Mathayo 23:23-28. “Ole wenu waandishi na
Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini
mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo
imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Viongozi vipofu, wenye
kuchuja mbu na kumeza ngamia. Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa
kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na
kutokuwa na kiasi. Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili
nje yake nayo ipate kuwa safi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa
kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa
mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. Vivyo hivyo ninyi
nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na
maasi.”
Utangulizi:
Katika Mathayo 23:13-36, kuna mahubiri makali ya maonyo kutoka kwa Yesu
Kristo kuelekea kwa mafarisayo na viongozi wa dini waliokuweko katia nyakati
hizo, Neno ole ni sawa na onyo la kulaani au kuonya juu ya hukumu kubwa ya
Mungu kwa watu ambao maonyo hayo yanaelekezwa kwao,Krito alikemea vikali kwa
maneno mazito hata wakati mwingine akitumia neno vipofu na wanafaiki, Sababu
kubwa ni kuwa watu hawa walikuwa wakiwashawishi watu wafuate imani zao na
matiokeo yake ilikuwa ni kama kuwapeleka Jehanamu, wakikazia katika mafundisho
yao maswala yasiyo ya msingi wa Neno la Mungu na kuwaelekeza katika mapokeo ya
kibinadamu zaidi, huku wakipuuzia msingi wa sharia ya Mungu ambayo ni ADILI, REHEMA na IMANI
Kwa maana nyingine Kristo
alikasirishwa na Jinsi ambavyo viongozi wa kidini walishindwa kuwatafasiria
watu kile ambacho sheria ya Mungu inakipa kipaumbele na badala yake wakaanza
kukazia sharia za kidini zinazotokana na mapokeo, mikazo hiyo haikuwa dhambi
hata hivyo lakini ilikuwa si Muhimu, tabia mbaya waliyokuwa nayo Mafarisayo ilikuwa
ni mkazo wa utoaji wa zaka hususani kutoka katika mazao ambao kimsingi ulikuwa
ni urithi wa watumishi wa Mungu yaani walawi kwa wakati ule
Hesabu 18:20-24 “ Kisha Bwana akamwambia
Haruni, Wewe hutakuwa na urithi katika nchi yao, wala hutakuwa na fungu lo lote
kati yao; mimi ni fungu lako, na urithi wako, katika wana wa Israeli. Na wana
wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo
utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania. Mwanzo wa sasa wana wa Israeli wasikaribie hema
ya kukutania, wasije wakachukua dhambi, nao wakafa. Lakini Walawi watatumika
utumishi wa hema ya kukutania, nao watauchukua uovu wao; hii itakuwa amri ya
milele katika vizazi vyenu vyote, na kati ya wana wa Israeli hawatakuwa na
urithi. Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa
kwa Bwana, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba,
katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote.”
Kumbukumbu la torati 14:24-29 “Na njia
ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno
atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia
Bwana, Mungu wako; ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo
mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako; na zile fedha
zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai,
au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za
Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako; na Mlawi aliye ndani ya malango
yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe. Kila mwaka wa tatu,
mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani
ya malango yako; na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na
mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako,
na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako, akubarikie katika kazi
yote ya mkono wako uifanyayo.”
Unaweza kuona Mafarisayo na
viongozi wa dini walikazia sana kuhusiana na vifungu vinavyokazia kuhusu utoaji
wa zaka na kwa kweli kutokana na uroho walikazia utoaji wa zaka mpaka ya mnanaa,
Bizari na jira kwa faida zao, Mnanaa ni mmea wenye majani madogo madogo ya
kijani kwa kiingereza unaitwa Mint mmea huu unatumika kutibu magonjwa mbalimbali
kama Aleji, kuvimbiwa, maumivu ya tumbo na kutibu magonjwa mengine kama
kisonono, bawasiri na maumivu katika njia ya mkojo, mmea huu ulitumika kama
tiba kwa miaka elfu nyingi sana duniani,
Bizari kwa kiingereza Dill ni kiungo cha manjano BINZARI ambacho tutumika kuweka rangi
ya mchuzi na kuifanya iwe wa manjano au mwekundu na shughuli nyinmginezo za
kimapishi na ladha au harufu nzuri kwenye chakula pia hutumika kama tiba ya
magonjwa
Jira kwa kiingereza cummin ni vijijani
vyenye vitunda vidogo vidogo sana vya kijana ambavyo vikianikwa huwa na rangi
ya kijivu hivi ni viungo ambavyo huchanganywa na viungo vingine na kuleta ladha
maalumu katika kama pilau na mchuzi na kadhalika, jira ina uwezo wa kutibu
magonjwa mbalimbali ikiwepo, kusaidia kupunguza uzito, kuondoa msongo wa
mawazo, kuyeyusha mafuta hatarishi mwilini, kisukari, na magonjwa mengineyo.
Kwa ujumla vitu hivi vilikuwa vinahusiana na UPONYAJI, UZURI NA UNONO. Mafarisayo walisisitiza sana utoaji wa
zaka hata wa vimimea hivi vidogo vidogo kwa mkazo mkubwa sana kwa makusudi tu
wakuu wa dini wanufaike na utamu wa vyakula vyao na afya nzuri, Yesu hakuhukumu
utoaji wala utoaji wa zaka lakini kuna kitu nyuma ya mkazo wa viongozi wa dini
ambacho Kristo alikuwa anakikemea huku akiwakemea kwa kuacha kusisitiza maswala
ya msingi na ya muhimu
Mafarisayo waliacha kuweka mkazo
katika maswala makubwa ya msingi ya kiroho ambayo yangekuwa na faida kubwa kwa
watu kuliko yale ambayo yangekuwa na faida kubwa kwao waliacha maswala ya ADILI – Maswala ya kuhukumu kwa haki linapokuja swala la Mtu
Fulani amekosea, REHEMA – Kushindwa
kuwahurumia watu waliokosea na wale wanaohitaji msaada wa kibinadamu au walio
kwenye mateso, IMANI - Biblia ya kiingereza inatumia neno FAITHFULNESS ambalo linahusiana na UAMINIFU
Kuchuja mbu na kumeza ngamia
Wakati mwingine unaweza kudhani
kuwa shida hii ilikuwa ya mafarisayo pekee wakati wa Yesu Kristo la hasha hata
sasa ziko tabia Fulani zinazoweza kukemewa katika mtindo kama huu wa Masihi,
Leo hii pia wako watu wameacha mambo ya msingi na kukazia mambio ya siyio ya
msingi, kwa mfano sio vipaya kuhubiri uponyaji na mafanikio kwa vile ni wazi
kuwa watu wanahitaji mafanikio na uponyaji na hakuna jambo baya kama umasikini,
lakini ni ukweli ulio wazi kuwa injili inahitaji balansi, lazima wahubiri
wasisahau kuwa tunapaswa kuhubiri injili kamili, mara kadhaa unaweza kukuta
wahubiri wansisitiza juu ya utoaji lakini sababu kubwa ni kwaajili ya mahitaji
makubwa waliyo nayo, na wakati mwingine
kwaajili ya ubinafsi na kujinufaisha, tunaweza kuhubiri kuhusu uponyaji lakini
tusisahahu kuwa watu wanapaswa pia kuishi maisha matakatifu na kukumbushwa
kuhusu toba na kusamehewa dhambi na sio uponyaji pake yake
Zaburi 103:3 “Akusamehe maovu yako yote,
Akuponya magonjwa yako yote,” unaona wakati tunasisitiza kuhusu
Uponyaji ni lazima vile vile tukumbuke kusisitiza toba na msamaha wa dhambi,
itajkuwa ni hasara kubwa sana kama mtu ataponywa magonjwa yake yote lakini
hajawahi kuambia atubu dhambi au aishi maisha matakatifu, na sio sahihi
vilevile kuhubiri mafanikio na afya njema bila kusahau kuwa afya halisi
inapaswa kuanzia rohoni
3Yohana 1:3 “Mpenzi naomba ufanikiĆ„e katika
mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo”
lakini vilevile inaweza kuwa
makosa sana kuwahukumu watu kutokana na muonekano wao, au hali yao ya kifedha
au cheo chao na kuacha kuweka uthamani wa mtu katika mizani ya kiroho, aidha
kumekuweko na upendeleo katika utoaji wa haki, wako watu kwa sababu ya utajiri
wao wanaweza kupewa heshima Fulani na hata wakifanya dhambi wanaweza
kuhifadhiwa lakini wewe ambaye huna kitu ukadhalilishwa
Yakobo 2:1-5 “Ndugu zangu, imani ya Bwana
wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu. Maana
akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri;
kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; nanyi mkimstahi yule aliyevaa
mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule
maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu, je! Hamkufanya hitilafu
mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu? Ndugu zangu wapenzi,
sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na
warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao? ”
Unaona watu hawajali umuhimu
thamani ya nasfi na roho ambayo ni moja bali wanaangalia muonekano, wako watu
ambao wanaweza kuhukumu mambo pia kwa sababu tu wamesikia umbeya na uongo bila
hata kujithibitishia uhalisia wa mambo,
Pamoja na mahitaji ya watu wenye njaa, wenye uhitaji lazima tuonyeshe
rahema kwa watu kwa kuwasaidia kukutana na mahitaji yao. Mtu anaweza akaonekana
anahudhuria ibada na kutii kila kinachoamuriwa kanisani lakini maisha yake
binafsi yakawa na uchafu wa kila aina, je tunaishi vipi na waume, zetu, wake
zetu, watoto wetu, na je akilini tunawaza nini?
Wako watu wanahukumu wengine lakini akilini mwao ni waongo, wana hasira, wachonganishi wamejaa fitina
majungu na uzushi, kutaka sifa na kujitwalia utukufu, Yesu anachokitaka ni tuwe
wakamilifu pande zote hatupaswi kuchagua kipi cha kutii na kipi sio cha kutii
Mathayo 23:23-24 “Ole wenu waandishi na
Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini
mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo
imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Viongozi vipofu, wenye kuchuja
mbu na kumeza ngamia.”
Yesu anacho kitaka wetu ni kuwa
pamoja na mambo mengine tusiache kukazia maswala ya muhimu na kuyapa
kipaumbele, kama tunahubiri injili na kuichukia dhambi basi tuhakikishe kuwa
tunapambana na kile kitu, ukikataza ulevi kataza na tamaa, ukikataza uzinzi
kataza na hasira, haki haki, rehema rehema na adili ni adili, hatuwezi kuhubiri
uaminifu katika eneo Fulani na wakati huo huo eneo lingine tukawa
tumelilegezea, huko ni kuchuja mbu na kumeza ngamia, nusu utii ni sawa na
kutokutii haya ni machukizo sawa na namna Mungu alivyochukizwa na Sauli
alipomwambia aangamize kila kitu cha amaleki yeye akabakiza nab ado akawa anasisitiza kuwa ametii
1Samuel 15:1-23 “Wakati huo Samweli akamwambia Sauli, Bwana alinipeleka
nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na
maneno ya Bwana. Bwana wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo
hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo
walipopanda kutoka Misri. Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu
kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na
mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda. Ndipo Sauli
akawaita watu, akawahesabu huko Telemu, askari waliopanda farasi mia mbili
elfu, na watu wa Yuda kumi elfu. Sauli akaufikilia mji wa Amaleki, akauvizia
bondeni. Sauli akawaambia Wakeni, Haya! Enendeni zenu, mkashuke ili kujitenga
na Waamaleki, nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao; maana mliwatendea wana wa
Israeli mema, walipopanda kutoka Misri. Basi hao Wakeni wakaondoka, wakajitenga
na Waamaleki. Sauli akawapiga Waamaleki, toka Havila uendapo Shuri, unaokabili
Misri. Akamkamata Agagi, mfalme wa Waamaleki, yu hai, akawaangamiza hao watu
wote kwa upanga. Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika
kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote
kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa
kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa. Ndipo neno la Bwana likamjia
Samweli, kusema, Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi
nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika,
akamlilia Bwana usiku kucha. Samweli akaondoka asubuhi na mapema ili aonane na
Sauli; Samweli akaambiwa ya kwamba, Sauli alifika Karmeli, na tazama,
akajisimamishia ukumbusho, akageuka, akapita, akatelemkia Gilgali. Samweli
akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na Bwana, nimeitimiza amri
ya Bwana. Samweli akasema, Maana yake nini, basi, hiki kilio cha kondoo
masikioni mwangu, na huu mlio wa ng'ombe ninaousikia? Sauli akasema, Wamewaleta
kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng'ombe walio wazuri,
ili wawatoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa.
Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami nitakuambia neno aliloniambia Bwana
usiku huu. Naye akamwambia, Haya, sema. Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa
mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha kabila za Israeli?
Naye Bwana akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli. Kisha Bwana akakutuma
safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi,
upigane nao hata watakapoangamia. Mbona, basi, hukuitii sauti ya Bwana, bali
ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana? Sauli akamwambia
Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya Bwana, nami nimemleta Agagi, mfalme wa
Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa. Ila watu waliteka nyara,
kondoo na ng'ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe
dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, huko Gilgali. Naye Samweli akasema, je! Bwana
huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana?
Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa
kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.”
Ukiyajua hayo heri wewe
ukiyatenda!
Rev. Innocent Samuel Kamote