Kwa nini utumie maelezo haya
SEXWISE inakusaidia kukupa:_ maelezo muhimu ambayo husaidia kujua na kufahamu juu ya hali ya maumbile yako_ ushauri wa kuboresha na kuendeleza ufahamuwako juu ya maumbile
yako.
‘SEXWISE’ Ni kitabu kilichoandaliwa kwa
muundo wa maelezo au muongozo kwa msafiri. Kitabu
hiki kinahusu usalama wa maumbile na maslahi
yako. Vile vile kinaelezea juu ya mbinu za
kujiandaa katika safari
ya maisha yako
ili kuwa na maamuzi ya busara juu ya
masuala ya kujamiiana. Hivyo, maelezo haya yatakusaidia
kufanya maamuzi muafaka juu ya
chaguo ulilo na
ufahamu nalo.
Kabla ya kuanza Umuhimu wa ujinsia katika maisha
yako hubadilika katika nyakati tofauti, na huenda
uwe unataka kujihusisha au kutojihusisha na
masuala ya kujamiiana. Sexwise ni kwa ajili
ya manufaa ya mtu binafsi. Unaweza usielewe
unaelekea wapi hadi utakapofika. Lakini udadisi au
utafiti unaweza kuwa sehemu ya uzoefu. Mapenzi, hisia
za maumbile, uwoga na wasiwasi vyote vina mchango
wake. Kila mtu hupevuka katika hatua tofauti na
mwingine ikiwa ni kimaumbile na kihisia, na si kila
mtu anapata hisia sawa na mwingine. Vishawishi toka
nje vinaweza kuwa na uwezo mkubwa wa kuchangia
katika ujinsia na hisia zako jambo ambalo baadaye
huweza kuathiri staha yako.
kabla ya kuanza 2
Orodha ya matukio
Mabadiliko ambayo hutokea wakati wa
kubalehe hufanyika hatua kwa hatua kwa kila kijana. Kwa kawaida kuanzia umri wa
miaka minane na huwa tofauti kati ya mtu na mtu. Kubalehe ni mabadiliko ya kuingia
hatua ya kuwa mwanamke au mwanamume mtu mzima, wakati viungo vya kike na kiume
vinaanza kukua na kudhihirika na mwili kuanza kujitayarisha na kuwa na uwezo wa
kuzaa. Wakati wa kubalehe mwili wako hupata mabadiliko ya haraka na hili laweza
kuwa jambo linaloweza kukupa wasiwasi na vile vile kufurahisha. Mabadiliko haya
yanaweza kukupa furaha lakini pia yanaweza kukuchanganya akili, kukutia fadhaa,
ama yote haya. Huu ndio wakati marafiki, jamaa zako na watu wengine wakiwemo wa
rika lako huweza kujaribu kukushawishi kuhusu mwenendo unaopaswa kufuata,
unavyopaswa kuonekana na ni watu aina gani unapaswa kuwa nao. Hayo yote ni muhimu
katika kufanya maamuzi ambayo utaweza kuhitaji majadiliano, kuitafuta taarifa
zaidi, na hata kujiuliza maswali magumu.
orodha ya matukio 3
Hedhi
Wasichana huzaliwa na vifuko
viwili vya kuhifadhia mayai (ovaries) ambavyo kila moja huwa na maelfu ya vijiyai
vichanga. Wakati wa balehe, vifuko hivyo hupokezana kwa yai moja likipevuka
kila mwezi. Kitendo hiki hujulikana kama kuchopoka kwa yai au “ovulation” kwa
lugha ya kiingereza na hutokea siku 14 kabla ya hedhi kuanza. Iwapo yai hili
halitakutana na mbegu ya kiume na kuungana, litakufa. Mji wa mimba kila mwezi
hujiandaa kutunza mimba kwa kujenga utandu mnene na laini kwa sehemu yake ya
ndani. Mwili unapopata habari kuwa yai hilo halikurutubishwa, utandu huo
hujiengua na kutoka pamoja na yai kupitia ukeni ikijulikana kama hedhi. Yai ni
dogo sana haliwezi kuonekana kwa macho. Mzunguko wa hedhi (menstrual cycle)
huanza pale msichana anapoona hedhi yake, hiyo huitwa siku ya kwanza ya
mzunguko wa hedhi ambao kwa kawaida huisha siku moja kabla ya kuona hedhi
nyingine.
Mzunguko wa hedhi hotofautiana
kati ya mtu na mtu na huchukua kati ya siku 21 hadi 35. Wakati wa hedhi
msichana anatakiwa kutumia vibandiko (sodo) ambavyo vitafyonza hedhi. Vibandiko
hivyo ni kama taulo za kike (maternity pads), au vitambaa safi. Ni vizuri
kutumia vijitabu kuweka kumbukumbu za siku zako, na hii itakusaidia kujua lini
utapata hedhi inayofuata. Mabadiliko ya viwango vya homoni kabla ama wakati wa
hedhi yanaweza kuathiri hisia zako. Unaweza kujisikia mwenye nguvu na kuwa na matamanio
ama ukajisikia una hasira, huna raha na hata pia kujisikia wataka kulia pasipo
sababu, hii hutokea wakati yai linatoka katika kokwa (ovulation) ama siku
chache kabla ya kuanza hedhi kwa baadhi matiti huuma na kuonekana makubwa zaidi
ya kawaida yake na unaweza kupata vipele usoni. Baadhi ya wanawake hukumbwa na
tatizo hili zaidi ya wengine na matokeo haya huenda yakabadilika katika
utaratibu wa maisha ya mwanamke. Wanawake huendelea kutoa mayai kwa utaratibu
huu hadi watakapotimia umri fulani katika maisha yao, na hukoma au kuacha
kupata hedhi (utu uzima) kwa kiingereza hujulikana kama “Menopause”. Hii kwa kawaida
hutokea wakati wanawake wanatimiza miaka ya mwisho ya arubaini na hamsini.
Baada ya kipindi hiki hedhi hukoma na wanawake hawawezi kutunga mimba. Ikiwa
una tatizo la kuumwa sana na tumbo wakati unapopata hedhi ama una maswali
mengine yanayokutatizo muone daktari unayemuamini kwa ushauri ama kituo cha
afya ya uzazi katika eneo lako.
mabadiliko yanayowapata
vijana wa kiume na wa kike wakati wa kubalehe
_ kimo chako, uzani na msuli hukua, viungo vya maumbile
ya jinsia yako hukua
_ unapata uwezo wa kuzaa sauti inabadilika
_ sehemu inayotayarisha virutubisho mwilini mwake katika
ngozi inatumika sana na huenda ikasababisha ukapatwa na vipele
_ vitundu vya kutoa jasho vinakua na kuongeza kiwango na
harufu ya jasho
_ nywele zinaota chini ya mikono (makwapani) na katika sehemu
za siri
_ unaweza kujikuta na mabadiliko ya hisia mbalimbali kwa
mfano hasira, furaha
_ huenda ukaanza kuvutiwa na watu wa jinsia isiyo yako
ama jinsia yako
_ utajihisi unaufahamu zaidi kuhusu masuala ya kujamiiana
Mabadiliko yanayowapata watoto
Wakike
_ matiti yanakuwa na huenda yakauma wakati yanakua
_ chuchu huanza kuchomoza
_ nyonga huanza kupanuka
_ maumbile ya jinsia yako huanza kukua, vifuko
vinavyohifadhi mayai ya uzazi (ovaries) huanza kutoa mayai
_ baadaye katika kubalehe, hedhi huanza
Mabadiliko yanayowapata watoto
wa Wavulana
_ kifua na mabega hupanuka
_ nywele (ndevu) huota katika sehemu fulani za uso na
pia huenda ukaota nywele kifuani
_ uume wako na kokwa (pumbu) huanza kuwa kubwa
_ kokwa hulegea na kubembea katika kifuko kinachozihifadhi
(Scrotum kwa kiingereza)
_ unaweza kusimamisha uume pasipo sababu
_ utapata kutoa maji yasio ya kawaida mara ya kwanza
kabisa kupitia kwenye Uume Utapata ndoto nyevu haya yanajulikana kama shahawa
(hii inaweza kukutokea
ukiwa usingizini)
Masuala
muhimu
Shirikisho la Kimataifa la Uzazi
wa Mpango (IPPF) lina vyama vingi vya Uzazi wa mpango katika nchi nyingi
ulimwenguni, na limejitolea kutoa habari kuhusu masuala ya ujinsia na Afya ya
Uzazi pamoja na huduma kwa watu wote wanaohitaji maelezo. Huduma sawa na hizi
hutolewa na baadhi ya mashirika mengine ya umma na ya kibinafsi. Chagua huduma
zile unazoweza kujimudu kugharamia na ambazo zitakufaa zaidi kwa mahitaji yako.
Kila mtu ana haki na uhuru wa kuchagua, uhakika na uwezo wa kupata maelezo
sahihi na usaidizi ufaao. Unachopaswa
kuwa nacho
Kujiandaa kutakuwezesha kuwa na
usalama zaidi, kuchagua na kwa hiyo kufurahia ikiwa unajihusisha na suala la
kujamiiana (ngono) itakuwa ya raha, lakini pia inataka itiliwe maanani vilivyo.
Ikiwa hauko tayari kushika mimba ama kuambukizwa magonjwa yatokanayo na
kujamiiana (zinaa), utahitaji kutumia kizuwizi cha mpango. Hapa kuna orodha ya
vizuwizi ambavyo vinaweza kutumiwa ili kuepuka kutunga mimba. Nyingi kati ya
njia hizi pia hutoa ulinzi dhidi ya magonjwa yaambukizwayo kwa njia ya
kujamiiana. Ikiwa una swali lolote kuhusu
vizuwizi hivi ama matatizo
wasiliana na kituo cha Afya ya Uzazi wa Mpango katika eneo lako ama mtoa huduma
wako.
masuala muhimu
• unachopaswa kuwa nacho
njia mbalimbali za uzazi wa mpango
Njia mbalimbali za uzazi
wampango
(i) Mpira wa kiume (male
condom)
(ii) Mpira wa kike (female
condom)
Ni mpira laini ambao huvaliwa
kwenye uume uliosimama au ukeni ili kuzuia mbegu ya kiume isikutane na yai la
kike. Mpira huu hutumiwa mara moja tu
jinsi unavyofanya kazi: unapovaliwa huzuia kukutana
kwa mbegu na yai na hivyo kkutotungwa kwa mimba
faida zake: ndio njia pekee inayozuia
magonjwa ya zinaa ikiwemo UKIMWI
- inahusisha mwanamume
katika kupanga uzazi
- zinapatikana kwa urahisi
Maudhi madogo madogo: Kuwashwa iwapo mpira au
dawa inayopakwa kwenye mpira haikukupenda
- uvaaji wa mpira wa kike
unahitaji uangalifu
njia za uzazi wa mpango kwa
wanawake
vidonge vya kumeza: ni dawa za kumeza zilizotengenezwa
kwa vichocheo (hormones)
vinavyofanya kazi: huzuia mayai ya mwanamke yasipevuke
- hutengeneza ute mzito
kwenye shingo ya mji wa mimba na kufanya mbegu za kiume zisipenye
- hufanya utandu
usijengeke kikamilifu na hivyo kutotungwa mimba
ubora wa njia hii: inarekebisha mzunguko wa
hedhi
- hupunguza wingi wa damu
ya hedhi
- hupunguza maumivu ya
tumbo wakati wa hedhi
- huzuia kansa (sarakani)
ya kokwa za mayai
maudhi madogo madogo: lazima vimezwe kila siku
- kichwa kuuma kidogo na
kinatibika
- ubora wake hutegemea
umezaji kila siku
- kichefuchefu au na kutapika
- haikingi dhidi ya
magonjwa ya yaenezwayo kwa njia ya kujamiiana Haya maudhi huweza kuja kutoka
miezi mitatu ya kwanza ambayo yataisha dawa ikikuzoea.
njia ya sindano: ni dawa iliyotengenezwa
kwa vichocheo (hormones) na hutolewa kila baada ya miezi mitatu
inavyofanya kazi: huzuia mayai yasipevuke
- hutengeneza ute mzito
kwenye shingo ya mji wa mimba
- hufanya mji wa mimba
(utando) usijiandae kutunga mimba
faida zake: ni njia ya muda mrefu
- ni njia yenye u-siri
(faragha)
- haina usumbufu hadi wakati
wa kuchoma sindano nyingine
maudhi madogo madogo: damu ya hedhi isiyo na mpangilio
(isiyotabirika) mfano: Kupata hedhi ya kidogo kidogo, kukosa hedhi, au siku
kupitiliza.
- kuongezeka uzito
- inaweza kuchelewesha
kurudisha uwezo wa kuzaa mteja anapoacha kutumia
- haikingi dhidi ya
magonjwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana.
vipandikizi: ni viplastiki sita vyenye
muundo wa vijiti vinavyowekwa chini ya ngozi ya mkono (kwa sehemu ya ndani)
viplastiki hivi vina dawa ya kichocheo cha aina moja ambacho hupenya taratibu
na kuingia mwilini kufanya kazi.
vinavyofanya kazi:
- huzuia mayai kupevuka
- hutengeneza ute mzito
kwenye shingo ya mji wa mimba
- hufanya utando wa mji wa
mimba usijengeke kikamilifu na hivyo kutotungwa mimba
faida zake:
- haina usumbufu hadi utakapotaka
kutoa
- ni njia ya muda mrefu
(miaka 5)
- inaweza kutolewa wakati
wowote na ikitolewa uwezo wa kushika mimba hurudi katika kipindi kifupi
- haikingi dhidi ya
magonjwa yatokanayo na kujamiiana.
maudhi madogo madogo:
- kupata hedhi ya matone
matone
- kukosa hedhi
- kuongezeka kwa damu ya
hedhi
- hedhi isiyotabirika
kitanzi: ni kiplastiki
kilichozungushiwa madini ya
shaba na huwekwa ndani ya
mji wa mimba.
inavyofanya kazi:
- shaba iliyopo hutoa dawa
inayopunguza kasi ya mbegu
za kiume
other methods • emergency
contraception
- dawa itolewayo
hudhoofisha na hatimaye kuua mbeguza kiume
- inafanya yai la kike
lisiungane na mbegu ya kiume
faida zake:
- haina dawa inayozunguka
kwenye damu
- haiingiliani na tendo la
kujamiina hivyo haina usumbufu
- ni njia ya muda mrefu
(miaka 10)
- ikitolewa, uwezo wa
kushika mimba hurudi katika
kipindi kifupi
Maudhi Madogo Madogo:
- haikingi na magonjwa
yatokanayo na kujamiiana ikiwemo UKIMWI
- maumivu kidogo sehemu ya
chini ya tumbo
- uwezekano wa kuongezeka
kwa siku na kiwango cha hedhi
- kupata damu ya matone
matone.
njia ya dharura ya uzazi wa
Mpango: hii
ni njia ya kumeza vidonge vyenye dawa ya vichocheo katika kipindi cha masaa 72
baada ya kitendo cha kujamiiana bila kizuizi. Kama ilivyo ni njia ya dharura kama
mtu amepata ajali kama vile kupasuka kwa kondomu wakati wa kujamiiana, kubakwa
au kusahau kumeza kidonge.
jinsi inavyofanya kazi:
- huzuia kutunga mimba kwa
kusitisha ama kuchelewesha kutolewa kwa yai
faida zake:
- ni njia pekee inayoweza
kutumika baada ya kujamiiana au hata baada ya njia nyingine kutofaulu kama
kupasuka kwa condom
- inaweza kutumiwa na
waliobakwa
maudhi madogo madogo:
- haina uhakika kamili
ukilinganisha na njia zingine za uzazi wa mpango kwani asilimia 75 tu ndio
hufaulu
- kusokotwa na tumbo
- kichefuchefu au kutapika
- kuumwa kichwa au
kizunguzungu
- haikingi dhidi ya
magonjwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana.
kuhesabu siku
salama/Kalenda: ni
njia ya uzazi wa mpango inayofanyika kwa kuhesabu siku za mzunguko wa hedhi na
kutambua siku salama na siku ambazo mwanamke anaweza kushika mimba.
inavyofanya kazi: wahusika huepuka
kujamiiana katika siku ambazo
mwanamke
anaweza kuwa amepevusha yai na hivyo yai
hilo kukosa mbegu.
faida zake:
- haina dawa hivyo hakuna
maudhi yahusuyo dawa inayozunguka mwilini
- inakubalika na dini zote
maudhi madogo madogo:
- inahitaji ushirikiano wa
hali ya juu ili kukubaliana kuacha kujamiiana kwa kipindi fulani
- ni vigumu kubashiri
suala la hedhi na wakati yai la uzazi liko tayari hasa kwa vijana
- haikingi dhidi ya
magonjwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana.
kushusha kando: ni njia ya kuzuia mimba ambapo
mwanaume hutoa uume kutoka kwenye uke na kumwaga mbegu nje.
inavyofanya kazi:
iwapo mbegu zitamwagwa nje
itazuia kukutana na yai hivyo mimba haitotungwa.
faida zake:
- haihusishi dawa yoyote
kuingia ndani ya mwili.
maudhi madogo madogo:
- usumbufu wa kukatisha
tendo la kujamiiana ili kumwaga mbegu nje
- si salama sana kwani
mbegu huenda zikawa ndani ya maji maji yanayotoka mwanzo. Kabla ya mtu kufikia mshindo
- haikingi dhidi ya
magonjwa yatokanayo na kujamiiana.
Kufunga uzazi kwa njia ya
upasuaji:
hii ni njia ya uzazi wa
mpango ambapo mirija ya uzazi ya mwanaume au ya mwanamke hufungwa ili kuzuia mbegu
au yai lisitoke na kuja kusabababisha mimba. Njia hii hutumika tu pale ambapo
mwanaume au mwanamke ameamua na ana uhakika kuwa hataki tena kuendelea kuzaa
watoto. Ni njia ya kudumu ikifanywa hakuna uwezekano wa kuzaa tena. Njia hii kwa
wanaume huitwa VASECTOMY na kwa wanawake ni MINILAPARATOMY au BILATERAL TUBAL
LIGATION
inavyofanya kazi: baada ya kufunga mirija,
yai la kike na mbegu ya
kiume
haviwezi kukutana na hivyo kutotungwa mimba.
faida zake: ni njia ya kudumu hivyo
haina usumbufu
maudhi madogo madogo:
- uwezekano wa kuzaa tena
ni sawa na hakuna kama njia imefanikiwa
- kwa kuwa ni upasuaji
kuna maumivu kidogo
- haikingi dhidi ya
magonjwa yatokanayo na kujamiiana
Sehemu nzuri za kutembelea Hakuna mmoja kati yetu anaweza
kuelezea ambavyo
tunaweza kufurahia uzoefu
tulioupata ama utatupeleka wapi. Hii pia ni dhahiri inapohusisha wenzi kitendo
cha kujamiiana na raha. Uzoefu huu utahusisha, kuutalii na kuuelewa mwili wako
na vile vile wa wengine. Hii itaongeza ujasiri wako juu ya mwili wako ulivyo,
hisia zako na unavyochukulia mambo. Ikiwa hujawahi kuangalia mwili wako, tafuta
sehemu ambayo ina faragha, hutasumbuliwa na kutumia kioo kuuangalia mwili wako
ikiwa ni pamoja na sehemu zako za siri. Kujichua ni njia nyingine ya kuutalii
mwili kwa wanaume na wanawake, ina maana kucheza na sehemu zako za siri,
kujichua ama kupiga punyeto. Unaweza kuwa na habari kwamba kujichua ama
kujipiga punyeto kutakuathiri, lakini hakuna dhihirisho la kisayansi katika dai
hili.
Hakuna madhara yanayoweza kutokea
kwa kufanya hivi.
sehemu nzuri za kutembelea
Marafiki wa kutembea nao
Uhusiano wa kujamiiana kati ya
wanaume na wanawake hujulikana kwa kiingereza “Heterosexual”. Uhusiano wa
kujamiiana kati ya watu kutoka jinsia moja hujulikana kama Usenge kwa
Kiingereza
“Homosexual”, Katika sehemu
nyingine watu hawa huitwa mashoga. Huwa ni wanaume wanaovutiwa na watu kutoka
jinsia yao. Usenge katika baadhi ya nchi umepigwa marufuku. Usenge ni chaguo
ambalo baadhi ya watu huamua, hali hii yaweza kutatanisha na unahitaji muda na
wasaa wa kuuelewa.
Nyingi kati ya masuala ya
kujamiiana ikiwa ni kati ya watu wa jinsia moja ama jinsia tofauti, kawaida uhusisha
kupapasa, furaha na huba. Hali ya uwana inaweza kuhusisha hisia sawa na
matendo. Uhusiano mzuri kati ya wapenzi unaweza kupata ushawishi wa moja kwa
moja katika uhusiano wa kujamiiana na hisia za kutamaniana baina ya wahusika.
Baadhi ya watu wanaamini hakuna tashwishi katika kuwa na uhusiano wa kujamiiana
kando ya urafiki wa mapenzi. Wengine huenda ikawa hawana mpenzi mmoja na bado
wanafurahia uhusiano wa kujamiiana. Kujamiiana na mapenzi sio sawa, hata hivyo,
kwa wengi mapenzi na kujamiiana vinaambatana. Ni muhimu kuelewa matokeo ya
uamuzi wa kujihusisha na kujamiiana na mtu mwingine. Inaweza kuwa vizuri sana,
lakini huenda ukaona dhamira inakusuta ama ukajutia baadae ikiwa utafikiri
hukufanya uamuzi mzuri na hukuwa tayari.
marafiki wa kutembea nao
marafiki wa kutembea nao
Watu huamua kujihusisha na masuala
ya kujamiiana kwa sababu tofauti. Wengine nikutokana na shinikizo kutoka kwa
wenzao amakutokana na marafiki zao kujihusisha na masuala ya kujamiiana kwa
sababu tofauti, wengine ni kutokana na shinikizo kutoka kwa wenzao ama kutokana
na marafiki zao kujihusisha na kujamiiana, ama kwa kuwa wanafikiri ni njia ya
kujitambulisha. Baadhi ya watu wengine huamua kungoja hadi watakapofunga ndoa ama
kumjua mtu vizuri. Kujamiiana ni uamuzi unaoweza kuuchukuwa ghafula na sio
wakati wote huwa uamuzi rahisi. Lakini usisahau kuwa unaweza kusema “Hapana”
kwa ombi la kujamiiana. Ikiwa utasema hapana au ndio fikiria kuhusu matokeo, pamoja
na raha. Baadhi ya watu wengine huamua kujiepusha na kabisa na kujamiiana.
kuchagua sehemu nzuri 18
Kuchagua sehemu nzuri Mawasiliano mazuri yanaweza
kukusaidia kuridhika ama kutosheka wakati wa
kujamiiana. Chanzo ni wewe mwenyewe na unapaswa ujipe ruhusa ya kutalii/kudadisi na kufurahia hisia zako za matamanio. Mwenzako hataweza kufahamu matakwa yako na hofu yako hadi utakapoweza na kutaka kumwambia, kwa mfano:
_ Unaweza kutamani kupapaswa na mpenzi wako kabla ya
kujamiiana
_ Huenda ukahitaji zaidi au usihitaji kujamiiana kila mara
kinyume na mwenzako
_ Unaweza kutaka ama kutotaka mtoto
_ Huenda usiwe na ufahamu zaidi kuhusu kujamiiana salama
kama anavyofahamu mwenzako
_ Huenda ukawa na ufahamu zaidi kuhusu kujamiiana salama
kumzidi mwenzako
_ Unaweza kuwa hutaki kujamiiana (uume kuingia ukeni)
_ Huenda usitake kujamiiana kabisa. Matamanio yanaweza kushughulikiwa
kupitia mawasiliano kati yako na mwenzako
kuhusu mahitaji
yako. Hii inaweza
kuwa vigumu kujamiiana kwa mara
ya kwanza ni kati ya
watu wawili waliokubaliana na
hakuna alielazimishwa
kufanya shughuli ambayo
haipendelei, katika
mtazamo wa masuala ya Afya
hakuna njia “sahihi”
ya kujamiiana. Kuna njia nyingi
za kuonyesha hisia
zako kwa mwenzako na mwili
wako utakuonyesha
unachotaka, wakati mwingine
busu peke yake
inatosha na sio lazima ujamiiane.
Unaweza kuridhika wakati wa
kujamiiana kwa njia mbalimbali, nyingi hazihusishi tendo hilo moja kwa moja.
Hii ni muhimu kutilia maanani katika enzi hii ambapo tunaendelea kupata ufahamu
zaidi wa kujamiiana salama {Mapenzi Salama}
Matamanio yako ya kujamiiana
huenda yakahusisha kujichua sehemu za siri, kujamiiana kwa ya kutumia mdomo
wako na ulimi kwa kiingereza “Oral Sex” kuwa na ashiki nyingi ama mtulivu na mtaratibu
kwa mwenzako wakati wa tendo hilo ama hata kufanya mapenzi bila kuingiliwa kimwili.
Yale unayoweza kufanya na mwenzako ni mengi na hayana mwisho, yategemea upeo wa
fikra zako lakini kumbuka kujilinda ama kujihifadhi wewe na mwenzako au
usifanye jambo usilolitaka.
kujamiiana •
mshindo/mshushio
Kucheza na sehemu zinazoleta
hisia za matamanio ya kukutana kimwili
Busu, kupapasa, kukumbatia vyote
hivyo ambavyo kwa kiingereza vinajulikana kama “Foreplay” huwatia ashiki/nyege
wanaume na vile vile wanawake. Haya yote hutuliza ama kuamsha hisia za
matamanio. Wanaume wengi wanaweza kupata matamanio haraka sana na kufanya uume
usimame. Kumvisha mwenzako kondom kunaweza kuorodheshwa katika mambo haya ya
kuamsha hisia. Kumpapasa, kumbusu au kumkumbatia mwanamke humsaidia mwanamke kupata
hamu ya kujamiiana (ashiki) kwa hiyo uke wake huanza kujitayarisha kuupokea
uume kwa urahisi bila ya kuumia. Wakati mwanamke anaposhikwa na hisia za
matamanio (nyege) uke wake hutoa maji fulani ya kiasili ambayo humsaidia mwanamume
kumuingia kirahisi (angalia ngono kavu).
Kuchukuwa muda wakati wa
kuchezeana huongeza hamu yakutaka kujamiiana pia husaidia kuimarisha imani ya
kimwili na kihisia kati ya watu, Imani hii inaweza kiukua na kubuni hali ambayo
wapenzi wahusika watahisi furaha na kujamiiana. Hii itasaidia sana katika
uhusiano wa kujamiiana na ule wa hisia. Kumfahamu mtu vizuri ni jambo la
kufurahisha.
Kujamiiana
Hii hufanyika na jamaa wanaovutiwa
na watu wa jinsia tofauti na yao. Tendo hili pia hujulikana kama ngono,
kukutana kimwili na kulalana ambapo uume huingia ukeni. Hii ndio njia mojawapo
ya kawaida kwa mtu kutunga mimba. Wakati mwingine inaweza kuwa tatizo, hasa
ikiwa ndio mara yako ya kwanza ama ukiwa na hofu. Mara tu uume unapokuwa ndani ya
uke ambao tayari unautelezi, mmoja ama wahusika wote wanaweza kuchezesha nyonga
zake ili uume uende mbele na nyuma kuambatana na mzungusho wa nyonga. Hii
inaweza kuchukuwa dakika kadhaa hadi saa nzima. Kawaida humalizika kwa kilele
cha raha ya kujamiiana na ndipo mtu hufikia mshindo kwa kiingereza inajulikana
“Orgasm”. Kuna njia nyingi za kujamiiana ya moja kwa moja na kwa kufanya uchunguzi
utaweza kutambua nini kitakufaa wewe na mwenzako. Kwa hiyo jiandae kwa safari
yenye mikondo mingi katika maeneo mapya kwa njia hii utapata kitakachokufaa
wewe na mwenzako.
Mshindo/mshushio
Wanaume na wanawake wote huwa na matamanio
na mahitaji ya kujamiiana. Lakini wanavyofikia kutosheka ama kuridhika na tendo
hilo ni tofauti.
Kujamiiana kunahusu ashiki na hii inaweza kujumuisha
mshindo ambao huleta raha kuu kwa wanaume na wanawake. Kufikia mshindo na mwenzako
hutegemea mazoea na maelewano. Wakati uume na kinembe vinapochangamshwa vya
kutosha mshindo hutokea ambao ambao unahusisha mfululizo
Mshindo/mshushio • maeneo
ya usumbufu
maeneo ya usumbufu 22
wa mpanuko wa misuli katika tupu
mbili hizo.
Mpanuko huo husikika kama kishindo
ama mpigo wa raha ambao huenea mwili mzima na kukupa raha isiyo kifani
ikifuatiwa na utulivu, wakati huu mwanamume hutokwa na shahawa uumeni mwake. Karibu
kila mwanamke anaweza kufikia mshindo kwa kuchezewa kinembe peke yake bila hata
ya kuingiliwa ndani. Ni wachache tu wanaweza kupata mshindo bila ya kinembe
kuguswa. Wanawake pia hufikia mshindo kwa kuguswa guswa ukeni. Mmoja wa
wahusika huenda akapata mshindo kabla ya mwenzake na hupatikana kila mara
unapojamiiana.
Hisia hutekeleza wajibu muhimu
katika maisha yetu ya kujamiiana kama vile miili yetu. Hii inahusisha fikra
zetu, hisia na matamanio ambayo husaidia katika raha za kujamiiana na
kuridhiana aukila mmoja kuridhika na tendo hilo.
Maeneo ya usumbufu
Sote tunaweza kuingia matatani
wakati fulani.
Wakati mwingine ni kutokana na
kuwa mambo hayaendi kama ilivyopangwa ama kwa kuwa hayakupaswa yafanyike
kabisa. Kuwa salama wakati mwingine hakufurahishi, lakini kuwa katika hali hiyo
salama ama kujihifadhi kunaweza kukusaidia usishike mimba ama kumtia mimba mtu
mwingine, kunaweza pia kukukinga na magonjwa na pia itasaidia kuwa na urafiki
ama uhisiano unaotaka. Ni vizuri kujihisi uko salama hasa ikiwa uko katika eneo
usilofahamu.
usalama wako
Kuna wakati mwingine unapotakiwa
ama kutarajiwa kujamiiana na mtu ambaye hutaki kujihusisha nae. Mtu huyu
anaweza kuwa na mahitaji mengi ama kuwa na fujo. Huenda humjui, huenda unamjua
sana na labda ni jamaa yako (una undugu naye). Mara nyingi watu hawa wana uwezo
zaidi na huenda wakajaribu kukuchokoza ama kukutisha kuwa watatoa siri zako ama
hata kukuhonga ili ujihusishe nao katika kujamiiana. Hii inajulikana kwa
kiingereza “Abuse” jambo lililo kinyume na sheria ambalo sio haki. Kile wanachokufanyia
huenda ni ukiukaji wa sheria na pia labda ni hatari.
Ikiwa uko katika tatizo lolote
tafuta ushauri kutoka kwa mtu unayemuamini na ambaye atakupa usaidizi, anaweza
kuwa mtu kutoka familia yako ama mtu wa nje. Kumbuka hakuna atakaye kulaumu.
Maslahi ya nafsi yako hayahusishi
matumizi ya nguvu wala malipo. Yanahusu imani na wewe mwenyewe kuridhia. Kusema
“Ndio” huenda kukawa na maana ndio lakini kusema “La” siku zote kuna maana
“La”.
Usalama wako
Shurutisho ni kitendo chochote iwe
ni cha masuala ya kujamiiana ama mengine ambapo watu hulazimika kufanya
wasioyapenda. Hii ni pamoja na kubakwa,
kutekwa,
kushambuliwa, kulazimishwa
kuwa ukahaba wa
aina yoyote ile, kushurutishwa kufanyiwa tohara {kukeketwa}, kuolewa bila ya hiari yako ama mwenzako
h a t a r i u n a p o s a f
i r i
Wakati ambapo vingi vya vitendo
hivi ni ukiukaji wa sheria bado hutekelezwa katika nchi kadhaa. Hii haivifanyi
vitendo vyenyewe kukubalika. Ni wanawake na vijana ambao hupatwa na vishawishi hivi
vya kujamiiana. Kuwa na uwezo wa kupata uhakika badala ya uzushi, elimu na
kujihusisha katika majadiliano, vinaweza kukusaidia kusimamia maslahi yako ya
kijinsia na afya ya uzazi.
Uamuzi unaofanywa na watu wengine
kuhusu maslahi yako ya kijinsia. Huenda ikawa kile wanachotaka wao sio
unachotaka wewe. Unapaswa uwe na uwezo wa kupata maelezo sahihi na maadilifu kama
inavyohitajika kabla ya kufanya chaguo lako. Chaguo lako halisi halihusishi
shurutisho ama kutishwa. Kuna itikadi nyingi kuhusu suala la kujamiiana,
ujauzito na kujifungua ambazo zimetekelezwa kwa miaka mingi lakini haziimarishi
ama kusaidia afya ama maslahi ya mtu binafsi, hasa wanawake. Kuwa sexwise ni
kuhusu kupata ufahamu na kujikimu. Pia inahusu kuwa salama. Hii haihusu kulazimishwa
kufanya jambo ambalo litakulete madhara wewe ama mtu mwengine, kimwili ama kiakili.
Ikiwa unashauku tafuta usaidizi ama ushauri kutoka kwa mtu unayemuamini ama
kituo chako cha Afya ya Uzazi.
Hatari
unaposafiri
Kusafiri kuna raha, lakini vile
vile kuna hatari yake.
Hakuna kitu kama
kujamiiana/mapenzi salama kabisa iwe ni ya moja kwa moja, sehemu ya nyuma au
ulimi.
h a t a r i u n a p o s a f
i r i
Njia mbili ambazo unaweza
kuzitumia dhidi ya mimba zisizotakikana ama magonjwa yatokanayo na kujamiiana,
ikiwa ni pamoja na UKIMWI ni kutojihusisha na kujamiiana kabisa ama kuzingatia njia
za kujikinga (angalia kutafuta sehemu nzuri ya kutembelea) unaweza kuwa na
mapenzi/kujamiiana salama kwa kutumia mpira wa kondomu. Magonjwa yaambukizwayo
kwa njia ya kujamiiana huambukiwa kutoka kwa mtu ambaye tayari ameambukizwa magonjwa
hayo kwa kuwa viini vya maradhi hayo huwa ndani ya shahawa, vile vile katika
maji maji yatokayo ukeni. Magonjwa haya hayawezi kuambukizwa kwa njia ya
kumbusu mtu, kutumia pamoja vyombo vya kulia ama kunywea ama vyoo vya umma.
Yeyote ambaye amejihusisha na kujamiiana bila kujikinga yuko katika hatari ya
kuambukizwa magonjwa haya na sio tu makahaba, watu walio na zaidi ya mpenzi
mmoja ama wasenge.
Hisia za aibu na hofu ni jambo la
kawaida miongoni mwa watu wanaoambukizwa magonjwa haya na hii inaweza kuwafanya
wasitafute usaidizi na ushauri juu ya matibabu. Lakini hakuna jambo la kuonea haya,
Magonjwa ya zinaa ni uambukizo yanahitaji kutibiwa mara tu unapoona dalili zake
kwa kuwa itasaidia kupunguza ama kukomesha magonjwa yenyewe na pia kukusaidia
usiyaeneze kwa wengine.
Magonjwa ya kawaida yaambukizwayo
na kujamiiana ni viotea, utando mweupe mdomoni, klamadia, kisonono, kaswende,
trichomonas {Pangusa} na UKIMWI.
h a t a r i u n a p o s a f
i r i 26
mwanamke anapaswa kutafuta
ushauri na msaada wa matibabu ikiwa anaziona dalili zifuatazo
_ maji maji katika uke wake yaliyo na rangi na harufu
isiyo ya kawaida au mengi zaidi ya kawaida
_ maumivu na hisia kama unaungua wakati wa kwenda haja
ndogo
_ maumivu na muwasho katika uke wako na maeneo kuzunguka
uke
_ uchungu au kupatwa na maumivu wakati wa kujamiiana
_ vidonda au malengelenge sehemu za siri
mwanamume anapaswa atafute
msaada wa matibabu ikiwa ataona dalili zifuatazo
_ majimaji kutoka kwenye uume yakiwa na rangi na harufu
isiyo ya kawaida na mengi kupita kiasi cha kawaida
_ hisia kama unaungua katika uume wako wakati ama baada
ya haja ndogo
_ vidonga viotea au malengelenge kwenye uume au maeneo
ya karibu wa uume
_ vipele katika maeneo ya siri ama sehemu nyingine za
mwili
nini hutokea ikiwa
hutatibiwa
_ unaweza kuugua sana na unaweza ukapoteza uwezo wa
kuzaa
_ kituo chako cha Afya ya Uzazi ama daktari wako atakupa
ushauri kuhusu kupimwa magonjwa haya
VIRUSI VYA UKIMWI NA UKIMWI
Wakati mwingine huwa hakuna dalili
za wazi kuonyesha kwamba umeambukizwa, kwa hiyo ni vyema kila wakati kujilinda
na pia kumlinda mwenzako ama wenzako kwa kutumia mpira wa kondomu. Ikiwa
unahofu ya kupata uambukizo wasiliana na kituo chako cha Afya ya Uzazi ama mtoa
huduma au daktari kwa ushauri. Ni busara kuwa na ngono salama.
VIRUSI
VYA UKIMWI NA UKIMWI
HIV ni kirusi ambacho huuwa ama
kumaliza nguvu zako za kukabiliana na magonjwa. UKIMWI (Ukosefu wa Kinga
Mwilini) hutokea wakati mwili umeambukizwa virusi vya HIV na mwili hauwezi kukabiliana
na magonjwa yote na hali nyingine. Virusi vya HIV haviwezi kupitia kizuwizi cha
mpira kama vile kondomu na haviwezi kudumu kwa muda mrefu nje ya mwili wa
mwanadamu. Virusi hivi haviwezi kupitishwa kupitia njia ya kawaida kama busu,
kujichua kusalimiana kwa mikono, vyoo vya kukalia, vyombo vya kulia na pia
wadudu hawawezi kupitisha ugonjwa huu kwa kukuuma.
Kuna njia mbili kuu ambapo virusi
vya HIV vinaambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine. Njia moja ni wakati
shahawa ama majimaji yanayotoka ukeni mwa mtu aliyembukizwa yanapoingia katika
mwili wa mtu mwengine wakati wa kujamiiana na nyingine ni kutoka katika damu ya
mtu mmoja hadi mwingine wakati ambapo damu ya mtu aliyeambukizwa inapoingia
katika mwili wa mtu mwingine. Kwa sababu hii wanaotumia madawa ya kulevya ambao
hutumia kwa pamoja sindano kupitisha madawa hayo katika mishipa yao huhatarisha
maisha yao na afya zao. Pia kuna watu wanaongezwa damu hospitalini ambapo vifaa
vya shughuli hiyo havijasafishwa ipasavyo ama damu wanaoongezwa ina virusi.
Wanawake walio na virusi hivyo wanaweza kuwaambukiza watoto wao wakati wakiwa
waja wazito, wakati wa kujifungua ama katika kuwanyonyesha.
Wakati virusi vinaingia katika
mwili wa mtu, husemekana mtu huyo ni “HIV Positive”. Mtu anaweza kuwa na virusi
hivyo HIV bila yeye mwenyewe kufahamu. Dalili zilizo wazi za mtu aliye na
virusi hivyo ama UKIMWI ni kupungua uzito kwa asilimia 10, homa kwa zaidi ya
mwezi mmoja, uchovu, kutokwa na jasho usiku. Watu wanaweza kuambukizwa na kuwa
na virusi vya HIV kwa miaka mingi kabla ya kukumbwa na UKIMWI. Moja ya njia za
kuepuka kuambukizwa HIV ni kufahamu tofauti kati ya jambo lililopo na lile la
kubuni. Moja ya hadithi nyingi kuhusu virusi vya HIV na Ukimwi ni kwamba
unaweza kupona maradhi haya kwa kujamiiana na Bikira. Hii si kweli nyingine ni
kuhusu UKIMWI ambapo yasemekana kuna matibabu ya kutibu maradhi haya. Ukweli ni
kwamba hakuna kinga wala dawa ya kumaliza maradhi haya. Walio na virusi vya HIV
hawapaswi kubaguliwa na haitokei tu ni watu fulani, hutokea wakati virusi
vinapopitishwa kutokana na kujamiiana kusiko salama na mtu aliye na virusi
hivyo na pia kuzingatia tabia nyingine za hatari. HIV ni kirusi ambacho
kinaweza kutudhuru sisi sote lakini kinaweza kuepukwa ikiwa una wasiswasi na
wataka maelezo zaidi (angalia anuwani).
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Unaweza kutunga mimba ikiwa
ndio mara yako ya kwanza kujihusisha na ngono?
Ndio, ikiwa wahusika wote
wanauwezo wa kuzaa na hawatumii njia yoyote ya uzazi wa mpango
Unaweza kutunga mimba,
kujihusisha na kujamiiana wakati una hedhi?
Ndio
Unaweza kupata mimba
unapojamiiana ukiwa umesimama?
Ndio
Ukioga mara tu baada ya
kujamiiana bado unaweza kupata mimba?
Ndio
Je kokwa zangu zaweza
kupasuka ikiwa sifikii mshindo?
Hapana
Je unaweza kuishiwa na
shahawa kwa kufikia mshindo zaidi?
Hapana, kila kokwa huwa na manii
yenye mbegu za uzazi kiasi cha milioni mia mbili kila siku
Je wanaume huugua ikiwa
hawashushi kila mara?
Hapana
Je ni kweli kwamba
matamanio ya kujamiiana huwa ya juu zaidi kwa mwanamume ikilinganishwa na
mwanamke?
Hapana, lakini wanaume mara kwa
mara
maswali yanayoulizwa mara
kwa mara
wanafahamu kwamba lazima
wajihusishe na masuala
ya kujamiiana, wawe na
wapenzi wengi na kuanzashughuli hiyo katika umri mdogo. Wasichanahufunzwa
wasijihusishe na masuala ya kujamiiana nawasijihusishe hadi pale watakapoolewa.
Mawazohaya yanaweza kuwa sehemu ya fikra zetu nakuonekana ni jambo la kawaida
la hisia kati yawanawake na wanaume.
Ni sawa kujamiiana kwa
kutumia sehemu yanyuma panapopitia haja kubwa
Baadhi ya watu (wake kwa
waume) hufurahia kuingiza uume katika tundu panapopitia haja kubwa, njia hii kama
ile ya moja kwa moja ya ukeni huongeza hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa
na matumizi ya mpira wa kondomu ndio njia ifaayo zaidi kujilinda ama kuepuka
maambukizo. Na katika nchi nyingi hili huhesabiwa kuwa kosa la jinai.
Je kuna uhusiano wowote
kati ya ngono panapotumiwa mdomo na ulimi katika kueneza virusi vya HIV ama
UKIMWI
Ni njia iliyo na hatari ya
kiwango cha chini cha uwambukizaji, virusi vya HIV huuwawa na asidi za tumboni.
Vinaweza kupitishwa katika mchanganyiko wa manii na damu (kutoka mtu aliye na
virusi hivyo kupitia sehemu zilizochanika za mdomo ama ikiwa manii yataingia
machoni ambako kuna mishipa mingi ya damu.
maswali yanayoulizwa mara
kwa mara
Maelezo Hapa tuna safari ndogo ya kuzuru viungo vya uwana na vya uzazi mwilini. Mwili wa
mwanamke
Vifuko viwili katika tumbo
la uzazi (ovaries): Kuna
vifuko viwili, kila moja kina ukubwa wa kiasi cha lozi.
Vifuko hivi hutengeneza
mayai ya uzazi.
Tumbo la uzazi ama mji wa
mimba: Ni
kiasi cha ukubwa wa tunda la pears likiwa limelazwa juu chini. Lina vifereji
viwili vinavyotoka katika vifuko vya kuhifadhi na kutengenea mayai ya uzazi
hadi katika tumbo la uzazi.
Kibofu cha mkojo: Kifuko cha misuli
inayohifadhi mkojo
Mshipa wa kupitisha mkojo
(Urethra): Mshipa
unaopitisha mkojo kutoka katika kibofu.
Uke: Eneo la sentimita karibu
nane kwa kina kutoka njia nyembamba ya tumbo la uzazi la mwanamke, ambapo hufunguka
kati ya miguu. Uke huwa kama mpira hupanuka kwa urahisi wakati unapoingiliwa na
uume ama wakati wa kujifungua.
Sehemu panapopitia haja
kubwa (mkundu): Njia
inayofungwa kwa misuli miwili inayopitisha haja kubwa.
Njia nyembamba ya tumbo la
Uzazi (Cervix): Kama
kijishingo cha tumbo Uzazi. Kawaida huwa imefungika kukiwa na sehemu ndogo ya
njia ambamo damu ya hedhi hupitia.
Kinembe: Kiungo kilicho juu ya uke,
ncha yake ndio huonekana wakati wa raha ya kujamiiana kinembe hupanuka na
kusimama na mara nyingi ndio husababisha mshushio
Mwili wa mwanamume
Uume: Ni kiungo kilicho kama
yavuyavu ambacho wakati kinasimika mishipa hujaa damu na kukifanya kusimama na
kuwa thabiti. Urefu wa kawaida wa kiungo hiki ni kuanzia sentimita 12 hadi 19
wakati kimesimika.
Mshipa wa kupitisha mkojo: Ni kama mfereji unaosafirisha
mkojo kutoka kwenye kibofu ama shahawa hadi Uumeni.
Kichwa cha Uume: Ni sehemu ya uume
inayofanana na kofia, ikiwa ni sehemu nyepesi
Govi: Ni ngozi inayofunika na
kukipa ulinzi kichwa kwa uume. Ni lazima govi kuvutwa na kurudishwa nyuma wakati
wa kuusafisha uume ili kuepuka kuambukizwa.
Tohara: Kutolewa kwa govi hutekelezwa
katika utaratibu unaojulikana kama tohara na hufanywa kwa watoto ama vijana wa
kiume kama sehemu ya utamaduni ama maadili ya kidini ama kwa maswala ya matibabu
(angalia tohara ya mwanaume).
Manii: Ni chembechembe za uhai
zilizo na mfano wa viluilui ambavyo wakati vikikutana na yai la uzazi la mwanamke
hulirutubisha na kutengeneza chembechembe mpya za uhai ambazo huwa mtoto
Shahawa: Ni majimaji ambayo mbegu
za uzazi za kiume huogelea, Mbegu hizi uhitajika kurutubisha yai katika mwanamke
ili kutengeneza mtoto. Mbegu hizi hushushwa katika shahawa kuitia mshipa
unaopitisha mkojo kwa kawaida lakini wakati wa mshushio mkojo huwezi kuingia
katika mbegu hizo. Kwa kiwango cha kawaida kijiko kimoja cha chai kilichojaa
shahawam huwa na mbegu milioni mia taatu za uzazi.
Kusimika: Kukauka ama kusimama kwa
uume kutokana na matamanio ya kujamiiana.
Mshindo au mshushio: Kutokwa na Shahawa kupitia
mshipa unopitisha mkojo, Hutokea wakati wa kujamiiana, ikiwa ni pamoja na
kujichua ama kuchuliwa.
Mfuko wa kokwa: Huu ni mfuko unaohifadhi
kokwa
Kokwa: Viungo vyororo vya duara
ambavyo hutengeneza mbegu za uzazi za kiume.
Sehemu panapopitia haja
kubwa (mkundu): Njia
inayofungwa kwa misuli miwili inayopitishia haja kubwa.
Kibofu cha mkojo: Kifuko cha misuli
inayovutana ambacho huhifadhi mkojo
mwili wa mwanamume
Ubikira
Bikira ni mtu ambaye hajawahi
kujihusisha na masuala ya kujamiiana. Wanawake huwa na utandu unaojulikana kwa
kiingereza “Hymen” katika lango
lao la uke. Baadhi ya watu
wanaamini utandu huo ndio thibitisho la mtu Bikira. Imani hii yaweza kusababisha
huzuni na wasiwasi kwa mwanamke ambaye hana utandu huu lakini ni Bikira. Utandu
huu unaweza kuvutika na kuchanika wakati wa mazoezi, michezo ama utumizi wa
visodo vya kuingiza ukeni kufyonza damu wakati wa hedhi. , Mwanamke anaweza
kuwa Bikira bila ya kuwa na utandu huu.
Kujamiiana moja kwa moja kwa mara
ya kwanza hutia hofu. Wakati mmoja ama wahusika wote ni bikira, ni vyema kuwa
mtaratibu na kuweza kueleweana. Utandu huu sio ukuta ambao utahitaji kubomolewa,
na wala si lazima damu ionekane, kuthibitisha mtu alikuwa bikira. Kuna baadhi
ya wanawake na watoto wa kike ambao huwaruhusu wanaume kutumia sehemu zao za
kupitishia haja kubwa, kwa njia hii ili wahifadhi ubikira wao. Bila ya kutumia
mpira wa kondomu ngono hii ni hatari. Mara ya kwanza kujamiiana moja kwa moja
utapatwa na uchungu na kuumia ikiwa wewe ni mwanamke au mwanamume unaweza
kutunga mimba katika jaribio lako la kwanza kabisa katika kujamiiana ikiwa hutaki
kufanya hivyo usijihusishe kabisa.
Uja uzito
Ili yai liweze kurutubishwa,
lazima liwasiliane na manii ya mwanamume, wakati Mwanamume anashusha, manii
husafiri kutoka katika pumbu zake hadi katika uume wake na kutoka na kuingia
katika uke wa mwanamke. Manii husafiri kuelekea katika tumbo la uzazi na
kukutana na yai hilo katika vifereji vya uzazi. Urutubishaji hufanyika hapa
wakati manii yanapoungana na yai. Ikiwa yai lililorutubishwa liko katika tumbo
la uzazi, mwanamke basi anatunga mimba, yai hili hutulia katika tumbo la uzazi
na kuanza kukua na baadaye katika kipindi cha kiasi cha miezi tisa motto huzaliwa.
Dalili za mapema za ujauzito ni
pamoja na kukosa kupata hedhi yako, matiti kuwa makubwa na kuwasha,
kichefuchefu na kutapika, ladha kama ya nyuma mdomoni, uchovu na kizunguzungu. Kuthibitisha
umetunga mimba unaweza kufanyiwa kipimo rahisi na kituo chako cha uzazi wa
mpango ama katika zahanati ya matibabu, (angalia anuwani) Una haki ya kuwa na
siri yako, unaweza kuomba hilo kutoka kwa mtaalamu wako wa afya ikiwa unataka matokeo
yako yawe siri.
Kuna hatari kadhaa zinazohusika na
mtu akiwa mja mzito katika umri mdogo. Hii ni pamoja na hatari za kiafya kama
vile kuzaa mtoto hajatimia muda wake, kupata uchungu wa uzazi kwa muda mrefu na
kuzaa mtoto mwenye uzani wa chini na mdogo. Hatari za kisaikolojia ni, hofu, kujihisi
unahatia, majonzi ama kutengwa na jamaa yako,
u j a u z i t o
mpenzi wako, shule ama jamii. Hatari
za kijamii ni kulazimishwa katika ndoa usioitaka, kufukuzwa shule ama
kuwategemea wazazi wako kwa mahitaji yako ya fedha.
Kutoa mimba Mtu kutunga mimba sio kila wakati
ni bahati njema, ikiwa utajikuta na mimba ambayo
hukuipangia, hali hii inaweza kuwa mbaya sana kwa
kiingereza neno “Abortion” ni utaratibu wa kutoa
mimba ambazo hazikutakiwa. Yaliyomo katika
tumbo la uzazi wa mwanamke hutolewa na mwanamke huyo
hupewa dawa za kutoa mimba hiyo. Utoaji
mimba ni suala ambalo limeleta utata kwa wengi,
lakini ni uamuzi wa mtu binafsi kwa wanawake. Kati
baadhi ya nchi ni kinyume cha sheria kutoa mimba na
katika baadhi ya nchi nyingine unaruhusiwa chini ya
masharti kadhaa kama vile kuokoa maisha ya mama. Baadhi ya watu wanaamini kwamba kunywa madawa ya miti shamba ama pombe nyingi ama kufanya mazoezi mengi, kuruka, kutumia homoni ama kujiingiza vifaa ama madawa ukeni ama kuoga na maji ya moto sana zitasaidia kutoa mimba ama kuavya. Hizi sio njia za kutoa mimba, ni za kuharibu afya yako, kwa manufaa yako mwenyewe ni muhimu kuchukuwa hatua za haraka na kuamua kama unataka kutoa mimba au la. Hili ni chaguo la mtu binafsi.
Ikiwa utoaji mimba unafanywa
katika njia isiyo salama, mwanamke anakabiliwa na hatari za kiafya na pia kifo.
Utaratibu huo unaweza kuharibu uwezo wake wa kuzaa kabisa ama hatari nyingine
za kiafya. Utoaji mimba katika baadhi ya nchi ni ukiukaji wa sheria.
Tohara kwa wanawake
Tohara kwa wanawake ni utaratibu
wowote unaohusisha kukatwa sehemu zao za siri ama jeraha lolote la kusudi
katika sehemu za siri za mwanamke.
Utaratibu huu unaambatana na
itikadi za kitamaduni na kidini, lakini ni tatizo kubwa kwa wale wanawake wanaokumbana
nalo.
Hatari za kiafya katika utaratibu
huu ni, uchungu wa hali ya juu, huenda mtu akazimia, kuvuja damu kupita kiasi,
kuambukizwa magonjwa, kujizuia kwenda haja ndogo na kidonda katika eneo la
ukeni.
Matokeo ambayo huwaathiri
waliofanyiwa tohara kwa muda mrefu ni kupata uvimbe wa ndani ulio na majimaji,
kuharibiwa kwa njia ya kusafirishia mkojo, kuambukizwa magonjwa na ukosefu wa
uwezo wa kuzaa. Kujamiiana pia kunaweza kumpa mwanamke aliyepitia utratibu huo
maumivu ya hali ya juu. Wengi wanayanyasika wakiwa kimya, na huenda wakapata
hisia mbaya za kiafya ama kisaikologia kutokana na maswala ya tohara. Hatari
hizi zinazohusisha afya ya wanawake zimeleta shauku nyingi katika maadili ya
kitamaduni na kidini na umuhimu wa kuendelea na utaratibu wenyewe. Nchi nyingi
zinapinga tohara ya wanawake.
tohara kwa wanawake
Vyama vya Uzazi wa Mpango
vinachunguza kwa makini hatari zinazoikabili afya ya mwanamke kutokana na
tohara ya wanawake. Ikiwa una wasiwasi kuhusu suala hili wasiliana na kituo
chako cha kitaifa cha Afya ya uzazi.
Tohara kwa wanaume
(Angalia pia maelezo)
Ili utaratibu huu uwe salama,
lazima utekelezwe kwa usafi wa hali ya juu, kwa vifaa vilivyo visafi na wataalamu
walio na ufahamu wa maswala ya afya kuhusu utaratibu huu.
Tohara kwa wanawake •
tohara kwa wanaume
Ngono kavu
Ngono kavu ni shughuli ya
kujamiiana kupitia uke ambako mwanamke huwa amekausha uke wake. Wakati mwengine
miti shamba hutumika kukausha zaidi yale majimaji ya ukeni na kuufanya uke kuwa
mkavu kabisa. Ngono hiyo huongeza hatari ya kuambukizwa magonjwa ikiwa ni
pamoja na virusi vya HIV. Ngono kavu pia humletea mwanamke maumivu mengi wakati
inapoendelea. Kuna imani kwamba wanawake walio na maji maji katika uke wao sio
waaminifu kwa waume zao. Uke huwa na majimaji kwa kawaida kusaidia kurahisisha ngono
ya moja kwa moja. Wanawake wengi wanauwezo wakutoa maji hayo asili yanayoleta utelezi
na kurahisisha uume kuingia bila matatizo. Kuwa “Tayari kwa ngono”
hakumaaninishi uko tayari kufanya ngono na yeyote na “kutokuwa na tayari kwa
ngono” ikiwa ni ngono kavu inamletea mwanamke maumivu zaidi (angalia kuchezea
sehemu zinazoamsha hisia za kujamiiana).