Ni muhimu kufahamu tafasiri na maana ya mambo kadhaa katika Uislamu ili kuweza kuyatambua kwa kina maana zake kama anavyochanganua Mchungaji Innocent kamote tafadhali fuatana nani.
·
Maana ya Uislamu na Muislam
(Islam) & (Muslim).
Neno uislam (Islam) ni neno lenye asili ya
kiarabu ambalo maana yake ni kutii “Submission”
na muislamu maana yake aliyejisalimisha kwa allah na Muhamad “one who submits” au mtu aliyesilimu
yako madai pia kuwa neno Islamu maana yake ni amani hatahivyo maana hii hutumika
kama njia ya kuficha uhalisia wa uislam ambao hauna amani kama tutakavyoona
huko mbele je uislam ni amani na je waislamu ni watu wa amani au la.
·
Maana ya neno Quran
(Koran).
Ni neno la kiarabu cha kikureshi ambalo
maana yake ni “Recitation”maana yake
“yaliyokaririwa” Hivyo quran ni
mjumuisho wa makusanyo ya aya “wahy”au mafunuo aliyoyatoa Allah kwa Muhamad
kupitia malaika jibril au kwa ndoto nk. Muhamad alipozitoa aya hizo watu
waliokuwa karibu walizikariri na baadae alipofariki zilikusanywa na kuwa kitabu
ambacho waislamu huamini kuwa ni kitabu kitakatifu.
·
Maana ya neno Imam.
Ni jina linalotumika kwa kiongozi wa dini
ya kiislamu, ambaye ana ujuzi wa quran, waislamu wasio na ujuzi wa quran huitwa
“maa mumah” na mwalimu wa ngazi ya juu zaidi wa kiroho kwa washiha huitwa “ayatollah” yaani aliye karibu na allah,
pia wale waliomrithi Muhamad baada yake huitwa khalifa au maswahaba neno ambalo
ni sawa na neno naibu
·
Maana ya jina Muhamad.
Hili ndilo jina la nabii wa waislamu, alikuwa
ni mwarabu wa jamii ya Makuresh(Quirsh-yaani
papa) alizaliwa katika mji wa Mecca mwaka wa 570 B.K. Baada ya Kristo, alikufa
mwaka wa 632 katika mji wa Madina, hivyo aliishi miaka 62, Jina hili Muhamad maana yake ni “praised” yaani aliyetukuzwa wenyewe hutumia neno la kiyunani “Periclutos”,habari
zaidi kuhusu muhamad tutazizungumzia katika somo maisha ya Muhamad huko mbele
na nakuhakikishia kuwa sitambakishia kitu katika maisha yake tangu kuzaliwa
hata kifo, tutaelezea maisha yake wazi kabisa sawa na Quran yenyewe.
·
Maana ya jina “allah”.
Hili ndilo jina la mungu wa Muhamad na
waislamu wenyewe wanadai kuwa jina hili haliwezi kuelezeka kwa neno god la
kiingereza, ni jina la pekee na la mola linalobeba ukamilifu wote na uzuri, wao
hulinganisha jina hili na jina YHWH “YHWH” la Kiebrania yaani Yehova, Ingawaje sifa za
Mungu hawa hazifanani kabisa kama tutakavyoona huko mbeleni,allah hana
mshirika,ni mkali sana si wakike wala wa kiume ana kigeugeu na hafai kutegemewa
ni muongo na mwenye hila hana nguvu au uwezo wa kufufua wakati kwetu sisi
wakristo Mungu kwetu ni kimbilio na nguvu msaada uonekanao tele wakati wa
mateso.
·
Mambo mengine ya kufahamu
katika Uislamu ni pamoja na;-
§
Sunnah-Ni maisha na tabia za
matendo yoote ya Muhamad, unapoigiza lolote ambalo Muhamad amelifanya ni sunnah
yaani unafuata njia au kielelezo cha maisha ya nabii muhamad mjumbe wa mwenyezi
Mungu
§
Quibla-Kibla ni muelekeo wa
maombi, unapoomba unapaswa kuelekea katika msikiti mkuu wa Mecca huko ndio kibla ya waislamu.Yaani muelekeo
wakati wa sala
§
Hafiz-Mtu aliyekariri quran kwa
moyo anaweza kuisema bila kusoma.
§
Sheikh-Kiongozi wa kiroho wa
kiislamu.
§
Halaal-Mambo yoote safi
yaliyoruhusiwa katika uislamu.
§
Haraam-Mambo yoote yasiyo safi
yaliyokatazwa katika uislamu(yaliyo harimishwa)
§
Mishkat-Hadhithi au kitabu cha
baadhi ya hadith zilizochaguliwa
§
Mansukh-Aya ambazo baadaye
zilibatilishwa.
§
Nasikh-Aya ambazo zilishuka
kuchukua nafasi ya aya zile zilizo harimishwa.
Mwishoni pia nitatoa
tafasiri za maneno yoote ya kiarabu kama hayo tutakayoyatumia na hata yale
ambayo hatutayatumia yatusaidie baadae tusomapo quran.
·
Ufahamu kuhusu jamii ya
waarabu (Arabs).
Waarabu tulionao leo kwa asili wanatokana
na uzao wa Shemu maarufu kama Semites
yaani jamii yenye asili ya shemu huyu alikuwa mojawapo ya watoto watatu wa
Nuhu, Shemu alikuwa na wajukuu moja ya wajukuu hao ni Eber baba wa waeber
(waebrania) ukoo ambao Ibrahimu alitokea,Eber
alizaa watoto wawili,Pelegi-ambako
ndiko Ibrahimu alitokea na Yoktani
ambae ndiye baba wa waarabu wengi,ingawa waarabu wengi hudai kuwa wao ni wa
uzao wa Ishimael si kweli, uarabu wa Ishimael ulitokana na mama yake Hajir
aliyetokea Misri Hivyo waarabu walikuwepo hata kabla ya Ibrahimu mwebrania (Mwanzo 10:21-23-29,11;10-26) jina hili
arabs limetokana na asili ya maneno mawili yaani “Nomads” na “ Bedouns”
Pichani jamii ya waarabu
nomads na beduians wakiwa na kondoo zao nyikani Picha na maelezo ni kwa Hisani ya maktaba ya
mwandishi wa Somo Mwalim Innocent
Mkombozi Kamote Mwandishi wa somo.
Au mabedui hii ni jamii ya watu waishio
jangwani na wanaoongea kiarabu wako kwa wingi mashariki ya kati Arabia shamu na
sehemu za kaskazini mwa Afrika ni jamii ya watu wenye pua kubwa, na walikuwa
jamii ya watu wasiomjua Mungu na wapinzani wa Mungu wa waebrania kwa karne nyingi
hata kabla ya Kristo soma (Nehemia 2:19)
Ishimael alikuwa mwebrania na alimuabudu Mungu wa baba yake na baadae aliishi
maisha yanayofanana na mabedui wa jangwani kwani ndiko alikokimbilia na kuishi
Mwanzo 25;17 Maneno Ismael akakusanyika kwa watu wake ni wazi kuwa alimwanimi
Mungu wa Baba Yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni