Lakini alifundisha kuwa kutokuoa au kuoa ni karama, karama ya kutokuoa au kuolewa ni wito wa hali ya juu sana na umewekewa watu maalumu sana Yesu akasema hivi “Awezae kulipokea neno hili na alipokee…” hii inamaanisha kuwa Mungu ameita au amendaa baadhi ya watu ambao hawataolewa au kuoa kwa huduma maalumu, Paulo mtume alikuwa na neema hii maalumu (1Korith 7;7). Wengi wa wamisionary wa zamani sana hawakuoa wala kuolewa akiwemo Mary Slessor mwanamke wa scotiland aliyeanzisha kanisa Nigeria na wengieo.Mungu bado anahitaji waume kwa wake waliuo single kwa matumizi yake katika ufalme wa Mungu bwana atupe fahamu hii Amen

 si kila mtu ataoa aku kuolewa!
Faida za kutokuolewa
Kihalisi na kwa uzoefu wa miaka katika huduma kuna faida ya kuwa single, wasioolewa wanapaswa kuitumia nafasi hii ya kuwa wenyewe kwa kumtumikia Mungu kwa uhuru zaidi,hizi ni miongoni mwa faida zenyewe;-
1.        Kuwa huru Muda woote,hii ni jambo gumu sana kwa wanandoa huwezi kuwa huru muda woote Mtu aliyeoa au kuolewa atagundua kuna mabadiliko mengi na changamoto nyingi zitakazofanya  Muda usiwe mali yako pekee bali unawajibika kujifunga kwa wengine
2.        Kuwa huru kujiendeleza kielimu,Kusoma huku unafamilia ni swala gumu sana lakini kama uko single ni jambo jepesi sana kujiendeleza kwa elimu ya juu vyovyote utakavyo
3.        Kuwa huru kusafiri kokote utakako,Mtu huru anaweza kuunganisha mikutano ya injili au semina kwa siku nyingi bila kubugudhiwa hii ni ngumu kwa mwenye familia
4.        Kuwa huru kutoka katika udhia na mateso ya ndoa,Ndoa zina mateso yanayogusa hisia na maumivu ya ndani sana si wakati woote katika ndoa kuna furaha na maraha tu waulize wana ndoa  unapojifunga na kuwa na mume na watoto kuna udhia tofauti nah ii inatengeneza nafasi ya kujiudhi zaidi Prophet T.B Joshua alisema “When you add any thing to your family you should also add Prayer” unapoongeza chochote katika familia yako ongeza pia maombi kwa nini kwa sababu umeongeza milango ya mashambulizi ya shetani kukushambulia, hii ni Lugha ya kivita Biblia inasema mmoja atafukuza elfu,wawili watafukuza kumielfu, kwa nini isiwe elfu mbili? Hii inamaana muwapo wawili nguvu inakuwa kubwa kwasababu vita inakuwa kubwa unaweza kuona!
5.        Uhuru wa kufanya huduma ambayo si rahisi kufanya ukiwa na ndoa mwenye hekima na alisikie neno hili ambalo Roho analiambia kanisa.