Paulo Mtume ni moja ya nguzo muhimu sana
Katika Ukristo na ulimwengu kwa ujumla kuliko hata Muhamad,Waislam wanaamini
kuwa kila jamii ina mtume wake na kuwa Muhamad ndilo jibu la Matumaini ya umma
wa Kiarabu, na mataifa mengine, Lakini ilivyo ni kwamba Matumaini ya mtume
anayefiti anayestahiki kwa ulimwengu Mzima yanajibika kibiblia kuwa Paulo mtume
ndiye Jibu hilo na ndio maana waislamu wanamchukia, ni wazi kuwa kama jinsi
ambavyo ni kufuru kumlinganisha Muhamad na Yesu kristo kwani Ni Mungu, lakini
ni kumvunjia Kristo heshima kwa kumlinganisha Paulo na Muhamad.
Paulo Mtume ni Mkuu Kuliko Muhamad mwanzilishi wa dini ya Kiisalamu
Paulo ni Mtume wa Mataifa.
Kama Waislam walikuwa wanaona kuna hitaji kwa kila taifa kuwa na Mtume wake ni
Muhimu kwao kufahamu kuwa Mpango wa Mungu tangu mwanzo haukuwa kuwapendelea
wayahudi tu, yeye tangu mwanzo alimkusudia Ibrahimu kuwa Baraka kwa jamaa zote
za dunia (Mwanzo 12;1-3),Baraka hii
ilitimizwa kupitia Yesu kristo ambaye alitolewa kwa kusudi lileliel la
kiulimwengu (Yohana 3;16),Katika
mpango huu mzima wa kuwafikia Mataifa yoote Masihi aliwaagiza wanafunzi wake
kuihubiri injili kwa kila taifa (Mathayo
28;19) inashangaza sana kufikiri kuwa Manabii waliotumwa Pamoja na Ujio wa
Kristo duniani uliihusu Israel tu au wayahudi tu na ndio maana hata ile siku ya
Pentekoste Roho mtakatifu alipo washukia wanafunzi wa Yesu waliwezeshwa
kuzungumza lugha mbalimbali ikiwemo kiarabu soma (Matendo 2;1-12).Hii maana yake ni kuwa Mungu alitaka kuufikia
Ulimwengu mzima kupitia Taifa teule alilolitenga la Kiyahudi maana huko ndiko
wokovu unakotokea(Yohana 4;22), na mwokozi wa ulimwengu ni mmoja
tu (Yohana 4;39-42).
Ni katika kusudi zima la kuufikia ulimwengu Mungu alimchagua Paulo mtume
aifanye kazi hii (Matendo 9;1-15).
Ni dhahiri kuwa hata Roho Mtakatifu alithibitisha kuwa amemuita Paulo kwa kazi
hii maalum (Mdo 13;1-3).Jambo hili lilikuwa bayana hata kwa Paulo mwenyewe kuwa
neema na utume alioitiwa ulikuwa maalum kwa mataifa (Warumi 1;5, Wagalatia 2;7-8,9-9).Mungu
bado hata sasa aweza kutumia watu mbalimbali na wakawa ni viongozi Maarufu sana
duniani toka jamii ya mataifa lakini woote watakuwa na kazi moja tu kumhubiri
Yesu Kristo, Hivyo kama ilikuweko haja ya mtume kwa waarabu angeinuliwa na
angemhubiri kristo na sivinginevyo,Kinyume chake basin a waafrika tutahitaji
nabii wetu, Wahindi nao, wazungu, nao nk. Kilichokuwa kinahitajika ni mtume na sio
injili Nyingnie kwani yeye aliyeleta
injili nyingine amelaaniwa!(Galatia 1;6-9).
Paulo alipewa mafunuo Makubwa sana kuliko Muhamad.
Woote tunajua kuwa Paulo Mtume alipewa
mafunuo makubwa sana kuliko aliyopewa muhamad,Injili aliyoihubiri si ya namna
ya kibina damu kwani aliipokea na kufundishwa kwa ufunuo wa Kristo Yesu
mwenyewe aliyemuita (Wagalatia 1;10-12),Paulo
alinyakuliwa mpaka peponi na kufika mbingu ya tatu kwa ajili ya maono na
mafunuo ya Bwana (yaani Yesu) soma (2Koritho12;1-7),Mungu
alimtumia Paulo mtume kwa namna ya kupita kawaida Biblia inasema (Matendo 19;11) “Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo
miujiza ya kupita kawaida;” Neema ya Mungu iliyokuwa juu yake
hailinganishwi kamwe na utume wa Muhammad kwanini waislamu wasione wivu zaidi
ya yoote tunaweza kuseama mambo ya msingi yafuatayo kumhusu Paulo.
Paulo ni Mtetezi Mkuu wa Ukristo na
Mafundisho yahusuyo kuhesabiwa haki kwa imani.Paulo
alizungumza, kufundisha, Kufafanua na kutetea
mafundisho yahusuyo haki inayotokana na Imani mafundisho yanayooonekana
kuwa Mwiba na tishio kwa waislamu ambao hufundisha kuwa haki inapatikana kwa
matendo, Kwa waislamu matendo mema yanahesabiwa kuwa thawabu na yanampa mwislamu
nafasi ya kuingia Paradiso, Hiki ambacho waislamu wanafundisha ni matendo ya
sheria kuwa mtu anaokolewa kwa matendo, na bidii ya kibinadamu nakwa kufuata
matendo ya sheria na Sikukuu zao,Paulo anafanyika mwiba wa mafundisho hayo na
ndio maana wanamchukia.(Galatia
2;15-16,3;10 Kolosai 2;16-22).
Paulo alikuwa na bidii na kuusambaza Ukristo duniani.(Mdo
13;46-48).
Paulo alifanikiwa kuipeleka injili nje ya mipaka ya Israel na mipaka ya
iliyokuwa himaya ya Rumikutoka huko injili ilifika hata ulaya na hatimaye
ulimwengu mzima wa wakati ule, Waislamu wanaona kuwa Paulo hakufanya sahihi
alifanya makosa kwa kuipeleka injili nje ya mipaka ya Wayahudi, Ukristo kwa
waislamu wanaamini kwamba uliwahusu wayahudi tu wanaamini ukristo ulikuja kwa
ajili ya kuwakosoa wayahudi,kuwarekebisha na kuwaongoza wao, Kwa kuupeleka kwa
Mataifa Paulo ameharibu ukristo halisi, na hivyo ameufanya Ukristo kuenea dunia
nzima hili linawaudhi sana waislamu na ndio maana Humpinga.
Wakolosai 1;3-6, Leo injili
imezaa matunda na kusambaa ulimwengu mzima kutokana na kazi aliyoifanya Paulo
Mtume Unadhani shetani atampenda? Sisi kama wasomi wa Biblia tunakubaliana kuwa
Paulo anamchango mkubwa sana usiopingika katika kusambaza nuru ulimwenguni
hivyo kumchikia yeye ni kuichukia nuru, aliisambaza injili kwa mafanikio kwa
amani wala hakutumia upanga kama Muhamad.Paulo mtume alikuwa na neema kuu sana
ambayo Muhamad hawezi kuifikia hata leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni