Wajibu wa kila mshirika wa kanisa
la nyumbani pia ni wajibu wa kila mshirika wa kanisa kuu, leo ni vema tukiwa na
wakati wa kujikumbusha majukumu aliyonayo kila mshirika wa kanisa letu la nyumbani
kila mtu katika kanisa akiyafahamu majukumu yake na kuyatekeleza tutaishi kama
familia moja na tutaona faida nyingi sana za kuwa wakristo tutajifunza somo
hili kwa kuzingatia majukumu hayo kama ifuatavo;-
§ Kujengana
na kufarijiana sisi kwa sisi
§ Kupendana
sisi kwa sisi
§ Kutiana
moyo wakati wa Misiba na kuzikana
§ Kujuliana
halia na kuombeana wakati wa ugonjwa
§ Kushirikiana
na wenzetu wakati wa furaha
§ Kuombeana
na kuchukuliana mizigo sisi kwa sisi
§ Kuhakikisha
kanisa letu linakuwa
Kujengana na kufarijiana sisi kwa sisi.
1Wathesalonike 5;11 Warumi 1;12
Ni muhimu kufahamu kuwa mara baada ya kuokolewa sisi wote tunafanyika watoto wa
Mungu Hivyo Baba yetu ni mmoja yaani
Mungu Yohana 1;12, Mara baada ya kokoka katika ulimwenu wa kiroho na wakati
mwingine hujitokeza katika halia ya mwili wengine wasiookoka kutuchukia kwa
sababu sisi sio wa ulimwengu huu, kwa hiyo wakati mwingine kila mmoja wetu
anaweza kupitia hali ya kuuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali 1Petro
1;6, hali hizi zinapoachiwa bila kufarijiana ni rahisi mtu huyo kukata tamaa na
kurudi nyuma au kuacha wokovu, Hapo ndipo unapkja umuhimu wa kutembeleana na
kufarijiana, Mpendwa anayepitia katika majaribu ili adumu katika imani hutiwa moyo anapomuona mwenzake, na
unapogundua kuwa mwenzako ana huzuni unaweza kumfariji na kumjenga upya kwa neno
la Mungu na kumfanya aendelee na wokovu, utamtia moyo kutokana na mateso kutoka
kwa Mume au wazazi, au ndugu kwa msingi
huo maneno ya kujengana kwa watu waliookoka ni ya msingi sana na sio ya
kukatishana tamaa Waefeso 4;29 endapo mshirika mwenzetu amepatwa na msiba ni
muhimu kuwa mstari wa mbele katika kufariji kumbuka Martha na Mariam walipopatwa
na msiba wayahudi wengi walijitokeza kuwafariji Yohana 11;19 Hata Yesu
alihusika katika kuwafariji Martha na Mariam na kuuhairisha msiba kwa Muuujiza
mkubwa Bwana atupe neema ya kulizingatia hili na kuzidi katika Jina la Yesu.
Kupendana sisi kwa sisi
Yohana 13;34 Ni muhimu kufahamu
kuwa kupenda ni amri kwa msingi huo kila
mmoja wetu asitafute kupendwa kabla yeye
mwenyewe hajaonyesha upendo kwa wengine , wajibu wetu ni kupenda na sio
kupendwa. Njia kubwa ya kuonyesha namna tunavyopendana ni pamoja na
kutembeleana sisi kwa sisi majumbani mwetu na kujuana hali 1Petro 4;8-9,
waebrania 10;24 hatupaswi kutumia kisingizio cha shughuli za dunia na kazi
kama kiasi cha kusiondwa kutembeleana,
si vema kuwa watu tunaokutana katika kusanyiko kubwa kasha kila mmoja baada ya
ibada anajua lake huu sio upendo kivitedno ni muhimu kutembeleana jambo la msingi ni kutembeleana katika
ustahivu kaka kwa kaka na dada kwa dada au wakina kaka kwa dada au akida dada
kwa kaka ili kumtunzia Mungu heshima
walimwengu wasifikiri kuwa tunafanya uasherati Matedno 24;16,2wakoritho
8;20-21, Waefeso 5;3.
Kutiana moyo wakati wa Misiba na kuzikana
Kuzikana nin jambo la kibiblia na
ni ukristo mwenzetu anapoondoka ni muhimu kujihusisha katika shughuli yake na
kumsindikiza kwa heshima kubwa kuzika ni jambo la Baraka Mungu mwenyewe
alionyesha mano kwa kumzika mtumishi wake Musa yeye mwenyewe Kumbukumbu 34;5-6,
wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walishirii kikamilifu katika kumzika Yohana
Mathayo 14;10,12, watakatifi katika nyakati za kanisa la kwanza walishiriki
katika kumzika mwenzao Stefano na kumfania
maombolezo makuu Matendo 8;2 ni muhimu sana kwa wakristo kuwa na tabia hii kama
tutasikia wenzetu wamepatwa na msiba ni
muhimu kwetu kujitoa na kuhakikisha kuwa tunahisika kipekee katika kumsindikiza
kwa heshima kubwa maswla ya kuzingatia;-
§
Taarifa ya msiba ikipatikana ipelekwe mapema kwa
Mchungaji.
§
Kwaya ya kanisa itahusika katika kuhakikisha
kuwa mahali pa msiba panaimbwa nyimbo za aina mbalimbali pasiwe kimya tu. Kama
ikibidi ni muhimu hata kukesha wakiimba na kuombea faraja familia husika
§
Wahusika watiwe moyo na kuulizwa utaratibu
utakavyokuwa.
§
Wahusika watahakikisha wanashiriki michango na
pia kuangalia au kuusika katika uchimbaji wa Kaburi na ubebaji wa jeneza na
mazishi kwa ujumla umoja na upendo na heshima itakayoonyeshwa itawafanya watu
kuvutiwa na imani yetu Jambo la kushangaza ni kuwa watu wengi waliookoka
wakimaliza kuzika tu hutawanyika ni muhimu kurudi nyumbani na kufanya maombi na
ibada ya faraja kwa waliofiwa na kukemea roho ya misiba isijitokeze tena
Ni jambo la
kushangaza kwamba watu wengi waliookoka maswala ya msiba huchukuliwa kipuuuzi
na kama maswala ya kubaatisha hivi hilo sio jambo zuri hata kidogo, kupitia
namna tunavyowazika wenzetu tunaweza kuwafikia wengi sana kwa Yesu kwani watu
wengi hupenda kuzikwa kwa Heshima kubwa na hilo pekee laweza kuwa kizuizi cha
kuokoka.
Kujuliana halia na kuombeana wakati wa ugonjwa
Ni muhimu
kufaamu kuwa tangu zamani za Biblia watu walitembeleana wakati wa uonjwa 2Wafalme
8;29 Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda
alikwenda kumtazama mfalme Yoramu alipokuwa anaumwa, Yehoashi mfalme wa
Israel alikwenda kumtazama nabii Elisha alipokuwa ameshikwa na ugonjwa na
kumlilia katika maombi 2Wafalme 13;14 ni
muhimu kufanya hivyo na kuzidi katika nayakati hizi za agano jipya hususani
sisi tuliookoka, mwenzetu anapoumwa na kuugua hatuna budi kwenda kumtazama kama
ni nyumbani kwake au Hospitalini na kuomba pamoja naye na kumfariji kwa kufanya
hivyo Kristo atatupa thawabu kubwa na kutuhesabu kuwa tulikwenda kumtazama yeye
Mathayo 25;36,40, hiyo ndiyo dini ya kweli iliyo safi isiyo na taka ni kuwajali
watu katika dhiki zao Yakobo 1;27 Taarifa za ugonjwa wa mpendwa awaye yote ni
muhimu zikajulikana kwa kanisa ili wazee waweze kuomba Yakobo 5;13-15.
Kushirikiana na wenzetu wakati wa furaha.
Ni muhimu kwetu kuwa na
ufahamu wa kushirikiana na wenzetu
wakati wa furaha kama mtu akijifungua hatuna
budi kufurahi pamoja naye na kumpelekea zawadi kama walivyofanya mamajusi kwa
Yesu Mathayo 2;11, mwenzetu akifanikiwa kujenga shiriki katika ibada ya kuweka
wakfu nyumba yake mpya na kuifungua kwa
furaha, mwenzetu anapofanikiwa kuoa au kuolewa katika harusi hatuna budi kumpa
zawadi au kufanikisha harusi yake kwa michango yetu ya hali na malipia kufurahi
pamoja na ndoa mpya 1Wakoritho 12;26. Ni muhimu kanisa kuwa na roho ya kupenda
mafaniko ya wengine na kuyafurahia badala ya kuoneana wivu.
Kuombeana na kuchukuliana mizigo sisi kwa sisi
Yakobo 5;16 Maandiko yanakazia
swala zima la kuombeana na kusameheana ni muhimu katika kanisa kila mmoja kuwa na
Orodha ya majina ya washirika wengine na kuwaombea mbele za Mungu kwa kuwataja
majina yao, na ni lazima kuwaombea viongozi wa kanisa na mchungaji wetu, wakati
huo huo tukichukuliana mizigo Wagalatia 6;2,10 kwa kadiri ya neema tuliyopewa
na Mungu kila mmoja wetu anapaswa aitumie neema aliyopewa kuchukua mizigo ya
wenziwe 1Petro 4;10, kama una nama ya kumtafutia mtu kazi mpatie kazi,
kuwalipia nauli kuja ibadani kutoa mitaji ya kibiashara na ushauri wa nini cha
kufanya kwa kufanya hivyo unajiwekea
hazina yao mbinmguni Mathayo 6;19-21.
Kuhakikisha kanisa letu linakuwa
Ni wajibu wa kila mshirika kuwa
na mzigo na maono ya kuhakikisha kanisa linakuwa na kuongezeka kamwe usiridhike
kuona watu ni wachache wakatai wengi wanamtumkia shetani, hakikisha
unawashuhudia wengine na kuwaalika kuja katika ibada kila mmoja aliyeokoka
anawajibu wa kumzalia Bwana matunda Yohana 15;2 kanisa linalozaa Yesu hulitunza
na maombi yetu mengi yatakuwa yakijibiwa Yohana 15;16 ndiyo maana ni muhimu
kuwaalika wengine kuja ibadani na siku ya mwisho tutang’aa kama jua kwa
kuongoza wengi katika kutenda mema.