Amini usiamini mpenzi
kama kuna jambo la msingi na la muhimu Duniani ambalo mkristo anaweza kulifanya
ni swala la kuabudu, Hili ni jambo ambalo linaweza kufanywa na Mkristo Binafsi au na wenzake kuinuia juu
mioyo yao na kumuhimidi Mungu wa
mbinguni, Kuabudu ndio kiini kikuu cha kuweko kwa mwanadamu, Ni jambo ambalo
liko katika Hisia, moyo, mawazo na shauku ya mwanadamu, Hakuna mahali duniani
ambako hakuna binadamu asiye na kiu au shauku ya kuabudu hali hii ni shauku ya
wanadamu ya kimaumbile kujibu hisia za upendo wa Mungu alionao kwa mwanadamu
Kumuabudu Mungu
na kumuhimidi Yeye na kujitoa kwake kunainua juu uwezo wa mkristo na mwanadamu
kujimimina kihisia na kufurahia uhusiano wake na Mungu, kila mkristo ni lazima akubaliane
nami kuwa kuabuni ni muhimu na ni lazima, Hakuna kanisa linaloweza kudumu kama
halina ibada ya kweli hivyo kuabu ni kwa
muhimu kwa uhai wa kanisa na mwandamu. Hata hivyo kwa kuwa kila binadamu ana
mipaka namna tunavyoweza kumuabudu Mungu inategemeana sana na jinsi Mungu
anavojifunua kwetu.
Kuabudu ni njia ya
neema kubwa sana ya msaada ulio juu sana wa mwanadamu, wana saikolojia
wanakubali kuwa watu wengi wanaoishi bila kuabudu na wale wenye kuabudu
wanatofauti kubwa sana ya kustahimili migandamizo ya masumbufu ya maisha “stress” kwamaana kuwa wanaoabudu
hupunguza kwa kiwango kikubwa kuliko wasioabudu aidha tunapoabudu Roho Mtakatifu
hutuunganisha na ndugu zetu na jamaa zetu katika Kristo katika ulimwengu wa
roho kumuabudu Mungu mmoja aliyejifunua kwetu
Somo hili basi ni
la muhimu kwani litakuwa likikupa maelekezo
ni namna gani tunaweza kumuabudu Mungu na kuchukuliana na mzingira ya
kumuabudu Mungu ikiwemo nafasi ya Muziki katika kuabudu na vionjo vingine mbalimbali
katika kukamilisha swala zima la kuabudu fuatana nami basi Mchungaji Innocent
Kamote katika uchambuzi wa somo hili Elimu kuhusu kuabudu Theology of wortship,
Maombi yangu ni kuwa somo hili litakusaidia kukuweka karibu katika mahusiano
yako na Mungu na wengine na ni maombi yangu pia kuwa utakapojifunza somo hili
utakuwa ni msaada mkubwa sana kwa wengine na katika makanisa ya Mungu katika
swala zima linalohusu kuabudu na kusababisha waweze kuwa na ukaribu sana na Baba
yetu wa mbinguni kupitia kuabudu, Mungu akubariki
SURA YA KWANZA KUABUDU NI NINI
Kwa kuwa kuabudu ni swala muhimu sana kwa katika
maisha ya mkristo na uhai wa kanisa asili yake ni lazima ikaeleweka kwani kuna
maelezo mengi sana kuhusu kuabudu, na kila iitwapo leo maelezo zaidi yanazidi
kutolewa, lakini kupata Maelezo yenye kutosheleza kwa ukamilifu sio kitu
rahisi, Hata ingawaje wengi wanaabudu na viongozi wa ibada wanaongoza kuabudu
lakini hawajawahi kujaribu kuelezea kwa wazi kwa watu maana yake ni nini?
Hakuna sababu za maana za kuelezea Kuhusu
uzoefu wa kuabudu ni ujuzi wa kiroho ni
kuingia katika mawasiliano ya kiroho na Mungu aliye juu sana uhusiano huo kamwe
hauwezi kuelezeka kwa maneno au kanuni za kawaida vyovyote iwavyo kuabudu
kutakuwa na maana kama mwabudu atakuwa na ufahamu wa asili ya kuabudu
1.
MAANA YA KUABUDU.
Kuabudu maana yake hasa inatokana na lile neno linalotokana na Kiingereza Worship
linatokana na neno la zamani sana la kiingereza cha kizamani likisomeka
kama Worthship au weorthscipe ambalo ni muunganao wa
maneno mawili worth na Ship na katika
matumizi ndipo likaweko neno worship
ambalo maana yeke ni kustahiliisha
au kukipa kitu uthamani, hivyo kuabudu ni kustahiliisha, au kutoa thamani,
kutukuza,kuhimidi na hili linafanyika kumuelekea Mungu kwani yeye ni mfalme
mkuu, ni Muumba wetu ni Baba ni kila
kitu Zaburi 95;1-7
Mtakatifu
Augustino alisema hivi “Thou hast made us, O God, and our hearts are restless
until they find rest in Thee.” Kwamba ingawa umetuumba sisi ee Mungu mioyo yetu
haipati utulivu mpaka tupate pumziko katika wewe. Kuabudu kwa kiibarania kunaelezwa kupitia neno “Shahah” hii ni hali ya kujitoa
wewe mwenyewe kwa Mungu kwa yale
aliyoyafanya , Kwa kawaida Mwanadamu
aliumbwa awe na uhusiano na Mungu kwa mfano wa Mungu hivyo iko kiu ndani ya
Binadamu ya kuabudu lakini uhuru wa kuchagua
alionao mwanadamu ndio unaomuongoza kuchagua matendo maovu. Kuabudu ni kumtumikia
Mungu ni kukubali yeye awe Bwana nasi watumwa wake Kutoka 3;11-12 kusudi kubwa
la Mungu kutuokoa na kuwaokoa Israel ni ili wapete kumuabudu Matendo 7;6-7 kila
mtu aliyeokolewa hawezi kuishi bila Ibada, Ibada ni njaa au kiu inayojitokeza
ndani ya mwanadamu kujisikia kuwa na ushirika na Mungu, kiu hii au njaa hii
hutimizwa pale tu tunapomfikia Mungu na tunapopata muda wa kuwa Naye.Katika
uwepo wake kuna ukamilifu wa Furaha Zaburi 16;11 Kwa msingi huo basi kama
katika Kanisa la Mungu hatusikii uwepo wake kuna uwezekano wa kuweko hitilafu
katika kuabudu kwetu yaani inatisha
jinsi gani?
2.
MAANA
YA KUABUDU KIBIBLIA
Usomaji wa Biblia ni moja ya njia ya
kupata picha itakayotuongezea ufahamu kuhusu kuabudu, Kuna Maandiko mengi katika Biblia na maneno yanayotafasiriwa
kama kuabudu, lakini maneno ya asili yahusuyo kuabudu katika Biblia yanatupa mwanga zaidi na neno
la Kiebrania Shahah hutumika kuelezea mtazamo wa akili na mwili
katika kuabudu ambako ni kujitoa kwa ukamilifu kwa Mungu Warumi 12;1. Kwa
kiyunani tuna neno Proskuneo ambalo maana yake ni kupiga busu
kiss, kuibusu mikono, uso, au kuinama hata chini kwa paji la uso ambalo kwa maana
nzuri ni kujitoa kikamilifu Martin Luther alisema “kuwa na Mungu ni kumuabudu
yeye”
Mungu alituumba kwa kusudi la kumuabudu yeye Ufunuo 4;11
inaonyesha kuwa tuliumbwa kwa kusudi lake, Ni mapenzi ya Mungu kutaka
kuwasiliana na kila mmoja na kujifunua kwake Biblia inaonyesha kuwa alijifunua
kwa namna nyingi Warumi 1;20,Ufunuo 4;11,2Timotheo 2;3-16, Warumi 8;16,Yohana
1;17-18 Mungu anataka kabisa tumuabudu yeye na anahitaji mwitikio wa kila mmoja
ni sehemu hiyo basi ya mwitikio wa Mwanadamu ndio unaopelekea kuhimidi,
kutukuza, kushukuru, kuadhimisha, n.k. Mtu anapomuomba Mungu au kupeleka
malalamiko yake kwa Mungu anawasiliana na Mungu lakini sio ibada ya kweli Mungu
anatafuta watu watakaomuabudu katika Roho na kweli Yohana 4;23-24.
SURA YA PILI UMUHIMU WA KUABUDU
Kama kuna jambo la Muhimu sana duniani ambalo
mwanadamu na kanisa wanaweza kulifanya basi ni kuabudu amini usiamini Kama kuna
jambo la muhimu ambalo ni la muhimu mkristo anaweza kulifanya basi ni kumuinua
Mungu juu yaani kumuabudu kama alivyowahi kusema askofu mkuu William Temple, wa
kanisa la Presbeterians, “Kumuabudu Mungu, kumsifu, kumuhimidi,
kumwadhimisha ndio njia ya juu kabisa ya
mkristo ya uhusiano kwa Mungu” lakini kuabudu pia ni zaidi ya swala hilo kwani
kuna faida nyingi zipatikanazo kupitia kuabudu Faida hizo ni zipi hapa ziko
kadhaa
Kuabudu
kunaimarisha umoja wetu na Mungu
Kwa kawaida
mwanadamu anapokuwa mbali na Mungu anakuwa mpweke na mnyonge na anakuwa hana furaha, kuasi kwake kunaleta
hatia na misiba moyoni na anakuwa hana amani ya kweli na kwa hivyo anakuwa na kiu ya kuungana na
Mungu na wanapotaka kufanya vizuri wanashindwa (Warumi 7;19) Njia pekee ya
kumsaidia mwanadamu kutoka katika hali
hizo ni kuabudu, kwa kadiri mtu anavyomkaribia Mungu ndivyo unavyojiona kuwa hufai na unajielewa
kuwa jinsi usivyomtii na kuwa mbali naye na kwa kuwa hupendi kuwa mbali
naye unatubu anakusamehe na unapata amani Isaya 6;1-8 Kutengwa na
Mungu ni adhabu kubwa sana kuliko zote duniani Mwanzo 4;12-14.na tatizo kubwa
tulilo nalo ni kuwa watu wengi hawana uhusiano mzuri na Mungu.
Kuabudu
kunakamilisha hitaji la kushirikiana na wengine.
Kama mwanadamu alivyo na kiu ya kuwa
na ushirika na Mungu hali kadhalika ndivyo pia anavyihitaji ushirika na wengine , mwanadamu aliumbwa kwa ajili ya ushirika na wengine “Human Being is a Social being” Mwanzo
2;18 hivyo kuna hali ya kuwahitaji wengine
na kuwa sehemu ya kundi hitaji
hili linaweza kutimizwa kwa ibada za pamoja katika Kanisa , familia,majirani,
kukutana pamoja kushirikiana, kutiana moyo kuomba na kusifu pamoja ,kusikiliza
mahubiri na kuombeana Wakolosai 3;16-17,WEaefeso 5;19-21
Kuabudu
kunatoa maana ya maisha na kusudi la kuishi.
Maisha hayana maana
kama hatujui kwa nini tunaishi, Mwanadamu siku zote ana hamu ya kujua yeye ni
nani? asili yake ni wapi? Ametoka wapi?na hatima yake ni nini?nani ameniumba
n.k. Zaburi 8;3-9, Tunapomuabudu Mungu ndipo ukweli kuhusu maana na kusudi
la la sisi kuishi linatiririka, sisi tu watu wake na kondoo za
malisho yake yeye ni Mchungaji wetu, na
kuwa ni Bwana tunapaswa kumtumikia Mungu na kuwa siku moja tutakuwa naye kweli hizi
zote zimejificha katika kuabudu
Kuabudu
kunatusaidia kutambua mipaka Yetu.
Kuabudu kunamfanya mwanadamu kutambua
mipaka yake, mwanadamu anapomuabudu mwenyezi Mungu wa milele anapata kujitambua jinsi alivyo dhaifu, na
kuwa ni wa Mudamfupi tu hapa duniani, na kuwa anamuhitaji Mungu na kuwa Bila
msaada wa Mungu hatuwezi na kuwa bila yeye hatuishi Mathayo 4;3-4, Hivyo
hatuwezi kujitegemea bali tunamtegemea Yeye hili tunaweza kulitambua kupitia
kuabudu
Kuabudu
kunatusaidia kupata majibu ya matatizo yetu katika maisha
Maisha yana matatizo
mengi sana na ni wachache tu wana weza kuyaepuka, Magonjwa, hali za kukata
tama, mishituko, kuudhiwa, huzuni, hatia ya dhambi, uovu, Migandamizo na
misongo ya mawazo n.k. hii ni mizigo ya kawaida katika maisha Yesu alitoa
mwaliko kuwa njooni kwangu ninyi nyote wenye kulemewa na mizigo nami
nitawapumzisha Mathayo 11;28 ni kwa kuabudu tu
tunaweza kuona tunapata faraja na kutiwa nguvu, wengi wanaokwenda
ibadani na mizigo wanatoka wakiwa wepesi na wenye amani na Furaha Muujiza wa
kumuabudu unachukua nafasi 1Samuel 1;6-20, Isaya 40;28-31 Kuna majibu ya maisha
katika kuabudu hali ngumu zinazo tuzunguka
na matatizo tuliyonayo yanaweza kupata ufumbuzi kupitia kuabudu 1Samuel
30;1-18.
Kuabudu
kunatupa nguvu za kuangusha ngome na vifungo vya adui.
Shetani ni adui
yetu mkuu na siku zote anatafuta kutushambulia huku akituzingira kwa namna
mbalimbali na kwa ngome nzito siri kuu ya ngome zake na mashambulizi yake
kushindwa ni kuabudu Matendo 4;14-31, Matendo 16;19-31.
Kuabudu Kunatupa
nafasi ya kupokea maelekezo au wito kwa utumishi.
Matendo
13;1-3 Ibadani ndipo mahali ambapo mwanadamu anaweza kupokea maelekezo
mbalimbali na nguvu za wito kwa utumishi, hapa tunakuwa na nafasi ya kupata
maelekezo kutoka kwa Mungu kupitia Roho wake Mtakatifu, kuzungumza na mioyo
yetu au akili zetu au kupitia mahubiri ya Neno la Mungu, unabii, nyimbo, maombi
n.k hapo ndipo hali za kumuinua Mungu hujitokeza na kiu ya kumtumikia
inahuishwa
SURA YA TATU MISINGI YA KUABUDU
Kuabudu kwa kweli lazima kuwe na misingi,
misingi hii ni sifa za kuabudu Kikristo ili ibainike kuwa tunamuabudu nani ni
muhimu basi kujifunza Misingi hii
1.
Kuabudu
kwa haki Lazima kumlenge Mungu
Hapa jambo la
msingi kwanza halijengwi ni namna gani tunaabudu lakini nani tunamuabudu ni
swali la msingi sana hata kabla ya kuangalia ni namna gani tunaabudu ni lazima
tujiulize nani tunamwabudu? Wote tutakubaliana nami kuwa katika kila jamii kuna
nguvu ambayo inaaminika kuwa iko juu ya mwanadamu na ina nguvu, hekima na uweza
kuliko tulivyo wanadamu na nguvu hii ina majina tofauti tofauti nguvu hii huitwa
Mungu, Mungu huyu amejifunua kwa wanadamu kwa njia nyingi na kwa namna tofauti
Lakini Biblia pekee ndio kitabu kilicho kitakatifu kuliko vyote na kinamfunua
Mungu kwa viwango halisi vyenye kutosheleza kiu ya mwanadamu ya kuabudu na
kupata thawabu kutoka kwa Mungu
Katika Zaburi
19;1-2 Tunaona Mungu akijifunua ukuu wake katika nguvu kubwa ya asili kama Radi
na mtiririko mzima wa kupambazuka kwa jua na machweo ya jua
Katika Zaburi
119;130 tunaona kwamba Mungu ame zungumza na wanadamu kupitia Neno lake kwa njia rahisi
Mungu pia anazungumza moja kwa moja kupitia mioyo yetu , katika Yohana 6;44 Yesu
alisema mtu hawezi kuja kwangu asipokuwa
amevutwa na Baba sauti hii yenye kuvuta ni sauti ya moyoni kwa njia nyingine
ndiye anayetufanya tuwe na ujuzi kumuhusu, tunahisi nguvu zake, upendo wake na
kwa msingi huo ibada ya kweli huchochewa na Mungu mwenyewe ndani yetu kupitia
Roho wake Mtakatifu kwa hiyo kile ambacho Mungu hukifunua katika mioyo yetu
hukubaliana na kile alichokifunua mwenyewe katika Biblia, katika uumbaji na
katika Maisha ya Yesu Kristo,Mungu hujifunua kama
a. Ni
Muumba wetu – Anastahili heshima na adhama Zaburi 139-15,8;3-4 ni kimbilio letu
na usalama wetu kwa hivyo tunapaswa kumtegemea.
b. Ni
wa kutumainiwa Zaburi 46
c. Ni
Mfalme wetu wa haki kwa hiyo anastahili kusifiwa Zaburi ya 47
d. Ni
baba yetu wa Mbinguni kwa hiyo anastahili upendo wetu na utii wetu Mathayo
6;32-33
Kwa msingi huo basi
kila kurasa katika Biblia zinatuonyesha ubora wa Mungu kwetu jinsi alivyo mkuu,
Kumuabudu pekee ndio muitikio wetu kwa kadiri anavyojifunua kwetu, Mitazamo
yetu na tabia zetu tunazipata kutoka kwake Yeye hutamani pendo lake limiminike
ndani yetu na ya kuwa tumuabudu ndio maana Yohana anasema tunampenda kwa sababu
alitupenda kwanza 1Yohana 4;19 na Zaburi ya 145 inafunua jinsi Mungu alivyo kwa
maneno haya yafuatayo;-
Ni mwenye kujali
Ni wa Rehema
Anataka kutusaidia
Anataka tuwe na furaha
Anaweza kukutana na
mahitaji yetu yote
Yuko wakati wote
Anasamehe
Ni mwema kwetu
Anapatikana wakati wote
Ni wa haki
Baada ya kujifunza jinsi Mungu alivyo mwema na anavyo tujali
mwandishi wa zaburi ya 8 anahoji upendo wa Mungu kwa mwanadamu kwa kusema
Mwanadamu ni nani hata umkumbuke? Na mwana wa Binadamu hata umwangalie sasa ni
muhimu kuona kuwa wale wanaomuheshimu na kumuabudu wana ahueni tofauti na wale
wasiomuabudu na kumuheshimu wao wanaitwa wapumbavu kwa sababu hawana kimbilio
wala msaada wakati wa mateso Zaburi 46;1-3, lakini wale wasioamini katika Mungu
huitwa wapumbavu Zaburi 53;1-3.
YEYE ASIYEMFUATA MUNGU
|
YEYE ANAYE MFUATA MUNGU
|
Hana
amani Isaya 57;20-21
|
Amebarikiwa
kwa amani Warumi 5;1
|
Amepungukiwa
na ufahamu wa kweli Matendo 28;26-27
|
Ana
uhakika wa Sauti ya Mungu Yohana 10;2-5
|
Amedanganyika
Yeremia 17;9
|
Anajulikana
kwa uaminifu kwa Mungu 2Koritho 1;12 Kolosai 3;9-10
|
Amejaa
dhambi Efeso 2;1
|
Huru
mbali na dhambi 1Yohana 1;9,Yakobo 3;17-18
|
Anangojewa
na kifo cha milele Efeso 2;1
|
Anatunukiwa
uzima wa milele Yohana 3; 36
|
2.
Kuabudu
ni lazima kuwe katika Roho na kweli Yohana 4;23-24 “Spiritual”
Tunapozungumzia
kuabudu katika Roho na kweli maana yake kuu hasa ni kwamba lazima kuabudu kwetu
kwanza kutokee ndani sana ya moyo, Ibada ni swala la moyo na ufahamu, pia
katika uwepo na upako wa Roho Mtakatifu Kwa kuwa Roho wa Mungu anaishi ndani
yetu Yohana 14;16-17 Roho hutenda kazi katika ibada hivyo ni muhimu akahusika
akaachiwa atuelekeze namna tunavyoweza kubudu.
Katika kweli ni
nini? Ni neno la Mungu Yohana 17;17 , Mathayo 26;27-30, Pia Kristo ndiye kweli
Yohana 14;6 hivyo ibada ya kweli lazima ifanyike sawa na Neno la Mungu kupitia
Yesu Kristo au sawa na injili ya Yesu Kristo Marko 7;6-7
3.
Kuabudu
ni Lazima kuanze na mtu Binafsi
“Personal”
Msingi mwingine wa
Ibada ya kweli ya Kikristo ni kwa mtu moja mmoja Binafsi, uhusiano wa Mungu kwa
mwanadamu hauanzi na mkumbo au kundi la watu bali na mtu mmoja mmoja Binafsi
anakuwa na uhusiano na Mungu “It is a direct Personal Encounter” Mwanzo 12;7,8,
5;24, Nehemia 1;1-10, Hata hivyo ingawa kuabudu ni swala Binafsi hii haina maana kuwa hatupaswi kushirikiana
na wengine katika ibada Mithali 18;1
4.
Kuabudu
ni lazima kuwe kwa ushirikiano Waebrania 10;25 “ Corporate”
Msingi wa kuabudu hautoshi tu kuwa kwa
mtu mmoja mmoja binafsi lakini pia kwa
ushirikiano, uhusiano Binafsi na Mungu
katika kusamehewa dhambi hili ni jambo la kwanza ambalo ndilo linalotuunganisha katika mwili
wa Kristo Warumi 12;5, 1Koritho 12;12-13 hivyo ingawa kuabudu binafsi ni muhimu lakini kuabudu pamoja nako
ni kwa muhimu zaidi
5.
Kuabudu
ni lazima kuwe kwa kumaanisha “sincere”
Kwa kuwa ibada ya Kikristo inahusu mtu
na watu ni rahisi kufanya ibada kwa
kusudi la kuwapendezesha watu, kwa kuwa wana macho na masikio na hivyo kunaweza kutolewa maombi, shuhuda,
Nyimbo na neno ambalo msingi wake ni
kuwapendeza watu, Ibada ya jinsi hii sio ibada ya kumaanisha au makini ibada za jinsi hii kwa mujibu wa mafundisho
ya Yesu zitakupatia thawabu yako kutoka kwa watu hapa hapa Duniani Lakini mbinguni ukawa umekataliwa
Jambo lolote lile linalofanywa katika ibada kwa kusudi la kuwapendezesha watu
halina thawabu mbinguni Mathayo 6;16-18,6;1-4,5-8 Ibada ni lazima ilenge
kupelekwa kwa Mungu neno Sincere maana yake pasipo kuigiza, ya kweli na ya
uaminifu hizi ndizo ibada zinazo mpendeza Mungu
6.
Kuabudu
ni lazima kuwe kwa unyenyekevu “Humble”
Ibada ya kweli ya Kikristo ni lazima
ijengwe au ifanyike katika msingi wa unyenyekevu, kwenda mbele za Mungu huku
tuna kiburi au tunajihesabia haki au tusio na moyo wa unyenyekevu kutaifanya
ibada yetu kuwa ibada isiyo na faida
Luka 18;9-14 Unapokwenda ibadani ubnapata Nafasi ya kujiona kama vile Mungu
anavyokuona hivyo utajiona jinsi ulivyo
na mapungufu na utakuwa mnyenyekevu Kumbuka Mungu anasema katika Isaya 57;15
Kuwa Mungu hukaa na mtu mwenye kupondeka au mnyenyekevu aliyetubu,Isaya 66;2
anayetetemeka.
7.
Kuabudu
ni lazima kuwe kwa uhuru “Free & Spontaneous”
Uhuru huu hauna maana kuwa mtu
anajifanya vyovyote atakavyo bila kufuata mpango, Lazima kuwe na utaratibu,
Lakini usiwe utaratibu chuma Bali utaratibu ambao utaruhusu Roho kutupeleka
atakako ikiwa ni pamoja na hisia zetu kama zilivyo 2Samuel 12-16,1Nyakati 15; 1-29,
Kuna wakati ambapo mtu anaweza kuabudu na kuchukuliwa katika uwepo wa Mungu
kiasi cha kushangaza lakini hata katika hali hiyo mtu hatakiwi kuingiliwa
anatakiwa kuachiwa huru
8.
Kuabudu
lazima kuambatane na kuishi
Kuabudu kwa mkristo
ni lazima kuambatane na kuishi sawa na Mungu anavyotaka, Ibada haiwezi
kukubalika kama hatuishi sawa na Neno Amosi 5; 21-24, ili ibada zetu zikubalike
hatuna budi kuishi au sawa na neno la Mungu ndipo tutapata kibali Mathayo 5;23-24
si kila mtu asemaye Bwana Bwana atakayeingia katika ufalme wa Mungu Bali kwa
kuishi au kutenda Mathayo 7;21 Hivyo
jambo lolote au yoyote tufanyayo tuyafanye kwa utukufu wa Mungu.
9.
Kuabudu
ni lazima kuwe kwa gharama.
Ni
muhimu kufahamu kuwa kuabudu ni gharama na Baraka za kweli za kiroho
hazipatikani kirahisi hivi hivi, wakati mwingine kuabudu kutatupelekea
kugharimika kwa maisha yetu, mali zetu au watoto wetu, Nyakati za agano la kale
ili kumuabudu Mungu watu walihusisha ibada zao na utoaji mkuu wa vitu
vilivyonona yaani wanyama na dhabihu Mwanzo 4;3-4, hakuna ibada inayoweza
kukubalika na Mungu isiyo na gharama, Kaini alileta sehemu zilizonona na Mungu
akakubali ibada yake, Nuhu aliposhuka salama kutoka katika safina iliyookoa
maisha yake na wanawe alimtolea bwana ibada ya thamani Mwanzo 9;18-22, Angalia
maisha ya Ibrahimu tangu alipoitwa na Mungu alikuwa Muabudu aliyejenga
madhabahu kila wakati na juu ya madhabahu hiyo alitoa kitu cha thamani dhabihu
Mwanzo 12;8,15;1-21. Daudi mfalme mkuu sana katika Israel alikuwa muabudu Mungu
aliyehakikisha anamuabudu Mungu kwa kila kitu chenya thamani 1Nyakati 11;15-19,
2Samuel23;15-17 alimtolea Mungu maji ya thamani sana yaliyogharimu maisha ya
watu, alikataa kupewa kiwanja Bure kwaajili ya kujenga nyumba ya kuabudia
2Samuel 24;24 “Wala sitamtolea BWANA, Mungu wangu sadaka za kuteketezwa
nisizozigharimia.” Kama tunataka kuona ibada zenye Baraka ni muhimu kwetu
tukakubali kugharimika kwaajili ya ibada hizo, Kujitoa, kuombea na kumpa Mungu
vitu vya thamani vya hali ya juu ili Baraka za Kiroho na za kimwili ziweze kuwa
pamoja nasi.
SURA YA NNE MATOKEO YA KUABUDU
Tunaishi katika ulimwengu ambao umejaa
matatizo mengi, vita, mafarakano, n.k na kadiri tunavyoendelea kuweko hapa
ulimwenguni ndivyo wakati mwingine tunavyochanganyikiwa zaidi na wakati
mwingine tunaweza hata kupoteza malengo yetu katika maisha kwa nini kwa sababu
ulimwengu pasipo Mungu unakuwa ulimwengu
wa kisanii usio na faraja na ulimwengu huu tulio nao wanaoishi ndani yake
hawajali kitu kuhusu Mungu wala hawampendi wala hawana hamu kuhusu mambo ya
Mungu, ili ndoto zetu katika maisha ziweze kutimia Basi njia ya kuabudu ni ya
muhimu sana katika maisha ya mwanadamu hili ndilo hitaji kubwa zaidi la
mwanadamu
Tunapoabudu wazo kuhusu Mungu hujengeka
Kadiri watu wanavyoabudu ndivyo wazo
kuhusu Mungu linajengeka, Mungu anatukumbusha kuhusu pendo lake kwetu,
utakatifu wake, na nguvu, tunakumbuka ukuu wake na kuona kuwa kumbe anaweza
kukaribiwa, hatujisiikii upweke, tunakuwa na matumaini kwa sababu ana nguvu za
kutosha kukutana na mahitaji yetu, hofu zetu zinakuwa kama ujinga tu kwa sababu
anatupenda na anatujali tunaanza kujitambua kuwa sisi ni watoto wake na raia wa
Mbinguni na kuwa Mungu ndiye mfalme wetu, Mungu huyaona mapito yetu kama njia
ya kujifunza na kukomaa anaziona huzuni zetu kama njia ya kumtafuta yeye,
anayaona magonjwa yetu kama njia ya kuonyesha pendo lake kwetu tunarejezwa
katika uhalisia kuwa Mungu ni pendo na kuwa anatuelewa na ni masaada ulio
karibu
Kuabudu sio jambo la kupuuuzia hata kidogo
ni jambo lenye manufaa na lenye kuleta mtiririko thabiti Biblia imejaa mifano
mingi sana kuhusu kuabudu na matokeo ya kuabudu swala hili limeleta matokeo
makubwa kwa watu binafsi na kwa kanisa kuabudu sio kupoteza muda ni lazima watu
wajijengee mazingira ya kupenda kuabudu
·
Muhubiri maarufu Duniani John Wesley alipenda
sana kuabudu na alipata mafanikio makubwa sana na kwa sababu hiyo yeye na familia yao walipata mafanikio makubwa kaka
yake Charles Weslay ni moja ya watunzi wa nyimbo nyingi sana katika tenzi za
Rohoni na mama yao aliwafundisha kuimba na kumuabudu Mungu
·
Muhubiri maarufu duniani Benny Hinny hufanya maombezi na huduma yake huambatana na
miujiza mikubwa kwani hafanyi maombezi bila kuabudu hupenda sana kuabudu
·
Muhubiri Wilifred Lay wa Mombasa nchini Kenya
miaka ya nyuma alikuwa na washirika 20,000 waliokuwa wakiabudu pamoja katika
mji huu amabao ni mji wa kiislamu amefanikiwa kwa sababu ya kuwa na ibada nzuri za kusifu na kuabudu kila
jumapili jioni na alilipa jina kanisa
lake Jesus cerebration center JCC
·
Miaka mingi nyuma huko Ufilipino watu waliabudu
na kufunga na kuomba kwa kusudi la kutafuta uso wa Mungu moto mkubwa uliwaka juu ya kanisa
lao na watu wengi wakajua kuwa labda kanisa linaungua kumbe Roho wa Mungu
alikuwa ameshuka na watu wengi waliokolewa wakiwemo askari wa zima moto
waliofikiri kuja kuzima moto
·
Nyakati za kanisa la kwanza watu walimuabudu
Mungu na kumuadhimisha na matokeo yake pale mahali pakatikiswa nguvu za Mungu
na Roho zikashuka,Matendo 4;23-31,16;25-28
·
Elisha nabii alipata ufunuo wa neno la Bwana
wakati fulani baada ya kuwa na muda wa kuimba kwa kinanda 2Wafalme 3;11-20 ,miujiza ya maji na ushindi
wa vita ulikuja baada ya watu hawa kuabudu
·
Wana wa Israel walimsifu Mungu na kutii maagizo
yake ya kuuzunguka ukuta wa mji ngome ya Yeriko
na ukuta ukaanguka kwa kuzama Yoshua 6;15-16,20-26
·
Wakati wa kuweka wakfu hekalu ibada ilimpendeza
Mungu na utukufu wa Mungu ulishuka kwa
sababu watu walifanya ibada ya kipekee sana 2Nyakati 5;7-14 kuabudu kuna
matokeo makubwa sana katika maeneo
mbalimbali ya maisha yetu kamwe hatupaswi kupuuzia kuabudu
·
Paulo na silla walifanya ibada gerezani na
malango ya gereza yakafunguka pamoja na vifungo vyake
·
Kuabudu kunaleta ushindi katika maisha na
mitazamo tofauti wakati waisrael wakimuangalia Goliath na kuliona ni jitu kubwa
na kuwa litawapiga wakaogopa Daudi ambaye ni muabudu Mungu alikuwa na matazamo
tofauti Yeye aliona kuwa Goliathi ni mkubwa kiasi ambacho akimpiga kwa kutumia
kombeo hatamkosa!
·
Kutoka 33;7-22 na 34;1-5, Mungu alimuahidi Musa
kuwa angeuona utukufu wake hii ilikuwa ni nafasi ya kipekee kwani alikuwa
Muabudu , Mungu alijenga uhusiano na
Musa kama wa mtu na rafiki yake aliongea na Mungu uso kwa uso, kuabudu
kunatufanya kuwa rafiki wa Mungu
SURA YA TANO KUABUDU PAMOJA
NA WENGINE. (THE CONGREGATION AT WORSHIP)
Moja ya mambo yanayo mpendeza Mungu ni
pamoja na watu wake kumuabudu pamoja kwa kujitoa kwa pamoja, kumuhimidi na
kumuomba na kumsifu katika ushirika Jambo hili linampendeza Mungu upeo , lakini
je kila kusanyiko linaweza kukubalika na Mungu ? je ni wapi tunaweza
kukusanyika na kuabudu pamoja na ni kwa namna gani na kwa utaratibu gani? Je
namna tunavyoabudu leo chimbuko lake ni wapi tunapo jaribu kujibu maswali haya
ndipo tunapoweza kupata nafasi ya kuonyesha umuhimu wa kuabudu pamoja na maana yake
Mwanzo wa kuabudu pamoja
Namna tunavyoabudu pamoja leo ni matokeo
ya mchanganyiko wa namna nyingi, lakini msingi imara na mzuri wa kuabudu pamoja
kibiblia unatoka kwa wayahudi na nyakati za kanisa la kwanza namna na jinsi
walivyoabudu ndiyo namna na jinsi tuwezavyo kuabudu
Chanzo kutoka kwa wayahudi
Kuabudu kwetu kama wakristo msingi wake
umetokana na msingi wa ndani sana wa ibada za kiebrania. Marabi au waalimu na
wanafunzi wao waliabudu hekaluni katika hekalu ambalo Herode alilijenga na katika
masinagogi, Yesu mwenyewe ilikuwa desturi yake kuabudu katika masinagogi wakati
wa sabato Luka 4;16, mpaka mwaka wa 70 B.K wakati hekalu lilipobomolewa ndipo
wakristo walipoacha kuabudu hekaluni, na hata ingawaje baada ya hekalu
kubomolewa na pamoja na ufa kati ya wakristo na wayahudi kuzidi kujitokeza
wafuasi wa Yesu waliendelea kuabudu katika masinagogi na kumbuka kuwa hata
injili ilipokuwa inahubiriwa mara nyingi Kina Paulo walianza kuhubiri kwa jamii
ya wayahudi katika masinagogi kabla ya kuanza kuwahubiri wapagani walifanya
hivyo katika masinagogi yote chini ya utawala wa kirumi na hata ilipokuja
kutokea utengano wa moja kwa moja kati ya imani ya kiyahudi na ukristo ,
wakristo waliondoka na vimelea vya ibada za kiebrania.
Ingawa kuabudu katika Hekalu hakukuwa na
nyongeza yoyote katika imani ya ukristo kwa sababu moja ya mambo muhimu ya
hekaluni ni pamoja na sadaka za kuteketezwa za namna mbalimbali athari za ibada
za kiebrania ziliendelea kuonekana katika ukristo ikiwemo utoaji wa sadaka
lakini sio za wanyama na matumizi ya
zaburi kama njia ya kumsifu Mungu, Zaburi ziliimbwa, zilikaririwa na
kurudiwarudiwa kama nyimbo rahisi hali hii iliambukizwa katika imani ya ukristo
na ibada zake ingawaje mfumo ulikuwa zaidi wa katika masinagogi kuliko hekaluni.
Mfumo wa kiibada katika kiibrania pia
ulibadilika baada ya kuvunjwa kwa hekalu na kwenda utwanyikoni ambapo huko
masinagogi yalijengwa na kusomwa kwa sheria na manabii ukawa ndio msingi mkuu
wa ibada za kiebrania kwani maswala ya sadaka za kuteketezwa na sanduku la
agano hayakuweza kufanyika tena lakini kabati la kutunzia magombo ya chuo
katika sinagogi yamekuwa kama aina mpya ya sanduku la agano, Ibada katika
masinagogi zilikuwa rahisi sana kuliko za hekaluni hakukuhitajika tena mfumo wa
makuhani na mkuu wa sinagogi alishirikiana ibada na watu wengine katika jamii
yao, Pamoja na kusoma maandiko , kusifu, kuomba na kumtukuza Mungu
kuliendelezwa, watu wote walijihusisha katika kusifu, kuomba na kukariri amri
kumi na “shema” kumbukumbu la Torati 6;4-5 “Sikia, Ee Israeli: BWANA Mungu wako, ni
BWANA mmoja. Mpende BWANA Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote
na kwa nguvu zako zote. Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako.
Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na
wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo. Zifunge kama alama juu ya mkono
wako, zifunge juu ya paji la uso wako. Ziandike kwenye miimo ya milango ya
nyumba yako na juu ya malango yako ukiri huu huitwa shema kiibrania ulikuwa ni kama tangazo la imani na watu waliitikia
Amin kama ishara ya muitikio.
Chanzo kutoka kwa mitume
Nyakati za kanisa la kwanza wakristo nao
waliendeleza mfumo wao wa kuabudu mfumo huu ulifanana na ule ulioendeshwa
katika masinagogi ya wayahudi kulikuwa na usomwaji wa maandiko kwa kawaida
ilikuwa maandiko ya manabii na mitume, kulikuwa na kutukuza, kusifu na maombi
pamoja na sadaka lakini zaidi ya hayo kulikuwa na swala la meza ya bwana au
kuumega mkate na swala la ubatizo, hii ni sawa na Matendo 2;42-47 hii ndio hasa
ibada kamili ya agano jipya iliyokuwa ikifanyika wakati wa mitume, Maswala kama
haya yalifanyika lakini ilikuwa jumapili kwa ajili ya kukumbuka siku bwana
alipofufuka, Ibada zilikuwa rahisi na isiyo na mfumo maalumu Roho wa Mungu
alipewa nafasi kubwa kuingilia kati mfumo wa ibada si kila wakati.
Umuhimu wa kuwa na mapangilio katika ibada
za pamoja
Pamoja na kuwa historia inaonyesha kuwa nyakati
za kanisa la kwanza ibada hazikuwa na mfumo maalumu lakini hii sio kibali cha
kutokuwa na mpangilio katika ibada, mpangilio katika ibada ni jambo la Muhimu
kwani Mungu sio Mungu wa machafuko bali ni Mungu wa utaratibu, kupangilia ibada
kutaweza kuleta msaada mkubwa kwa wale wanaohusika katika kuabudu, sasa ibada
inaweza kupangiliwa vipi kwani kuna maandiko ya kusomwa, maombi, muziki, nyimbo
vyombo, mahubiri, sasa basi kipi kianze na kipi kimalizie kwa ujumla hakuna
mfumo maalumu katika ibada kuwa nini kianze na nini kimalizie lakini kuna
vimelea fulani vya namna ya kuabudu
ambavyo vimekusanywa kitaalamu vimelea hivyo ni kama ifuatavyo
Utambuzi
Moja ya jambo muhimu sana katika ibada ambalo ni la msingi
lakini gumu kidogo kulielezea ni kutambua kile unachokiabudu, makanisa mengi
huwa na tabia ya kujisahau na kuanza moja kwa moja na nyimbo bila kwanza kuweka mazingira yanayomfanya mtu
kutambua kuwa anamwabudu nani kwa hivyo kunaweza kuwako wimbo au maneno
yanayowakumbusha washiriki katika ibada kuwa wamekuja kumuabudu Mungu.
Kusifu
Baada ya kuwa watu wametoa nafasi ya kutambua kuwa yuko Mungu
basi wanapaswa kufurahia uwepo wake kwa msingi huo watakuwa na muda wa kusifu
kwa nyimbo na muziki au watu wanaweza kusifu kwa kutumia maombi
Toba au
kujitakasa
Baada ya kuwa watu wamemsifu Mungu kwa kutambua uwepo wake
bado ni muhimu watu wakatambua kuwa Mungu huyo ni mtakatifu na kuwa tunapaswa
kuziungama dhambi zetu kwa hiyo kunaweza kuwako nafasi ya ukimya ambapo
washiriki wanapata nafasi ya kutubu dhambi zao wana weza kutumia nyimbo au
maombi binafsi au sala maalumu kama baba yetu n.k
Utayari
wa kupokea kutoka kwa bwana
Hii ni hali ya kukaa kimya kwa muda ili yamkini watu waweze
kusikia kutoka kwa Mungu kwa kupata mwanga maalumu illumination ili kujua Bwana
anataka nini kwao wanaweza kuangaziwa au kupata neema na kusikia kutoka kwa
Bwana kupitia Neno la Mungu au Roho Mtakatifu
Kujitoa
Baada
ya kuwa watu wamesikia kutoka kwa Bwana basi ni muhimu kwao kukubali kukutana
na Mungu na kujitoa kwake kwa akili zake na nguvu zake na moyo wake wote hili linaweza pia kufanyika wakati wa maombi
baada ya watu kulisikia Neno la Mungu hili ni jambo la muhimu
Kanuni za kupanga maswala ya ibada
Mpangilio kuhusu ibada una kanuni zake za
msingi na uandaaji mzuri na mpangilio mzuri wa ibada unaonyesha ubora wa
mpangilio huo, tunapo zipangilia ibada zetu kwa mantiki nzuri. Mambo ya msingi
ya kuzingatia katika upangaji wa ibada ili ilete matokeo yanayokusudiwa ni
pamoja na
Umoja.
Moja ya ubora wa kupangilia maswala ya ibada ni kuleta
umoja ibada ni lazima ionekane kuwa ni
moja hii haina maaana kuwa ndani ya ibada hakuna vitu vingine vipo vitu vingi
vinavyounda ibada lakini lazima ionekane
kuwa inategemeana hususani katika kiini chake ambacho ni kumuabudu Mungu kwa
ujumla, kusudi la kumuabudu Mungu ni kuwako amani, kumshukuru na kupokea neema
yake kusudi moja la kuabudu ni kumuabudu Mungu katika Roho na kweli vyovyote
vile ibada itakavyokuwa lengo liwe kuleta umoja katika kumuabudu Mungu na mfumo
wake
Utaratibu.
Jambo lingine la Muhimu katika ibada ni utaratibu, ingawaje
umoja unasaidia kuifanya ibada yote kuwa kamili katika Lengo moja kusudi
lilelile la kuifanya ibada iwe moja litaleta utaratibu “order within the
service” Mungu ni Mungu wa utaratibu na hivyo lazima ibada iwe na uataratibu
Uwiano
Ili ibada izidi kuwa na umuhimu katika taratibu lazima uweko
uwiano wa kila shughuli ndani ya mtiririko wa Ibada, Lazima utoe uwianao wa
Muda unaolingana kulingana na uzito wa kila uanchotaka kifanyike yaani kama
ibada ni ya dakika 60 basi ingawaje kila sehemu inayokamilisha ibada ipewe muda
unaolingana yaani tunazungumzia swala zima la kusifu, maombi, kusoma neno,
mahubiri n.k Mchungaji anatoa muda husika wa mahubiri yake kisha anahakikisha
kuwa sehemu zinazobaki zinapewa uwiano sawa wa mwenendo mzima wa ibada kwa
msingi huo ibada itakuwa inakwisha pia kwa wakati uliokusudiwa na kanisa la
mahali pamoja
Mwenendo
Ibada haiwezi kuwa boara kama haina mwenendo ulio na mpangilio
hii ni hali halisi ya mwenendo mzima wa ibada inatoka wapi na inakwenda wapi
hili linaweza kusimamiwa vema kama anakuweko kiongozi wa ibada mwenye kutoa
maelekezo kipi kinafuata ibada ambayo imesukwa vema kuanzia kuwaalika watu
kuabudu mpaka mwaliko wa mwisho mara nyingi sana inaonyesha mwenendo makanisa
mengine unaweza kuingia kuabudu usijue unatoka wapi na unakwenda wapi jambo
kama hili si jema
Kilele.
Kufikia kilele ni moja ya maeneo muhimu sana ya maeneo ibada,
na kwakuwa inaeleweka wazi kuwa ujumbe wa neno ndio sauti ya Mungu kuzungumza
na watu wake kupitia mchungaji, kilele cha mahubiri ni lazima kiwe kilele cha
ibada pia ingawaje katika makanisa
mengine mwaliko wa watu kuja kuliitikia Neno la Mungu ndio huhesabika kama
kilele cha ibada watu wanapoitikia ile kweli ya neno walilolisikia kwa maana
hii basi si vema kuweka neno kwanza kabla ya mengineyo au tunaweza kusema ni
muhimu katika mpangilio wako Neno likawa mwishoni.
Vichocheo
tofauti
Ni
muhimu kwa makanisa ambayo hawapendelei mfumo fulani wa ibada kuwa na tabia ya
kubadilibadili aina za ibada kila wakati kwani ukiisha kuwa na mfumo fulani
mmoja wa ibada sasa unakuwa umejiundia utaratibu ambao ndio unaitwa “liturgy”liturujia ambalo maana yake ni
utaratibu wa ibada kama mtu anachukizwa na utaratibu wa ibada nikiwa na maana
kuwa haitaji liturujia basi anapaswa kuwa na vichocheo au vionjo tofauti
tofauti visivyozoeleka katika kila mfumo wa ibada ,nyakati za kanisa la kwanza
hakukua na mfumo maalumu wa ibada lakini
tatizo la jambo hili ni kuwa kutakuwa hakuna Muda maalumu wa kutoka katika
ibada ama itawapasa viongozi wa ibada
kuwa na Muda wa kutengeneza muundo na mfumo wa ibada ya kila jumapili ijayo ili
kuweko tafauti
Ushauri unaoweza kusaidia kuzifanya ibada
za pamoja kuwa na maana zaidi
1.
Fanya
maandalizi “Preparation”
Ili ibada iweze kuwa
na maana inahitaji maadalizi ya kutosha ni lazima viongozi wachukue hatua za
kuiandaa ibada kulingana na vigezo hivyo hapo juu, kiongozi wa ibada na waabudu
ni lazioma wajiandae wenyewe, baadhi ya maanadalizi ni ya kimwili si unajua si
vema mtu kuhudhuria ibada akiwa amechoka mwili na akili au wanasinzia ibada
nzima hii itawafanya kuwa nusunusu kwenye uwepo wa Mungu swala kama hilo ni
chukizo la uharibifu kwa Mungu tunaye muheshimu sana
Ingawaje maandalizi
makuu ni maandalizi ya rohoni, kila mwabudu anapaswa kuziandaa akili zake na
moyo wake kwa ajili ya ibada, Fanya tafakari, omba na jikabidhi kwa upya hapo
mwabudu atakuwa amejikita katika katika mkondo wa upendo ambapo atapata uzoefu
mpya wa nguvu za kiroho unafikiri nini kitatokea endapo itatokea katika ibada
wahusika wakaomba kwamba Roho wa Mungu ashuke katika mkutano uliokuwa
ukimsubiri akashuka kwa hakika ibada itakuwa yenye kuvutia sana.
2.
Hakikisha
watu wanajihusisha “Participation”
Jambo la muhimu sana
katika ibada ni kuhusisha watu , kila mtu ni lazima ahusike katika kuabudu kama
mtu atakuja katika ibada kama mtafiti tu
atakuwa amekoma kuabudu, bahati mbaya tuliyo nayo ni kuwa watu wengi
huja ibadani kama watafiti au wachunguzi tu, mtu anafanya kazi ya kuangalia
huyu kavaa nini , hapa wanaimbaje, kwaya ikoje , muhubiri kahubirije matokeo yake hawaimbi, hawaombi, hawapokei
ujumbe wa mahubiri, hawa ni wachunguzi tu wala sio waabudu, siku zote wito wa
ibada ni kututaka tuhusike kikamilifu katika kuabudu kwenyewe ni lazima
tukubali kushiriki ibada na kufikia hata uwezo wa kusema wimbo ni wimbo wangu
nitauimba, maombi ni maombi yangu nitaomba ,sadaka yangu nitaitoa kwa Bwana,
maneno ya Mungu ni maneno ya Mungu wangu kwangu ni ujumbe wangu aseme nami
nitaupokea tu tabia kama hii na mtazamo kama huu unaifanya ibada iwe na maana
3.
Hakikisha
ibada inaheshimika “Reverence”
Heshima bado ni moja ya misingi muhimu ya ibada Bwana Mungu wetu anaabudiwa , ni wakati wa
utulivu wa kujali, kuhusika na kujitiisha, wako watu wana weza kuja ibadani na
mambo ya mitaani wako ibadani lakini akili zao haziko pamoja na Mungu wanasahau
kuwa wako nyumbani mwa Mungu, kuwa katika uwepo wa Mungu na kuwa nyumbani mwake
hakuna tofauti kubwa Mungu ni Mungu na
hakuna Mungu mwingine aliye kama yeye
unawezaje kuwa mbele ya mfalme wa wafalme wa dunia nzima na mbingu na
bahari kisha ukawa mapepe, kumuabudu Mungu katika kweli ni pamoja na akili
zetu na mawazo yetu na kumpa yeye Nafasi
kwa kadiri iwezekanavyo hii inaleta maana pale unapo inama mbele zake kwa
utulivu na unyenyekevu mkubwa jambo hili sisi wapentekoste hulipuuzia sana kama
hakuna unyenyekevu na heshima na kumaanisha katika kuabudu basi hakuna ibada.
Jinsi ya kupanga ibada
Jinsi tunavyopanga ibada inategemea na aina
ya urithi wa mpango kamili wa ibada na mashauri kuhusu namna ya kushiriki ibada
kama yalivyojadiliwa, Hali ya kupangilia ibada katika muonekano huu wa kawaida
wa kuonekana kwa macho unapaswa kuchunguzwa uweje sasa hii ni kwa sababu mpaka
mwaka wa 200 B.K yaani baada ya Kristo wakristo bado walikuwa hawajaanza
kuabudu katika majengo kama tuliyo nayo leo wao walikutana pale gorofani,
kwenye mapango na kwenye makaburi au sehemu zozote ambazo wangepata utulivu
bila muingiliano wa mambo mengine , Nyumba za kuabudia wakristo zilipoanza
kujengwa zilikuwa rahisi na zenye
kufanana na masinagogi ya kiyahudi baada ya hapo jengo lililofuata lilikuwa ni
jengo la Roman basilica ambalo lilijengwa kama hall (Jengo hili liko katika
makazi ya Pope huko Vatican) lakini kanisa lenyewe lilikuwa rahisi tu na hata
ingawaje bado kuna majengo tofauti tofauti leo lakini mengi ni ya kawaida wabaptisti kwa mfano hutenga madhabahu ya
neno na meza ya kuwekea meza ya Bwana kwani wao huona kuwa kiini kikuu cha
ibada ni Neno la Mungu vyovyote iwavyo muundo wa jengo na mitazamo ya waamini
wa mahali hapo inaweza kuamua ni namna gani wajipange wakiabudu, hata hivyo ni
muhimu kutotilia maanani maswala ya alama fulani fulani na pia kama watu wa
mahali fulani wataamua kulifanya Jengo lao kuwa lenye thamani hawagombwi
kufanya hivyo lakini wamishionari wa zamani walijenga vijengo kilingana na
mahitaji ya mahali na kwa kusudi la kukusanyika na kukutana na waamini hivyo
majengo mengi yalikuwa rahisi tu.
SURA YA SITA MUZIKI NA KUABUDU.
Kusifu na kuabudu kwa njia ya muziki ni
mapokeo tuliyoyapokea wakristo kwa wingi na utajiri wake kutoka katika dini ya
wayahudi ambao wana utajiri wa ajabu kutoka katika maandiko na kusifu na kuomba
na kuabudu tangu zamani, kwa karne nyingi wayahudi wamekuwa na ujuzi wa kutosha
katika kumsifu Mungu aliye hai hususani
kwa kuimba,Uimbaji huo uliambatana na vyombo mbalimbali vya muziki na
uliwashirikisha watu wote, Ukristo uliposhika kasi kusifu kwa njia hiyo
kulikuwa ni sehemu ya ibada zao watu wote waliimba na zaburi zilikuwa ndio kama
kitabu chao cha nyimbo ingawaje wakristo waliziimba zaburi katika maana
nyingine mpya kwani Mungu waliyekuwa wakimsifu wakati huu alikuwa amekuja
kuwaokoa kupitia Yesu Kristo
Kuabudu Kwa njia ya Muziki ni Urithi
Wakristo walianza mara moja kutumia zaburi
na hii ilikuwa ni kawaida ya maswala ya ibada za katika masinagogi ingawaje
matumizi ya zaburi hizi zilikuwa na maana pana zaidi kutokana na wakristo
kuamini katika ukombozi na umasihi wa Yesu. Kwa mfano Yesu Kristo mwenyewe
katika karamu yake ya mwisho na wanafunzi wake aliimba Zaburi Marko 14;26,
Tabia hii iliendelezwa na wakristo wa nyakati za kanisa la kwanza Baadhi ya
wasomi huamini pia katika nyimbo zilizomo ndani ya agano jipya kama ule wa
Zakaria, Mariam, na simeoni na pia kuna
salamu za neema ambazo zilitumika katika ibada, Aidha inasemekana Pia Paulo
alinukuu baadhi ya nyimbo zilizokuwa zikiimbwa wakati huo mfano katika Waefeso
5;14 na ule wa 1Timotheo 3;16
kwa kuwa
nuru ndiyo hufanya kila kitu kionekane. Hii ndiyo sababu imesemekana:
“Amka, wewe usinziaye,
ufufuke katika wafu,
Na
Kristo atakuangazi.”
Bila shaka
yo yote, siri ya utauwa ni kubwa:
Alidhihirishwa katika mwili wa kibinadamu,
alithibitishwa kuwa na haki katika Roho,
akaonekana na malaika,
akahubiriwa miongoni
mwa mataifa,
akaaminiwa
ulimwenguni,akachukuliwa juu katika utukufu.
Hizo ni baadhi ya nyimbo
ambazo zilikuwa zikiimbwa nyakati za kanisa la kwanza na inaonekana pia mitume
walihimiza swala zima la uimbaji wa namna mbalimbali mfano ni katika Waefeso
5;19 na katika wakolosai 3;16 lakini baada ya kipindi fulani katika kanisa
uimbaji wa jumla ulikoma mpaka wakati wa
mageuzi ya kiprotestant ndipo uimbaji
ulirejezwa kwa watu, Moja ya nyota wa
kimapinduzi wa uprotestant John Huss wa Bohemia
alianzisha uimbaji na kuchapisha kitabu cha uimbaji mwaka wa 1501,
Martin Luther pia alisisitiza sana uimbaji wa jumla na aliandika nyimbo zaidi ya 30 na hivyo
mpaka mwaka 1552 waluther walikuwa ni waimbaji wakubwa sana na uimbaji tulionao
leo ni matokeo ya uimbaji uliotokea wakati wa uamsho wa Isaac Watts na John na
Charles Wesley uamsho wa wakati wao huko Uingereza na uamsho mkubwa wa huko
Marekani vyote vilichangia aina za
uimbaji tulio nao leo.
Katika Agano la kale na jipya Muziki ulikuwa ni sehemu muhimu sana ya
kumuabudu Mungu, kwa mfano katika agano la kale wao walichagua waimbaji kwa
uangalifu mkubwa sana ili kuongoza watu katika kufurahia kuabudu 1Nyakati 15;16-22
jamii ya waimbaji na watu wa muziki walichaguliwa kutoka miongoni mwa familia
za kabila za kikuhani yaani walawi watu ambao walikuwa wamewekwa wakfu kwa
ajili ya utumishi wa Mungu na waliofunzwa kwa ufanisi maswala ya muziki, Sasa
tunaishi katika ulimwengu wa Muziki duniani kuna kila aina za uimbaji Ndege
wanaimba na kuna sauti za kila aina za kufurahisha haishangazi endapo muziki
huo utaimbwa kutoka katika hisia za ndani sana za pendo la Mungu jambo la
kumsifu Mungu kwa njia inayoambatana na muziki linampendeza Mungu sana Zaburi
147; 1 inasema “Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa,
jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu
Yeye! ”
Kusudi
la msingi la Muziki ni kwa ajili ya kumuabudu Mungu na kumsifu yeye, Muziki
umekuwa ni msaada wa karibu sana katika swala zima la kuabudu unasaidia sana
watu kumuabudu Mungu, Biblia inatoa mifano mingi sana ya matumizi ya vifaa vya
muziki na sauti stadi kwa msingi huo tunajifunza umuhimu wa kuabudu kupitia
muziki, msisitizo mkubwa wa kuabudu kwa kutumia vyombo vya Muziki umetolewa
katika agano la kale zaidi kuliko katika agano jipya Biblia inanukuu matumizi
ya kwanza ya muziki kwa kuonyesha vyombo vya muziki Mwanzo 4;21 vyovyote Biblia
inavyosisitiza swala zima la Muziki na vyombo vya muziki kusudi kuu ni kuabudu
na kumsifu Bwana
Je Muziki katika Ibada ni dhambi?
Muziki
ni wa muhimu kwa kila tamaduni kwani unawakilisha mawazo na hisia za watu sawa
na tamaduni zao, kwa hivyo lazima muziki utunzwe katika tamaduni ya mahali hapo
kwa gharama yoyote, tunapojifunza umuhimu wa muziki na nafasi ya muziki katika
maisha ya watu tutaanza kupata picha kwa nini ni muhimu kutunzwa kwa gharama
yoyote, Muziki ni moja ya alama za kawaida katika tamaduni zote kila aina ya
kabila duniani wana aina zao za Muziki na katika tamaduni nyinginezo muziki
huambatana na maswala ya kuabudu kadiri ulimwengu unavyokua kumekuweko na
mwingiliano wa tamaduni za kimuziki na hivyo Muziki wa kanisa umetoka nje na
kuathiri baadhi ya tamaduni na miziki ya baadhi ya tamaduni imeingia kanisani
au kuchanganyika na ya jamii nyingine
kwa hivyo sasa Muziki hauna mwenyewe
Mungu aliutumia Muziki kama njia ya kurithishana mafundisho toka kizazi
hata kizazi hii iko wazi katika Kumbukumbu la torati 31 na 32 kabla kidogo ya
kifo cha Musa Mungu alimwambia Musa sasa jiandikie wimbo huu na uwafundishe
wana wa Israel wimbo huu utawashuhudia
kwa sababu hautasahaulika na vizazi vyao Kumbukumbu 31;19,21;32 44-47.
Kwa msingi huo basi hatuwezi kuhukumu kuwa
aina fulani ya muziki ni dhambi kwani muziki unatokana na tamaduni mbalimbali na
historia na unatofautiana kulingana na maeneo mbalimbali na makusudi mbalimbali
lakini linapokuja swala la kuabudu bila kujali ni aina gani ya muziki inapigwa
mambo kadhaa ya msingi ni laziama yazingatiwe ili kuifanya ibada iwe ibada na
iweze kuwa tofauti na makusudio mengine ya muziki mambo ya kuzingatia ni pamoja
na ;-
·
Wimbo wa kusifu na kuabudu ni lazima umtukuze
Mungu- Ibada ya kweli huleta furaha na
Mungu anataka watu wawe na furaha hakuna ubaya kuwa na hisia nzuri ingawaje
miziki mingi haijali kitu kuhusu Mungu wala haitupi hisia kuhusu Mungu kwa
msingi huo hata kama muziki huo utakuwa mzuri na wenye hisia kali lakini kama
hauusu Mungu katika kuabudu Muziki huo haumpi Mungu utukufu.
·
Wimbo wa kusifu na kuabudu lazima uwe unatoka
moyoni kwa kumaanisha- kama
kumsifu kwetu Mungu na kumuabudu hakutokani na ukweli kutoka moyoni Mungu
hawezi kufurahia nyimbo zetu Nabii Amosi alikemea maswala ya unafiki wa
wayahudi waliokuwa wamerudi nyuma na kumuacha Mungu lakini waliendelea kufanya
ibada lakini hawakumaanisha kile walichokifanya bali walifikiri mambo mengine
Mungu hapendezwi na ibada za namna hiyo Amosi 5;23
·
Wimbo wa kusifu na kuabudu lazima useme kile
maandiko yanachokisema- ni muhimu
kufahamu kuwa uimbaji ni muhimu pia ukaimbwa sawa na mafundisho sahii ya Biblia
kwa mfano mtu anaweza kutunga Nyimbo inayosema kuwa wakristo tutawekwa huru
mbali na majaribu ya kila aina lakini maandiko yana sema tutajaribiwa 1Petro
1;6-7 wimbo wa aina hiyo utakuwa haukuzingatia uwiano wa maandiko haufai,
Muimbaji anaweza kuwa mwema na mwaminifu lakini wimbo hauko sawa na mafundisho
ya Biblia kwa msingi huo ni lazima wimbo
uzingatie kuwa baraka na sio kuwapotosha watu kutoka katika neno la Mungu
ushauri wa bure kwa waimbaji wa nyimbo za injili kwenda kusoma katika vyuo vya
biblia kwao ni muhimu sana ili waimbe sawa na tafasiri halali za maandiko.
·
Wimbo wa kusifu na kuabudu lazima uguse
mahitaji mbalimbali ya watu – Ni muhimu
pia nyimbo zikagusa mahitaji ya watu pamoja na shuhuda zao wimbo unaoongoza
watu kuabudu siku zote uendane na makusudi ya kuabudu kwenyewe kwa msingi huo
tunapoimba na kusifu yale ambayo bwana ametufanyia ni sehemu ya shukurani
kwetu, na uchaguzi wa nyimbo unapofanyika lazima uzingatie lile kusudio la
wimbo na mahitaji ya watu na wakati
·
Wimbo wa kusifu na kuabudu haupaswi kuwatoa
watu katika kusudi la kuabudu- watu
huabudu vema sana na wimbo wanaoufahamu kuliko wimbo mpya ingawaje ni vema
kujifunza wimbo mpya ili kwamba ibada isiwe yenye mazoea lakini jambo la msingi
ni kuwa lisiwachukue watu nje ya kusudi la kuabudu Mungu na utukufu wake ni
lazima vipewe kipaumbele kama kiini cha ibada
Aina
mbalimbali za kusifu.
Kutokana na vyanzo mbalimbali vya urithi wa Muziki kumekuweko na aina
mbalimbali za kusifu ujuzi kuhusu aina mbalimbali za kusifu utamsaidia kila
kiongozi wa ibada kutumia sauti na vyombo kusaidida katika kumuabudu Mungu kwa
namna mbalimbali tulizo nazo
Kianzilishi
Ni
aina ya muziki wa mwanzoni ambao unaweza kupigwa au aina ya sifa ya mwanzo
ambayo inaweza kutolewa kama kiashiria cha kuwa ibada inaanza nyimbo hizo za
uanzilishi zinapaswa kuwa zenye kutengeneza mazingira ya kumuandaa muabudu
kujua kuwa ibada sasa inakaribia kuanza au inaanza
Wito wa
kuabudu
Huu ni wimbo
wa kuabudu au sifa amabao unamkubusha mwabudu kuwa amweke Mungu kati sasa kama
kiini cha kuabudu, wimbo wa aina hiyo utawajulisha watu kuwa Bwana yu hekaluni
mwake au utaita watu kuabudu na kujihusisha katika kuabudu
Mwitikio
Hii ni aina
ya sifa inayoonyesha mwitikio inawezekana yakawa ni maombi na watu wakaitikia
amen hili ni itikio la kuonyesha kuwa Mungu ameitikia maombi yao
Vyombo vya
Muziki
Zinaweza kupigwa ala fulani za vyombo vya
muziki au muziki maalumu unaoashiria kuinua mkutano katika kumsifu na kumuabudu
Mungu Muziki wa aina hiyo uwe unampa Mungu utukufu ama munaweza kuimba wimbo
Kuabudu sio tu kuko kwa namna nyingi lakini
pia ni lazima kuweko na viini vya kuabudu wakati wa kutumia Muziki viiini hivyo
ni pamoja na
Ø
Swala zima
la kuabudu
Ø
Kumuabudu
Mungu baba
Ø
Kumuabudu Bwana
Yesu
Ø
Kumuabudu
Roho matakatifu
Ø
Kufundisha
neno la Mungu
Ø
Kuzungumzia
wokovu
Ø
Kukumbusha
maisha ya kikristo
Ø
Kukumbusha
wajibu wa kanisa
Ø
Kuhusu ufalme
wa Mungu
Ø
Kuhusu
umishenari
Ø
Kuhusu jamii
bora
Ø
Kuhusu
maisha ya milele
Lakini ni muhimu pia unapoimba kuhusu
wokovu kukumbushia swala la wokovu kwa
neema, toba na maungamo ya kweli na wito wa kukubali na unapozungumzia maisha
ya ukristo unaweza kukazia imani,
uhakika, tumaini, upendo, amani na faraja, furaha, maombi, kujiwejka wakfu,
ushirika na maisha bora ya wakristo
majumbani mwao
Sifa za
Muziki unaofaa katika kumsifu Mungu
Unaokubalika
kitheolojia
Rahisi na
wenye lugha ya kueleweka
Unaoimbika
Unaoeleweka
SURA YA SABA BIBLIA NA KUABUDU
Maandiko yamekuwa siku zote ni ya lazima ya
muhimu katika swala zima la kuabudu Kikristo, Nyakati za kanisa la kwanza wakristo
walipokuwa wanakutana walichagua maandiko ya kusoma kutoka agano la kale na
baadaye injili zilipoandikwa na nyaraka nazo zilianza kusomwa, Na kwakuwa tangu
awali kuabudu kwa kikristo kulikuwa ni pamoja na kusikia Neno la Mungu linasema
nini Maandiko yamekuwa ni sehemu muhimu ya kila ibada ya kiagano jipya,Unapoipitia
Biblia utaweza kuiona inapotumika kwa ibada na itakupa mwanga wa aina
mbalimbali
1.
Inatoa mwito wa kuabudu
2.
Inatupa mafundisho
3.
Inaweza kutumika katika kutoa baraka na kutoa
neema mwishoni mwa ibada Hesabu 6;22-27,2Koritho 13;14,Warumi 16;24,Wagalatia
6;18,Efeso 6;23,1Tomotheo 6;20-21 ni maandiko yanayotumika sana kwa salamu za
neema au baraka baada ya ibada
4.
Inatumika kwa ajili ya Mahubiri na usomaji wa
maandiko.
Namna ya kuisoma Biblia katika kuabudu
1.
Pangilia
namna ya kuisoma Biblia kwakuwa Biblia hutumiwa na watu wengi katika
maswala ya kuabudu ni muhimu basi kwa kiongozi wa Ibada kujiandaa au kuandaa
sehemu za maandiko ya kuyasoma ,si jambo la kushangaza kuwa kuna watu wanaweza
kuisoma Biblia na kuipenda inaposomwa lakini kuna uwezekano wasiweze kujua sura
aya na hata kitabu kwa msingi huo
maandalizi ni lazima yafanyike kuandaa wapi pa kusoma au vifungu vya kusoma ili
kwamba kama watu wamekuja na Biblia zao waweze kufuatilia kwani wasipojua ni kitabu gani kinasomwa na
ili waweze kufuatilia aidha ni muhimu pia kuelezea kuwa ni toleo gani
linatumika ili wafuatiliaji waweze kujua ni Biblia toleo gani inatumika
2.
Biblia
isomwe kwa sauti biblia ni muhimu ikisomwa kwa sauti ya kueleweka kwa uwazi
na maana yake ni lazima ieleweke, yaani maana ya kifungu kinachosomwa kwa msingi huo kifungu cha maandiko
kinachosomwa wakati wa kuabudu ni lazima kieleweke na kusomwa kwa sauti safi na
na inapowezekana anaweza kurudia mara mbili, wakati Ezra na waandishi
walipokuwa wakisoma sheria pia ilikuwa ikirekodiwa pia na kufafanuliwa ili kwamba watu waweze kuelewa kile
kilichokuwa kinasomwa Nehemia 8;8 aina hii ya usomaji wa maandiko ni muhimu
ikifuatwa.
3.
Usiisome
Biblia kupita kawaida Do not overread ni muhimu kufahamu kuwa si vema sana
kuisoma Biblia kwa mtindo wa kuiigiza au kuisoma kwa namna ambayo itawatowa
watu katika usikivu wa kwamba wanasoma Biblia lakini isomwe katika namna ambayo watu watajua
kuwa inayosomwa ni Biblia iadha msomaji anapiosoma asababishe watu waone jinsi
Biblia ilivyo ya ajabu na nzuri na sio waseme jamaa anasoma vizuri sana, Biblia
isomwe katika misisitizo yenye kufundisha maana
au kukazia maana ili kuipa nafasi
ionyeshe kile inayosema , Biblia inaweza kuwa sauti ya Mungu kwa watu wake na hivyo isomwe katika namna ambayo watu wataona
kuwa Mungu anasema na watu wake
4.
Biblia
ndio kiini kikuu cha ibada kwa msingi huo sio tu Mungu huzungumza kwa
usomaji wa maandiko lakini pia kupitia mahubiri hapo huzungumza na watu
aliowaita hivyo Mungu pia huzungumza na
watu wake kupitia neno lake linapohubiriwa na wahubiri
a. Kiini cha mahubiri- Mahubiri ya
Kikristo ni tofauti na mahubiri ya desturi nyingine kwa ufupi mahubiri ya
Kikristo mwanzoni hayakuwa yenye kufurahisha sana kwani wanafalsafa walikuwa na
wasemaji wao waliokuwa wasemaji hodari aidha wayahudi pia walikuwa na wahubiri
wao maalumu lakini katika ukristo kiini
kilikuwa si wasemaji hodari bali ujumbe na mwanzoni injili ilikuwa ni tangazo
kuwa Mungu yu awakomboa watu wake na mahubiri yalitokana na nguvu za Roho
Mtakatifu na ujumbe aliowapa katika mioyo yao, Yesu alikuwa muhubiri wa kawaida
aliyekuwa akitembea huko na huko akihubiri habari njema kwa watu wa
kawaida na kila mtu alimwelewa aidha
aliwatuma wanafunzi wake kuhubiri na mwisho aliacha agizo kwa watu wote
kuhubiri, kuhubiri ilikuwa ni kiini cha ujumbe wa Mungu kuwafikia watu na mwito
wa watu kufikiwa na injili ili wakombolewe Warumi 10;14 kwa msingi huo kiini
kikuu cha mahubiri ni kufikisha habari za ukombozi kwa watu wa Mungu kwa njia
ya upumbavu yaani iliyodharaulika kanisa la kwanza watu walikuwa na utiliaji
maanani mahubiri ya aina hiyo kwani kukosekana kwa hilo kunaweza kuyafanya
mahubiri yasiwe na maana jambo ambalo linaikumba jamii yetu leo katika mahubiri
sio sehemu ya kuonyesha uwezo wetu wa kujieleza au kunena bali kumtangaza Mungu
ili kwamba tabia na mwenendo wa watu uweze kuguswa na kubadilika kumuelekea
Mungu Mtu mwenye ujumbe wa Mungu huwa na mvuto wa tofauti na kuwafanya watu
wavutike kutaka kusikia Mungu anazungumza nini nao sio namna unavyovaa au muonekano
Luka 7;24-29 ujumbe wa Yohana uliweza kubadilisha maisha ya watu wengi
waliohesabika kama wenye dhambi na kuwaacha wale tu wenye kiburi na kujihesabia
haki yaani mafarisayo
b. Asili ya mahubiri- Kama kuhubiri ni
muhimu sana basi lazima asili ya kuhubiri ieleweke vema mahubiri asili yake
lazima itoke katika mawazo ya Mungu, mahubiri hayapaswi kuwa asili ya muhubiri,
maoni au mtazamo wake bali ujumbe wa Mungu kwa msingi huo muhubiri lazima awe
na uwezo wa kupokea mawazo ya juu sana ambayo ni mawazo ya Mungu Isaya 55;9, “Mawazo
yenu si mawazo yangu ….” Kwa msingi huo uhusiano wa maandiko na ujumbe utaonekana ukijengwa katika maandiko hii ikiwa ni pamoja
na utoaji wa mifano itakayoendana sawa na kiini cha ujumbe uliokusudiwa kwa maana nyingine mahubiri ni sauti ya Mungu
na ili mtu ahubiri sauti ya Mungu Mwanatheolojia Donald Miller alisisitiza hivi
“Mahubiri ya kweli lazima yawe yanafunua biblia (Expository Preaching) na
mahubiri yasiyiofunua biblia(Expository Preaching) hayo siyo mahubiri”ingawaje kauli hii inaweza
kuwa imevuka mipaka kwani kunaweza kuweko mahubiri ya kibiblia yasiyo funua
Expository lakini mkazo ukawa ni kweli ya kibiblia jambo la msingi ni muhubiri kuisoma Biblia
kutambua kiini na kuhubiri kwa makutano
c. Mahubiri Kama sehemu ya ibada- kuna
uhusiano kati ya mahubiri na ibada na mahubiri ni ibada au sehemu ya ibada kuna
maoni mbalimbali yanayotolewa kuhusu uhusiano wa mahubiri na ibada
Kuna
wanaofikiri kuwa mahubiri sio ibada
hili ni kundi la wakristo wanaoona kuwa mahubiri sio ibada
na huyavumulia tu kwa mazoea
na ziko sehemu nyingine ambazo mahubiri
yamekuwa yakikimbiwa au kuachwa na watu yanapoanza tu watu huondoka zao
wakifikiri kuwa sio sehemu ya ibada baadhi ya madhehebu kama Anglican na Roman
catholic waliamua kuyaondoa au kuyaweka kwa kiasi sana au kuyaondoa kabisaa
katika taratibu zao za ibada ikifikiriwa kuwa sio sehemu muhimu ya ibada
ingawaje makanisa mengi ya kiinjili huona mahubiri kuwa sehemu muhimu ya ibada.
