Jumatatu, 7 Machi 2016

Kujitia Nguvu Katika Bwana!


Mstari wa Msingi: 1 Samuel 30:6

Utangulizi.
1.      Unapopatwa na majaribu na mateso na vipingamizi vya aina mbalimbali hapa Duniani ni lipi jambo la kwanza kulifanya?
a.       Kila mtu ana majaribu na changamoto za aina mbalimbali anazozipitia katika maisha, Lakini si kila mtu anaweza kutatua matatizo hayo katika njia iliyo sahii
b.      Nnjia iliyo sahii ni ipi nalo ni swala gumu kulitambua
2.      Daudi ni moja ya mashujaa wa imani tunaowasoma katika Biblia lakini alipitia Majaribu ya aina mbalimbali.
1.      Alitafutwa kuuliwa na Mfalime Sauli
2.      Aliponeachupuchupu kuuawa kwa mkuki
3.      Aliiishimaisha ya kujificha nyikani na katika majabali
4.      Familia yake yote iliwahi kutekwa na nyumba kuchomwa moto
5.      Rafiki zake walimgeuka na walitaka kumuua kwa uchungu
6.      Alipitia aibu na mateso ya aina mbalimbali baada ya kufanya zinaa na kuua Mume wa mtu
7.      Amnoni mwanaye alimbaka dada yake Tamari
8.      Mwanaye mwingine Absalom alimuua Amnoni kaka yake
9.      Absalom mwamnaye daudi alitaka kumpindua baba yake
10.  Mwanaye mpendwa Absalom aliuawa katika vita na kusababisha uchungu.

 

Mtumaini Bwana siku zako zote Maana Bwana Yehova ni mwamba wa Milele Isaya 26:4

Je wewe umewahi kupitia mambo magumu kiasi hicho? Daudi alipitia nabado akawa shujaa wa imani
Jinsi gani Daudi aliweza kukabiliana na maswala magumu kiasi hiki nabado akaitwa mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu? Ni muhimu kwetu tuka mchunguza daudi na kuangalia alifanya nini wakati wa mambo magumu na hili ni somo kuu kwetu leo.

1.      Daudi alifanya nini wakati wa matatizo. 1Samuel 30:1-6

Yaliyomo:-
Daudi alikuwa anaishi katika mji wa sklagi 1Samuel 30:1-6
-          Alikuwa amemkimbia sauli aliyekuwa akitafuta kumuua
-          Na sasa alikuwa amejiunga na wafilisti ( ni kama alikuwa anakaribia kutumikia miungu mingine)
-          Wafilisti walikuwa wakijiandaa kwa vita na Mfalme Sauli wakati huu na Daudi na watu wake wamejiunga na wafilisti
-          Hata hivyo Wafilisti hawakuwa wakimuamini sana Daudi, hivyo walimuomba abaki katika mji wa Sklagi
2.      Tunaposoma 1Samuel 30:1-6 tunagundua ya kuwa
1.      Mji wa Sklagi ulikuwa umevamiwa na wa Amaleki I Samuel 30:1
2.      Kama haitoshi wanawake zao wote na watoto wao na kila kitu kilikuwa kimechukuliwa mateka I Samuel 30:2-5
3.      Kwa asili kila mtu alifadhaika na daudi pia alifadhaika sana. Lakini zaidi ya hilo wenzake walikasirika zaidi wakijua kuwa wamepata taabi hiyo kwaajili yake na wakataka kumuua I Samuel 30;6 Lakini Daudi alifanya nini?
4.      Ni muhimu kuangalia kwa makini kile alichokifanya Daudi 1Samuel 30:6
Wakati ambapo Familia imetekwa, wenzako wamekugeuka Biblia inasema Daudi alijitia nguvu katika Bwana  Mungu wake
Haya ndiyo aliyokuwa akiyafanya Daudi wakati wa shida
A.    Kwa nguvu alizozipokea aliweza kushughulika tena na Tatizo lililokuwa likimkabili
B.     Lakini nini nini maana ya kujitia nguvu katika Bwana?
C.     Ilikuwa ni tabia ya daudi kujitia Nguvu katika Bwana
1.      Alipozingirwa na sauli ili auawe Zaburi 59: 1-4
2.      Alipokuwa amefungwa na wafilisti Zaburi 56:1-2
3.      Alipokuwa anamkimbia Absalom Zaburi 3:1-2
4.      Alipokuwa amejificha Jangwani Zaburi ya 63
D.    Kutokana na Zaburi hizi tunawezxa kujifunza tabia ya Daudi  alikuwa ni mtu wa namna gani na pia tunaweza kupata Picha ya maana ya kujitia nguvu katika Bwana
Alimtegemea Bwana na kutegemea Msaada kutoka mbinguni Zaburi 56:3-4,9-11
Aliendelea Kumsifu Mungu kama Msada wake na tumaini lake Zaburi 59:16-17
Alishinda  hali ya upweke kwa kuamua kumtafuta Mungu Zaburi 63:1-2, Kusifu na Kuomba Zaburi 63:3-5, Kutafakari Zaburi 63:6-7

Daudi anatufundisha kupitia Zaburi zake kuwa ni jinsi gani tunaweza kujitia Nguvu katika Bwana!
1.      Wakati wa shida lazima tumtegemee Mungu
2.      Lazima tumkaribie yeye kumtafuta na kumsifu, na kuomba
3.      Tukiyafanya hayo tutatiwa nguvu  na Bwana ataleta Msaada Zaburi 63:8 Hivi ndivyo Daudi alivyofanya wakati wote wa mapitoa mateso na mapambano ya aina mbalimbali, na Mungu akamtia nguvu na kumuwezesha kukabiliana na kila changamoto iliyokuwa ikimkabili.
Tunakabiliana na matatizo na changamoto za aina mbalimbali kila iitwapo leo,
-          Mengine binafsi
-          Mengina ya kifamilia
-          Mengine ya uchumi mbovu na umasikini au kutokujitosheleza
-          Kazini, mashambani na mahospitalini, magonjwa
-          Lakini mara nyingi tumejaribu kutatua matatizo yetu wenyewe na kumuacha mungu pembeni na kusahau kuwa yeye ndio kimbilio letu,
-          Wakati mwingine tumeacha hata kuomba na kumsifu. Tumeacha hata kukusanyika katika Ibada tukijaribu kutatua matatizo yetu wenyewe, wengine husema ngoja niweke mambo sawa kisha nitamrejea Mungu baadaye,
-          Mungu hafurahii kama tutajaribu kutaua matatizo yetu wenyewe, huko ni kujitegemea na kuwategemea wanadamu ni laana Yeremia 17:5-8
-          Mungu alikasirishwa Isarael walipofikiri kuwa Misri itawasaidia walipavamiwa na waashuru Isaya 30:15-16 Mungu anataka tumtegemee yeye hata leo Yakobo 4:8 1Petro 5:6-7
-          Mungu hasaidiii wale wanaojisaidia wenyewe na kuzitegemea akili zao Mithali 3:5-6 Tunapomuacha Mungu nje wakati wa matatizo yetu jambo moja ni dhahiri kuwa Mungu anatuacha, tushughulikie wenyewe matatizo yetu na tutapata shida mpendwa usisahamu kuwa Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu.
Hitimisho.
1.      Ni muhimu kujifunza kutoka kwa daudi namna alivyotatua matatizo yake mwenyewe
2.      Lazima tumtegemee Mungu na kumuamini nyeye peke yake
3.      Hakuna sababu ya kumuacha Mungu kwa sababu ya mambi magumu
4.      Si vema kuacha kuabudu au kutokuhudhuria Ibada kwa sababu ya shida tulizo nazo
5.      Nafsi zetu na zimuandame bwana ili atutegemeze kwa mkono wake Zaburi 63:8
6.      Kumbuka wale wanaomtegemea Mungu watatiwa nguvu Bwana ampe neema kila mmoja wetu kumtegemea Mungu na Bwana atatuokoa na kutuwezesha!

Hakuna maoni: