Jumatano, 2 Machi 2016

Hapa yupo Aliyemkuu Kuliko Sulemani


Mathayo 12: 38-42 Biblia inasema “38. Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. 39. Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona.  40. Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi.  41. Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona. 42. Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.” 



Kifungu hicho hapo juu cha maandiko ni cha muhimu sana na tunapokifanyia uchambuzi yakinifu itatupa mwanga wa kumfahamu Yesu Kristo kwa kina na upana na urefu zaidi, kifungu hiki ni matokeo ya mjadala uliokuweko kuhusu Yesu Kristo, Baada ya Wayahudi hasa jamii ya  mafarisayo kumnenea Yesu maneno mabaya zaidi, Baada ya kuwa Yesu amemponya mtu aliyekuwa ana pepo, kipofu na ni Bubu, Mathayo 12:22-23, Muujiza huu uliwashangaza watu na kumfanya Yesu aanze kukubalika miongoni mwa jamii kuwa “MWANA WA DAUDI” hii ilikuwa ni wazi kuwa walikubali kuwa Yesu ndiye MASIHI, ni wazi kuwa kwa kazi hii na nyinginezo alizozifanya Yesu zilipelekea watu kumuamini na kuondoa shaka kuwa ndiye mfalme ajaye kwa JIna la Bwana, Hata hivyo kwa sababu ya wivu wa Mafarisayo ambao waliona Yesu anaheshimika zaidi na kuwa gumzo kuliko wao waliamua kwa makusudi kuharibu kibali cha Yesu kwa kusema kuwa anatoa pepo kwa nguvu za mkuu wa Mapepo Belzebuli (Mathayo 12:24)

Yesu Kristo akitambua hilo alitoa hutuba kali sana ya maonyo dhidi ya watu wanaopinga kazi ya Mungu Roho mtakatifu, na zaidi ya yote aliwaonya watu kuhusu kuzungumza maneno yasiyo na maana kwa vile watatoa hesabu kwa kila neno lisilo na maana wanalolitoa katika vinywa vyao, Mathayo 12:33-37.

Baada ya hutuba hii ya Yesu ambayo ilikuwa kali na yenye maonyo baadhi ya Mafarisayo waliogopa sana Lugha “Hapo” inatumika kuonyesha kuwa iliwalazimu sasa waombe ishara ya kumfahamu Yesu vema kuwa yeye ni nani, Tupe ishara itakayotusaidia kukutambua wewe ni nani? Ndipo Yesu aliwajibu kwamba watamtabua kupitia Ishara kuu mbili.

1.       Ishara ya Nabii Yona.
Yesu aliwaeleza kwa uwazi kuwa Ishara ya kumtambua Masihi iko wazi, ishara hii ndiyo iliyowavutia watu wa Ninawi wakatubu na kumgeukia Mungu kupitia mahubiri ya Yona, Mathayo 12:38-41, Kimsingi Yesu alitaka kukazia kuwa kile kilichomtokea Yona kilikuwa ni ishara halisi, na kilikuwa ni kivuli cha kumtambua Masihi, ambaye Yesu alikazia kuwa ni mkuu kuliko Yona, Yesu alikazia kuwa namna njema ya kumtambua yeye nip ala atakapokufa na kufufuka siku ya Tatu, hii ndio kazia kubwa ya ukombozi itakayowavuta wengi katika ufalme wa Mungu.

2.       Ishara ya Malkia wa Sheba.
Yesu aliwapa Mafarisayo Ishara nyingine ya muhimu. Ambapo sasa anaeleza kuhusu Malkia wa kusini yaani Sheba kwamba alitoka mbali sana pande zamwisho wa Nchi kuja kusikiliza Hekima ya Sulemani, Yesu ni kama alikuwa anakazia kuwa njia nyingina ya kumtambua ni kumsikiliza, usikivu ungeliwasaidia kujua kuwa hakuna mwingine anayeweza kunena au kutenda katika kiwango kama cha Yesu, Mathayo 12:42 hata hivyo  mahali hapa ndipo paliponisukuma zaidi kufanya Uchambuzi hususani Yesu alipohitimisha kuwa malikia huyu alisafiri kutoka mbali kusikiliza Hekima ya Sulemani, hata hivyo Yesu alitamka wazi kuwa Yeye ni mkuu kuliko Sulemani.

Suleimani ni mfalme aliyeishi kwa anasa na ufahari wa hali ya juu, mfalme huyo alikuwa na Hekima na ufahamu na maarifa ya hali ya juu sana kuliko wafalme wote ambao wamepata kuweko, Biblia inasema kabla yake hajakuweko na badala yake hatokuweko 1Wafalme 3:9-13, 4;29-34 unaweza kuona!, wengi waliosikia Hekima ya Suleimani katika enzi zake walisafiri kutoka mbali ili kwenda kumsikiliza, Lakini ziara ya kifahari na maarufu sana na iliyoelezewa kwa kina ni safari ya Malkia wa Sheba au Ethiopia ambaye alikwenda kwa mikogo mingi na mikubwa  1Wafalme 10:1, 2Nyakati 9:1-6 Biblia inasema malkia huyu alikwenda akiwa na maswalai magumu sana “She came to Jerusalem to test him with Hard Questions” pamoja na ziara yake ya kifahari na zawadi kibao alizozibeba alipofika Yerusalem kwa Suleimani alijibiwa maswali yake yote  na mambo yake yote hata aliyokuwa ameyaficha sirini, hakuna kilichofichika kwa Suleimani, alitosheleza mahitaji yake yote na hisia zake zote zilijibiwa na kuzidi.

Dunia ya leo ina maswali magumu mengi yasiyo na majibu, pamoja na kuendelea na kukua kwamaarifa na uvumbuzi wa kisayansi na Teknolojia, Watu wanazidi kuharibikiwa dunia imejaa hekina ya uharibifu, wizi,ufisadi,uchochezi,uchoinganishi, majungu na fitina, kuliza wengine, kutoa mimba udanganyifu, na hakuna majibu ya maswala muhimu katika matatizo ya watu, Sulemani alikuwa na ujuzi zaidi ya wa kibailojia, Chemistry, Physics, aliishi kwa anasa kuliko mtu yeyote, mwisho aliona hekina na maarifa bila ya Mungu ni upuuzi au ubatili,alishauri watu kumkubuka Muumba wao siku za ujana wao, Muumba huyu ndiye mkuu kuliko Sulemani, Yesu Kristo anatajwa kama Hekima yetu 1Wakoritho 1:18 kwa kiyunani Epignosis sofia, Full of wisdom Knowledge and Understanding, yesu aliposema Hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani alimaanisha Yeye ndiye aliyemuumba huyo Sulemani, Yeye ndiye mwenye majibu yote hata ya mambo magumu, Yeye ndiye Masihi, ni zaidi ya mfalme Sulemani, watu watatoka kila pande za dunia kumjia yeye, na atawahukumu wote waliomkataa yey.

Hapa yupo aliye mkuu Kuliko Sulemani.

Jumatatu, 29 Februari 2016

Mwitaliano Orijino Akaletwa Kwangu!


Nakumbuka mwaka lakini tarehe na mwezi umenitoka kidogo, lakini ilikuwa ni mwaka 2002 Nilikuwa nauza duka la jamaa yangu kule temeke wakati ule, nilikuwa ndiyo nimemeliza kidato cha sita , nasubiri kwenda zangu vyuoni  Nilifika hapo temeke nikitokea nyumbani Handeni, nilipofika hapo niliona nijifanye mimi kuwa mtoto wa mjini  ili nipokelewe vizuri na vijana wenzangu. Ni kweli nilijifanya najua vitu vingi sana, nilikuwa naawaambia rafiki zangu kuwa nimesoma sekondari nchini Namibia ambapo baba alikuwa akifanya kazi kwenye ofisi za FAO. 


Mwitaliano Orijino alitaka kujichanganya jamaa wakaniletea


Nilikuwanawaambia kwamba nilikuwa natembea kwenye inchi kadhaa  za ulaya kwani baba yangu alikuwa akipata tiketi za bure kila mwaka  kusafiri na familia yeke kwa kweli sio siri nilibaini kuwa vijana wa Dar ni washamba  kuliko wale wa vijijini, kwa nini niliamini hivyo? ni kwa sababu waliamini kila nilichokuwa nikiwaambia na kuonyesha kuvutiwa sana kiasi kwamba pale dukani pakawa ni kijiwe kilichositawi, mara nyingi nilikuwa napenda kusisitiza sana kuwa nchini Italia tulikaa kwa miaka mitatu  wakati baba anasoma ambapo aliruhusiwa kwenda na familia yake niliwaambia kuwa hata masomo nilikuwa nasoma kwa kiitaliano na kuwa ninakikumbuka sana.

Nilizidi kuwaambia kwamba huwa ninakwenda ubalozi wa Italia hapa nchini  kupiga stori na baadhi ya watumishi wa pale kwa kiitaliano, niliwaambia huwa nafanya hivyo ili nisikisahau, Walikubaliana name na  kunitazama kwa heshimna kubwa , siku hiyo ya tukio  nikiwa dukani  walikuja jamaa zangu wawili  na Mwitaliano mmoja ambaye gari lake lilikuwa limaharibika  na alikuwa anatafuta msaada na pia ilionekana kuwa kuna jambo linguine anataka kulijua , niliposikia hivyo mashuzi na jasho vilianza kunitoka niliona wazi wazi kuwa kuadhirika kumewasili, Niliwaambia kuwa wakati ule niko bize  siwezi kwenda kumwona muitaliano huyo, wale jamaa zangu walinishawishi wakisema ni jambo zuri kwangu kwenda kani litanipandishia ujiko zaidi,, niliwaambia ni sawa lakini nisingeweza kuacha duka peke yake wala kulifunga. 

Wale jamaa zangu waliridhika na kuondoka, lakini kiasi cha dakika kumi baadaye  niliwaona wakija na mzungu alipofika na wale jamaa zangu waliniambia kuwa Yule ni muitaliano,  nizungumze naye , sikuwa najua hata neno moja la kiitaliano  ilibidi nizuge kwa kusema kwamba Yule jamaa huenda anatoka Italia ya kusini ambapo kiitaliano chao hata wenzao hawakielewi, nilijifanya namsemesha Yule mzungu kiitaliano kwa kusema Fkorsia deminati maneno ambayo hata mimi nilikuwa siyajui maana yake mwitaliano alibaki ameshangaa  na kuonyesha ishara ya kuwa hanielewi, wakati huo huo alipiata mzee mmoja ambaye aliuliza kinachoendelea  na kuamua kuingilia kati  kwa kuzungumza na Yule mzungu , walielewana sana na Yule mzee akampa Yule muitaliano maelekezo, alipoondoka Yule mzee aliniuliza nilipokuwa ninaishi kule Italia Nilimwambia Rome aliniuliza mtaa nikakwama  aluniuliza mambo mengine ambayo wala sikuwa nayajua nikakwama kabisa jamaa zangu walianza kucheka hadi machozi yakawatoka , kwa kweli nilibaki nimeduwaa, Yule mzee alisema hujafika Italia hata kwa kusoma kitabuni, Halafu aliondoka Jamaa zangu hawakuwa na mbavu, ilinibidi nifunge duka siku ile  kwa muda , kilitokea kitu gani baada ya hapo? Unataka nikujibu subiri naomba unionyeshe cheti chenye kuthibitisha kuwa niliwahi kuishi Mirembe.

Ukawa ni ugeni wa kupiga deki !



Nilitoka huko kwetu liwetwe Songea mara baada ya kumaliza elimu ya msingi, shangazi yangu alimuomba kaka yake ambaye ni baba yangu anichukue huku Dar es Salaam ili nimsaidie shughuli zake za mama nitilie, tulipanda basi la shabiby hadi hapa Dar safari yetu haikuwa nzuri nilisikia kizunguzungu na kutapikaa nia nzima, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kusafiri na kupanda basi kutoka kijiji chetu. 

 Mara yangu ya kwanza kupanda basi kutoka Songea kuja Dar es Salaam

Kijana niliyekuwa naye jirani alionekana kunihurumia sana kutokana na ile hali, Tulipofika ubungo kijana Yule alionesha wema kwangu kwani alitusaidia kushusha mizigo, tulipanda basi la ubungo mwenge – mbagala ili tufike keko shangazi alikokuwa anaishi.

Nilipenda sana mazingira ya keko kwani watu wa nyumbani walikuwa wengi hivyo sikuchelewa kuwa mwenyeji Shangazi alinichukua kwenye shughuli zake kutokana na ucheshi niliokuwa na adabu ya watu wa Songea hasa kitendo cha kuamkia watu, kuwapa chakula wateja na kuwakaribisha , kushukuru nikiwa nimepiga hatua  nikiwa nimepiga magoti kiliwafurahisha wateja . kati ya wateja waliokuwa wanajaza wateja wanajaza mgahawa wetu  ni pamoja na kijana niliyekaa naye siti moja wakati wa safari ya kutoka songea kuna vitu ambavyo  hutokea kwa njia ya ajabu  sana, tuilizidi kumpenda na kumuona ni ndugu yetu hasa, hatimaye kijana Yule aliutumia mwanya huo kumweleza shangazi nia yake ya kutaka tuwe wawili ili tuijaze dunia, sijui ni kwa nini  shangazi aliniruhusu kuhamia kwa Yule kijana kwani tulianza kuunganisha mwili na kuwatafuta hao watoto hata kabla ya ridhaa ya viongozi wa dini au wa mila  yetu na wazazi pia au alifanya hivyo ili kutoa muda kwetu wa kupimana tabia na mengineyo.

Siku ya nne baada ya kuhamia kwa huyo mshirika wangu, wifi yangu alikuja kunisalimia , aliniletea zawadi  ya unga mweupe wa muhogo  unaorowekwa kwenye maji, kule Songea tunaita kindowole na dagaa wa ziwa nyasa Niliushambulia ugali huo kama vile sina akili nzuri vile. Yaani niliula kwa pupa sana , Mshirika wangu siku ile alienda kazini  usikui ili arudi asubuhi. Hivyo ilipotimu majira ya saa sita hivi usiku nilisikia tumbo linauma kwa mtindo unaoashiria kuwa vyakula vyote vilivyomo tumboni vitoke nje Nilitoka chumbani kuelekea mlango wa kutoka nje  Mlango ulinishinda kufungua  na Uharo usiokuwa wa kawaida wala adabu ulinitoka, na kinyesi kilitapakaa pale mlangoni, kumbe inzi wa huku Dar hawalali waliamshana usiku ule na kushangilia neema ile iliyokuwa imewazukia. Wapangaji wenzangu  waliamshana na kusimama  kwenye milango ya vyumba vyao  huku wakiwa wameshangaa wazi na kunidharau, labda kwa kuniona mshamba . Kazi ya kupiga deki  ilianza usiku  huo huo Mpenzi wangu aliporudi kutoka kazini nilimsimulia yote yaliyotokea  na nilimuomba tuhame ila Mpenzi wangu hakuwa tayari kuhama  kwa wakati ule, kwa hiyo asubuhi ya silku ile  na siku zilizofuata zilikuwa ni za fedheha kwangu, Hatimaye hata hivyo tulihama, Hadi leo nikiona unga wa muhogo au ugali wa muhogo tumbo linafanya  fujo ya ghafla, kama vile kunipa tahadhari lakini huwa ninaula unapokuja kwenye anga zangu.  

Dada akaagiza tena Bwana!


Napenda watu wengine wajifunze kutokaa na uzoefu wangu na ndio maana naelezea kisa hiki najua wale wanaonifahamu watajua kwamba ni mimi, naomba hawa wachukulie kuwa nasimulia ili wengine wajifunze siyo kwa sababu nyingine, Mwaka 1996 nilikuwa nafanya kazi katika duka la vipuri vya magari lililokuwa eneo la msimbazi jijini Dar es Salaam, ukweli ni kwamba nilikuwa natengeneza pesa sana kwenye duka hili  zilikuwa ni fedha za wizi, labda ndio maana duka lenyewe halikudumu kwani lilifungwa mwaka 1996.

  
Nilikodolewa Mijimachi kila kona ya bar na Disco kwa kujifanya ninano kumbe ulofa tu!


Kwa hiyo baada ya duka kufungwa nikawa sina kazi, kwa sababu nilikuwa mtu wa matumizi sana, sikutaka kujishughulisha ghafla nilitaka kulinda hadhi na heshima yangu, kwa hiyo niliendelea na matanuzi yangu  nakumbuka ilikuwa juni 1997  yaliponikuta maswaiba haya 

Siku hiyo nilikwenda kwenye ukumbi mmoja maarufu wakati ule hapa Dar nasema wakati ule kwa sababu ndio ulikuwa unafunguliwa, nilikwenda pale kwa kupewa ofa ya kuingia ukumbini na rafiki yangu mmoja , aliniambia atanikatia tiketi  halafu maswala ya vinywaji ningejua mwenyewe, Nilikubali. Ni kweli baada ya kuingia ukumbini akamchukua bibi yake wakaenda kukaa kivyao, nilikuwa na shilingi 1000 mfukoni ambapo ningeweza kunywa bia kama mbili kwa wakati ule kwenye ukumbi kama ule, wakati naanza kunywa  bia niliyokuwa nimeagiza akaja msichana mmoja  ambaye awali sikuwa nimemtabua, baada ya kunisalimu kwa kunitaja nilimtambua  alikuwa ni msichana ambaye wakati nawika kwa fedha  niliwahi kufanya naye mapenzi, kwa bahati mbaya alisafiri kwenda Mauritius kwa kaka yake, haki ya Mungu leo nataka nikunywe hadi ukimbie nina hamu na pombe yako na mwili wako alisema, kabla sijajibu alimwita muhudumu  na kuagiza pombe kali nilijua kuwa ile oda moja tu ilihitaji 1000, nilijichangamsha na kujifaragua  lakini moyo wangu ulikwenda mbio nikianza kufikiria deni  la hiyo pombe nikiwa nafikiri aliagiza nyama choma, mazungumzo yalikuwa makali sana, huku binti Yule akinisanifu kwamba ninazo, nilijisikia vibaya ila sikuweza kusema, kufika saa sita usiku alikuwa amekunywa na kula kiasi cha shilingi 9000 mfukoni nilikuwa na 1000, bili ililetwa nilijua sina hela lakini ajabu sikusema hivyo, nilitulia huku nikitafakari, ingawa akili haikufanya kazi, baadaye kidogo  muhudumu alirudi kuchukua malipo. Alikuta sahani ya kuwekea hela iko tupu, aliondoka baadaye kidogo alirudi tena na kukuta sahani iko tupu haina kitu.

Aliuliza kwa upole ni nani anatakiwa kulipa , naomba malipo kwani namaliza shifti nilimwambia Yule mwanamke mwambie anayekupokea aje  nitamlipa yeye, Yule muhudumu alisema inanibidi nikamilishe hesabu ndipo niondoke, nilinyamaza halafu Yule msichana alianza kupayuka, alianza kunitukana na kunisimanga kwamba najifanya nina kitu wakati nimechoka, alinitukana hadi matusi ya nguoni, ilibidi watu waache burudani zao watupe macho na masikio kule kwetu na wengine walifika kabisa pale kwenye vurugu akiwemo na meneja wa ukumbi, kama unavyojua tena mitanzania kwa umbeya!

Nitalipa mimi achaneni na huyu bwege aende zake Pamoja na kuwa alikuwa amelewa nilijua alikuwa ananikomoa, nilitoka nje ya ukumbi kama aliyenyeshewa Nilikuja kugundua kuwa ile ilikuwa ni njama ya yule rafiki yangu aliyenipa ofa kunikomesha kujifanya bado nina pesa wakati nawapa shida wengine, ingawa haikuwa njia ya kiungwana kunifundisha lakini nashukuru kwani tangu wakati ule hadi leo maisha yangu sio ya kujionyesha bali naishi kama mimi. Cheki ulivyokodoa mimacho ishi kama Mungu alivyokujalia acha kujiinua!

Mtendeeni Yule Kijana Absalom kwa Upole kwaajili yangu!



Utangulizi
(2 SAMUEL 18:1-5) “1. Kisha Daudi akawahesabu watu waliokuwa pamoja naye, akaweka maakida wa elfu elfu, na maakida wa mia mia juu yao. ,2. Daudi akawapeleka hao watu vitani, theluthi moja chini ya mkono wa Yoabu, na theluthi ya pili chini ya mkono wa Abishai, mwana wa Seruya nduguye Yoabu, na theluthi ya tatu chini ya mkono wa Itai, Mgiti. Mfalme akawaambia watu, Bila shaka mimi mwenyewe nami nitatoka pamoja nanyi. ,3. Lakini watu wakasema, Wewe usitoke nje; kwa maana tukikimbia, hawatatuona sisi kuwa kitu; au tukifa nusu yetu, hawatatuona kuwa kitu; lakini wewe u wa thamani kuliko watu elfu kumi katika sisi; kwa hivyo sasa ni afadhali ukae tayari kutusaidia toka mjini. 4. Mfalme akawaambia, Yaliyo mema machoni penu ndiyo nitakayofanya. Basi mfalme akasimama kando ya lango, na hao watu wakatoka kwa elfu zao na mia zao. 5. Mfalme akawaamuru Yoabu na Abishai na Itai, akasema, Mtendeeni yule kijana, Absalomu, kwa upole kwa ajili yangu. Nao watu wote wakasikia, mfalme alipowaagiza maakida wote katika habari za Absalomu.” 
  
 Uzuri wake Absalom na tamaa yake, moyo wa kisasi, hila, uchungu na kutenda kwa upumbavu viligharimu Maisha yake, Daudi alilia laiti ningelikufa mimi mwanangu Absalom
      
Moja ya maswala magumu sana katika maisha ni pamoja na kufanya maamuzi hususani wakati mtu unayempenda na kumthamini anapokufanyia jambo bay asana na jambo hilo ukawa umelithibitisha, katika nyakati kama hizo

·   Watu wengi huweza kutoa adhabu kali sana za kukomesha na kuangamiza pale wanapokuwa wamefanyiwa mambo mabaya,
    Tumeshuhudia watu wakiwachoma moto watoto wadogo kwa sababu tu wamechukua fedha ua wameiba
·       Wengine wamewaadhibu kwa kuwachapa vibaya kwa mikanda na kuwajeruhi wakosaji
·       Wengine wamemwagiwa tindi kali
·       Wengine wamepeleka taarifa katika vyombo vya habari na magazeti
Makanisani pia tunashuhudia watu wakitengwa na kufukuzwa utumishi bila malipo yoyote, wakinyimwa posho, kutengwa miezi kadhaa, kufungiwa huduma kuchafuliwa na kuwauia kihuduma ili yamkini ikiwezekana wasiinuke tena
Je unafanya nini wakati uwapendao, watoto, ndugu, jamaa, rafiki, na kadhalika wanapokuasi na kusimama kinyume nasi na kuanza kutubomoa, wale tuliowagharimia wanapotukosea tunafanya nini?
2 Samuel 18:1-5 Katika kifungu hiki Daudi analazimika kupigana vita, vita hii ni mbaya kuliko zote alizowahi kupigana katika maisha yake ni vita ngumu safari hii mfalme hapigani na wafilisti wala Goliath wala maadui za Bwana anapigana na ndugu zake mwenyewe Israel wakiongozwa na mwanaye mwenyewe
Hakuna vita mbaya duniani kama vita vya wenyewe kwa wenyewe, ni vita ngumu, ukisema ummalize adui ni kama unajimaliza mwenyewe Mathayo 12:25-26 Yesu anaonyesha ubaya wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vita hii ndio iliyokuwa ikimkabili Daudi wakati huu, hapa ilikuwa vita inayoweza kuleta ukiwa mkubwa sana
Vita yoyote ya Taifa kwa taifa yaani taifa lililogawanyika
Vita yoyote ya Familia iliyogawanyika
Vita yoyote ya mtu na mkewe au mtu na mumewe
Vita vya mtu na rafiki yake
Vita ya mtu na mchumba wake
Vita ya watoto na wazazi
Vita vya mtu uliyengharimia
Vita vya mchungaji na wachungaji wenzake au na wazee wa kanisa
Au wanakwaya kwa wanakwaya
Vita za namna hii zinakuwa mbaya sana na vinasababisha ukiwa mkubwa hasa inapotokea kuwa upande mmoja unakusudia kuumlaliza upande mwingine kabisa huku hakuna anayefaidika na vita hiyo
Haya ndiyo yaliyomkuta Daudi mara hii anapigana vita na mwanaye mpendwa mzuri aliyeitwa Absalom
Absalom alikuwa kijana wa mfalme aliyesifiwa sana , alikuwa mzuri namsafi, alipendeza na kuvutia  na alikuwa na ushawishi kwa watu, alikuwa na nywele nzuri na ndefu ambazo zlilikatwa mara tatu tu kwa mwaka , hakuwa na ila ya aina yoyote kwa habari ya uzuri, pia alikuwa na akili hata hivyo mambo kadhaa yalichangia kuharibu maisha ya kijana huyu
Alikuwa na Uchungu
 Alikuwa ni kisasi
Alikuwa na Hila
Alikuwa na kiburi na mwenye kukosa Subira pia hakuwa na msamaha
Mambo haya yalipelekea kijana huyu kumuasi baba yake na kujitangaza kuwa Mfaleme 2Samuel 14:25-26.

Kijana huyu alikuwa na uwezo wa kutumia hila na akili aliyonayo aliweza kuhadaa mioyo ya watu kwa muda wa miaka kama minne hivi 2Samuel 15:1-12, Safari hii uasi wake ulikuwa na nguvu ya kupita kawaida na alitaka kuithibitishia Isarael ya kuwa kweli amaemuasi baba yake 2Samuel 16:21-23 Mshauri wa Absalom alishauri kuwa anayepaswa kuuawa hapa ni Daudi peke yake na sio vinginevyo ili watu wakae katika amani 2Samuel 17:1-4
Unaweza kuona kuwa kijana wako uliyemzaa mwenyewe na ni Mashuhuri anakuasi waziwazi na anakusudia kukumaliza kabisa, amekuvunjia heshima yako hadharani amekudhalilisha  anakuweka katika wakati mgumu je katika hali kama hii unafanya nini hivi ndivyo Daudi alivyofanya nasi ni muhimu tukafanya

1.       Kubali kushuka
Watu wengi sana hususani vijana  na viongozi mbalimbali watu wao wanapowaasi, hawakubali kujishusha hata siku moja, wanataka kushughulikia matatizo wakiwa katika mamlaka yao ileile au katika mfumo wa cheo chao hujui mi mumeo, hujui mi askofu wako, Daudi alijua kuwa nia hii sio rahisi kufanikiwa kumpata mpendwa wake yeye aliamua kujishusha, aliachia ikulu na kukimbia pekupeku alijua kuwa hawezi kujiokoa wala kuwaokoa watu wake na mwanaye kama atabakia ikulu aliondoka 2samuel 15:14,30 Ili kumpata mwanadamu aliyeasi Yesu alikubali kuacha Enzi na utukufu, akanyenyekea kama mwanadamu mtumwa, watu wanavutiwa na mtu aliyejishusha, na sio Yule anayebaki ikulu, anayebaki katika haki yake na mamlaka yake , Absalom aliweza kuihadaa mioyo ya watu kwa sababu alijinyenyekeza kwao watu wakampenda 2Samuel 15:5-6, alifahamu kuwa ili aipate mioyo ya watu  hana budi kujishusha katika kiwango chao, ili kuipata mioyo ya watu jishushe katika kiwango chao,Kamwe usitumie mamlaka yako katika kutatua matatizo, hujui mimi ni mzazi wako?, hujui mimi ni mumeo? Hajui mimi ndiye Rais?, hujui mimi ndiye Askofu? Atanitambua atajua kuwa mimi ndiye mwenyeji, mimi ndiye mwangalizi, mimi ndiye alwatani, mimi ndiye nimeshika mpini. Daudi aliacha viatu, alichukua namna ya mtumwa, aliondoka ikulu, Kujishusha kunasaidia kutatua matatizo, 1Samuel 25:1-4, Mungu humwangalia mtu mnyonge, mwenye roho iliyopondeka na kumuinua Wafilipi 2:5-8, Hatuwezi kutatua matatizo yetu bila kuamua kujishusha, kujishusha na rohoya unyenyekevu kumesaidia kujenga maisha ya watu wengi sana , kiongozi anayekaa ofisini tu bila kujali wala kujua matatizo ya watu na mahitaji yao, hawezi kukubaliaka na kufaa kwa Mungu na watu.

2.       Rudisha sanduku la Mungu mahali pake 2Samuel 15:24-29
Sanduku la Agano la Mungu lilikuwa chombo muhimu sana chenye kuwakilisha uwepo wa Mungu, Ni chombo kinachoonekana kinachowakilisha uwepo wa Mungu asiyeonekana, Chombo hiki kilimwakilisha Yesu Kristo, aliye chapa ya mng’ao wa utukufu wa Mungu, Isarael waliamini kuwa hata ukiingia vitani na chombo hiki lazima utashinda, Viongozi wengi sana wanapokuwa madarakani, huwa wanasahau kuwa unaweza kuwepo madarakani lakini Mungu au uwepo wa Mungu ukawa hauko pamoja nawe, unaweza kuwa mpakwa mafutalakini Mungu akawa amekuacha , kama ilivyokuwa kwa Sauli mfalme, nNi lazima kwa nza ufahamu Mungu yuko upande wa nani unapokuwa na miggogoro, Absalom au wewe? Mungu yuko upande gani Hakuna mtu mwenye hati miliki ya uwepo wa Mungu, Mungu yuko kwaajili ya watu wote, si vema kuwahesabu wengina na kuwahukumu kama waasi tu, Daudi alitaka apate muda wa kupata na kusikia neno la bwana ili kujua kuwa Bwana amempa kibalia nani kati yake na Absalom, kama Bwana yuko na Absalom basi Absalom awe na uhuru nwa kuabudu kupitia sanduku la agano, na kama Bwana yuko naye basi atampa neema ya kuliona sanduku hilo tena lakini sio kuondoka nalo, halikuwa la kwake lilikuwa kwaajili ya watu wote wa Mungu,
·         Viongozi wengi sana wa kiroho nimeona wakiwatenga watu wanaodhani kuwa ni wenye dhambi na zaidi ya yote huwafukuza na kuwanyimba hata kuabudu, aku kufanya huduma fulanifulani kabisa wakiwahesabia dhambi na kuwapimia muda wa miezi na hata miaka lakini huwa wanasahau kuwa kipimo cha utii katika moyo wa Mwanadamu anacho Mungu tu, Mtu hapimwi kwa kumzuia asihubiri, asiombe au kutoa sadaka huko ni kuhukumu na kujichukulia madaraka makubwa
·         Au wanaweza kumzuia mtu asifanyie wengine maombezi, swala la Ibada kwa binadamu liko wazi kwa kila mtu,swala la ibada halina hakimiliki, kuabudu ni swala huru kwa kila mtu hata kama sio wa dhehebu lako, Mungu si wa dehebu Fulani au dini Fulani kila mtu anahaki ya kuabudu na anapaswa kuabudu, kila mtu anapewa nafasi na maandiko na anapewa haki ya kuufikia uwepo wa Bwana Luka 9:49-50, Matendo 4:18-20 Ni kwa kujua haya Daudi aliwaambia makuhani walirudishe sanduku la agano mahali pake, Mungu atusaidie kuwa na moo kama wa daudi wa kutambua kuwa uwepo wa Mungu sio hatimiliki  ya mtu gfulani, au kanisa Fulani au mchungaji Fulani au askofu Fulani kila mtu ana haki ya kuabudu.

3.       Fanya maombi ya kujidhili ( Kujishusha). 2samuel 15:30-32
Daudi alifanya maombi ya kujidhili yaani alijishuhsa, alilia, hakwenda mbele za Mungu kama mwanamume na mfalme bali alikwenda kama mjakazi wa kike , alijifunika kichwa alipokuwa akimuomba Mungu Kutoka 34:29-35, 1Korith0 11:3-7, Mwanamume hapaswa kufunika kichwa anapoingia katika uwepo wa Mungu, kuomba, hivyo maombi na dua za Daudi zilihusisha kujishusha kwa kiwango kikubwa na cha halia ya juu, Luka 18:9-14 Mungu hakubalia maombi ya watu wenye kujihesabia haki, Daudi alifahamu kuwa anahitaji maombi ya kujinyenyekesha wakati huu kupita kawaida ili hatimaye Mungu aweze kumuinua tena, alirusha michanga juu alitembea pekupeku alijifunika kichwa na kulia

4.       Panga vita (Mikakati) ya ukombozi
Nimuhimu kukumbuka kuwa hakuna vita ngumu duniani kama vita ya ndugu kwa ndugu, vita ya aina hii haina mshindi, ni ngumu na ni lazima  itaacha majeraha yanayoweza kudumu kwa muda mrefu, huwezi kupanga vita ya ndugu ikawa vita ya kumalizana, mwisho wa yote utalia mwenyewe, Ni lazima vita ya aina hii iwe vita ya ukombozi 2Samuel 18:1-5 Daudi aliona uzito wa vita hii kwani sasa hapigani na Mfilisti wala Goliath anapigana na mwanaye aliyetoka katika viuno vyake
Vita unayopigana na nduguyo ni lazima iwe vita ya ukombozi, Mara nyingi viongozi weni wa kiroho na Kikristo, kunapotokea shida za ikmahusiano mioyo yao hubadilika na kusahahu hili, mapambano yao na makusudi yao yanakuwa ni kukumaliza kabisa au kumlaiza nduguyo, kumpoteza, kufuta jina lake kumfanya akome, asione suluhu tena Daudi hakutaka kabisa kumpoteza Absalom aliagiza wazi mbele ya makamanda wote “MTENDEENI YULE KIJANA ABSALOM KWA UPOLE KWAAJILI YANGU” haya ni maneno mazito Daudi aliyasema haya hadharani, na watu wote walisikia , alikuwa na moyo, Daudi alikuwa na moyo wa kiungu, siku zote Mungu anapotuadhibu kwaajili ya makosa yetu na dhambi hutuadhibu kwa kusudi la kuturekebisha na kuturejesha, na sio kutuangamiza, Daudi alitambua udhaifu wa mwanawe Absalom kuwa ni ujana ndio unaomsumbua ni mchanga ni kuwa hajakomaa hajajua maisha, ni dasarindogondogo zinamsumbua na aliona ni afadhali angelikufa yeye badala ya mwanawe Asalom 2Samuel 18:33-19:4 Biblia inasemaje ndugu yako anapokukosea ni laazima arejeshwe kwa upole Wagalatia 6:1 Daudi alikuwa na moyo wa urejeshi huu ndio moyo wa Mungu ndio moyo wa mtu aliyekomaa kiroho
Mungu kamwe hafurahii kufa kwake mtu mwenye dhambi Ezekiel 33:11 Daudi hakufurahia kifi cha Absalom mwanawe, ambaye kwa vyovyote alikuwa hajaifikilia toba, Upendo wa kweli haufurahii udhalimu, Moyo wa daudi ulikuwa tayari, kufanya kitu kwaajili ya mtu muovu, kuliko watu wema waliokuwa upande wake 2Samuel 19:5-6 Ulikuwa ni moyo wa ajabu sana na upendo mwingi usioweza kupimika najua angaekuwa mtu mwingine angesema ndio afadhali kafa, Mungu kamlipizia kisasi, Mungu ameshughulikia adui zangu lakini huu haukuwa moyo wa Daudi na sio moyo wa Mungu.

5.       Mtendeeni kwa Upole
Ingawa Absalom alikuwa amekusudia kumuua baba yake na kuwaacha watu hai, Daudi alikusudia wazi kwamba Absalom aachwe hai, Daudi alitoa nafasi ya pili kwa mkosaji, alitoa nafasi ya tatu na ne na tano na kuendelea, ni vema kuwapa wakosaji nafasi nyingine tena nani ajuae kuwa mioyo yao itabadilika nani ajuaye kuwa watakuwa wamejifunza maswala kadhaa?
Daudi hakutaka kushindana na Absalom ni muhimu kufahamu kuwa hatupaswi kushindana na mtu aliye chini yako, Daudi hakuhesabu kuwa yuko vitani huwezi kupigana na mwanao hata kama yeye ni shetani, Mungu hapigani na shetani, hata siku moja ingawa yuko chini yake ni ujinga, daudi hakufurahia kufa kwa mwanaye, hakufurahia kifo cha kudhalilika cha mwanaye ingawa yeye alikuwa amedhalilishwana mwanaye, Daudi anaumia sana asiposamehe, alipenda kama angelipata nafasi ya kumtangazia mwanaye msamaha, alijuta kuikosa  nafasi hiyo alitamnani kama laity angelipata nafasi ya kumwambia mwanangu nimekusamehe, Dhambi ya Absalom ni maumivu kwa Daudi Isaya 43:25 Mungu anapotusamehe dhambi hutusamehe kwaajili yake mwenyewe upendo wake unamsukuma kusamehe na anaumia anapokosa nafasi ya kutusamehe, “Mtendeeni Yule kijana Absalom kwa upole kwaajili yangu” Tabia ya Daudi ni tabia ya uungu inayoonyesha ukomavu wa hali ya juu.
Daudi hakumuhukumu Absalom kwa vyovyote vile alimuachia Mungu ahukumu adui zakena wote waliomkataa na kumkana.
Mungu ndiye hakimu wa kweli atakayehukumu kwa haki dhidi nya maisha yetu
Mtazamo wako si ukweli kuhusu Mungu wakati wote.