Andiko: Ayubu 9: 25 -26 Biblia inasema “ Basi siku zangu zina mbio kuliko Tarishi; Zakimbia wala hazioni mema, Zimepita kama merikebu ziendazo mbio; Mfano wa tai ayashukiayemawindo.”
Leo tutachukua muda kutafakari
kwa kina somo kuhusu Mfano wa tai ayashukiaye Mawindo, Ni muhimu kuwa na
ufahamu kuwa Mungu aliviumba viumbe vingi duniani kwa makusudi mbali mbali
lakini mojawapo ya kusudi kuu ni kutufunza mambo mbalimbali ya msingi, Tai ni
moja ya Ndege au kiumbe ambaye biblia imezungumza sifa zake kwa kina na mapana
na marefu na tunaweza kujifunza mambo kadhaa ya muhimu kutoka kwa kiumbe hiki.
Kuna usemi wa wahenga kuwa ndege
wa aina moja huruka pamoja, Usemi huu kwa Tai ni tofauti tai wanaruka pekeyo na
wanafurahia kuruka juu sana, sifa zake zinawekwa katika Biblia kwa vile ni
ndege mwenye sifa za kipakee ni ndege asiyeshindwa na ukubwa wa mawindo yake.
Kwa nini Biblia inampa Tai sifa
za hali ya juu sana ni muhimu kwetu kujifunza sifa zake na kuzilinganisha na
maisha yetu.
1. Tai ni wenye uwezo mkubwa wa kuona mbali.
Ayubu 39:27-29
Biblia inasema hivi “ Je! Tai hupaa juu kwa amri yako, Na kufanya kioto chake
mahali pa juu? Hukaa jabalini, ndiko
kwenye malazi yake, Juu ya genge la jabali, na ngomeni. Toka huko yeye huchungulia
mawindo; Macho yake huyaangalia toka mbali.”
Tai kama
utamfanyia uchunguzi na kumchungulia kwa mbali ni ndege makini sana Biblia
inamsifia kuwa “macho yake huyaangalia mawindo toka mbali” ndi ndege hodari
katika kuwinda macho yake amebarikiwa uwezo wa kuona mbali sana na anaona kwa
uwazi kabisa inasemekana anauwezo wa kumuona mwenzake akiwa Maili 50 kwa uwazi
kabisa! Jambo hili linatufundisha nini? Naamini unaweza kupata picha Fulani
Mamia ya watu
hodari wamewahi kuishi duniania na kupita wakiwemo watu maarufu sana duniani na
viongozi wakubwa
Ili dunia iweze
kuwa na Mafanikio makubwa sana inahitaji watu na viongozi wenye uwezo wa kuona
mbali sana, Abraham Lincoln rais wa 16 wa Marekani aliongoza katika wakati
mgumu sana wenye matatizo mengi na inchi ikiwa katika vita vya wenyewe kwa
wenyewe, lakini ndiye aliyefanikiwa kuweka misingi ya umoja na kukomesha utumwa
na kuifanya Marekani iwe kama ilivyo leo,
Ili dunia iweze
kuwa na mafanikio ni lazima iwe na watu wenye uwezo wa kuona mbali, wanaoangalia
faida za mbeleni za kwao na za kizazi kinachokuja badala yao
·
Watu wasio na maono ya mbali wanaweza kutugawa
kupitia dini na ukabila
·
Watu waioona mbali hawajali kutunza Mazingira
·
Watu wasioona mbali hawaogopi kuharibu mahusiano
·
Watu wasioona mbali hawaogopi kuua wanyama kama
tembo kwa faida yao
·
Watu wasioona mbali hawaogopi kufanya Ufisadi
kwa kuifilisi nchi
·
Watu wasioona mbali hawafikiri kujisomea kwa
bidii
·
Watu wasioona mbali hawafikiri kujiwekea akiba
·
Watu wasioona mbali hawafikiri kuhusu maisha yao
baada ya kufa duniani
Awaye yote aliye
kama tai atakuwa na ujuzi wa kuona mbali na kuzingatia faida za siku zijazo
kuliko kuangalia leo. Unayaona mwindo yako kwa mbali. Ni lazima tuwe na maono
makubwa yaliyopimwa kwa kina na yatakayoleta faida kubwa na matokeo makubwa
katika jamii.
2. Tai ni ndege wasioogopa Mawindo.
Tai ni ndege
asiyeogopa hata kidogo, wakati wote anapambana kuhakikisha anashinda,
atapambana kuhakikisha anapata mawindo yake au anatawala,unapoangalia sinema za
maisha ya tai utaweza kuona hawaogopi
mawindo haijalishi mawindo yao ni makubwa kiasi gani hata kama ni mbuzi ambaye
anaonekana kuwa mkubwa kuliko uwezo wake tai ni lazima atabeba, wana ujuzi
mkubwa wa kuwinda na ni mahodari, tai haogopi
Ni muhimu
kufahamu kuwa kama unataka kufanikiwa katika maisha haya usiogope kufanya jambo
gumu, usiogope kukabiliana na watu wakubwa au waliokuzidi umri, hakikisha kuwa
unakipigania kile unachokipenda,
·
Usiogope kupigania unachokipenda
·
Usiogope kusimama katika kweli hata kama
itakuletea madhara
·
Usiogope ukubwa wa tatizo unalopambana nalo
pigania mpaka kieleweke
·
Usiogope ugumu wa masomo unayosoma
·
Usiogope au kuonea aibu aina ya kazi unayoifanya
·
Lengo lako kuu ni kuhakikisha unafanikiwa
·
Usiogope mateso utakayoyapata kwaajili ya imani
au kile unachokipigania
·
Usiogope kuanzisha huduma au kufungua kanisa,
usiogope kuwa mmisionary, usiogope kugombea urais kama Mungu anataka ufanye
jambo kwa faida yako lifanye
·
Uisogope kufanya lolote ili kufafikia malengo
yako, Tai hawaogopi mawindo yao hata kama anachokiwinda ni kikubwa kuliko
umbile lake.
3.
Tai
ni Hodari hawaogopi Dhuruba.
Ukitaka kujua
uhodari wa Tai utaweza kuuona wakati wa dhoruba, wakati huu ndege wengine wote
hukimbia na kujificha kwa kuogopa dhoruba , kwa tai mambo ni tofauti anafunua
mbawa zake na kuzitanua na kupaa kwenda juu zaidi, taia wanatabia ya kutumia
dhoruba kwa faida, wakati ndege wa kawaida wakiogopa, ni muhimu kufahamu kuwa
watu wanaolinganishwa na tai hawakimbii changamoto zozote bali huzitumia
changamoto kusimama na kuongeza viwango, Mungu anataka watu wasiokimbia
changamoto bali wenye uwezo wa kukabiliana nazo huku wakisimama katika kusudi
au kuelekea juu zaidi
4.
Tai
wanaruka juu sana.
Ndege huyu ndiye
anayejulikana kama mfalme wa ana inasemekana tai wanauwezo wa kuruka juu kiasi
cha fiti 10,000, katika kiwango hicho hutaweza kumuona ndege mwingine na
ukimuona ni lazima atakuwa tai, Tai haruki wala kutafutiza chakula pamoja na
njiwa, alisema Dr, Myles Munroe Marehemu, alisema wakati njiwa wakiwa ardhini
wanacgakuachakua siku nzima na kulalamika, Taia hawanung’uniki, hawapigi
kelele, wanapaa juu sana wakisubiri mawindo wakisubiri nafasi waweze kuitumia,
watu wakuu duniani ni wale wanaotatua matatizo na sio wanaolalamika, wanatumia
nafasi na changamoto yoyote kama tai dhoruba inapotokea.
5.
Tai
hawali kibudu
Ni muhimu
kufahamu kuwa sifa nyingine ya tai ni pamoja na kutokula kibudu tai hawali
wasichokiua wenyewe, siku zote wanakula nyama ya mawindo yao wenyewe, wanakula
nyma safi na mpya hivi ndivyo watu wakuu katika dunia wanavyopaswa kuwa
Watu wakubwa
duniani hukaa na watu wenye mawazo mapana na wenye kufikiri na wenye uwezo wa
kuamua, watu hodari wasiokata tamaa, hawa ndio watu wanaoweza kulete mabadiliko
makubwa Duniani, watu wenye uwezo wa kuleta badiliko unapowasikiliza au kukaa
nao karibu, watu wenye ushawishi
Kamwe usipoteze
muda na watu wanaopoteza muda
Kamwe usipoteze
muda na watu wenye kusengenya
Kamwe usipoteze
muda na watu wasio na imani
Kamwe usipoteze
muda na watu wenye kuzungumzia wengine
Kamwe usipoteze muda
na watu wenye kupiga majungu na fitina
Kamwe usipoteze muda
na watu ambao kuanguka kwa wengine ndio furaha yao
Kamwe usipoteze
muda na watu wenye kuhukumu
Kamwe usipoteze muda
na watu wenye mitazamo hasi wenye kujihusisha na rushwa na uovu hivyo ni
vibudu, tafuta vya kwako mwenyewe mawindo yako mwenyewe.
Huyu ni aina nyingine ya tai ambaye hupatikana mashariki ya kati nyikanani na katika mbuga za wanyama Afrika tai huyu ndiye anayekula mizoga kiingereza sahii anaitwa VULTURE huyu ndiye ambaye Yesu anazungumza katika injili ya Mathayo
Tai anayekula Mizoga!
Ni muhimu
kufahamu kuwa tai tunayemzungumzia hapa mwenye sifa tulizozitaja anaitwa Eagle huyu
hali mizoga na taia anayetajwa katika Mathayo
24:28 huyu ndiye taia anayekula mizoga huyu anaitwa VULTURE
§ Mathayo 24:28 “ Kwa kuwa popote ulipo
mzoga ndipo watakapokusanyika tai”
§ Matthew 24: 28 "Whenever
there is carcass, there the VULTURE will gather” NIV.
§
Matthew 24: 28 "For wheresoever' the carcase is there will eagles be gathered together KJV
Tai anayekula
Mizoga haitwi “Eagle” anaitwa “Vulture”Huyu ni aina nyingine ya tai ambaye hupatikana mashariki ya kati nyikanani na katika mbuga za wanyama Afrika tai huyu ndiye anayekula mizoga kiingereza sahii anaitwa VULTURE huyu ndiye ambaye Yesu anazungumza katika injili ya Mathayo
Tai aina ya Vulture ndiye anayekula Mizoga na sio Tai aina ya Eagle
6.
Tai wanauwezo
wa kujitia nguvu mpya
Zaburi 103:4-5 “ Akusamehe
maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya
fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai;”
Isaya 40:31 “Bali wao wamngojeao Bwana watapata
nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka;
watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”
Moja ya tabia ya
tai ya kushangaza sana ni uwezo wake wa kujitia nguvu kwa upya ukiacha kuwa
wanauwezo wa kuona mbali lakini wana maisha marefu inasemekana Tai anapofikisha
miaka 30 anakuwa anachakaa na manyoya yake yanakuwa yamezeeka hivyo kuathiri
uwezo wake wa kiutendaji, inapofikia hivyo tai hakati tamaa ya kuishi badala
yake hutafuta kilele kikubwa cha mlima na kutulia kwa miezi mitano anagonga
mdomo wake katika mawe ya miamba na kungoa ngozi ya juu, hujinyonyoa manyoa
nyake yote wakati huu ajajigomoa na kuanza kuwa na manyoya mapya mdomo mpya na
magamba mapya jambo hili humfanya tai awe na uwezo wa kurejexza uhai wake kwa
miaka mingine 30-40, Ndo maana biblia inasema ujana wako utarejezwa kama tai
Watu wenye akili ni watu wanaoweza
kujitafakari na kuangalia yote waliyoyafanya katika maisha yao liwe jema au
baya linapokuwa baya unaachana nalo
wanatafuta nini lililo jema na lipi wanaweza kuliendeleza na jipya gani
wanaweza kuenda nalo, na kujifunza jambo jipya la kufanya siku hadi siku.
Kamwe sukubali
kudumaaa
Usikubali kubaki
vilevile siku zote
7.
Tai
wanatoa mafunzo kwa vifaranga vyao
Amini usiamini
tai wanaotoa mafunzo kwa vijana wao, tai wanafikiriwa kuwa ni ndege katili sana
wakati wa kutoa mafunzo na kama hujui makusudi yao unaweza kukubaliana kuwa ni
ndege wakatili, jambo moja la kushangaza kuhusu tai ni uwezo wake wa kutoa
mafunzo kwa vifaranga vyake, utafiti unaonyesha kuwa hakuna aina ya ndege
mwenye mvuto na mpole kama tai kwa watoto wake kushinda tai
Mama wa tai
anapogundua kuwa wakati umefika kwa vifaranga vyake kujifunza kuruka, anawabeba
vifaranga wake mgongoni na kupanua mbawa zake anaruka juu sana kisha anajiondoa
kutoka kifaranga chake na kukiachia kiangukekinapoanguka kinajifunza kuruka
akiona kinaogopa na kinataka kuanguka anakidaka na kukirejeza katika kiota
chake, atafanya hivyo mpaka kimejifunza kuruka.
Watu wakubwa
sana duniani sio mabosi, wakati wote wanawafanya wengine kukua katika jamii na
wanawapa changamoto lakini wanawasaidia kukua na kujiamini na kuendelea kuwapa
maelekezo wengine mpaka wameweza kufanya vilevile kama wao wafanyavyo.
Rev. Innocent
Kamote
Mkuu wa Wajenzi
mwenye Hekima
0718990796