Somo la kumi na tatu
Vijana na athari za Utandawazi
Utandawazi Globolaization ni mwingiliano
mkubwa wa maendeleo ya kisayansi, kiteknolojia, kiuchumi, kihabari na hata
kitamaduni ni mkaribiano wa mataifa makubwa yaliyoendelea na mataifa ya dunia
ya tatu yanayoendelea ambapo zamani ule upande wa pili tulikua tunausikia kama
mbinguni lakini kwa sasa kwa sababu tumeungwa katika utandawazi dunia imekuwa
kama kijiji yaani yanayotokea upande wa pili sasa kwa sekunde tu yanakuwa yameenea dunia nzima na lolote utakalo
kulijua unalijua bila kipingamizi kupitia teknolojia kutokana na mwingiliano
huu kuna athari za kitabia kimaadili na kitamaduni zinazojitokeza kwa sababu ya
utandawazi.
Tutaliangalia somo hili fupi
kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatyavyo;-
- Athari za utandawazi kitamaduni.
- Tofauti ya tamaduni za mashariki ,Afrika na Tamaduni za kimagharibi.
- Mambo ya kuyazingatia.
Athari za utandawazi
kitamaduni.
Kwa kawaida watu amabao hawajawafahamu sana
wazungu hupenda kuwaiga tabia zao lakini kumbuka kuwa si mambo yoote ya wazungu
ni mazuri au yanafaa na hasa mataifa na tamaduni za kimagharibi,kihistoria
woote tunajua kuwa ustaarabu na uungwana uko mashariki zaidi kuliko
magharibi,aidha ni muhimu kufahamu kuwa kama kuna watu ambao wangeeathiriwa
sana kitamaduni ni watu wa Afrika ya kusini maana wamekaa na wazungu kwa muda
wa karne nyingi sana lakini kwa sababu ya tabia mbaya ya kibaguzi na
unyanyasaji waliyonayo wazungu kwa watu weusi jamii ya watu wa Afrika ya kusini
walitunza tamaduni zao na hata leo tunaziona bila kuathiriwa na wazungu
Tofauti
ya tamaduni za mashariki Afrika na Tamaduni za kimagharibi.
Kuna
tofauti kubwa kati ya utamaduni wa Afrika na tamaduni za kimagharibi,Sisi
tunathamini jamii wao wanathamini uthamani wa mtu binafsi,utambuzi wa kijamii
utambuzi wa mtu binafsi,kuishi kwa umoja kuishi kibinafsi,Muingiliano wa
familia kubwa familia peke yao,umuhimu kwenye matukio,umuhimu kwenye Ratiba,Maisha
halisi maisha ya kanuni,kiroho,kisayansi,mazungumzo maandishi,Heshima kwa
wakubwa heshima kutokana na elimu,kurithishana madaraka,kupigiana kura,Hizi ni
baadhi tu ya tofauti za kiafrika na kimagharibi yapi ni maisha bora nay a kuiga
na ya kibiblia ni haya tunayoishi wa afrika kwa msingi huu basi hatupaswi
kufikiri tu kuwa kila kilichochema ni cha wazungu tu.
Mambo
ya kuyazingatia.
Tunaweza
kuiga na kujifunza mambo ya msingi ya maendeleo kama ya kiteknolojia lakini
tusiruhusu utandawazi kutuharibia tamaduni zetu wakati umefika wa sisi nasi
kuwa na mambo ambayo wazungu watayaiga kutoka kwetu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni