Waebrania 12:2-3 “tukimtazama Yesu, mwenye
kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa
mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume
wa kiti cha enzi cha Mungu. Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili
mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije
mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.”
Utangulizi:
Usiudharau Msalaba wa Yesu!
Angalia iko nguvu ya ajabu na uwezo wa ajabu katika Msalaba, Msalaba unaweza
kukupa ushindi dhidi ya changamoto zozote unazozipitia katika maisha, Ushindi
mkubwa katika maisha yetu utapatikana kwa kitafakari kazi kubwa iliyofanya na
Yesu Kristo pale Msalabani, wokovu kamili umekuja kwetu kupitia Msalaba na ndio
maana ni muhimu sana kuutafakari , na kukumbuka kazi aliyoifanya Yesu Pale
Msalabani
Paulo Mtume anaonyesha kuwa
msalaba una nguvu, na kwa watu wanaopotea unaokana kuwa ni upuuzi lakini kwetu
sisi tunaookolewa ni Nguvu ya Mungu angalia katika 1Wakoritho
1:18 “Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni
upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.” Ulimwengu
unafahamu kuwa katika Historia Mfalme mmoja wa kipagani wa Rumi aliyejulikana
kama CONSTANTINE akiwa pamoja na askari wake vitani tarehe 27/10/312 Baada ya
Kristo, akiwa katika kambini Jeshini na wanajeshi wake aliona alama ya Msalaba
upande wa juu wa jua na maandishi yaliyoansikwa kwa lugha ya Kiyunani, Lakini
yanasomeka au yamepata umaatrufu zaidi katika Lugha ya Kilatini “IN HOC SIGNO VINCES” Kwa kiinregreza “IN THIS SIGN YOU WILL CONQUER” Yaani kwa ishara
hii Utashinda. Unaona kwa mujibu wa mwana historia maarufu wa karne ya tatu
Askofu Eusebius wa Kaisaria anaeleza kuwa Contantine alikuwa akisonga mbele na
jeshi lake bila kutaja ni mahali ganina
alipoangalia juu ya jua aliona msalaba unaong’ara juuyake
yaliandikwa maneno hayo, inasemekana kuwa Contantine hakuwa ameelewa
maana ya maono yale lakini usiku alipokuwa amelala aliona katika ndoto Yesu
akimfafanulia kwamba anaopaswa kuitumia alama ya msalaba dhidi ya adui
zake na kuwa atapata ushindi, Tangu
wakati huo wakristo wengi wa maeneo ya kilatini huutumia msalaba kama alama ya
ushindi, wachezaji wa mpira wa miguu wanapoingia viwanjani hugusa uwanja na
kuonyesha alama ya msalaba, alama ya msalaba ilipata umaarufu mkubwa kutokana
na ushindi alioupata Contsntine ambaye baada ya ushindi wake aliifanya Roman
kuwa himaya ya Kikristo.
Msalaba si jambo la kupuuzi ni ushindi wa maisha yetu, nilipokuwa
nikitafakari kwamba ni jambo gani naweza kuzungumza na waomaji wangu na
wasikilizaji wangu, Roho Mtakatifu aliniambia waaembie wasiudharau Msalaba, hii
haina maana ya kuwa watu waubusu na kuuheshimu msalaba wenye sanamu ya Yesu
hapana, maana yake ni lazima wakubali na kumtafakari Yesu mwenyewe aliyekubali
kufa msalabani kwaajili yao/yetu.
Unapofungua Biblia yako katika injili ya Luka 23:35-43 tunapata habari
za watu wawili wanaowakilisha jambo mmoja watu wanaodharau kazi ya msalaba na wa pili
watu wanaouheshimu msalaba watu hawa walikuwa karibu kabisa na Yesu aliyekuwa
anasulubiwa hali kadhalika na wao walikuwa wakisulubiwa siku ile hebu tusome
kwanza tuone
Luka 23:35-43 “Watu wakasimama wakitazama. Wale
wakuu nao walikuwa wakimfanyia mzaha, wakisema, Aliokoa wengine; na ajiokoe
mwenyewe, kama ndiye Kristo wa Mungu, mteule wake. Wale askari nao wakamfanyia
dhihaka, wakimwendea na kumletea siki, huku wakisema, Kama wewe ndiwe mfalme wa
Wayahudi, ujiokoe mwenyewe. Na juu yake palikuwa na anwani; HUYU NDIYE MFALME
WA WAYAHUDI. Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je!
Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi.Lakini yule wa pili akamjibu
akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo? Nayo
ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu;
bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa. Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke
utakapoingia katika ufalme wako. Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi
utakuwa pamoja nami peponi.”
Unaweza kuona watu walimdharau Yesu pale msalabani, wakatoa maneno ya kejeli
na kumfanyia mzaha walisema aliokoa wengine na ajiokoe mwenyewe hapa msalabani
hususani kama yeye ndio masihi, aidha mhalifu mmoja aliyekuwa anasulubiwa
pamoja na Yesu naye bila aibu alimtukana Yesu na kusema je wewe sio Kristo
jiokoe nafsi yako na sisi, huyu aliupuuzia Msalaba na kujikuta yuko jehanamu
milele na milele
Lakini yule muhalifu mwingine alikuwa na dalili kadhaa zilizomletea
wokovu:-
a.
Alikuwa
na Hofu ya Mungu Luka 23:40 alimuuliza mwenzake Je wewe humuogopi Mungu
b.
Alitambua
kuwa yeye ni mwenye dhambi Luka 23:41 alimweleza mwenzake kuwa sisi
tunasulubiwa kwa sababu ya maovu yetu na uhalifu wetu, hivyo tunapata kilicho
halali yetu ni malipo ya maovu yetu
Lakini sivyo ilivyo kwa Yesu yeye yuko pale akiwa hata hatia
c.
Alimuamini
Yesu kuwa anaweza kumuokoa Luka 23:42 alimwambia Yesu unikumbuke utakapokuja
katika ufalme wako, Yeye aliamini kuwa Yesu huyu aliyetundikwa Msalabani ni
mfalme na atatawala ilikuwa ni imani ya ajabu alikuwa na utambuzi kuwa msalaba
sio mwisho wa maisha ya Yesu
d.
Mwisho
Luka 23:42 alijiombea aweze kuokolewa alimwambia Yesu unikumbuke utakapokuja
katika ufalme wako, jamaa alijitambua kuwa amefanya maovu mengi na kuwa
hasathili chochote alijiombea rehema kwa Yesu palepale msalabani, huyu alikuwa
ni kama mtu anayejua kuitumia nafasi aliyoipata katika dakika ya mwisho, ni
kama timu iliyokuwa imekwisha kufungwa kisha ikasawazisha goli katika dakika ya
nyongeza, Yesu alimjibu Lao utakuwa pamoja nani peponi
Unapopitia changamoto za iana yoyote,
mitihani ya aina yoyote, mateso ya aina yoyote, majonzi ya aina yoyote, dhuluma
ya aina yoyote machozi ya aina yoyote,kuonewa kwa namna yoyote, unyama wa aina
yoyote, uonevu wa aina yoyote, majaribu ya aina yoyote, kucheleweshwa kwa aina
yoyote, ni lazima ukumbuke na kuuangalia msalaba hapo ndipo palipo siri ya
ushindi wako, ushindi wangu uko Msalabani, siogopi chochote Nauangalia msalaba
kwa alama hii nitashinda kama alivyoshinda Mfalme Constantine, wewe nawe ni
mshindi ni mshindi kupitia kazi iliyofanya na Yesu pale msalabani, mwangalie Yesu,
katika mapito yako mwangalie Yesu , katika mateso yako mwangalie Yesu, katika
ugumu wa maisha unaoupitia mwangalie Yesu, katika kesi yako na majonzi na
mateso na njaa, na uchgu na kupungukiwa na aibu nadharau nakukataliwa na
kutokufaanamakosa wewe mwangalie Yesu tu, na kwa kuiangalia kazi aliyoifanya
pale msalabani wewe ni mshindi, Kumbuka Msalaba! Usiudharau!
Na Mkuu wa wajenzi mwenye hekima
Rev. Innocent Kamote.
0718990796.