Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu kwamba
Mojawapo ya Maandiko ambayo yamekuwa na changamoto kubwa sana kwa wasomi wengi
wa Biblia na kukutana na ugumu katika tafasiri zake ni Pamoja na andiko hili katika Zaburi 51:5 “Tazama, mimi naliumbwa katika
hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani” wote tunajua
wazi kuwa zaburi hii imeandikwa na Daudi, na maneno yake ni sehemu ya toba
aliyokuwa akiifanya baada ya kufanya dhambi, ya zinaa na mke wa Huria na
kufanya njama ya mauaji dhidi ya Uria ili kuficha ushahidi, ni baada ya
kukabiliwa na Nabii Nathan na kuonywa
kuhusu kosa lake Daudi alitubu na kusema maneno haya yaliyopo katika zaburi ya
51. Kuna maneno mengi sana aliyasema
katika zaburi hii kama sehemu ya toba yake lakini neno kuu na ambalo linazua
mjadala mkubwa sana kwa wasomi wengi wa Biblia ni maneno haya “MAMA YANGU ALINICHUKUA MIMBA HATIANI!” Swali kubwa likiwa ni kwanini Daudi
anazungumza maneno haya? Anamaanisha nini, Daudi anazungumzia hali ya mwanadamu
kuzaliwa akiwa na asili ya dhambi? Au anamaanisha kuwa mwanadamu anaanza kuwa
mwenye dhambi tangu siku mimba inapotungwa? Lakini pia inaweza kumaanisha kuwa
Daudi aliamini kuwa mama yake alimzaa katika hali ya dhambi?
Kumbuka maneno haya- “Hatiani” Kama ilivyoaminika katika
jamii yake kuwa mama yake alimzaa mtoto huyo kutokana na zinaa. Maandiko haya
yenye uzito mkubwa na majonzi makubwa yanatusaidia kuelewa kitu fulani na
kingine cha ziada katika maisha na mapito ya Daudi ambacho kinaweza vilevile
kuhuisha maisha yetu kwa upya, Kwa msingi huo leo tutachukua muda kuweza
kufanya uchunguzi wa kina sana na wa ndani zaidi kuhusu utata wa andiko hili na
maana zake kwa kadiri ya mawazo mbalimbali ya wasomi wa Biblia na kwa kadiri ya
neema kwa msaada wa Roho Mtakatifu mwalimu mkuu;-
Nani mwandishi wa Zaburi hii?
Ili andiko hili liweze
kutafasirika vema jambo la kwanza ni lazima tuwe na uhakika wa mwandishi wa
Zaburi hii, Mfano kama Zaburi hii imeandikwa na Sulemani na Sulemani labda
ndiye aliyekuwa anatubu hapa kwa sababu zaburi hii ni zaburi ya toba ni zaburi
ya kuomba rehema kwa Mungu unaweza kuona inavyoanza katika mstari ule wa kwanza
hivi;-
Zaburi 51:1-2 “Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha
wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu,
Unitakase dhambi zangu.”
Ni wazi kuwa
mstari wa tano ungeweza kufikiriwa kuwa labda Sulemani anakumbuka historia ya
kuzaliwa kwake, kupitia makosa ya Daudi kwa mama wa Sulemani ambaye ni
Bathsheba mke wa Uria, Lakini
maandiko yako wazi kuwa Bathsheba siye aliyekosea yeye alikosewa na adhabu ya
Mungu ilianguka kwa mtoto wa kwanza ambaye Daudi alizaa na Bathsheba na ambaye
alifariki mapema kama njia ya kutiwa nidhamu na Mungu,
2Samuel 12:14 “Lakini, kwa kuwa kwa tendo
hili umewapa adui za Bwana nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako
hakika yake atakufa.”
na kwa vile Uria aliyekuwa mume wa Bathsheba
alikuwa amekwisha kuawa, na maandiko yako wazi kuwa Daudi alikuwa amemchukua
Bathsheba kama mke wake sasa basi Sulemani anazaliwa kama mtoto halali wa Daudi
kwa Bathsheba akitambuliwa na maandiko namna hii
Mathayo 1:6 “Yese akamzaa mfalme Daudi.
Daudi akamzaa Sulemani kwa yule mke wa Uria;”
kimsingi hapa kosa
lilikuwa la Daudi kuliko Bathsheba (japo wote wlifanya dhambi) na kama Zaburi
hii ingekuwa ya Sulemani basi Mstari wa tano ungepaswa kusomaeka “Baba yangu alinitungisha mimba Hatiani”
tukinena kiwazimu! Kwa msingi huo
kwa namna fulani hatuoni wazi kuwa toba hii ni ya Sulemani, Lakini wote
tunakubaliana wazi kuwa uchunguzi wa kimaandiko unaonyesha wazi kuwa zaburi hii
ni miongoni mwa zaburi za toba na ni wazi kuwa iliandikwa na Daudi kwa kusudi
la kutubia dhambi yake aliyoifanya kwa kumuingilia Mke wa Uria na pia kula
njama za kumuua Uria na toba hii ilifanyika baada ya kukabiliwa na nabii Nathan
ili Daudi arejee katika uhusiano wake na Mungu, Na kama hivyo ndivyo basi swala
la msingi linabaki pale pale kwamba zaburi hii ni ya Daudi na maneno hayo ni
toba ya Daudi na sio Sulemani, Sasa basi maneno yale “Mama yangu alinichukua Mimba hatiani!”
yana maana gani? Kwanini Daudi anayasema maneno hayo je alikuwa
amamaanisha nini Hapa ziko dhana mbalimbali kuhusu maneno hayo:-
Mama yangu alinichukua Mimba hatiani!
1. Mtazamo wa wayahudi: Kwa mujibu wa
masimulizi ya Marabi, na maandishi ya kihistoria ya kiyahudi na tamaduni zao
inaaminika kuwa maneno haya yalikuwa yakimaanisha kuwa Daudi alizaliwa nje ya
ndoa yaani mama yake Daudi aliyeitwa NIZBETH
alifanya zinaa kumpata mtoto huyo, swala hili liliaminika hivyo miongoni mwa
Familia ya Yese, akiwemo Yese mwenyewe na kaka zake Daudi. Kwa hivyo kulikuweko
na imani kwamba Daudi ni mwana wa haramu na wala sio mwana wa halali wa mzee
Yese ona Zaburi 69:7-8 “Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha
imenifunika uso wangu. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa
mama yangu.” Maneno haya nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, kwa
kiingereza “Stranger” katika Lugha
ya kiibrania yanasomeka “MUZAR”
yaani kwa kiingereza “Bastard” yaani
mtoto asiye safi, mwana haramu!, na neno
lingine “Msikwao” kwa kiingereza “Alien” asiyetambulika yaani mwana wa
mashaka, mgeni au mkimbizi, Kimsingi zaburi ya 69 kwa mujibu wa wanazuoni wa kiyahudi ni zaburi ya Daudi
aliyoandika wakati wa maisha yake ya mapema akiwa kijana ikionyesha kuwa kijana
huyu alikuwa na maumivu makali moyoni yanayotokana na mateso na kukataliwa
kabisa, na ndugu zake wakiamini kuwa ni mwana wa haramu, na alichukiwa sana
akihesabika kama sababu ya kusambaratika kwa familia na kudharaulika kwa mama
yao. Zaburi ya 69 inafunua aina ya maisha magumu sana aliyopitia Daudi ya
kukataliwa na kunyanyapaliwa na kudharauliwa na kila mtu aliyemuona inasemekana
kuwa wakati wa maisha yake ya utotoni hadi ukubwani hakuwa na rafiki hata mmoja
wa kumtia moyo alikuwa mtu wa kulaumiwa, kuaibishwa na kufedheheshwa tu,
Zaburi 69:19-20 “Wewe
umejua kulaumiwa kwangu, Na kuaibika na kufedheheka kwangu, Mbele zako Wewe
wako watesi wangu wote. Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja
aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu”.Zaburi hii ya 69 ilikuwa ni sauti ya mtu aliyeteseka mno, akidhalilishwa na
kuaibishwa, Daudi alikuwa amezungukwa na Maadui wa ndani na nje katika jamii
yake na wengi wakiwaza kumuua na wakati mwingine kitu kilipopotea alisingiziwa
yeye na alilipishwa kwa nguvu ona habari
zake Zaburi 69:4 “Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa
changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo
kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.” Hiki
kilikuwa kipindi kigumu sana katika maisha ya Daudi Zaburi ya 69 ni sauti ya
mtu aliyelemewa na mzigo mzito sana na ni maombi ya ukombozi dhidi ya maisha ya
mateso na Daudi inasemekana anayazungumza haya katika kipindi cha miaka 20-28
hivi cha maisha yake yaliyojawa na utata mwingi na kugubikwa na huzuni na
kukataliwa.
Je nini sababu kubwa ya mateso haya ya
Daudi nyumbani kwao?
Daudi alizaliwa
katika familia ya Mzee Yese, Wayahudi wenyewe wanamuita Yishai, Mzee huyu
alikuwa miongozi mwa wazee sabini waliokuwa wafanya sheria na waamuzi wa sheria
za kiyahudi “Sanhedrin” yaani
mahakama kuu ya Wayahudi, na alikuwa ni mtu aliyejipatia umaarufu mkubwa sana
katika kizazi chake na katika mji wao Bethelehemu, inasemekana kuwa alikuwa mtu
wa haki kiasi ambacho TALMUD (Shabbat
55b) imenukuu kuwa “Yese alikuwa mtu
mwenye haki kiasi ambacho hakustahili kifo isipokuwa kwa sababu ya tatizo la
Nyoka tu” yaani alikufa kwa sababu ya tatizo la Bustani ya Eden tu na tamko
la Mungu kwa Adam na Eva kuwa watakufa siku watakapokula matunda
waliyokatazwa, inasemekana kuwa hakuna dhambi wala hatia iliyowahi kuonekana
ndani ya Mzee Yese.
Hata hivyo
kulikuwa na tatizo moja kubwa sana katika familia ya Yese na hili ndilo
lilopelekea Daudi kusema yeye amekuwa kama Mgeni kwa ndugu zake, Daudi
hakuruhusiwa kula pamoja na familia yake, yeye aliwekewa chakula chake pembeni
sana, alipewa kazi ngumu ya kuchunga kondoo sehemu yenye wanyama wakali kama
Simba na Dubu ili yamkini ikiwezekana afie huko, Kwa hiyo Maisha ya Daudi ya
ujanani yalikuwa maisha magumu mno na ni mtu mmoja tu aliyekuwa akiumizwa na
maisha ya Daudi ambaye ni mama yake tu ambaye kukataliwa kwa mwanaye
kulimjumuisha na yeye hata hivyo naye hakuwa na nguvu ya kuzuia kile alichotendewa
yeye na mwanaye!, Daudi alihesabika kama mdudu tu na hakuna mtu alimhesabu kuwa
kitu, alilaumiwa na watu na kufanyiwa dhihaka, kufyonywa na kuchekwa ona Zaburi 22:6-7 “Lakini
mimi ni mdudu wala si mtu, Laumu ya wanadamu na mzaha wa watu. Wote wanionao
hunicheka sana, Hunifyonya, wakitikisa vichwa vyao;” ukweli ni kuwa
Daudi na mama yake Nizbeth walikuwa wakimuomba na kumsubiria Mungu awasaidie tu
katika hali waliyokuwa wakiipitia wakati huu bado ilionekana kana kwamba Mungu
amewaacha walikuwa wakimsubiria Mungu awaokoe na ukatili wa kifamilia uliokuwa
ukiwakabili Zaburi 22:1-5 “Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha? Mbona U mbali
na wokovu wangu, Na maneno ya kuugua kwangu?
Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibu Na wakati wa usiku lakini
sipati raha. Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli. Baba zetu
walikutumaini Wewe, Walitumaini, na Wewe ukawaokoa. Walikulilia Wewe wakaokoka,
Walikutumaini wasiaibike.” Haya yalikuwa maisha ya Daudi
NIZBETH ni nani hasa? Mwanamke huyu ni
moja ya wanawake muhimu sana katika historia ya wayahudi, japo hatajwi katika
maandiko lakini waebrania wanamuita Nitzevet
Adael, kwa mujibu wa kitabu cha masimulizi ya Kiyahudi TALMUD mwanamke huyu ndie mama wa Mfalme Daudi na alikuwa na watoto
tisa na wote alizaa na mzee Yese, watoto hao ni Eliabu, Abinadab, Shama,
Nethaneel, Raddai, Ozem, Daudi, Seruiah na Abigaili.
Kwa mujibu wa
masimulizi hayo ya kiyahudi ni Kwamba Mzee Yese ambaye wayahudi wanamuita Yishai
alikuwa ni mjukuu wa Boaz na Ruthu,
baada ya miaka mingi sana ya ndoa yake yeye na Nizbeth na baada ya kuzaa watoto
wa kiume kadhaa kabla ya kuzaliwa Daudi Mzee Yese alianza kuwa na mashaka
kuhusu uzao wake hasa kwa sababu ya historia ya babu yake Boazi na Bibi yake
Ruthu, kwamba ingawa Ruthu alikuwa amemuamini Mungu wa Israel lakini Ruthu
alikuwa mmoabu hivyo kulikuwa na mashaka kama watoto waliozaliwa na huyu mmoabu
wana haki ya kumtumikia Mungu wa Israel kama wayahudi wa asili? Japo Yese
alikuwa mtu mkubwa lakini tafasiri za Torati kati yake na wenzake ziliwapa
mashaka makubwa sana kama wajukuu wa Boazi yeye na wanawe wanaweza kuwa wenye
kufaa kwa utumishi wa Mungu na utawala au ufanya sheria, hii ni kwa sababu
wakati wana wa Israel wanatoka Misri wamoabu walisimama kikatili kinyume na
Israel ili wasipite katika nchi yao na hivyo torati ya Musa ilikataza kabisa
wana wa Israel wasioane na wamoabu ona::-
Kumbukumbu la Torati 23:2-3 “Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa Bwana; hata
kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana. Mwamoni wala
Mmoabi wasiingie katika mkutano wa Bwana; wala hata kizazi cha kumi mtu wao
asiingie katika mkutano wa Bwana milele;”
Biblia ya kiingereza
NIV inasomeka vema zaidi katika mistari hii
Deuteronomy 23:2-3 “No one born of a FORBIDDEN
MARRIAGE nor any of his descendants may enter the assembly of the LORD, even
down to the tenth generation, No Ammonite or Moabite or any of his descendants
may enter the assembly of The LORD even down to the tenth generation.”
Kwa mujibu wa
masimulizi ya Kiyahudi Boazi alipomuoa Ruthu alikuwa ni mfanya sheria na
alikuwa na ufahamu kuhusu Sheria hii na labda angepata muda wa kufafanua kwa
jamii kwa nini alioa mwanamke mmoabu na torati ilikataza? Je mwanaume akimuoa
mwanamke wa Moabu ambaye amemuamini Mungu wa Israel je wanawe wataweza kuwa
halali kuingia katika mkutano wa Bwana? Bahati mbaya inasemekana kuwa Boazi
baada ya kumuoa Ruthu alikufa mara moja akimuacha mja mzito na kumzaa Obedi,
Obedi yeye alimtumikia Mungu kwa Heshima kubwa na jina lake Obedi maana yake ni
Mtumishi wa Mungu aliishi maisha ya haki sana na kuwa na heshima kubwa katika
jamii jambo lililofanya akubalike katika jamii bila kujali kuwa mama yake
alikuwa mmoabu, Hali kadhalika mwanaye yaani Yese naye aliishi maisha ya haki
sana kiasi cha kukubalika na jamii ya Israel kuwa ni mwenye kufaa na watoto
wake pia, hata hivyo wakati wa maisha ya
Yese kuliibuka mijadala mikubwa sana kuhusu Sheria ya Musa kwamba Israel
wasioane na wamoabu na kuwa wamoabu wasiingie katika mkutano wa Bwana milele
jambo hili lilimpa wasiwasi mkubwa sana Yese, jamii yake iliona kuwa Yese
mwenye Damu ya kimoabu toka kwa bibi yake Ruthu na hata watoto wake wasingeweza
tena kwa namna yoyote kuwa wenye kufaa kwa vile walijulikana kuwa na damu ya
kimoabu kwa hivyo wametokana na ndoa zilizokatazwa na Torati ya Musa unaweza
kuona! ushahidi wa maisha ya Daudi wakati wa mapambano na Sauli unathibitisha
kwamba Daudi aliwakimbiza wazazi wake kwa mfalme wa Moabu ona 1Samuel 22:3-4 “Basi
Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na ndugu zake na watu wote
wa mbari ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko. Na kila mtu
aliyekuwa katika hali ya dhiki, na kila mtu aliyekuwa na deni, na watu wote
wenye uchungu mioyoni mwao, wakakusanyika kwake; naye akawa jemadari wao; nao
waliokuwa pamoja naye walipata kama watu mia nne. Kutoka huko Daudi akaenda
Mispa ya Moabu; akamwambia mfalme wa Moabu, Tafadhali ukubali baba yangu na
mama yangu watoke huko waliko, wakakae kwenu, hata nitakapojua Mungu
atakalotenda kwa ajili yangu. Akawaleta
mbele ya mfalme wa Moabu, nao wakakaa pamoja naye wakati wote Daudi alipokuwa
ngomeni.” Inasemekana moja ya sababu ya familia hii ya Yese kwenda
kujificha huko Moabu ni kwa sababu ya uhusiano wa Bibi yao Ruthu aliyetokea
katika nchi ya Moabu
Kutokana na
kuweko kwa mkanganyiko huo kuwa wayahudi wenye damu ya kimoabu wanafaa kuoana
na wayahudi halisi au la? Yese na wanawe ni Wayahudi wenye asili ya kimoabu
kutokana na babu yao Boazi kumuoa Ruth aliyekuwa mwongofu wa kiyahudi kutoka moabu na
mke wa Yese, Nizbeth alikuwa myahudi halisi wakati huu akiwa na watoto saba wa
kiume na wawili wa kike, Daudi akiwa hajazaliwa wazee wa mji walimuamuru Yese
aachane na Nizbeth na wala wasigusane tena! Na kusiweko uhusiano tena kati ya Yese na
Nizbeth, Hivyo familia ilikubaliana kuwa Yese na Nizbeth kuwa waachane (na kwa
vile haukuwa ugomvi) waliachana katika hali ya upendo tu kwamba Nizbeth ambaye
ni myahudi halisi asitende dhambi na myahudi mwenye damu ya kimoabu kwa hivyo
Yese aliahidi kuwa atamtuza Nizbeth na kumlisha isipokuwa tu hakutakuwa na
uhusiano wa kindoa ili kutunza heshima zao katika jamii!, watoto wote wakubwa
wa Yese walifahamu utengano huo na walikubaliana. Jambo hili lilikubalika na
Wazee ambao waliitwa “WAKETIO LANGONI”
waketio langoni walikuwa ni wazee wa mji wenye kuheshimika kwa kufanya maamuzi
ya kimahakama ona mfano Ruthu 4:1-12 “Basi Boazi akakwea kwenda mpaka langoni, akaketi pale; na
tazama, yule mtu wa jamaa aliyekuwa karibu, ambaye Boazi amemnena, akapita.
Naye akamwita, Haya! Wewe, karibu, uketi hapa. Naye akaja akaketi. Kisha
akatwaa watu kumi miongoni mwa wazee wa mji, akawaambia, Ninyi nanyi, ketini
hapa. Wakaketi. Kisha akamwambia yule jamaa, Huyu Naomi, aliyerudi hapa kutoka nchi
ya Moabu, anauza sehemu ya ardhi aliyokuwa nayo ndugu yetu, Elimeleki; nami
ilikuwa nia yangu nikujulishe wewe, na kukuambia, Uinunue mbele ya hawa waliopo
na mbele ya wazee wa watu wangu. Kama wewe utaikomboa, haya, uikomboe; lakini
kama hutaikomboa, uniambie ili nijue mimi; kwa kuwa hakuna mtu wa kuikomboa ila
wewe, na baada yako ni mimi. Naye akasema, Nitaikomboa mimi. Ndipo Boazi aliposema, Siku ile
utakapolinunua shamba mkononi mwa Naomi, unamnunua Ruthu pia, huyu Mmoabi,
mkewe marehemu, ili makusudi umwinulie marehemu jina katika urithi wake. Basi
yule jamaa aliyekuwa wa karibu akasema, Mimi sitaweza kulikomboa kwa nafsi
yangu, nisije nikauharibu urithi wangu mwenyewe; basi haki yangu ya kulikomboa
ujichukulie wewe, maana mimi sitaweza kulikomboa. Basi hii ilikuwa desturi
zamani za kale katika Israeli, kwa habari ya kukomboa na kubadiliana, ili
kuyahakikisha yote; mtu huvua kiatu chake na kumpa mwenziwe; ndivyo
walivyohakikisha neno katika Israeli. Basi yule jamaa akamwambia Boazi, Wewe
ujinunulie mwenyewe. Akavua kiatu chake. Naye Boazi akawaambia wale wazee na
watu wote, Leo hivi ninyi ni mashahidi ya kwamba mimi nimenunua yote yaliyokuwa
ya Elimeleki, na yote yaliyokuwa ya Kilioni na Maloni, mkononi mwa Naomi. Tena,
huyu Ruthu Mmoabi, mkewe Maloni, nimemnunua awe mke wangu, makusudi nipate
kumwinulia marehemu jina katika urithi wake, jina lake marehemu lisikatike
miongoni mwa ndugu zake, wala langoni pa mji wake; leo hivi ninyi ni
mashahidi. Na watu wote waliokuwapo
langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. Bwana na amfanye
mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili
walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri
katika Bethlehemu. Nyumba yako na ifanane na nyumba yake Peresi, ambaye kwamba
Tamari alimzalia Yuda, kwa wazao atakaokupa Bwana katika mwanamke huyu.”
Unaona waketio Langoni walikuwa ni wazee wenye ujuzi wa torati waamuzi na ndio
waliokuwa wakifanya maamuzi, kwa hiyo Langoni ilikuwa ni kama mahakamani, Hapo
walipitisha kuwa Boazi amnunue Ruthu na kuwa mkewe kama jamaa aliye karibu,
lakini kumbuka baadaye wazee waliokuweko katika kizazi za Yese ndio walioamua
Yese aachane na Nizbeth na ndio vilevile walikuwa miongoni mwa watu waliomuona
Daudi kama mtoto asiyefaa nao walishiriki kumsema vibaya ona Zaburi 69:10-12 “Nilipolia
na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga, Ikawa laumu juu yangu. Nilipofanya gunia
kuwa nguo zangu, Nikawa mithali kwao. Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za
walevi hunidhihaki.” Mtazamo wa wazee hao ilikuwa Yese na wanawe
ingawa ni wema lakini wamezaliwa katika ndoa zilizokatazwa na torati ya Musa!
Baada ya miaka
kadhaa kupita Yese alitamani tena kuwa na mtoto ambaye hatakuwa na maswali
kuhusu asili yake kwamba asiwe mwamoni wala mmoabu, hivyo aliazimia kuanzisha
uhusiano na mjakazi wa Nizbeth ambaye alikuwa mkanaani, Yese alimwambia mjakazi
huyo maneno haya “Kama nitakubalika kama Myahudi halali basi
wewe utafaa kuwa mke halali uliyemuamini Mungu wa Israel kwa hiyo utaweza
kunizalia mtoto halali asiye na lawama kwa vile haikubaliki kwa mtu mwenye damu
ya mmoabu au mwamoni kuzaa na myahudi hivyo utakuwa huru wala hutakuwa mtumwa
tena” Mjakazi huyo wa Nizbeth alielewa mpango huu wa Yese na alimueleza
Nizbeth kwa vile alikuwa mwaminifu sana kwa bibi yake, Nizbeth alikuwa anapitia
uchungu mkubwa sana wa kukaa hivihivi akiwa ametengwa na mumewe hivyo
walikubaliana na mjakazi wake kwamba usiku ule Yese atakapotaka kuingia
kwako tafadhali uniache niingie mie kama Leah alivyofanyiwa na Raheli na mjakazi
alikubali ombi la Nizbeth huku Yese akiwa hajui mpango huo, Nizbeth aliingia na
kulala na mumewe na kwa bahati njema alipata ujauzito alitoka asubuhi na mapema
kama ilivyo desturi za wakati huo na Yese hakujua kuwa alilala na mkewe halali
Nizbeth (Ilikuwa desturi zamani katika
jamii ya kiyahudi mwanamke kumuendea mwanaume wakati wa usiku na kuondoka
asubuhi baada ya kumhudumia kwa tendo la ndoa) ona Ruthu3:1-14 “Kisha Naomi akamwambia mkwewe,
Je! Mwanangu, si vizuri nikutafutie raha, ili upate mema? Basi na huyu Boazi,
je! Siye wa mbari yetu, ambaye ulikuwapo pamoja na wasichana wake? Tazama,
usiku wa leo atakuwa akipepeta shayiri pale ugani. Basi wewe oga, ujipake
mafuta ujivike mavazi yako, kisha uende kwenye uga; walakini usijionyeshe kwake
mtu yule, ila atakapokwisha kula na kunywa. Nayo itakuwa wakati atakapolala,
utapaangalia mahali alalapo, nawe uingie, uifunue miguu yake ujilaze hapo; na
yeye atakuambia utakalofanya. Akamwambia, Hayo yote unenayo mimi nitayafanya.
Basi akashuka mpaka ugani; akafanya yote kama vile mkwewe alivyomwagiza. Ikawa
huyo Boazi alipokwisha kula na kunywa, na moyo wake umekunjuka, alikwenda
kulala penye mwisho wa chungu ya nafaka; na huyo mwanamke akaja taratibu,
akaifunua miguu yake, akajilaza papo hapo. Na ikawa usiku wa manane yule mtu
akasituka, akajigeuza; na kumbe! Yupo mwanamke amelala miguuni pake. Akasema,
Ama! Ni nani wewe? Akamjibu, Ni mimi, Ruthu, mjakazi wako; uitande nguo yako
juu ya mjakazi wako; kwa kuwa ndiwe wa jamaa aliye karibu. Akamwambia,
Mwanangu, ubarikiwe na Bwana; umezidi kuonyesha fadhili zako mwisho kuliko
mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, kama ni maskini kama ni matajiri. Basi,
mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana mji wote pia wa
watu wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema. Tena ndiyo kweli ya kuwa mimi ni wa jamaa
yako aliye karibu; lakini kuna mtu wa jamaa aliye karibu kuliko mimi. Wewe
ungoje usiku huu; kisha, asubuhi, kama akikubali kukufanyia impasavyo jamaa,
haya, na akufanyie; lakini ikiwa hataki yeye, basi mimi nitakufanyia impasavyo
jamaa; Bwana aishivyo. Ulale wewe hata asubuhi. Hivyo huyo mwanamke akalala
miguuni pake hata asubuhi; akaondoka mapema asijaweza mtu kumtambua mwenziwe;
maana Boazi amesema, Isijulikane kabisa ya kuwa mwanamke alifika penye uga.”
Unaona kwa mujibu wa mila hii, Nizbeth alikwenda kulala na mumewe na kuondoka asubuhi bila Yese kujua.
Baada ya miezi
kama mitatu hivi ilibainika kuwa Nizbeth ana mimba, boma zima lilifahamu na
watoto wake wakubwa walijua na mzee Yese pia alitambua kuwa Nizbeth ana mimba
boma zima walikusudia apigwe mawe afe kwa sababu huenda mimba hiyo ameipata kwa
uzinzi, Nizbeth hakutaka kabisa kuelezea namna alivyopata mimba hiyo kwa sababu
alijua Yese atafadhaika sana na hakutaka kumuudhi, Nizbeth aliamua atakaa kimya
tu! Aliweka nadhiri ya kukaa kimya mpaka Mungu mwenyewe alete haki, Yese akiwa
hajui kabisa kuwa mimba hiyo imetokea vipi aliwaamuru watoto wake wasimuue Nizbeth
wamuache aishi, lakini mtoto atakayezaliwa na ahesabike kama mtumwa tu na mwana
wa haramu! Na asiruhusiwe kuoa Myahudi.
Tangu wakati huu
hiki ndio kikawa chanzo kikubwa zaidi cha chuki dhidi ya Nizbeth na mwanaye
Daudi, walichukiwa na jamii na kuhesabika kama watu wasiofaa na walioleta aibu
kubwa sana katika familia ya Yese! Kijana huyu alianza kupitia maisha magumu na
ya kukataliwa na jamii akihesabika kama mwana wa zinaa na mtoto wa dhambi! Na mtumwa. Alipelekwa kuchunga kondoo na kutokuhesabika
kama sehemu ya familia ya Yese, habari zilienea Bethelehemu yote, na kama kitu
kuilipotea alisingiziwa yeye na hata kulipishwa! Watu walisema mambo yote mema
ya Boazi yamejulikana kwa Mwanae Yese na watoto wake saba lakini mambo mabaya
ya kuoa Mmoabu ya Ruthu yamejulikana kupitia mtoto huyu mlaaniwa! Na ndio maana
Daudi alikuwa akikaripiwa na nduguze na kuhesabika kama motto mwenye kiburi na
anayestahili kushinda porini tu akiwachunga kondoo ona 1Samuel 17:12-28 “Basi Daudi alikuwa mwana
wa yule Mwefrathi, wa Bethlehemu ya Yuda, aliyeitwa jina lake Yese; naye huyo
alikuwa na wana wanane; na yeye mwenyewe alikuwa mzee siku za Sauli, na mkongwe
miongoni mwa watu. Nao wale wana watatu wa Yese waliokuwa wakubwa walikuwa
wamefuatana na Sauli kwenda vitani, na majina ya hao wanawe watatu waliokwenda
vitani ni haya, mzaliwa wa kwanza Eliabu, na wa pili wake Abinadabu, na wa tatu
Shama. Naye huyo Daudi alikuwa mdogo wa wote; na hao watatu waliokuwa wakubwa
wakafuatana na Sauli.Basi Daudi alikuwa akienda kwa Sauli na kurudi ili
awalishe kondoo za baba yake huko Bethlehemu.Naye yule Mfilisti hukaribia
asubuhi na jioni, akajitokeza siku arobaini. Ndipo Yese akamwambia Daudi
mwanawe, Haya! Sasa uwachukulie ndugu zako efa ya bisi, na mikate hii kumi,
ipeleke upesi kambini kwa ndugu zako; ukampelekee akida wa elfu yao jibini hizi
kumi, ukawaangalie, wa hali gani, kisha uniletee jawabu yao. Basi Sauli, na
watu wote wa Israeli, walikuwa katika bonde la Ela, wakipigana na Wafilisti.
Daudi akaondoka asubuhi na mapema, akawaacha kondoo pamoja na mchungaji,
akavitwaa vitu vile, akaenda, kama Yese alivyomwamuru; akafika penye magari,
wakati lile jeshi walipokuwa wakitoka kwenda kupigana, wakipiga kelele za vita.
Nao Waisraeli na Wafilisti wakajipanga, jeshi hili likikabili jeshi hili. Basi
Daudi akaviacha vile vyombo vyake katika mkono wa mlinda vyombo, akalikimbilia
jeshi, akafika, akawasalimu ndugu zake. Hata alipokuwa akisema nao, kumbe! Yule
shujaa alitokea, yule Mfilisti wa Gathi, jina lake Goliathi, akitoka katika
jeshi la Wafilisti, akasema maneno yale yale; naye Daudi akayasikia. Na watu
wote wa Israeli walipomwona yule mtu wakakimbia, wakaogopa sana. Watu wa
Israeli wakasema, Je! Mmemwona mtu huyu aliyepanda huko? Hakika ametokea ili
awatukane Israeli; basi, itakuwa, mtu yule atakayemwua, mfalme atamtajirisha
kwa utajiri mwingi, naye atamwoza binti yake, na kuifanya mbari ya baba yake
kuwa huru katika Israeli. Daudi akaongea na watu waliosimama karibu, akisema,
Je! Atafanyiwaje yeye atakayemwua Mfilisti huyo, na kuwaondolea Israeli aibu
hii? Maana Mfilisti huyu asiyetahiriwa ni nani hata awatukane majeshi ya Mungu
aliye hai? Nao watu wakamjibu vivyo hivyo, wakisema, Ndivyo atakavyofanyiwa mtu
yule atakayemwua. Naye Eliabu, mkubwa wake, alisikia hapo alipoongea na watu;
na hasira yake Eliabu ikawaka juu ya Daudi, akasema, Mbona wewe umeshuka hapa?
Na kondoo wale wachache umemwachia nani kule nyikani? Mimi nakujua kiburi
chako, na ubaya wa moyo wako; maana umeshuka ili upate kuvitazama vita.”Unaweza
kuona moyo wa kaka mkubwa dhidi ya Mdogo wake akimkemea Daudi na kumuona kama
kiburi na mwenye moyo mbaya! haya ndio yalikuwa aina ya maisha ya Daudi,
kutokana na kuzaliwa kwake kwa utata ilihesabika kama aliyezaliwa kwa zinaa ama
kwa vile Nizbeth alikuwa amekiuka makubaliano na Yese na wazee.
Kwaajili ya haya
Maisha ya Daudi yalikuwa ya kudharauliwa, kukataliwa, na kuhesabika kama mtu
asiyefaa kitu au aliyelaaniwa, alilaumiwa kama mtu aliyesababisha kusambaratika
kwa familia, alifedheheshwa na kuonekana kama mgeni na asiyetambulika au
mkimbizi, Zaburi 69:7-8 “Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika
uso wangu. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu.” Sio tu kwa ndugu zake lakini hata jamii
iliamini maneno ya ndugu wa Daudi na kufuata mfano wa familia yake Zaburi 69:10-12 “Nilipolia
na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga, Ikawa laumu juu yangu. Nilipofanya gunia
kuwa nguo zangu, Nikawa mithali kwao. Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za
walevi hunidhihaki.” Daudi aliishi maisha ya uchungu akimlilia Mungu
kutokana na fedheha alizokutana nazo wakati wote ndugu zake walihakikisha kuwa
wanampa uchungu kama chakula alifunga na kuomba na bado kwake ikawa kama ni
swala la dhihaka Zaburi 69:17-21 “Wala usinifiche uso wako, mimi mtumishi wako, Maana mimi
nimo taabuni, unijibu upesi. Uikaribie nafsi yangu, uikomboe, Kwa sababu ya
adui zangu unifidie. Wewe umejua kulaumiwa kwangu, Na kuaibika na kufedheheka
kwangu, Mbele zako Wewe wako watesi wangu wote. Laumu imenivunja moyo, Nami
ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji,
wala sikumwona mtu. Wakanipa uchungu kuwa chakula changu; Nami nilipokuwa na
kiu wakaninywesha siki.” Licha ya mapito ya aina hii Daudi
hakuruhusiwa kuikaribia nyumba ya Bwana wala kujihusisha na maswala ya ibada,
yeye na mama yake walikuwa wakisubiri siku moja kweli itadhihirika kuhusu
shutuma dhidi yake na mwanaye.
Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu
la Pembeni!
Habari za Daudi
zinabadilika sasa baada ya Nabii Samuel kuamuriwa na Mungu aende Bethelehemu
kwa kusudi la kumtia mafuta moja ya watoto wa Yese ambaye yeye Mungu
atamuonyesha nabii Samuel ona 1Samuel
16:1-5 “Bwana akamwambia Samweli, Hata lini
utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako
mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia
mfalme katika wanawe. Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari,
ataniua. Basi Bwana akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili
kumtolea Bwana dhabihu. Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha
utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako. Samweli akafanya
hayo aliyosema Bwana, akaenda Bethlehemu. Wakaja wazee wa mji kumlaki,
wakitetemeka, nao wakasema, Je! Umekuja kwa amani? Naye akasema, Naam, kwa
amani; nimekuja kumtolea Bwana dhabihu; jitakaseni; njoni pamoja nami kwenye
dhabihu. Akawatakasa Yese na wanawe, akawaita kwenye dhabihu.”
Maandiko
yanaonyesha kuwa Samuel alipofika Bethelehemu wazee wa mji walikwenda kumlaki
na kumsalimu na huku wakitetemeka, wote waliogopa na hofu hii haikuwa ya
kawaida walihisi ujio huu wa nabii sio ujio wa kawaida hivyo walimuuliza kama
amekuja kwa amani kwa mujibu wa maelezo ya marabi ni kuwa waliogopa kuwa huenda
Samuel amesikia au kujulishwa dhambi yao dhidi ya kijana Daudi na labda amekuja
kuwakemea vikali tabia yao na ile hali ya kumtesa kijana aliyeachwa machungani,
Samuel aliwahakikishia kuwa amekuja kwa amani, na aliwataka wazee na Yese na
wanae wajiunge katika ibada ya kumtolea Mungu dhabihu, Kama mzee aliyeheshimika
ilikuwa ni kawaida kwa Yese kualikwa, Lakini wanae walipoalikwa hili lilikuwa
jambo la kushitua kidogo, waliogopa kuwa mm huenda wamekosea sana kuwatenga
watoto wa Yese na walijua kuwa labda Samuel atawakemea hadharani na kumbe
Samuel alikuwa amefunuliwa kuwa Mfalme mpya ajaye ni mwana wa Yese na mbaya
zaidi alikuwa ni Yule aliyekataliwa na
tena wala hakuletwa katika ibada hii ikifikiriwa kuwa hakuwa mwenye kufaa!
Swali la Samuel
lilikuwa la kinabii, Mungu sio tu alimtuma kuchagua mfalme ajaye bali pia
kuponya Moyo wa Nizbeth na mwanaye aliyekataliwa na jamii yake lakini pia
kuuweka sawa moyo wa Yese na wazee kuwa machoni pa Mungu Yule mtoto alikuwa ni
halali kwa Yese na Nezbeth na kuwa watoto wote wa Yese na Yese mwenyewe walikubaliwa
na Mungu. Na wanastahili kumtumikia Mungu na kukaribia mkutano wa watu wa Mungu
kama ilivyo kwa wayahudi wengine.
Swali Baada ya
wana wote wa Yese kupitishwa mbele ya Samuel, Samuel alimwambia Yese Bwana
hakuwachagua hawa kisha akamuuliza “Kisha Samweli akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo
hapa?” hapa ndipo palikuwa
mahali pagumu sana kwa Yese kwa taarifa yako kwa vile alikuwa anaamini kuwa
hawa ndio watoto wake wote angejibu tu kuwa ndio wote wapo hapa lakini ona “Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na
tazama, anawachunga kondoo” Daudi alikuwa hakubaliki na baba yake Yese
alidhani kuwa mawazo ya Mungu na Samuel yatakuwa kama yake na kuwa atakubali
kijana huyo abaki huko huko porini tu Lakini Samuel aliagiza aletwe mara moja
na kuwa hakuna kitakachoendelea mpaka aje, kwaajili ya kumuheshimu nabii walitumwa
wajumbe akamlete kijana huyo!
Inawezekana
kwamba kila mmoja alishangaa tukio lile na huenda hata Samuel hakuweza kuamini
kama huyu anaweza kuwa mtiwa mafuta sauti ya Mungu ikamwambia Samuel “Ondoka, umtie
mafuta; maana huyu ndiye.” Baada ya Samuel kumtia mafuta Sauti ya
Nizbeth iliisikika ikipiga kelele za furaha kumbuka ni yeye pekee aliyekuwa
akimuunga mkono mwanaye na pekee ndiye aliyekuwa faraja miaka 28 ya kuteseka
kwake na ukimya wake wakikabiliwa na lawama sasa unafikia mwisho kwa Mungu kuingilia
kati na kuthibitisha kuwa mtoto alikuwa na haki na mama yake alikuwa na haki na
alikuwa mtoto halisi wa Yese! Na huu ukawa ndio mwisho wa mateso ya Nizbeth na
mwanaye Daudi wakifurahi Nizbeth na Daudi waliimba Zaburi ya 118 na Mstari wa 22-23
wanasema maneno mazito Zaburi 118:22-23
“Jiwe walilolikataa waashi Limekuwa jiwe kuu la
pembeni.Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu.” Ilishangaza
kuwa kijana aliyekataliwa na mji mzima ndiye Masihi wa bwana ndiye mpakwa
mafuta ndiye mfalme ajaye! Wao walikuwa wamemkataa Daudi na Bwana alikuwa
amemchagua Daudi, uchaguzi wa Daudi ulitoka kwa Mungu na ukawa ajabu kubwa sana
machoni pa kila mmoja!
Kuna maswala
mengi sana kuhusiana na habari hizi za siri katika maisha ya Daudi na familia
yake lakini kama taarifa hizo zina ukweli na Yese na familia yake waliamini
hivyo ndio maana na Daudi anayasema hayo kama taarifa ambayo ilienea katika
jamii Zaburi 51:5 “Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu
alinichukua mimba hatiani” Mstari
huu umekuwa mgumu kutafasirika kwa sababu tu wayahudi hawakuwa na hawaamini
katika dhambi ya asili na Daudi alipata ufunuo mdogo sana kuhusu asili ya dhambi
na ndio maana tafasiri ya maandiko hayo katika mtazamo wa agano jipya ni rahisi
kuliko mtazamo wa kiyahudi! hata hivyo
kwa kuwa mama wa Daudi Nizbeth na mjakazi wake walikuwa na uelewa kuhusu jambo
hili Daudi alifahamu pia kupitia wao kwa upande mwingine kwamba habari zile
kwamba amezaliwa kwa zinaa sio za kweli, hivyo alionewa kwa sababu isiyo kweli
ona Zaburi
69:4 “Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za
kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu
isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.”
na zilikuwa ni shutuma tu katika jamii yake na Mungu alilimaliza swala lile
kupitia nabii Samuel na kutiwa mafuta kwa Daudi kama mwana wa Yese!.
Mapito haya ya Daudi
kinabii pia yanatoa picha ya kile kilichokuwa kinaendelea katika familia ya
Yusufu na Mariam, Mambo mengi yaliyompata Daudi yalikuwa ni unabii, yanatabiri
jinsi mwanae yaani Masihi atakayoyapitia, Biblia haijaeleza kila kitu lakini
kuna ukweli kuwa Yesu hakukubalika na Ndugu zake, Hata ingawa Mungu aliweka
wazi kwa Yusufu kuwa mkewe alipata Mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, ni wazi
kuwa katika jamii jambo hilo halikuweza kukubalika kama unavyoweza kufikiri
Biblia inaonyesha kuwa ndugu wa Yesu Kristo walikuja kumkubali baadaye kama iliyokuwa
kwa Daudi, wao hawakumuamini kama masihi
na ni Mariamu pekee ndiye aliyekuwa na uelewa kuwa Yesu ni mtoto wa namna gani
kama ambavyo Nezbeth alivyomuelewa Daudi Yohana
7:1-5 “Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea
katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Uyahudi, kwa sababu Wayahudi
walikuwa wakitafuta kumwua. Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa
karibu. Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako
nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. Kwa maana hakuna mtu afanyaye
neno kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi
jidhihirishe kwa ulimwengu. Maana hata nduguze hawakumwamini.” Aidha
watu wengine pia hawakuamini kuwa Yesu alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na
ili kumkatisha tamaa adui zake waliwahi kumjibu kuwa wao hawakuzaliwa kwa zinaa
ona Yohana 8:41 “Ninyi mnazitenda kazi za baba yenu. Ndipo walipomwambia, Sisi
hatukuzaliwa kwa zinaa; sisi tunaye Baba mmoja, yaani, Mungu.” Unaweza
kuona kwa ufupi mapito aliyopitia Daudi kinabii yalimtokea Yesu Kristo! Daudi
anaposema mama yangu alinichukua Mimba hatiani wakati huu hakukuwa na ufunuo wa
mwanadamu kuwa na asili ya dhambi, kwa hivyo watafasiri wengi wa biblia
wakiwemo marabi, walikuwa wanafikri kuwa Daudi alikuwa akiizungumzia hali ya
maneno yaliyoenea katika jamii yaje kuwa mama yake alimchukua mimba hatiani, na
kama yalikuwa ni mapatano na Yese kuwa wasikutane ni dhahiri kuwa Nizbeth
alifanya makosa kuchukua mimba na Yese nje ya mapatano na amri ya wazee, lakini
kama mke halali wa Yese mama huyu ni shujaa wa imani kwani kupitia tendo hili,
alivishinda vita vya kishetani vya kupamaba na uzao wa Masihi.
Sasa basi Daudi
alikuwa na maana gani kusema mama yangu alinichukua Mimba hatiani kama tunaona
kuwa Daudi ni mwana halali wa Yese hapa kuna mawazo mbalimbali kuhusu tafasiri
za mstari huu ukiacha masimulizi ya Kiyahudi:-
2.
Asili
ya dhambi: Mstari huu pia unaweza kumaanisha kuwa watoto wachanga
wanazaliwa wakiwa na dhambi ya asili, kwamba tendo la Daudi kufanya dhambi,
licha ya kuwa ni mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu na bado alikuwa analenga
kumpendeza Mungu na kamwe hakwepi ule wajibu wa kuwa anawajibika kwa Mungu kwa
dhambi aliyoitenda lakini anapata utambuzi kuwa ameumbwa katika hali hiyo na
sio kwaajili ya Muumba mwenyewe lakini kwa kurithi, kwa damu, tangu alipokuwa
akitungishwa mimba au tangu mama yake anapokea ujauzito kuhusu yeye tayari
alikuwa na dhambi ya asili inayotokana na uwepo wa dhambi kwa baba yetu Adamu Ezekiel 16:4 . “Na
katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako
hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo,
wala hukutiwa katika nguo kabisa.” Ezekiel anazungumzia kitovu cha
kiroho japo kila mtoto anapozaliwa anakatwa kitovu, lakini kuna kitovu cha
rohoni kinachotuunga kurithi maswala kadhaa kutoka kwa baba zetu kwa hiyo sisi
tumefanya dhambi tangu tukiwa viunoni mwa baba yetu Adamu kama vile maandiko
yanavyotufundisha kuwa Lawi alitoa zaka wakati Abraham anatoa zaka kwa Melkizedeki
kwa vile alikuwa katika viuno vyake ona Waebrania
7:9-10 “Tena yaweza kusemwa ya kuwa, kwa njia ya
Ibrahimu, hata Lawi apokeaye sehemu ya kumi alitoa sehemu ya kumi; kwa maana alikuwa
katika viuno vya baba yake, hapo Melkizedeki alipokutana naye.” Kwa hivyo watoto wanarithi hatia
kutoka kwa wazazi wao, na wanashiriki mema kutoka kwa wazazi wao kitendo cha Abrahamu
kutoa zaka kinahesabika kibiblia kuwa Lawi naye alitoa zaka hata kabla ya
kuzaliwa kwa vile alikuwa viunoni mwa baba yake na ndio maana watoto vilevile
hufa kwa sababu mshahara wa dhambi ni mauti ona Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi
ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
Urithi wa kifo umetokana na urithi wa dhambi na vyote hivi tumevirithi
kutoka kwa Adamu baba yetu kwa msingi huo wanadamu wote ni wenye dhambi
isipokuwa Yesu Kristo pekee, sasa basi Daudi anapotubia kosa lake anaakisi
asili yake ya dhambi kwa kusema Tazama mimi naliumbwa katika hali ya uovu, mama
yangu alinichukua mimba hatiani, akimaanisha kuwa alikuwa mwenye dhambi tangu
inatungishwa mimba, kama vile adui alivyopanda magugu kwenye ngano mapema kabla
havijaanza kuota na hii ilikuwa moja ya dhana ya kiyahudi pia kwamba mwanadamu huzaliwa katika hali
ya dhambi Yohana 9:34 “Wakajibu, wakamwambia, Ama! Wewe ulizaliwa katika dhambi
tupu, nawe unatufundisha sisi? Wakamtoa nje.” Hii inaweza kuwa
tafasiri nzuri ya andiko hilo kwa mtazamo wa kikristo, japo katika agano la
kale mtazamo huu na kwa wayahudi ulikuwa haujafunuliwa wazi.
3.
Mwenye dhambi kwa kuzaliwa: Daudi hapa
ni kama anatambua kuwa yeye sio mwenye dhambi tu kwa kuzitenda lakini pia ni
mwenye dhambi kwa kuzaliwa au kwa asili, Paulo mtume aliliambia kanisa la
warumi kwamba Warumi 5:12 “Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa
kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na
kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili
ya wale wengi.” Wala Daudi hakumaanisha kuwa tendo la ndoa katika
ndoa ni dhambi, au mimba iliyotungwa kwa wazazi wake halali ilikuwa kosa lakini
alikuwa na wazo kuwa mwanadamu ana asili ya uharibifu tu, Kama jinsi ambavyo mwembe huzaa mwembe, Mwanadamu hufanya dhambi
kwa sababu ni mwenye dhambi kwa asili
Warumi 3:10-12, 23 ”kama ilivyoandikwa, ya kwamba,
Hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. Wote
wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja., kwa sababu
wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;” Kwa
msingi huo kwa vile wanadamu wote ni wenye dhambi kwa asili na kwa kuzitenda,
hatuwezi kuingia katika ufalme wa Mungu bila kupokea asili mpya kwa neema ya
Yesu Kristo na ndio maana pamoja na dua yake Daudi alijiombea moyo safi na
kuumbwa upya kwa roho yake ona Zaburi
51:10-11 ”Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye
upya roho iliyotulia ndani yangu Usinitenge na uso wako, Wala roho yako
mtakatifu usiniondolee.” Wakati huu kazi za Kristo na Roho Mtakatifu
zilikuwa sio dhahiri sana Lakini Daudi alikuwa na hisia za kinabii za kutamani
kuzaliwa mara ya pili ili asili yake ya dhambi iweze kudhoofishwa kwa msaada wa
Roho Mtakatifu na kufanywa upya Yohana
3; 4-7 “Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa,
akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yesu
akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi
kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa
kwa Roho ni roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya
pili.” Mungu anapoingilia kati na kudhoofisha asili ya dhambi ndipo
tunapata neema ya kuwa washirika wa tabia ya uungu ndani yetu 2Petro 1:4 “Tena
kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate
kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa
sababu ya tamaa.” Bila neema ya Mungu na uwezo war oho Mtakatifu
kuingilia kati na kudhoofisha nguvu ya asili ndani yetu hatuwezi kuchagua
kutokuitenda dhambi, isipokuwa kwa msada wa Mungu.
4.
Dhana
ya tangu ujana au utoto: Daudi alikuwa kwenye maombi binafsi na toba yake
kwa Mungu alikuwa ameelewa kuwa amemkosea Mungu na wala hakuwa anatafuta
kujitetea kwa Mungu wake wala kusingizia dhambi yake kwa wazazi wake wala kujihesabia
haki, Ezekiel 18:20 “Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana
hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake
mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.”
Daudi alikuwa anataka kuikamilisha toba yake kwamba sio tu nimekutenda dhambi
binafsi, lakini kwa asili mimi ni mwenye dhambi, Matendo ya maisha yangu
yameathiriwa tangu namna ya kuumbwa kwangu na hata kuzaliwa kwangu, Mama yangu
alinichukua mimba hatiani, hamaaniishi anataka kumshutumu mama yake yeye
alikuwa akijianika kwa Mungu na kumueleza Mungu mtazamo wake kwamba anastahili
kuwa chombo cha hasira ya Mungu, lakini
zaidi sana anahitaji rehema, zaidi ya dhambi aliyoifanya lakini hata na tangu
kuzaliwa kwake na kuumbika kwake ndani ya tumbo la mama yake. Mzizi wake wa
dhambi unatoka mbali. Daudi anakubali kuwajibika kwa dhambi yake wala hamtwishi
awaye yote maovu yake, kuumbwa katika hali ya uovu kwake pia haimaanishi kuwa
anamlaumu Mungu muumba bali yeye anakubali kuwa mwanadamu kwaasili ni muovu,
wayahudi wakati mwingine walitumia neno ujana, wakimaanisha vievile hatua za
ukuaji kutoka mwaka 0-28 miaka ya ujana kwa hiyo walikuwa na semi kama mwanadamu
ameharibika tangu ujana wake wakiwa na maana tangu mtu anajua mema na mabaya
ona kwa mfano au tangu anaanza maisha Mwanzo
8:21 “BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; BWANA
akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu,
maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu UJANA wake; wala sitapiga
tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.” Ona pia Yeremia
3:25 “Na tulale kwa aibu yetu, haya yetu na
itufunike; kwa maana tumemwasi Bwana, Mungu wetu, sisi na baba zetu, tangu UJANA
wetu hata leo; wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu.” Isaya 7:15 “Siagi na asali atakula, wakati ajuapo kuyakataa mabaya na
kuyachagua mema.” Waebrania
walikuwa na dhana kuwa mwanadamu huanza kuhesabiwa haki wakati wa ujana wake
yaani wakati ajuapo kutenda mema au mabaya Lakini Daudi anaona kuwa tangu mimba
inapotungwa tayari hali ya kutenda tusiyoyataka inampata mwanadamu.
5.
Lugha
ya kimashairi
Wengine hudhani
kuwa Zaburi 51:5 ni Lugha ya kishairi tu ya kukuza mambo “hyperbole” Daudi alikuwa anatubu dhambi na kuikiri dhambi aliyokuwa
ameifanya mbele za Mungu na kati kati ya toba yake anajutia na kujikuza kuwa yeye ni mwenye
dhambi zaidi ya kawaida na kuwa amekuwa mwenye dhambi kwa asili tangu
kutungishwa mimba, Kwa hiyo wataalamu wa kimaandiko hufikiri kuwa ni lugha tu
ya kishairi kama vile mtu anavyoweza kusema analowesha kitanda chake kwa
machozi Zaburi 6:6 “Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakieleza kitanda
changu; Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu” au kama vile
Paulo anavyodai kuwa Mungu alikuja kuwaokoa wenye dhambi na wa kwanza wao ni
mimi 1Timotheo 1:15 “Ni neno la
kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja
ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.”
6.
Lugha
tu!
Wakati mwingine
Lugha tu inaweza kusababisha mstari uweze kuwa mgumu kutafasirika kwa msingi
huo tunapoangalia lugha zilizotumika katika Biblia mbalimbalia utaweza kugundua
kuwa lugha iliyotumika hapo imefanywa kuwa ngumu na baadhi ya tafasiri za
biblia na baadhi zimeifanya kuwa rahisi kwa Mfano:-
NIV Psalm 51:5 “Surely I was sinful at
Birth, sinful from time my mother conceived me “Kwa hakika nalikuwa mwenye
dhambi tangu kuzaliwa, mwenye dhambi tangu mama yangu anatunga ujauzito”
KJV Psalm 51:5 “Behold I was shapen in
iniquity, and in sin did my mother conceive me” Tazama nimeumbwa katika hali ya
uovu, na katika hali ya dhambi mama yangu alinipokea”
ESV.Psalm 51:5 “Behold I was brought
forth in iniquity, and in sin did my mother conceive me” Tazama naliletwa
katika hali ya uovu na katika hali ya dhambi mama yangu alinipokea
NLT Psalm 51:5 “For I was born a
sinner,Yes from the moment my mother conceived me” Kwa dhambi nalizaliwa ndio
tangu wakati mama yangu ananipokea”
SUV Zaburi 51:5 ““Tazama,
mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani”
Tunajifunza
kwamba wakati mwingine ili andiko liweze kuekleweka vema tunaweza kupitia
tafasiri mbalimbali za kimaandiko na tukapata maana iliyokusudiwa kwa njia
rahisi, na kifungu au mstari ukawa ni mwepesi kueleweka.
7.
Tamaa
ya mama
Kwa mujibu wa
uchunguzi wa ndani zaidi wa kimaandiko wenye lengo la kuuangalia mstari huu
bila kuwa na mtazamo wa Kikrito wa kuwa mwanadamu ni mwenye dhambi kwa asili,
unapoangalia Lugha zilizotumika hapa ni wazi kuwa Daudi hamaanishi dhambi
kutoka kwa Adamu, bali anamaanisha dhambi ya mama yake, yaani kuwa mama yangu
alinichukua mimba hatiani, bila kuweka mtazamo wa Kikristo unapochunguza maneno
yaliyotumiwa na Daudi katika Mstari huu kuhusu mama yake kumchukua mimba
hatiani kwa kawaida kwa waebrania neno kushika mimba au kuchukua mimba
linatumika neno “HARAH” ambalo
linamaanisha kuwa mwanamke ameshika mimba, sasa katika kifungu hiki Daudi
anatumia neno “YACHAN” ambalo neno
hili ni baya sana kutumika kwa mwanadamu neno hili linamaanisha kushika mimba
katika tama ya kinyama yaani kama vile kondoo au Mbuzi ama Ngombe
anavyopandisha joto akiwa anataka kupata ujauzito ndio hali inayoitumia Daudi
kwa mama yake kuwa mjamzito, kwa hiyo huenda Daudi anamaanisha ile tama ya mama
yake ya kutaka kupokea ujauzito ilikuwa ni tama kama ya mnyama mwenye joto, kwa
hiyo Daudi anapotumia neno YACHAN anatumia
neno gumu sana kuonyesha kwamba alizaliwa akiwa na hali ya tama na mama yake
alimchukua mimba katika hali ya tama ambayo ni tama kama ile ya mnyama kwa hiyo
mimba ya daudi ilipatikana kama matokeo ya tama ya mama yake iliyokuwa kama ya
mnyama na huenda kwa tamaa kama ile ya Nizbeth naye alifanya unyama kumkabili
mke wa Uria, Hivyo basi kama Nizbeth hakufanya zinaa kumpata Daudi, alimpata
kwa kuvunja patano alilowekewa, alimpata kama matokeo ya tama kali ya mama yake
Zaburi 51:5 ““Tazama,
mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani”
huu unaweza kuwa Mtazamo sahihi wa andiko hili kama hatutaweka fundisho la
mwanadamu kuzaliwa akiwa na asili ya dhambi, lakini bado tunaona urithi wa aina
ileile ya asili ya dhambi kwamba kama kulikuwa na tamaa ya kinyama kwa Nizbeth,
Mwanae naye aliipata kwa Nizbeth na kama hivyo ndiyo ni tama ileile ya Eva
kutamani lile tunda katika bustani ya edeni
Hitimisho!
Ni muhimu kukubali kuwa Mstari
huu ni mstari wa Msingi sana na dhana zote zinazotolewa na wanatheolojia kuhusu
Mstari huu ni za msingi sana, zote zinatusaidia kufikiri vema na kujifunza vema
neno la Mungu, Nimefurahia mtazamo wa kiyahudi kuhusu mstari huu kwa sababu
ziko kweli kadhaa kuwa kuna mambo tulikuwa hatuyafahamu kuhusu maisha ya Daudi,
sasa tunaweza kuisoma zaburi katika mtazamo mpana mno na kuelewa maumivu
aliyoyapitia kijana huyu, lakini vilevile kinabii tunapata picha ya wazi kuhusu
kile alichokipitia Mariamu na Mwanaye Yesu Kristo, kwamba kinafanana kwa
ukaribu na kile kilichompata Daudi na Nizbeth!
Lakini ninaporejea sasa
katikamstari wa msingi wa Zaburi 51:5
“Tazama,
mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani”
naweza kuhitimisha kwa kusema haya Daudi hamaanishi kuwa Tendo la ndoa
katika ndoa halali ni dhambi, wala hamaanishi kwamba kutungishwa mimba kwa mama
yake na baba yake ni dhambi, Daudi aliwaheshimu sana Wazazi wake na kuwatunza
na amani iliporeja nyumbani kwao ni yeye ndiye aliyewapeleka na kuwatunza kwa
mfalme wa Moabu ona 1Samuel 22:3-4. “Kutoka huko Daudi akaenda Mispa ya Moabu; akamwambia
mfalme wa Moabu, Tafadhali ukubali BABA YANGU NA MAMA YANGU watoke huko waliko,
wakakae kwenu, hata nitakapojua Mungu atakalotenda kwa ajili yangu. Akawaleta
mbele ya mfalme wa Moabu, nao wakakaa pamoja naye wakati wote Daudi alipokuwa
ngomeni.” Ni wazi kuwa kama kulikuwa na utata uliisha baada ya
Samuel Nabii kumaliza tatizo, Kwa hiyo ni dhahiri Mungu alitambua kuwa Yese na
Nezbeth walikuwa wazazi halali wa Daudi na mapito yalikuwa ya kinabii tu, Daudi
aliwaheshimu baba yake na mama yake na aliwatunza na kuhakikisha wako salama,
Daudi hamaanishi kuwa alizaliwa kwa zinaa, kama mama yake alikwenda kwa mumewe
usiku na kupata ujauzito bado ilikuwa ni ndoa halali, na iliathiriwa tu na
utafutaji wa kweli za uchambuzi wa torati, tendo la Ndoa ni takatifu na ni
zawadi ya Mungu na Mungu ameamuru kuwa ndoa na ziheshimiwe Waebrania 13:4, Zaburi 51:5 ni wazi kabisa kuwa kwa mtazamo na
ufunuo wa kiagano jipya unamaanisha kuwa kwa kuwa sisi ni watoto wa Adamu
tunazaliwa na hali Fulani ndani yetu inayotusukuma kuasi hata wakati mwingine
mioyo yetu ikiwa haipendi, kwa hiyo kwa bidii ya kibinadamu hatuwezi kamwe
kuishinda dhambi bila msaada wa kiungu
Warumi 7:21-24 “Basi nimeona sheria hii, ya kuwa
kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya. Kwa maana
naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, lakini katika viungo vyangu naona
sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya
mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.Ole wangu, maskini
mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu.
Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu,
bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.” Kwa ufunuo Fulani Daudi
aliishia kusema aliumbwa katika hali ya uovu na alichukuliwa mimba hatiani,
lakini ni wazi alikuwa ni kama mtu anayejiuliza ilikuwaje hata akatenda uovu
ule mkubwa mtu ambaye moyo wake siku zote ulikuwa unalenga kumpendeza Mungu,
kwa hiyo Daudi ni kama alitaka kusema hili anachokisema Paulo Mtume kuwa iko
sheria ndani yetu ambayo inapingana na lile jema unalotaka kulitenda na ni kwa msaada wa Roho Mtakatifu tu na Kazi
aliyoifanya Yesu msalabani tutaweza kuwa huru kutoka katika vita vyetu vya
asili vinavyotupinga ndani kwa ndani kama nguvu ya “gravitation force” ama nia
ya mwili Warumi 7:24-25 “Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili
huu wa mauti? Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni
hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili
wangu sheria ya dhambi.” Na Warumi
8:1-3 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao
walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika
Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. Maana yale
yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili,
Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na
kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;”
Na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye hekima
0718990796