Hatuhitaji kutubu kwa wanadamu.
Baada
ya wokovu ni muhimu kufahamu kila mtu aliyeokoka anakuwa ameungwa kwenye
uhusiano wa moja kwa moja na Mungu kupitia kazi aliyoifanya Yesu wewe sasa
umekuwa mwana wa Mungu, Mungu amekuwa baba kwako huu ndio uhusiano tulio nao na
Baba yetu, wote tunajua uhusiano wa kawaida tulio nao na wazazi wetu katika
hali ya kawaida huwa unafanya nini uhusiano na baba yako au mama yako unapokuwa
umeharibika? Kristo anatufundisha wazi jinsi ya kurejesha uhusiano na baba yetu
wa mbinguni pale kunapokuwa na tatizo katika mfano ule wa mwana mpotevu Yesu
alionyesha wazi jinsi toba ya kweli kwa mwana huyo aliyetumia vibaya urithi na
mal alizopewa na baba yake kwa kutaka kujitawala ni wazi kuwa alipozingatia
moyoni mwaka kurudi kwa baba yake kamwe hakuwaza kutafuta mpatanishi kati yake
na baba aliamu kurudi moja kwa moja kwa baba Luka 15; 17-18 “alipozingatia moyoni mwake alisema Ni watumishi wangapi wa
baba yangu wanakula na kusaza na mimi hapa ninakufa kwa njaa Nitaondoka
nitakwenda kwa baba yangu na Kumwambia
baba nimekosa juu ya mbingu na mbele yako” ni wazi kabisa fundisho
kuhusu toba ndani ya Agano jipya kwa mtu ambaye Mungu ni baba yake halihitaji
kupitia kwa mwanadamu hata kidogo, tunaweza kuwaomba radhi au msamaha wanadamu
wenzetu tunapokuwa tumewakosea lakini linapokuja swala la kumosea Mungu dawa
sio mtu dawa ni kumuedea Mungu mwenyewe hakuna mwanadamu mwenye haki ya
kutupatanisha na Mungu nje ya Mungu mwenyewe na sisi tuliomkosea Biblia
inatuonyesha wazi kuwa Kristo ndiye kuhani wetu mkuu huyu ni Mungu na
tunapomuendea Yeye hutupatanisha na Mungu Waebrania 4;14-16 “……Basi na
tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri ili tupewe Rehema na kupata neema ya
kutusaidia wakati wa mahitaji yetu” Kwa nini mitume wa bwana
hawakuchukua nafasi ya makuhani badala yake walielekeza watu kuwa mpatanishi
kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja tu Kristo Yesu 1Timotheo 2;5 Biblia inasema
hivi “Kwa sababu
Mungu ni mmoja na mapatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja , Mwanadamu
Kristo Yesu” wahubiri wengi sana wamejitukuza aidha kwa kujua au kwa
kutokujua na wamechukua nafasi ya Kristo msomaji wangu hata na mimi nilikuwa
hivyo nilifikiri kuwa toba ya kweli lazima ipitie kwa mtumishi wa Mungu ili
akuombee neema pia kuna wakati nilifikiri unapotubu dhambi zako na kuzikiri
wazi kwa wanadamu unapokea msaaada kama ule anaoutoa Yesu yaani msamaha lakini badala yake nilihukumiwa vibaya,
wokovu umeingiliwa leo kuna watu ambao wanataka ukiri makosa yako kwao wao
wamekuwa kama ndio Kristo wanahubiri hukumu na kuwafunga washirika na watumishi katika vifungo vya hukumu
wakichukua nafasi ya Mungu watu hawapaswi kuungama kwa mchungaji au kuhani
mwanadamu au padre, hatuja wakosea wao tumemkosea Mungu peke yake Mtumishi wa
Mungu Daudi ingawa alikuwa amefanya dhambi mbaya zenye kuumiza watu wengine
hatuoni kamwe akielekeza toba yake kwa wanadamu Badala yake alimuelekea Yule
mwenye haki na mwenye rehema angalia yu asema hivi katika Zaburi 51;1-4 “Ee Mungu unirehemu sawasawa na na fadhili zako kiasi cha
wingi wa rehema zako uyafute makosa yangu unioshe kabisa na uovu wangu
unitakase dhambi zangu maana nimejua mimi makosa yangu na dhambi yangu mbele
yangu daima Nimekutenda dhambi, Wewe peke yako na kufanya maovu mbele za macho
yako wewe ujulikane kuwa na haki unenapo na kuwa safi utoapo hukumu” unaona Ni Mungu pekee
anayehitaji kupelekewa toba zetu,yeye peke yake ndiye mwenye haki hatupaswi
kufungwa na viongozi wa dini ambao ni vigumu kuwafikia kwa sababu a ukubwa
walio nao leo hii Yesu ni rahisi kufikiwa na kuombwa radhi na kupokea msamaha
tele kuliko kwa viongozi Fulani wa kidini ambao wanajifikiri kuwa ni miungu
watu msomaji wangu mwendee Yesu kwa imani kwa kuvunjika sirini tubu uovu wako
na dhambi zako atakusamehe kabisa huhitaji kumwambia Yeyote wao dhambi zao
wanazitubia wapi? Ni lazima ujiulize na kujua kuwa wao pia ni watu na sio
wakamilifu wengine wanaiba sadaka za kanisa wamenunua gari na majumba kwa
sadaka za watu masikini kwa manufaa yao na kwa majina yao na wakisimama katika
madhabahu utafikiri kuwa wao ndio miungu unapaswa sasa kuimama na neno la Mungu
na kuliamini acha kwenda kujianika kwa wanadamu, Mungu angekuonyesha maovu yao
wanayoyafanya sirini je ungewapelekea dhambi zako? Wao pia ni watu Makuhan
wakati wa agano la kale walitakiwa pia kutoa dhabihu kwaajili yao binafsi na
kwaajili ya watu wengine pia maana nao walikuwa wenye dhambi.
Toba ya kweli kamwe haipaswi kupitia kwa wanadamu wenye damu na nyama kama wewe atoba ya kweli huelekea kwa Mungu aliye hai peke yake
Watu wa
Mungu wameteseka kwa Muda mrefu na kuishi chini ya hofu kwa kugopa kuhumiwa na
wachungaji mapolisi na wakati mwingne wamekaa na dhambi kwa muda mrefu bila
kuzitbia wakifikiri kuwa hawawezi kusamehewa mpaka kwa neno la Mchungaji au
maombi yake Hapana ! hilo ni kongwa wamekufungia unaweza ukakosa ufalme wa
Mungu Yesu u Karibu na wewe kuliko mchungaji wako na kwa kweli yeye ni
mwaminifu ukiziungama dhambi zako atakusamee na kuondoa udhalimu wote changamka
acha kujikunyata kwa mafundisho yasiyokupa furaha Dhambi ikitendwa kwa Mungu
dawa yake ni Mungu na sio Binadamu swali la Eli Yule kuhani linajibika kirahisi
leo kuliko wakati wao kabla Kristo hajaja Eli aliuliza hivi 1Samuel 2;25”Mtu mmoja akimkosa mwenzake Mungu atamuhukumu lakini mtu
aklimkosa Bwana ni nani atakayemtetea?Ngoja nimjibu Eli jibu ni rahisi
sana Yesu atamtetea mtu huyo kwa nini yeye ndiye kipatanisho kwa dhambi
zetu,Mungu hawaweka Mitume,Manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu kwa kusudi
la kusamehe dhambi au kusikiliza dhambi za watu na kutoa hukumu hiyo sio kazi
yao wala sio kazi ya malaika Kazi ya watumishi hao ni kuujenga mwili wa Kristo
yaani kanisa katika kuujenga wanaweza kuombea washirika kukua kiroho n.k lakini
kamwe hawawezi kufanya kazi ya kutupatanisa na Mungu ndugu kinachohitajika ni
ujasiri na kujisamehe ujasiri huu utokane na kulijua neno la Mungu na kufahamu
kle unachopaswa kukifanya Waebrania 10;19-22 “Basi
ndugu kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu njia ile
aliyotuanzia iliyo mpya iliyo hai ipitayo katika pazia yaani mwili wake na kuwa na kuhani mku juu ya nyumba ya Mung na
tukaribie wenye moyo wa kweli kwa utimilifu wa imani hali tumenyunyiziwa
mioyo tuache dhamiri mbaya tumeoshwa
miili kwa maji safi” Msaada wa Mungu unapatikana kwa imani isiyo na
shaka ni imani ndiyo inayotuwezesha
kumpendeza Mungu ndugu yangu amini katika wema wa Mungu , mjie kpitia Kristo
kwa mo wa kweli hu ndio unyoofu utapata
rehema na neema msaada wako utatoka wapi utatoka katika Bwana wa majeshi huko
utasamehewa ndugu yangu toba ni Ibada na hakuna ibada inayopelekwa kwa
mwanadamu ikiwa haifai kuomba Mariam aliyemzaa Yesu kutuombea sisi wakosefu ni
wazi kuwa haifai kupeleka dhambi zako kwa mwadamu awaye yote eti ili akuombee
toba kwa Mungu, kuna faida gani kupeleka toba kwa Mungu kwake yeye anatujua
umbo letu na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi Yeye ndiye aliyetuumba na
anaoufahamu kamili kutuhusu anasoma mawazo yetu kabla hatujawaza Zaburi 139
1-12 na kuendelea inaonyesha jinsi Mungu anavotufahamu wachungaji wetu
hawatufahamu na hakuna nguvu ya kuwaeleza kwa ukamilifu dhambi tuzifanyazo
kwani wao nao hawatuambii zao basi tumwambie Mungu kwake Mungu tunaweza
kumueleza kwa uwazi na upana na uhuru na kumuomba atusaidie na baada ya hapo
atatusamehe wala hatutasikia mitaani dhambi zetu zikianikwa hata baada ya kuwa
tumemueleza Mungu uovu wetu wote, lakini kama unataka kuaibika na kufedheheka
duniani wapelekee wanadamu maovu yako utakoma! mimi sijajua mpaka sasa ni
andiko gani wanalisimamia kutaka kusikia dhambi za watu au toba zipitie kwao
hili ni kongwa Bwana akupe neema na kukuponya katika maumivu yaliyokupata kwa
sababu Yoyote ile inayotokana na mafundisho yasiyo ya kibiblia na ambayo ni
mapokeo ndio maana nilikuambia mapema kitabu hiki hakiko mkononi mwako kwa
bahati tu kwani zawadi kutoka kwa Mungu kwa ajili yako Nanyi mtaifahamu kweli
na hiyo kweli itawaweka Huru!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni