Jumatano, 19 Julai 2023

Msipoona Ishara na maajabu hamtaamini kabisa?


Yohana 4: 45-48 “Basi alipotoka Galilaya, Wagalilaya walimpokea; kwa kuwa wameyaona mambo yote aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu; maana hao nao waliiendea sikukuu.  Basi alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja ambaye mwanawe hawezi huko Kapernaumu. Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Uyahudi mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa kufani. Basi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa?”


Utangulizi:

Yesu alikuwa ni mtenda miujiza mkubwa Zaidi kupata kutokea Duniani, Mungu alimpa neema kubwa sana ya kufanya kazi ya uponyaji na kufundisha kwa uweza wa Roho Mtakatifu kila alikokwenda

Mathayo 4:23-25 “Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu. Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya. Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Uyahudi, na ng'ambo ya Yordani

Sababu kubwa ya Yesu kusukumwa na Roho Mtakatifu kufanyahuduma hizi zote ni kwa sababu aliwahurumia watu na kusikitishwa na taabu zao na uonevu wa Shetani aliokuwa ameufanywa kwa wanadamu  hivyo alifanya kazi hiyo ya kuwaponya na kuwafundisha neno la Mungu

Mathayo 9:35-36 “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.”

Kwa hiyo kazi zote alizozifanya Kristo alizifanya kwa sababu ya moyo wake wa upendo kwa wanadamu, alitumia karama zake na vipawa vyake kwa faida ya kuwajenga watu, kuwasaidia, kuwakwamua na kuwatoa katika shida na changamoto kubwa zilizokuwa zikiwakabili, Hata hivyo kwa upande wa watu waliokuwako nyakati zile wao walianza kumfuata Yesu kila alikokwenda wakifurahi na kushangilia kwaajili ya kuona miujiza na kufurahia ishara alizokuwa akizifanya, Kimsingi Isahara na maajabu sio kitu kibaya na ndio maana Yesu alifanya, lakini kimsingi wanadamu wanatakiwa kujifunza kumuamini Mungu na kujua ya kuwa Mungu anawajali na kuhusika na maisha yao hata bila ya Ishara na maajabu nahiki ndicho kiwango ambacho Yesu alitamani watu wakifikie:- tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-

·         Kusudi kuu la ishara na miujiza

·         Msipoona ishara na maajabu hamtaaamini kabisa

·         Jambo kubwa la msingi

Kusudi kuu la Ishara na miujiza.

Ishara na miujizaa ni mojawapo ya matukio makubwa ya kushangazwa yanayoyanywa na Mungu kupitia watumishi wake ambao amewapa karama mbalimbali kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kuwawezesha watu hao kufanya mambo makubwa nay a kushangaza kwa idhini au kwa jina la Mungu, Tangu zamani katika Israel na hata baadaye nyakati za kanisa la kwanza na siku zoa leo katika jumuia nyingi za kikristo za uamsho kama Charismatic Movements na Pentecostal movements Ishara na miujiza imekuwa ni moja ya sehemu muhimu sana ya kiibada kwa kusudi la kuwaaminisha watu juu ya uwepo na utendani wa Mungu na kudhihirisha kuwa mungu hayuko mbali na watu wake na kuwa yeye ni msaada ulio karibu

 Zaburi 46:1 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.”

Kwa hiyo kumekuweko na msisistizo mkubwa sana wa injili na huduma nyingi za ukombozi na uponyaji, ambavyo kimsingi sio vibaya kwa sababu watu wanasaidiwa na kuponywa magiojwa yao na kusaidiwa kimwili, kiroho na hata kisaikolojia unapoona makundi makubwa ya watu wakitafuta uponyaji unaweza kuhisi huruma na hata kutamani kama ungekuwa na uwezo wa kuwasaidia watu wote ungeweza kuwasaidia lakini hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa kuna makusudi ya kuweko kwa ishara na miujiza , na ni muhimu kujiuliza kwanini Mungu anafanya hizi ishara na miujiza ?

1.       Kufunua ukuu wa Mungu -  Ishara zote zilizofanyika katika agano la kale na zinazofanyika hata sasa katika agano jipya makusudi yake makuu ni kufunua ukuu wa Mungu, ni ili watu wenye kiburi wanaojifikiri kuwa wao ni ka a miungu duniani wapate kutiishwa wajue ya kuwa Yuko Mungu anayetawala Dunia  na kila mmoja aweze kumjua yeye na jina lake na uweza wake na utendaji wake hatimaye waweze kumuabudu na kumuheshimu yeye ona

 

Warumi 9:17 “Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.”

 

Maana yake ni nini kwamba miujiza yote ambayo Mungu aliitenda kuanzia wakati anawatoa wana wa Israel Huko Misri na mingine mingi muda usingeweza kutosha kutaja yote lakini kusudi mojawapo kubwa ni kuufunua ukuu wa Mungu ili dunia ipate kumuheshimu, kumtukuza, kumshukuru, na kutambua kuwa yeye ndiye kila kitu.

 

2.       Kuufunua utukufu wake – ishara zote alizozifanya Mungu katika agano la kale na jipya hata kuanzia kazi zake za uumbaji na maajabu yote na ishara ni kwaajili ya kuufunua utuklufu wake ni ili watu wote wajue na kumsifu Mungu kuwa ndiye Mungu,

 

Zaburi 19:1 “Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.”

 

Unaona Mungu wetu anataka tumtukuze yeye, kumtukuza yeye ni sehemu ya ibada, ni sehemu ya kutambua ukuu wake, ni sehemu ya heshima , ni sehemu ya shukurani ni sehemu ya kuonyesha kuwa yuko mwenye serikali mbunguni na duniani na kuwa tunapaswa kumpa yeye utukufu, hii ni mojawapo ya sababu kwanini Mungu hufanya ishara na miujiza ona pia

 

Yohana 2:11 “Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.”

 

3.       Kwaajili ya huruma na upendo wake  Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai na Baba wa Mbinguni ni wamoja kwa uweza wa Roho Mtakatifu Yesu alitenda kazi ya uponyaji kwaajili ya kufunua huruma na upendo wa Mungu kwa wanadamu kama tulivyoona katika utangulzizi kuwa alifanya yote aliyoyafanya kwaajili ya huruma zake

 

Mathayo 9:35-36 “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.”

 

Kazi hizi alizozifanya Kristo ni kwaajili ya maelekezo yote kutokwa kwa baba yake hivyo alifanya kile ambacho baba yake anakifanya

 

Yohana 5:19-20 “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile. Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; hata na kazi kubwa zaidi kuliko hizo atamwonyesha, ili ninyi mpate kustaajabu.”

 

Kwa hiyo kile alichokitenda Bwana Yesu kwa neno au kwa tendo kinadhihirisha na kufunua Moyo wa Mungu baba kwetu, Kristo Yesu ni chapa ya mng’ao wa utukufu wa Mungu kumuona Yesu ni Kumuona baba, kwa sababu hiyo ni Dhahiri kuwa Yesu/Mungu alifanya ishara na miujiza kwa kusudi la kufunua huruma na upenzo wake kwetu.      

 

4.       Kwaajili ya kulithibitisha neno Neno la Mungu linapotoka kwake au kwa kinywa cha nabii wake huwa haliendi bure naposema nabii hapa namiaanisha mtu anayesema kwa niaba ya Mungu yaani walimu, wachungaji, wainjilisti manabii na mitume, watmishi wote halali ambao wanazungumza kwa niaba ya Mungu wanapolisema neno lake halitekwenda bure litazaa matunda

 

Isaya 55:10-11 “Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.”

 

Kwa hiyo Mungu hulithibitisha neno lake kwa ishara  na miujiza, watu wanapotoka kwenda kulitangaza neno lake Mungu hufanya ishara na miujiza kwa kusudi la kulithibitisha neno lake ili watu wapate kusadiki ona 

 

Marko 16L17-20 “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu. Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]

 

Matendo 14:3 “                Basi wakakaa huko wakati mwingi, wakinena kwa ushujaa katika Bwana, aliyelishuhudia neno la neema yake, akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao.”

 

Waebrania 2:3-4 “Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki, sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia; Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.”

 

Kwa hiyo tunaona wazi kuwa Mungu hufanya ishara na miujiza kwa kusudi la kulithibitisha neno lake lengo kuu likiwa watu wapate kusadiki kuamini, waokolewe wawekwe huru, waponye, wajengeke wakue katika Imani wakiamni kuwa yuko Mungu

 

5.       Ili watu wapate kumuamini – Kusudi kubwa na la juu Zaidi la Mungu kufanya ishara na miujiza ni ili watu wapate kumuamini wakubali kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, wamwamini yeye ili wapate wokovu wamjue Mungu na Yesu Kristo aliyemtuma

 

 Yohana 20: 30-31 “Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.”       

Kusudi kubwa na la juu kabisa la ishara na miujiza ni ili watu wamamwini Mungu na wapate kuokolewa wamwamini Yesu Kuwa ni Bwana na mwokozi ili waokolewe, na wayahudi wapate kujua kuwa Yesu ndiye Masihi mwana wa Mungu aliye hai kwa hiyo kila muujiza alioufanya Yesu pamoja na maneno yake na matendo yake hitimisho lake ni ili watu wapate kumwamini kuwa yeye ni mwana wa mungu na ndiye njia na kweli na uzima

Yohana 2:11 “Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.”

               

Yohana 2:23Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizozifanya.”

Msipoona ishara na maajabu hamtaaamini kabisa.

Baada ya kuwa tumejifunza na kupata ufahamu kuhusu kusudi kuu la Isara na miujiza sasa swali kubwa la Msingi ni kwanini Bwana Yesu alitoa maonyo kwa watu waliokuwa tu wanataka kusaidiwa na kupata miujiza yao?

Yohana 4: 45-48 “Basi alipotoka Galilaya, Wagalilaya walimpokea; kwa kuwa wameyaona mambo yote aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu; maana hao nao waliiendea sikukuu.  Basi alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja ambaye mwanawe hawezi huko Kapernaumu. Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Uyahudi mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa kufani. Basi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa?”

Kimsingi sio kuwa Yesu alikuwa anazungumza na diwani pekee hapana Yesu alikuwa anazungumza na diwani na watu wote waliokuwa wamemkusanyikia mioyoni mwao wakiwa wanataka kuponywa na kuona ishara na miujiza aliyokuwa akiifanya hata kabla hawajamuamini, yaani kismingi watu walikuwa wana hamu na shauku ya kuona miujiza na ishara kuliko hata mwenye kufanya hizo sihara na miujiza, Yesu aliwakemea maalumu kwaajili yao, Hakumaanisha kuwa ishara na maajabu ni jambo baya kwao hapana lakini kuna kitu cha ziada Zaidi ya muujiza nah ii sio mara ya kwanza Yesu kutoa maonyo haya  ona

Yohana 6:25-29 “Hata walipomwona ng'ambo ya bahari, walimwambia, Rabi, wewe umekuja lini hapa? Yesu akawajibu, akasema, Amin, amin, nawaambieni, Ninyi mnanitafuta, si kwa sababu mliona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba. Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu. Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye.”

Nadhani sasa tunaweza kuona katika moja ya kemeo la Yesu kwamba watu walimfuata kwa sababu tu waliziona ishara na jambo hilo liko wazi Yohana 6:1-2 “Baada ya hayo Yesu alikwenda zake ng'ambo ya Bahari ya Galilaya, nayo ndiyo ya Tiberia. Na mkutano mkuu wakamfuata, kwa sababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa.”

Kwa hiyo hoja ya Yesu Kristo ina umuhimu na msingi sana hususani katiika nyakati za leo, kuna watu leo ambao wameacha kumtafuta Mungu na mafundisho sahihi na badala yake wanatafuta ishara na miujiza , wanashindwa hata kuamini injili nyepesi tu ya wokovu  na kumjua Mungu wa kweli badala yake wanatafuta ishara na miujiza hii inadhoofisha sana nafasi ya kanisa kuwahudumia na kupata nafasi ya kuwajengea Imani sahihi, tumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaotafuta maombezi kila wakati, wakristo wamedumaa na hawafikii ngazi ya kukomaa na kukua kiroho ili wao nao wawe na karama za Rohoni na kuwahudumia wengine badala yake wanahangaika huko na huko kutafuta maombizi kila likija wimbi moja na lingine, Yesu mwenyewe alikuwa anaonya hapa kwamba Imani hii ya kutaka kuhudumiwa tu kwa ishara na miujiza japo hiana ubaya lakini haitoshi kuwafanya watu wawe na imani ya kweli, Ishara na miujiza ni mwanzo tu wa swala zima la Imani ili tujenge Imani yetu kwa mtenda miujiza ambaye ni Bwana Yesu, onyo la Yesu ni kwa watu wote Msipoona na sio usipoona kwa hiyo kila mmoja wetu anakumbusha kuwa ishara huwa ainatuongoza katika jambo moja kubwa na la muhimu sana ambalo ni Yesu  

Jambo kubwa la msingi.

Ni muhimu kufahamu kuwa hakuna watu ambao wamewahi kushuhudia miujiza mikubwa na utendaji mkubwa wa Mungu kama wana wa Israel hivyo neno la Mungu linalalamika kuwa hawakuamini na hatimaye wengi waliangamizwa jangwani

 1Wakorintho 10:1-5 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; wote wakala chakula kile kile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.”

Wana wa Israel Jangwani waliona muujiza mmoja baada ya muujiza mwingine Makusudi makubwa ya Mungu ni ili waoa wamuamini, wamtukuze, wamuheshimu na kumuabudu, watambue ya kuwa yeye ndiye anayemiliki, wamuamini yeye na neno lake na hatimaye waweze kuwa na badiliko la ndani linalotokana na kuamini, lakini badala yake hawakuamini, walinungunika roho zao hazikufanyika imara hawakumwamini na hivyo Mungu alichukizwa nao

Waebrania 3:14-19 “Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho; hapo inenwapo, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha. Maana ni akina nani waliokasirisha, waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa? Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa? Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale walioasi? Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao.”

Kristo Yesu alikuwa anataka kuwaepusha wana wa Israel na jambo kama hili, fundisho lake ni kwa watu wote waaminio na hata wale ambao bado, muhimu tu kama kwetu sote Ishara na miujiza ikatuongoza katika kumtii Mungu na kumuheshimu, Yesu anataka tmuamini yeye hata tuspoona ishara na miujiza, Imani sahihi wakati wote hailazimishi Mungu atende kila tunataka inalazimisha mioyo yetu iamini katika Mungu katika namna ya iliyopitiliza na hiki ndicho Mungu anachokitaka

-          Ayubu 19:25-26 “Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi. Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu;”  

 

-          Daniel 3:14-18 “Nebukadreza akajibu, akawaambia, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hammtumikii mungu wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha?      Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu? Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”        

Hitimisho:

Lazima ufikie wakati Imani yetu iwe kwamba Mungu ni Mungu tu na atabaki kuwa Mungu na kwamba lazima aonyeshe miujiza yake, na tunapaswa kumuamini iwe kuna muuiiza au hakuna muujiza, iwe tuna kazi au hatuna kazi, iwe tumeponywa au hatujaponywa, iwe amaejibu maombi aua amekataa, iwe amatuponya au hajatuponya iwe tumeolewa au hatujaolewa, iwe tumechumbiwa au hatujachumbiwa, iwe tumepata au tumekosa, iwe tumefaulu au tumefeli, iwe kuna raha au kuna shida, tuwe tunapata mema au mabaya tunamwamini Mungu hata pasipo ishara na maajabu tunamwamini Mungu kuwa yeye ndiye anayetawala kila jambo katika maisha yetu na tunaendelea kumuheshimu na kumpa utukufu

Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!.



Jumatatu, 10 Julai 2023

Umuhimu wa kurudisha Shukrani wakati wa mavuno !


Mambo ya walawi 23:9-11. “Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu;  naye atautikisa mganda mbele za BWANA ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya Sabato kuhani atautikisa.”


Utangulizi:

Leo ni ni jumapili ya muhimu sana katika maisha yetu, kwa sababu ni siku ya Bwana ambayo ni maalumu kwa kumpa Bwana sadaka ya shukurani ni wakati wa kumshukuru Mungu kwa matendo yake makubwa na miujiza yake mikubwa mingi anayotufanyia ikiwa ni pamoja na kutupatia chakula mashambani mwetu.

Mungu alikuwa amewaelekeza watu wake kwamba walete sadaka ya shukurani, ambayo ingekuwa sababu ya Baraka kubwa sana kwao sadaka hii kwa lugha ya kiibrania iliitwa “BIKKURIM” kimsingi sadaka hii BIKKURIM maana yake waebrania waliita MBEGU YA MAMBO YAJAYO na sadaka hii ilijulikana kama MALIMBUKO.  Sadaka hii ilikuwa inaashiria kuwa mambo mazuri Zaidi yanakuja kama ukimshukuru Mungu, kwa hiyo walipolima mazao yao kabla hawajaanza kuvuna wao wala kula au walipokuwa wamevuna na kabla hawajaanza kutumia walichukua kiasi kulingana na ukarimu wa moyo wa mtu na wakakileta Hekaluni, ambako siku ya jumapili kuhani alipaswa kuiinua na kuitikisa na kuiombea na hapo mkulima huyu angeondoka kwa Imani kuwa Mungu atambariki tena.

Kwa nini Mungu aliagiza watu wamtolee shukurani ya mavuno? Kwa sababu mwanadamu alipewa kila kitu na Mungu ikiwemo mbegu, na ni Mungu ndiye anayefanya kazi ya kuziongeza, kwa hiyo mbegu sio zetu ni mali ya Mungu na chakula sio chetu ni mali ya Mungu na hivyo katika ibada ya shukurani tunamrudishia Mungu vile vinavyotoka kwake kwa hiyari yetu wenyewe

1Nyakati 29:9-14 “9. Ndipo hao watu wakafurahi, kwa sababu wametoa kwa hiari yao wenyewe, kwa sababu kwa ukamilifu wa moyo, kwa hiari yao wenyewe, wamemtolea Bwana; mfalme Daudi naye akafurahi kwa furaha kuu. 10. Kwa hiyo Daudi akamhimidi Bwana, mbele ya mkutano wote; naye Daudi akasema, Uhimidiwe, Ee Bwana, Mungu wa Israeli baba yetu, milele na milele. 11. Ee Bwana, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na kushinda, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee Bwana, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.  12. Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote. 13. Basi sasa, Mungu wetu, twakushukuru na kulisifu jina lako tukufu. 14. Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.” 

Kwa hiyo unapofika wakati wa kumtolea Mungu, tusifikiri kuwa sasa wachungaji wanatuchosha sasa utoaji umezidi hapana wakati wa kutoa ni wakati wa kupanda, ni wakati wa kurudhisha mbegu kwa Mungu na Mungu anapoipokea huizidisha Mungu hupima tu mioyo yetu na kutaka kuona shukurani zetu, Ndio maana wakati wa Daudi watu walipotoa yeye alikuwa na ujuzi kuwa vitu vyote vinatoka kwa Mungu na kuwa tunarudisha tu kwa mwenyewe  kwa sababu ya ukarimu wake mkuu. Tutajifunza somo hili umuhimu wa kurudisha shukurani wakati wa mavuno kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:- 

·         Sadaka ya Mavuno

·         Umuhimu wa kurudisha shukurani.

·         Jinsi ya kutoa sadaka ya shukurani. 


Sadaka ya mavuno.

Ni shukurani inayotolewa na watu waliomuamini Mungu, kwaajili ya kumshukuru Mungu kutokana na uwezo wake wa kuzizidisha mbegu za mazao alizotubarikia, Nyakati za Biblia kila mtu alimtolea Mungu kwa kadiri ya neema aliyopewa na Mungu, Jamii ya wafugaji walimtolea Mungu katika mifugo yao na jamii ya wakulima walimtolea Mungu kutoka katika mazao yao unaweza kuona 

 Mwanzo 4:3-4 “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake;”

Kwa hiyo wafugaji wlitoa mzao wa kwanza na wakulima walitoa malimbuko yaani sehemu ya kwanza nay a muhimu ya mazao waliyopewa na Mungu, kwanini kwa sababu wanadamu hatuna uwezo wa kuzidisha wanyama wetu wala hatuna uwezo wa kuzidisha mazao yetu, muujiza huu hufanywa na Mungu kwa hiyo tunapokuwa na sadaka ya mavuno maana yake nini tunawapa watu nafasi au siku maalumu ambayo watakuja kumshukuru Mungu kwa muujiza wake wa kuwapa mazao na swala hili linakuwa ni akiba kwa Mungu kwaajili ya kuwakumbuka tena BIKKURIM yaani malimbuko au mbegu ya mambio yajayo , kazi ya mwanadamu inaweza kuwa kupanda au hata kumwagilia lakini mwenye kukuza na kuzidisha ni Mungu ona 

1Wakorintho 3:6-7 “Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.” 

Unaona kwa hiyo siku ya mavuno ni siku ya kumshukuru yeye mwenye kukuza, huyu akuzaye ndiye wa muhimu sana yaani yeye mwenye kutuzidishia, kwa msingi huo tunapozungumzia sadaka ya mavuno tunazungumzia siku ya wakulima kumshukuru Mungu, Ni siku ya kuonyesha kuwa tunatambua mchango wa Mungu katika hiki tulichokipata wakati huu wa mavuno au kikiwa bado kiko shambani na kumshukuru Mungu kuna Baraka kubwa sana kama tunavyoweza kujifunza katika kipengele kifuatacho:- 

Umuhimu wa kurudisha shukurani.

1.       Kuna nguvu ya ufufuo na urejesho katika shukurani

 

Tunapomshukuru Mungu, kwa maneno yetu na sadaka zetu, tunatambua umuhimu wa utebndaji wake katika maisha yetu na Mungu hufufua au kurejesha kile tunachompa sio hivyo tu kila fursa ambayo inaonekana kufa katika maisha yetu inahuishwa kwa upya 

 

Yohana 11:41-44 “Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.”

Yesu alimshukuru Mungu tu na Lazaro akafufuka kutoka kwa wafu, hii maana yake tunapomshukuru Mungu, yeye anafufua firsa zote zilizokufa katika maisha yetu.

 

2.       Shukurani inakupa nguvu ya kuwashinda maadui.

 

Daudi alikuwa ni mfalme na Jemadari mpiganaji katika vita za aina mbalimbali na hajawahi kushindwa vita hata moja, moja ya siri kubwa ya ushindi wake dhidi ya maadui zake ni pamoja na kuwa na tabia ya kushukuru, inasemekana Daudi alikuwa na tabia ya kumshukuru Mungu mara saba kwa siku Zaburi 119:164 “Mara saba kila siku nakusifu, Kwa sababu ya hukumu za haki yakokutokana na tabia yake hii Mungu alimuahidi Daudi kuwa atampigania dhidi ya maadui zake

 

Zaburi 89:20-24 “Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu. Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake, Na mkono wangu utamtia nguvu. Adui hatamwonea, Wala mwana wa uovu hatamtesa. Bali nitawaponda watesi wake mbele yake, Nitawapiga wanaomchukia. Uaminifu wangu na fadhili zangu atakuwa nazo, Na kwa jina langu pembe yake itatukuka

 

3.       Shukurani inaleta uponyaji mkamilifu.

 

Tunapomshukuru Mungu tunaruhusu uponyaji wa Mungu katika maeneo mbalimbali ya maisha yetu Yesu aliwaponya wakoma kumi katika Luka 17:11-19 jambo la kushangaza wakati wote wameambiwa wakajionyesha kwa makuhani njiani walipona lakini ni mmoja tu aliyerudi kutoa shukurani na aliporejea Yesu alimwambia kuwa Imani yako imakuponya, uponyaji huu ni uponyaji mkamilifu sio tu wa magonjwa bali na uchumi wetu tunapomshukuru Mungu tunapata uponyaji mkamilifu katika maeneo yetu yote

 

Luka 17:11-19 “Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya. Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali, wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika. Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu; akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria. Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu? Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.”

 

4.       Unapomshukuru Mungu unajipatia kibali Zaidi kwa Mungu.

 

Sadaka ya shukurani kwa mavuno, au wanyama, au kwa maneno au kwa fedha ina nguvu ya kutufungulia kibali kwa Bwana Mungu wetu hasa inapoletwa kwa moyo wa kudamiria na usio na manung’uniko, Mungu anapokukubali anasababisha mambo yako yanyooke, anasababisha ukubalike kila unakokwenda na kufanikiwa sana Neno lake limeagiza kumfanyi ayeye shukurani ili atupe kibali ona

 

Mambo ya Walawi 22:29 “Tena mtakapomchinjia BWANA dhabihu ya shukrani, mtamchinja ili mpate kukubaliwa.”

 

5.       Maandiko yameamuru Kushukuru

 

Kama mwanafunzi wa Yesu Kristo na mfuatiliaji wa neno la Mungu na watu tunaotafuta kuyafanya mapenzi ya Mungu utaweza kugundua kuwa unaposoma neno la Mungu utagundua kuwa Kushukuru ni agizo la kibiblia na ni mapenzi ya Mungu hasa ona 1Wathesalonike 5:18 “shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu

 

Zaburi 136:1-26 “Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyefanya mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawaua wafalme mashuhuri; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Sihoni, mfalme wa Waamori; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Na Ogu, mfalme wa Bashani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Urithi wa Israeli mtumishi wake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Kila chenye mwili akipa chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.”

Jinsi ya kutoa sadaka ya shukurani:

-          Andaa sadaka yako ya Mavuno ambayo unataka kuitoa hii ni tofauti na zaka, unaweza kuchukua kiasi unachotaka kulinga na neema ya Mungu aliyokupatia, unaweza kuibadili sadaka yako kuwa fedha hakuna ubaya na unaweza kuitoa kama ilivyo pia hakuna ubaya.

-          Ombea sadaka yako weka dua na maombi ambayo unataka Mungu akufanyie Zaidi kwa mwaka wa mavuno unaokuja

-          Iweke sadaka yako katika madhabahu unayopata neno la Mungu na unapoabudu

-          Mchungaji, kuhani na mashemasi wa kanisa husika watakapokuwa wnahitimisha ibada ya mavuno wataweka mikono juu ya sadaka hizo au wataziinua mbele za Mungu na kutamka Baraka kwaajili nya sadaka hizona kwaajili ya watu waliotoa


Na. Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!



Jumamosi, 1 Julai 2023

Kufunguliwa mlango wa kufaa sana


1Wakorintho 16:7-9 “Maana sipendi kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu nataraji kukaa kwenu muda kidogo, Bwana akinijalia. Lakini nitakaa Efeso hata Pentekoste; kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao.”


Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa katika maisha yetu ya kila siku duniani, hatupaswi kuwa na huzuni pale tunapoona jambo moja katika maisha yetu limekwama, na ukajaribu na lingine likakwama, na lingine likakwama, hii haimaanishi kuwa unatakiwa kukata tamaa, na kama ulikuwa unamuomba Mungu au wewe ni mtu wa Mungu acha kufikiri kuwa ndio basi, Mungu katika mpango wake ameweka majira na nyakati mbalimbali kwa makusudi maalumu wakati mwingine tusiyoajua au tutakayoyajua baadaye kwa manufaa yetu

Muhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu

Kwa msingi huo kila changamoto unayoipitia katika maisha yako kumbuka kuwa wewe sio wa kwanza, wako na wenzako au na wengine waliopitia, alieleza dada mkoja ambaye aliwahi kufungwa gerezani kwa kosa la kusingiziwa na akaa gerezani mwaka mmoja tena akiwa ananyonyesha anasema kule gerezani hali aliyoiona alimsamehe hata mtu aliyemfikisha gerezani, kwani alikutana na watu wenye changamoto kubwa kuliko zake na waliofungwa miaka mingi Zaidi kuliko yake na walisingiziwa makossa makubwa Zaidi na kudhulumiwa hata kuliko yeye, Maandiko yamejaa mifano ya watu kadhaa wa kadhaa katika maandiko ambao walipitia changamoto za aina mbalimbali wengine wakisingiziwa n ahata kufungwa gerezani lakini hatimaye walitoka au Mungu alitafuta njia ya kuwatoa huko, Mungu atakutoa na wewe vilevile Haleluyaaa! Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-

·         Kufunguliwa mlango wa kufaa sana

·         Mifano ya watu waliofunguliwa milango ya kufaa

·         Jinsi ya kufunguliwa mlango wa kufaa

Kufunguliwa mlango wa kufaa sana

1Wakorintho 16:7-9 “Maana sipendi kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu nataraji kukaa kwenu muda kidogo, Bwana akinijalia. Lakini nitakaa Efeso hata Pentekoste; kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao.”

Paulo mtume anafunua mpango wake uliokuwa moyoni mwake kwaajili ya Kanisa lililokuwako Korintho, anaelezea mpango wake kuwa ilikuwa apate nafasi ya kwenda Korintho na kukaa nao kwa muda wa kutosha hususani wakati wa baridi, hata hivyo vilevile alikuwa na makusudi ya kukaa Efeso mpaka wakati wa Pentekoste, lakini hata hivyo ilikuwa ngumu pia kuwaaachaWaefeso kwa sababu huko alikuwa amefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, ni kwa jinsi gani Paulo anaelezea kuchelewa kwenda Korintho na kuendelea kubaki Efeso sababu kubwa ni kuwa amefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana !

Paulo anatumia mfano wa mlango akimaanisha kuwa injili yake imepata kibali na watu wa Efeso wanalipokea neno la Mungu kwa kiwango kikubwa sana na cha hali ya juu , Kila wakati Paulo mtume alipopata nafasi na kibali cha kuihubiri injili mahali na mahali hapo pakawa na moyo mkubwa wa kuikubali injili aliitqa swala hilo kufunguliwa mlango ona

2Wakorintho 2:12 “Basi nilipofika Troa kwa ajili ya Injili ya Kristo, nikafunguliwa mlango katika Bwana”,

Hii ni kwa sababu ziko sehemu au maeneo mengine ambayo kuipokea kwao injili kulikuwa ni kwa ugumu sana na wakati mwingine kwa upinzani mkubwa sana, iko miji ambayo Paulo alitamani sana aihubiri injili lakini shetani akiwatumia watu alipinga vikali sana na huduma ya Paulo mtume, wakati mwingine alikimbia usiku kutoka mji mmoja kwenda mji mwingine

Matendo 17:1-10 “Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi. Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu, akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo. Wengine miongoni mwao wakaamini, wakashikamana na Paulo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye cheo si wachache. Na Wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji; na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako, na Yasoni amewakaribisha; na hawa wote wanatenda mambo yaliyo kinyume cha amri za Kaisari, wakisema na kwamba yupo mfalme mwingine, aitwaye Yesu. Wakafadhaisha ule mkutano na wakubwa wa mji walipoyasikia hayo. Nao walipokwisha kumtoza dhamana Yasoni na wenziwe wakawaacha waende zao. Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi.”      

Kutokana na upinzani huu wa mara kwa mara dhidi ya injili, Paulo mtume aliwaomba wakristo wa makanisa ya miji mingine kuwa na maombi rasmi ya kumuombea ili kwamba afunguliwe mlangowa injili,

Wakolosai 4:2-3 “Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani; mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,”

Katika mji wa Efeso mambo yalikuwa ni tofauti sana na maeneo mengine, watu wa Efeso walipomuona Paulo mtume kwa mara ya kwanza na kumsikia katika sinagogi hata wayahudi wa Efeso walimtaka Paulo akae kwao siku nyingi Zaidi, Paulo alikuwa na safari ya kwenda Syria (Shamu) na hivyo aliwaahidi kuwa angerejea tena ona

Matendo 18:18-19 “Baada ya hayo Paulo akazidi kukaa huko siku nyingi, kisha akaagana na ndugu akaabiri kwenda Shamu; na Prisila na Akila wakaenda pamoja naye, alipokwisha kunyoa kichwa chake huko Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri. Wakafika Efeso, akawaacha huko. Yeye mwenyewe akaingia katika sinagogi, akahojiana na Wayahudi. Walipomtaka akae wakati mwingi zaidi, hakukubali;

Paulo aliporejea Efeso baadaye mlango mkubwa sana wa injili ulifunguka, watu walilipokea neno la Mungu kwa furaha kubwa sana pamoja na kuwa injili huwa inapingwa lakini Pale Efeso alipata neema ya kukaa muda mrefu zaidi na hivyo kuwa na kanisa imara sana, Katika mji huu Paulo alitumiwa na Mungu kwa miujiza mikubwa sana na kupita kawaida, watu wengi walikuja kwa Bwana na sio hivyo tu waliokuwa wachawi na waaguzi waliacha uchawi na kuchoma moto vifaa vyao vya kiroho na vitabu vyao vya thamani kubwa sana na kushikamana na Paulo

Matendo 19:8-11 “Akaingia ndani ya sinagogi, akanena kwa ushujaa kwa muda wa miezi mitatu, akihojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu. Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; basi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi, akahojiana na watu kila siku katika darasa ya mtu mmoja, jina lake Tirano. Mambo haya yakaendelea kwa muda wa miaka miwili, hata wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana, Wayahudi kwa Wayunani. Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida;”

Matendo 19:18-20 “Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao. Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote; wakafanya hesabu ya thamani yake, wakaona ya kwamba yapata fedha hamsini elfu. Hivyo ndivyo neno la Bwana lilivyozidi na kushinda kwa nguvu.”  

Ni kutokana na mafanikio makubwa sana Paulo mtume anaelezea kuwa katika huduma yake ambayo kimsingi ilikuwa na upinzani mkubwa sana anaona kuwa amefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana Pale Efeso licha ya kuwepo kwa upinzani wa hapa na pale, Muda alioutumia Pale Efeso ulimkosesha Fursa ya kwenda Korintho kwa kusudi la kuwaimarisha huko nako na ndipo alipowaandikia kuwa anatamani kuwa nao lakini alikuwa amefunguliwa mlango mkubwa sana wa kufaa japo kuna upinzani mdogo

1Wakorintho 16:7-9 “Maana sipendi kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu nataraji kukaa kwenu muda kidogo, Bwana akinijalia. Lakini nitakaa Efeso hata Pentekoste; kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao.”

Mifano ya watu waliofunguliwa milango ya kufaa

Mungu alimfungulia mtume Paulo mlango mkubwa wa kufaa sana kwaajili ya injili, kama tunavyoweza kuona katika maandiko kwamba Upinzani dhidi ya injili ulimkabili Paulo mtume kila mahali kiasi cha kuhatarisha maisha yake japo watu wengi walikuja kwa Bwana, Ni muhimu kufahamu kuwa sio katika huduma tu watu hufungiwa mlango, lakini hata katika maisha yetu ya kawaida kuna milango inaweza kufungwa yako mambo ambayo ungetamani yakae sawa lakini yamefungwa, ni huduma yako bado haijapata nafasi ya kutulia na kuwafikia wale ambao ulikuwa unawafikiri, ni  tumbo lako na uzao wako umefungwa hushiki mimba, au huwezi kumpa mwanamke mimba, biashara haijapata mpenyo unaokusudiwa, Hata hivyo haupaswi kukata tamaa, Neno la Mungu linatukumbusha kuwa katika kila jaribu Mungu huweka mlango wa kutokea

 1Wakorintho 10:13 “Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.”

·        Yusufu alipitia katika mitihani ya namna mbalimbali katika maisha yake hata kufungwa gerezani kwa kusingiziwa tu lakini hatimaye Mungu alimfungulia mlango na akawa mtu mkubwa sana katika incho ya Misri

-          Mwanzo 37:12-36 “Ndugu zake wakaenda kuchunga kondoo za baba yao huko Shekemu. Israeli akamwambia Yusufu, Je! Ndugu zako hawachungi kondoo katika Shekemu? Njoo, nikutume kwao. Akamwambia, Mimi hapa.  Akamwambia, Enenda, basi, ukaone kama ndugu zako hawajambo, na kundi nalo li salama, ukaniletee habari. Basi akampeleka kutoka bonde la Hebroni, akafika Shekemu. Mtu mmoja akamkuta, naye alikuwa anazunguka-zunguka katika nyika; yule mtu akamwuliza, akisema, Unatafuta nini? Akasema, Nawatafuta ndugu zangu; tafadhali uniambie mahali wanakochunga. Yule mtu akasema, Wametoka hapa, maana niliwasikia wakisema, Twendeni Dothani. Basi Yusufu akawafuata ndugu zake akawakuta huko Dothani. Wakamwona toka mbali, na kabla hajawakaribia, wakafanya shauri juu yake ili wamwue. Wakasemezana wao kwa wao, Tazama, yule bwana wa ndoto anakuja. Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake. Reubeni akasikia akamwokoa katika mikono yao, akasema, Tusimwue. Reubeni akawaambia, Msimwage damu; mtupeni katika birika hii iliyopo nyikani, wala msimguse; ili apate kumwokoa katika mikono yao, akamrudishe kwa baba yake. Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake, wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa, wakamtwaa wakamtupa katika birika; na hiyo birika ilikuwa tupu, hamna maji. Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane, wakisafiri kuvichukua mpaka Misri. Yuda akawaambia ndugu zake, Kwafaa nini kumwua ndugu yetu, na kuificha damu yake? Haya, na tumwuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu. Ndugu zake wakakubali. Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika birika, wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri. Akarudi Reubeni birikani, kumbe! Yusufu hayumo katika birika, akararua nguo zake. Akarudi kwa ndugu zake, akasema, Mtoto hayuko, nami niende wapi?  Wakaitwaa kanzu ya Yusufu, wakachinja mwana-mbuzi, na kuichovya kanzu katika damu. Wakaenda nayo ile kanzu ndefu, wakamletea baba yao, wakasema, Tumeona hii; basi, utambue kama kanzu hii ni ya mwanao, ama siyo. Akaitambua, akasema, Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa. Yakobo akararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni, na kumlilia mwanawe siku nyingi. Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia. Nao Wamidiani wakamwuza huko Misri, kwa Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari.”

·        Ayubu alipitia mitihani migumu sana kufiwa na watoto wote, kupoteza mali zake zote, kupata hasara ya mifugo yake yote na wafanyakazi wake wote waliuawa na kutekwa na kubakiwa na watoa taarifa tu, kama haitoshi yeye aliugua na kufilisika kwa kiwango kikubwa, hata hivyo Mungu alimfungulia mlango wa kufaa baadaye

-          Yakobo 5:10-11 “Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu. Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.”

Mpenzi haupaswi kukata tamaa na kudhani ya kuwa wewe una nuksi au balaa, kila changamoto unayoipitia kumbuka kuwa Mungu atafanya mlango wa kutokea, Mlango ambao Mungu atakufungulia utakuwa ni mkubwa na wa kufaa Zaidi, Mungu aliyewafungulia mlango watakatifu waliotutangulia na wale ambao wako leo na tnasikia shuhuda zao hatakosa kukufungulia mlango mkubwa wa kukufaa Zaidi wewe nawe katika maisha yako   

Jinsi ya kufunguliwa mlango wa kufaa

Ni muhimu kufahamu kuwa hata sasa Mungu anakuwazia mema, Paulo mtume hakukata tamaa kwa sababu ya magumu aliyokuwa akiyapitia, aliendelea kuhubiri injili, kila alikokuwa akikataliwa alikimbia katika mji mwingine na hatimaye kule Efeso Mungu alimfungulia mlango mkubwa wa kufaa Zaidi, ziko sababu nyingi kwako kwanini Mungu atakufungulia mlango

1.       Mungu tunayemwambudu na kumtumikia nidye mwenye funguo yeye anauwezo wa kufungua na hakuna wa kufunga na ana uwezo wa kufunga na hakuna afunguaye kwa msingi huo ni Mungu mwenyewe anayeweza kuingilia katika hali unayoipitia na kukufungulia mlango  na ni yeye anayeweza kukupa mlango uliofunguliwa mbele yako ona

 

Ufunuo 3:7-8 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye. Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.”

 

2.       Mungu amelipa Kanisa mamlaka ya kushangaza sana wewe kama mtu uliyemwamini Bwana Yesu wewe ni kanisa na Mungu amekupa uwezo na mamlaka ya kufungua lolote kiasi hata mbinguni likafunguliwa na una uwezo wa kufunga lolote nahata mbinguni likafungwa, kwa msingi huo katika kila jambo ambalo unahisi limefungwa unaweza kumuomba Mungu na akakufungulia mlango  ona

 

Mathayo 18:18 “Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.”

3.       Washirikishe wale unaowaamini katika maombi yako, kuna nguvu kubwa sana kama watu wawili au zaidi wakipatana na kuomba Mungu huwafanyia, kile walichokiomba, Mungu huwa kati kati ya watu Zaidi ya wawili au watatu wakiungana katika maombi, hiki ndicho alichosema Kristo ona

 

Mathayo 18:19-20 “Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.”        

 

Na ndio maana Paulo mtume alipoona changamoto zilizokuwa zinamkabili aliwaomba kanisa wamuombee neema ili kwamba wamuombee ili afunguliwe mlango

Wakolosai 4:2-3 “Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani; mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,”

Daniel alipopata changamoto kazini wakati wenye hekima walipotakiwa kutafasiri na kumkumbusha mfalme Nebukadreza kuhusu Ndoto aliyoiota akaisahau na kuwataka wamkumbushe kwanza kisha wamuelezee maana vinginevyo angewaua Daniel aliamua kumuomba Mungu na kuwashirikisha na wenzake na wakamuomba Mungu, shirikisha watu muhimu unaowaamini ombeni pamoja kuhusu changamoto inayokukabili na Bwana atakufungulia mlango mkubwa wa kufaa Zaidi.

Daniel 2:17-19 “Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake; ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli. Ndipo Danieli alipofunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku. Basi Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni.”


Bwana kupe neema na kukufungulia mlango mkubwa wa kufaa Zaidi katika kila jambo ambalo unakutana nalo katika maisha yako, Mungu ni mwema na ni mwingi wa huruma amejaa neema hakika hatakuacha ulie tu atakufungulia mlango wa kufaa na utafanikiwa sana katika maisha yako!

Na Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!


Jumanne, 27 Juni 2023

Jinsi ya kufanya agano la chumvi




Wakati wa kufanya agano la chumvi.

  1. Mizimu, mapepo, shetani na wachawi na waganga au makuhani wa kichawi huwaathiri watu katika maisha yao na kusababisha msongo wa mawazo, kwa kutumia nguvu za giza, kwa kutumia nguvu hizo za giza na za kichawi wanawasababishia watu kupoteza mwelekeom kuwa na bumbuwazi, kuteseka, kuelemewa, kuwa na uzito na kupata changamoto za kifedha na kiuchumi na changamoto nyinginezo nyingi.

 

Uchawi ni silaha ya giza inayotumiwa na wachawi kwa kusudi la kuharibu maisha ya watu wanaofanikiwa na kufanikiwa  katika mazingira mbalimbali, silaha hiyo ya giza ni silaha ya kiroho lakini matokoe yake hutokea katika hali halisi.kuteseka kwa watu waliorogwa au kuchawiwa kunategemeana na nguvu iliyotumika katika kunuiziwa nguvu za mashambulizi

Pepo watatafasiri uchawi na manuizo na kuyawasilisha kwa watu waliolengwa na kuwashambulia na matokeo yanaweza kutokea katika ulimwengu wa miili yao, mambo magumu na matukio ya ajabu huanza kutiokea katika maisha yao na njia pakee ya kuimarisha na kuleta ukombozi ni agano la chumvi

 

Ukombozi kupitia gano la chumvi ni rahisi sana kwa muonekano lakini una nguvu kubwa za ajabu sana, ukombozi huu una nguvu ya kuondoa kabisa maedhara ya nguvu zisizoonekana za kichawi na kuukausha au kuuondoa kabisa na kuondoa hali ya kushindwa kwa sababu zozote zile, kwa kufanya hivyo haimaanishi oia mkuwa tutaacha kabisa kuschughulikia nguvu za giza kwa namna za kawaida, lakini tutaendelea ili kuhakikisha kuwa tunaendelea kukua kiroho.

 

  1. Unafanya gano la Chumvi wakati gani?

 

Tunafanya agano la chumvi wakati tunapohisi kuwa kuna matukio ya vita za kiroho zilizohusisha nguvu za giza, ni kweli kwamba mtu aliyeokoka hawezi kushambuliwa na nguvu za giza kwa sababu imeandikwa hakuna ugaga wala uchawi juu ya Yakobo Hesabu 23:23  “Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!

 

Lakini kumbuka tuna mashambulizi kutoka kwa mamadui, tuko vitani, majeshi ya pepo yanatumwa kwetu kwa mauizo na sadaka za iana mbalimbali na kwa maelekezo ya aina mbalimbali kwa hiyi kuna kiwango cha mashambulizi ambayo tunakutana nayo wakati mwingine kwa asilimia 30 au 60 au 90 kwa hiyo wote kwa kiwango Fulani tunashambuliwa na nguvu za giza kulingana na kiwango za kuzaa kwetu matunda kumbuka mfano wa zile mbegu zilizoangukia kwenye udongo mzuri Marko 4:8 “Nyingine zikaanguka penye udongo ulio mzuri, zikazaa matunda, zikimea na kukua, na kuzaa, moja thelathini, moja sitini, na moja mia.” Kama ukuaji wetu wa kiroho unaweza kuzaa matunda kwa asilimia hizo zilizotajwa ni dhahiri na mashambulizia yanaweza kuwepo kutokana na kiwango kwa hiyo niia nyepesi ya kuondoa kiwango hicho cha mashambulizi ya nguvu za giza ni kwa kutumia ganano la chumvi  na ukifanya mara kwa mara unaziondoa kabisa katika mwili wako  tunaweza kujitibu kwa agano la chumvi mara unapohisi au kusikia changamoto hizi:-

 

-          Uchovu wa kimwili na kiroho

-          Kupoteza hamasa

-          Kupoteza uwezo wa kufikiri

-          Kuelemewa na mawazo

-          Hasira za kupita kawaida

-          Mgandamizo wa mawazo stresses

-          Aina yoyote ya ugonjwa na wakati wowote unapokuwa unahisi kuwa kuna uvamizi na hali isiyo ya kawaida katika mwili wako, uchumi wako, kazi yako, huduma yako na roho yako.

-          Lakini pia udhaifu wowowte wa kimwili, kiroho na kihisia ujue kuna mashambulizi ya mizimu, mapepo, wachawi na kadhalika basi unahitaji tiba ya agano la chumvi.

 

  1. Mambo unayohitaji kwaajili ya kutekeleza agano la chumvi

 

-          Utahitaji ndoo au beiseni

-          Utalijaza maji safi kwa asilimia 50% yaani nusu

-          Utahitaji chumvi yam awe kwa kiwango chochote kana huna ya mawe unaweza kutumia ya mezani lakini ya mezani uwezo wake utapungua kwa asilimia 30% ukilinganisha na ile ya mawe

-          Taulo la kujikaushia

-          Na sehemu ya kukanyajia

-           

  1. Jinsi ya kufanya ibada ya agano la chumvi.

 

1.       Weka maji kwenye ndoo yajae kwa asilimia 50% yaani nusu yake kwa kiwango tu cha kufunika enka za miguu

2.       Weka vijiko vidogo viwili vya chumvi ya mawe

3.       Omba kwa kumaanisha na kwa imani kwamba Mungu akuondolee nguvu zote za giza, pia omba maalumu kwaajili ya kuziharibu kabisa na kuzibomboa nguvu zote za mizimu, pepo, waganga na wachawi na kila manuizo yaliyofanywa kinyume nawe na kukuletea athari, omba maombi ni muhimu sana na yana uwezo mkubwa sana yanapofanyika sambaba na ibada hii ya ukombozi.

4.       Hakikisha umekaa sawa sawa na miguu yako hususani enka ziwe zimezama katika maji, miguu yako isigusane bali iwe mbalimbali kati ya sentimita 2-3 hii inasaidia kuodoa uchawi wote uliorogwa kwa nguvu za giza, kama miguu yako itagusana itakuwa kikwazo kwa ibada hii, 

5.       Hakikisha miguu inakaa kati ya dakika 10-15 na usizidishe zaidi ya dakika 15, ukizidisha nguvu za giza zinazotoka kwa njia ya miguu zinaweza kuingia mwilini mwako

6.       Wakati miguu yako inapokuwa katika maji yenye chumvi anza kuomba au kunuiza kwa jina la Yesu  Mungu au kuimba maombi

7.       Wote wenye pumzi wote waishio duniani wote wampendao  (Wamchao) Mungu na waseme fadhili zake ni za milele

8.       Wote wanaoeneza habari zake watangazao habari njema duniani kote na waseme fadhili zake ni za milele.

 

Kwa ufupi utaimba zaburi 118:1-14         

1. Haleluya. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.

2. Israeli na aseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.

3. Mlango wa Haruni na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.

4. Wamchao Bwana na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.

5. Katika shida yangu nalimwita Bwana; Bwana akanijibu akaniweka panapo nafasi.

6. Bwana yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

7. Bwana yuko upande wangu, msaidizi wangu, Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.

8. Ni heri kumkimbilia Bwana Kuliko kuwatumainia wanadamu.

 

9. Ni heri kumkimbilia Bwana. Kuliko kuwatumainia wakuu.

10. Mataifa yote walinizunguka; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

11. Walinizunguka, naam, walinizunguka; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

12. Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

13. Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini Bwana akanisaidia.

14. Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu.

 

Hitimisho:

Baada ya kumaliza maombi haya ya ukombozi kulinga nan a mahitaji yako unaweza kuanza kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake anaokupa na namna anavyokuzunguka

Utayamwaga maji yake chooni na kisha utasafisha ndoo na maji safi. Utakausha miguu yako vema kwa taulo na kisha utajipaka mafuta ya mzeituni na kuomba Mungu akupeleke kwenye kiwango kingine cha maswala mbalimbali uyatakayo. Ibada inaweza kufanyika pia kwa makusudi mbalimbali ambayo mengine hayajaainishwa katika somo hili mfano kuweka wakfu, kiongozi, kujilinda na cheo chako na kadhalika

Mwisho wa ibada hii.

Matokeo:

  1. Athari zote za nguvu za Giza na mashambulizi ya wachwi, waganga na mapepo na shetani zinaondoka
  2. Maji ya agano la chumvi yana nguvu kubwa sana yenyewe tu kunyonya nguvu zote za giza
  3. Nguvu za giza na magonjwa yote yanayoambatana na nguvu hizo yanaondoka na wakati mwingine maji yanaweza kuwa na rangi nyeusi kama ishara ya kuondoka kwa nguvu hizo, au yanaweza kuwa na uvuguvugu au yakawa na harufu mbaya hii ni shara ya vitu vibaya kuondoka mwilini mwako

 

KUMBUKA:  Somo hili lina uhusiano na huduma za kinabii, sio vizuri kufundisha au kulifanyia kazi kanisani ikiwa huamini katika huduma za kinabii

 

Na Rev. Innocent Samuel Kamote

 

Mkuu wa wajenzi mwenye hekima