Matendo 26: 24-25 Biblia inasema:-
“Alipokuwa akijitetea hivi, Festo akasema kwa
sauti kuu, Paulo, una wazimu, kusoma kwako kwingi kumekugeuza akili. Lakini Paulo akasema, Sina wazimu, Ee Festo
mtukufu, bali nanena maneno ya kweli na ya akili kamili.”
Wala sikuyakana yale Maono Matendo
26:19,- "Paulo Mtume"
Utangulizi:
Kifungu hiki ni maneno ya Mtume Paulo, alipopewa
nafasi ya kujitetea mbele ya Mfalme Agrippa na Gavana wa Kirumi aliyeitwa
Festo, Paulo alikuwa amepewa nafasi ya kujitetea kutokana na mashitaka ya
wayahudi waliokuwa wakiipinga Injili, Katika namna ya kushangaza Paulo
aliitumia nafasi hiyo kutoa ushuhuda wa Yesu Kristo na wokovu.
Watawala hao wa kipagani walikuwa wanafahamu vema
matukio yaliyotokea katika uyahudi na walikuwa wanamfahamu vema Paulo mtume
kama mtu msomi, hata hivyo Paulo alikuwa akimuelezea Bwana Mungu aliyemtokea
katika maono na jinsi alivyoweza kumuokoa na kumuita katika utumishi huu Festo
alipiga kelele kwamba mtu huyu huenda
kusoma kwake kwingi kumempeleka pabaya na kuwa sasa amekuwa na wazimu
Kuwa na wazimu maana yake ni kurukwa na akili ni
kuwa nje ya akili zako za kawaida, nje ya usomi wako na utaalamu wako wa
kawaida, ni kuwa chizi ni kuwa kichaa
Viongozi hao walimuelewa Paulo alivyokuwa na
walimuelewa alivyokuwa akizungumza kabla hajaokoka, baada yakuokoka na
kinachoendelea tangu alipokutana na Yesu nay ale ambayo Yesu anaendelea
kuyatenda maishani mwake walihitimisha kuwa sasa amekuwa kichaa Lakini Paulo
alikazia kuwa Yuko kamili na anazungumza maneno ya kweli na akili kamili
Hivi ndivyo ulimwengu unavyowaona watu waliomuamini
Yesu, wanaonekana kama vichaa na ni
vigumu kueleweka kwa akili za kawaida zawadi hii kubwa ya wokovu, ni vigumu
hata kuuelwa Ukristo ulivyo makubwa yaliyomchanganya Festo na Agrippa yalikuwa
ni maswala haya katika hutuba ya kujitetea ya Paulo
Matendo
26:12-13 Nuru
ipitayo Mwangaza wa jua wakati wa Mchana adhuhuri
Matendo
26: 14- 18 Kutokewa
na Yesu na kuagizwa kuhubiri injili
Ni vigumu kuelewa kile anachokisema Paulo kama bado
hujaokoka na ni rahisi kudhani kuwa wokovu ni ukichaa lakini kilichomtokea
Paulo ni wazi kuwa kinampata kila Mkristo aliyemwamini Yesu
1.
Kila
aliyemwamini Yesu ameona Nuru kuu 2Wakoritho 4:6 1Petro 2:9 Yesu ni Nuru
kila aliyeokoka ametolewa gizani kuna nguvu katika nuru hii uwe umekutana nayo
usiku iwe imekutana nayo mchana ni nuru ya ajabu ina nguvu ya kuweka Giza lote
pembeni na wala havichangamani Yohana 1:1:1-5, tulipokutana na Yesu
maisha yalibadilishwa na nguvu mpya ya nuru imeingia ndani yetu
2.
Kukutana
na Yesu njiani hili lilikuwa
jambo la kuwashangaza viongozi hao wa kipagani walifahamu kuwa Yesu alisulubiwa
na alikuwa amekufa, alikuwa mtu dhaifu tu liwali wa kirumi Pilato alikuwa
amemuhukumu kifo na kesi yake iko kwenye majalada, ni vigumu sana kuona Yesu
anavyowatokea watu na kukutana nao kama uko nje ya wokovu lakini kila
aliyeokoka anaelewa uhai wa Yesu Kristo anajua kuwa Kaburi halikumuweza
anaelewawazi uwezo wake kwamba yuko hai Ufunuo 1:17-18
3.
Anabadilisha
watu bila kujali historia yao
Walimfahamu Paulo kuwa alikuwa
·
Msomi
mzuri sana
·
Mtu wa
Dini ya kiyahudi aliyebobea
·
Mtu
tajiri, mweye uwezo na cheo na ushawishi katika jamii
Sasa amebadilika kabisa tangu
alipokutana na Yesu amekuwa kitu kingine kumbe mtu awaye yote wa hadhi yoyote
ile akikutana na yesu anakubadilisha 2 Cor. 5:17.Kama watu hawataeewa kuwa Bwana Yesu yuko hai, basi
watatambua kuwa yuko hai kwa uwezo wake wa kubadilisha, hakuna kiongozi yeyote
Duniani ambaye amewahi kuweko duniani na kuwa na uwezo wa kubadilisha maisha ya
watu wake kama Yesu Kristo
Mazungumzo
ya Paulo yalikuwa hayaeleweki tena, alikuwa anaonekana kama amevuta bangi
§
Tunaposema Yesu amezaliwa na Bikira,
alisulubiwa akafa akazikwa na akafufuka
§
Tunaposema tunaenda kubatizwa na
kuzamishwa katika maji mengi kama sehemu ya agizo la kumtii Yesu Kristo watu
wanaweza kufikiri kuwa tunawazimu
§
Tunapozungumza kuwa Damu yake
inauwezo wa kuosha dhambi zetu
§
Tunaposema nyumbani kwetu ni
mbinguni
§
Tunaposema Yesu atakuja tena
§
Tunaposema kanisa litanyakuliwa
§
Wafu watafufuliwa, kutakuwa na
hukumu ya mwisho na mengine yanayofanana
na hayo
Watu
wanaokuelewa
Sasa amekamatwa na kushitakiwa kwa
sababu hakuyakana yale maono Matendo
26:19 Paulo alikuwa katika vifungo kwaajili ya injili.
Wanaweza
kudhani kuwa tumechanganyikiwa kwa sababu ya kumuamini Yesu lakini kuna
badiliko kubwa na la ajabu hutokea ndani ya kila aliyemwamini Bwana Yesu, zaidi
ya yote tunalo agizo la kuihubiri injili na kutokana na kuihubiri injili
tunaweza kupitia majaribu ya aina mbalimbali hata kuwekwa Gerezani kama
ilivyokuwa kwa Paulo, Festo alifikiri kuwa kusoma kwake kwingi kumemgeuza akili
amekuwa na wazimu lakini Injili Ni maneno ya kweli nay a akili timamu.
Rev.
Innocent Kamote
Mkuu
wa wajenzi mwenye Hekima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni