Jumatatu, 7 Machi 2016

Ufahamu kuhusu shule kuu sita za Kiislamu !



Waislamu duniani ni zaidi ya billioni moja na milioni mia nane ni dini inayokuwa kwa kasi sana na walio wengi zaidi ni kutoka dhehebu la suni wakifuatiwa na wengineo tutayachambua madhehebu hayo kama ifuatavyo;-

·   Suni “Sunnite”
Hii ndio shule au dhehebu lililo kubwa zaidi kuliko yote asilimia 90% ya waislamu wote duniani ni wasuni, wasuni wanaamini mafundisho kutoka kwa Makhalifa wakuu wanne ambao wanaamini kuwa ndio wakwanza waliomrithi Muhamad moja kwa moja baada ya kufa na si vinginevyo.Wasuni wako kwa wingi huko mashariki ya kati na na pwani ya Afrika mashriki nchi.


                                                Imamu mkuu wa Madhehebu ya Suni Nchini Irani Khamenei


·   Shiha “Shiites”
     Hii ndio shule au dhehebu la pili kwa ukubwa, jina shiha linawahusu waislamu wa mwanzo kabisa  wanaoamini mafundisho ya Imam Ali mwana wa kufikia wa nabii Muhamad ambaye wao huamini kuwa ndie kiongozi mrithi wa Waislamu aliyemrithi Muhamad ambae alifuatiwa na maimam kumi na mbili ambao nao walikuwa viongozi na wengi wao waliuawa, wao walidai kuwa Ali alikuwa mzee wao,na imam wa mwisho kabisa aliitwa Muhamad yeye alitoweka kama mtoto mwaka 878 bk. Inaaminika kuwa atakuja tena kwa watu wake kimuujiza (mahdi) na kwa njia ya mwili wa mtu mwingine na atafanya uislamu uchanue duniani kabla ya siku za mwisho(….will bring the golden age before the end of the world).(ndio maana rais wa sasa wa Iran hujifikiri ni yeye kwa kuwa anaitwa Mohamed Nejad na kiburi cha nyukilia) tofauti na wasuni washiha ingawa ni wachache kuliko suni washiha ni maarufu sana duniani hasa baada ya mapinduzi ya kiislamu yaliyofanywa na Ayatollah Khomein na kuchukua uongozi wa Iran mwaka 1979 na kuifanya Iran kuwa nchi ya kiislamu ya dhehebu hilo na hivyo wako kwa wingi katika nchi ya Azerbaijan, Bahrain, Iraq, Afaghanstan na Pakistan.Hawa ni maarufu kwa siasa kali.

·   Ismailia “Ishimailites”.
Hii ni shule au dhehebu la tatu la kiislamu ni jamii ya washiha ambao wanaamini mafundisho ya Imam aliyeitwa Ismail ambaye inaaminiwa kuwa ndie imam wa mwisho tofauti na shule nyingine wao wana kiongozi wa kidunia wa dhehebu lao ambaye ni billionaire bilionea  ambe huitwa Prince Agha Khan.
                              Prince Karim Agha Khan kiongozi wa madhehebu ya Ismailia Duniani


·   Ahamadia “ahamadiyan”.
Hii ni shule au dhehebu la nne la kiislamu ambalo limeanza hivi karibuni kwenye miaka ya 1800 hivi ilianzishwa na mtu aliyeitwa Mizra Ghulam ahmad aliyeishi kati ya (1839-1908) huko Punjab nchini India alidai kuwa yeye ndiye masihi na kuwa ndie mfano halisi kamili wa Muhamad alifundisha kuwa Yesu alizimia na kutibiwa kwa madawa na kupona na kwenda kuishi huko Kashimir nchini India alikofia, Ahamadia wana vikundi vikali sana vyenye kuushambulia ukristo na hukataliwa kuwa wao sio waislamu 

 Mizra Gulam Ahamad

·   Shafi “Sufi”.
     Hii ni shule ya tano ya kiislamu au dhehebu la tano hawa hupingwa sana na waislamu wenzao kama wasuni na washiha na wanaitwa kuwa ni imani potofu wazushi hasa kwa sababu ya mafundisho yao ambayo hukiri kuwa Mungu si mmoja na kuwa mwanzo wa uislamu ulikuwa miungu mingi na kuwa allah alikuwa mungu mwezi jambo linalopingwa na wislam ingawa ni la kweli kihistoria kama tutakavyoona.

·   Ansar “Ansar suni” .
     Ni jamii mpya ya shule au dhehebu la hivi karibuni inawezekana kuwa ni jamii ya wasuni hata hivyo neno ansar kwa kiarabu maana yake ni nzuri au safi au njema inawezekana kuna mambo hawakubaliani nayo katika Usuni kama Ibada za wafu,ushirikina, uchawi nk ni wenye siasa kali na msimamo mkali huwahi kufunga ramadhani siku moja kabla ya wenzao na husheherekea iddi siku moja kabla ya wenzao hivyo ni wasuni safi hata hivyo hadi tunakuja mitamboni utafiti zaidi kuhusu shule hii ulikuwa unaendelea kwani ni dhehebu jipya.

Mambo Muhimu ya kuyafahamu Katika uislamu



Ni muhimu kufahamu tafasiri na maana ya mambo kadhaa katika Uislamu ili kuweza kuyatambua kwa kina maana zake kama anavyochanganua Mchungaji Innocent kamote tafadhali fuatana nani.

·   Maana ya Uislamu na Muislam (Islam) & (Muslim).
     Neno uislam (Islam) ni neno lenye asili ya kiarabu ambalo maana yake ni kutii “Submission” na muislamu maana yake aliyejisalimisha kwa allah na Muhamad “one who submits” au mtu aliyesilimu yako madai pia kuwa neno Islamu maana yake ni amani hatahivyo maana hii hutumika kama njia ya kuficha uhalisia wa uislam ambao hauna amani kama tutakavyoona huko mbele je uislam ni amani na je waislamu ni watu wa amani au la.

·   Maana ya neno Quran (Koran).
     Ni neno la kiarabu cha kikureshi ambalo maana yake ni “Recitation”maana yake “yaliyokaririwa” Hivyo quran ni mjumuisho wa makusanyo ya aya “wahy”au mafunuo aliyoyatoa Allah kwa Muhamad kupitia malaika jibril au kwa ndoto nk. Muhamad alipozitoa aya hizo watu waliokuwa karibu walizikariri na baadae alipofariki zilikusanywa na kuwa kitabu ambacho waislamu huamini kuwa ni kitabu kitakatifu.

·   Maana ya neno Imam.
     Ni jina linalotumika kwa kiongozi wa dini ya kiislamu, ambaye ana ujuzi wa quran, waislamu wasio na ujuzi wa quran huitwa “maa mumah” na mwalimu wa ngazi ya juu zaidi wa kiroho kwa washiha huitwa “ayatollah” yaani aliye karibu na allah, pia wale waliomrithi Muhamad baada yake huitwa khalifa au maswahaba neno ambalo ni sawa na neno naibu

·   Maana ya jina Muhamad.
     Hili ndilo jina la nabii wa waislamu, alikuwa ni mwarabu wa jamii ya Makuresh(Quirsh-yaani papa) alizaliwa katika mji wa Mecca mwaka wa 570 B.K. Baada ya Kristo, alikufa mwaka wa 632 katika mji wa Madina, hivyo aliishi miaka 62,  Jina hili Muhamad maana yake ni “praised” yaani aliyetukuzwa wenyewe hutumia neno la kiyunani “Periclutos”,habari zaidi kuhusu muhamad tutazizungumzia katika somo maisha ya Muhamad huko mbele na nakuhakikishia kuwa sitambakishia kitu katika maisha yake tangu kuzaliwa hata kifo, tutaelezea maisha yake wazi kabisa sawa na Quran yenyewe.

·   Maana ya jina “allah”.
     Hili ndilo jina la mungu wa Muhamad na waislamu wenyewe wanadai kuwa jina hili haliwezi kuelezeka kwa neno god la kiingereza, ni jina la pekee na la mola linalobeba ukamilifu wote na uzuri, wao hulinganisha jina hili na jina YHWHYHWH”   la Kiebrania yaani Yehova, Ingawaje sifa za Mungu hawa hazifanani kabisa kama tutakavyoona huko mbeleni,allah hana mshirika,ni mkali sana si wakike wala wa kiume ana kigeugeu na hafai kutegemewa ni muongo na mwenye hila hana nguvu au uwezo wa kufufua wakati kwetu sisi wakristo Mungu kwetu ni kimbilio na nguvu msaada uonekanao tele wakati wa mateso.

·   Mambo mengine ya kufahamu katika Uislamu ni pamoja na;-
§  Sunnah-Ni maisha na tabia za matendo yoote ya Muhamad, unapoigiza lolote ambalo Muhamad amelifanya ni sunnah yaani unafuata njia au kielelezo cha maisha ya nabii muhamad mjumbe wa mwenyezi Mungu
§  Quibla-Kibla ni muelekeo wa maombi, unapoomba unapaswa kuelekea katika msikiti mkuu wa Mecca  huko ndio kibla ya waislamu.Yaani muelekeo wakati wa sala
§  Hafiz-Mtu aliyekariri quran kwa moyo anaweza kuisema bila kusoma.
§  Sheikh-Kiongozi wa kiroho wa kiislamu.
§  Halaal-Mambo yoote safi yaliyoruhusiwa katika uislamu.
§  Haraam-Mambo yoote yasiyo safi yaliyokatazwa katika uislamu(yaliyo harimishwa)
§  Mishkat-Hadhithi au kitabu cha baadhi ya hadith zilizochaguliwa
§  Mansukh-Aya ambazo baadaye zilibatilishwa.
§  Nasikh-Aya ambazo zilishuka kuchukua nafasi ya aya zile zilizo harimishwa.
Mwishoni pia nitatoa tafasiri za maneno yoote ya kiarabu kama hayo tutakayoyatumia na hata yale ambayo hatutayatumia yatusaidie baadae tusomapo quran.

·   Ufahamu kuhusu jamii ya waarabu (Arabs).
    Waarabu tulionao leo kwa asili wanatokana na uzao wa Shemu maarufu kama Semites yaani jamii yenye asili ya shemu huyu alikuwa mojawapo ya watoto watatu wa Nuhu, Shemu alikuwa na  wajukuu  moja ya wajukuu hao ni Eber baba wa waeber (waebrania) ukoo ambao Ibrahimu alitokea,Eber alizaa watoto wawili,Pelegi-ambako ndiko Ibrahimu alitokea na Yoktani ambae ndiye baba wa waarabu wengi,ingawa waarabu wengi hudai kuwa wao ni wa uzao wa Ishimael si kweli, uarabu wa Ishimael ulitokana na mama yake Hajir aliyetokea Misri Hivyo waarabu walikuwepo hata kabla ya Ibrahimu mwebrania (Mwanzo 10:21-23-29,11;10-26) jina hili arabs limetokana na asili ya maneno mawili yaani “Nomads” na “ Bedouns”




Pichani jamii ya waarabu nomads na beduians wakiwa na kondoo zao nyikani Picha  na maelezo ni kwa Hisani ya maktaba ya mwandishi  wa Somo Mwalim Innocent Mkombozi Kamote Mwandishi wa somo.

 Au mabedui hii ni jamii ya watu waishio jangwani na wanaoongea kiarabu wako kwa wingi mashariki ya kati Arabia shamu na sehemu za kaskazini mwa Afrika ni jamii ya watu wenye pua kubwa, na walikuwa jamii ya watu wasiomjua Mungu na wapinzani wa Mungu wa waebrania kwa karne nyingi hata kabla ya Kristo soma (Nehemia 2:19) Ishimael alikuwa mwebrania na alimuabudu Mungu wa baba yake na baadae aliishi maisha yanayofanana na mabedui wa jangwani kwani ndiko alikokimbilia na kuishi Mwanzo 25;17 Maneno Ismael akakusanyika kwa watu wake ni wazi kuwa alimwanimi Mungu wa Baba Yake.

Kujitia Nguvu Katika Bwana!


Mstari wa Msingi: 1 Samuel 30:6

Utangulizi.
1.      Unapopatwa na majaribu na mateso na vipingamizi vya aina mbalimbali hapa Duniani ni lipi jambo la kwanza kulifanya?
a.       Kila mtu ana majaribu na changamoto za aina mbalimbali anazozipitia katika maisha, Lakini si kila mtu anaweza kutatua matatizo hayo katika njia iliyo sahii
b.      Nnjia iliyo sahii ni ipi nalo ni swala gumu kulitambua
2.      Daudi ni moja ya mashujaa wa imani tunaowasoma katika Biblia lakini alipitia Majaribu ya aina mbalimbali.
1.      Alitafutwa kuuliwa na Mfalime Sauli
2.      Aliponeachupuchupu kuuawa kwa mkuki
3.      Aliiishimaisha ya kujificha nyikani na katika majabali
4.      Familia yake yote iliwahi kutekwa na nyumba kuchomwa moto
5.      Rafiki zake walimgeuka na walitaka kumuua kwa uchungu
6.      Alipitia aibu na mateso ya aina mbalimbali baada ya kufanya zinaa na kuua Mume wa mtu
7.      Amnoni mwanaye alimbaka dada yake Tamari
8.      Mwanaye mwingine Absalom alimuua Amnoni kaka yake
9.      Absalom mwamnaye daudi alitaka kumpindua baba yake
10.  Mwanaye mpendwa Absalom aliuawa katika vita na kusababisha uchungu.

 

Mtumaini Bwana siku zako zote Maana Bwana Yehova ni mwamba wa Milele Isaya 26:4

Je wewe umewahi kupitia mambo magumu kiasi hicho? Daudi alipitia nabado akawa shujaa wa imani
Jinsi gani Daudi aliweza kukabiliana na maswala magumu kiasi hiki nabado akaitwa mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu? Ni muhimu kwetu tuka mchunguza daudi na kuangalia alifanya nini wakati wa mambo magumu na hili ni somo kuu kwetu leo.

1.      Daudi alifanya nini wakati wa matatizo. 1Samuel 30:1-6

Yaliyomo:-
Daudi alikuwa anaishi katika mji wa sklagi 1Samuel 30:1-6
-          Alikuwa amemkimbia sauli aliyekuwa akitafuta kumuua
-          Na sasa alikuwa amejiunga na wafilisti ( ni kama alikuwa anakaribia kutumikia miungu mingine)
-          Wafilisti walikuwa wakijiandaa kwa vita na Mfalme Sauli wakati huu na Daudi na watu wake wamejiunga na wafilisti
-          Hata hivyo Wafilisti hawakuwa wakimuamini sana Daudi, hivyo walimuomba abaki katika mji wa Sklagi
2.      Tunaposoma 1Samuel 30:1-6 tunagundua ya kuwa
1.      Mji wa Sklagi ulikuwa umevamiwa na wa Amaleki I Samuel 30:1
2.      Kama haitoshi wanawake zao wote na watoto wao na kila kitu kilikuwa kimechukuliwa mateka I Samuel 30:2-5
3.      Kwa asili kila mtu alifadhaika na daudi pia alifadhaika sana. Lakini zaidi ya hilo wenzake walikasirika zaidi wakijua kuwa wamepata taabi hiyo kwaajili yake na wakataka kumuua I Samuel 30;6 Lakini Daudi alifanya nini?
4.      Ni muhimu kuangalia kwa makini kile alichokifanya Daudi 1Samuel 30:6
Wakati ambapo Familia imetekwa, wenzako wamekugeuka Biblia inasema Daudi alijitia nguvu katika Bwana  Mungu wake
Haya ndiyo aliyokuwa akiyafanya Daudi wakati wa shida
A.    Kwa nguvu alizozipokea aliweza kushughulika tena na Tatizo lililokuwa likimkabili
B.     Lakini nini nini maana ya kujitia nguvu katika Bwana?
C.     Ilikuwa ni tabia ya daudi kujitia Nguvu katika Bwana
1.      Alipozingirwa na sauli ili auawe Zaburi 59: 1-4
2.      Alipokuwa amefungwa na wafilisti Zaburi 56:1-2
3.      Alipokuwa anamkimbia Absalom Zaburi 3:1-2
4.      Alipokuwa amejificha Jangwani Zaburi ya 63
D.    Kutokana na Zaburi hizi tunawezxa kujifunza tabia ya Daudi  alikuwa ni mtu wa namna gani na pia tunaweza kupata Picha ya maana ya kujitia nguvu katika Bwana
Alimtegemea Bwana na kutegemea Msaada kutoka mbinguni Zaburi 56:3-4,9-11
Aliendelea Kumsifu Mungu kama Msada wake na tumaini lake Zaburi 59:16-17
Alishinda  hali ya upweke kwa kuamua kumtafuta Mungu Zaburi 63:1-2, Kusifu na Kuomba Zaburi 63:3-5, Kutafakari Zaburi 63:6-7

Daudi anatufundisha kupitia Zaburi zake kuwa ni jinsi gani tunaweza kujitia Nguvu katika Bwana!
1.      Wakati wa shida lazima tumtegemee Mungu
2.      Lazima tumkaribie yeye kumtafuta na kumsifu, na kuomba
3.      Tukiyafanya hayo tutatiwa nguvu  na Bwana ataleta Msaada Zaburi 63:8 Hivi ndivyo Daudi alivyofanya wakati wote wa mapitoa mateso na mapambano ya aina mbalimbali, na Mungu akamtia nguvu na kumuwezesha kukabiliana na kila changamoto iliyokuwa ikimkabili.
Tunakabiliana na matatizo na changamoto za aina mbalimbali kila iitwapo leo,
-          Mengine binafsi
-          Mengina ya kifamilia
-          Mengine ya uchumi mbovu na umasikini au kutokujitosheleza
-          Kazini, mashambani na mahospitalini, magonjwa
-          Lakini mara nyingi tumejaribu kutatua matatizo yetu wenyewe na kumuacha mungu pembeni na kusahau kuwa yeye ndio kimbilio letu,
-          Wakati mwingine tumeacha hata kuomba na kumsifu. Tumeacha hata kukusanyika katika Ibada tukijaribu kutatua matatizo yetu wenyewe, wengine husema ngoja niweke mambo sawa kisha nitamrejea Mungu baadaye,
-          Mungu hafurahii kama tutajaribu kutaua matatizo yetu wenyewe, huko ni kujitegemea na kuwategemea wanadamu ni laana Yeremia 17:5-8
-          Mungu alikasirishwa Isarael walipofikiri kuwa Misri itawasaidia walipavamiwa na waashuru Isaya 30:15-16 Mungu anataka tumtegemee yeye hata leo Yakobo 4:8 1Petro 5:6-7
-          Mungu hasaidiii wale wanaojisaidia wenyewe na kuzitegemea akili zao Mithali 3:5-6 Tunapomuacha Mungu nje wakati wa matatizo yetu jambo moja ni dhahiri kuwa Mungu anatuacha, tushughulikie wenyewe matatizo yetu na tutapata shida mpendwa usisahamu kuwa Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu.
Hitimisho.
1.      Ni muhimu kujifunza kutoka kwa daudi namna alivyotatua matatizo yake mwenyewe
2.      Lazima tumtegemee Mungu na kumuamini nyeye peke yake
3.      Hakuna sababu ya kumuacha Mungu kwa sababu ya mambi magumu
4.      Si vema kuacha kuabudu au kutokuhudhuria Ibada kwa sababu ya shida tulizo nazo
5.      Nafsi zetu na zimuandame bwana ili atutegemeze kwa mkono wake Zaburi 63:8
6.      Kumbuka wale wanaomtegemea Mungu watatiwa nguvu Bwana ampe neema kila mmoja wetu kumtegemea Mungu na Bwana atatuokoa na kutuwezesha!