Jumamosi, 3 Agosti 2024

Zikimbie tamaa za ujanani

2Timotheo 2:20-22 “Basi katika nyumba kubwa havimo vyombo vya dhahabu na fedha tu, bali na vya mti, na vya udongo; vingine vina heshima, vingine havina. Basi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hao, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema. Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.”



Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa asilimia 25 ya wanadamu waishio Duniani ni vijana, Idadi ya vijana duniani kwa sasa ni Bilioni 1.7, na asilimia 86 ya vijana hao wanaishi katika inchi zinazoendelea, Wastani wa umri wa vijana wanaoongezeka ni kati ya miaka 15-24 na wengi wao wako Afrika, Asia na Amerika ya kusini, kwa hiyo utaweza kuona kundi hili linakuwa na kuongezeka kwa kasi, aidha kundi la vijana ndio nguvu kazi kubwa ya jamii na kanisa kwa ujumla, Vijana ni kundi muhimu sana kwaajili ya jamii na kanisa la sasa na baadaye, Mungu amekuwa akiwahitaji vijana na amekuwa akiwatumia sana katika kazi yake kama inavyoonekana katika maandiko, ni ukweli uliowazi kibiblia kuwa wakati wa ujana ndio wakati muhimu sana wa kumcha Mungu na kumtumikia kuliko wakati mwingine wowote,

Muhubiri 12:1-7 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo. Kabla jua, na nuru, na mwezi, Na nyota, havijatiwa giza; Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;Siku ile walinzi wa nyumba watakapotetema; Hapo wenye nguvu watakapojiinamisha; Na wasagao kukoma kwa kuwa ni haba; Na hao wachunguliao madirishani kutiwa giza; Na milango kufungwa katika njia kuu; Sauti ya kinu itakapokuwa ni ndogo; Na mtu kusituka kwa sauti ya ndege; Nao binti za kuimba watapunguzwa; Naam, wataogopa kilichoinuka Na vitisho vitakuwapo njiani; Na mlozi utachanua maua; Na panzi atakuwa ni mzigo mzito; Na pilipili hoho itapasuka; Maana mtu aiendea nyumba yake ya milele, Nao waombolezao wazunguka njiani. Kabla haijakatika kamba ya fedha; Au kuvunjwa bakuli la dhahabu; Au mtungi kuvunjika kisimani; Au gurudumu kuvunjika birikani; Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.”         

Pamoja na ushauri mzuri wa kimaandiko kwa vijana kutoa muda wao wa ujana katika kumtumikia Mungu, kundi hili linamashambulizi makali sana kutoka kwa Shetani, Dunia na miili yao, kimsingi ni kundi ambalo linashambuliwa kwa kiwango kikubwa kupitia tamaa, kwa hiyo hata wanapojitoa katika kumtumikia Mungu bado watazingwa na tamaa za ujanani ambazo Paulo mtume anamsihi Timotheo kuhakikisha kuwa anazikimbia tamaa hizo, Kwa msingi huo leo tutachukua Muda wa kutosha kujifunza jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo za ujanani kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-


·         Maana ya tamaa za ujanani.

·         Athari  ya tamaa za ujanani.

·         Jinsi ya kukimbia tamaa za ujanani


Maana ya tamaa za ujanani:

2Timotheo 2:22 “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.”

Neno tamaa za ujanani katika Biblia ya kiingereza linasomeka Youthful lusts au evil desires of Youth yaani tamaa za ujanani au tamaa mbaya za ujanani katika Biblia ya kiyunani neno tamaa linalotumika hapo ni Epithumia ambalo kwa kiingereza tafasiri yake ni Longing for what is forbidden au concupiscence ambalo tafasiri yake strong sexual desire, nymphomania, abnormally intense sexual desire, the tendence of human to sin, tamaa ya kutenda dhambi.

Wakolosai 3:5-6 “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.”

kwa hiyo tafasiri yake ni tamaa ya kutaka kufanya kitu kilichokatazwa na Mungu, au tamaa kali ya ngono, au tamaa isiyokuwa ya kawaida inayotaka utamani ngono, kiufupi ni tamaa kali na inaweza kuwa ya ngono au ya mambo mengine ambayo huwasonga zaidi vijana, tamaa hizi za ujanani zinaweza kuchukua umri kati ya miaka 15-70 hivi kwa wanawake na 15-80 hivi kwa wanaume. Kwa msingi huo utaweza kuona ni katika umri ule ule Muhimu ambao Mungu anataka kumtumia mtu, kwa hiyo ili zisiingiliane na mapenzi ya Mungu, au kuharibu mwenendo wa mtu wa Mungu, Paulo anamuasa Timotheo kujihami nazo tamaa hizo tunaweza kuzianisha kama ifuatavyo:-

1.       Tamaa ya mwili – Wakati wa ujana, kipindi ambacho mwili wa kijana unajijenga na kuzalisha vichocheo vingi sana, mahitaji ya kingono pamoja na mihemko mingine kwa vijana huwa yanawaka kwa kiwango kikubwa sana na hayatajali kuwa umeokoa, unafunga sana na kuomba sana na kuhudhuria sana ibada wakati wote unaweza kujikuta unamtumikia Mungu lakini nguvu ya mwili, kuhitaji na kutamani ngono inakuwa iko pale pale, mihemko na kushindwa kujitawala kihisia kunakuwepo vilevile, jambo hili limesumbua sana vijana wengi mpaka wanachanganyikiwa, vijana wengi wanajichua, na wengi wanaangalia picha za ngono, wakitafuta kwa kila namna kutimiza kiu yao ya kingono ambayo inaonekana kama haina kitoshelezo taabu hii wanayoipitia vijana ni kama watumishi wengi wa Mungu hawaijui au hawaijali, na wanachojua wao ni kusubiri wasikie wamefanya uasherati na kuwatenga na kuwaharibu zaidi, na wala kwa kufanya hivyo hawawezi kujiondoa katika kifungo hicho cha tamaa, kuwaka kwa hasira, wivu, husuda, ulafi, uvivu na kadhalika kunawapelekesha sana kundi hilo, kwa sababu vichocheo katika miili yao vinakuwa bado havijapata utengemavu wa utulivu, kwa hiyo kundi hili linateseka sana bila kupata njia ya kujiokoa katika hilo

 

1Petro 2:9-11 “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.”

 

Wagalatia 5:16-21 “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.”              

 

1Wathesalonike 4:3-4 “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;”

 

Vijana wanateseka katika eneo hili, Watumishi wa Mungu wanapokwena katika vyuo vya Biblia huwa tunawafundisha somo la kufanya UTAFITI, Research, Somo hili linaelekeza kuwa kazi ya Mchungaji sio kuchunga na kuhubiri tu, lakini lazima ufanye utafiti, na pia tunawafundisha  somo la Saikolojia (Pyschology) ili kwa pamoja wafanye utafiti wa kisayansi kuhusu tabia, jamani si tunashughulika na tabia za watu, wakati mwingine tufanye utafiti kwanini kundi hili la watu au kabila hii, au wanaume au wanawake au watoto wana tabia ya ina Fulani ili tujue namna ya kuwasaidia kila mmoja sawa na uhitaji wake na kwa njia za kiroho tutaweza kuwasaidia na kutatua changamoto zao na nyingine zinachukua muda mrefu, usiwe kama mjinga kila kitu unakimbilia kukitangaza na kutenga tu, Fahamu Paulo alijua kuwa ziko tamaa za ujanani, na alikuwa akimuonya Timotheo azikimbie kwa hiyo tabia hizo ni za kimaumbile na kuwa rohoni haimaanishi uko nje ya.

 

2.       Tamaa ya mali na vitu – Changamoto nyingine ya tamaa ya vijana ni mafanikio ya haraka haraka, jambo ambalo linawaletea Matamanio ya kuwa na vitu vya anasa, utajiri wa haraka na mali za dunia, jambo hili limesababisha mtego mkubwa kwa vijana na maumivu katika mioyo yao na kukata tamaa au kutoka nje ya neema ya Mungu pale wanapokosa, kuwa na mali na utajiri  na Fedha sio dhambi kama utapata katika njia halali, lakini wakati wa ujana spidi ya uhitaji wa mafanikio ya haraka hara huwa kubwa kiasi ambacho unaweza kuingia mtegoni hilo ndilo ambalo maandiko yanaonya.

 

1Timotheo 6:9-10 “Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.”

 

3.       Tamaa ya mashindano – Changamoto nyingine katika tamaa za ujana ni kutaka kujulikana ni tamaa ya kujifurahisha, ni tamaa ya ubinafsi, na kutaka kushindana na wengine na kuwashinda ikiwezekana kwa njia yoyote, kugombea ukubwa, kugombea nafasi, kuoneana wivu, kuwa na uadui, uchonganishi, kutafuta cheo, kumchukia mtu mwenye kila kitu, na kadhalika.

 

Wafilipi 2:3-4 “Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.”

 

4.       Tamaa za Dunia – Ni changamoto ya kutaka kujihusisha na dunia na anasa zake, katika njia ambayo taratibu inaweza kumuondoa mtu katika kumcha Mungu, tunataka kujihusisha na burudani zisizo za kiroho, vyama visivyo vya kiroho, kusheherekea vitu kupita kiasi, tamaa ya kunywa pombe, kudhamiria kuchukia watu, ushirikina, mawasiliano na pepo, kujiunga na vyama vya kishetani, uangaliaji wa picha za ngono, kujifurahisha kwa sinema za ngono, majarida ya ngono, picha za maumbile yenye kuvutia, na anasa nyinginezo

 

1Yohana 2:15-17 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.”                                             

Kwa hiyo vijana wawapo duniani, wawapo ulimwenguni, au tuwapo duniani, au tuwapo ulimwenguni, pamoja na ufahamu mzuri, na kuelimishwa vema njia ya Bwana, na pamoja na wokovu, na kumpenda Mungu, na kumshinda shetani adui mmojawapo mkubwa tunayekabiliana naye ni mambo ya mwili na tamaa za ujanani, hizi ni muhimu vijana wakajua namna wanavyoweza kutiisha miili yao na kujinasua kutoka katika mtego huu mkubwa kwani tamaa hizi zina athari zake.

Athari ya tamaa za ujanani

Tamaa za ujanani zinaathari kubwa sana kiroho, zinaunda tabia na mfumo ambao unaanza kumuweka mtu mbali na Mungu taratibu bila kuelewa na hatimaye mwisho kumnyima mtu huyo nafasi ya uzima wa milele ambao Mungu ameukusudia, kimsingi Mungu anapokuokoa hakusudii hata kidogo kwamba uukose uzima wa milele, lakini kupitia tamaa za ujanani, dunia na shetani taratibu tamaa hizi zinafanya kazi ya wewe mwenyewe kujiondoa katika mpango huo wa Mungu, kwa kudumaa kiroho, kwa kupoteza uadilifu, kwa kukukosesha Amani, kwa kuharibu uhusiano wako na Mungu na hatimaye kukuharibia mpango wa Mungu wa umilele

1.       Kutengana na Mungu – tamaa za ujanani zikitimizwa mara moja ainaanza kuharibu ukaribu wetu na Mungu, zinavunja uhusiano wetu na Mungu, kwa hiyo hata kama wanadamu hawatuoni lakini sisi wenyewe tunapoteza urafiki na uhusiano wa karibu na Mungu na kuwa adui wa Mungu, jambo ambalo litapunguza au kuondoa kabisa neema za Mungu katika maisha yetu na mwili unapata nguvu ya kututawala

 

Yakobo 4:4-6 “Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu. Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.”

 

Mwanzo 39:7-9 “Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami. Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?

               

2.       Kudumaa kiroho – Tamaa za ujanani huchukua muda mrefu sana kupambana na uwezo wa kijana kukua kiroho na kumfuata Yesu kwa ukamilifu, na matokeo yake inasababisha udumavu wa Kiroho, na badala ya kukua kiroho Mwili (Sarx) yaani ile asili ya mwanadamu na tamaa mbaya inakuwa na nguvu kuliko utawala wa kiroho na hivyo kuathiri tabia na mwenendo wa Mkristo, anakuwa wa mwilini na anakosa makuzi ya kiroho. Mtu wa mwilini anashindana na mtu wa rohoni na kusababisha udumavu wa kiroho.

 

1Wakorintho 3:1-3 “Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?”

 

Waebrania 5:11-14 “Ambaye tuna maneno mengi ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia. Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga.Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.”

 

Luka 8:14 “Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote.”

 

3.       Kukosa Amani – Tamaa za ujanani zinapoyatawala maisha yetu hutujengea mashaka, wasiwasi na woga na wakati mwingine kupoteza Amani,  na kusinyaa kwa Imani yetu katika wokovu na Mungu,  Japo Mungu ni mkuu  na anatujua umbo letu. Lakini tunaweza kuwa na watu ambao wanaonekana kuwa wako vizuri, katika idara zote, wako mstari wa mbele na wanaimba na kuabudisha vizuri lakini kwenye mioyo yao hawana Amani, nimefanya kazi na vijana kwa muda mrefu na mara nyingi nilijiwa na vijana ambao walikuwa na dhambi za siri, wamezidiwa na tamaa, na wanapiga punyeto zinawakosesha Amani, Amani hii ni tofauti na ile wanayoitafuta katika zile tamaa, Amani hii wanakuhumiwa na dhamiri au Roho wa Mungu kuwaonya kuwa wanapoteza Amani na Mungu, kwa hiyo kumbe wakati mwingine uhusiano wetu na Mungu unapokuwa umeingiliwa na kitu cha tofauti mwanadamu anapoteza amani na Mungu wake, furaha ya Roho Mtakatifu inatoweka, furaha ya wokovu inatoweka, unajihukumu na kujiona mwenye hatia na unakuwa na uzito wa Moyo.

 

Zaburi 51:1-12 “Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani. Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri, Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji, Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi

 

4.       Mtego wa uadilifu – Kila mtu duniania anavutiwa na watu waadilifu, na kila mwanadamu anapenda kuwa na sifa ya uadilifu, hata hivyo kupitia tamaa za ujanani shetani amewaharibiwa watu wengi sana sifa ya uadilifu kwa kutumia tamaa yao na kuwaingiza katika mtego huo, Daudi alikuwa ni mtu aliyependwa na Mungu, na alimpenda Mungu upeo, Lakini aliwahi kuingia katika mtego wa uadilifu bila shaka wakati wa ujana wake, kijana anapokosa uadilifu katika Israel alihesabika kama mojawapo ya watu wapumbavu

 

2Samuel 13:10-14 “Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani. Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, ndugu yangu. Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinitenze nguvu; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu. Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa. Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye.”

 

Tamaa za ujana zinaposhindikana kudhidhibiti maana yake tunaweza kufanya mambo ya kipumbavu na yakaleta aibu katika maisha yetu Bwana atupe neema ya kuwa mbali na upumbavu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth aliye hai, Ni muhimu kumuomba Mungu atusaidie na kuihuisha miili yetu tupate kuwa safi.

Jinsi ya kukimbia tamaa za ujanani

Ni muhimu kufahamu kuwa maandiko hayataadharishi tu kuzikimbia tamaa za ujanani, lakini vile vie yanatupa na njia za namna ya kutoka, na njia hizo ni muhimu sana kwa kila mtu kuzizingatia ili tuweze kuishi maisha ya ushindi.

 2Timotheo 2:22 “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.”

Ziko mbinu kadhaa ambazo maandikio yanatoa lakini leo nitazungumzia sana moja ya muhimu sana na kuichambua kwa undani sana na yenyewe ina maswala kadhaa ya kufanya

Kuenenda kwa Roho.

Wagalatia 5:16-18 “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.”

Ni Muhimu kufahamu kuwa tamaa za ujanani hazina tofauti na tamaa za mwili, na iko namna ambayo watu wa Mungu tunapaswa kuifahamu ili tuweze kupata ushindi katika maisha ya kiroho na ili tuweze kuwa na ufahamu katika jambo ninalotaka kulisema na kulifundisha hapa ni muhimu kufahamu kuwa mwanadamu ana sehemu kuu tatu katika asili ya uumbwaji wake kuna utatu katika uumbwaji wa mwanadamu na nataka kufafanua kama ifuatavyo:-

a.       Soma – Neno la kiyunani kwa kiingereza The body, the living body, the wholeness of human being, It’s a biological body Mwili wa kibailojia, mwili unaotokana na baba na mama

 

b.      Sarx – Neno la kiyunani kwa kiingereza Flesh, human body, earthly body, sinful human nature, Sarks refers to the human way of interacting with and responding to the world. Hii ndio inatafasiriwa kama mwili katika Kiswahili, mwili wa kibinadamu, mwili wa duniani, mwanadamu wa asili mwenye dhambi, mwili huu ndio unaotusaidia kuelewa mambo na kuyatambua mambo na kuitikia mambo tukiwa hapa duniani. Maandiko yanaposema enendeni kwa roho wala hamtayatimiza kamwe mambo ya mwili inamaanisha Sarx. Kwa kiibrania (Nephesh) kwa Kiswahili Nafsi. Sarx inatawaliwa na ufahamu Nafsi, kwa uwezo wa kuona, kusikia, kunusa, kuonja, na kuhisi kwa kutumia ngozi, Mtu anapofanya dhambi kama ya zinaa anafanya juu ya mwili wake wote ni huu ndio unaozungumzwa kwamba ukifanya zinaa inakamata nafsi, inaunganisha nafsi

 

1Wakorintho 6:18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.”

 

c.       Pneumatikos – Neno la kiyunani kuhusu roho ya mwanadamu, kwa kiingereza Soul a part of human that is relating to human spirit, a part of man which is akin to God, the part of human being that belongs to the Divine, it is Higher than man but inferior to God, inaitwa, roho, ni sehemu ya mwanadamu inayohusiana na roho ya mwanadamu, ni sehemu ya mwanadamu au mtu ambayo ni ya thamani au ni ya juu zaidi kuliko mwili, na iko chini ya Mungu mahusiano yote na ulimwengu war oho hufanyikia kwenya nafsi na kuamua roho iwe upande gani wa Mungu au shetani.

 

1Wakorintho 2:14-15 “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu”.

 

Kwa hiyo Soma – ni mwili, Sarx ni Nafsi na Pneumatikos ni roho, Soma kukua kwake na kuishi kwake kunategemea chakula, wanga, protins, mafuta, vitamin, kupumzisha mwili, kunywa maji ya kutosha, kuchukua mazoezi na kuzingatia kanuni za kiafya na kadhalika, Nafsi kulishwa kwake kunategemeana na maarifa, kusikia, kuona na yote unayoyaingiza kupitia milango ya fahamu,  na roho kulishwa kwake kunamtegemea Mungu au maswala yote ya ibada, unapoilisha Soma unastawisha uhai wa nafsi na roho, unapoilisha nafsi unastawisha akili na roho, kusinyaa kwa roho kunategemeana na unailisha nini roho yako au nafsi yako, kukua kwako kiroho kunategemeana na unailisha nini nafsi yako na roho yako!

Zaburi 103:1-2 “Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu.Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote.”

Mathayo 4:4 “Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.”

Wakati mkate ulikuwa unahusu mwili huu wa kawaida, “Rhēma” neno la Mungu ni chakula cha mtu wa rohoni, shetani alipoona Yesu anamlisha sana mtu wa rohoni, na mtu wa mwilini ana njaa alimshawishi afanye mkate ili kumlisha mtu wa mwilini kwa sababu ana njaa, na Yesu alikuwa akimjibu shetani kuwa atendelea kumlisha mtu wa rohoni sawa na ufunuo wa kiungu, kwa sababu mtu sio mwili tu bali mtu pia ni roho sasa maandiko yanamanisha nini

2Timotheo 2:22 “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.”

Wagalatia 5:16-18 “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.”

Lakini zikimbie tamaa za ujanani – Neno zikimbie kwa kiyunani linasomeka kama neno “Pheugōlinalosomeka kimatamshi fyoo-go, ambalo kwa kiingereza Vanish – to shun or to disappear from sight, especially quickly, became invisible, kwa Kiswahili usionekane, jiepushe, usijitokeze, usitokee, kabisa kwenye tamaa za ujanani, usiache tamaa za ujanani zikachomoza, zima kabisa tamaa za ujanani, kwa hiyo kukimbia huku kunakozungumzwa hapo, yalikuwa ni mausia ya Paulo mtume kwa Timotheo kuhakikisha ya kuwa wakati wote haruhusu au asiruhusu tamaa za ujanani kumshinda katika maisha yake, swala hili linauhusiano na kila mmoja wetu halikuwa tu agizo kwa Timotheo sisi nasi kwa neno hilo tunaagizwa kutokuruhusu tamaa za mwili kabisa katika maisha yetu, hii maana yake ni nini ni pamoja na kujitia nidhamu, na kuuweza mwili (Sarx) na (Soma)

1Wathesalonike 4:3-5 “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.”             

Neno kuuweza katika kiyunani “Ktaomai” ambalo maana yake ni “possess” kuutawala mwili sasa katika hali ya kawaida ukiulisha sana mwili roho itazimia na mwili utakuwa na nguvu na utatimiza mapenzi ya mwili, na ukiilisha sana roho utaenenda kwa roho, sasa ni namna gani mtu anaweza Kuendenda kwa Roho hilo nalo sio jambo jepesi, lakini pia sio kazi yetu, ni kazi ya Mungu Roho Mtakatifu hata hivyo tunao wajibu wa kufanya, hatuwezi kuutawala mwili kwa ukali lakini tunaweza kuutawala mwili kwa neema ya Mungu kwa kuruhusu Roho Mtakatifu atawale.

Wakolosai 2:20-23 “Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani, Msishike, msionje, msiguse; (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu? Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.”

Kutiisha huko hakumaanishi ya kuwa sasa unatumia nguvu au ukali kuutawala mwili na badala yake unajiachia katika uwepo wa Mungu Roho Mtakatifu ili akusaidie,  uhai wa kiroho wa kila mkristo na kanisa kwa ujumla unategemea sana uwepo wa Roho Mtakatifu na utendaji wake katika maisha yetu, kwa bahati mbaya kanisa huwa linakazia ujazo wa Roho Mtakatifu, kunena kwa lugha, Karama za Roho Mtakatifu huku wakisahau kabisa swala zima la kuenenda kwa roho, yaani kuhakikisha kuwa Mungu Roho Mtakatifu anatuongoza na kutupa msaada kila wakati na kila iitwapo leo katika maisha yetu tukiwa na yeye, tunapofurahia neema juu ya neema maana yake neema ya wokovu na neema ile inayotusaidia kuenenda katika Kristo, ushirika wetu wa kudumu na Roho wa Mungu utatusaidia katika maisha yetu kuushinda mwili bila kutumia nguvu, ukiona unapambana sana katika kushindana na dhambi wewe mwenyewe kwa miguvu yako uko mwilini bado na bado uko chini ya sheria.

Wagalatia 5:16-18 “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.”

Sasa tunawezaje kuenenda kwa roho?

-          Ishi kulingana na Neno la Mungu – Soma neno la Mungu na kulitafakari na kulitii, Neno la Mungu ndilo dira yetu, katika kutembea na Mungu, tunapojifunza na kulitafakari tunajiweka katika nafasi ya kuyajua mapenzi ya Mungu na wakati huo tunampa Roho Mtakatifu nafasi ya kutuongoza katika kweli yote na haki yote, Paulo alimtaka Timotheo kufuata haki, kufuata haki maana yake ni nini? Neno haki katika Biblia linajitokeza karibu mara 92 na neno hilo kwa kiyunani ni Justfication au righteousness tunapomtii Mungu sawa na maagizo yake katika neno tunafuata haki na hii inatuweka katika nafasi ya kutembelewa na Roho Mtakatifu na kuanza kuongozwa na Roho na kuenenda kwa Roho.

 

Matthayo 3:13-17 “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.”

 

Wakolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.”

 

-          Ishi kwa Imani – Kudumisha uhusiano wetu na Mungu na kuishi kwa kumpendeza Mungu ni pamoja na kuishi kwa Imani, tunaokolewa kwa Imani, na tunapaswa kudumisha uhusiano wetu na Mungu kwa Imani, Pasipo Imani haiwezekani kumpendeza yeye, watu wote waliokuwa mashujaa wa Imani na waliojaa Roho Mtakatifu walikuwa watu walioishi kwa Imani, Paulo akamwambia Timotheo ukafuate haki, na imani, kwahiyo kukimbia tamaa za dunia hii kunahitaji kuendelea kuamini na kuishi kwa Imani

 

Yohana 14:16-17 “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.”

 

Wagalatia 3:1-3 “Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?

 

Matendo 6:5 “Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia;”

 

Waebrania 11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.”

 

-          Ruhusu hali ya kukua kiroho -  Kusudi kuu la kuitwa kwetu ni ili tumzalie Bwana matunda, tukiulisha mwili tutazaa matunda ya mwili na kudumaa kiroho, tukilisha roho tutakomaa kiroho na kumzalia Bwana matunda ya Roho, matunda ya roho ni Pamoja na upendo na amani Paulo Mtume akamwambia Timotheo “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na Amani” hatuwezi kuzaa matunda haya hasa la upendo  na Amani kama hatujakomaa kiroho!

 

Waefeso 4:11-15 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.”

 

Wagalatia 5:22-23 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.”

 

-          Uwe na Ushirika – Hakuna jambo zuri duniani kama ushirika, ni katika ushirikia ndipo tunapoweza kutiwa moyo hii ni kwa ushirika unaojitambua, tunasaidiana, na kuwajibika kwaajili ya maisha ya kila mmoja, Paulo alimwambia Timotheo “Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi

 

Waebrania 10:24-25 “tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri; wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.”

 

-          Enendeni kwa Roho - hatua zote hapo juu zinatuandaa kuja katika eneo muhimu ambalo kuenenda kwa Roho, ni muhimu kufahamu kuwa neno enendeni linasomeka katika lugha ya kiyunani kama “Peripateōkwa kiingereza go be Occupied ambalo limetumika mara 93 katika biblia ya KJV “be busy” au Be Active, au be used Kiswahili tungesema uwe bize, uwe katika utendaji, ushughulishwe wakati wote au uingie kazini na Roho Mtakatifu, tumika naye, hali hii huchochea moto wa utendaji wa Roho Mtakatifu usizimike, Roho wa Mungu huonekana na kutenda kazi tunapojishughulisha naye kila wakati na kila siku, kama umechunguza sana kwa makini watumishi wengi wa Mungu wanaoshughulika na kufanya kazi na Roho Mtakatifu huwa hawapoi na huwa ni vigumu kuona matunda ya mwili yakizaliwa, Daudi alipoacha kwenda vitani ndipo, alipoona mwanamke anayeoga na kuvutiwa naye aku kumtamani, na tamaa za ujanani zikachukua nafasi.

 

Luka 4:1 “Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,”

 

 Luka 4:14 “Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.”

 

Matendo 4:8-10 “Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli, kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa, jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu. Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni.”

 

Matendo 6:8-10 “Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu. Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano; lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye

 

Hitimisho:

 

Kutembea na Roho Mtakatifu na kuwa karibu naye siku zote, kusikia uongozi wake sio kazi rahisi, lakini ndio njia yenye thawabu ya kuutunza wokovu wetu na kumzalia yeye matunda zaidi ya yote inatupa ushindi na kutufanya kuishi kwa Amani na furaha kwa utimilifu wake, wakati huo hatutayaona tena matendo ya mwili yakiwa mwiba na usumbufu mkubwa katika maisha yetu, tutaweza kuzikimbia tamaa za ujanani bila kutumia nguvu wala kupambana na dhambi katika miili yetu, mwili hautatutawala wala hautatuvuta, mtu wa mwilini atazikwa kabisa na mtu wa Rohoni atakuwa na nguvu, wachungaji na walimu wa neno la Mungu tukiwaelekeza watu kuhusu kutembea na Roho, kuongozwa na roho kuenenda kwa roho, hatutakuwa na kazi ya kukemea dhambi, kutenga, kutishia kujifanya wakali wakati wewe na mimi sio Mwokozi, kuhukumu watu, kote kutamalizwa kwa kuwaambia watu kwa urahisi tu hivyo enendeni kwa Roho, wala hamtayatimiza KAMWE mambo ya mwili Neno kamwe kiyunani  “ou mēKiingereza “Not at All” maana yake haitakuja itokee kamwe kwa hiyo suluhu ya dhambi ni Roho Mtakatifu ambaye tatizo kubwa watu hawamtumii, katika maisha yao bali wanajaa, wananena, wana karama kisha inaishia hapo tu ni Muhimu kujiongeza.

 

Warumi 8:5-10 “Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.”

 

Bwana ampe neema kila mmoja wetu, aweze kuelewa somo hili na kufaidika na maswala ya rohoni sawasawa na mapenzi ya Mungu katika jina la Yesu Kristo aliye hai, naomba kwaajili ya wote ambao mwili unawasumbua Mungu ukapate kuwafunulia na kuwasaidia ili mwili na tamaa za ujanani zisiwasumbue tena katika jina la Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai ameen!

 

 

Na Rev. Innocent Samuel Kamote

 

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Jumapili, 28 Julai 2024

Hukumu ya Mungu isiyoepukika!


Warumi 2:1-8 “Kwa hiyo, wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru; kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale. Nasi twajua ya kuwa hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao hayo. Wewe binadamu, uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayo hayo mwenyewe, je! Wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu? Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu, atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake; wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele; na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu;”




Utangulizi:

Hukumu ya Mungu kwa wanadamu ni jambo lisiloepukika,Tangu mwanzo Mwanadamu na viumbe wengine walipokosea Mungu mara moja alitoa hukumu, alimuhukumu Shetani, alimuhukumu mwanadamu, Alimuhukumu mwanaume na alimuhukumu mwanamke kila mmoja kwa kadiri ya uhusika wake katika kosa lile la bustanini mwa Edeni, kwa hiyo hukumu ya Mungu ni jambo lisiloepukika, ukweli kuhusu hukumu ya Mungu ni jambo lenye kutisha sana kwa wanadamu, hata hivyo leo tutachukua Muda kutafakari kwa undani kuhusu hukumu ya Mungu na umuhimu wake katika mtazamo wa upendo wake na rehema zake na tabia yake ya uungu ambayo itakushangaza!

Warumi 2:12-16 “Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria. Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki. Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea; katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.”

Swala zima la hukumu kwa mujibu wa maandiko Mungu hakuwapa wanadamu, na tumekatazwa kuhukumu, bali amepewa Yesu Kristo na Baba yake aliye mbinguni, kwa hiyo hakuna mtu awaye yote mwenye mamlaka ya kuhukumu isipokuwa mwana wa Adamu yaani Yesu Kristo mwenyewe, kuhukumu ni kukaa katika kiti cha Mungu. Fundisho kuhusu hukumu linatawala maandiko yote katika agano la kale na jipya, Utukufu wa Mungu unaonekana na kufunuliwa katika namna anavyohukumu, Mungu anamtaka kila mmoja awajibike na kwa sababu hiyo hakuna mwanadamu wala taifa litakaloweza kuiepuka hukumu ya Mungu na Yesu ndiye Mwamba wa hukumu hiyo:-

Yohana 5:22-30 “Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote; ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka. Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani. Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai. Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake. Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu. Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.”

Kwa nini Masihi amepewa kuhukumu? Kwa sababu uwezo wake wa kuhukumu ni mkubwa sana na uko juu na sio wa kibinadamu, na kwa sababu yeye amepitia uanadamu anatujua vema lakini pia kwa sababu kuhukumu kwake hakutokani na yale yanayoonekana kwa macho, wala yale ayasikiayo kwa masikio yake lakini hukumu yake ni ya haki kama alivyosema mwenyewe na uwezo wake ni mkubwa sana kwa sababu ya Roho wa Mungu na hekima yake kuu

Isaya 11:1-5 “Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana; na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya. Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia.”

Kumbukumbu 1:17 “Msitazame nafsi za watu katika hukumu; mwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso wa mtu awaye yote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo mniletee mimi, nami nitalisikiza.”

Kumbukumbu 32:3-4 “Maana nitalitangaza Jina la Bwana; Mpeni ukuu Mungu wetu.Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.”

Leo tutachukua muda moja kwa moja kutafakari kwa kina na mapana na marefu kuhusu hukumu za Mungu ambazo kimsingi ziko aina nne za hukumu ambazo tutaziangalia kwa kuzingatia vipengele vinne vifuatavyo sawa na ufunuo.

 

1.       Hukumu iliyoko sasa – Paroúsa Krisi

2.       Hukumu ya adhabu – Krima

3.       Hukumu isiyo ya adhabu – Krino

4.       Hukumu isiyotarajiwa – Aprosmenos   

 

Hukumu iliyoko sasa – Paroúsa Krisi

Hukumu hii kwa kiingereza inaitwa Present Judgement kwa kiyunani Paroúsa Krisi yaani hukumu hii inategemeana na mkao ulioko sasa wa hali ya kiroho za wanadamu, kama mwanadamu ameukubali mpango wa Mungu wa ukombozi kwa kumwamini Bwana Yesu kama Bwana na mwokozi wake huyo kwa sasa haukumiwi, na yule ambaye hajaukubali mpango wa Mungu wa ukombozi kupitia Yesu Kristo huyo amekwisha kuhukumiwa, Instant Judgement.au “Quckly Decision” “quicly judgemnt

Yohana 3:16-18 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.     Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.”

Yohana 5:24 “Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.”

Kwa hiyo katika ulimwengu huu wako watu ambao wamehukumiwa tayari yaani hivi tunavyozungumza hapa wako watu wa aina mbili duniani na wote wanaendelea na shughuli zao wakiwa wamehukumiwa yaani wale wasiomwamini Yesu na kundi la pili ni watu ambao hawako chini ya hukumu hawahukumiwi hawa ni wale waliomuamini Bwana Yesu na kumkubali kama Bwana na mwokozi wao, Hukumu hii inaendelea ikiendeshwa na Roho Mtakatifu kupitia kazi anayoifanya sasa ya kuwashuhudia watu kwa habari ya dhambi, haki na hukumu, kila wakati na kila siku injili ihubiriwapo mtu akimpokea Yesu anahama kutoka upande wa wale waliohukumiwa kwenda upande wa wale wasiohukumiwa,Injili ikihubiriwa ukaikubali sasa uko nje ya hukumu, na ukiikataa uko hukumuni.

Yohana 16:7-8 “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.”
             

Hukumu ya adhabu – Krima

Hii ni moja ya kundi la hukumu (Judgement or Condemnation) ambayo inahusiana na siku ya mwisho wakati Kristo atakapokalia kiti cha enzi cha hukumu na kumuhukumu kila mmoja kwa kadiri ya matendo yake hukumu hii pia inaitwa hukumu ya adhabu au hukumu ya aibu, siku ya hukumu hii kila mtu atasimama mbele ya kiti hicho cha hukumu cha Mungu na kutoa hesabu yake mwenyewe. Hukumu hii kiyunani Krima au Krinete maana yake to Condemn, au making a negative assessment of a person or thing, kufanya maamuzi hasi dhidi ya mtu au kitu.

Warumi 14:10-12 “Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu. Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.”

2Wakorintho 5:10 “Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.”


Daniel 12:2-3 “Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele. Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele.”

Muhubiri 12:14 “Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.”

Ufunuo 20:11-12 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.”  
     

Ufufuo huu ni wa hukumu ya adhabu,(Krima) na itakuwa ni hukumu ya aibu kwa sababu Neno Krima linalotumika kuelezea hukumu ya adhabu lina maana ya hukumu isiyohukumu matokeo tu bali inayohusu utafiti wa kina na uzingativu wa kila kilichofanyika kuanzia kwenye dhamiri na machakato mzima wa tukio pamoja na uzito wa ushahidi na mazingira  katika mtazamo wa kibinadamu, lakini katika mtazamo wa kiungu hukumu hii inahusisha hukumu iliyo sawasawa na Haki ya Mungu na tabia yake, na kwa kuwa Mungu ni mkamilifu hukumu yake itakuwa sahihi  na madhara au adhabu itakayoambatana na hukumu hii itakuwa ni sahihi, kwa hiyo hukumu yake itakuwa ni matokeo na ufunuo ulio sahihi ukiingia ndani katika dhamiri ya mwanadamu kwa hiyo itakuwa ni hukumu ambayo hata yeye anayehukumiwa atakubaliana na ile adhabu atakayopewa au ataridhishwa na maamuzi ya jaji mkuu Yesu Kristo.   
     

Hukumu isiyo ya adhabu – Krino

Hukumu hii isiyo ya dhabu ni hukumu inayowahusu wale wote ambao wamemuamini Yesu Kristo hawa kimaandiko hawahusiki katika hukumu ya adhabu (Krima), na badala yake hawa wana adhabu iitwayo Krino hii ni hukumu isiyo ya adhabu imetajwa na Paulo Mtume katika:-

Warumi 8:1-2 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti

Warumi 8:33-34. “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.”

Krino ni hukumu isiyo ya adhabu ambayo itawahusu watu waliookolewa, yaani wale waliomuamini Yesu hawatakutana na hukumu ya adhabu lakini watakutana na hukumu itakayofuatilia kwa haki, kwanini mtu Fulani alifanya jambo Fulani na thawabu yake itakuwa ni thawabu gani? Hukumu hii katika tamaduni za kiyunani Mgeni rasmi hukaa katika kiti kinachoitwa Bema au jukwaa au sehemu maalumu iliyoinuka kwaajili ya kutoa thawabu, za kimichezo ambapo wanamichezo wanapata thawabu au medali kulingana na kazi waliyoifanya na hakuna madhara kwa waliokosa medali. Hii ni hukumu ya watakatifu ni hukumu ya kutoa hesabu mbele za Kristo kwa kile tulichofanya. Katika somo la ufahamu kuhusu maswala ya hukumu The doctrine of Judgement Krino kiyunani kwa kiingereza ni to separate, put asunder, to pick out, Select, choose, to approve, esteem, to prefer, to give an opinion, to determine, resolve, decree, ni hukumu ya kutenganisha, kuchanganua, kuchagua, kuidhinisha, kuthaminisha, kupendelea, kutoa maoni, kuazimia, kuthibitisha, kwa hiyo itakuwa ni hukumu ya kuja kuthibitisha nani anafaa kuwa nini katika ufalme wa Mungu na sio kwa kusudi la kuadhibu.

1Wakorintho 3:12-15 “Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.”

Mathayo 25:14-28 “Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri. Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano. Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida. Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao. Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida. Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida. Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako. Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi

Mathayo 24:45-46 “Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo.”

Hukumu hii ni hukumu ya watakatifu, kila mtu aliyeokolewa anapaswa kumtumikia Mungu, na Kristo atakapokuja kulinyakua kanisa, pale mawinguni itakuwepo nafasi ya kutoa taji na karamu ya mwana kondoo wakati huu kila mkristo atahukumiwa sawa na kazi aliyoifanya na jinsi na namna alivyoitumia talanta aliyopewa kwa uaminifu au vinginevyo na hapo thawabu zitatolewa, hakutakuwa na adhabu lakini kila mtu atastahili heshima yake kulingana na bidii, akili, muda na namna tunavyojitoa kwa Mungu ikiwa ni pamoja na kuwalisha watu wake, kwa hiyo kama sisi ni wachungaji tuwalishe watu chakula yaani neno la Mungu kwa wakati wake, kama una kipawa chochote kile kitumie kwa kadiri uwezavvyo na kwa kadiri ya neema huku ukiwa na dhamiri safi kwa sababu hukumu hii ni hukumu isiyoepukika pia katika hukumu hii hakuna mtu anayeweza kuwashitaki watu wa Mungu kwa sababu zozote wala hakuna mtu anayeweza kutuhukumu na kudai kuwa hawa ni wakosa, hukumu hii ni hukumu isiyo na madhara.        
    

Hukumu isiyotarajiwa – Aprosmenos

Katika hukumu zote zilizotajwa hapo juu, hii ndio hukumu itakayoshangaza watu kuliko hukumu zote, katika hukumu hii maamuzi atakayoyatoa Yesu Kristo yatadhihirisha uwezo wake mkubwa na hekima yake kubwa na ile hali ya kuwa yeye ni Bwana na hakuna mtu wa kumuamulia lolote wala kutabiri lolote, hukumu hii inadhihirisha kwamba Mungu mwenyewe ana haki ya kuamua na uwezo wake wa kuhukumu ni wa hali ya juu na wa tofauti sana.
 

Hukumu hii iko katika maamuzi ya Mungu mwenyewe na inaitwa hukumu isiyotabirika katika lugha ya kiyunani linatumika neno hilo Aprosmenos ambalo kwa kiingereza ni unanticipated, unforeseen, unexpected, difficulties  predicted kwa hiyo ni hukumu isiyotegemewa, ni hukumu isiyotarajiwa, ni hukumu isiyotabirika ni hukumu ambayo ni ngumu kimatazamio, hukumu hii iko chini ya maamuzi ya Mungu mwenyewe bila kujali kuwa kuna haki au hakuna haki mfano lakini iko haki ambayo Mungu mwenyewe katika mtazamo wake huiona lakini wanadamu hawawezi.

Warumi 9:10-16 “Wala si hivyo tu, lakini Rebeka naye, akiisha kuchukua mimba kwa mume mmoja, naye ni Isaka, baba yetu, (kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye), aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo. Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha! Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu.”

Warumi 9:20-21 “La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi? Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima? 

Unaona ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua Maneno haya yanaonyesha kuwa mwanadamu awaye yote anapokuwa na kesi mahakamani awe amekosa au awe hajakosea bado anakuwa na mashaka kwa sababu mwenye maamuzi ya mwisho ni hakimu au jaji mwenyewe, kwa hiyo ni muhimu kufahamu kuwa iko mamlaka ya Mungu mwenyewe inayoweza kuamua na kuhukumu hata kama jambo linaonekana kuwa sawa machoni pako mfano;

1.       Luka 10 38-42 “Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake.Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake.Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie.Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.”

Kwa mila na tamaduni za kimashariki wewe na mimi tunge muhukumu Mariamu kama binti mvivu na tungemkubali Martha kama mwanamke mchapakazi, lakini pale Martha alipoinua kinywa chake kumuhukumu Mariamu Bwana katika hukumu yake isiyotarajiwa anahukumu kuwa Martha ni changamoto kubwa sana na Mariamu ndiye yuko sahihi. Martha alikuwa na makosa makubwa sana kuliko Mariamu, Martha alikuwa akimfokea Yesu!  BWANA HUONI VIBAYA? Ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu?

Kumsikiliza Yesu ndio tukio la Heshima kubwa sana, na alikuwa akipokea Baraka kubwa za ushirika na Yesu, ambapo Martha kwa sababu ya kulalamika kwake alikuwa na msongo tu wa mawazo, haikuwa vibaya kuandaa kwaajili ya mgeni, lakini alijaa hukumu dhidi ya Yesu na Ndugu yake Mariamu, na kwa sababu hiyo alipoteza point katika hukumu kwa sababu ya manung’uniko

 

Wafilipi 2:14-15 “Yatendeni mambo yote pasipo manung'uniko wala mashindano,mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,”

                 

Yesu hakumwambia Martha akae chini, kwani alikuwa anafanya jambo jema, na wala hakumwambia Mariamu inuka kwani naye alikuwa akifanya jambo jema, mmoja akimtumikia na mwingine akisikiliza,  wako wakristo na watumishi wa Mungu ambao hutumika sana, na wako ambao huomba sana na kutafakari wote wanaitenda kazi iliyo njema, kosa kubwa ni pale unapoanza kuwakosoa wengine na kufikiri kuwa wewe ndiye bora zaidi kwa sababu unafanya hicho unachikifanya, Jambo kubwa na la msingi na la muhimu ni uhusiano na Yesu Kristo, na Mariamu alikuwa ameligundua hilo, na hakuna mtu angeweza kumtenga na hilo, Mariamu kwa jicho la kibinadamu alionekana ni mvivu lakini kwa jicho la Yesu Mariamu alikuwa anampenda Yesu, alichukua muda kuwa na Yesu kwake Yesu alikuwa muhimu kuliko kupika, unalolifanya linaweza kuwa sio tatizo, lakini tatizo ni pale unapoanza kuamsha kinywa kwaajili ya wengine, Uhusiano wetu na Mungu ni jambo jema ambalo hakuna mtu anaweza kutuondolea. Mariamu alichagua fungu jema na hakuna wa kumuondolea, Ukichagua ushirika na Yesu hakuna mtu atakuondolea ushirika huo watakuondoa kwenye mengine lakini hakuna kitakachokutenga na Upendo wake Kristo.

 

2.       Marko 9:38-40 “Yohana akamjibu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi; tukamkataza, kwa sababu hafuatani nasi. Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninenea mabaya;kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu.”

 

Hakuna mtu aliyekwenda kwa Yesu Kristo/Mungu akiwa anamshutumu mwingine na Yesu akakubaliana naye hata siku moja, kila wakati katika maisha ya Yesu alipoletewa kesi, Kesi hiyo iliwageukia walioleta, na hukumu kuwapata wao, katika tamaduni za kikanisa na madhehebu watu hujidhania kuwa wao ni wao na wao ndio wenye Yesu peke yao kama Yohana hapo, kwa hiyo walivyoona kuna anayetoa pepo kama wao lakini si wa dhehebu lao alitaka kuwazuia kuwanyima kibali, Lakini Yesu alikosoa vikali mtazamo wao.Wako watu wanaofikiri kuwa ni wao tu ndio wenye mamlaka au hatimiliki na Yesu, wao ndio bora, tabia ya aina hii inamuuzi sana Mungu, unaposhindana na kila mtu anayetumia jina la Yesu kwa kujifikiria kuwa wewe ndio wa muhimu na unapaswa kulitumia jina hilo unajiweka kwenye hatari ya kupingana na Yesu mwenyewe.

 

3.       Warumi 11:2-4 “Mungu hakuwasukumia mbali watu wake aliowajua tokea awali. Au hamjui yale yaliyonenwa na maandiko juu ya Eliya? Jinsi anavyowashitaki Waisraeli mbele za Mungu,Bwana, wamewaua manabii wako, wamezibomoa madhabahu zako, nami nimesalia peke yangu, nao wananitafuta roho yangu.Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali.”

 

Eliya alikuwa nabii mkubwa sana wa Mungu, aliwahukumu waisrael kuwa wamewaua manabii wote wa Mungu na kuvunja madhabahu, zote za Bwana na kuabudu baali na kuwa ni yeye pakee amesalia (1Wafalme 19:10) Lakini Mungu alimjibu kuwa wako wengi ambao hawajapiga goti lao kwa baali, Mungu alikuwa anamthibitishia Eliya kuwa asijidhanie kuwa yuko pake yake Mungu ana watu wengi, hukumu ya Mungu wakati wote huthibitisha kuwa sisi ni wanadamu na hatuko sawa katika mitazamo yetu, Mungu ana jicho lake la kipekee katika kuyatazama mambo na hivyo tunapaswa kuwa wanyenyekevu sana na kuacha kuwashitaki watu wengine kwa Mungu.

 

4.       Katika mifano ya ufalme wa Mungu pia ambayo imebeba siri nyingi za Mungu utaweza kuona imejaa hekima na maarifa na uweza wa kiungu katika maamuzi ya namna ya kuhukumu, Yesu anafunua kuwa kuhukumu kwake kutakuwa mara zote kukiwaacha watu midomo wazi yatakuwa ni maamuzi ambayo yatawashangaza wengi kwa matokeo yake.

 

a.       Farisayo na mtoza ushuruLuka 18:9-14 “Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote. Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.”

 

Katika mfano huu tunajifunza juu ya watu wawili waliopanda kwenda hekaluni kusali, mmoja alikuwa farisayo kwa hiyo ni wazi kuwa alikuwa myahudi wa madhehebu ya mafarisayo, alikuwa mcha Mungu na mtu aliyemwamini Mungu, pia alikuwa mtii kwa sheria (Torati) na aliielewa vema, na alikuwa mtu wa haki, hakutii tu sheria lakini alifanya zaidi ya sheria, kwa mujibu wa torati waisrael walitakiwa kufunga mara moja tu siku moja kwa mwaka (Siku ya upatanisho) lakini yeye alifunga mara mbili kila wiki  kwa hiyo alizidisha na kufanya zaidi ya sheria, Sheria ilimtaka mtu atoe fungu la kumi angalau ya sehemu Fulani tu ya mapato yake lakini yeye alitoa sehemu ya kumi ya kila aina ya kipato (mapato yangu yote) kwa hiyo hakuwa na dhambi, hakuwa myang’anyi, wala hakuwahi kudhulumu mtu, wala hakuwahi kuzini, kwa msingi huu basi kama ingelikuwa ni wewe na mimi farisayo huyu ni peponi moja kwa moja au tungekubaliana na sala yake na katika hukumu hatungemuhesabia kuwa hana shida yoyote Lakini hitimisho la Hakimu mkuu ni kuwa ajikwezaye atatushwa na ajishushae atakwezwa, Farisayo alikataliwa tatizo lilikuwa ni nini katika hukumu hii? Alijihesabia haki, alijidhania ya kuwa yeye ni mtakatifu, alijivuna, alipata kiburi cha kidini, hakufikiri kuwa naye anahitaji msamaha wa Mungu na rehema zake, alijifikiri ya kuwa anaweza kununua rehema za Mungu kwa matendo yake, alipiga vita wengine na kujiona ni mkamilifu kwa sababu ya matendo yake na kiburi, Katika macho ya Mungu alikataliwa Mungu huwapinga wenye kiburi na kuwapa neema wanyenyekevu, sio hivyo tu moyo wake ulijaa dharau dhidi ya watu wengine na alikuwa hana upendo, na zaidi ya yote alikalia kiti cha Mungu kwa kujifanya ndiye muhukumu,  

 

Mathayo 7:1-5 “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.”

 

Mathayo 23:23-24 “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia.”

 

Farisayo alikataliwa katika hukumu, hii ndio hukumu ya kushangaza na isiyoweza kutabirika, tuna watu wengi sana wanaopanda kwenda kusali, tuna watu wengi sana wanafunga, sio wazinzi, ni wasafi lakini usafi huo ni wakwao wenyewe mioyoni mwao Mungu atawakataa, hukumu isiyotarajiwa itatufunulia mengi sana, tutaona mambo ya ajabu ya watu wote wanaojifikiria kuwa hawahitaji toba wamekamilika na wako safi lakini Yesu atawakataa hii itatushangaza ni hukumu isiyotarajiwa. Wote wenye juhudi ya kutenda mema na kudharau wengine kwa kujifikiri kuwa wao ni safi kuliko wengine, mahubiri yao yamejaa hukumu, maneno yao yamejaa kuhukumu wengine na kujifikiri kuwa wao wako sahihi na ni wasafi mno kumbe katika macho ya Mungu tunahitaji kuwa wanyenyekevu, na ni muhimu kwetu kukumbuka kuwa matendo mema sio kitu cha kushangaza kwa Mungu, tuliumbwa tukiwa wema, kwa hiyo unaweza kukuta mtu jhajamuamini Yesu na akawa ana matendo mema, Mungu anataka tuipokee zawadi ya wokobu kwa neema na kwa Imani na kutembea kwa neema na Imani, pasipo hiyo huwezi kumpendeza Mungu.

 

Waefeso 2:8-10 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.”    

 

b.      Wafanyakazi katika shamba za mizabibu – Mathayo 20:1-16 “Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu. Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu. Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi; na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda. Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile. Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?  Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu. Kulipokuchwa, yule bwana wa shamba akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ujira wao, ukianzia wa mwisho hata wa kwanza. Na walipokuja wale wa saa kumi na moja, walipokea kila mtu dinari. Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari. Basi wakiisha kuipokea, wakamnung'unikia mwenye nyumba, wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa.Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari? Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe.Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema? Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho

 

Kuna mengi ya kujifunza pia kuhusu hukumu ya Mungu katika mfano huu, sitaki kueleza kila kitu kilichomo katika mfano huu lakini mfano huu unazungumzia mwenye nyumba, Biblia ya kiingereza inatumia neno landowner yaani mwenye shamba ambaye alikuwa amekusudia kazi yake iishe, alitoka kutafuta wafanya kazi, kwaajili ya shamba lile, siku zile malipo ya siku nzima yalikuwa ni dinari, mwenye shamba aliajiri yeye mwenyewe aliajiri watu wa saa 12 alfajiri, kisha saa 6 kisha Saa 9 na kisha saa 11,  na alipatana nao kuwalipa (zingatia malipo kwa siku ni Dinari) au unaweza kuweka Elfu kumi kwa siku, kwa kazi ya masaa 12.  Hawa wengine waliajiriwa tu kwa mapenzi ya mwenye shamba na aliwaahidi atawapa haki yao, ilipofika jioni aliamuru wote walipwe akianza na wale wa saa 11 ambao kimsingi walifanya kazi saa moja tu. Hii ni kwa sababu mwenye shamba ni mkarimu, lakini walipolipwa wale walioajiriwa wa saa 12 alfajiri walilalamika na kulaumu kuwa mwenye shamba hakuwa ametenda haki kwa sababu wako watu wamefanya kazi saa moja tu na amewalipa sawa na wao waliofanya kazi tangu asubuhi, Kwa hiyo walimuhukumu mwenye shamba kwa kuwa mkarimu na mwema. Hii inatufundisha nini? Mungu anauwezo wa kuamua na lolote atakaloliamua sawa na ukarimu wake huna haki ya kulalamika kwa sababu hajakudhulumu yeye huweza kuamua kumrehemu yeyote yule na hatupaswi kuwa na wivu?

 

Warumi 9:18-21 “Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu. Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake?La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi? Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?

 

Waefeso 2:8-9 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.”

 

Dinari inazungumzia wokovu, ambapo Mungu anaweza kumuokoa mtu wakati wowote na thawabu ikawa moja kama alivyomuokoa mwizi pale msalabani, lakini wale waliokuweko kazini wali lalamika mbona unatulipa sawa?  Mara kadhaa tumekasirika na kuona wivu pale Mungu anapombariki mwingine, na kumuinua kuliko sisi kwa mapenzi yake tunalalamika kwa sababu ya wivu, tunalalama na kumuona Mungu kama hayuko sawa vile ni kama anapendelea wakati tunapojilinganisha na wengine na wakati mwingine tumewapiga vita watu kwa sababu ya wivu wetu, tunafanya ujinga na Mungu anazo sababu za kutuhukumu kwa kuhukumu wema wake na ukarimu wake, wokovu ni kwa neema tu na kamwe hatuwezi kuutendea kazi, wale wanaofikiri kuwa kwa kazi zao watapata kibali kikubwa kwa Mungu wanajidanganya mfano huu unafunua vilevile hukumu isiyotarajiwa ya Mungu.

 

c.       Mfano wa yule kaka mkubwaLuka 15:11-32 “Akasema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia. Akawagawia vitu vyake. Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati. Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji. Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu. Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako. Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana.Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena. Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni; mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi; kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia. Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo. Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini? Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima. Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi. Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu;lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona. Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako.Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.”

 

Nauita mfano wa kaka mkubwa kwa sababu katika mtazamo wa Mungu ndiye aliyekuwa na matatizo makubwa zaidi ya Mwana mpotevu, Baba wa mwana mpotevu alikuwa anasikitika kumpoteza kijana wake na aliporejea nyumbani alilia akamkumbatia na kumvika mavazi mazuri kisha akamfanyia sherehe kubwa, Kaka mkubwa alikasirika, akasusa na kugoma kuingia ndani, akamuhukumu baba yake na mdogo wake, alimshutumu kuwa mdogo wake huyo ametapanya mali pamoja na makahaba, na baba yake ameonyesha ukirimu jambo ambalo hajawahi kulifanya kwa kaka mkubwa, kwa hiyo alijawa na hasira, na wivu na kulaumu ukarimu wa baba yake mfano huu kama mingine iliyotangulia unatahadharisha kuwa Mungu atakapohukumu wanadamu atafanya mapinduzi ambayo wale wanaojifikiria kuwa ni wenye haki watalia na kushangaa, wale wanaojifikiria kuwa hawajawahi kumkosea Mungu kwa lolote, basi wanaweza kumkosea Mungu kwa kuhukumu wengine, au kwa kumlaumu Mungu au maamuzi ya Mungu ya kikarimu, iko mifano Mingi ambayo muda usingeliweza kutosha kuichanganua lakini unaanza kuelewa

Kwaajili ya Hukumu hizi za kushangaza za Mungu, na tabia zake ni muhimu sana kuwa wanyenyekevu na kuogopa sana hukumu ya Mungu, hakuna kitu kinatisha kama hukumu ya Mungu, wakati wote kujifikiri kuwa sisi ndio tuko sawa na wenzetu hawako sawa, kunakuweka katika hatari ya kuingia katika hukumu isiyoepukika na hukumu za kushangaza kwaajili ya aina hii ya mtazamo ni lazima tukubali na kuelewa ya kuwa hata siku ya mwisho siku ya hukumu Mungu akisema nimekusudia kuwarehemu watu wote na watu wote nataka waingie peponi au katika ufalme wake je wewe na Mimi tutakubaliana na hukumu hiyo? Tutaona kuwa Mungu amehukumu kwa haki? au tutadhani kuwa Mungu ana upendeleo acha kujifikiri kuwa wewe ni bora zaidi kuliko wengine, acha kukomalia makosa ya wengine Mungu nadhani anataka tushughulike na maisha yetu zaidi kuliko ya wengine.

Mathayo 7:3-5 “Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.”

Je utaweza kuiepuka hukumu ya Mungu? Ni hukumu isiyoepukika inatutaka tuwe wanyenyekevu sana sisi kama wanadamu hatuna cha kujivuna katika jambo lolote lile, wakati wote tuombe rehema na neema ya Mungu na kuendelea kumtafuta bwana kwa mioyo yetu yote, na zaidi ya yote turuhusu wakati wote neno la Mungu lituhukumu na kutubu pale linaposhughulika na maovu yetu, Mungu atatubariki na kwa neema yake atatufunulia kweli yetu yote Bwana yu karibu na moyo uliopondeka tutembee kwa unyenyekevu na kujishusha mbele za Mungu aliye hai.

Na Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye hekima

Tafadhali naomba maoni yako 0718990796

Jumapili, 21 Julai 2024

Utamlilia Sauli hata lini?


1Samuel 16:1-3 “Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe. Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi Bwana akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea Bwana dhabihu. Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako.”


Utangulizi:

Kaka zangu dada zangu Leo tutachukua muda kiasi kutafakari ujumbe wa Muhimu wenye kichwa “Utamlilia Sauli Hata lini?” Kama tulivyosoma katika kifungu cha msingi, ujumbe huu una maana kubwa na zaidi sana leo unatufundisha umuhimu wa kusahau mambo yaliyopita ambayo kimsingi yanaweza kuwa kikwazo cha kutupeleka katika mambo mapya au hatua nyingine ambayo Mungu ametuandalia. Wote tutakuwa tunakumbuka kuwa Mungu alimfunulia Samuel Nabii kuhusu Mfalme Mpya wa Israel na kumuagiza akampake mafuta.

1Samuel 9:15-17 “Basi Bwana alikuwa amemfunulia Samweli, siku moja kabla Sauli hajamwendea, akisema, Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikilia.Hata Samweli alipomwona Sauli, Bwana akamwambia, Huyu ndiye niliyekuambia habari zake; huyu ndiye atakayewamiliki watu wangu.”                

Pamoja na kuwa ni kweli Sauli alikuwa ni chaguo la Mungu, Na Samuel alimtia mafuta Lakini ulifika wakati ambapo Mungu alikuwa na mpango mwingine, na hivyo alimkataa Sauli na kumtaka nabii Samuel ampake mafuta Mfalme mwingine mwenye nguvu zaidi na mwenye kuupendeza moyo wake na aliye mwema kuliko Sauli, Mfalme huyo alikuwako Bethelehemu katika nyumba ya Yese. Kukataliwa kwa Sauli kuliwekwa wazi mapema kwa neno la kinabii ona;-

1Samuel 15:26-28 “Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la Bwana, Bwana naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli. Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka. Basi Samweli akamwambia, Leo Bwana amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe

Hata hivyo Samuel kama nabii inaonekana aliendelea Kumuombea neema Saul kwa majuma kadhaa, alimpenda, alitamani aendelee kuwa naye, ilikuwa ni tabia ya Samuel kuwaombea wana wa Israel na mfalme pia kwa mujibu wa maandiko Samuel kuacha kuwaombea Israel kwake ilikua ni kama kufanya dhambi

1Samuel 12:23 “Walakini mimi, hasha! Nisimtende Bwana dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka

Kwa hiyo huenda Samuel aliendelea kumuombea Sauli kwa Mungu,  na hakuacha alisikitika moyoni kumpoteza kijana yule mzuri aliyemtia mafuta yeye mwenyewe shujaa, mtu mrefu Mzuri kutoka kabila la Benjamin lakini Mungu aliyakataa maombi ya Samuel kwa sababu alikuwa amekusudia kuwapa Israel Shujaa, kijana mzuri zaidi, anayeupendeza Moyo wa Mungu mtu aliye mwema na atakayekuwa bara kubwa kwa Israel, Hivyo Mungu alimkemea Samuel na kumuuliza utaendelea kumlilia Sauli mpaka lini ikiwa mimi nimemkataa, inawezekana ikawa ni stori nzuri sana na imenyooka haiitaji tafasiri yoyote, lakini leo hii katika kisa hiki, Mungu anataka kusema nasi kuhusu swala la kuachilia Mambo ya kale  ili aweze kutuingiza katika mambo mapya, hupaswi kukaa chini na kuyalilia mambo yaliyopia hata kama ni mazuri kiasi gani kwani kuyalilia hayo kunatufanya tusipige hatua katika kuuendea ukurasa mpya ambao Mungu anataka uufungue, ili tukue na kuelekea katika kiwango kingine, Tutajifuza somo hili Utamlilia Sauli Hata lini kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-


·         Umuhimu wa kusahau yaliyopia.

·         Umuhimu wa kutambua mapenzi ya Mungu.

·         Utamlilia Sauli hata lini?.


Umuhimu wa kusahau yaliyopita.

1Samuel 16:1 “Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.”

Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu anapokuwa na mpango mpya katika maisha yetu, anapenda tuelewe na kusonga mbele na kuyasahau yaliyopita, siku zote kuendelea kulia lia kwaajili ya mambo ya zamani kunaweza kutuzuia kuona yale mapya ambayo Mungu ametuwekea mbele yetu, na siku zote mbele ni kuzuri zaidi, kwa hiyo ni lazima tuukubali kusahau yaliyopita, ni vigumu sana wakati mwingine kusahau yaliyo nyuma na wakati mwingine inaonekana kama ni jambo lisilowezekana lakini historia ya nyuma inaweza kuwa kikwazo kikubwa cha mpango na mapenzi ya Mungu kwaajili yetu na kwa sababu hiyo ni lazima tuyachuchumilie yaliyo mbele na kukubali kusahau yote yaliyopita.

Wafilipi 3:13-14 “Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.”

Paulo mtume aliyepitia dhiki na mateso mengi sana Hakubali hata kidogo kukaa katika hayo lakini wakati wote alikuwa akijitahidi kuwaza mbele, Ni mapenzi ya Mungu kwetu kusahau mambo yaliyopita hususani yale ambayo yametuletea maumivu makubwa katika maisha yetu,  au makosa amkubwa ambayo tumewahi kuyafanya huko nyuma, Mungu mwenye rehema na neema wakati wote hutupa nafasi ya pili, na ya tatu na ya nne na ya tano na ya sita na ya saba na ya nane na kadhalika yeye anatutaka wakati wote tusilie kwaajili ya yaliyopita na badaa yake tusonge mbele bila kujali kile ulichokipitia, iweni talaka, au uonevu, au umepoteza kazi, au umeingia katika changamoto zozote nzito, au umekosea sana, au umefiwa au ulifeli vyovyote vile Mungu anatutaka tusonge mbele na kuacha kumlilia Sauli kwa sababu ana mpango mpya nawe, Mwana riadha wakati wote anapaswa kuangalia mbele, na kuendelea na mbio, kwani kuangalia nyuma kunaweza kuwa kikwazo, kwa msingi huo usipoteze muda na maswala yaliyopita yawe mazuri au mabaya wewe angalia mbele, Mungu anayekuwazia mema na mpango mpya!

Isaya 43:18-19 “Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.”

Ilikuwa ngumu kwa Samuel kuacha kumlilia Sauli, kwa kuwa alikuwa Mfalme Mzuri na alipewa na Mungu, Lakini sasa Mungu ana mpango mpya ulio bora zaidi, kwa hiyo, yuko Daudi mwana wa Yese kwaajili yako hivyo sahahu utawala na ufalme uliopita chukua chupa yako umtie mafuta yule ambaye Mungu atakuelekeza     

Umuhimu wa kutambua mapenzi ya Mungu

Mungu alikuwa na mpango mpya kwaajili ya Israel Kama alivyo na mpango mpya kwaajili yako, Mungu alikuwa amechagua mmoja wa wana wa Yese na alikuwa yuko tayari kumpaka mafuta Ili atawale baada ya Sauli na ulikuwa ni wajibu wa Samuel kwenda Bethelemu na Chupa yake ya mafuta  na kumtia mafuta yule ambaye Mungu alikuwa amemkusudia, hapa ulikuweko mtihani wa kuyajua mapenzi ya Mungu na ulikuwepo mpango unaohitaji subira, wakati huo ni lazima tuaachane na mambo tuliyoyazoea kwa sababu Mungu ana mpango mpya, sauti zinaweza kuwa nyingi sana wakati tunauendea mpango mpya wa Mungu na tunaweza kufikiri kuwa ni huu au ule  lakini hatimaye Mungu atakufunulia mpango wake kamili ambao huo Yesu yumo ndani yake, The best is yet to come !

1Samuel 16:6-11 “Ikawa walipokuja, alimtazama Eliabu, akasema, Yakini masihi wa BWANA yupo hapa mbele zake. Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo. Ndipo Yese akamwita Abinadabu, akampitisha mbele ya Samweli. Naye akasema, Bwana hakumchagua huyu. Ndipo Yese akampitisha Shama. Naye akasema, wala Bwana hakumchagua huyu. Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa. Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama, anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese, Tuma watu, wamlete; kwa sababu hatutaketi hata atakapokuja huku.”            

Kujua mapenzi ya Mungu kwaajili ya mpango mpya sio kazi nyepesi, ilimsumbua Samuel ilimsumbua Yese, hawakujua mfalme mpya ni nani, na kwakuwa hakuwepo pale walihitaji subira, tunahitaji subira kuyajua mapenzi ya Mungu, Katika maisha yetu tunaweza kukutana na changamoto kama hizi, wakati huu tunapaswa kuongeza uwezo wa kuisikia sauti ya Mungu, na kuwa na moyo wa Subira, ili kuachana na mazoea na kuyajua mapenzi yake kwa hiyo kuna umuhimu wa kuyatambua mapenzi ya Mungu, kuna mambo matatu tu tunaweza kuyafanya wakati huu

1.       Kujaza pembe Mafuta – hii inahusiana na kufanya maandalizi ya kiroho kwa hiyo ni muhimu kwetu kujitoa kwa Roho Mtakatifu, kwa kuomba na kujitakasa na kutubu, tendo hili litatuweka karibu na Roho Mtakatifu  na kutusaidia kuijua sauti yake  na zaidi ya yote inatusaidia kuyatii mapenzi yake na kuyajua

 

1Samuel 16:4-5  “.Samweli akafanya hayo aliyosema Bwana, akaenda Bethlehemu. Wakaja wazee wa mji kumlaki, wakitetemeka, nao wakasema, Je! Umekuja kwa amani? Naye akasema, Naam, kwa amani; nimekuja kumtolea Bwana dhabihu; jitakaseni; njoni pamoja nami kwenye dhabihu. Akawatakasa Yese na wanawe, akawaita kwenye dhabihu

 

Matendo 13:1-3 “Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.”

 

2.       Kutii maagizo ya Mungu – Samuel alitii maagizo ya Mungu na kukubalia kumsahau Sauli na akaenda kwa Yese ili kumtia mafuta Daudi, Tunapaswa kuyatii maagizo ya Mungu na kusonga mbele bila kuchelewa, ni muhimu kufahamu kuwa mambo ya zamani yanakamata sana na yanataka kuturudisha nyuma, Lakini Mungu ameruhusu tusonge mbele kwa hiyo hatuna budi kwenda pale Mungu anaposema twende Samuel akafanya hayo aliyoyasema Bwana, akaenda Bethelehemu kule Bwana atakakosema wende nenda na yale maagizo ambayo Bwana amekuagiza kuyafanya yafanye kwa kutumia Hekima chini ya neema yake.

 

3.       Ruhusu Mpango mpya wa Mungu -  Samuel na Yese walikubali mapenzi ya Mungu, alipokuja yeye aliyesubiriwa na asiyetazamiwa Samuel alimtia mafuta kwani Bwana alisema naye huyu ndiye, kwa hiyo walilazimika kumsahau Sauli na kumkubali Daudi, Mambo ya zamani ambayo hayana nafasi tena katika maisha yetu na ambayo hayako katiika mpango wa Mungu ni lazima tuyafukuzilie mbali, ili lile jipya ambalo Mungu amekusudia kulifanya liweze kuchukua nafasi.

 

1Samuel 16:12-13 “Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. Bwana akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye. Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.”                

Utamlilia Sauli hata lini?

Utamlilia Sauli hata lini? Ni swali ambalo Mungu alimuuliza Samuel na ni swali ambalo linatuita katika kutafakari maisha yetu, Je kuna jambo bado unalishikilia? bado una shikilia mambo ya zamani ambayo Mungu anataka tuyaache na kuyasahau? Je unajiandaa kwa mambo mapya?  Tunapotulia katika maombi hatuna budi kuendelea kumuomba Mungu atuongoze na kutuandaa na kutuweka tayari ili tukubali kuyatii mapenzi yake, na kupokea kile kipya ambacho Mungu amekikusudia katika maisha yetu  na Mungu ni mwema atakutendea mema usilie!

Kuacha mambo ya zamani kunahitaji ujasiri, na Imani, Samuel alihitaji ujasiri na kukubali mabadiliko kwa Imani, kwa sababu Mungu alimthibitishia kuwa ana mpango bora zaidi kwaajili ya Israel Mpango wenye manufaa sio kwaajili ya Israel tu  bali kwa ulimwengu mzima, Mungu alikuwa amemkusudia mwana wa Daudi kuja kukaa katika kiti cha Enzi milele na huyo ni Yesu Kristo, uwepo wa Mungu uko mbele, Mungu alikuwa amekwisha kumuacha Sauli na sasa Roho Mbaya ilikuwa inamkalia, Mahali ambapo uwepo wa Mungu umeondoka, Shetani na mapepo huchukua nafsi

1Samuel 16:14-15. “Basi, roho ya Bwana ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua. Nao watumishi wa Sauli wakamwambia, Angalia, sasa roho mbaya kutoka kwa Mungu inakusumbua.”

Mungu alikwisha ondoa uwepo wake kwa Sauli na kuruhusu mashetani kumkalia, Mungu anapotushauri jambo ni vema kwenda nalo, kwa kuwa huko ndiko uwepo wake unakokwenda hatupaswi kujivunia Sauli tena kwani sasa ni nyumba ya mapepo na uwepo wa Mungu umehama, uwepo wa Mungu sasa ulikuwa uko juu ya Daudi kwa nguvu!

1Samuel 16:13 “Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.”

Acha kulilia ya nyuma Songa mbele Mungu anampango mwema zaidi msahau Sauli, Mungu anaye Daudi wako je utaendelea kumlilia Sauli hata lini ikiwa mimi nimemkataa? Uwepo wa Mungu uko mbele!, Usilie kwaajili ya kazi uliyofukuzwa, usilie kwaajili ya nyumba uliyohama, usilie kwaajili ya mchumba ambaye ameondoka, usilie kwaajili ya mke aliyekuacha, usilie kwaajili ya mume aliyekuacha, usilie kwaajili ya bosi aliyekuacha Mungu anao mpango mwingine kwaajili yako, usilie kwaajili ya uhamisho uliohamishiwa kuna kusudi kubwa na jipya kwaajili ya Mungu. Na Kwaajili yako na familia yako na watu wako!

1Wafalme 9:5 “ndipo nitakapokifanya imara kiti cha ufalme wako juu ya Israeli milele; kama nilivyomwahidia Daudi, baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Israeli.”

Na Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!.