Waislamu duniani ni zaidi
ya billioni moja na milioni mia nane ni dini inayokuwa kwa kasi sana na walio
wengi zaidi ni kutoka dhehebu la suni wakifuatiwa na wengineo tutayachambua
madhehebu hayo kama ifuatavyo;-
·
Suni “Sunnite”
Hii ndio shule au dhehebu lililo kubwa zaidi kuliko yote
asilimia 90% ya waislamu wote duniani ni wasuni, wasuni wanaamini mafundisho
kutoka kwa Makhalifa wakuu wanne ambao wanaamini kuwa ndio wakwanza waliomrithi
Muhamad moja kwa moja baada ya kufa na si vinginevyo.Wasuni wako kwa wingi huko
mashariki ya kati na na pwani ya Afrika mashriki nchi.
Imamu mkuu wa Madhehebu ya Suni Nchini Irani Khamenei
·
Shiha “Shiites”
Hii ndio shule au dhehebu la pili kwa
ukubwa, jina shiha linawahusu waislamu wa mwanzo kabisa wanaoamini mafundisho ya Imam Ali mwana wa
kufikia wa nabii Muhamad ambaye wao huamini kuwa ndie kiongozi mrithi wa
Waislamu aliyemrithi Muhamad ambae alifuatiwa na maimam kumi na mbili ambao nao
walikuwa viongozi na wengi wao waliuawa, wao walidai kuwa Ali alikuwa mzee
wao,na imam wa mwisho kabisa aliitwa Muhamad yeye alitoweka kama mtoto mwaka
878 bk. Inaaminika kuwa atakuja tena kwa watu wake kimuujiza (mahdi) na kwa njia ya mwili wa mtu
mwingine na atafanya uislamu uchanue duniani kabla ya siku za mwisho(….will bring the golden age before the end of
the world).(ndio maana rais wa sasa wa Iran hujifikiri ni yeye kwa kuwa
anaitwa Mohamed Nejad na kiburi cha nyukilia) tofauti na wasuni washiha ingawa
ni wachache kuliko suni washiha ni maarufu sana duniani hasa baada ya mapinduzi
ya kiislamu yaliyofanywa na Ayatollah
Khomein na kuchukua uongozi wa Iran mwaka 1979 na kuifanya Iran kuwa nchi
ya kiislamu ya dhehebu hilo na hivyo wako kwa wingi katika nchi ya Azerbaijan, Bahrain,
Iraq, Afaghanstan na Pakistan.Hawa ni maarufu kwa siasa kali.
·
Ismailia “Ishimailites”.
Hii ni shule au dhehebu la
tatu la kiislamu ni jamii ya washiha ambao wanaamini mafundisho ya Imam
aliyeitwa Ismail ambaye inaaminiwa kuwa ndie imam wa mwisho tofauti na shule
nyingine wao wana kiongozi wa kidunia wa dhehebu lao ambaye ni billionaire
bilionea ambe huitwa Prince Agha Khan.
Prince Karim Agha Khan kiongozi wa madhehebu ya Ismailia Duniani
·
Ahamadia “ahamadiyan”.
Hii ni shule au dhehebu la
nne la kiislamu ambalo limeanza hivi karibuni kwenye miaka ya 1800 hivi
ilianzishwa na mtu aliyeitwa Mizra Ghulam ahmad aliyeishi kati ya
(1839-1908) huko Punjab nchini India alidai kuwa yeye ndiye masihi na kuwa ndie
mfano halisi kamili wa Muhamad alifundisha kuwa Yesu alizimia na kutibiwa kwa
madawa na kupona na kwenda kuishi huko Kashimir nchini India alikofia, Ahamadia
wana vikundi vikali sana vyenye kuushambulia ukristo na hukataliwa kuwa wao sio
waislamu
Mizra Gulam Ahamad
·
Shafi “Sufi”.
Hii ni shule ya tano ya kiislamu au
dhehebu la tano hawa hupingwa sana na waislamu wenzao kama wasuni na washiha na
wanaitwa kuwa ni imani potofu wazushi hasa kwa sababu ya mafundisho yao ambayo
hukiri kuwa Mungu si mmoja na kuwa mwanzo wa uislamu ulikuwa miungu mingi na
kuwa allah alikuwa mungu mwezi jambo linalopingwa na wislam ingawa ni la kweli
kihistoria kama tutakavyoona.
·
Ansar “Ansar suni” .
Ni jamii mpya ya shule au dhehebu la hivi
karibuni inawezekana kuwa ni jamii ya wasuni hata hivyo neno ansar kwa kiarabu
maana yake ni nzuri au safi au njema inawezekana kuna mambo hawakubaliani nayo
katika Usuni kama Ibada za wafu,ushirikina, uchawi nk ni wenye siasa kali na
msimamo mkali huwahi kufunga ramadhani siku moja kabla ya wenzao na
husheherekea iddi siku moja kabla ya wenzao hivyo ni wasuni safi hata hivyo
hadi tunakuja mitamboni utafiti zaidi kuhusu shule hii ulikuwa unaendelea kwani
ni dhehebu jipya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni