1Samuel 15:1-3 “Wakati huo Samweli
akamwambia Sauli, Bwana alinipeleka nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake
Israeli; basi sasa, isikilize sauti na maneno ya Bwana. Bwana wa majeshi asema
hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi
walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. Basi sasa enda ukawapige
Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali
waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia
na punda.”
Utangulizi:
Mapema sana miaka mingi Mungu
alikuwa amemuahidi rafiki yake Abrahamu kuwa atampa nchi ya mkanaani, lakini
alimueleza wazi kuwa atayatimiza haya katika kizazi cha nne wakati huo uovu wa
wakanaani utakuwa umefikia kiwango cha juu ona
Mwanzo 15:13-16 “BWANA akamwambia Abramu,
Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake,
watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne. Hata na taifa
lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi. Lakini
wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema. Na kizazi
cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado.”
Unaona moja ya makabila ambayo
uovu wao ulikuwa umefikia kiwango ni pamoja na waamaleki ambao kimsingi Mungu
alikasirishwa nao kwa sababu ndio walikuwa wa kwanza kupinga na kusudi la Mungu
kwa kupingana ana kusudi la Mungu kwa kutaka kwiazuia wana wa Israel njiani ili
wasiweze kwenda katika nchi ya mkanaani ona
Kutoka 17:14 “BWANA akamwambia Musa, Andika
habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya
kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu.”
Mungu alikasirishwa na Amaleki na
alikusudia kuwafuta wasiwepo milele kwa sababu ya uovu wao na moja ilikuwa ni
kuwauzia wana wa Israel wasiende kwa amani katika nchi ya kanaani lakini pili
ni kwa kutokuwahurumia watu wanyonge waliokuwa wamechoka jangwani wagonjwa na
waliokuwa wamechoka jangwani
Kumbukumbu la Torati 25:17-19 “Kumbuka aliyokufanya
Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri; jinsi alivyokukuta katika njia,
akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako,
ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu. Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha
Bwana, Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo
Bwana, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini
ya mbingu; usisahau.”
Kwaajili ya hayo Mungu alikuwa
anataka kumbukumbu ya watu hawa wasiofaa iondolewe kabisa milele katika uso wa
ardhi na kwa bahati njema agizo hili alipewa mfalme Sauli ambaye kwa bahati
mbaya na kwa kukosa utii aliwabakiza kinyume na maagizo ya torati jambo
lililolata laana Mungu anapotupa agizo ni lazima yuhakikishe kuwa tunalitimiza
kwa usahihi na hatupaswi kuhurumia chochote kinachowekwa mbele yetu maandiko
yanasema amelaaniwa mtu yule aifanyaye kazi ya Mungu kwa ulegevu ona
Yeremia 48:10 10. “Na alaaniwe mtu afanyaye
kazi ya Bwana kwa ulegevu; na alaaniwe auzuiaye upanga wake usimwage damu.”
Mungu anachokitaka kwetu leo ni
kuhakikisha kuwa tunaangamiza kabisa kila kizuizi tunachokutana nacho kisibaki
katika kumbukumbu zetu kuwa tuna kitu tumebakiza hakikisha unafutilia mbali
kila kikwazo, kinachokukabili, iwe ni mitihani ya kidato cha pili au kidato cha
nne au cha sita amaa lolote linalokusibu hakikisha kuwa unatimiza wala
usishindwe wala usiuhurumia wala usibakize kama Sauli, leo ni siku yak o na
wiki hii ni wiki yako kuhakikisha kuwa unampiga mwamaleki sio kwa ulegevu bali
kwa bidii ukijua ya kuwa unamtumikia Mungu,
Warumi 12:11 “kwa bidii, si walegevu; mkiwa
na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;”
Kutokutii agizo la kumtumikia
Mungu na kufanya kinyume na maagizo yake kunaweza kutuleta katika wakati mgumu
wa kukataliwa kama Sauli na kurfananishwa na waasi au wachawi, Sauli alipoteza
nafasi ya kutimiza mapenzi ya Mungu alipofanya vile alivyotaka yeye,
1Samuel 15:7-11 “Sauli akawapiga Waamaleki,
toka Havila uendapo Shuri, unaokabili Misri. Akamkamata Agagi, mfalme wa
Waamaleki, yu hai, akawaangamiza hao watu wote kwa upanga. Lakini Sauli na watu
wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na
vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali
kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho
walichokiangamiza kabisa. Ndipo neno la Bwana likamjia Samweli, kusema, Najuta
kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala
hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia Bwana usiku kucha.”
Leo hii Mungu anamtuma kila mmoja
kwenda kuyatimiza mapenzui yake na kuhakikisha kuwa anaangamiza kila kikwazo
kinachozuia mafanikio yake kwa asilimia 100, Na tukifanya hivyo Mungu
hatasikitika badala yake atatufurahia kwani tunatimiza mapenzi yake kupiia kila
kilichoko moyoni mwake ambacho kimeandikwa katika neno lake weka bidii katika
kila ulifanyalo ukijua ya kuwa unayatenda mapenzi ya Mungu, soma kwa bidii,
fanya kazi kwa bidii, acha majungu, acha unafiki, acha kuigiza, kila mmoja na
amtangulize Mungu mbele na bwana atampa neema kila mmoja wetu na kumfanikisha
katika jina la Yesu Amen
Na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye hekima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni