Jumanne, 11 Aprili 2023

Naona Kiu - Nina kiu!

 

Yohana 19:28-30 “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, NAONA KIU. Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani. Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.”


Utangulizi

Hivi karibuni Wakristo wote duniani tunaingia katika moja ya Majuma muhimu sana katika kukumbuka mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo ambaye aliteseka na kufa kwaajili yatu pale msalabani, Katika wakati huu moja ya maswala ya msingi ambayo huwa tunayakumbuka kwa Pamoja ni pamoja na maneno ya Yesu Kristo pale Msalabani wakati alipokuwa anateseka, kwa ujumla katika injili zote nne unapokusanya maneno yote aliyoyatamka Yesu kabla kidogo ya kukata roho ni Pamoja na maneno haya saba ya mwisho ambayo wakristo huyachukulia kwa uzito mkubwa, Moja ya maneno ambayo tutayatafakari kwa pamoja leo ni pamoja na neno Naona kiu, au Nina kiu,ambalo ni neno la tano katika manenio hayo muhimu, Pamoja na neno hili, lakini maneno yote saba aliyozungumza Kristo ni Pamoja na :-

1.       Baba uwasamehe kwa maana hawajui walitendalo Luka 23:34

2.       Amin nakuambia leo hii utakuwa pamoja nani peponi Luka 23:43

3.       Mama tazama mwanao, mwana tazama mama yako Yohana 19:26-27

4.       Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha Mathayo 27:46

5.       Naona kiu au Nina kiu Yohana 19:28

6.       Imekwisha Yohana 19:30

7.       Baba mikononi mwako naiweka roho yangu Luka 23:46

Tutajifunza somo hili Naona kiu au Nina kiu kwa kuzingatia maswala mawili ya msingi yafuatayo:-

·         Maana ya neno KIU

·         Naona kiu

Maana ya neno Kiu.

Neno kiu kwa kiingereza THIRST ni hali ya  kuhisi au kutaka kunywa kitu Fulani na hasa maji, ni Hali yenye msukumo wenye nguvu wa kutaka kutimiza kitu au jambo Fulani, hali hii wakati mwingine kama ni katika mwili wa mwanadamu inatokana na umuhimu wa mwili kuhitaji maji, kutokana na umuhimu wake na pia kutokana na joto au ukavu Fulani unaojitokeza katika mwili, Neno hilo Kiu katika biblia ya kiyunani linasomeka kama “DIPSAO” kimatamshi  “DIP – SAH – O” Ambalo maana yake kiu halisi au kiu ya jambo Fulani  (to thirst for LITERALLY or FIGURATIVELY) Kwa hiyo Yesu alipozungumza kuhusu kiu kimsingi inaweza kuwa ilikuwa kiu halisi ya kutaka kunywa maji au kiu ya kutaka kuyatimiza mapenzi ya Mungu, nani wazi kuwa kiu aliyokuwa nayo Yesu haikuweza kutimizwa na dunia kwani badala ya kumpa maji wao walimpa divai, na sifongo jambo lililopeleka Yesu kutokunywa, kwa kuwa hiyo haikuwa kiu yake sahihi, Leo tunapotafakari kiu aliyokuwa nayo Yesu Msalabani ni Muhimu kula mmoja wetu kujihoji ana kiu  ya namna gani na je kiu yake inaweza kutimizwa na dunia au inaweza kutimizwa na Mungu? Kiu ya Yesu ilitimizwa na Mungu na haikuweza kutimizwa na wanadamu! Marko 15:23 “Wakampa mvinyo iliyotiwa manemane, asiipokee.” Kile alichokitamani Kristo katika shauku na kiu yake hakikuwa kile ambacho dunia imempa, Mungu atupe neema ya kuweza kutimiza kiu sahihi tuwapo ulimwenguni katika jina la Yesu!

Naona kiu!

Yohana 19:28 “Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.”   

Moja ya namna ya kuadhimisha Pasaka ni pamoja na kukumbuka Mateso na siku ya mateso ya Bwana wetu Yesu ambayo yametuletea ukombozi, katika siku ile ya mateso Kristo alizungumza maneno Saba muhimu sana katika maisha ya kila Mwanadamu, Katika maneno hayo saba Neno Noana kiu ndio neno la Msingi sana na kiini kikubwa sana cha Mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo na katika uhitaji wa Mwanadamu wakati tunapopitia mateso kutoka kwa wanadamu wenzetu huku tukiwa na lengo la kudumisha uhusiano wetu na Mungu!, Hapo ndipo Kiu ya kila jambo tulilonalo inapokutana na shida na changamoto mbalimbali,  maneno yote sana yana umuhimu wake na kila moja lina ujumbe wake ingawa leo tutalipa uzito neno la Tano NAONA KIU ;-  bila kupuuzia jumbe katika maneno mengine:-

1.       NENO LA MSAMAHA – Tunapopitia katika wakati Mgumu hasa unaosababishwa na wanadamu wenzetu hatuna budi kufahamu kuwa wakati huo wao wanaona kuwa wako sahihi katika lile wanalokufanyia nan i wewe ndio unaonekana kuwa mkosaji, wakati hio wao huwa dhaifu sana na wewe unayepelekwa matesoni ndio unapaswa kuonyesha ukomavu hivyo kwaajili ya mafanikio Yako samahe – Baba uwasamehe kwa maana hawajui walitendalo

2.       NENO LA UHAKIKA – Wakati tunapopitia mateso tunapaswa kukumbua ya kuwa wako watu wanaoona umuhimu wetu, na bado wanatutegemea wana wanapaswa kuhakikishiwa kuwa wanakuwa na wakati mzuri hata pamoja na kuteseka kwetu au kuteseka pamoja nao, wahakikishie ya kuwa Mateso ni njia ya kutupeleka katika hali iliyo bora zaidi – Leo hii utakuwa pamoja nani peponi

3.       NENO LA HESHIMA – Wako wale wanaodhalilika unapodhalilika, wako wanaoteseka unapoteseka wako wanaokutegemea ni muhimu kwetu kufahamu kuwa Yesu alikuwa anategemewaa na Ndugu zake na wazazi wake, wakati akiwa katika mateso alitaka kuhakikisha kuwa wazazi wake wanakuwa salama na hivyo alikabidhi Majukumu ya usimamizi wa familia kwa mwanafunzi aliyeaminika kuwa anaweza kumsaidia – Mama tazama mwanao, mwana tazama mama yako

4.       HALI YA UPWEKE – Kila mwanadamu anahitaji kuwa na watu wa kumtia moyo, upweke ni moja ya changamoto kubwa sana kwa mwanadamu hasa anapokuwa mtu mzima lakini zaidi sana tunapopitia katika mateso, wanadamu kwa kawaida hudhani ya kuwa Mungu amemuacha  hsusani anapopita katika magumu au anapokuwa amelemewa na dhambi, - Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha

5.       NAONA KIU – kiu inawakilisha kiini kikuu cha mateso, kila mwanadamu anateseka kwa sababu ya kiu, kila mwanadamu ana kiu anayotaka kuiona inatimizwa katika maisha yake, Kwa bahati mbaya wakati mwingine kiu zetu huharibiwa na watu wenye nia mbaya ambao wanataka kuona kiu yetu ikitimizwa kwa mlango mwingine, Yesu Kristo katikati ya mateso na katika kilelel cha mateso alijisikia kiu bila shaka ilikuwa ni kiu nzuri kiu ya maji safi lakini tunaambiwa watesi walimpa siki badala ya maji, jambo lililopelekea yeye kukataa kunywa Mathayo 27:33-34 “Na walipofika mahali paitwapo Golgotha, yaani, Fuvu la kichwa, wakampa kunywa divai iliyochanganyika na nyongo; lakini yeye alipoionja hakutaka kunywa.” Dunia haita kubali utimize kiu yako, na wakati mwingine utapewa  kitu mbadala kinyume na kiu yako, na kama kiu yako imetoka katika kwa Mungu ni dhahiri kuwa dunia haitakubali uitimize kiu hiyo na badala yake watataka unywe kitu kingine Kiu ya Kristo ilikuwa ni kuwakomboa wanadamu na kuona kuwa watu wote wanaishi kwa amani huku yeye akiwa ni mfalme wa amani, lakini badala yake Dunia ilimfanyia mambo mengine, katika wakati huu tulio nao ni lazima tuwe wakali ili kwamba kiu yetu sisitimizwe kwa njia nyingine, Mapenzi ya Mungu yasikataliwe, Baraka za Mungu zisigeuzwe kuwa laana,

-          Wengi walikuwa na kiu ya kuolewa na kuoa ili wawe na amani katika ndoa zao lakini dunia imewapa machungu badala ya amani

-          Mungu alikusudia tuishi kwa furaha na amani lakini leo hii dunia imewapa vilio na mateso kiu yao ya kuwa na furaha duniani imeharibiwa badala ya maji wamepewa sifongo

-          Wengi wamelima na kupanda wakitarajia mvua itanyesha wapate mazao, lakini dunia imewanyima mvua na imawapa ukame na hali ya uchumi imakuwa sio

-          Mungu alikusudia dunia iwe kama paradiso ka ma watu wangeitunza lakini watu wameharibu mazingira  na hatimaye leo dunia inashuhudia mabadiliko mabaya ya hali ya hewa na ukiharibika kwa anga linalozuia miali mikali ya jua kutufikia moja kwa moja Ozone layer, kuongezeka kwa hewa ya ukaa na hali joto ma mabadiliko makubwa

-          Dunia ilitarajiwa iwe ni sehemu ya ustaarabu, uadilifu na yenye kutunza utamaduni lakini leo tunashuhudia uharibifu mkubwa wa ustaarabu na mmomonyoko mkubwa wa uadilifu, kuharibika kwa tamaduni zenye manufaa na badala yake dunia leo inataka kuwe na ndoa za jinsi moja na kuzalishwa kw agenda ya tatu isiyo ya kiume wala ya kike, Haya pamoja na mambo mengine ni uharibifu wa kiu ya Yesu Kristo unaofanywa na wanadamu

-          Mungu alikuwa na kiu ya kuona haki ikitendeka na dunia ikifanikiwa kila mahali, maana haki huinua taifa lakini dhambi ni aibu ya taifa zima, leo hii wote tunashuhudia haki ikipindishwa kwa rushwa na upendeleo na hukumu zikipotoshwa huo nao ni uharibifu wa kiu ya Mungu

-          Wewe una kiu gani na dunia imekupa maji ya namna gani? Hatuna bhudi kujiweka katika neema ya Mungu na kumuomba Mungu atufanikishe ili kiu yetu na kiu yake isiharibiwe katika maisha yetu tuwapo duniani

6.       KILIO CHA USHINDI – Imekwisha, Yesu alitimiza majukumu yake yote duniani kwa ushindi mkubwa TETELESTAI  Neno hili Imekwisha TETELESTAI limetokana na neno TELEO la kiyunani ambalo maana yake ni Kukamilisha kazi, kumaliza kazi, kutimiza kazi, to complete or to accomplish, kila mmoja wetu analo jukumu la kutimiza awapo duniani

7.       KILIO CHA UTII – baba mikononi mwako naiweka roho yangu, Yesu alitii mambo yote ambayo Mungu alikuwa amemuagiza ayatende, usikubali kuondoka duniani bila kutimiza ndoto ambazo Mungu amekukabdihi uzitimilize

Hitimisho!

Kwa hiyo unapoangalia maneno haya saba ya Bwana wetu Yesu Krist utagundua kuwa yote yana umuhimu mkubwa sana lakini neno la tano lina umuhimu mkubwa sana katika swala zima la matarajio ya mwanadamu na kile ambacho dunia inatupa kwa msingi huo basi usalama wetu na kutimia kwa kiu yetu vinaweza kupatikana kwa Mungu mwenyewe

-          Mathayo 5:6 “Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa” Kama kiu yetu itakuwa ni ya haki na bila shaka hii ni kiu yenye kutaka kuyatimiza mapenzi ya Mungu basi kiu hiyo itatimizwa

-          Yohana 7: 37 “Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.”  Yesu anatoa mwaliko wa kila mtu mwenye kiu aje kwake anywe unaona ni dhahiri kama kiu aliyoisema Yesu ingekuwa kiu HALISI literal Maandiko yasingeweza kuzungumza katika hali kama hii haba ni uhitaji wote wa kimwili na Kiroho Dunia haiwezi kututimizia kiu halisi tuliyo nayo Lakini Yesu anaweza na ametyuahidi kuwa atatimiza hivyo kiu yetu atatupa maji halisi tunywe

Ni maombi yangu kwako katikka pasaka hii kuwa Mungu akutane na kiu yako hamu yako na shauku yako inaweza kutimizwa na Yesu aliyegharimika kufa kwaajili yako pale Msalabani

Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima!


Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?

 

Mathayo 27:46 - 49. “Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Na baadhi yao waliohudhuria, waliposikia, walisema, Huyu anamwita Eliya. Mara mmoja wao akaenda mbio, akatwaa sifongo, akaijaza siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha. Wale wengine wakasema, Acha; na tuone kama Eliya anakuja kumwokoa.”


Utangulizi:

Leo tutachukua Muda kujifunza kwa undani mojawapo ya maneno Muhimu katika maneno yaliyosemwa na Yesu Kristo wakati wa Mateso yake pale msalabani MUNGU WANGU MUNGU WANGU MBONA UMENIACHA, tunataka kujifunza maana ya maneno haya kwa kina na kuangalia uhalisia wa ubinadamu hususani wakati wanadamu wanapopitia mateso, Pamoja na menono haya muhimu, tutakayoangalia leo maneno mengine kwa mfululizo katika maneno saba aliyozungumza Kristo pale msalabani kwa mujibu wa injili zote nne ni pamoja na :-

·         Baba uwasamehe kwa maana hawajui walitendalo Luka 23:34

·         Amin nakuambia leo hii utakuwa pamoja nani peponi Luka 23:43

·         Mama tazama mwanao, mwana tazama mama yako Yohana 19:26-27

·         Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha Mathayo 27:46

·         Nina kiu Yohana 19:28

·         Imekwisha Yohana 19:30

·         Baba mikononi mwako naiweka roho yangu Luka 23:46

Maana ya Maneno Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha?

Mathayo 27:46 “Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”

Ni muhimu kufahamu kuwa Mwandishi wa kitabu cha Mathayo anajaribu tu kufupisha kile ambacho Yesu Kristo alikisema na pia anajaribu kutafasiri lugha kiaramu ambayo Yesu aliitumia wakati anazungumza maneno hayo. Maneno hayo Eloi, Eloi, Lamasabakthan, katika lugha ya asili yanasomeka kama Eli, Eli, Lama Sabachthan ni sehemu ya maneno kamili ambayo Yesu aliyazungumza ka lugha ya kiaramu, maneno hayo yanatafasirika hivi Eli, (Adonai) Eli (Adonai) Lama (Why?) kwanini ?, mbona? Sabachthani (You have left, Abandoned) me) Umeniacha.  Kimsingi ni kuwa katika kini cha mateso yake Yesu Kristo alikuwa anatimiza na kumuomba Mungu sawa na Zaburi ya 22:1-22 ambapo katika Zaburi hii Daudi ambaye alipendwa sana na Mungu alikuwa akimuomba Mungu kutokana na Mapito aliyokuwa akiyapitia ambayo kimsingi pia yalikuwa ni mapito ya kinabii yaliyohusiana na Yesu Kristo Mwenyewe Mwana wa Daudi, Kumbuka kuwa Yesu alikuja kutimiza maandiko ambayo torati na manabii na maandiko yote yaliweka bayana kuwa Masihi hana budi kuteseka 

Luka 23:13- 27 “Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. Macho yao yakafumbwa wasimtambue. Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao. Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote; tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha. Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo; tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema, wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai. Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona. Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.”

Unaona kimsingi Yesu alikuwa ameandikiwa kila atakalokuja kulitenda na kulinena katika Torati, Manabii na Zaburi au maandiko hivyo Neno Mungu wangu Mungu wangu ilikuwa ni nukuu ya Zaburi ya 22 ambayo ina mukhtasari wa Mateso ya Bwana Yesu yaliyotabiriwa na Daudi katika zaburi hiyo hebu tuyaangalie tuweze kuona 

Zaburi 22:1-20 “Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu? Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu Na wakati wa usiku lakini sipati raha. Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli. Baba zetu walikutumaini Wewe, Walitumaini, na Wewe ukawaokoa. Walikulilia Wewe wakaokoka, Walikutumaini wasiaibike. Lakini mimi ni mdudu wala si mtu, Laumu ya wanadamu na mzaha wa watu. Wote wanionao hunicheka sana, Hunifyonya, wakitikisa vichwa vyao; Husema, Umtegemee Bwana; na amponye; Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye. Naam, Wewe ndiwe uliyenitoa tumboni, Ulinitumainisha matitini mwa mama yangu.  Kwako nalitupwa tangu tumboni, Toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu. Usiwe mbali nami maana taabu i karibu, Kwa maana hakuna msaidizi. Mafahali wengi wamenizunguka, Walio hodari wa Bashani wamenisonga; Wananifumbulia vinywa vyao, Kama simba apapuraye na kunguruma. Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya mtima wangu. Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenizua mikono na miguu. Naweza kuihesabu mifupa yangu yote; Wao wananitazama na kunikodolea macho. Wanagawanya nguo zangu, Na vazi langu wanalipigia kura. Nawe, Bwana, usiwe mbali, Ee Nguvu zangu, fanya haraka kunisaidia. Uniponye nafsi yangu na upanga, Mpenzi wangu na nguvu za mbwa.”

Kimsingi maombi ya Daudi na Maombi ya Yesu Kristo yanafanana na hatujawahi kuona wakati wowote Mungu akimuacha Daudi au akimuacha Yesu Kristo lakini kwanini walilia maneno hayo na kuomba dua hizo wakati wa mateso yao ilihali wote tunajua kuwa maandiko yanamsifia Daudi kama mtu aliyeupendeza Moyo wa Mungu ona

Matendo 13:22 “Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote.”

Aidha katika namna kama hiyo Mungu katika neno lake vilevile anajivunia Kristo Yesu mwanae kama mtu aliyeupendeza moyo wake ona

Mathayo 3:16-17 “Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.”

Inawezekanaje Mungu kuwaacha awapendao? Mungu anatujali sana katika kiwango ambacho hata mama anaweza kumsahau mtoto wake lakini sio Mungu wetu ona

Isaya 49:15-16 15. “Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe. Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima. Kimsingi kila mwanadamu anapokuwa na mafanikio watu”               

Mungu wetu anatujali mmno lakini katika hali ya kawaida kila mwanadmu anapopitia mateso na changamoto za aina mbalimbali kwa kawaida wanadamu wana tabia ya kuwa mbali nawe wanatabia ya kukuacha ubaki peke yako na wakati huu Mungu hukaa kimya ili mateso yale yaweze kuleta somo linalokusudiwa kwako hivuo kibinadamu zinakuweko fikra ya kuwa huenda Mungu amekuacha, Ayubu alipokuwa na mafanikio makubwa sana tunaambiwa watu wengi sana walimwendea na nyumba yake ilijaa watu wa kila aina maandiko yanasema na watu wa nyumbani wengi sana ona

Ayubu 1:3 “Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, NA WATU WA NYUMBANI WENGI SANA; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.”

Tunaambiwa kuwa wakati wa mateso yake Ayubu watu wote waliokuwa nyumbani mwake walimkimbia mpaka pale Ayubu alipobarikiwa tena ndio tunaelezwa kuwa watu wote wakamwendea ona

Ayubu 42:10-12 “Kisha Bwana akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; Bwana naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza. Ndipo wakamwendea nduguze wote, waume kwa wake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakamlilia na kumtuza moyo katika habari za huo uovu wote Bwana aliouleta juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja. Basi hivyo Bwana akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng'ombe elfu, na punda wake elfu.”

Ni swala la kawaida kwamba wakati wa mateso watu wanakukimbia na mara kadhaa inadhaniwa kuwa Mungu amekuacha nani kilio cha kawaida Pale mtu anapopita katika magumu kufikiri mkuwa ni Mungu ndiye aliyemtendea hayo, Ndio maana Daudi alilia katika Zaburi ya 22 japo ilikuwa pia ni unabii kw Mwanaye Yesu Masihi ambaye naye alilia akijua ya kuwa anaitimiza Zaburi ya 22 yote alitioandikiwa humo yalitokea siku ya mateso yake maneno mabaya , kugawanywa kwa nguo zake kwa kuzipigia kura, kugomelewa mikono yake na miguu yake msalabani, kudharauliwa na kuwekwa katika mikono ya watu wabaya wapate kumdhihaki, na kumdhalilisha, Kifo cha Msalabani hakikuwa kifo cha kawaida kilikuwa ni kifo cha maumivu ya kila aina kisaikolojia na nafsi na mwili Yesu ni kama alikuwa amabaki pake yake msalabani, saa ya kujaribiwa huwa ni kama tunabaki peke yetu, kundi kubwa la watu waliofaidika na huduma yake hakuna hata mmoja aliyeweza kusogea na kufanya utetezi wakati Masihi alipokuwa anateseka Msalabani na ndio maana akaisema zaburi ya 22 ambayo hutambulika zaidi kwa Mstari wake wa kwanza Mungu wangu Mungu wangu mbiona umeniacha!

Msalabani Yesu hakuwa ametundikwa kwa sababu nya dhambi yake ilikuwa ni kwaajili ya dhambi zetu mimi na wewe, nani mimi na wewe ndio ambao tulipaswa kuyabeba maumivu yale, lakini Mwokozi alibeba kwa niaba yetu na kilio kilikuwa kwa ajili yetu na ubinadamu wetu, alilia kuonyesha kuwa wanadamu wakati wote tunahitaji msaada wa Mungu na kuwa peke yetu hatuwezi, adui yetu yu aweza kufanya jambo lolote la kutuumiza sana kama tutabaki bila msaada wa Mungu, Mtu mmoja aliimba wimbo unasema nafikiria ukiniacha roho yangu itakuwaje Bwana ? itakuwa ni mawindo ya adui kwa wepesi sana… wakati wote tunapokuwa na maisha yetu bila ya Mungu tunajiweka katima hatari ya kushambuliwa na kuumizwa na ibilisi, magonjwa matesi na dhiki za dunia hii, lakini ashukuriwe Mungu kuwa pale msalabani Yesu Kristo alikuwa anateseka kwaajili yatu na kwaajili ya ukombozi wetu ili kuukaribisha uwepo wa Mungu katika maisha yetu

Isaya 53:4-5 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.”

Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!


Mama tazama mwanao


Yohana 19:26-27 “Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.”


Utangulizi

Moja ya maneno saba aliyoasema Bwana Yesu pale msalabani ni Pamoja na Maneno haya Mama tazama mwanao, neno hili ni moja ya neno Muhimu sana linalotukumbusha wajibu wetu Muhimu sana wa kuhakikisha kuwa wazazi wetu na jamii yetu na familia zetu zinajengewe uhakika wa maisha ya baadaye hata pale wakati sisi tunapokuwa hatupo, leo tutachukua muda kujifunza kwa undani kwa kina na mapana na marefu kuhusiana na maana ya maneno haya, hata hivyo ni muhimu kama ilivyo kwa masomo yote ya mfululizo wa maneno saba ya Kristo pale Msalabani kujikumbusha maneno yote sana kwa mfululizo wake kisha tutaendelea na uchambuzi wa neno husika leo, Maneno yote sana ya Msalabani ni pamoja na :-

·         Baba uwasamehe kwa maana hawajui walitendalo Luka 23:34

·         Amin nakuambia leo hii utakuwa pamoja nani peponi Luka 23:43

·         Mama tazama mwanao, mwana tazama mama yako Yohana 19:26-27

·         Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha Mathayo 27:46

·         Nina kiu Yohana 19:28

·         Imekwisha Yohana 19:30

·         Baba mikononi mwako naiweka roho yangu Luka 23:46

Tutajifunza somo hili, Mama tazama mwanao kwa kuzingatia maeneo makuu matatu yafuatayo:-

*      Utata kuhusu Ndugu wa Yesu Kristo

*      Kwa nini Mariam mikononi mwa Yohana ?

*      Mama tazama mwanao

Utata kuhusu Ndugu wa Yesu Kristo.

Yohana 19:26-27 “Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.”

Kabla ya kuzungumzia umuhimu na maana ya maneno ya Bwana Yesu ya awamu ya tatu Mama tazama mwanao… Ni muhimu kwanza tukaondoa utata wa kitheolojia unaotoka na msimamo wa kanisa katoliki na msimamo wa makanisa ya kipentekoste kuhusu Maana ya mstari huu!

Katika mtazamo wa kikatoliki wao wanajenga hoja ya kuwa mstari huu wa Yesu akiwa msalabani kumwambia Mama tazama mwanao Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama mama yako, Na tangu saa ile Mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake, ni suhahidi wazi kuwa Mariamu hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu, wakatoliki wanajenga hoja kuwa ni jambo la kushangaza kumuona Yesu akimkabidhi mama yake kwa Mtu mwingine mbali na watoto wake mariamu kama mama huyo angelikuwa na watoto wengine kwa hiyo kwao mstari huu ni ushidi ulio wazi kuwa Mariamu hakuwa na watoto wengine tofauti na wapentekoste wanavyodai!

Katika mtazamo wa kipentekoste ni wazi na dhahiri kuwa kulikuwepo sababu maalumu za Yesu kumkabidhi mama yake Kwa mwanafunzi aliyempenda sana ambaye kiushahidi mwanafunzi huyu ni Yohana, ukweli wa kuweko ndugu za Yesu kristo sio ukweli na mtazamo wa kipentekoste bali ni ukweli na mtazamo wa Biblia yenyewe Maandiko yanaionyesha wazi kuwa Yesu alikuwa na ndugu zake wa kuzaliwa mara baada ya yeye kuzaliwa nao walikuwa ni Yakobo, Yusufu, Simoni na Yuda pamoja na dada zake wawili ona :-

Mathayo 13:53-56 “Ikawa Yesu alipoimaliza mifano hiyo, alitoka akaenda zake. Na alipofika nchi yake, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii? Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda? Na maumbu yake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote?

Biblia imeweka wazi kuwa Yesu Kristo alikuwa na ndugu zake na imetueleza kuwa mwanzoni nduguze walikuwa bado hawajamuamini, na pia mara kwa mara walimtembelea kutaka kumuona hata wakati akiwa anawahudumia watu ona

Mathayo 12:46-47 “Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye. Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe.”

Marko 3:31-32 “Wakaja mamaye na nduguze; wakasimama nje, wakatuma mtu kumwita. Na makutano walikuwa wameketi, wakimzunguka, wakamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta.”

Luka 8:19-20 “Wakamwendea mama yake na ndugu zake, wasiweze kumkaribia kwa sababu ya mkutano. Akaletewa habari akiambiwa, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje wakitaka kuonana nawe.”

Yohana 7:1-10 “Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Uyahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua. Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu. Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. Kwa maana hakuna mtu afanyaye neno kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi jidhihirishe kwa ulimwengu. Maana hata nduguze hawakumwamini. Basi Yesu akawaambia, Haujafika bado wakati wangu; ila wakati wenu sikuzote upo. Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu. Kweeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi sikwei bado kwenda kula sikukuu hii, kwa kuwa haujatimia wakati wangu. Naye alipokwisha kuwaambia hayo, alikaa vivi hivi huko Galilaya. Hata ndugu zake walipokwisha kukwea kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye alipokwea, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri.”

Matendo 1:13-14 “Hata walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yohana, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo.Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.”

Wagalatia 1:18-19 “Kisha, baada ya miaka mitatu, nalipanda kwenda Yerusalemu ili nionane na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano. Lakini sikumwona mtume mwingine, ila Yakobo, ndugu yake Bwana.    

Kwa hiyo tunapoyachunguza maandiko unaweza kuona kuwa yanabainisha wazi kuwa Yesu alikuwa na ndugu wa kibailojia ndugu wa damu ndugu wa kuzaliwa mara baada yaye ye kuzaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kwa msingi huo ni dhahiri ya kuwa Yesu alikuwa na ndugu,  na ndio maana utaweza kuona kwa asili wanapotajwa wanatajwa wakiwa pamoja na mama yao, wakatio mwingine wakatoliki wamefikiri kuwa ndugu hao wa Yesu ni binamu zake lakini iko wazi kuwa hao hawakuwa binamu zake Neno la asili la kiyunani linalotumika katika maandiko kuelezea maana ya Ndugu ni Adelphos au Delphus ambalo maana yake connective particle au Morphological ties Neno hilo Ndugu limetumika mara 346 katika Biblia likimaanisha Ndugu wa damu au ndugu wa tumbo Moja wakati ndugu wa kiimani limetumika mara 226 kwa msingi huo Yesu alikuwa na ndugu wa damu na wa kuzaliwa baada ya kuzaliwa yeye kwa muujiza nduguze wa karibu walizaliwa Nduhu hao wa Yesu wanatajwa katika maandiko baada ya Yesu kuzaliwa na sio kabla kwa kuwa wangeweza kutajwa wakati Yusufu alipoenda Bethelehemu au walipokimbilia Misri au wakati wa kurudi Nazarethi kwa msingi huo Maandiko yanabainisha wazi kuwa Yesu alikuwa na ndugu zake wa damu na wa kuzaliwa mwenye sikio la kusikia na alisikie neno hili.

*      Kwa nini Mariam mikononi mwa Yohana ?

Swali kubwa wanalouliza wengi ni kuwa kama Yesu alikuwa na ndugu zake iweje Yesu amkabidhi Mariama kwa Mwanafunzi wake aliyempenda aitwaye Yohana? Jibu ni rahisi sana Yohana ndiye mwanafunzi pekee aliyekuwa karibu sana na Msalaba pamoja na Mariamu mama yake Yesu wakati wanafunzi wengine walikimbia au walikuwa wakiangalia kwa mbali sana

Mathayo 26:58 “Na Petro akamfuata kwa mbali mpaka behewa ya Kuhani Mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.”

Mathayo 27:55-56 “Palikuwa na wanawake wengi pale wakitazama kwa mbali, hao ndio waliomfuata Yesu toka Galilaya, na kumtumikia.Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yusufu, na mama yao wana wa Zebedayo.”

Marko 15:40-41 “Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na Salome; hao ndio waliofuatana naye huko Galilaya, na kumtumikia; na wengine wengi waliopanda pamoja naye mpaka Yerusalemu.”

Luka 23:49 “Na wote waliojuana naye, na wale wanawake walioandamana naye toka Galilaya, wakasimama kwa mbali, wakitazama mambo hayo.”

Wakati injili zote zikithibitisha kuwa watu wote walikuwa mbali sana na Yesu wakati wa mateso yake habari njema ni kuwa waliokuwako karibu kabisa na msalaba kiasi cha kusikia maneno ya Yesu akizungumza ni Mariamu mama yake Yesu na Yohana mwanafunzi mpendwa wa Yesu Kristo  ona

 Yohana 19:26-27 “Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.”

Yesu alipokuwa msalabani aliweza kumuona mama yake na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu unaona jukumu la kumuangalia Mariamu mama yake Yesu alipewa Yohana na Jukumu la Mama kumuona Yohana kama mwanae walipewa kwa sababu ndio waliokuwa karibu na Yesu na sio vinginevyo, wakati wa mateso  na majaribu watu muhimu ni wale wanaokuwa karibu na wewe na sio wale wanaokuwa mbali na wewe

*      Mama tazama mwanao

Ukiacha sababu ya Yesu kumuona Yohana na mama yake kuwa karibu kiasi cha kuweza kuzungumza nao na kuwapa majukumu ya kutunzana maneno haya mama tazama mwanao na mwana tazama mama yako, ni fundisho lililowazi kuwa Yesu pamoja na mambi mengine alikuwa anaijali famlia yake, Historia ya kimasimulizi ya kale inaona wazi kuwa huenda Yusufu baba mlezi wa Yesu Kristio na baba mzazi wa ndugu zake Yesu huenda atakuwa alifariki kitambo kidogo kabla ya kusulubiwa kwa Yesu na huenda kuwa ni kwa muda Fulani Yesu alikuwa ndio nguzo ya Familia na ndio maana utaweza kuona ndugu zake na mama yake mara kadhaa walikuwa wakimuendea, Sasa Yesu Yuko Msalabani alimkabidhi mama yake kwa Yohana na kumtaka amuangalie na pia alimkabidhi Mariamu kwa Yohana ili wawe na ushirika naye

Agizo hili linatukumbusha wote majukumu yetu ya kuwaangalia wanafamilia wote na kuhakikisha tunawatunza,  kukabidhiwa kwa Mariamu kwa Yohana ni sawa na kukabidhiwa kwa wanafunzi wote na Yesu angeagiza hivyuo kwa owte kanma wote wangekuwa karibu naye Mungu hana upendeleo, baadaye tunamuona Yesu akiwaoa wanafunzi wake majukumu kadhaa akionyesha kuwa amewaamini, mfano alimwambia Petro Lisha kondoo zangu lakini pia aliwaambia wanafunzi wote waihubiri injili na kuwa anagekuwa pamoja nao zaidi ya yote tunawaona wanafunzi wote baadaye wakiwa na Mariamu mama yake Yesu na nduguze wakiwa na ushirika mmoja wote kwa pamoja, 

Matendo 1:13-14 “Hata walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yohana, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo.Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.”

Unaona Katika majira ya Pasaka ni muhimu kila mmoja kukumbuka kuwa karibu na familia na kuangaliana na kutunzana lakini ni wakati wa kujikumbusha umuhimu wa kuwa karibu na wale wanaopitia changamoto za aina mbalimbali, na wakati wote kuhakikisha kuwa tunawakumbuka wazazi wetu na kuwapa msaada wa karibu unaowezekana heshima hii ni ya Muhimu wakati wote tunapokuwa hai.

Na Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima



Leo hivi utakuwa pamoja nami Peponi!


Luka 23:39-43 “Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi. Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo? Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa. Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.”


Utangulizi

Wote tunafahamu kuwa Mateso na hukumu ya kusulubiwa na kufia Msalabani halikuwa tukio Jepesi, lilikuwa tukio gumu na la maumivu mengi ya kimwili, kisaikolojia na kiroho, Yesu alisulubiwa akiwa hana hatia wala hakuwa amefanya kosa lolote, wote tunajua sasa ya kuwa alisulubiwa na kuteswa kwaajili ya dhambi zetu, lakini kwa wakati ule wa mateso haikuwa rahisi kueleweka namna hiyo, akiwa Msalabani Pale Golgotha Yesu alisulubiwa pamoja na wanyang’anyi wawili, ambao kimsingi wao walikuwa na hatia! Lakini katika namna ya kushangaza wahalifu hao mmoja alijiunga katika kumshutumu Bwana Yesu na Mwingine kumtetea

Luka 23:36-43 “Wale askari nao wakamfanyia dhihaka, wakimwendea na kumletea siki, huku wakisema, Kama wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi, ujiokoe mwenyewe. Na juu yake palikuwa na anwani; HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI. Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi. Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo? Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa. Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.”

Tukio hili linapelekea Yesu kutamka neno la pili Muhimu miongini mwa maneno saba aliyoyatamka akiwa msalabani, kwa kujikumbusha maneno mengine aliyoyatamka Yesu akiwa Msalabani ni Pamoja na :-

·         Baba uwasamehe kwa maana hawajui walitendalo Luka 23:34

·         Amin nakuambia leo hivi utakuwa pamoja nani peponi Luka 23:43

·         Mama tazama mwanao, mwana tazama mama yako Yohana 19:26-27

·         Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha Mathayo 27:46

·         Nina kiu Yohana 19:28

·         Imekwisha Yohana 19:30

·         Baba mikononi mwako naiweka roho yangu Luka 23:46

Uchambuzi kuhusu Neno “Leo hivi utakuwa pamoja nami Peponi”

Ni muhimu sana kufahamu kuwa Maneno hayo ya pili yaliyotamkwa na Yesu pale msalabani kwa mtu yule aliyekuwa muhalifu, yana uzito mkubwa sana linapokuja swala la wanafunzi wa kimaandiko wenye kufikiri sana, watafasiri wengi wa maandiko wanaweka hoja ngumu zinazopelekea mstari huu wakati mwingine usiwe mstari mwepesi kutafasirika ona kwa mfano Maneno hayo yanasomeka hiviYesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponiwataalamu wa maandiko wakati mwingine kwa sababu ya kufikiri sana wanajenga hoja kuwa Yesu alikata roho na kufa na kuzikwa na siku ya tatu akafufuka  na akaonekana mara kadhaa duniani kwa watu mbalimbali mpaka alipopaa, kwa msingi huo inawezekanaje Yesu kuwa Pamoja na muhalifu yule Peponi siku ileile, kwa sababu hiyo waoa wanajenga hoja kwamba kwa vile Maandiko ya awali hayakuwa na vituo wala koma huenda maneno maneno ya Yesu yalitakiwa yasomoke hivi Yesu akamwambia, Amin nakuambia leo hivi, utakuwa pamoja nami peponikwa hiyo wataalamu hao wa maandiko hifikiri kuwa kulikuwa na makosa kuweka koma mbele ya neno Amin na neno nakuambia na kuwa sentensi …AMIN NAKUAMBIA LEO HIVI, Yalikuwa ni sentesi moja na hivyo kuifanya ahadi ya Yesu iwe ni neno UTAKUWA PAMOJA NAMI PEPONI, kuweka neno LEO HIVI UTAKUWA PAMOJA NAMI PEPONI Kungeweza kupotosha maana halisi ya tafasiri ya maandiko hayo, Kwa tafasiri hiyo wao wanaamini ya kuwa Yesu alikuwa anamthibitishia Mwizi yule aliyemuamini kuwa anayioyasema ni hakika kwamba atakuwa naye Peponi, Kwahiyo uthibitisho huo wa Yesu kusema ukweli umebebwa na neno …AMIN NAKUAMBIA LEO HIVI ni kwamba Yesu alikuwa anamueleza ukweli wa kuweko kwake peponi mtu yule anayemuamini, lakini haikuwa lazima kuwa Yesu alikuwa anamaanisha kuwa angekuwa naye peponi siku ileile!

Wakati mwingine kufikiri sana na kutumia akili sana kunaweza kuleta upotofu katika maandiko, ushahidi wa kibiblia kutoka katika biblia nyingine unathibitisha wazi kuwa koma iliwekwa mahali sahihi vilevioe kama ilivyowekwa katika Biblia ya kiswahili ya Union version Mfano

·         Biblia ya Kiingereza ya KJV inasema “Verily I say unto thee, To day shalt thou be with me in paradise”

·         Biblia ya kiingereza ya Amplified inasema “Assuredly I tell you, today you will be with me in Paradise”

·         Biblia ya kiingereza ya RSV inasema “And he said to him truly, I say to you, today you will be with me in paradise”

Unaweza kuona tafasiri zote za Biblia zimeweka Koma katika eneo sahihi na kama ilivyo ada ni kweli kuwa Yesu kila alipotaka kuzungumza neno lenye mantiki kubwa sana alitumia neno Amin Nakuambia, na neno la namna hiyo limerejewa katika biblia zaidi ya  mara 76 hata hivyo katika maeneo yote hayo hajawahi kutumia neno LEO,  Kwa msingi huo ni wazi kabisa kuwa Yesu alikuwa akisisitiza kuwa Peponi na Mtu yule kuanzia siku ile ile Angekuwa naye Peponi.

Ni ukweli ulio wazi kuwa Yesu aliposulubiwa na kufa na kuzikwa mwili wake uliwekwa Kaburini, Lakini Nafsi yake na Roho yake alikabidhi kwa Mungu baba na hivyo alikuwa mbinguni au Paradiso tangu wakati ule Luka 23:46 “Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.”  Maneno ya Yesu yako wazi na hayahitaji tafakari pana inakayoweza kututoa nje ya maana halisi japo kufikiri kama mhivi ni kuzuri na kunapanua ufahamu lakini ni ukweli usiopingika kuwa Mwivi yule alipata tiketi ya kuwa na Yesu Peponi tangu siku ile ile.

Leo hivi utakuwa pamoja nani peponi.

Ni ahadi ya uhakika ya kuwa kila anayermkubali Yesu Mungu mwenyewe anatuhakikishia kuwa atakuwa pamoja nasi Peponi, haijalishi kuwa ulikuwa muovu kiasi gani, hatujaelezwa wazi kuwa muhalifu huyu alikuwa amefanya makosa gani lakini iko wazi kuwa kama mtu amehukumiwa kuuawa bila shaka hakuwa mtu mwenye kufaa tena katika jamii, mhalifu huyu sio tu alistahili kuuawa lakini alikuwa hastahili hata kuwekwa Gerezani, kwa vyovyote vile akuwa muovu, mtu huyu hata toba yake ilikuwa sio toba ya kueleweka lakini ni ukweli ya kuwa alikuwa anajua kuwa yuko Msalabani kwa makosa yake naya kuwa anastahili kupata yanayompata, lakini pia alikuwa anatambua kazi ya Yesu pale Msalabani alijua wazi kuwa yeye hakuwa na hatia kama wao na alitambua kuwa Yesu anao ufalme na kuwa sio mwanadamu wa kawaida na alijiombea kukumbukwa katuika ufalme huo, Yesu alimkakikishia kuwa atakuwa pamoja naye peponi, Yesu aliteseka Msalabani si kwa sababu yake ilikuwa ni kwaajili ya dhambi zetu

Isaya 53:3-5 “Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona

Na kwa msingi huo toba ya muhalifu yule kama ilivyo kwetu sisi ilikuwa ni ahadi thabiti yay a kweli yenye kutuhakikishia wote tunaomkiri Yesu hadharani ya kuwa Mungu atakuwa pamoja nasi na sisi tunakuwa pamoja naye, hakuna mtu mbaya kiasi cha kutokuweza kusafishwa au kusamehewa na kusafishwa kwa Damu ya Yesu!, hakuna jambo la msingi kama kuingia peponi tunaweza kuona wivu kwa jamaa huyu Msalabani laki Kristio ameahidi kuwa kila amuaminiye hatatahayarika katika msimu huu wa Pasaka ni Muhimu basi kwa kila mmoja wetu kusogelea Msalabani na kutubu na kumkiri Kristo ili tupate uhakika wa neema yake ya kutupa kibali cha kuingia naye peponi

Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!



Baba uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo!

 

Luka 23:33-37 “Na walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, ndipo walipomsulibisha yeye, na wale wahalifu, mmoja upande wa kuume, na mmoja upande wa kushoto. Yesu akasema, BABA, UWASAMEHE, KWA KUWA HAWAJUI WATENDALO. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura. Watu wakasimama wakitazama. Wale wakuu nao walikuwa wakimfanyia mzaha, wakisema, Aliokoa wengine; na ajiokoe mwenyewe, kama ndiye Kristo wa Mungu, mteule wake. Wale askari nao wakamfanyia dhihaka, wakimwendea na kumletea siki, huku wakisema, Kama wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi, ujiokoe mwenyewe



Utangulizi:

Mojawapo kati ya usemi wenye maana sana kati ya semi saba za Yesu alizozisema akiwa msalabani na ambazo zinatajwa katika sehemu mbalimbali za injili, ni pamoja ya usemi huo wa muhimu ni usemi wa Kwanza wenye Neno BABA UWASAMEHE KWA MAANA HAWAJUI WALITENDALO ambalo leo katika msimu huu wa pasaka tutachukua muda kulijadili kwa undani na kupata maana Muhimu sana iliyokusudiwa, maneno mengine kati ya maneno saba aliyoyasema Yesu msalabani ni pamoja na:-

1.       Baba uwasamehe kwa maana hawajui walitendalo Luka 23:34

2.       Amin nakuambia leo hii utakuwa pamoja nani peponi Luka 23:43

3.       Mama tazama mwanao, mwana tazama mama yako Yohana 19:26-27

4.       Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha Mathayo 27:46

5.       Nina kiu Yohana 19:28

6.       Imekwisha Yohana 19:30

7.       Baba mikononi mwako naiweka roho yangu Luka 23:46

BABA UWASAMEHE KWA MAANA HAWAJUI WALITENDALO.

Leo ni siku ya ijumaa kuu, ni siku ambayo wakristo wote duniani, tunaungana katika kuadhimisha na kukumbuka kusulubiwa kwa Yesu Kristo huko Golgota miaka zaidi ya 2000 iliyopita katika siku hii basi basi sisi tutachukua Muda kuangalia usemi huu wa Kwanza katika maneno saba yaliyozungumzwa na Yesu Pale Msalabani wakati wa mateso yake , Neno hili ni miongoni mwa maneno saba ya Yesu akiwa matesoni ambayo yamekusanywa kutoka maeneo mbalimbali ya vitabu vya injili na hili mojawapo tutaangalia umuhimu wake katika msimu huu wa Pasaka. Hapa tunazungumzia Msamaha.

Kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine amewahi kujeruhiwa moyo na mtu mwingine, kila mmoja amewahi kujeruhiwa na kuathiriwa kiakili, kihisia na hata kimwili, na kwa sababu hiyo tunaweza kujawa na maumivu ya aina Fulani mioyoni mwetu, ama uchungu wa aina Fulani, vyovyote vile iwavyo ukomavu wa kiroho katika maisha yetu ya ukristo unapimwa na namna tunavyoweza kusamehe, uwezo wa kusamehe ukiwa pamoja nasi  unatuwezesha kuishi kwa furaha na amani duniani na huku tukiwa huru bila kifungo chochote endapo tutakuwa na uwezo wa kusamehe wengine.

Yesu Kristo akiwa Msalabani aliangalia chini na kutafakari katika hali ya ukimya akiwaangalia wote waliokuwa wanahusika katika kumtesa, Askari ambao walisimamia mateso yake wakigawana nguo yake kwa kuipigia kura, Yesu hakuwahi kutenda neno lolote ovu, siku zote alikuwa akiwafundisha watu neno la Mungu na kuwaponya watu magonjwa yao, aliwahudumia watu akifufua, akiponya, akilisha akihurumia na kurehemu, hata hivyo kwajili ya wivu wakuu wa dini walikusudia kumuua, waliandaa mpango mkakati wa kumuua, walitoa rushwa kwa Yuda ili aweze kumsaliti, waliandaa mashahidi wa uongo ili wamshitaki, walimuweka katima mikono ya wenye dhambi ili asulubiwe, hakimu aliyekuwepo alipindisha hukumu ilihali akijua wazi kuwa Yesu hakuwa na hatia, zaidi ya yote aliamuru Yesu apigwe mijeledi

Yohana 19:1-6 “Basi ndipo Pilato alipomtwaa Yesu, akampiga mijeledi. Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau. Wakawa wakimwendea, wakisema, Salamu! Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga makofi. Kisha Pilato akatokea tena nje, akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa mimi sioni hatia yo yote kwake. Ndipo Yesu alipotoka nje, naye amevaa ile taji ya miiba, na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, Tazama, mtu huyu! Basi wale wakuu wa makuhani na watumishi wao walipomwona, walipiga kelele wakisema, Msulibishe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi basi, mkamsulibishe; kwa maana mimi sioni hatia kwake.”

Ni ukweli usiopingika kuwa Yesu aliharibiwa sana kiasi ambacho ilikuwa ni ngumu kumtamani sawa kabisa na alivyotabiri Isaya katika Isaya 53:2-5Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.”

Pamoja na mateso haya na suluba kali pia walimfanyia dhihaka za namna nyingi, mateso yake yamerekodiwa na Mel Gobson katika filamu yake ijulikanayo kama Passion of Jesus ambayo wayahudi walipoiona kwa mara ya kwanza waliikataa na kusema kuwa inaweza kuchochea chuki kati ya wakristo na wayahudi wakifikiri kuwa Mel Gibson ametia chumvi, lakini kitaalamu Mel Gibson ameonyesha karibu robo tatu tu ya mateso halisi aliyoyapata Kristo, mateso mengine :-

Yohana 19:23-24, “Nao askari walipomsulibisha Yesu, waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu. Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, Na vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari.

Mathayo 27:27-31 “Ndipo askari wa liwali wakamchukua Yesu ndani ya Praitorio, wakamkusanyikia kikosi kizima.Wakamvua nguo, wakamvika vazi jekundu. Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika mkono wake wa kuume; wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki, wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi! Kisha wakamtemea mate, wakautwaa ule mwanzi, wakampiga-piga kichwani. Walipokwisha kumdhihaki, wakalivua lile vazi, wakamvika mavazi yake, wakamchukua kumsulibisha.

Wahalifu wawili waliokuwa kulia kwake na kushoto kwake wakimshutumu, Mathayo 27:44, “Pia wale wanyang'anyi waliosulibiwa pamoja naye walimshutumu vile vile.” Viongozi wa dini waliofanya fitina na kutengeneza ushahidi wa uongo na kushinikiza kwamba Yesu asulubiwe na waliokuwa wakimdhihaki Mathayo 27:41-43,“Kadhalika na wale wakuu wa makuhani wakamdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakisema, Aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini. Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu

Hakimu Pilato ambaye alifahamu kabisa kuwa Yesu hakuwa na hatia, lakini akapindisha kesi haya yote na ile aina ya mateso kwa mwana wa Mungu, kungeweza kwa namna yoyote ile kuleta hisia za maumivu, uchungu, kinyongo, kisasi, ugumu wa moyo, hasira, ghadhabu, ubaridi, kujihami na kuhakikisha kuwa unawashughulikia wote waliokutenda uovu, Lakini Bwana Yesu anatangaza kusamehe na kuwaombea wakosaji wote kwa BABA KUWA WASAMEHEWE, Hali hii inaashiria uwezo mkubwa wa ukomavu mkubwa wa kiroho aliokuwa nao Yesu wa kutangaza Msamaha, ni ngazi ya juu sana ya Rehema na upendo, kwamba hata katika hali ngumu kama hii ya kuteseka bado Yesu anatangaza Msamaha dhidi ya maadui zake ! wote tunafahamu kuwa msamaha sio jambo rahisi, lakini katika msimu huu wa Pasaka Bwana Yesu anatukumbusha kwamba tunapaswa kuachilia na kutangaza msamaha kwa wote waliotukosea lakini vilevile kuwaomba radhi wale ambao tumewakosea, wakati huu wa Kwaresma ni wakati wa kuachilia ni wakati wa kusamehe ni wakati wa kuonyesha kuwa tumekomaa kiroho na kiakili na kuwa kusamehe ndio njia ya juu kabisa ya kuonyesha tabia ya uungu na ukomavu wetu, tusamehe.!

Kusamehe ni nini hasa?

Kusamehe ni kuachilia, unaachilia mambio yaende, unaacha kuhesabu ubaya uliofanyiwa unaufunika kwa kuendelea kupenda, unaacha kutafuta kulipa kisasi au nkulipiwa kisasi, unaondoa moyoni mwako hali ya kumfikiri mtu aliyekukosea unajiweka huru mbali na kifungo cha aina yoyote cha kuwa na mtu moyoni, unamuhurumia mtu, unachukuliana naye, unamuhesabu kuwa yeye ni dhaifu, hivyo unamuachilia

Faida za kusamehe

·         Unadumisha mahusiano, mahusiano yanakuwa mazuri, Ndoa inakuwa nzuri, unampata ndugu yako

·         Unaiweka akili yako kufikiri mambo ya msingi na kuzungumza mambo ya msingi

·         Unajiweka huru kutoka kwenye migandamizo na msongo wa mawazo

·         Unakuwa na afya nzuri, unakuwa mwenye furaha, hutakuwa na pressure, hutaugua magonjwa ya moyo, na unakuwa mtu mwenye uwezio wa juu wa kujitambua

·         Kusamehe kunakufanya wewe nawe usamehewe na Mungu

Mathayo 18:21-35Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi.Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni.Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia akamkamata,akamshika koo,akisema Nilipe uwiwacho.Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni. Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote. Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.”

Kutokusamehe hasara zake

Hakuna sababu ya kuwabeba watu moyoni, hii hali kiroho inakuweka wewe mwenyewe gerezani na kukunyima furaha, dua, sala, sadaka na maombi yetu vinakutana na kikwazo kama hatujawasamehe wengine Mathayo 6:12 “Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.” Mathayo 6:14-15 “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenukuna hasara nyingi sana za kiroho na kimwili kama watu hawatasamehe na kuna faida nyingi sana kama watu watasamehe.Lakini kama mtu hatasamehe yafuatayo yatamkabili:-

·         Unakuwa na moyo wenye uchungu, huwezi kufurahia mahusiano hata katika ndoa

·         Unakuwa na mawazo mabaya kwa kudhani Fulani ni adui yako

·         Utakuwa na mgandamizo wa mawazo

·         Unafungua mlango wa kuvamiwa na mapepo, unafukuza uwepo wa Mungu

·         Unazuia Baraka za Mungu na kufanya ibada zako zikataliwe

Bwana na ampe neema kila Mmoja wetu, kuwa na uwezo wa kusamehe ili tuweze kuwa wana wa Mungu sawasawa na mafundisho ya Bwana wetu Yesu!

 

Na. Rev. Innocent Kamote.

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.