Hapo juu
tulikuwa na swali upi ni muongozo wa Mungu wa kweli Quran au Biblia? Swali lile
lilikuwa tamu maana tuliona jinsi qurani inavyokiri yenyewe kuwa Biblia ni
Muongozo wa kweli,swali hilo halina tofauti na hili tunalojiuliza sasa
isipokuwa tu hili la sasa ni gumu zaidi lakini ni muhimu likajibiwa tena mapema
kwani kizazi hiki ni kizazi chenye utafiti mkubwa na kinachotatizwa sana na
ukweli uko wapi?Kati ya viongozi hawa wakubwa ambao wameanzisha dini na
hatimaye wamefanikiwa sana na wana wafuasi wengi sana duniani je katika hawa
mkubwa nani? nani anastahili heshima na kuaminiwa?tutaangalia mambo ya msingi
ya maisha yao.
Ufahamu kuhusu kuzaliwa kwa Muhamad na
kuzaliwa kwa Yesu.
Katika somo nyeti kamahili ni vema tukaanza kuchambua
maisha ya viongozi hawa polepole na taratibu kiasi cha kumsaidia kila mmoja
aweze kuelewa yampasayo kuelewa Muhamad alizaliwa akiwa na Baba na mama kama
mtu wakawaida,babae aliitwa Abdallah na mamae aliitwa Amina hivyo Muhamad
alikuwa mtu wa kawaida,hatuambiwi kuwa alitabiriwa na manabii,alitangazwa na
malaika au neno la Mungu hapana!Tena wazazi wake waliabudu sanamu nayeye
mwenyewe wakati wa utoto wake aliabudu sanamu zilizokuwepo pale al-kaaba(soma
maisha ya Muhamad uk 5kifungu cha mwisho).
Yesu
hakuzaliwa kwa njia ya kawaida kama watu wengine alizaliwa kwa uwezo wa Roho
mtakatifu wa Mungu,alichukuliwa mimba na bikira Mariam tendo hili pekee
linamfanya Yesu asiwe wa kawaida yeye ni Roho iliyotoka kwa Mungu hivi ndivyo
Quran isemavyo (an – nisaa 4;171)
Yesu ni muujiza kwa ulimwengu (al-anbiyaa
21;91)Yesu ni roho inayotokana na Mungu (tahryym 66;12) Malaika alimtangazia Mariam habari njema kutoka kwa
mungu kuwa yeye angemzaa Yesu (al-imran
3:45),alizaliwa mtakatifu bila dhambi (Maryam
19;19)Kwa hivyo quran inatupa ushahidi kuwa Yesu hakuwa mwanadamu wa
kawaida alipozaliwa alipelekwa hekaluni na wazazi wake walikuwa wacha Mungu.
Ufahamu kuhusu heshima ya Muhamad na Heshima
ya Yesu
Katika
quran Tunasoma moja ya heshima aliyopewa Yesu masihi hata kabla hajazaliwa
katika (al-Imran 3;45)Tunaona kuwa
Yesu ana heshima huko Mbinguni na Duniani na kuwa Yu karibu na Mungu,pia
anaitwa Neno (au Tamko)la Mungu(al-Imran3;45 na nisaa4;171)Manabii wote
walipewa au kuamriwa kuusema neno la Mungu,Lakini yesu sio kuwa alisikia au
kuamriwa bali yeye Mwenyewe alikuwa Neno la Mungu maana yake ndani yake
kulikuwa na Mamlaka kamili ya neno la mungu lenye nguvu ya kuumba, kuhuisha, kusamehe
kufariji na kutia Nguvu mpya (Yohana 1;1-3,14). Quran haituambii popote kuwa
Muhamad alikuwa ni neno la Mungu, lakini alikuwa tu akipokea aya (wahy) kupitia
malaika na kuzikariri kwa wasikilizaji wake, mama yake hajapata kujulishwa juu
ya kuzaliwa kwake, Wala hakujazwaRoho mtakatifu kama ilivyokuwa kwa Mariam
ambae quran inasema alitukuzwa kuliko wanawake woote soma (al-imran 3;42).
Jina Mariam
limetajwa mara 34 katika Quran ambapo jina la mama wa Muhamad halikutajwa hata
mara moja, tunaambiwa muhamad alipomuombea mama yake aliyekuwa ameshakufa mungu
alimkatalia ombi lake jambo lililomfanya alie kwa uchungu sana
Ufahamu kuhusu maisha ya dhambi kati ya
Muhamad na Yesu masihi
Inasimuliwa katika hadithi kwamba siku moja wakati wa
utoto wa Muhamad,Malaika wawili walifika wakamchukua kando na wakampasua kifua
na kusafisha moyo wake kwa maji ya zamzam,Wanazuoni wa kiislamu kwa kuzingatia
kifungu hiki katika Quran (surat
alm-Nashrah 94;2-5). Baada ya kuondolewa Dhambi (mizigo mizitomizito) ndipo
akaambiwa ajipendekeze kwa Mola wake (aya ya 8).
Kwa upande
wa Yesu masihi alikuwa mtakatifu tangu
kuzaliwa (Maryam 19;19)Maulaamaa na wanazuoni wa
kiislamu wanakubali kuwa neno Mtakatifu sana linalotumika katika aya hiyo hapo
juu maana yake ni kutokuwa na waa lolote au dosari au dhambi,Yesu alimpendeza
Mngu na wanadamu (Luka 2;52),wanazuoni
hao wa kiislamu ni pamoja na
al-Tabari,al-Baidan na al-Zamakhshari.Quran imeshuhudia kuwa manabii
mbalimbali walitenda dhambi isipokuwa Yesu peke yake,Muhamad alikiri wazi mara
tatu katika Quran kwamba alilazimika
kuomba msamaa kwa Mungu allah(al-Muumin
40;55.Muhamad 47;19,al-Fat’h 48;1-2.)
Hivyo
tunahitimisha kifungu hiki tukiwa na uhakika wazi kuwa Muhamad alikuwa wa
kawaida kama wanadamu wengine wowote,aliishi maisha ya kawaida kama mwanadamu
mwengine wowote,alikuwa mwenye dhambi na alitenda dhambi na ndio maana aliomba
asamehewe,Bali Masihi alizaliwa kwa uwezo wa Roho mtakatifu,alikuwa ni Neno la
Mungu .alizaliwa pasipo kufanya dhambi,aliishi maisha matakatifu bila kufanya
dhambi jiridhishe kwa kusoma (Yohana
8;46,2Korithian 5;21,Ebrania 4;15,1Petro2;22,1Yoh 3;5)
Ufahamu kuhusu Ishara na miujiza Aliyotenda
Muhamad na aliyotenda Yesu Kristo.
Bado
tunaendelea na utafiti wetu kutaka kujua Muhamad na Yesu mkubwa nani, tukimpata
huyo tutakuwa tunamsikiliza zaidi kama Tulivyopata kitabu ambacho ni muongozo
wa kweli wa Mungu sasa Tunatafuta Nabii ambae tutamuamini na kumsiliza zaidi.
Wasomi na
waalimu wa Kiislamu wanadai kwamba miujiza pekee ambayo Mungu alimpa Muhamad
imejidhihirisha kwenye aya zaQuran, Hii ina maana ishara na mijiza ya Muhamad
ilikuwa ni maneno tu na sio vitendo!
Kama hivyo
ndivyo mimi sioni ajabu kwani manabii wengi walipewa vitabu na aya hata
wanafunzi wa Yesu kama Yohana alipewa kitabu cha ufunuo namna wanavyopokea aya
hizo ni vilevile
Lakini Quran
Inamshuhudia Kristo kwamba alikuwa na uwezo wa pekee wa kuponya
wagonjwa,hakulaani,wala kuhukumu,alikuwa na huruma na upendo na rehema,Uweza wa
kimungu ulidhihirika kwake kwaIshara na miujiza mingi ambayo aliifanya
waziwazi, Quran inasema aliwezesha vipofu kuona bila dawa na aliponya kwa
kutamka maneno yake yenye uweza na nguvu kuu Maryam 19;31,Mungu alimfanya mbarikiwa popote alipo yeye ni
chemchem ya uzima na Baraka kwa watu woote wa vizazi vyoote (al-Imran 3;49 na al-Maida 5;110) aliwaponya wenye ukoma,Alifufua
wafu,aliumba ndege na yule ndege akawa hai al Imran 3;49,alilisha watu kwa mikate al-Maida 5;112-115,Yesu alijua siri za Mungu huku Muhamad alikiri kuwa
hajui siri za ndani za Mungu isipokuwa yale yale ambayo alidai kwamba
amefunuliwa na Mungu al- Imran 6;50,Lakini
Kristo yeye ni tofauti Muhamad mwenyewe ameshuhudia kuwa Kristo alijua siri al-Imran 3;49 Aidha quran inatuambia
kwamba Kristo alileta sheria iliyojaa neema na hekima,aliwaruhusu watu wake
kula vyakula vilivyokatazwa katika sheria ya Musa sawa na Mathayo 15;19 Qurani inathibitisha kuwa Kristo alikuwa na mamlaka
ya pekee na kukiri kwamba hakuwa na sababu ya Kuwa chini ya sheria bali alikuwa
juu ya sheria na mkamilishaji wa sheria ( Imran
3;50)Muhamad alishauriwa kuwa kama anaona shaka juu ya hayoaliyoteremshiwa basi awaulize wakristo na wayahudi yaani waliopewa
kitabu kabla yake soma Yunusi 10;94; Kristo hakuhitaji
kutafuta waalimu kuhusu ufafanuzi wa sheria kwani yeye mwenyewe alikuwa ni neno
la Mungu Hivyo anapaswa kufuatwa na Watu kumtii Al-Imran 3;50.
Kristo haelekezi wale wanao mfuata Mungu tu Bali
anaamuru wamfuate na kuzishika amri zake, qurani inasisitiza na kuwapa majina
ya pekee wafuasi wa kristo na kuwaita wasidizi wa Mungu.
Wale wanaomfuata
Yesu quran inasema wamewekewa Upole na Rehema katika mioyo yao Al-Hadyd (Chuma) 57; 27.quran pia
imeahidi kuwa Yesu na wale wanaomfuata watawekwa juu ya wale wanaokufuru al-Imran 3;55
Aidha quran
inathibitisha kuwa wanaomfuata Yesu ni wa tofauti na wapekee kati ya wanadamu
ni wapole hawaqjivuni wala hawajitakii makuu ona hayo katika Al-maida 5;82,Hii ni sawa kwani Kristo
ni mnyenyekevu wa moyo hivyo wamfuatao pia ni wanyenyekevu.
Ufahamu
kuhusu Kifo cha Muhamadi na Kristo
Ibn Hishim
ametueleaza kwamba kifo cha Muhamadi kilitokana na homa kali,inasemekana kwamba
muhamad alipokaribia kufa alisema kwamba sumu alivyolishwa na Myahudi ndiyo
iliyovunja moyo wake,Hii ilitokana na kwamba mjakazi wa kiyahudi (Mtumwa wa
kike ambaye Muhamad alitaka kumuoa baada ya kutekwa vitani alikataa) hivyo siku
moja alitia sumu kwenye chakula cha Muhamad ambacho alikuwa amemwandalia Mgeni
wake ambae alipokula alikufa palepale,Muhamad alipokionja alikitema upesi na
baadae inasemekana ndio ilipelekea kifo chake.
Hata hivyo
Kifo cha Yesu Kristo kilitabiriwa wazi kabisa katika quran kwamba ni kwaajili ya kutimiza mpango wa Mungu wa
kuwa baraka kwa wanadamu wote Surat Al-Imran 3;55 “Nitakufisha Kisha
Nitakuinua Kwangu” Ingawa maneno hayo hayaonekani katika Biblia hata hivyo
yanathibitisha kwamba Kristo hakufa kama wanadamu wa kawaida bali alikufa kwa
kusudi na mpango kamili wa Mungu kwa ajili ya amani ya wanadamu (surat Maryam 19;33). Baada ya vifo vyao
ni wazi kuwa Muhamad alizikwa Madina na kaburi lake liko pale hadi leo na
waislamu wanaamini kuwa roho yake iko mahali pa wafu (yaani Barzakh) ikingoja siku ya hukumu na waislamu woote
wanahimizwa kumuombea mtume wao ili kwamba Mungu amrehemu. Bali tunasoma kwamba
Mungu alimpaisha Kristo kama alivyomuahidi na anakaa huko mbinguni soma surat al-Imran 3;35 na inathibitishwa ahadi hii katika an-Nisaa 4;158 “Mwenyezi Mungu
alimnyanyua kwake”. Kaburi la Yesu liko wazi kwa sababu hayuko kaburini Amefufuka
kama alivyosema kabla hajakamatwa na wayahudi na kuuawa.
Maoni 1 :
Nisawa kwa mtazamo wako pia mtume huja baada ya mtume.hivyo mtume yeyote alie tumwa na Mungu ali stahiki kufuatwa kwa kipindi chote ambacho hajafa na kuletwa mtume mwingine. Anae stahiki kufuatwa mafundisho yake hadi sasa ni Muhammad.kwa maana yeye ndiye mtume wa mwisho.
Chapisha Maoni