Luka 23:39-43 “Na mmoja wa wale wahalifu
waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na
sisi. Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata
Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo? Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa
tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote
lisilofaa. Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.
Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.”
Utangulizi
Wote tunafahamu kuwa Mateso na
hukumu ya kusulubiwa na kufia Msalabani halikuwa tukio Jepesi, lilikuwa tukio
gumu na la maumivu mengi ya kimwili, kisaikolojia na kiroho, Yesu alisulubiwa
akiwa hana hatia wala hakuwa amefanya kosa lolote, wote tunajua sasa ya kuwa
alisulubiwa na kuteswa kwaajili ya dhambi zetu, lakini kwa wakati ule wa mateso
haikuwa rahisi kueleweka namna hiyo, akiwa Msalabani Pale Golgotha Yesu
alisulubiwa pamoja na wanyang’anyi wawili, ambao kimsingi wao walikuwa na
hatia! Lakini katika namna ya kushangaza wahalifu hao mmoja alijiunga katika
kumshutumu Bwana Yesu na Mwingine kumtetea
Luka 23:36-43 “Wale askari nao wakamfanyia
dhihaka, wakimwendea na kumletea siki, huku wakisema, Kama wewe ndiwe mfalme wa
Wayahudi, ujiokoe mwenyewe. Na juu yake palikuwa na anwani; HUYU NDIYE MFALME
WA WAYAHUDI. Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je!
Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi. Lakini yule wa pili akamjibu
akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo?
Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo
yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa. Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke
utakapoingia katika ufalme wako. Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi
utakuwa pamoja nami peponi.”
Tukio hili linapelekea Yesu
kutamka neno la pili Muhimu miongini mwa maneno saba aliyoyatamka akiwa
msalabani, kwa kujikumbusha maneno mengine aliyoyatamka Yesu akiwa Msalabani ni
Pamoja na :-
·
Baba uwasamehe kwa maana
hawajui walitendalo Luka 23:34
·
Amin nakuambia leo hivi utakuwa
pamoja nani peponi Luka 23:43
·
Mama tazama mwanao, mwana
tazama mama yako Yohana 19:26-27
·
Mungu wangu Mungu wangu mbona
umeniacha Mathayo 27:46
·
Nina kiu Yohana 19:28
·
Imekwisha Yohana 19:30
·
Baba mikononi mwako naiweka
roho yangu Luka 23:46
Uchambuzi kuhusu Neno “Leo hivi utakuwa pamoja nami Peponi”
Ni muhimu sana kufahamu kuwa
Maneno hayo ya pili yaliyotamkwa na Yesu pale msalabani kwa mtu yule aliyekuwa
muhalifu, yana uzito mkubwa sana linapokuja swala la wanafunzi wa kimaandiko
wenye kufikiri sana, watafasiri wengi wa maandiko wanaweka hoja ngumu
zinazopelekea mstari huu wakati mwingine usiwe mstari mwepesi kutafasirika ona
kwa mfano Maneno hayo yanasomeka hivi “Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja
nami peponi” wataalamu wa maandiko wakati mwingine kwa sababu ya
kufikiri sana wanajenga hoja kuwa Yesu alikata roho na kufa na kuzikwa na siku
ya tatu akafufuka na akaonekana mara
kadhaa duniani kwa watu mbalimbali mpaka alipopaa, kwa msingi huo inawezekanaje
Yesu kuwa Pamoja na muhalifu yule Peponi siku ileile, kwa sababu hiyo waoa
wanajenga hoja kwamba kwa vile Maandiko ya awali hayakuwa na vituo wala koma
huenda maneno maneno ya Yesu yalitakiwa yasomoke hivi “Yesu akamwambia, Amin nakuambia leo hivi,
utakuwa pamoja nami peponi” kwa hiyo wataalamu hao wa maandiko
hifikiri kuwa kulikuwa na makosa kuweka koma mbele ya neno Amin na neno
nakuambia na kuwa sentensi …AMIN
NAKUAMBIA LEO HIVI, Yalikuwa ni sentesi moja na hivyo kuifanya ahadi ya
Yesu iwe ni neno UTAKUWA PAMOJA NAMI
PEPONI, kuweka neno LEO HIVI UTAKUWA PAMOJA NAMI PEPONI Kungeweza kupotosha
maana halisi ya tafasiri ya maandiko hayo, Kwa tafasiri hiyo wao wanaamini ya
kuwa Yesu alikuwa anamthibitishia Mwizi yule aliyemuamini kuwa anayioyasema ni
hakika kwamba atakuwa naye Peponi, Kwahiyo uthibitisho huo wa Yesu kusema
ukweli umebebwa na neno …AMIN NAKUAMBIA
LEO HIVI ni kwamba Yesu alikuwa anamueleza ukweli wa kuweko kwake peponi
mtu yule anayemuamini, lakini haikuwa lazima kuwa Yesu alikuwa anamaanisha kuwa
angekuwa naye peponi siku ileile!
Wakati mwingine kufikiri sana na
kutumia akili sana kunaweza kuleta upotofu katika maandiko, ushahidi wa
kibiblia kutoka katika biblia nyingine unathibitisha wazi kuwa koma iliwekwa
mahali sahihi vilevioe kama ilivyowekwa katika Biblia ya kiswahili ya Union
version Mfano
·
Biblia ya Kiingereza ya KJV inasema “Verily I say unto thee, To day
shalt thou be with me in paradise”
·
Biblia ya kiingereza ya Amplified inasema “Assuredly I tell you,
today you will be with me in Paradise”
·
Biblia ya kiingereza ya RSV inasema “And he said to him truly, I say
to you, today you will be with me in paradise”
Unaweza kuona tafasiri zote za
Biblia zimeweka Koma katika eneo sahihi na kama ilivyo ada ni kweli kuwa Yesu
kila alipotaka kuzungumza neno lenye mantiki kubwa sana alitumia neno Amin
Nakuambia, na neno la namna hiyo limerejewa katika biblia zaidi ya mara 76 hata hivyo katika maeneo yote hayo
hajawahi kutumia neno LEO, Kwa msingi
huo ni wazi kabisa kuwa Yesu alikuwa akisisitiza kuwa Peponi na Mtu yule
kuanzia siku ile ile Angekuwa naye Peponi.
Ni ukweli ulio wazi kuwa Yesu
aliposulubiwa na kufa na kuzikwa mwili wake uliwekwa Kaburini, Lakini Nafsi
yake na Roho yake alikabidhi kwa Mungu baba na hivyo alikuwa mbinguni au
Paradiso tangu wakati ule Luka 23:46 “Yesu
akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.” Maneno ya Yesu yako wazi na hayahitaji
tafakari pana inakayoweza kututoa nje ya maana halisi japo kufikiri kama mhivi
ni kuzuri na kunapanua ufahamu lakini ni ukweli usiopingika kuwa Mwivi yule
alipata tiketi ya kuwa na Yesu Peponi tangu siku ile ile.
Leo hivi utakuwa pamoja nani peponi.
Ni ahadi ya uhakika ya kuwa kila
anayermkubali Yesu Mungu mwenyewe anatuhakikishia kuwa atakuwa pamoja nasi
Peponi, haijalishi kuwa ulikuwa muovu kiasi gani, hatujaelezwa wazi kuwa
muhalifu huyu alikuwa amefanya makosa gani lakini iko wazi kuwa kama mtu amehukumiwa
kuuawa bila shaka hakuwa mtu mwenye kufaa tena katika jamii, mhalifu huyu sio
tu alistahili kuuawa lakini alikuwa hastahili hata kuwekwa Gerezani, kwa
vyovyote vile akuwa muovu, mtu huyu hata toba yake ilikuwa sio toba ya
kueleweka lakini ni ukweli ya kuwa alikuwa anajua kuwa yuko Msalabani kwa
makosa yake naya kuwa anastahili kupata yanayompata, lakini pia alikuwa
anatambua kazi ya Yesu pale Msalabani alijua wazi kuwa yeye hakuwa na hatia
kama wao na alitambua kuwa Yesu anao ufalme na kuwa sio mwanadamu wa kawaida na
alijiombea kukumbukwa katuika ufalme huo, Yesu alimkakikishia kuwa atakuwa
pamoja naye peponi, Yesu aliteseka Msalabani si kwa sababu yake ilikuwa ni
kwaajili ya dhambi zetu
Isaya 53:3-5 “Alidharauliwa na kukataliwa
na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu
humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika
ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa
amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,
Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa
kupigwa kwake sisi tumepona”
Na kwa msingi huo toba ya
muhalifu yule kama ilivyo kwetu sisi ilikuwa ni ahadi thabiti yay a kweli yenye
kutuhakikishia wote tunaomkiri Yesu hadharani ya kuwa Mungu atakuwa pamoja nasi
na sisi tunakuwa pamoja naye, hakuna mtu mbaya kiasi cha kutokuweza kusafishwa
au kusamehewa na kusafishwa kwa Damu ya Yesu!, hakuna jambo la msingi kama
kuingia peponi tunaweza kuona wivu kwa jamaa huyu Msalabani laki Kristio
ameahidi kuwa kila amuaminiye hatatahayarika katika msimu huu wa Pasaka ni
Muhimu basi kwa kila mmoja wetu kusogelea Msalabani na kutubu na kumkiri Kristo
ili tupate uhakika wa neema yake ya kutupa kibali cha kuingia naye peponi
Na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni