Kumbukumbu la Torati 31:19-22 “Basi sasa jiandikieni wimbo huu, uwafundishe wana wa Israeli;
kawatie vinywani mwao, ili uwe shahidi kwangu wimbo huu, juu ya wana wa
Israeli. Kwa kuwa nitakapokwisha kuwatia katika nchi niliyowaapia baba zao,
imiminikayo maziwa na asali; nao watakapokwisha kula na kushiba, na kuwanda;
ndipo watakapoigeukia hiyo miungu mingine, na kuitumikia, na kunidharau mimi,
na kulivunja agano langu. Tena itakuwa, wakiisha kujiliwa na mambo maovu mengi
na mashaka, utashuhudia wimbo huu mbele yao kama shahidi, kwa maana
hautasahauliwa katika vinywa vya uzao wao; kwani nayajua mawazo yao wayawazayo,
hata sasa kabla sijawatia katika nchi niliyoapa. Basi Musa akauandika wimbo huu
siku iyo hiyo, akawafundisha wana wa Israeli.”
Utangulizi:
Moja ya urithi wa Muhimu sana
ambao wanadamu wameurithi tokea enzi za baba zetu ni habari ya kuimba, Maswala ya
uimbaji yanaonekana kabisa yalianzishwa na watu waliokuwa wametengwa na uso wa
Mungu kwa sababu ya dhambi za wanadamu, hivyo watu hao walitumia nyimbo kama
njia ya kujifariji wakiwa na matumaini kuwa Mungu atawarehemu
Mwanzo 4:17-22 “Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe. Henoko akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli; Mehuyaeli akamzaa Methushaeli; Methushaeli akamzaa Lameki. Lameki akajitwalia wake wawili, jina la wa kwanza ni Ada, na jina la wa pili ni Sila. Ada akamzaa Yabali; huyo ndiye baba yao wakaao katika hema na kufuga wanyama. Na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba yao wapigao kinubi na filimbi. Sila naye akamzaa Tubal-kaini, mfua kila chombo cha kukatia, cha shaba na cha chuma; na umbu lake Tubal-kaini alikuwa Naama.”
Kwa hiyo Biblia inamtaja Yubal kama mwanzilishi wa wapiga kinubi na filimbi, wao ulikuwa ni uzao wa Kaini ambao walitengwa na uso wa Mungu na hivyo walitafuta faraja na rehema na unafuu wa mioyo kwa kuimba hapa duniani.

Mziki leo hii umekuwa ni Lugha ya
kihisia ambayo inaunganisha watu kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwa mpira
wa Miguu, kwa Karne nyingi sana Mziki umekuwa faraja kubwa sana na njia ya
kuwasilisha hisia kali za kibinadamu, kutuliza nafsi na kujitia nguvu katika
roho zetu, Inaonekana kabisa katika maandiko kwamba moja ya njia kubwa sana ya
kujijenga nafsi hasa kwa mtu aliyepitia mateso na magumu kuimba ni njia ya hali
ya juu sana ya kujitia moyo hata katika Mungu, Biblia inashauri wazi kuwa mtu
wa kwenu akipatikana na mabaya aombe na ana moyo wa kuchangamka na aimbe zaburi
angalia katika
Yakobo 5:13 “Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.”
Unaona andiko hili lina suluhu mbili maana yake hasa wakati mtu anapopatwa na maswala mazito, majaribu na kadhalika au mafanikio na furaha vyote hisia zote mbili zinaweza kupokelewa kwa kuomba na kuimba, Lakini vilevile wakati wa Mateso unaweza kuliitia jina la Bwana kwa maombi na anapokujibu unaweza kumuimbia kwaajili ya utukufu wake na Rehema zake alizotuonyesha kwa sauti
Zaburi 50:15 “Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.”

Mziki uko karibu katika kila
tamaduni za watu wa Duniani, na unatofautiana kutokana na mazingira, kwa sababu
kila utamaduni una namna yake ya kutafasiri maana ya muziki na wimbo na kwa
mujibu wa historia ya hiyo jamii, Utafiti mdogo pia usio wa kisayansi unaonyesha
kuwa watu wa jamii iliyoteseka sana huwa wanaimba kwa hisia kali zaidi. Kwa
hiyo mziki unawakilisha hisia za watu duniani na wakati mwingine hata bila ya
kujua maneno yaliyomo kwenye wimbo husika kama umeimbwa kwa hisia unagusa hisia
ya aina binadamu mwingine aliyepo popote. Paulo mtume aliweza kuwatia moyo
Wefeso kuwa tunaweza kujengana na kusemezana kwa namna ya kipekee kwa njia
Zaburi, tenzi na nyimbo za rohoni, kwa hiyo mziki na wimbo unaweza kabisa
kuijenga jamii na kutunza mafundisho na maonyo na kuhekimisha watu na kutoa
shukurani
Waefeso 5:19 -20“mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;” Kwa hiyo muziki una uwezo mkubwa sana wa kujenga maendeleo ya Kanisa na taifa kwa ujumla!

Katika kifungu cha Msingi kwa
somo hili, Mungu anamwambia Musa aandike wimbo, bila shaka ulitungwa na Mungu
mwenyewe na kuwa awape wana wa Israel ilikuweza kutunza historia ya matendo
makuu ya Mungu, na kusudi jamii ijayo au kizazi kijacho kisiweze kusahau
matendo makuu ya Mungu, hata baada ya Musa kumaliza kazi zake duniani, Mungu
alijua wimbo utadumu na utaenda kizazi na kizazi na utawafunza watu na
kuwakumbusha kuhusu matendo yake
Kumbukumbu 32:44-47 “Musa akaja akasema maneno haya yote ya wimbo huu masikioni mwa watu, yeye na Yoshua, mwana wa Nuni. Musa akamaliza kuwaambia Israeli wote maneno haya yote; akawaambia, Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo nashuhudia kwenu hivi leo; nayo waamuruni watoto wenu, wayatunze na kuyafanya maneno yote ya torati hii. Kwa maana si jambo lisilofaa kwenu; maana, ni maisha yenu, na kwa jambo hili mtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki.”

Kama uimbaji wa mziki ni swala
linalokubalika kwa Mungu basi ni muhimu kwetu, kuangalia neno la Mungu
linatuambia nini kuhusu Muziki na kuimba.
Neno la Mungu na umuhimu wa kuimba na mziki!
Maandiko matakatifu yaani agano
la kale na agano jipya yanaunga mkono swala zima la kuimba na muziki kama
mojawapo ya njia ya juu kabisa ya kuabudu, uwepo wa swala la Muziki na uimbaji
katika maandiko unaonyesha wazi kuwa Mungu ameupa mziki na nyimbo umuhimu
mkubwa sana na kuwa njia ya juu kabisa ya kuonyesha uwezo wetu wa kumuabudu
Mungu ni pamoja na kumuimbia kabla ya wanadamu kugundua swala la muziki na
uimbaji inasemekana huko Mbinguni nyimbo na muziki vilikuwa vinatumika na
vinaendelea kutumika katika kumuabudu Mungu angalia
Isaya 14:11-15 “Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika. Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo”
.Maandiko haya yametumika sana na wanatheolojia kuyahusisha na anguko la Shetani aliyekuwa malaika mkuu na kiongozi mkubwa wa sifa nyota ya alfajiri au Lucifer yeye aliumbwa na uwezo mkubwa sana na kuimba na muziki akiwa moja ya maserafi wanaojua kusifu na kumuabudu Mungu kwa vinanda kama wazo hilimni kweli basi ninwazi kuwa uimbaji umetoka Mbinguni, na kama Mungu aliona umuhimu wa kumfundisha Musa wimbo kwaajili ya wana wa Israel ni wazi kuwa Mungu ndie mwanzilishi wa mziki na uimbaji, kwa hiyo ni wazi kuwa neno la Mungu linakubali kuwa uimbaji katika kusanyiko la watu wa Mungu yaani kanisa ni wa thamani kubwa sana katika kuonyesha namna na jinsi tunavyomuheshimu Mungu, kwa hiyo neno la Mungu linaruhusu matumizi ya vyombo vya muziki na aina flani ya mtindo wa kuabudu kwa vyombo hivyo wenye kufaa, na amri rahisi ni kumuimbia Mungu sawa na neno lake
Wakolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.”
Unaona sasa Neno la Mungu linaagiza kwamba tujae neno, yaani tulijue neno, tujifunze neno la Mungu kwa kina na mapana na marefu kisha tunaweza kulitumia kwa mafundisho kwa kuonyana, kwa kuliimba kama zaburi, tenzi na nyimbo kwa kadiri ya neema yake Mungu katika mioyo yetu! Kwa mtazamo wangu kuimba ndio ngazi ya juu zaidi ya maombi, naweza kusema kuwa mtu mwenye uwezo wa juu zaidi wa kuimba ndiyemwenye uwezo wa juu zaidi wa kukaribia uwepo wa Mungu au wa ibilisi, tunaweza kuonyesha kiwango chetu kikubwa sana cha kumpenda Mungu kupitia uwezo wetu mkubwa zaidi wa kuimba, mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu zaidi pia ndiye aliyekuwa muimbaji zaidi, na ndiyemwenye kitabu kirefu zaidi kuliko vyote katika agano la kale kitabu chenye zaidi ya asilimia saba ya agano la kale cha zaburi ni ushairi wa juu zaidi wa hisia za mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu, kadiri unavyoimba kwa hisia kali zaidi ndivyo unavyoweza kuugusa na kuufikia moyo wa Mungu na moyo wa mwanadamu hivyo uimbaji ni huduma kubwa sana ya upatanishi ni huduma ya kikuhani!.

a.
Biblia
imeagiza watu waimbe
Mungu ametuumba
ili tumuabudu, sisi ni vyombo vyake na ametuumba tukiwa na uwezo wa kuimba na
kutengeneza muziki, wote tunajua sasa kwamba muziki ni wa muhumu sana katika
kuabudu biblia imeamuru sisi tumuimbie watu wasiojua umuhimu wa kuimba hawatoi
sauti zao wala hawajishughulishi kusikiliza maneno, kujumuisha hisia zao na
kufuatilia au kuitikia uimbaji katika ibada ni muhimu kufahamu kuwa Mungu
anataka tuimbe ni amri
i.
Zaburi
95:1-3 “Njoni, tumwimbie Bwana, Tumfanyie shangwe
mwamba wa wokovu wetu. Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa
zaburi. Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.”
ii.
Zaburi
98:1-8 “Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Kwa maana ametenda
mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea
wokovu. Bwana ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki
yake. Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho
yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu. Mshangilieni Bwana, nchi yote,
Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi. Mwimbieni Bwana zaburi kwa
kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi. Kwa panda na sauti ya baragumu.
Shangilieni mbele za Mfalme, Bwana. Bahari na ivume na vyote viijazavyo,
Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake. Mito
na ipige makofi, Milima na iimbe pamoja kwa furaha.”
iii.
Zaburi
150:1-6 “Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu
pake; Msifuni katika anga la uweza wake. Msifuni kwa matendo yake makuu;
Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. Msifuni kwa mvumo wa baragumu;
Msifuni kwa kinanda na kinubi; Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze
na filimbi; Msifuni kwa matoazi yaliayo;
Msifuni kwa matoazi yavumayo sana. Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya.”
iv.
Waebrania
2:12 “akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu;
Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa.”
v.
Waebrania
13:15 “Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu
ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.”
vi.
Unaweza kuona maandiko yanaamuru sisi
tumuimbie Mungu, Kama shauku yetu ni kuyatenda mapenzi ya Mungu, basi hakuna
kitu cha ziada cha kukitafuta zaidi ya kile ambacho Mungu ameagiza katika neno
lake jinsi na namna ya kumuabudu
b.
Watu wakubwa sana katika Biblia waliimba.
i.
Yesu Kristo na
wanafunzi wake waliimba angalia Mathayo
26:30“Nao walipokwisha kuimba, wakatoka nje kwenda mlima wa Mizeituni.”
ii.
Mtume
Paulo na Sila waliimba gerezani Matendo 16:25 “Lakini
panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia
nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.”
iii.
Mariam
mama yake Yesu aliimba Luka 1:46-55 “Mariamu akasema,
Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;
Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa
Vizazi vyote wataniita mbarikiwa; Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na
jina lake ni takatifu. Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao
wanaomcha. Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika
mawazo ya mioyo yao; Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; Na wanyonge
amewakweza. Wenye njaa amewashibisha mema, Na wenye mali amewaondoa mikono
mitupu. Amemsaidia Israeli, mtumishi wake; Ili kukumbuka rehema zake; Kama
alivyowaambia baba zetu, Ibrahimu na uzao wake hata milele”
iv.
Malaika
waliimba siku aliyozaliwa Masihi Luka 2:13-14 “Mara
walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu,
na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu
aliowaridhia.”
v.
Musa
na wana wa Israel na Miriam walipovuka bahari ya shamu Kutoka 15:1-3 “Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu
wakanena, na kusema, Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana; Farasi na
mpanda farasi amewatupa baharini. BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye
amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu,
nami nitamtukuza. BWANA ni mtu wa vita, BWANA ndilo jina lake.”
Aidha Nabii Musa kabla ya kifo chake ama wakati
anahitimisha maisha yake duniani alihitimisha kupitia nyimbo Kumbukumbu 32:1-43. Lakini pia
inaaminika kuwa Zaburi ya 90 ni
utunzi wa nabii Musa.
vi.
Yoshua
na Israel walipoukaribia Yeriko walipiga tarumbeta Yoshua 6:8-9 “Basi ikawa Yoshua alipokwisha kusema na watu, wale makuhani
saba, wenye kuzichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele za Bwana,
wakatangulia, wakazipiga hizo tarumbeta; nalo sanduku la agano la Bwana
likawafuata. Wale watu wenye silaha walikwenda mbele ya hao makuhani
waliozipiga tarumbeta, na wale waliokuwa nyuma wakalifuata hilo sanduku;
makuhani wakizipiga tarumbeta walipokuwa wakienda.”
vii.
Deborah
na Baraka waamuzi waliimba baada ya ushindi wao Waamuzi 5:1-3 “Ndipo Debora, na Baraka mwana wa Abinoamu, wakaimba siku ile,
wakisema; Kwa sababu wakuu walitangulia katika Israeli, Kwa sababu watu
walijitoa nafsi zao kwa hiari yao, Mhimidini Bwana. Sikieni, enyi wafalme;
tegeni masikio, enyi wakuu; Mimi, naam mimi, nitamwimbia Bwana; Nitamhimidi
Bwana, Mungu wa Israeli”
viii.
Sulemani
ni moja kati ya watu wakubwa sana ambao Mungu alipata kuwainua yeye naye
alikuwa muimbaji biblia inasema alitunga nyimbo 1005 japo nyingi zilipotea 1Wafalme 4:29-34 “Mungu
akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko
pwani. Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima
zote za Misri. Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi,
na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya
mataifa yote yaliyozunguka. Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake
zilikuwa elfu moja na tano. Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko
Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege,
na vitambaavyo, na samaki. Wakaja wa mataifa yote ili waisikie hekima ya
Sulemani, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima
yake.”
ix.
Daudi huyu
ndiye mtu mkubwa zaidi katika maswala ya kuimba na muziki au tungeweza kusema
huyu ndiye mwanamziki mkubwa zaidi kuliko wote katika maandiko, Katika Zaburi
150 zilizomo katika maandiko zaidi ya 75 hivi zimeandikwa na Daudi yeye
anatajwa kama mtungaji wa nyimbo za Israel
2Samuel 23:1 “Basi haya ndiyo maneno ya mwisho ya Daudi. Daudi, mwana wa Yese, anena, Anena huyo mtu aliyeinuliwa juu, Yeye, masihi wake Mungu wa Yakobo,Mtungaji wa nyimbo za Israeli mwenye kupendeza;” alikuwa na uwezo wa kuimba kwa upako kiasi cha kutoa pepo
1Samuel 16:14-23 “Basi, roho ya Bwana ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua. Nao watumishi wa Sauli wakamwambia, Angalia, sasa roho mbaya kutoka kwa Mungu inakusumbua. Basi bwana wetu na atuamuru sisi watumishi wake waliopo hapa mbele yako watafute mtu aliye stadi wa kupiga kinubi; basi itakuwa, roho ile mbaya kutoka kwa Mungu itakapokujilia, yeye atapiga kinubi kwa mkono wake, nawe utapona. Basi Sauli akawaambia, Vema, nitafutieni mtu aliye stadi wa kupiga kinubi, mkaniletee. Ndipo akajibu mmoja wa watumishi wake akasema, Tazama, nimemwona mwana mmoja wa Yese, Mbethlehemi, aliye stadi wa kupiga kinubi, tena ni mtu shujaa, hodari wa vita, anenaye kwa busara, mtu mzuri, ambaye Bwana yu pamoja naye. Basi Sauli akampelekea Yese wajumbe, akasema, Nipelekee Daudi mwanao, aliye pamoja na kondoo. Yese akatwaa punda, wa kuchukua mikate, na kiriba cha divai, na mwana-mbuzi, akampelekea Sauli kwa mkono wa Daudi mwanawe. Basi Daudi akamwendea Sauli, akasimama mbele yake, naye akampenda sana; naye akapata kuwa mtu wa kumchukulia silaha zake. Kisha Sauli akapeleka watu kwa Yese, akasema, Tafadhali, mwache Daudi asimame mbele yangu; maana ameona kibali machoni pangu. Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha.”
Wakati wa utawala wake Daudi aliunda kwaya ya makuhani kwaajili ya kumuabudu Mungu kwa njia ya mziki 1Nyakati 15:16-19
“Kisha Daudi akamwambia mkuu wa Walawi, kwamba awaagize ndugu zao waimbaji, pamoja na vyombo vyao vya kupigia ngoma, vinanda, na vinubi, na matoazi, wavipige na kupaza sauti kwa furaha. Basi Walawi wakamwagiza Hemani mwana wa Yoeli; na wa nduguze, Asafu mwana wa Berekia; na wa wana wa Merari ndugu zao, Ethani mwana wa Kishi; na pamoja nao ndugu zao kwa cheo cha pili, Zekaria, na Yaasieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu; na Benaya, na Maaseya, na Matithia, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na Yeieli, mabawabu. Hivyo hao waimbaji, Hemani, Asafu, na Ethani, wakaagizwa kupiga matoazi yao ya shaba kwa sauti kuu;”
1Nyakati 23:1-5 “Basi Daudi alikuwa mzee, ameshiba siku; akamtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme juu ya Israeli. Akawakusanya wakuu wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi. Nao wakahesabiwa Walawi wenye miaka thelathini na zaidi; na jumla yao kwa vichwa, mtu kwa mtu, ikapata thelathini na nane elfu. Katika hao ishirini na nne elfu walikuwa wa kusimamia kazi ya nyumba ya Bwana; na sita elfu walikuwa maakida na makadhi; na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu Bwana kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia.”

Kwanini muziki nimuhimu kwa mujibu wa neno la Mungu!
a.
Hutumika
kwaajili ya kuagana – Mwanzo 31:27 “Mbona umekimbia kwa
siri ukanihadaa, wala hukuniambia, nipate kuagana nawe uende zako kwa furaha,
na nyimbo, na ngoma, na kinubi?”
b.
Hutumika
kuiimbia miungu – Kutoka 32:17-18 “Na Yoshua aliposikia
kelele za watu walipokuwa wakipiga kelele, akamwambia Musa, Kuna kelele ya vita
maragoni. Akasema, Hiyo si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushinda
vitani, wala si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushindwa; bali
kelele za watu waimbao ndizo ninazozisikia mimi.”
c.
Hutumika
wakati wa kusimika viongozi – 1Wafalme 1:39-40 “Na
Sadoki, kuhani, akatwaa ile pembe ya mafuta katika Hema, akamtia Sulemani
mafuta. Nao wakapiga panda; na watu wote wakasema, Mfalme Sulemani na aishi!
Kisha watu wote wakapanda juu nyuma yake, watu wakapiga mazomari, wakafurahi
furaha kubwa mno, hata nchi ikapasuka kwa sauti zao.”
d. Hutumika kufundishia - Kumbukumbu la Torati
31:19-22 “Basi
sasa jiandikieni wimbo huu, uwafundishe wana wa Israeli; kawatie vinywani mwao,
ili uwe shahidi kwangu wimbo huu, juu ya wana wa Israeli. Kwa kuwa
nitakapokwisha kuwatia katika nchi niliyowaapia baba zao, imiminikayo maziwa na
asali; nao watakapokwisha kula na kushiba, na kuwanda; ndipo watakapoigeukia
hiyo miungu mingine, na kuitumikia, na kunidharau mimi, na kulivunja agano langu.
Tena itakuwa, wakiisha kujiliwa na mambo maovu mengi na mashaka, utashuhudia
wimbo huu mbele yao kama shahidi, kwa maana hautasahauliwa katika vinywa vya
uzao wao; kwani nayajua mawazo yao wayawazayo, hata sasa kabla sijawatia katika
nchi niliyoapa. Basi Musa akauandika wimbo huu siku iyo hiyo, akawafundisha
wana wa Israeli.”
e.
Hutumika
kuhamashisha – Muhubiri 2:7-9 “Nami nikanunua watumwa
na wajakazi, nikawa na wazalia nyumbani mwangu; tena nikawa na mali nyingi za
ng'ombe na kondoo, kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; tena
nikajikusanyia fedha na dhahabu, na tunu za kifalme na za kutoka katika
majimbo. Nikajipatia waimbaji, waume kwa wake, nao wale ambao wanadamu
wanawatunuka, masuria wengi sana. Basi nikawa mkuu, nikaongezeka kupita wote
walionitangulia katika Yerusalemu; pia hekima yangu nikakaa nayo.”
f.
Hutumika
kujenga umoja – Mziki unafanya kazi muhimu sana ya kuwaleta watu pamoja, aidha
katika huzuni au katika furaha au shereh, watu wanaweza kukusanyika pamoja na
kuburudika Luka 15:25-27. “Basi, yule mwanawe mkubwa
alikuwako shamba na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya
nyimbo na machezo. Akaita mtumishi
mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini? Akamwambia, Ndugu yako amekuja,
na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima.”
g.
Hutumika
kwaajili ya kujipa moyo – Yesu na
wanafunzi wake waliimba mara ya mwisho kabisa wakati Yesu anakaribia Marko
14:26 “Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda mlima wa
Mizeituni”. Zaburi 23:1-6 “Bwana ndiye mchungaji
wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando
ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika
njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa
mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo
yako vyanifariji. Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka
mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili
zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.”
h.
Hutumika
kwa maombolezo – Mathayo 9:23 “Yesu alipofika nyumbani
kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo,”
i.
Hutumika
katika kutoa Pepo 1 Samuel 16:14-23 “Basi, roho ya
Bwana ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua. Nao
watumishi wa Sauli wakamwambia, Angalia, sasa roho mbaya kutoka kwa Mungu
inakusumbua. Basi bwana wetu na atuamuru sisi watumishi wake waliopo hapa mbele
yako watafute mtu aliye stadi wa kupiga kinubi; basi itakuwa, roho ile mbaya
kutoka kwa Mungu itakapokujilia, yeye atapiga kinubi kwa mkono wake, nawe
utapona. Basi Sauli akawaambia, Vema, nitafutieni mtu aliye stadi wa kupiga
kinubi, mkaniletee. Ndipo akajibu mmoja wa watumishi wake akasema, Tazama,
nimemwona mwana mmoja wa Yese, Mbethlehemi, aliye stadi wa kupiga kinubi, tena
ni mtu shujaa, hodari wa vita, anenaye kwa busara, mtu mzuri, ambaye Bwana yu
pamoja naye. Basi Sauli akampelekea Yese wajumbe, akasema, Nipelekee Daudi
mwanao, aliye pamoja na kondoo. Yese akatwaa punda, wa kuchukua mikate, na
kiriba cha divai, na mwana-mbuzi, akampelekea Sauli kwa mkono wa Daudi mwanawe.
Basi Daudi akamwendea Sauli, akasimama mbele yake, naye akampenda sana; naye
akapata kuwa mtu wa kumchukulia silaha zake.Kisha Sauli akapeleka watu kwa
Yese, akasema, Tafadhali, mwache Daudi asimame mbele yangu; maana ameona kibali
machoni pangu. Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo
Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na
ile roho mbaya ikamwacha.”
j.
Unashusha
uwepo wa Mungu 2Nyakati 5:12-14 “tena Walawi waimbaji,
wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, hali
wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa
mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani mia na ishirini wakipiga panda;)
hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti
moja ya kumsifu na kumshukuru Bwana nao wakipaza sauti pamoja na panda na
matoazi na vinanda, wakimsifu Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana
fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya
Bwana, hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya
lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa Bwana.”
Vyanzo vya muziki:-
Mziki kutoka kwa Mungu Zaburi 40:3 “Akatia wimbo mpya kinywani mwangu, Ndio sifa zake Mungu wetu.
Wengi wataona na kuogopa, Nao watamtumaini Bwana”
Mziki kutoka kwa shetani- hii inakuwa na upako wa kishetani na huchochea na kuhamasisha na kukuza maswala ya uasi dhidi ya Mungu wa kweli.
Mziki kutoka kwa Mwanadamu Zaburi 57:7 “Ee Mungu, moyo wangu u thabiti, Moyo wangu u thabiti.
Nitaimba, nitaimba zaburi,”
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!
0718990796/0784394550
0718990796/0784394550
Maoni 2 :
If you're attempting to lose kilograms then you certainly need to start following this totally brand new custom keto meal plan.
To create this keto diet service, certified nutritionists, fitness trainers, and cooks united to develop keto meal plans that are useful, convenient, economically-efficient, and fun.
Since their first launch in early 2019, hundreds of clients have already completely transformed their body and well-being with the benefits a good keto meal plan can provide.
Speaking of benefits: in this link, you'll discover 8 scientifically-tested ones given by the keto meal plan.
Ahsante ndugu Mchungaji nimelielewa vizuri sana somo hili kwakweli umelifundisha kwa kina MUNGU wa Mbinguni may bless you
Chapisha Maoni