Mstari wa Msingi: Yohana 15:18” Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa
umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.”
"Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu,
kama usingepewa kutoka juu"
Utangulizi.
Chuki ni hisia za kutokupendezwa
na kitu au mtu Fulani kwa sababu mbalimbali, ni hisia za kutokumpenda mtu,
Biblia imeonyesha mikasa mingi ambapo watu kadhaa waliwachukia wengine kwa
sababu mbalimbali, au wakati mwingine bila sababu, ingawa ukweli unabaki kuwa
ziko sababu Fulani, Je wewe umewahi kuchukiwa na mtu? Je ni Bila sababu?
Nadhani unaweza kudhani kuwa hakuna sababu lakini neno la Mungu linafunua
sababu mbalimbali za wewe kuchukiwa, na linakutaka ujue kwa nini watu
wanakuchukia na nini cha kufanya iwapo watakuchukia, ni kwa msingi huo leo
tutachukua muda kutafakari kwa kina somo hili muhimu IWAPO WATAKUCHUKIA kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo.
·
Amri ya kutokumchukia awaye yote.
·
Iwapo watakuchukia!
Amri ya kutokumchukia awaye yote.
Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu
katika neno lake tangu nyakati za agano la kale alikemea chuki, alikataza mtu kuwa
na chuki moyoni dhidi ya ndugu yako yaani aina binadamu wa aina zote, Mambo ya walawi 19:17-18 “Usimchukie ndugu
yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, wala usichukue dhambi kwa
ajili yake. Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako;
bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi BWANA”. Kwa
kiwango cha maandiko chuki inahesabika sawa na uuaji na kwamba hakuna ufalme wa
Mungu kwa mtu mwenye chuki dhidi ya mwingine1Yohana 3:15 “Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa
kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.” Aidha biblia
imeonyesha wazi kuwa awaye yote amabaye anamchukia mwingine kwa sababu yoyote
ni muongo uongo wake unadhihirishwa na chuki yake na hivyo haweze kuwa na madai
ya kuwa anampenda Mungu iwapo ana mchukia binadamu mwenzake anayemuona kwa
macho 1Yohana 4:20-21 “Mtu akisema,
Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda
ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. Na amri hii
tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.”
Maandiko yanakemea na kukataza chuki, lakini wewe ni shahidi wa wazi kwamba
ulimwengu wa sasa umejawa na chuki, katika taarifa nyingi za habari
tunazozisikia kila leo, matendo ya kikatili na mauaji vita na kadhalika kwa
asilimia kubwa yanaongozwa na chuki, chuki zimeenea kama sumu katikajamii,
chuki iko miongoni mwa wakristo kwa wakristo
hata wale wanaosali katika kanisa moja, kama haitoshi chuki ikokwa
kiwango kikubwa hata kwa watumishi wa Mungu yaani wale walioko katika mstari wa
mbele kutuhudumia kwa neno la Mungu na kuishi kama kielelezo cha injili unaweza
kushangaa kwamba kuna chuki, vijembe, uadui na hata ugomvi, visa na visasi,
Chuki chuki chuki kila mahali ulimwenguni, ziko chuki za watu kwa sababu ya
ukabila, ziko chuki za watu kwa sababu ya rangi, ziko chuki za watu kwa sababu
ya kuishi maisha ya mashindano, ziko chuki kwa sababu ya mafanikio ya mtu
mwingine, ziko chuki kwa sababu ya kuchukuliana waume, wake,tofauti za kiimani
au kihistoria na kadhhalika, Chuki ni ushahidi ulio wazi kuwa bado watu wako
gizani 1Yohana 2:9 “Yeye asemaye kwamba yumo nuruni,
naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa.” Mwanafunzi wa Yesu
ni yule anaweza kudhihirisha upendo wake hata kwa wale wanaomuudhi na kumtendea
vibaya.
Iwapo watakuchukia.
Iwapo watakuchukia! Ni ishara
kwamba ziko sababu ambazo kwazo zinaweza kupelekea ulimwengu ukakuchukia kama
umeokoka lakini vilevile hata kama hujaokoka bado unaweza ukachukiwa na watu
wengine kwa sababu kadhaa, Biblia ina majibu ya kutia moyo kwa niniwatu
wanakuchukia ziko sababu nyingi lakini zifuatazo ni baadhi na zinaweza kukutia
moyo ukiona watu wanakuchukia fahamu!
1. Wewe si wa ulimwengu huu,
Yohana 15:18-25 “Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi
kabla ya kuwachukia ninyi.Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda
walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua
katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno
nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi,
watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu. Lakini haya
yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka.
Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana
udhuru kwa dhambi yao. Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba yangu. Kama
nisingalitenda kwao kazi asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi;
lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia. Lakini litimie lile
neno lililoandikwa katika torati yao, Walinichukia bure.” Yesu anazungumza maneno ya kutia moyo sana
kama mkuu wa wajenzi sitamani kuongeza lolote ni kama Yesu amemaliza kila kitu
kwamba ukiona watu wanakuchukia wewe ujue si wa ulimwengu huu viwango vyako zi
vya kawaida wewe uko juuu, wewe sio kama bata au kuku ndege wa chini wewe ni wa
viwango vya juu, Maandiko yanaonyesha wazi kuwa Yesu alikiri kuwa yeye mwenyewe
sio wa ulimwengu huu, Yohana 17:16 “Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.”
Yesu hakuwa wa ulimwengu huu na ndio maana walimchukia kila mtu aliyeokolewa
anapaswa kufahamu kuwa yeye sio wa ulimwengu huu na kamwe ulimwengu hauwezi
kukufurahia wakufurahiaje wewe ni wa tofauti wakuungeje mkono umewazidi wewe ni
wa juu wao ni wa chini wakupendee nini? Wewe ni mtu ambaye ulimwengu haukustahili
kuwa nawe Waebrania 11: 32-38 “Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta
habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za
manabii; ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata
ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali
ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita,
walikimbiza majeshi ya wageni. Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa.
Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate
ufufuo ulio bora; wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa
mafungo, na kwa kutiwa gerezani; walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno,
walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo
na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya; (watu ambao
ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na
katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi.”
2. Ndoto zako kubwa sana!
Mwanzo 37:3-19 “Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa uzee
wake, akamfanyia kanzu ndefu. Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao anampenda
kuliko ndugu zake wote, wakamchukia, wala hawakuweza kusema naye kwa amani.
Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia; akawaambia,
Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. Tazama, sisi tulikuwa tukifunga
miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda
yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. Ndugu zake wakamwambia, Je!
Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa
ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake. Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia
ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi
na nyota kumi na moja zikaniinamia. Akawaambia baba yake na ndugu zake; baba
yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako
na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi? Ndugu zake wakamhusudu; bali baba
yake akalihifadhi neno hili. Ndugu zake wakaenda kuchunga kondoo za baba yao
huko Shekemu. Israeli akamwambia Yusufu,
Je! Ndugu zako hawachungi kondoo katika Shekemu? Njoo, nikutume kwao.
Akamwambia, Mimi hapa. Akamwambia, Enenda, basi, ukaone kama ndugu zako
hawajambo, na kundi nalo li salama, ukaniletee habari. Basi akampeleka kutoka
bonde la Hebroni, akafika Shekemu. Mtu mmoja akamkuta, naye alikuwa
anazunguka-zunguka katika nyika; yule mtu akamwuliza, akisema, Unatafuta nini?
Akasema, Nawatafuta ndugu zangu; tafadhali uniambie mahali wanakochunga. Yule
mtu akasema, Wametoka hapa, maana niliwasikia wakisema, Twendeni Dothani. Basi
Yusufu akawafuata ndugu zake akawakuta huko Dothani. Wakamwona toka mbali, na
kabla hajawakaribia, wakafanya shauri juu yake ili wamwue. Wakasemezana wao kwa
wao, Tazama, yule bwana wa ndoto anakuja”. Unapokuwa na ndoto kubwa kamwe usitarajie
dunia itakukubali dunia haiwezi kuvumilia ndoto zako ndugu zake Yusufu
walimchukia kwa sababu alipendwa sana na baba yake na alikuwa mtu mwenye maono
ya mbali, watu wanaweza kukuonea wivu na kukuchukia kwa sababu umewazidi
viwango vya kufikiri, haushikiki, wewe sio wa kawaida una kitu cha ziada
wakupendee nini ndugu ukiona watu wanakuchukia usiwasimulie ndoto zako
haiyamkini hawawezi kustahimili ndoto na maono na akili na uweza ulio nao.
3. Sifa zako ni kubwa kuliko zao.
1Samuel
18:6-9 “Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi
aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya
Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari,
na shangwe, na vinanda. Nao wale
wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi
makumi elfu yake. Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza;
akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena
awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme? Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile”. Ndugu yangu ukiona watu wanakuchukia,
wanakuhusudu, wanataka kukuua, wanataka uangamie kabisa, wanataka uanguke,
wanataka mabaya yakupate wanapanga mabaya na magumu dhidi yako jua ya kuwa sifa zako ni
kubwa sana, nikubwa mno adui zako hawawezi kustahimili kuzibeba watafanya nini
sasa watatafuta kukuua watakuchukia watakuogopa wewe umekuwa tishio kwao,
unawazidi una kitu cha ziada una akili una kibali kwa Mungu, kama hungelikuwa
na kitu wangekuhurumia tu, Kumbuka kila mara unapopata sifa kubwa kuliko
wengine wanadamu wenye wivu watatafuta kuchafua sifa zako, watashangilia
utakapojikwaa, watakuza udhaifu wako ili wakumalize kabisa Daniel 6:1-5 “Ilimpendeza Dario kuweka juu
ya ufalme maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote; na juu yao akaweka
wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao; ili maliwali hawa watoe hesabu
kwao, mfalme asipate hasara. Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na
maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka
juu ya ufalme wote. Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za
kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu
wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia
ndani yake. Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli
huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake”.
4. Umejaa neema na uwezo.
Matendo 6:8-15
Mungu anapokuwa amekupa neema na uwezo jambo hili pia linaweza kualika maadui
angalia Matendo 6:8-15 “Na Stefano, akijaa neema na
uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu. Lakini baadhi ya
watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la
Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na
Stefano;lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na
huyo Roho aliyesema naye.Hata wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu
akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu. Wakawataharakisha watu na wazee na
waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza. Wakasimamisha
mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya
mahali hapa patakatifu na juu ya torati; maana tumemsikia akisema kwamba Yesu
huyo Mnazareti atapaharibu mahali hapa, na kuzibadili desturi tulizopewa na
Musa. Watu wote walioketi katika ile baraza wakamkazia macho yao, wakamwona uso
wake kuwa kama uso wa malaika”. Unaona Stefano alikuwa amejaa neema na
uwezo wa Mungu.Mungu alikuwa akimtumia kwa miujiza na ishara kubwa sana , Mungu
alimpa hekima ya kupita kawaida, alikuwa mmnenaji Hodari, alijaa Roho
mtakatifu, watu walioshindana naye hawakumuweza, walimchukia na kumzushia
maneno ya uongo na kutafuta kumuua,mtu huyu alikuwa mwema alijaa upako na uzuri
uso wake ulikuwa kama wa malaika, watu walitafuta kumuangamiza na wakamuua,hii ilikuwa chuki dhahiri kwani
Stefano hakutenda neno ovu lolote, Lakini kwa vile alikuwa amewazidi watu
katika neema na uwezo aliuawa, kumbuka kila talent utakayopewa na Mungu wenzako
wakigundua kuwa inawafunika wakaacha kumtazama Mungu anayewapa watu bila
upendeleo wakakuangalia wewe watakuchukia na matokeo yake watakuua.
5. Wewe ni wa Roho.
Wagalatia
4:29 “Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa
kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa.”
Biblia inaonyesha kati ya chuki zilizokuweko kati ya Ishmael kwa Isaka na
inaonyesha kuwa sababu kubwa ya chuki ya Ishmael kwa Isaka ni kwa sababu mmoja
alikuwa wa mwilini na mwingine alikuwa wa Roho, chuki na uonevu unaoletwa juu
yako unatokana na wewe kuwa rohoni wewe umezaliwa kwa roho wewe ni mwana wa Mungu
weweni mrithi wa ahadi zilezile za Ibarahimu na Isaka na Yakobo.Mi lazima
utachukiwa,wewe umezaliwakwa Mapenzi ya roho na sio ya mwili Yohana 1:12-13 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio
wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya
mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu”
6. Bwana yuko Pamoja nawe na umebarikiwa
Ni
muhimu kufahamu hata kama wakati mwingine huwezi kujua kuwa una kitu gani cha
ziada lakini pale unapoona watu wanakuchukia ni muhimu ukafahamu kuwa sio
wakati wote unachukiwa kwa sababu wewe haufai, hapana, watu wanaweza kukuchukia
na hata kukufukuza kwa sababu wanaona katika ulimwengu war oho Bwana yuko
pamoja nawe na kuwa umebarikiwa angalia Mwanzo
26:12-31 “Isaka akapanda mbegu katika nchi ile,
akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, BWANA akambariki. Na mtu huyu akawa
mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana. Akawa na mali ya kondoo, na mali
ya ng'ombe, na watumwa wengi. Hao Wafilisti wakamhusudu. Na vile visima vyote
walivyochimba watumwa wa baba yake, siku za Ibrahimu babaye, Wafilisti walikuwa
wamevifukia, wakavijaza kifusi.
Abimeleki akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana
kuliko sisi. Basi Isaka akatoka huko akapiga kambi katika bonde la Gerari,
akakaa huko. Isaka akarudi akavichimbua
vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye; maana wale
Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye akaviita
majina kufuata majina alivyoviita babaye. Watumwa wa Isaka wakachimba katika
lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika. Wachungaji wa Gerari
wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo akakiita
jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye. Wakachimba kisima
kingine, wakagombania na hicho tena. Akakiita jina lake Sitna. Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala
hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa
BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi. Akapanda kutoka hapo mpaka Beer-sheba. BWANA
akamtokea usiku uleule, akasema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako, usiogope,
maana mimi ni pamoja nawe, nami nitakubarikia, na kuzidisha uzao wako kwa ajili
ya Ibrahimu mtumishi wangu. Akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.
Akapiga hema yake huko, na watumwa wa Isaka wakachimba kisima huko. Ndipo
Abimeleki akamwendea kutoka Gerari, pamoja na Ahuzathi rafiki yake, na Fikoli,
jemadari wa jeshi lake. Isaka
akawauliza, Mbona mwanijia, nanyi mmenichukia, mkanifukuza kwenu? Wakasema,
Hakika tuliona ya kwamba BWANA alikuwa pamoja nawe; nasi tukasema, Na tuapiane,
sisi na wewe, na kufanya mapatano nawe ya kuwa hutatutenda mabaya, iwapo sisi
hatukukugusa wewe, wala hatukukutendea ila mema, tukakuacha uende zako kwa
amani; nawe sasa u mbarikiwa wa BWANA. Basi
akawafanyia karamu, nao wakala, wakanywa. Wakaondoka asubuhi na mapema,
wakaapiana wao kwa wao, kisha Isaka akawapa ruhusa, nao wakaenda zao kwa amani.”
7. Maisha yako yanapoathiri yao kuliko yao
kuathiri yako.
Tabia na mwenendo utendaji na maisha ya Yesu Kristo ulikuwa
na athari kubwa sana kwa Mafarisayo na masadukayo ni ukweli uliokuwa wazi kuwa
Yesu alikuwa anaendelea kupata umaarufu mkubwa
na mafarisayo walijiona kuwa wanapoteza umaarufu, ulimwengu ulikuwa unakwenda
nyuma ya Yesu hii ilijumuisha Yesu kukubalika sio na wayahudi tu bali hata
wagiriki yaani wayunani dunia ilikuwa imamuendea Yesu, Yesu alikuwa ni kama
chumvi inayofanya mboga inoge na bila yeye isinoge unapoona wakati mwingine
watu wakikuchukia fahamu wazi kuwa Maisha yako yaanaathiri uwepo wao, unapoteza
Heshima yao,kupitia wewe Mungu yu afanikisha mambo na wao wanajiona kuwa sio
kitu nakwa sbabu hiyo watakuchukia Yohana
12:9-22 “Basi watu wengi katika Wayahudi walipata kujua
ya kuwa yeye yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili yake Yesu tu, ila wamwone na
Lazaro, ambaye Yesu alimfufua katika wafu. Nao wakuu wa makuhani wakafanya
shauri la kumwua Lazaro naye;maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi
walijitenga, wakamwamini Yesu. Nayo siku ya pili yake watu wengi walioijia
sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu; wakatwaa matawi ya
mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana! Ndiye
mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli! Naye Yesu alikuwa amepata
mwana-punda, akampanda, kama vile iliyoandikwa, Usiogope, binti Sayuni; tazama,
Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda. Mambo hayo wanafunzi wake
hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya
kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba walimtendea hayo. Basi wakamshuhudia wale
mkutano waliokuwapo pamoja naye alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua.
Na kwa sababu hiyo mkutano walikwenda kumlaki, kwa kuwa wamesikia ya kwamba
ameifanya ishara hiyo.Basi Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, Mwaona kwamba
hamfai neno lo lote; tazameni, ulimwengu umekwenda nyuma yake.Palikuwa na
Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye
sikukuu. Basi hao walimwendea Filipo,
mtu wa Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka
kumwona Yesu.Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kisha Andrea na Filipo
wakamwambia Yesu.
Yohana mbatizaji
alikuwa kiongozi mwenye nguvu sana hakuwa na wivu wala hakuathiriwa na hali ya
Yesu kuwa maarufu, wako watu wengine kwa sababu tu pale wengine wanapokuwa
maarufu kiasi cha kuathiri maisha yao,wanakuwa hawatambui mchango wa wengine na
wanaukataa, Yesu alikuwa anafanya kazi na kuwa na wanafunzi wengi kuliko Yohana
mbatizaji, hata wanafunzi wengine wa Bwana Yesu walikuwa wanahama kwa Yesu na
watu walimletea habari, lakini yohana hakuogopa wala kufadhaika bali alisema
yeye hana budi kuzidi bali mimi kupungua, huu ni moyo wa kipakee sana na ndipo
ukristo wetu unapopimwa unajisikiaje mwengine anapofanikiwa, anaposifiwa
anapokuwa maarufu kuliko wewe? Kama unajisikia vibaya unahitaji toba! Ni muhimu
kutambua mchango wa wengine kwani hakuna mtu asiyefanya kitu, viongozi dhaifu huponda kabisa kazi za
waliowatangulia kana kwamba hawana mchango wowote hili sio jambo jema, je
tunajisiakiaje pale washirika wa kanisa letu wanapoondoka kwenda kwa mchungaji
wakanisa lingine? Kama tunajisikia vibaya badala ya kusubiri neema ya Mungu
kutuinua na sisi kwa wakati wetu Yohana
3:22-30 “Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake
walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi; akashinda huko pamoja nao, akabatiza. Yohana
naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa
na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa. Maana Yohana alikuwa hajatiwa
gerezani. Basi palitokea mashindano ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja juu
ya utakaso. Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabi, yeye aliyekuwa pamoja nawe
ng'ambo ya Yordani, yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote
wanamwendea. Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa
amepewa kutoka mbinguni. Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi
siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake. Aliye naye bibi arusi ndiye bwana
arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia
sana sauti yake bwana arusi. Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi
kuzidi, bali mimi kupungua.”
8. Wanataka uwaabudu na kuwasujudia.
Ni
muhimu kufahamu kuwa wanadamu wanapokuwa na mafanikio makubwa sana na kadiri
wanavyobarikiwa na kupelekwa juu sana wanapaswa kukumbuka kuwa wanyenyekevu
sana vinginevyo ni rahisi kwao kuwa na kiburi na kutaka kuabudiwa na kusujudiwa
Biblia inasema imeandikwa utamuabudu na kumsujudia bwana Mungu wako peke yake Luka 4:5-8 5. “Akampandisha
juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia,
Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami
humpa ye yote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa
yako. Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu
yeye peke yake.” Unaona sio rahisi kwa mwanadamu aliyetukuka kujijua
kuwa anataka ibada lakini kiburi kinapoinuka ndani ya mwanadamu na shetani
akapata nafasi wanadamu hupenda kuchukua nafasi ya Mungu na kutaka waabudiwe
wao, je umewahi kusoma kisa cha
Mordekai na Haman umewahi kuona ni kwa kiasi Gani hamani alimchukia Mordekai na
sio yeye tu na kabila zima la wayahudi kwa sababu gani kwa sababu Mordekai
hakuinama wala kumsujudia, tunaposimama kidete katika imani yetu kwa Mungu
tunapaswa kutambua kuwa ni dhambi kumpa mwanadamu nafasi ya Mungu, wako watu
wengine wakishaona wamepewa kumiliki watu,au wameajiri watu, au ni wasimamizi
wa watu basi wanataka kila mtu awaogope na kuwa tetemekea na kama wanaona una
msimamo thabiti wala hutetemeshwi na mafanikio yake wala kile alicho nacho
anatafuta namna ya kukufanya umnyenyekee kwa kiwango cha kumuabudu na
kumsujudia Esta 3:1-6 biblia inasema
hivi “Baada ya hayo mfalme Ahasuero alimwongezea cheo
Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, akampandisha, akamwekea kiti chake juu ya
maakida wote waliokuwapo pamoja naye. Nao
watumishi wote wa mfalme, walioketi mlangoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia
Hamani, maana ndivyo alivyoamuru mfalme kwa habari zake. Bali Mordekai
hakuinama, wala kumsujudia.Basi watumishi wa mfalme walioketi mlangoni pa
mfalme wakamwambia Mordekai, Mbona wewe waihalifu amri ya mfalme? Ikawa,
waliposema naye kila siku asiwasikilize, wakamwarifu Hamani, ili kuona kama
mambo yake Mordekai yatasimama; maana alikuwa amewaambia ya kuwa yeye ni
Myahudi. Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia,
alighadhibika sana. Akaona si shani kumtia mikono Mordekai peke yake; maana
wamemjulisha kabila yake Mordekai; kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza
Wayahudi wote waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani,
watu wake Mordekai.” Katika injili pia tunao mfano wa Yesu Kristo
alipokuwa mbele ya Pilato Yesu hakujibu neno katika mashitaka yake, kwa namna
ya kustaajabisha Pilato alitumia mamlaka yake kumlazimisha Yesu amjibu na hapa
ndipo Yesu alipomjua kuwa ulicho nacho umepewa kutoka juu Yohana 19:10-12 “Basi Pilato akamwambia,
Husemi nami? Hujui ya kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua, nami nina mamlaka
ya kukusulibisha? Yesu akamjibu, Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu,
kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi
iliyo kubwa zaidi.” Majibu ya Yesu yalimfanya pilato kuogopa na kuwa
mpole, watu wengi waliopewa kitu na Mungu au mamlaka na Mungu huyatumia vibaya huyatumia
kunyanyasa wanyonge na pale wanapoona wanyonge hawako tayari kusujudia
wanawachukia je wewe unapendwa kuogopwa? Unachukia watu wanapoonyesha
kutokukutetemekea jifunze kukubali kushughulishwa na mambo manyonge na
tumuachie anayestahili kupokea utukufu apokee yeye tu.
9. Mungu amelikuza Jina lako.
Mungu
anapokusudia kumbariki mtu pia hulibariki jina la mtu huyo na kulikuza sana
angalia Mwanzo 12:1-3 Biblia inasema
“BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako,
na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami
nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe
uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na
katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa” Katika ahadi za Mungu kwa
Ibarahimu mojawapo ilikuwa ni kulikuza jina lake, ni wazi kama umepata kibali
kwa Bwana na wewe umrithi sawa wa ahadi zilezile za Ibrahimu Baba yetu wa
Imani, Jina lako litakuzwa sana kutokana na aina ya utumishi na Baraka ambazo
Bwana amezikusudia kwako, katika namna ya kushangaza sana Yesu alisema watu
wanaotuchukia au wanaokuchukia pia watafanya kila liwezekanalo kulitupa nje jina lako ili uonekane kuwa
hufai au uonekane kama kitu cha hovyo au kiovu angalia Luka 6:22-23 “Heri ninyi watu watakapowachukia,
na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa
ajili ya Mwana wa Adamu.Furahiwani siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama,
thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo”
Je umewahi kukutana na hali za namna hiyo maadui zako wanataka kukuchafua ili
kwamba usiinuke tena, ili kwamba uonekane kuwa hufai kwa lolote? Nini
kinatafutwa hapo wanataka kulifuta jina lako! Wanataka kulishusha wanataka
kuliharibu wanataka kulichafua kwa sababu gani Mungu amelikuza jina lako. Yesu
anatutia moyo kuwa hata hivyo thawabu yetu ni kubwa mbinguni.
10. Iwapo utainuka tena!
Endapo itatokea
kuwa maadui zako watagundua kuwa ulianguka aidha kimaisha, kiroho, kibiashara
kikazi na kwa njia nyingine zozote, wakati wote adui au dunia au ulimwengu
haauwezi kufurahi kugundua kuwa unainuka tena, watatamani ubaki vilevile,
watatamani usiinuke tena, swala hili lilikuwa dhahiri pale wakuu wa makuhani
walipogundua kuwa Yesu atafufuka angalia kwamba kwa ujinga mkubwa kabisa
waliomba wawekewe askari walilinde kaburi barabara ili kwamba Yesu asifufuke Mathayo 27:62-66. “Hata siku ya pili, ndiyo iliyo baada ya Maandalio, wakuu wa
makuhani, na Mafarisayo wakamkusanyikia Pilato, wakasema, Bwana, tumekumbuka
kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa akali hai, Baada ya siku tatu nitafufuka.
Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hata siku ya tatu; wasije wanafunzi
wake wakamwiba, na kuwaambia watu, Amefufuka katika wafu; na udanganyifu wa
mwisho utapita ule wa kwanza. Pilato akawaambia, Mna askari; nendeni mkalilinde
salama kadiri mjuavyo. Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile
jiwe muhuri, pamoja na wale askari walinzi”. Unaona ni tabia iliyo wazi
kwa watu wenye chuki kutofurahjia maendeleo yako watataka uendelee kuharibikiwa
na pale unapofanya matengenezo na kujipanga tena na wakagundua kuwa unainuka
tena ndipo maneno ya kejeli huanza kwanini kwa sababu hawawezi kufurahia
mafanikio yako na hata kuinuka kwako tena, watatoa maneno ya kejeli, watatukana
na wataweza hata kupigana nawe au kuipinga vikali kazi unayoifanya Nehemia 4:1-9 “ Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta,
akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi. Akanena mbele
ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge
wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa dhabihu? Au watamaliza katika
siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo
yameteketezwa kwa moto? Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata
hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe. Sikia, Ee
Mungu wetu; maana tunadharauliwa; ukawarudishie mashutumu yao juu ya vichwa
vyao, ukawatoe watekwe katika nchi ya uhamisho; wala usiusitiri uovu wao, wala
isifutwe dhambi yao, mbele zako; kwa maana wamekukasirisha mbele ya hao
wanaojenga. Basi tukaujenga ukuta; nao ukuta wote ukaungamanishwa kiasi cha
nusu ya kimo chake; maana watu walikuwa na moyo wa kufanya kazi. Lakini ikawa,
Sanbalati, na Tobia, na Waarabu, na Waamoni, na Waashdodi, waliposikia ya kuwa
kazi ya kuzitengeneza kuta za Yerusalemu inaendelea, na ya kuwa mahali
palipobomoka panaanza kuzibwa, basi wakaghadhibika mno; wakafanya shauri wote
pamoja kuja kupigana na Yerusalemu, na kufanya machafuko humo. Bali sisi
tulimwomba dua Mungu wetu, tena tukaweka walinzi, mchana na usiku, kwa sababu
yao, ili kuwapinga.” Unaona hakuna mwanadamu anayefurahia mafanikio yaw
engine, wako wachache tu wanaofurahia wengine kuwa kama wao au hata kuwazidi,
lakini kumbuka adui zako watafurahi kuona umeangamia, umeanguka na hauinuki
tena, iwapo wataona unainuka hawatafurahia.
11. Bila sababu.
Yohana 15;25
biblia inasema “Lakini litimie lile neno lililoandikwa
katika torati yao, Walinichukia bure” Biblia inaonyesha wazi kuwa wakati
mwingine sababu hizo za chuki hazijulikani torati ilitabiri kuwa kuna kuchukiwa
bure tu, pasipo sababu, hata hivyo wanasaikolojia wanasema kuwa mtu mwenye
chuki mara kadhaa huwa ni kama mtu anayejidhuru mwenyewe, ni mgonjwa
kiakili,kwa sababu mwisho wa siku hakuna faida atakayoipata, tu mwenye chuki
anaweza kumchukia mwingine kwa sababu hawezi kuwa kama wewe,unaweza kuchukiwa
kwa sababu ya vipawa na uwezo uliokuwa nao, au kwa sababu ya changamoto
unazotoa, au kwa sababu unafanya sana kuliko wengine, unaimba sana kuliko
wengine, nk lakini biblia imesema wakati mwingine bila sababu. Yaani walinichukia
bure!
1. Samehe wote wanaokuchukia.
Katika ulimwengu
uliojaa chuki kamwe hatuwezi kuiondoa chuki kwa kutumia chuki,ulimwengu
utaharibika kwaninsisi ni chumvi ya ulimwengu, ni muhimu kwetu kuwalipa mema
wale wanaotutendea mabaya na kuwahakikishia kuwa tumewasamehe kabisa, sisi sio
badala ya Mungu,Mungu mwenyewe atalipa kisasi,wala wanaotuchukia ni wadhaifu,
ni wagonjwa wanaumwa hivyo wahurumie kwa kuwasamehe kabisa, kiumbe mwenye nguvu
kabisa duniani ni yule anayesamehe na sio yule anayelipa kisasi. Mwanzo 50: 15-21 “Ndugu zake Yusufu walipoona ya kwamba baba yao amekufa,
walisema, Labda Yusufu atatuchukia; naye atatulipa maovu yetu tuliyomtenda.
Wakapeleka watu kwa Yusufu, kunena, Baba yako alitoa amri kabla ya kufa kwake,
akasema, Mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwaachilie ndugu zako kosa lao na dhambi
yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utuachilie kosa la watumwa wa
Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye. Nduguze wakaenda tena,
wakamwangukia miguu, wakasema, Tazama, sisi tu watumwa wako. Yusufu akawaambia,
Msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu? Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali
Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo
leo.Basi sasa msiogope; mimi nitawalisha na watoto wenu. Akawafariji, na kusema
nao vema.”
Watu wa daraja
la juu kabisa la kiroho husamehe, wenye chuki wanahitaji msamaha kwa sababu
wana matatizo ya kisaikolojia wanahitaji kuhurumiwa waombee kwa Mungu kwa
sababu “Luka 23:33-35 “Na walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, ndipo
walipomsulibisha yeye, na wale wahalifu, mmoja upande wa kuume, na mmoja upande
wa kushoto. Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa
mavazi yake, wakipiga kura. Watu wakasimama wakitazama. Wale wakuu nao walikuwa
wakimfanyia mzaha, wakisema, Aliokoa wengine; na ajiokoe mwenyewe, kama ndiye
Kristo wa Mungu, mteule wake”
2.
Chuki
itakupeleka Mahali pa Heshima.
Hakuna mtu
aliyechukiwa na wengine na huku anamtegemea Mungu ambaye mambo yake
yaliharibika au Bwana asimtokee tena, Ni muhimu kukumbuka kuwa chuki dhidi ya
Yusufu ilileta mafanikio katika maisha yake na hata ya wale waliomchukia,
3.
Kuna
thawabu kubwa sana Mbinguni.
Luka 6:22-23 “Heri
ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina
lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.Furahiwani siku ile na
kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao
waliwatenda manabii vivyo hivyo”
Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!
Rev. Innocent Kamote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni