Utangulizi
(2 SAMUEL 18:1-5) “1. Kisha Daudi akawahesabu watu waliokuwa pamoja
naye, akaweka maakida wa elfu elfu, na maakida wa mia mia juu yao. ,2. Daudi
akawapeleka hao watu vitani, theluthi moja chini ya mkono wa Yoabu, na theluthi
ya pili chini ya mkono wa Abishai, mwana wa Seruya nduguye Yoabu, na theluthi
ya tatu chini ya mkono wa Itai, Mgiti. Mfalme akawaambia watu, Bila shaka mimi
mwenyewe nami nitatoka pamoja nanyi. ,3. Lakini watu wakasema, Wewe usitoke
nje; kwa maana tukikimbia, hawatatuona sisi kuwa kitu; au tukifa nusu yetu,
hawatatuona kuwa kitu; lakini wewe u wa thamani kuliko watu elfu kumi katika
sisi; kwa hivyo sasa ni afadhali ukae tayari kutusaidia toka mjini. 4. Mfalme
akawaambia, Yaliyo mema machoni penu ndiyo nitakayofanya. Basi mfalme akasimama
kando ya lango, na hao watu wakatoka kwa elfu zao na mia zao. 5. Mfalme akawaamuru Yoabu na
Abishai na Itai, akasema, Mtendeeni yule kijana, Absalomu, kwa upole kwa ajili
yangu. Nao watu wote wakasikia, mfalme alipowaagiza maakida wote katika habari
za Absalomu.”
Uzuri wake Absalom na tamaa yake, moyo wa kisasi, hila, uchungu na kutenda kwa upumbavu viligharimu Maisha yake, Daudi alilia laiti ningelikufa mimi mwanangu Absalom
Moja ya maswala magumu sana
katika maisha ni pamoja na kufanya maamuzi hususani wakati mtu unayempenda na
kumthamini anapokufanyia jambo bay asana na jambo hilo ukawa umelithibitisha,
katika nyakati kama hizo
· Watu wengi huweza kutoa adhabu kali sana za
kukomesha na kuangamiza pale wanapokuwa wamefanyiwa mambo mabaya,
Tumeshuhudia watu wakiwachoma moto watoto wadogo
kwa sababu tu wamechukua fedha ua wameiba
· Wengine wamewaadhibu kwa kuwachapa vibaya kwa
mikanda na kuwajeruhi wakosaji
· Wengine wamemwagiwa tindi kali
· Wengine wamepeleka taarifa katika vyombo vya
habari na magazeti
Makanisani pia tunashuhudia watu
wakitengwa na kufukuzwa utumishi bila malipo yoyote, wakinyimwa posho, kutengwa
miezi kadhaa, kufungiwa huduma kuchafuliwa na kuwauia kihuduma ili yamkini
ikiwezekana wasiinuke tena
Je unafanya nini wakati
uwapendao, watoto, ndugu, jamaa, rafiki, na kadhalika wanapokuasi na kusimama
kinyume nasi na kuanza kutubomoa, wale tuliowagharimia wanapotukosea tunafanya
nini?
2 Samuel 18:1-5 Katika kifungu hiki Daudi analazimika kupigana vita,
vita hii ni mbaya kuliko zote alizowahi kupigana katika maisha yake ni vita
ngumu safari hii mfalme hapigani na wafilisti wala Goliath wala maadui za Bwana
anapigana na ndugu zake mwenyewe Israel wakiongozwa na mwanaye mwenyewe
Hakuna vita mbaya duniani kama
vita vya wenyewe kwa wenyewe, ni vita ngumu, ukisema ummalize adui ni kama
unajimaliza mwenyewe Mathayo 12:25-26
Yesu anaonyesha ubaya wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vita hii ndio iliyokuwa
ikimkabili Daudi wakati huu, hapa ilikuwa vita inayoweza kuleta ukiwa mkubwa
sana
Vita yoyote ya Taifa kwa taifa yaani taifa lililogawanyika
Vita yoyote ya Familia iliyogawanyika
Vita yoyote ya mtu na mkewe au mtu na mumewe
Vita vya mtu na rafiki yake
Vita ya mtu na mchumba wake
Vita ya watoto na wazazi
Vita vya mtu uliyengharimia
Vita vya mchungaji na wachungaji wenzake au na wazee wa kanisa
Au wanakwaya kwa wanakwaya
Vita za namna hii zinakuwa mbaya sana na vinasababisha ukiwa mkubwa
hasa inapotokea kuwa upande mmoja unakusudia kuumlaliza upande mwingine kabisa
huku hakuna anayefaidika na vita hiyo
Haya ndiyo yaliyomkuta Daudi mara
hii anapigana vita na mwanaye mpendwa mzuri aliyeitwa Absalom
Absalom alikuwa kijana wa mfalme
aliyesifiwa sana , alikuwa mzuri namsafi, alipendeza na kuvutia na alikuwa na ushawishi kwa watu, alikuwa na
nywele nzuri na ndefu ambazo zlilikatwa mara tatu tu kwa mwaka , hakuwa na ila
ya aina yoyote kwa habari ya uzuri, pia alikuwa na akili hata hivyo mambo
kadhaa yalichangia kuharibu maisha ya kijana huyu
Alikuwa na Uchungu
Alikuwa ni kisasi
Alikuwa na Hila
Alikuwa na kiburi na mwenye kukosa Subira pia hakuwa na msamaha
Mambo haya yalipelekea kijana huyu kumuasi baba yake na kujitangaza
kuwa Mfaleme 2Samuel 14:25-26.
Kijana huyu alikuwa na uwezo wa
kutumia hila na akili aliyonayo aliweza kuhadaa mioyo ya watu kwa muda wa miaka
kama minne hivi 2Samuel 15:1-12, Safari
hii uasi wake ulikuwa na nguvu ya kupita kawaida na alitaka kuithibitishia
Isarael ya kuwa kweli amaemuasi baba yake 2Samuel
16:21-23 Mshauri wa Absalom alishauri kuwa anayepaswa kuuawa hapa ni Daudi
peke yake na sio vinginevyo ili watu wakae katika amani 2Samuel 17:1-4
Unaweza kuona kuwa kijana wako
uliyemzaa mwenyewe na ni Mashuhuri anakuasi waziwazi na anakusudia kukumaliza
kabisa, amekuvunjia heshima yako hadharani amekudhalilisha anakuweka katika wakati mgumu je katika hali
kama hii unafanya nini hivi ndivyo Daudi alivyofanya nasi ni muhimu tukafanya
1.
Kubali
kushuka
Watu wengi sana hususani
vijana na viongozi mbalimbali watu wao
wanapowaasi, hawakubali kujishusha hata siku moja, wanataka kushughulikia
matatizo wakiwa katika mamlaka yao ileile au katika mfumo wa cheo chao hujui mi
mumeo, hujui mi askofu wako, Daudi alijua kuwa nia hii sio rahisi kufanikiwa
kumpata mpendwa wake yeye aliamua kujishusha, aliachia ikulu na kukimbia
pekupeku alijua kuwa hawezi kujiokoa wala kuwaokoa watu wake na mwanaye kama
atabakia ikulu aliondoka 2samuel
15:14,30 Ili kumpata mwanadamu aliyeasi Yesu alikubali kuacha Enzi na
utukufu, akanyenyekea kama mwanadamu mtumwa, watu wanavutiwa na mtu
aliyejishusha, na sio Yule anayebaki ikulu, anayebaki katika haki yake na
mamlaka yake , Absalom aliweza kuihadaa mioyo ya watu kwa sababu
alijinyenyekeza kwao watu wakampenda 2Samuel
15:5-6, alifahamu kuwa ili aipate mioyo ya watu hana budi kujishusha katika kiwango chao, ili
kuipata mioyo ya watu jishushe katika kiwango chao,Kamwe usitumie mamlaka yako
katika kutatua matatizo, hujui mimi ni mzazi wako?, hujui mimi ni mumeo? Hajui mimi
ndiye Rais?, hujui mimi ndiye Askofu? Atanitambua atajua kuwa mimi ndiye
mwenyeji, mimi ndiye mwangalizi, mimi ndiye alwatani, mimi ndiye nimeshika
mpini. Daudi aliacha viatu, alichukua namna ya mtumwa, aliondoka ikulu,
Kujishusha kunasaidia kutatua matatizo, 1Samuel
25:1-4, Mungu humwangalia mtu mnyonge, mwenye roho iliyopondeka na kumuinua Wafilipi 2:5-8, Hatuwezi kutatua matatizo yetu bila kuamua kujishusha,
kujishusha na rohoya unyenyekevu kumesaidia kujenga maisha ya watu wengi sana ,
kiongozi anayekaa ofisini tu bila kujali wala kujua matatizo ya watu na
mahitaji yao, hawezi kukubaliaka na kufaa kwa Mungu na watu.
2.
Rudisha
sanduku la Mungu mahali pake 2Samuel 15:24-29
Sanduku la Agano
la Mungu lilikuwa chombo muhimu sana chenye kuwakilisha uwepo wa Mungu, Ni
chombo kinachoonekana kinachowakilisha uwepo wa Mungu asiyeonekana, Chombo hiki
kilimwakilisha Yesu Kristo, aliye chapa ya mng’ao wa utukufu wa Mungu, Isarael
waliamini kuwa hata ukiingia vitani na chombo hiki lazima utashinda, Viongozi
wengi sana wanapokuwa madarakani, huwa wanasahau kuwa unaweza kuwepo madarakani
lakini Mungu au uwepo wa Mungu ukawa hauko pamoja nawe, unaweza kuwa mpakwa
mafutalakini Mungu akawa amekuacha , kama ilivyokuwa kwa Sauli mfalme, nNi
lazima kwa nza ufahamu Mungu yuko upande wa nani unapokuwa na miggogoro,
Absalom au wewe? Mungu yuko upande gani Hakuna mtu mwenye hati miliki ya uwepo
wa Mungu, Mungu yuko kwaajili ya watu wote, si vema kuwahesabu wengina na
kuwahukumu kama waasi tu, Daudi alitaka apate muda wa kupata na kusikia neno la
bwana ili kujua kuwa Bwana amempa kibalia nani kati yake na Absalom, kama Bwana
yuko na Absalom basi Absalom awe na uhuru nwa kuabudu kupitia sanduku la agano,
na kama Bwana yuko naye basi atampa neema ya kuliona sanduku hilo tena lakini
sio kuondoka nalo, halikuwa la kwake lilikuwa kwaajili ya watu wote wa Mungu,
·
Viongozi wengi sana wa kiroho nimeona wakiwatenga
watu wanaodhani kuwa ni wenye dhambi na zaidi ya yote huwafukuza na kuwanyimba
hata kuabudu, aku kufanya huduma fulanifulani kabisa wakiwahesabia dhambi na
kuwapimia muda wa miezi na hata miaka lakini huwa wanasahau kuwa kipimo cha
utii katika moyo wa Mwanadamu anacho Mungu tu, Mtu hapimwi kwa kumzuia
asihubiri, asiombe au kutoa sadaka huko ni kuhukumu na kujichukulia madaraka
makubwa
·
Au wanaweza kumzuia mtu asifanyie wengine
maombezi, swala la Ibada kwa binadamu liko wazi kwa kila mtu,swala la ibada
halina hakimiliki, kuabudu ni swala huru kwa kila mtu hata kama sio wa dhehebu
lako, Mungu si wa dehebu Fulani au dini Fulani kila mtu anahaki ya kuabudu na
anapaswa kuabudu, kila mtu anapewa nafasi na maandiko na anapewa haki ya
kuufikia uwepo wa Bwana Luka 9:49-50,
Matendo 4:18-20 Ni kwa kujua haya Daudi aliwaambia makuhani walirudishe
sanduku la agano mahali pake, Mungu atusaidie kuwa na moo kama wa daudi wa
kutambua kuwa uwepo wa Mungu sio hatimiliki
ya mtu gfulani, au kanisa Fulani au mchungaji Fulani au askofu Fulani kila
mtu ana haki ya kuabudu.
3. Fanya maombi ya kujidhili ( Kujishusha).
2samuel 15:30-32
Daudi alifanya
maombi ya kujidhili yaani alijishuhsa, alilia, hakwenda mbele za Mungu kama
mwanamume na mfalme bali alikwenda kama mjakazi wa kike , alijifunika kichwa
alipokuwa akimuomba Mungu Kutoka
34:29-35, 1Korith0 11:3-7, Mwanamume hapaswa kufunika kichwa anapoingia
katika uwepo wa Mungu, kuomba, hivyo maombi na dua za Daudi zilihusisha
kujishusha kwa kiwango kikubwa na cha halia ya juu, Luka 18:9-14 Mungu hakubalia maombi ya watu wenye kujihesabia haki,
Daudi alifahamu kuwa anahitaji maombi ya kujinyenyekesha wakati huu kupita
kawaida ili hatimaye Mungu aweze kumuinua tena, alirusha michanga juu alitembea
pekupeku alijifunika kichwa na kulia
4.
Panga
vita (Mikakati) ya ukombozi
Nimuhimu
kukumbuka kuwa hakuna vita ngumu duniani kama vita ya ndugu kwa ndugu, vita ya
aina hii haina mshindi, ni ngumu na ni lazima
itaacha majeraha yanayoweza kudumu kwa muda mrefu, huwezi kupanga vita
ya ndugu ikawa vita ya kumalizana, mwisho wa yote utalia mwenyewe, Ni lazima
vita ya aina hii iwe vita ya ukombozi 2Samuel 18:1-5 Daudi aliona uzito wa vita
hii kwani sasa hapigani na Mfilisti wala Goliath anapigana na mwanaye aliyetoka
katika viuno vyake
Vita unayopigana
na nduguyo ni lazima iwe vita ya ukombozi, Mara nyingi viongozi weni wa kiroho
na Kikristo, kunapotokea shida za ikmahusiano mioyo yao hubadilika na kusahahu
hili, mapambano yao na makusudi yao yanakuwa ni kukumaliza kabisa au kumlaiza
nduguyo, kumpoteza, kufuta jina lake kumfanya akome, asione suluhu tena Daudi
hakutaka kabisa kumpoteza Absalom aliagiza wazi mbele ya makamanda wote “MTENDEENI YULE KIJANA ABSALOM KWA UPOLE
KWAAJILI YANGU” haya ni maneno mazito Daudi aliyasema haya hadharani, na
watu wote walisikia , alikuwa na moyo, Daudi alikuwa na moyo wa kiungu, siku
zote Mungu anapotuadhibu kwaajili ya makosa yetu na dhambi hutuadhibu kwa
kusudi la kuturekebisha na kuturejesha, na sio kutuangamiza, Daudi alitambua
udhaifu wa mwanawe Absalom kuwa ni ujana ndio unaomsumbua ni mchanga ni kuwa
hajakomaa hajajua maisha, ni dasarindogondogo zinamsumbua na aliona ni afadhali
angelikufa yeye badala ya mwanawe Asalom 2Samuel
18:33-19:4 Biblia inasemaje ndugu yako anapokukosea ni laazima arejeshwe
kwa upole Wagalatia 6:1 Daudi
alikuwa na moyo wa urejeshi huu ndio moyo wa Mungu ndio moyo wa mtu aliyekomaa
kiroho
Mungu kamwe
hafurahii kufa kwake mtu mwenye dhambi Ezekiel
33:11 Daudi hakufurahia kifi cha Absalom mwanawe, ambaye kwa vyovyote
alikuwa hajaifikilia toba, Upendo wa kweli haufurahii udhalimu, Moyo wa daudi
ulikuwa tayari, kufanya kitu kwaajili ya mtu muovu, kuliko watu wema waliokuwa
upande wake 2Samuel 19:5-6 Ulikuwa
ni moyo wa ajabu sana na upendo mwingi usioweza kupimika najua angaekuwa mtu
mwingine angesema ndio afadhali kafa, Mungu kamlipizia kisasi, Mungu
ameshughulikia adui zangu lakini huu haukuwa moyo wa Daudi na sio moyo wa Mungu.
5.
Mtendeeni
kwa Upole
Ingawa Absalom alikuwa
amekusudia kumuua baba yake na kuwaacha watu hai, Daudi alikusudia wazi kwamba
Absalom aachwe hai, Daudi alitoa nafasi ya pili kwa mkosaji, alitoa nafasi ya
tatu na ne na tano na kuendelea, ni vema kuwapa wakosaji nafasi nyingine tena
nani ajuae kuwa mioyo yao itabadilika nani ajuaye kuwa watakuwa wamejifunza
maswala kadhaa?
Daudi hakutaka
kushindana na Absalom ni muhimu kufahamu kuwa hatupaswi kushindana na mtu aliye
chini yako, Daudi hakuhesabu kuwa yuko vitani huwezi kupigana na mwanao hata
kama yeye ni shetani, Mungu hapigani na shetani, hata siku moja ingawa yuko
chini yake ni ujinga, daudi hakufurahia kufa kwa mwanaye, hakufurahia kifo cha
kudhalilika cha mwanaye ingawa yeye alikuwa amedhalilishwana mwanaye, Daudi
anaumia sana asiposamehe, alipenda kama angelipata nafasi ya kumtangazia
mwanaye msamaha, alijuta kuikosa nafasi
hiyo alitamnani kama laity angelipata nafasi ya kumwambia mwanangu
nimekusamehe, Dhambi ya Absalom ni maumivu kwa Daudi Isaya 43:25 Mungu anapotusamehe dhambi hutusamehe kwaajili yake
mwenyewe upendo wake unamsukuma kusamehe na anaumia anapokosa nafasi ya
kutusamehe, “Mtendeeni Yule kijana
Absalom kwa upole kwaajili yangu” Tabia ya Daudi ni tabia ya uungu
inayoonyesha ukomavu wa hali ya juu.
Daudi
hakumuhukumu Absalom kwa vyovyote vile alimuachia Mungu ahukumu adui zakena wote
waliomkataa na kumkana.
Mungu ndiye
hakimu wa kweli atakayehukumu kwa haki dhidi nya maisha yetu
Mtazamo wako si
ukweli kuhusu Mungu wakati wote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni