Mathayo 5:1-5 “Naye alipowaona makutano,
alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia; akafumbua
kinywa chake, akawafundisha, akisema, Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme
wa mbinguni ni wao. Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. Heri wenye
upole; Maana hao watairithi nchi.”
Utangulizi.
Nimekuwa kiongozi na Mchunjaji
kwa Muda mrefu sana nimemtumikia Mungu kwa karibu robo tatu ya maisha yangu
yote sasa, nimekutana na changamoto nyingi na za aijna mbalimbali, Pia nimewahi
kupigana vita za aina mbalimbali za kiroho na naweza kukiri wazi kuwa hakuna
vita nimewahi kushindwa kwa sababu wakati wote nilipopigana nalimtafuta Bwana
ili awe upande wangu kwanza kwa hiyo ushindi wangu umetokana na Bwana mwenyewe
kunipigania!, Moja ya changamoto kubwa kutoka kwa watu wanaonipiga vita katika
uongozi wangu ni pamoja na kunishutumu kuwa mimi sifai kwa sababu ni MPOLE sikuhuzunika lakini hili
lilinipa kutafakari kwani Upole ni sifa mbaya kwa mwanadamu? Au ni sifa Njema?
Hili lilinifanya nianze kurejea katika maandiko na kuanza kujifunza kwa kina na
mapana na marefu ili nipate kujua kuhusiana na UPOLE. Viongozi wakubwa sana katika maandiko wanaelezwa kuwa
walikuwa wapole akiwemo Musa ona katika Hesabu
12:3 “Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana
zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.” Unaona lakini
sio hivyo tu Yesu akitoa mwaliko wa watu wenye kuelemewa na changamoto
mbalimbali anajitaja mwenyewe kuwa ni mpole na mnyenyekevu wa Moyo unaweza
kuona katika Mathayo 11:28-29 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na
mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi
ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;” Upole ni nini hasa je ni sababu ya kulaumiwa?
Ni sifa mbaya? Ama ni sifa njema? Hili swala litupa nafasi ya kutafakari kwa
kina na mapana na marefu katika somo hili katika jina la Yesu Kristo amen!
Maana ya Upole!
Katika hutuba maarufu sana ya
Yesu Kristo inayojulikana kama Hutuba ya Mlimani, Yesu alifundisha pamoja na
mafundisho mengine mafundisho ya HERI kama
nane hivi ambazo kwa kiingereza zinaitwa Beatitudes ambalo maana yake ni “Supreme Blessedness” yaani mtu
aliyebarikiwa sana sasa katika moja ya sifa hizo za watu waliobarikiwa sana
mojawapo ni UPOLE kwa hiyo Mathayo 5:5 “Heri
wenye upole; Maana hao watairithi nchi.” Maana yake wamebarikiwa
sana wenye upole maana hao watairithi nchi kwa hiyo UPOLE ni Baraka UPOLE ni
neema ya Mungu ya ngazi ya juu sana, lakini ni lazima nan i muhimu kuelewa
maana na neno hilo UPOLE
Neno upole linalotumika katika
Kiswahili kwenye Biblia ya kiingereza linasomeka kama MEEK ambalo kwa ujumla linabeba maana tajiri sana ambazo kimsingi
zinaweza kukomba matunda yote ya roho yanayotajwa katika maandiko MEEK - MILD, SUBMISSIVE, MODERATE, QUITE,
GENTLE, LONG-SUFFERING, PATIENT. Maneno
hayo yote yanayozingumzia upole kama
MEEK katika unyambulisho wake yanatupa picha pana sana kuwa mtu mwenye
upole kwa vyovyote vile ni mtu mkamilivu na momavu na katika maswala ya kiroho
ni mtu wa ngazi ya juu sana kwani ameweza kubeba matunda mengi ya rohoni ona
maana hizo kwanza
MILD – MTARATIBU, SUBMISSIVE – MTIIFU, MNYENYEKEVU, MODERATE – MTU WA WASTANI
(KIASI), ULINGANIFU USAWA, QUITE MKAMILIFU, GENTLE – MUUNGWANA, LONG-SUFFERING
– MVUMILIFU, ASIYEKASIRIKA KWA HARAKA, PATIENCE – ALIYE NA SUBIRA.
Unaona kwa hiyo tunaposoma katika
kitabu cha Wagalatia 5:22-23 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu,
utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna
sheria.”
Aina hii ya upole Yakobo aliita
Upole wa hekima Yakobo 3: 13 “N'nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi
zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima”.
Aidha neno hili katika Biblia ya
kiyunani linatumika kama neno PRAUS au
PRAEIS ambalo tafasiri yake ni
MILD ikimaanisha mtu mwenye uwezo wa
kujishusha kwa Mungu na wanadamu, au mtu mwenye uwezo wa kutumia nguvu na
mamlaka lakini akawa na subira kwa faida ya wengine, Kimsingi hii ilikuwa sifa
kubwa sana ya viongozi wa kibiblia na hata mfalme Daudi alikuwa miongoni mwa
watu wa namna hata alipotafuta kuuawa na
Sauli aliyekuwa anamchukia sana yeye hakufanya haraka kumdhuru waola kujitakia
kisasi hata pale ambapo Mungu alimwambia kufanya hivyo yeye alisubiri wakati
muafaka wa Mungu hii ona
Zaburi 37:10-13 “Maana bado kitambo kidogo
asiye haki hatakuwapo, Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo. Bali wenye
upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani. Asiye haki hunuia
mabaya juu ya mwenye haki, Na kumsagia meno yake. Bwana atamcheka, Maana ameona
kwamba siku yake inakuja.”
Unaona kwa msingi huo ni vema
ikaeleweka wazi kuwa Upole sio udhaifu bali Nguvu za Mtu mwenye uwezo chini ya udhibiti wa Nguvu za Mungu, kwa hiyo
mtu Mpole ni mtu anayeachia mambo chini ya udhibiti wa Mungu, ili Mungu
mwenyewe achukue hatua za haki, ni mtu ambaye hajifikiri kuwa bora nje ya neema
ya Mungu, upole ni hali ya kufikiri kuwa nguvu zetu na mamlaka yetu ina mipaka
ya kufikiri katika Mungu kwa nia njema kuliko kuitikia haraka kwa hasira za
kibinadamu Yakobo 1:20 “kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu.”
Mtu mwenye upole hutembea katika neema ya Mungu na hanaga mpango wa kunia
makuu kuliko impasavyo kunia.
Warumi 12:3 “Kwa maana kwa neema niliyopewa
namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali
awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.”
Heri wenye upole!
Maana yake kuna amebarikiwa sana
Mtu mwenye upole hii maana yake ni kuwa kuna faida kubwa sana za upole kama
ifuata vyo:-
ü Watu wenye upole ni watu waliobarikiwa kwa
kiwango kikubwa Mathayo 5:5 “Heri wenye upole;
Maana hao watairithi nchi.” Hii maana yake ni nini maana yake ni
kuwa na uhusiano na Muumba wa mbingu na Nchi, urithi mtu huupata kutokwa kwa
yule eliyemzaa au aliyekuandikisha uupate kwa sababu ya wema wake mtu akiwa
mpole maana yake anafanana na Mungu ni mwana wa Mungu hivyo anastahili urithi,
Ni Mungu ndiye aliyeumba mbingu nan chi na hivyo kuwa mwanae kwa sababu ya
upole kwa msingi huo lazima tutarajie Baraka za Mungu hata pale atakapoiumba
mbingu mpya nan chi mpya Mungu atawarithisha watoto wake
ü Watu wenye upole hutetewa na Mungu Hesabu
12:1-9 “Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa
sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke
Mkushi. Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia?
Bwana akasikia maneno yao. Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi
ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi. Bwana akanena ghafula na Musa,
na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa
kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje. Bwana akashuka katika nguzo ya wingu
akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje
wote wawili. Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati
yenu, Mimi, Bwana, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto.
Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu
yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na
umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi
wangu, huyo Musa? Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake.”
ü Watu wenye upole hudumu muda mrefu katika
nafasi zao na katika maisha Zaburi 37:10-13 “Maana
bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, Utapaangalia mahali pake wala
hatakuwapo. Bali wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa
amani. Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki, Na kumsagia meno yake.
Bwana atamcheka, Maana ameona kwamba siku yake inakuja.” Unaona kama
unataka kudumu Muda mrefu uwe mwenye haki, kama watu wapole kuna stori moja ya
kuchekesha kuhusu Meno na Ulimi, siku moja ulimi ulimwambia Mungu kuwa
tafadhali umeniweka mimi katika wito wangu pamoja na meno na meno ni mgumu
kuliko mimi kwa hiyo mara kwa mara katika kutimiza wajibu wetu meno amekuwa
akinumiza na kuniacha na majeraha nikipona tena baada ya Muda meno hufanya
hivyo hivyo ndipo Mungu akamjibu meno kazi yenu ni ya muda tu lakini wewe ulimi
ni wa muda mrefu zaidi kuliko meno hivyo ni lazima ujifunze kuvumilia, baada ya
miaka 70 au 80 hivi ya maisha yenu uje unipe majibu, baada ya muda huo kupita
kumbe meno mengi yalioza na kung’oka lakini ulimi ulibaki, ni wazi kabisa kama
maandiko yasemavyo aggressive people shall not live longer but Mild people will
live more than normal , watu wakali
hawadumu lakini watu wapole hudumu, in the workplace the arrogant and powerful
seems to win but in the end they lose
alisema mtu mmoja kazini watu jeusi na wanaojiinua huonekana kama washindi
lakini mwishoni wanyenyekevu ndio wanaoshinda, Ni changamoto kubwa sana kuachia
mamlaka zetu na nguvu zetu katika mikono ya Mungu na kujinyenyekesha, tunaweza
kuona raja kwa kitambo kutumia mamlaka zetu, kufukuza watu, kumarisha watu lakini
ni ukweli ulio wazi kuwa hatima yake ni huzuni, hawafanikiwi katika lolote watu
jeuri hawana marafiki wala hata wakipata fedha hawatosheki, wanaweza kudhani
kuwa wanaumiliki ulimwengu lakini ni ukweli kuwa ulimwengu unawamiliki,
Mwanamke na mwanaume wanaojikweza na kutaka kuonyesha nguvu zao huishia katika
aibu na upweke hakuna mtu anaweza kuwa na urafiki na mtu jeuri!, wanawake
huvutiwa sana na mwanaume mpole. Mwaname mkali hawezi kufaidi lolote hata
katika ndoa yake! Mithali 22:24-25 “Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala
usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia
nafsi yako mtego.”
ü Upole unakaribisha uwepo wa Mungu Isaya
66:1-2 “Bwana asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha
enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna
gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani? Maana mkono wangu ndio
uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu
huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka,
atetemekaye asikiapo neno langu.” Uwepo wa Mungu unakaa na watu
wanyenyekevu wanyonge na wapole bila upole nafsi ya mwanadamu inakuwa katika
mgogoro wa ndani, inasababisha hasira, kuchanganyikiwa, uchungu, na kukosa
utulivu, Upole unaweka mambo sawa na
kupunguza mawimbi, unaleta utaratibu wakati wa machafuko unaponya nafsi na
kutiisha mawimbi, Lazima mwanadamu akumbuke kuwa yeye ni mavumbi, ukikumbuka
kuwa wewe ni udongo itakusaidia, Upole unaleta furaha na amani ya kweli, kama
Mungu akiwa na ghadhabu na hasira kama tulizonazo sisi kwa wengine tungekuwa
wapi leo? Watu wengine hata wakisikia masengenyo tu mahali wanakurupuka na kufanya maamuzi hata
bila kufanya uchunguzi wa kina na wa kutosha je Mungu anekuwa mwepesi wa hasira kama wewe
na mimi ingekuwaje ?
ü Upole ni alama ya ukomavu wa kiroho
Wagalatia 5:22-23 “Lakini tunda la Roho ni upendo,
furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya
mambo kama hayo hakuna sheria.” Hakuna jambo linachosha duniani kama
kuchunga wakristo wa Mwilini yaani wakristo ambao hawajakomaa kiroho au
waliodumaa, Paulo mtume alisikitishwa sana na Kanisa lililodumaa na la wakristo
wa mwilini kwani jamii hii ya wakristo wana taabu sana kuliko hata wapagani
kutokana na kufarakana na kugombana na kufanya mambo ya ajabu yanayotukanisha
ukristo 1Wakorintho 3:1-3 “Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na
watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na
watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa
kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasa ninyi
ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si
watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? ” unaona watu waliokomaa kiroho hawana muda
wa majungu, fitina na husuda na maswala mengine, UPOLE ni alama muhimu sana kwa
mtu aliyekomaa kiroho, lakini mtu wa tabia ya mwilini asiyekomaa kiroho hawezi
kuwa na utulivu, kwa sababu hana matunda ya rohoni!
Hitimisho:
Ni mmuhimu kuelewa kuwa tunaweza
kumuomba Mungu atupe upole kama jinsi ambavyo tunaomba Mambo mengine Yakobo 1:5 “Lakini
mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa
ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.” Ingawa Yakobo hapo anaelezea swala la kuomba Hekima ni muhimu
pia kujua kuwa Upole ni Hekima kwa hiyo tunapoomba Hekima tunaweza kupokea na
upokle ndani yake hekima ya kiungu ikoje? Yakobo
3:17-18 “Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi,
tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na
matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Na tunda la haki hupandwa katika
amani na wale wafanyao amani.” Kumbe tunaweza kuiomba Hekima hii
iliyojaaa amani, rehema, matendo mema na iko tayari kusikiliza kwa hiyo ni
lazima tumuombe Mungu atupe upole. Martin Luther King Alipingana na ubaguzi
uliokuwepo Marekani, alitaka watu wote wahesabike kuwa sana alifanya maandamano
ya amani hakuwahi kufanya vurugu wala kuruhusu wafuasi wake kufanya fujo
akitumia falsafa ya Mahatma Ghandi ya non-violence resistance, kupinga maswala
yasiyo haki bila kumwaga Damu, hii maana yake ni kuwa alikuwa Mpole Bwana na
ampe neema kila mmoja wetu kuwa mpole katika jina la Yesu Kristo, kwa hiyo
ieleweke wazi kuwa Upole sio udhaifu upole ni sifa kubwa na ya kipekee sana
katika uhusiano wetu na Mungu, hivyo wale wanaonishutumu kuwa mimi ni Mpole
sasa nimewaelewa vema asanteni!
Na Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni