UJUMBE: UPIGANE NAO WANAOPIGANA NAMI!
Zaburi 35:1-38
Zaburi ni mojawapo ya vitabu vya kipekee
sana katika Biblia ni moja ya kitabu maarufu kilichoko katika kundi la vitabu
viitwavyo vitabu vya mashairi ya kiebrania na ndicho kitabu kirefu kuliko vyote
katika Biblia kwani kina sura karibu 150 zilizogawanywa katika vitabu vitano,
inaaminika kuwa ndicho kitabu kinachosomwa zaidi na kuhubiriwa zaidi kuliko
vyote katika agano la kale, aidha waimbaji wengi sana na watunzi wa nyimbo hutoa nyimbo zao katika
zaburi, sababu moja kuu inayovutia wengi katika zaburi ni kwa sababu zinagusa
hisia za watu
·
Zaburi ziliandikwa kwa sababu
mbalimbali za kihisia kama vile watu walipokuwa na furaha, huzuni, nk, Mfano
mwandishi wa wimbo nionapo amani kama shwari kwa hiyo kuna sababu nyingi
zilizopelekea zaburi kuandikwa kati ya hizo ni pamoja na
1. Zaburi kwa ajili ya hekima na maadili mfano zaburi ya 1
2. Zaburi kwa ajili ya shukurani nyingi huanza kwa kusema mshukuruni Bwana!
3. Zaburi za kujitia moyo mfano zaburi ya 27
4. Zaburi za kifalme au za kimasihi
5. Zaburi za kihistoria au za kukumbuka matukio maalumu
6. Zaburi za kusifu au “Halel Psalms” ambazo huanza na neno Haleluya
7. Zaburi za maombolezo
8. Zaburi za dua na maombi pamoja na kulaani Mfano Zaburi ya 35 : 1-8
Leo
nataka tuchukue Muda kuitafakari zaburi hii ambayo huangukia katika kundi la
zaburi za kulaani, au zaburi za maombi lakini wakati huu mwandishi wa zaburi
hii anaomba mabaya au hukumu ndhidi nya adui zake! Ni zaburi ngumu wakati
mwingine kuitafasiri ukilinganisha na Mafundisho nya Bwana Yesu kuwa
tusiwalaani maadui zetu bali tuwaombee mema hata wale wanaotuudhi! Luka 23:34
na Mathayo 5:39,44. Hata hivyo ni muhimu kujiuliza Kwanini Roho Mtakatifu
ameruhusu Zaburi hii kuweko!
1. Kila mtu aliyeokoka anayo haki ya kudai ulinzi wa Mungu dhidi ya watu
waovu na wanaotuonea, Mungu hakutuita duniani tu ili tutukanwe na kudhulumiwa
na kusemwa vibaya na kuteswa na kuonewa na kuuawa na kuchukuliwa wake zetu,
waume zetu, kujaziwa mimba watoto wetu, kusemwa vibaya kukandamizwa kuzibwa
vinywa eti kwa vile sisi ni walokole Hapana! Simama na kuitetea haki yako!
2. Mwandishi wa zaburi hii hatufundishi kujichukulia sheria mkononi na
kujilipia Kisasi lakini anatufundisha Kumtegemea na Kumsihi Mungu awaadhibu
waovu kulingana na uovu wao anayeteta name Bwana atete naye!, anayepigana nani
Bwana apigane naye! Hatuwezi kama wakristo kukaa kimya pale uonevu unapofanyika
kisha Mbingi ziko kimya na serikali iko kimya Biblia inatufundisha kuidai haki,
naweza kushindwa kuandamana, kubeba silaha, kujitetea mwenyewe, kwenda
mahakamani n.k lakini siwezi kushindwa kuingia Magotini na kuidai haki yangu
Mungu ni Lazima anilipie Zaburi 28:4 Unasema Hivi “ Uwape sawasawa na Vitendo
vyao Na kwa kadiri ya Ubaya wa kufanya kwao, Uwape sawa sawa na Kazi za mikono
yao Uwalipe stailizao”
3. Biblia kupitia Zaburi hii inatufundisha kuwa kiko kiwango cha uvumilivu
lakini kama uovu utaendelea kupita kiasi na kufikia kilele Ni lazima
Kumkumbusha Mungu katika Haki yake kutoa haki na hukumu, ni lazima tusimame
kuhakikisha kuwa Uonevu na ukatili vinakomeshwa na kuharibiwa Yesu Mwenyewe
alifundisha Mfano wa Mwanamke mjane Katika Luka 18:3 aliendelea kuomba bila
kukata tama mpaka haki yake ikapatikana tena Kristo alihahidi kuwa Mungu
hataacha kuwapatia haki wateule wake wanaomlilia Mchana na Usiku Luka 18:7
4. Zaburi hii inatufundisha kuwa ingawa tunatamani kuona watu wanamgeukia
Mungu na kuja kwake kupitia Upole wetu, upendo na Unyenyekevu, Lakini pia
tutamani kuona Uovu ukiharibiwa na watu wakatili wakishughulikiwa, Nimlazima
tumuombe Mungu ashughulikie adui zetu ndio adui yetu mkuu ni shetani lakini na
wale anaowatumia kutuonea na kutubughudhi na kutukerehesha ni muhimu kumsihi
Mungu ashughulike navyo ni lazima tumuulize Mungu Maswali ambayo hata Daudi na
upendo wake na huruma na rehema alimhoji Mungu!
Mbona Mataifa wamefanya ghasia
Na kabila za watu wametafakari Ubatili?
Wafalme wa Dunia wamejipanga
Na wakuu wamefanya shauri pamoja
Juu ya Bwana na juu ya Mpakwa mafuta wake.
Ni wakati wa kusimama na kudai haki yako dhidi ya Udhalimu wa kila aina,
lazima umwambie Bwana ashughulike na kila kinachokukosesha raha na amani hapa
duniani, kama ni magonjwa, Mapepo, Mateso, Ugaidi, Uonevu, Dhuluma, Kunyanyaswa
n.k. Usikubali ukaonelewa Yuko awezaye Kupambana navyo mweleze ashughulike
navyo!
Ujumbe:
Na Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.