1Wakorintho 13:1-3 “Nijaposema kwa lugha za
wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu
uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote,
nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina
upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena
nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.”
Utangulizi:
Imani imekuwa ni mojawapo ya
jambo Muhimu sana ambalo limeelezewa kwa ajabu katika maandiko, Imani imetumiwa
na mashujaa wote wa imani tunaowasoma katika maandiko kama nyenzo ya kipekee
sana ambayo iliwaletea matokeo makubwa sana katika maisha yao
Waebrania 11:32-35 “Nami niseme nini tena?
Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na
Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani walishinda milki za
wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima
nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa
dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni. Wanawake
walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa,
wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora;”
Maandiko yanasema pasipo imani
haiwezekani kumpendeza Mungu, mtu awaye yote anayemuendea Mungu ni lazima
aamini kuwa Mungu yupo na kuwa huwapa thawabu wale wawamtafutao Waebrania 11:6 “Lakini
pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima
aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” Kwa msingi huo basi ni muhimu kufahamu
kuwa mashujaa wote wa imani tunaowasoma katika maandiko, pamoja na mambo mengine
vilevile walimuamini Mungu katika kiwango cha imani ya juu sana kiasi cha
kukubalika kwa Mungu, Abraham kwa mfano alipojaribiwa na Mungu kumtoa Isaka kwa
imani alikubali, yeye aliamini ya kuha hata akimkata kichwa Mungu atamfufua
tena kutoka kwa wafu na atarejea na mwanaye Waebrania 11:17-19 “Kwa
imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea
hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee; naam, yeye aliyeambiwa,
Katika Isaka uzao wako utaitwa, akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata
kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.”
Aina za imani!
Katika agano jipya iko imani
iokoayo, imani hii ni kumuamini Bwana Yesu kwa kukubali kazi aliyoifanya pale
msalabani, na kwamba alikufa na kufufuka imani hii hutupa zawadi ya wokovu,
imani hii kila mmoja anaweza kuipata kwa kumkubali Yesu kuwa bwana na mwokozi
Warumi 10:9-12 “Kwa sababu, ukimkiri Yesu
kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu
alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata
haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila
amwaminiye hatatahayarika. Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani;
maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao;”
Vilevile iko imani inayotokana na
kuwepo kwa karama ya Roho Mtakatifu, ambayo huitwa neno la Imani au neno la
mamlaka hii imetajwa katika 1Wakoritho
12:4-11 “Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni
yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. Kisha pana
tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika
wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja
kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye
yule; mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya
katika Roho yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na
mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;
lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu
peke yake kama apendavyo yeye.” Karama ya imani ni karama kwa mtu
aliyeokoka kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kutamka neno na likawa au
likasababisha muujiza mfano 1Wafalme
17:1 “Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi,
akamwambia Ahabu, Kama Bwana, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama
mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu.”
Hapa Eliya anatamka kwa neno la Mungu na kile anachokitamka kinakuwa
vilevile, Elisha pia alitamka kuuzwa kwa chakula kwa bei nafuu wakati kulikuwa
na njaa kali haijawahi kutokea njaa ambayo ilipelekea hata watu kula watoto wao 2Wafalme 6:24-30 24. “Ikawa baada ya hayo, Ben-hadadi mfalme wa Shamu
akakusanya majeshi yake yote, akakwea akauhusuru Samaria. Njaa ikawa kuu huko
Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa
vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya
fedha. Ikawa mfalme wa Israeli alipokuwa akipita ukutani, mwanamke mmoja
akamwita akisema, Unisaidie, bwana wangu, mfalme. Akasema, Bwana asipokusaidia, nikusaidieje
mimi? Ya sakafuni, au ya shinikizoni? Mfalme akamwambia, Una nini? Akajibu,
Mwanamke huyu aliniambia, Mtoe mtoto wako, tumle leo, na mtoto wangu tutamla
kesho.Basi, tukamtokosa mtoto wangu, tukamla; nikamwambia siku ya pili, Mtoe
mtoto wako, tumle; naye amemficha mtoto wake. Ikawa, mfalme alipoyasikia maneno
ya huyo mwanamke, aliyararua mavazi yake; (naye alikuwa akipita juu ya ukuta;)
na watu wakaona, na tazama, alikuwa amevaa magunia ndani mwilini mwake.”
Wakati hali halisi ikiwa ngumu kwa
kiasi hicho Elisha anatamka kuwa kesho panapo saa hii chakula kipimo cha unga
mzuri kitauzwa kwa shekeli ona 2Wafalme
7:1-10, “Elisha akasema, Lisikieni neno la Bwana;
Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa
shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria. Basi
yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa
Mungu, akasema, Tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili
lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini
hutakula. Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji;
wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe?
Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi
tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami;
wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu. Basi wakaondoka kabla ya
mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo
cha Washami, kumbe! Hapana mtu. Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami
kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi
kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na
wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi. Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali
giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile
vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao. Basi wale wenye
ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na
kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha;
wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda,
wakavificha. Ndipo wakaambiana, Mambo haya tufanyayo si mema; leo ni siku ya
habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara
yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme. Basi wakaenda,
wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama,
hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda
wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha.” Kisha ikawaje ona neno la Mungu alilolisema
Elisha lilitimizwa vilevile kama alivyotamka 2Wafalme 7:16-20 “Basi watu wakatoka,
wakaziteka nyara hema za Washami. Ikawa kipimo cha unga mzuri kikauzwa kwa
shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, sawasawa na neno la Bwana.
Naye mfalme akamweka yule akida, ambaye alitegemea mkono wake, awasimamie watu
langoni; na watu wakamkanyaga langoni, akafa; kama alivyosema yule mtu wa
Mungu, aliyenena hapo mfalme alipomshukia. Ikatukia kama vile yule mtu wa Mungu
alivyomwambia mfalme, Vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, na kipimo cha unga
mzuri kwa shekeli, ndivyo vitakavyokuwa kesho, panapo saa hii, katika lango la
Samaria; na yule akida akamjibu mtu wa Mungu, akasema, Sasa tazama, kama Bwana
angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akasema, Angalia,
wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula. Ikampata vivyo hivyo, kwa kuwa
watu wakamkanyaga langoni, akafa.”
Mungu anatutaka tuwe na imani,
tujiungamanishe naye katika kiwango cha kuwa na imani ya kuhamisha milima,
kimsingi Mungu hafurahii sana kuona wakristo wanashindwa jambo, Yesu aliwakemea
wanafunzi wake mara kwa mara kwa sababu walikuwa wanakosa imani hii
Mathayo17:15-20 “Bwana, umrehemu mwanangu,
kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na
mara nyingi majini. Nikamleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya. Yesu
akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi
hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu. Yesu akamkemea
pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile. Kisha wale wanafunzi
wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa? Yesu
akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia,
Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa
uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.”
Sasa ni imani ya namna gani
inahitajika ili kuhamisha milima Yesu anasema mkiwa na imani ndogo tu kiasi cha
punje ya haradali mtauambia mlima huu ondoka hapa nao utaondoka huitaji imani
kubwa sana unahitaji imani kidogo sana katika Mungu kukuletea ushindi na kutoa
matamshi yenye mamlaka ya kiungu na mara moja utaweza kuona dunia ikishikishwa
adabu
Mathayo 13:31-32 “Akawatolea mfano
mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali,
aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake; nayo ni ndogo kuliko mbegu zote;
lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti, hata nyuni wa
angani huja na kukaa katika matawi yake.”
Kumbe kiasi cha imani
kinachohitajika ni kidogo tu nah ii ni kuonyesha kuwa watu wengi hawana imani,
Mungu arupe kuwa na imani, Musa alikuwa mtu wa imani na alipokuwa akitamka
jambo wakati mwingine hata kabla, hajaliomba Mbingu ziliweza kutekeleza matakwa
yake ona:-
Hesabu 16:28-32 “Musa akasema, Kwa jambo
hili mtajua ya kwamba Bwana amenituma, ili nifanye kazi hizi zote; kwa kuwa
mimi sikuzifanya kwa akili zangu mwenyewe. Kama watu hawa wakifa kifo cha
sikuzote, kama watu wote wafavyo, au kama wakipatilizwa kwa mapatilizo ya watu
wote; hapo basi Bwana hakunituma mimi. Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo
nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia
shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau Bwana Basi
ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao
ikapasuka; nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na
wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote.”
Matamshi haya ya kimamlaka
yatatuletea ukombozi, mkubwa sana katika maisha yetu Mungu ataifanya dunia
ijuie na ifahamu ya kuwa yuko Mungu, mwenye nguvu na mamlaka nay a kuwa neno
lake haliongopi kamwe, wakristo tuinuke na kuwa waombaji na kuitafuta mamlaka
hii ili kushikisha adabu watu wasio na uelewa kuhusu Mungu
Ni milima ya namna gani inayozungumzwa hapa?
Niliwahi kumsikia mwanatheolojia
mmoja mkubwa sana na msomi akizungumzia kuwa Yesu alipokuwa akizungumzia mlima
au milima alikuwa akizungumzia mlima halisi au milima halisi, ni ukweli ulio
wazi kuwa lugha inayozungumzwa kibiblia ni lugha ya kinabii, na kinabii maandiko yanapozungumzia mlina
yanamaanisha kikwazochochote kigumu, jambo lolote lililogumu, kwa hiyo
inahitajika wazo la kinabii na kimaandiko kujua kuwa Yesu aliposema utahamisha
mlima au Paulo mtume anapozungumzia imani ya kuhamisha milima wote kwa pamoja
katika mioyo yao na jamii ya wale waliokuwa wakizungumza nao walielewa alikuwa
anazungumzia vikwazo vinavyoinuka juu ya mtu, au jaribu au jambo gumu unaweza
kuona, Milima hii ni vikwazo vya namna mbalimbali vinavyoweza kujitokeza katika
maisha yetu, lolote linalozuia breakthrough au mpenyo katika maisha yako,
upinzani, magonjwa, kifo, Magumu, yanayoonekana hayawezekani, na hali zenye
utata katika maisha yetu hizi zote zinaweza kuitwa mlima ona
Zakaria
4:6-7 “Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno
la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa
roho yangu, asema Bwana wa majeshi. Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya
Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu
kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie.”
Unaona lugha ya kinabii kamwe
haimaniishi kuwa mlima unaotajwa ni mlima halisia HAPANA Mungu hawezi kupinga
ana kanuni yake ya kimaumbile kumbuka wakati anaumba ulimwengu alihitimisha kwa
kusema tazama kila kitu ni chema, sisi tu nao uwezo wa kuchagua ni mahali gani
pa kuishi unaweza kuamua kuishi bondeni au mlimani kwa kadiri ya uumbaji wa
kiungu, hatusomi katika historia wala shuhuda kuwa kuna mtu aliweza kuondoa
mlima mahali, lakini kwa lugha ya kinabii mlima ni changamoto ngumu
zinazikinzana na maisha yetu ya kila siku
Isaya 40:3-5 “Sikiliza, ni sauti ya mtu
aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Nyosheni jangwani njia kuu kwa
Mungu wetu. Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa;
Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patasawazishwa; Na utukufu wa
Bwana utafunuliwa, Na wote wenye mwili watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha
Bwana kimenena haya.”
Unaona? milima hapa sio halisi
ndugu zangu, milima inayotajwa hapa ni lugha ya mficho (Figurative) kama nilivyosema awali ni imani pekee ndiyo inayoweza
kutuondolea mambo magumu ya kuyasawazisha hii maana yake yala yaliyoinuka juu
yetu yanakuwa si kitu tena mbele yetu, kwa hiyo hakuna kitakachoweza kusimama
mbele yako kutoka kwa mwaname au mwanamke kama utakuwa na imani
Marko 11:22-24 “Yesu akajibu, akamwambia,
Mwaminini Mungu. Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka
ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo
asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo
mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.”
Mathayo 21:21-22. “Yesu akajibu,
akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si
hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng'oka, ukatupwe baharini,
litatendeka. Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.”
Lugha hiyo pia ni lugha ya
kukazia (hyperboles)kuonyesha namna
na jinsi imani isivyoshindwa kitu na kuwa tunapomuamini Mungu na hata
tunapomuomba Mungu kwa imani ni lazima tuamini na kusadiki kuwa lazima
kutakuwepo matokeo makubwa sana.
Je imani yetu inaweza kuhamisha milima?
Ndio wakati wote tunapokuwa na
imani imani hufanya mambo makubwa sana, lakini kuna maswala kadhaa ambayo
yakikosekana katika maisha yetu tunaweza kuona mambo yakiwa ndivyo sivyo! Mathayo 17:14-21 1 “Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti,
akisema, Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya;
maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini. Nikamleta kwa
wanafunzi wako, wasiweze kumponya. Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi
kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana
nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu. Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule
kijana akapona tangu saa ile. Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha
wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa? Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu
wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya
haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala
halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. [Lakini namna hii haitoki ila kwa
kusali na kufunga.]”
Wanafunzi wa Yesu walishindwa
kumtoa pepo na Yesu aliwaonyesha sababu za kushindwa kwao, na kwanza aliwakemea
mara kadhaa kwa sababu ya kukosa imani, kutia shaka, kuogopa jambo ambalo ni
kinyume na imani.
Marko 4:40 “Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?”
Marko 9:19 “Akawajibu, akasema, Enyi kizazi
kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Nichukuliane nanyi hata lini? Mleteni
kwangu.”
Mathayo 14:31 “Mara Yesu akanyosha mkono
wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? ”
hawakuwa na imani kabisa kuna
maswala kadhaa ambayo yakikosekana kwako hutawexa kuona Baraka za kiutendaji
katika imani
1.
Ukikosa imani
2.
Ukiacha kuomba
3.
Ukiacha kufunga
4.
Ukiacha kulitumia neno la Mungu
Siri kubwa ya ushindi na imani
inayoweza kuleta matokeo inakaa katika maswala hayo niliyoyataja ukiwa na tabia
hizo unaweza kuondoa mlima wowote unaoweza kujitokeza katika maisha yako, Mathayo 17:21 “[Lakini
namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]” Lakini kama
inavyoelezwa katika maandiko ya kwamba silaha za vita vyetu zina uwezo katika
Mungu hata kuangusha ngome 2Wakoritho
10:4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali
zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) ni kukosa muda wa
kuomba, kusoma neno la Mungu na kufunga ndiko kunakotuletea changamoto kuwa
gumu katika maisha, tunapofanyia kazi maombi, neno na kufunga tunaifanya imani
yetu kukomaa na kuwa kali sana na kwa
sababu hiyo hakuna mlima unaowezxa kusimamam mbele yetu neno la Mungu ambalo ni
upanga war oho utarahisisha sana kazi yetu ya kuhamisha milima kwa haraka
wakati wote Yesu alikema kukosekana kwa imani na mambo yanayoweza kuifanya
imani kuwa imara ni hayo
Na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Maoni 1 :
Mungu akubariki sana kwa neno la kujenga na kukuza imani zetu
Chapisha Maoni