Kuna
wanaoona kuwa mahubiri ni sehemu ya ibada iliyo ya muhimu sana
hawa ni baadhi ya wakristo au madhehebu
ambayo huona kuwa mahubiri ndio sehemu muhimu sana kuliko zote katika ibada
imefikia hatua ambayo wengine hawahudhurii ibada isiyo na mahubiri au wengine
hufikia hatua pale wanapokuwa wamechelewa mambo mengine kama sifa n.k. lakini
mahubiri akayawahi huona kuwa hajachelewa kitu kwani amewahi mahubiri hili ni
kosa kwani ibada ni kiini kikuu cha kuabudu na hivyo kila sehemu ya ibada ni sehemu
ya kuabudu pia hivyo hakuna sehemu iliyo muhimu kuliko nyingine zote ni sehemu
za ibada na matendo yote kwa ujumla ndio hufanya jumla ya kuabudu.
Mahubiri
ni sehemu ya ibada tunaweza kujiuliza swali na kujijibu kuwa ni nini
umuhimu wa mahubiri? Mahubiri ni sehemu ya ibada
ni tendo la kuabudu hata ingawaje ni sehemu
muhimu ya ibada lakini sio sehemu ya pekee ya ibada kwani maombi, nyimbo, u somaji
wa maandiko na utoaji wa sadadka ni sehemu za muhimu za ibada, mahubiri ni ya
kwanza miongoni mwa hayo na hivyo ni lazima yawe msingi na kilele cha
ibada
lakini kamwe hayawezi kusimama
peke yake tu
ni moja ya matendo ya
kuabudu miongoni mwa mengi yaliyo sawa na kwakuwa
kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu basi
jaribio lolote lile la kupunguza au kutenganisha matukio mengine na mahubiri ni
upotevu wa misingi ya ibada
kwani katika
kuabudu Mungu husema na wanadamu husikia
na muhubiri anapohubiri Mungu huzungumza na hiyo ndiyo ibada ya kweli
Mahubiri
na meza ya bwana
Baadhi ya wanatheolojia
hawakubaliani na wazo la kuwa mahubiri ni kiini kikuu cha ibada na badala yake
wao huona kuwa kiini kikuu cha ibada ni Meza ya bwana au Ekaristi kabla ya
kukubali au kukataa wazo lao agizo kuu kuhusu kuhubiri injili liliambatana na
neno fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu, Ni muhimu kufahamu kuwa meza ya bwana ni
miongoni mwa tangazo la kifo cha Bwana Yesu sio tu ni miongoni mwa tangazo
lakini haionekani kuwa ndio ya msingi wa utangazaji injili katika agano
jipya.Swala la meza ya bwana ni tukio la kikuhani zaidi katika historia za
kibiblia Yesu alifanya kazi kubwa ya kinabii na kichungaji zaidi kuliko ya
kikuhani kwa hiyo ni muhimu kufahamu kuwa Mungu kupitia mwana wake Yesu Kristi
ndio njia kuu ya kupata neema na sio
meza ya Bwana kama mtu atakazia kuwa
meza ya bwana ni sehemu ya neema na ya muhimu kuliko Kristo mwenyewe itakuwa ni
imani nyingine potofu au injili nyingine kwa hiyo ulingano ulio sahii kati ya
mahubiri na meza ya Bwana ni muhimu ukawekwa sawa mapema kila moja lina sehemu
katika ibada unaweza kutoa umuhimu kwa meza ya bwana bila kuacha meza ya bwana
kuchukua nafasi ya mahubiri jambo la muhimu kufahamu ni kuwa meza ya bwana ni
moja ya njia ya kuhubiri au kutangaza kazi ya ukombozi iliyofanywa na Mungu
d.
Wajibu
wa waamini kama sehemu ya mahubiri
Waamini wana wajibika kuhusika
kutimiza sehemu yao kama sehemu ya mahubiri hayo wajibu huu ni zaidi ya
kuonyesha mwitikio wa ujumbe wakati wa mahubiri, wajibu mmoja wa waamini ni
kwanza kukumkubali muhubiri na kumuona kuwa ni mmoja wa watu waliopakwa mafuta
na Mungu waliseme neno lake au kuleta ujumbe kwao na ujumbe wake ni muhimu
ukipokelewa kama ujumbe wa Mungu jambo kama hili likijengeka litawawezesha
waamini kukaa kwa usikivu na utii , 1Wathesalonike 2;13 “Kwa sababuhiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma kwa kuwa
mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisilkia kwetu mlilipokea si kama
neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu ;na ndivyo lilivyo kwelikweli
litendalo kazi ndani yenu ninyi mnao amini”
kwa msingi huo pia ni wajibu wa waamini kuombea muhubiri kila wakati
siku zote ili kwamba waseme ujumbe utokao kwa Mungu na kuwa hakuna mwenye haki
ya kumkosoa muhubiri kama hukuhusika katika kumuombea 2Thesalonike 3;1 “Hatimaye ndugu tuombeeni…”lazima
tusikilize neno katika hali ya kuomba na
mwisho tuitikie mwito wa mahubiri kwa hiyo basi Biblia ni moja ya sehemu muhimu
ya ibada.
SURA
YA NANE MAOMBI NA KUABUDU
Maombi ni moja ya sehemu ya Muhimu sana ya
kuabudu Mtu fulani husema kuwa ndio roho
ya kuabudu kunauwezekano ikawa
hivyo lakini maombi ni moja ya sehemu ya
ibada yanamtambua Mungu kwa sababu yanaelekezwa
kwake yanasaidia kutuunganisha na Mungu
kwani moja ya sababu ya kuishi kwetu ni ili tuunganishwe na Mungu na nisehemu pia ya kumshukuru sana Mungu mara
nyingi maombi pia yametumika kama sehemu ya siri ya uhusiano na Mungu kwa msingi huo basi dakika anagalu kumi au
kumi na tano hivi ya siku za jumapili ibadani ni muhimu zikitolewa kwaajili ya
maombi tutayazungumzia maombi ya Binafsi kwa wakati wake lakini hebu
tuzungumzie maombi ya pamoja
Asili ya maombi ya Pamoja.
Asili ya maombi ya pamoja kwa ujumla
haieleweki lakini maombi ya pamoja ni ya muhimu kuliko maombi ya binafsi katika
maombi ya binafsi mkristo anakuwa hana mipaka anazungumza na Mungu kwa kadiri
awezavyo kwa kufuata hali yoyote aitakayo lakini katika maombi ya pamoja
kiongozi hufanya zaidi ya maombi ya mtu mmoja mmoja muombaji Binafsi anaweza
kuombea yoyote ayatakayo lakini katika maombi ya pamoja hitaji fulani moja huafanyika kwa ajili ya kuwakilisha watu
wote waliopo au kanisa katika maombi ya Pamoja kiongozi hutaja hitaji kisha
watu wote huombea pamoja na wakati mwingine kiongozi huomba kwa niaba ya watu
wote
Aina mbalimbali za maombi.
Kumtukuza Mungu adoration
Maombi ni njia
mojawapo ya kumuabudu Mungu lakini kumtukuza Mungu ni moja ya njia muhimu sana
za kumuabudu hii ni hali ya kumtukuza Mungu na kulisifu jina lake aina hii ya
maombi ni ya lazima kwa sababu huwekwa mbele zaidi kuliko aina nyingine za
maombi kwa kawaida maombi ya kumtukuza Mungu huwa ndo ya kwanza kumbuka msingi
was ala ya Bwana unasema Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe
Shukurani
thanksgiving
Maombi
yanakwenda kilaini ikiwa baada ya kumtukuza Mungu unaunganisha na kushukuru
kwani kumtukuza mungu huambatana na kumuinua na kukumbuka wema wake na upendo
wake na fadhili zake ni kana kwamba mwabaudu anatambua kuwa bila Mungu hawezi
kufanya jambo lolote anakumbuka zawadi nyingi au fadhili nyingi za Bwana, ikiwa
pamoja na wokovu kupitia Yesu Kristo na neema yake ya ajabu kwetu ndipo sa
tunajihisi kushukuru na kwa mambo mengine mengi swana
Toba au maungamo
Comfession
Aina hii ya maombi ni maombi ya toba au
maungamo au kujitakasa Mungu wetu ni mtakatifu na kuwepo katika uwepo wake
pasipo utakatifu ni kujiweka katika uhusiano mwema na yeye, Toba inasaidia
kuleta mapatano na Mungu mara nyingi msamaha huu tunaouomba sio lazima iwe kwa
ajili yetu tu bali na kwa ajili ya wengine kumbuka msingi katika sala ya bwana
“Utusamehe makosa yetu…” ina weza kuwa toba ya dhambi Fulani maalumu katika
kanisa kwa ujumla au kujiweka sawa kwa ajili ya kumkaribisha Mungu.
Dua Petition
Dua ni sehemu ya maombi kuomba dua ni
kumshirikisha Mungu mahitaji yetu aina hii ya maombi inaweza kusisitizwa katika
msingi was ala ya Bwana tunaona maneno “utupe leo riziki yetu…” Mathayo 6; 11-13
na 7;7-8
Maombezi
Intercession
Maombezi yanafanana sana na Dua
lakini maombezi ni kuomba kwa niaba ya aina hii ya maombi pia ni ya muhimu
kutiwa moyo ni kuacha mahitaji yetu binafsi na kuinua mahitaji ya wengine kwa
mujibu wa Yakobo maombi ya mwenye haki yafaa sana akiomba kwa bidii
Kujitoa Dedication
Haya ni maombi ya kujitoa upya kwa
Mungu kila wakati maranyingi aina hii ya maombi hutolewa mwishoni mwa kumalizia
ibada.
Aina
za maombi katika ibada
1.
Maombi
ya ufunguzi
Kwa kawaida ni maombi yanayoombwa mwanzoni kwa ajili ya
ufunguzi wa ibada lengo la maombi hayo ni kuziita Baraka za Mungu kumiminika
katika ibada hayapaswi kuwa maombi yanayogusa kila sehemu ya ibada yanatakiwa
kuwa ya kifupi na yenye viini viwili yaani kuabudu na dua ya kumuhitaji Mungu
yanatakiwa yamtukuze Mungu na kuhiytaji Baraka zake kwaajili ya ibada
2.
Maombi
ya kichungaji.
Maombi ya msingi sana mi maombi ya ibadani haya huitwa maombi
ya kichungaji kwa sababu hutolewa na mchungaji ni maombi kwa ajili ya kondoo ni
marefu kisi kuliko maombi mengine lengo lake kuu ni kushukuru, kuomba toba kwa
ajili ya watu wote, dua na maombezi kwa ajili ya shida za watu wengi wa
wachungaji huyafanya maombi ya jinsi hii mwishoni mwa ibada
3.
Maombi
kwa ajili ya sadaka.
Hii ni aina ya maombi inayotolewa katika uhusiano na sadaka
inweza kuwa kabla watu hawajatoa au baada ya watu kutoa maombi haya hulenga
kubariki zawadi za watu walizozileta kwa Mungu
4.
Maombi
baada ya mahubiri.
Ni aina ya maombi yatolewayo baada ya mahubiri watumishi wengi
wa Mungu huombea watu baada ya mahubiri maombezi haya hulenga kjuombea watu
toba, au magonjwa au kuhitimisha ibada au mahubiri na kujikabidhi tena kwa
Mungu
5.
Maombi
ya neema.
Ni
maombi yatolewayo mwishoni kabisa mwa ibada kwa ajili ya kuwabariki watu
ingawaje yanapaswa kuwa mafupi sana “Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo
wa Mungu Baba mwenyezi na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote amen”
NAMNA YA KUOMBA
Sio
tu kwamba kuna aina tofauti za maombi lakini pia kuna aina tofauti za uombaji
1.
Maombi
huria aina hii ya maombi katika ibada ni maombi ambayo kiongozi wa ibada
anaacha kila mmoja ajiombee kwa namna iwayo yote atakayo au maarufu kama Roho
atakavyokuongoza haya ni maombi
yanayotoka katika moyo wa muombaji na huomba kwa kadiri ya muda uliotolewa aidha kunaweza kuweko na uingiliaji kati wa
kiongozi wa ibada kuelekeza nini cha kuombea kama toba ,kujitakasa na shukurani
kisha kila mmoja kujiombea kama atakavyo, aina hizi za maombi ndio maombi
yaliyoombwa sana nyakati za kanisa la kwanza , inatumika na itaendelea
kutumika tatizo kubwa la maombi ya aina
hii ni uwezekano wa kukosa utaratibu lakini ni maombi mazuri na yenye nguvu za
Roho na uponyaji
2.
Maombi ya
mpangilio ya jumla hii ni aina ya maombi ambayo huandaliwa kiongozi aweza
kupangilia nini kiwemo katika maombi na namna gani atatumia aina za maombi
katika ibada anaweza kuandaa aina za
maombi na kuyachanganua wanaweza
kuytaandika ubaoni au kuyasoma kwa waombaji ingawaje maombi haya ya mpangilio
yaweza kuwa na tatizo la utumiaji wa akili zaidi lakini huingia akilini na
kuonyesha umaana kwa wamini
3.
Maombi
yaliyoandikwa hii ni aina ya maombi ambayo imeandikwa katika vitabu mfano
ni sala ya Bwana ni miongoni mwa mifano ya maombi hayo
4.
Litania
hii ni njia ya maombi ya dua inayotolewa
na kiongozi huku waamini wakiitikia
aina hii ya maombi ni kama maombi ya mapatano ambapo kiongozi husoma
baadhi ya vifungu vya dua na kasha waamini huitikia inaweza kuwekwa katika
mtindo wa kuimba hivi mfano wa maombi hayo ni kama litania iliyotungwa na
Mwanatheolojia T.B. McDormand ambayo
alituna mfano wa litania kama ifuatavyo
Kiongozi;-
Mungu mwema mpaji wa kila kilicho chema
na kila kilicho kamili ambaye kwa ukarimu wako ulionyesha upendo wako kwa mwanadamu kwa
kumuumba kwa njia ya ajabu na kumuokoa kwa mwana wako Yesu kristo bwana wetu ee
bwana usikie kuomba kwetu
Waamini;-
Pokea shukurani zetu ee Bwana kilio chetu kikufikie
Kiongozi;-Kwa
hakika umeamuru majira na nyakati duniani umetupa chakula mali na watoto ee
bwana usikie kuomba kwetu
Waamini;-
Pokea shukurani zetu ee Bwana kilio chetu kikufikie
Kiongozi;-
upendo wako kwa wenye dhambi, wadahaifu na
kujali kwako wanadamu na kwa
neema na rehema zako kupitia mwokozi wetu kwa imani tunakuwa washindi zaidi ya
kushinda dhambi na mauti ee bwana usikie
kuomba kwetu
Waamini;-
Pokea shukurani zetu ee Bwana kilo chetu kikufikie
Mwishoni kwa pamoja waamini wote
humshukuru Mungu.
5.
Maombi ya
kukemea ni aina nyingine ya maombi ambayo pia kiongozi wa maombi huingilia
kati kutoa maelekezo ya nini cha kuombea
anweza kusema hebu na tuombe kwa ajili ya wagonjwa na kisha kila baada
ya maombi watu wanaamuriwa kukemea kwa
nguvu utendaji wa ibilisi wakitumia mamlaka waliyopewa na kuangusha ngome na kuyteka nyara kila
fikra ipate kumtii Kristo ni maombi yenye nguvu na uweza na kila muamini hufurahia
Baraka za kiroho anapoomba aina hii ya maombi
6.
Maombi ya
kimyakimya hii ni aina ya maombi ambapo kiongozi wa ibada ataruhusu mkutano
kuomba kimyakimya ingawaje aina hii ya
maombi inahitaji inahitaji kutoa muda wa kutosha kwa msingi hiuo maombi hayako katika mfumo wa
aina moja ya maombi kuna hazina kubwa sana ya aina za maombikwa msingi huo
inashauriwa kutumia aina mbalimbali za maombi na sio aina moja tu ya maombi
ikakazaniwa
Mambo ya kuzingatia ni
kuwa
-
Kiongozi wa maombi anaweza kuwa mchungaji au mtu
yeyote mwenye ukomavu wa kiroho kama mashemasi au wazee wa kanisa wanaweza
kuongoza maombi
-
Maombi yatolewe katika namna ambayo ni rahisi
kwa waamini kukumbuka
-
Sauti katika maombi iwe yenye kusikika
-
Maombi lazima ikumbukwe kuwa yanaelekezwa kwa
Mungu na sio kuzungumza kitu kuhusu Mungu kwani kuna wakati wa kuhubiri na
wakati wa kuomba
SURA YA TISA MAHALI PA KUABUDU.
Nyakati za Agano la kale kazi ya kuabudu
ilifanyika katika hema ya kukutania, mahali hapa uwepo wa Mungu ulipafunika na
ile hema ikajawa na utukufu wa Mungu Kutoka 40; 34-35, Baadaye Mfalme Suleimani
alijenga Heakalu la kwanza kabisa la kuabudia katika agano la kale na
alipolikamilisha alipaita mahali akaapo Mungu 1Wafalme 8;10-12 Kisha akaomba
dua hii
“Lakini je Mungu atakaa duniani? Mbingu
nahata mbingu za Mbingu haziwezi kumtosheleza jinsi gani hekalu nililojenga
lilivyo dogo kwake Lakini sasa ee Bwana uisikie dua ya mtumwa wako niombayo Kwa
rehema zako ee Bwana Mungu usikie kilio cha mtumishi wako na maombi ya mtumishi
wako ninayoyaomba hivi leo, Macho yako yafumbuke kulielekea hakalu hili usiku
na mchana, mahali hapa ulipopatakja ukasema, ukasema hapa ndipo litakapokuwako
jina langu ili uyasikie maombi ya mtumwa wako aombapo akikabili mahali hapa, uisikie
dua ya mtumwa wako nay a watu wako Israel watakapoomba wakikabili mahali hapa
naam sikia huko mbinguni nawe usikiapo samehe….” 1Falme 8;22-53. Nyakati za
agano la kale Mungu alichagua mahali ili apaweke jina lake hapo na mahali hapo
watu wangeelekea kuabudu mahali hapo palikuwa ni lazima kwa ajili ya ibada
mwanzoni Mungu aliagiza kuhusu Ujenzi wa hema ya kukutania kama mahali pekee pa
kuabudia lakini baadaye Suleimani alijenga Hekalu na baada ya uhamisho wa
babeli kulikuja maswala ya masinagogi ambayo kwa asili ndiyo yaliyotuletea
makanisa pamoja na kuwa misnbgi wa ibada ni rohoni lakini kwa namna moja ama
nyingine inatupasa kukusanyika kama ilivyokuwa nyakati za kanisa la kwanza
Matendo 2;46, aidha Kristo mwenyewe ingawa alikuwa Mungu na alikuwa wa Kiroho
kuliko mtu awaye yote hakuacha kamwe kuelekea katika nyumba za ibada Luka 2;49
aidha mitume na watakatifu waliotutangulia waliheshimu ibada za pamoja na saa
maalumu zilizowekwa kwa ajili ya kuabudu Luka 2;36-37,24;53.Matendo 3;1,pia
walifurahi kuweko nyumbani mwa Bwana zaburi 84;1-2,10 na 122;1 kwa nini Biblia
inasisitiza kuelekea nyumbani kwa Bwana? Kumbukumbu la Torati 12; 25 “Lakini
mahali atakapopachagua Bwana Mungu wenu….apaweke jina lake maana ni makao yake
mahali hapo ni lazima uende” aidha inasisitizwa kuwa yusiache kukusanyika
Waebrania 10;25 hivyo basi mahali pa kuabudu ni lazima kwenda.
Leo
hii waamini wanaabudu katika nnjia iliyo bora zaidi kuliko zile za agano la
kale lakini wapi ni mahali sahii pa luabudia leo? Leo hii ni muhimu kufahamu
kuwa mahali pa kuabudia sio swala swala ni mkao wa mtu anayeabudu moyo wake
ukoje? Hapa simaanishi kuwa yale majengo yetu tunayokutania kuabudiu yawe
mabaya au yasiheshimike hapana Mungu ameweka jina lake hapo na ni lazima uende
huko kuabudu lakini Muhimu ni mkao wa moyo wa muabudu na uhusiano wake na Mungu
ulivyo mahali pa kuabudu pako na Yesu mbinguni soma Waebrania 3;6, na makao ya
mungu leo ni watu wake Mungu sasa anafanya makazi katika mioyo ya wanadamu na
ndio maana nakazia tena kuwa swala la ibada ni mkao wa moyo wa muhusika, Yesu
alisema walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu name niko katikati
yao unaona Mungu anaweza kuwako kokote pale ambapo watu wamekusanyika kwa ajili
yake kwa faida yake kwa moyo unaoelekea kwake, kwa hivyo hata mtu binafis
akitaka kuabudu anaweza kuabudu pake yake , lakini bado anapaswa kuyatiii
maandiko kwani yanakazia kutokuacha kukusanyika.
Mahali
pa kuabudu nyakati za agano la kale palikuwa ni mahali pa kuheshimika sana
Kristo pia alikemea wale waliokuwa wakiidharau nyumba ya Mungu na kulifanya
kuwa pango la wanyang’anyi hata leo tunapaswa kuendelea kuheshimu mahali
panapofanyikia ibada bila kusahau mioyo yetu kuandaliwa kama sehemu muhimu ya
ibada unaloliona ni mfano wa hekalu lililojengwa na Herode mkuu na kutumiwa
wakati wa Yesu hii ni ramani yake huko Israel ikiwa imejengwa kwa mfano Picha
na maelezo kwa hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote
SURA YA KUMI KUABUDU BINAFSI NA KUABUDU KIFAMILIA
Ni muhimu sana pia kufikiri kuhusu kuabudu
binafsi pamoja na kuabudu kifamilia
kwani vyote kwa pamoja vinakamilisha uabudu wa pamoja na ibada hizo zote
ni muhimu kwa ajili ya kufikia kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo
yaani ukuaji au ukomaaji wa Kiroho
Kuabudu Binafsi
Kuabudu Binafsi ni kwa muhimu sana kwa
ajili ya ukomaaji wa kiroho na kukua kiroho katika maisha, wakristo pia
wanapaswa kutiwa moyo katika swala zima la kujihusisha na kuabudu binafsi na kujitoa ingawaje hakuna mpangilio maalumu
wa namna ya kuabudu kwa msingi huo namna ya kuabudu Binafsi inaachwa kwenye
uwezo wa muhusika Binafsi kwani ibada binafsi ni maswala ya mtu binafsi na
Mungu wake na unapotoa Muongozo itakua
ni swala la kukazia kulikopita mipaka na
itakuwa ni mapngilio wa swala la kidini zaidi kuliko uhusiano binafsi wa Mtu na
Mungu wake ingawaje wale wenye tabia ya ibada binafsi na kujitoa wanaweza kuwa
na vidokezo muhimu vinavyoweza kuwasaidia wengine katika tabia ya ibada za
binasfi mambo ya msingi ya kuzingatia katika utendaji wa Ibada binafsi ni
pamoja na ;-
1.
Mahali
pa Ibada
Mahali pa kufanyia
ibada ni muhimu sana kwa mtu anayetaka kuwa na ibada binafsi kwani kama ilivyo
kwa ibada nyinginezo kufanyia katika mazingira ambapo familia iko karibu nawewe
kunaweza kuifanya ibada hiyo kuingiliwa na mambo mengine na hivyo kuharibu usikivu unaohitajika kwa
hiyo wapi pa kuabudu mara nyingi huchaguliwa na muhusika kulingana na maeneo
husika kama ni nyumbani,Kazini ak katika jamii wengine hujibanza katika kona ya
chumba na kukutana na Mungu hapo na
usomaji wa Biblia unaweza kufanyika katika meza, baadhi ya wakristo huamua
kwenda kanisani kwa malengo hayohayo ya Ibada binafsi, wengine wanavyo vyumba
maalumu kwa ajili ya maombi, wengine hufanyia maombi yao makazini wakati wa
mapumziko ya chai au chakula wao huyatumia kwa maombi mahali pa utulivu, au
wengine nyumbani wakati watoto wanapokuwa wamekwenda shule na wengine kama kina
mama hata jikoni vyovyote iwavyo jambo
la msingi ni kupata eneo zuri lenye utulivu litakalokupa mtazamo wa kuweza kuabudu Binafsi
2.
Muda
wa inada Binafsi
Hakuna muda maalumu
wa kuamua kufanya ibada binafsi kwani unaweza kuwa katika kuabudu Binafsi na
kuwa katika uhusiano wa kimaombi na Mungu kila wakati hata hivyo inashauriwa na
washauri wa kiroho kuwa na wakati maalumu wa kuomba au kuwa na ibada binafsi
ingawa biblia inasema ombeni bila kukoma lakini ni muhimu kuwa na namna muda
maalumu wa kufanya ibada binafsi ingawa
nmna gani utapanga muda inategemea au inaachwa katika uwezo wa mwabudu mwenyewe
kwani ni yeye anayeyajua mazingira yake wengine wana nafasi asubuhi, wengine
jioni au wengine hutumia muda wa kuelekea kulala kwa ajili ya ibada binafsi
ingawaje asubuhi unaweza kuwa wakati mzuri wa kuanza na Mungu na jioni unaweza
kuwa wakati mzuri wa kujichunguza na kumshukuru Mungu kwa uongozi wake wa kutwa
nzima na Baraka zake kwa hiyo haijalishi
ni Muda gani vyovyote iwavyo lakini ni vema kuanza na Mungu na kumaliza na
Mungu
3.
Namna
ya kuabudu binafsi.
Tunaabudu vipi je
tunapiga magoti au tunakaa au tunasimama ni maswali ya msingi lakini jibu moja
haliwezi kumtosheleza kila mmoja kanuni kubwa nay a msingi ni kuabudu katika namna ambayo itakuwa nyepesi
kwako na yenye kukufanya ufurahie na unayoiona kuwa inatoa heshima kwa mungu na
kuonyesha unyenyekevu na heshima kwa
msingi huo wengine hupenda kupiga magoti
wanapoomba au kusoma Biblia
wengine wanakuwa wameketi kimya na wachache hupenda kusimama jambo la msingi mkao huo ukupe tu muda wa
kutosha kuweza kutimiliza ibada yako binafsi uliyoikusudis kuifanya
4.
Ibada
yenyewe inakuaje?
Wengi wanaweza
kuuliza maswali kama ni utaratibu gani unaweza kufuatwa na ni kitu gani
kitumike kwa ajili ya ibada ya binafsi hapa pia funguo kuu ni kila mmoja yuko
hurukufanya apendavyo katika ibada binafsi
ingawaje matukio Fulani yatakuwa ni ya kawaida kama ilivyo katika ibada
nyinginezo kwa msingi huo ili mtu aweze kuabudu Binafsi aweza kuimba wimbo wa
kuabudu au tenzi za Rohoni kwa ajili ya kujiandaa na kuyapeleka mawazo yake kwa
Mungu , wengine huanza kwa kujisomea neno la Mungu katika kifungu Fulani anachochagua
cha kibiblia au kutumia kalenda za usomaji wa Biblia kila siku baadaya anaingia katika kuomba maombi yanaweza kuwa ya aina yoyote katika
aina zile za maombi tulizojifunza kuhimidi,kushukuru,dua, kuombea wengine, au
vyinginevyo kama Roho wa Mungu anavyokuongoza au moyo wako upendavyo, katika
ibada Binafsi maombi ya kumuabudu Mungu yaani kuhimidi ni ya muhimu sana ,
kujitoa pamoja na kushukuru hatimaye unaweza kuiombea familia na mahitaji yako
binafsi au kuombea shughuli za kikanisa jamaa na marafiki au ndugu aliyerudi
nyuma na kwa mahitaji mengine ya
wakristo usomaji wa maandiko unaweza kusaidia katika toba na kujitoa upya kwa
Mungu ibada Binafsi ni maombi ya kipekee yasiyoingiliwa na mtu kwa msingi huo
kila mmoja na afanya kama anavyojisikia bila kuingiliwa au kupata maelekezo
Fulani tabia ya kufanya ibada binafsi hupelekea katika kufungua mlango wa
ukuaji kiroho.
Ibada za kifamilia
Kuabudu kifamilia ni moja ya jambo la
muhimu sana katika maisha ya kiriho na kujitoa kwa Mungu kila familia inaweza
kuwa na ibada hizi mara kwa mara ibada za namna hii zinasaidia katika kushirikiana ukuaji wa kiroho na
huweza kusababisha badiliko kubwa la jamii kwa viwango vikubwa kama
ikizingatiwa
Ugumu au kikwazo cha ibada za kifamilia
Ziko familia nyingine ambazo watu ni
wafanya kazi na watoto ni wanafunzi na wakati mwingine hurudi kwa muda mmoja
kila mtu akiwa amechoka kwa sababu ya shughuli mbalimbali, na kutokana na
shughuli mbalimbali ulimwenguni kunaweza kukaweko na ugumu Fulani katika
utekelezaji wa ibada hizi ingawaje zamani ibada za kifamilia lilikuwa ni jambo
la msingi na linalofanyika karibu katika kila familia za wakristo hata hivyo njia pakee inayoweza kusaidia
katika utekelezaji wa ibada hizi ni mipango, Ibada hizi huzikutanisha familia
pamoja na wote kwa unyenyekevu hukaa pamoja na kuungana katika kumuabudu Mungu
kwa pamoja na kujenga imani moja na roho moja Ayubu mtumishi wa Mungu alikuwa
hodari kama kuhani wa kuingilia kati na kiongozi wa ibada kwa ajili ya familia
yake Ayubu 1;5. Ibada hizi hupanda kitu katika mioyo ya watoto na kuandaa
kizazi kijacho kuweza kupokea roho na moyo wa uchaji Mungu mara nyingi katika
ibada hizi wanafamilia huimba nyimbo na kasha Baba au mama husoma neno la
Mungu kisha wanafamilia hutoa mchango
wao namna walivyolielewa neno kisha wote
huingia katika maombi ibada za kifamilia zinaweza kuchukua Muda wa Nusu saa tu
familia zinazofanya ibada za pamoja hujenga uwanja mzuri wa ukuaji wa kiroho na
kujenga umoja wa kifamilia ibada za kifamilia zinaweza pia kufanyika katika matukio
kama haya yafuatayo
a.
Chakula
cha pamoja – wanafamilia wanweza kufanya ibada yao muda mfupi kabla ya kula
chakula maarufu kama chakula cha neema
b.
Mna weza kufanya ibada za kifamilia kwa wiki mara moja kama endapo ratiba zenu zinzkuwa zimebana na
hivyo siku kama za mwisho wa wiki ni nzuri kwa ajili ya ibada ya pamoja hii
inaweka heshima kwa wanafamilia kuweza kuheshimu ule muda unaokusudiwa kwa
ibada ya pamoja
c.
Mna weza kutumia
pia tukio kubwa kama sehemu ya kuabudu pamoja matukio haya ni kama vile
anapozaliwa mtoto, harusi sikukuu za kukumbuka kuzaliwa na matukio mengine yanayoweza kuikutanisha
familia pamoja kwa kusudi la kuabudu
d.
Wakati wa
magumu - kama familia inapitia mambo
magumu mfano tatizo la kifedha , magonjwa
mijadala ya kifamilia basi muda kama huo unaweza kutumika kwa ajili ya
ibada ya pamoja
e.
Nyakati za kufanya uamuzi – inapotokea wakati wa
kufanya maamuzi Fulani ya kifamilia kam shamba liuzwe au lisiuzwe n.k. pia
familia inapokutana kwa hali kamqa hizo watu wanaweza kufanya ibada
f.
Kila
jumapili – hii ni ibada ambayo inaweza kufanyika kila jumapili jioni kabisa
au usiku tifauti na ibada za kanisani ibada za pamoja kifamilia zina faida
kubwa sana na zinajenga umoja nakuleta
nguvu hususani wakati wa mambo magumu vyovyote itakavyo fanyika kwa wakati
wowote ukweli unabaki kuwa ibada za kifamilia ni muhimu na zina msaada mkubwa
sana Bwana ampe neema kila mmoja kuwa na uwezo wa kuzufanya ibada hizi.
Faida za kuabudu pamoja
Moja ya faida kubwa ya kuabudu pamoja ni
kupata neema ya kuifanya familia iwe na ukristo uliofunzwa kivitendo kuliko kwa
maneno hii itawafunza watoto wawe na ujuzi wa kuabudu zaidi ya ule wanaoupata kwa kuabudu pamoja
kanisani ibada inakuwa ni sehemu ya
asili ya maisha ya familia aidha matatizo ya kifamilia yanatatuliwa lupitia
maandiko mnayojifunza nyumbani watu wanajifunza kumtumaini na kumtegemea Mungu
,familia inamuona Mungu akihusika moja kwa moja na maisha yao kupitia kujibiwa
kwa maombi yanayoombwa pamoja kiufamilia, kunakuwa na ugumu kwa wanafamilia
kuiacha imani , watu watajadili maswala ya kifamilia katika mtazamo wa Kikristo
inakuwa ni njia ya kupandikiza imani kwa watoto kwa msingi huo basi ni muhimu
kwa wazazi kuwa na ujuzi wa kutosha kuhusu Mungu na Neno la Mungu ili
kuwarithisha watoto imani iliyo sahii hii itawafanya watoto kuwa wema.
Kuabudu kwa kikundi au makanisa ya nyumbani
Mtindo huu hauna tofauti na ibada za
kifamilia isipokuwa tofauti ni kuwa hapa sasa mnakutana aidha kundi Fulani au
wana mtaa Fulani kwa kusudi la kumuabudu Mungu pamoja ibada hizi ni muhimu pia
kwa ajili ya kuifikisha injili kwa wengine ibada za vikundi zinaweza labada
kukutanisha wafanyakazi wa eneo Fulani au wafanya biashara au wanafunzi walioko
mbali na kanisa au nyumbani hizi nazo ni ibada njema na zenye mafanikio makubwa
sana ya kuwalea na kuwasaidia katika makuzi ya kiroho.
SURA YA KUMI NA MOJA KUABUDU KATIKA MAISHA
Mara nyingi sana inasisitizwa kuwa makini
na ibada za sdanamu kuna jaribu wakati wote la kujaribu kuabudu vilivyoumbwa
kuliko muumba wakati mwingine inaweza
kuwa sio rahisi kugundua kuwa umeabudu sananmu lakini unaweza kujikuta unaabudu
bila kujua ibada inapokuwa haina matokeo
yenye kuwafanya watu kubadilika au wakristo kuishi maisha ya ushindi ndipo inapotokea
kuwa hata kama hakuna sanamu ya kuonekana kwa macho basin tayari ibada ya sanamu
inakuwa imechukua nafasi ibada yoyote ya kweli ni lazima iwe na matunda
1.
Lazima
watu wamuhisi Mungu
Kila watu
wanapokuwa wamekutana na Mungu kunakuwa na badiliko jipya linalochukua nafasi
kunakuwa na athari ya kiungu kila wakati muamini anapokuwa amekutana na Mungu,
maisha yanakuwa ni yenye kutiririka kwa uhusiano na Mungu Mungu hawi wa
jumapili tu bali anakuwa ni wa mtu huyo siku zote Mungu anakuweko kazini shuleni na kila mahali
mtu anakokwenda
2.
Kuabudu
kwa Ghafla
Inapotokea kuwa
watu wamemuhisi Mungu na kujenga uhusiano naye na kuwa na tabia endelevu ya
kuabudu asubuhi na jioni kuna uwezekano wa kutokea nafasi za ghafla za
kuabudu ambazo huweza kusababishwa na
Mungu mwenyewe kwa kadiri mwamini anavyokuwa makini katika kuutunza uwepo wa
Mungu maishani mwake hii inaweza kutokea
hata wakati wa mambo magumu
3.
Utumiaji
mzuri wa mali na vyeo na muda
Kadiri mtu
anavyokuwa na uhusiano mzuri na Mungu katika maisha pia anajikuta kuwa
anawajibika katika kila eneo la maisha kuwa kama wakili wa Mungu akitambua kuwa
Mungu Mungu amempa dhamana ya kila kitu ikiwemo muda, cheo na mali tulizo nazo
tunajiona kuwa tunawajibika kwa kila kitu katika Mungu hii ndio maana Taifa linalomcha
Mungu hufanikiwa katika kila eneo ikiwemo utendaji bora aidha waamini watatoa
zaka kwa uaminifu na kupenda watu wote bila ya ubaguzi mtu akijitoa kwanza kwa
Mungu ndipo anapokuwa na nafasi ya kujitoa nay eye mwenyewe 2Koritho 12;14
4.
Utumiaji
wa Mudaau kuukomboa wakati
Mwabudu wa kweli
siku zote atatoa wakati wake kwa Mungu Muda ni maisha na unapozungumzia kuabudu
maana yake unazungumzia kutoa muda kwa ajili ya Mungu hii ni gharama na ndio maana mtume anatoa mwito wa kuukomboa
wakati Efeso 5;16 Muda ni maisha na kama maisha yanatolewa kwa mungu maana yake
lazima uutoe muda wako kwa hivyo mwabudu wa kweli atakuwa na wakati wa kuokoa
muda apate nafasi ya kujitoa kwa Mungu muda utakuwa kitu cha maana kwake
5.
Kumtumikia
Mungu
Kwa asili muitikio
wa kuabudu katika roho na kweli hujumuisha pamoja na kumtumikia Mungu kwa
sababu kadiri unavyomuabudu mungu kunazaliwa kiu au shauku ya kutaka kuibebe
bendera yake yaani kumtumikia Warumi
12;11, wote kama wanafunzi wa biblia tutakuwa tunafahamu kuwa Isaya alipata
witowa kumtumiukia Mungu akiwa hekaluni yaani katika Ibada na
kama mwitikio wake katika kuabudu alisema ndio nitume mimi bwana Isaya
6;8 Yesu alimuuliza Simeon je wanipenda
kama unanipenda basi lisha kondoo zangu kumbe kumpenda kwetu Mungu kunaweza
kuhitimika katika kujitoa kwa kweli na kumtumikia Yohana 21. Nitengeeni barnaba
na sauli kwa kazi ile niliyowaitia ni maneno ya Roho Mtakatifu kwa watu
waliokuwa wakimuabudu huko antiokia Matendo 13;1-3.
6.
Kujitambua
kama mwana wa Mungu
Kadiri tunavyomuabudu
Mungu kama baba hatuwezi kuepuka ukweli wa utambuzi kuwa sisi ni watoto wa
Mungu na watoto wa baba mmoja hii inatuunganisha na wana wa Mungu wengine
duniani na inaua ubaguzi wa kila aina kadiri unavyoabudu na kuona Baraka za
Mungu zikimmiminikia kila mtu ndivyo unavyoweza kutambua kuwa Mungu hana
upendeleo Matendo 10 ; 34-35 tutajitambua kuwa wote ni warithi wa Mungu
7.
Kuendelea
kuwa watakatifu
Kadiri mtu
anavyokuwa mwabudu ndivyo anavyopata utambuzi wa kuwa anahitaji kujitoa zaidi
ndio kwani tunamuabudu Mungu aliyemtakatifu Isaya 6; 1,5. Mtu anapomkaribia
Mungu hujiona kuwa na mapungufu hupata nafasi ya kujichunguza Isaya alisema ole
wangu na kupata neema ya kutakaswa Biblia inatuamuru kuwa watakatifu hakuna
namna yoyote ile inayoweza kutusaidia kuishi maisha matakatifu kama sio Ibada
1Petro 1; 15 Efeso 4;1
8.
Kushuhudia
wengine
Kuabudu wakati wote
husababisha ushuhuda kwa wengine kwani kushuhudia, kunatukumbusha tendo la
Mungu la kumkomboa mwanadamu kwa niaba yetu hii inatokea pale mwana wa Mungu
anapokuwa ameacha dhambi na kujitoa na kujitakasa huweza kupata naffasi ya
kubadilika kitabia na mwenendo na kuwafundisha wakosaji zaburi 51;9,13 na kule
kuabudu kunatupa msukumo wa kujali wengine na kuwashuhudia injili Matendo 1;8
9.
Kuishi
kwa matumaini
Kuabudu
kunaqmpa muamini uhakika kuwa ataishi milele ni wazi au bayana kuwa kuna uzima
wa milele au kuna maisha baada ya kufa
na kuwa Yesu ndio ufufuo na uzima Yohana 11;25-26, 14;2-3 10;28 kadiri
mtu anavyomuamini Mungu aliye hai ndani yake kunakuweko tumaini lililo hai ya
kuwa ataishi milele hata baada ya juondoka ulimwenguni pia wanaobaki
hawasikitishwi na maisha maovu uliyoishi duniani watasikitika kuwa umejitenga
mbali nao lakini watakuwa na uhakika kuwa uko mahali salama kwa sababu ulikuwa mcha
Munguhebu basu tujijengee mazoea ya kumuabudu Mungu wetu ili tuwe na tumainai
lililo bora Zaburi 95;6-7
SURA YA KUMI NA MBILI WAJIBU WA KIONGOZI WA IBADA
Yesu kristo alichagua viongozi ambao
aliamini kuwa watakuwa msaada kwa waamini wengine kwa ajili ya kuawaidia katika
kuwafundisha na kuwasaidia katika ukuaji wa kiroho na maswala ya kuabudu Ni
yeye (Yesu) anayetoa wengine kuwa mitume na wengine kuwa manabii na wengine
kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu kwa kusudi la kuukamilisha
mwli wa kristo Efeso 4; 11-16.katika kifungu hiki tunajifunza mambo ya msingi
nay a muhimu kwa viongozi wa kiroho na wajibu walio nao
1.
Kwamba viongozi wa kiroho yaani mitume manabii
wainjilisti wachungaji na waalimu ni zawadi inayotolewa na Mungu kwa kanisa
2.
Viongozi hawa ndio wanaoandaa watu kwa ajili ya
kazi ya huduma
a. Kuujenga
mwili wa Kristo
b. Kufikisha
watu kwenye umoja wa imani na maarifa ya kumjua kristo
c. Kuwafanya
watu wawe kama Kristo
Kwa
msingi huo utaweza kuona kuwa wajibu huu ni mkubwa na hakuna mwanadamu wa
kawaidia anayeweza kuutimiza pasipo msaada wa Roho Mtakakatifu kumbuka kuwa
viongozi hawa ndio kichwa kwa mwili wa Kristo hapa simaanishi ile maana ya
kuchukua nafasi ya Kristo kama kiongozi mkuu wa kanisa bali nazungumzia ile
hali ya viungo vya mwili basi viongozi ni kichwamaisha ya waumini au kundi la
mahali pamoja linategemea sana na aina ya kiongozi waliye naye wote tunafahamu
kuwa kuna aina nyingi za uongozi lakini ziko aina tatu za uongozi
1.
Viongozi wa imla Authoritarian leader – hawa ni viongozi
ambao katika maongozi yao hakuna mtu mwingine anaweza kufanya jambo mpaka yeye
aseme ni wenye amri na kuamrisha yeye ndiye mamlaka ya mwisho
2.
Kiongozi huria au ruksa Pamissive leader – Huyu
ni kiongozi ambaye huliacha kundi liamue ni namna gani linaweza kuendesha mambo
na kuamua kila kitu huyu ni ruksa
3.
Kiongozi mshiriki Participatory leader – huyu ni
kiongoshi wa kidemokrasia aanahamashisha lakini anashiriki anaongoza kwa
kuwaacha watu huru lakini anasimamia utaratribu uweze kufuatwa
Viongozi
ambao wamechaguliwa na Mungu wanajitoa kwaa jili ya maswala ya kiungu na
kluwajibika kwa kila jambo katika kuhakikisha kuwa ibada zinafanyika sawa na
mapenzi ya Mungu kwa msingi huo tunasema kuwa wachungaji ndio viongozi wakuu wa
ibada lakini kwa bahati mbaya wengi wao hawafikiri kuwa wao ni viongozi wa
ibada Mtu moja aliwauliza swali baadhi
ya wachungaji vyuoni kuwa ni kazi gani ambayo ni wajibu wenu wengi walisema kuwa wao ni wachungaji na
majibu machache tu yalijibu kuwa wao ni viongozi wa ibada hii ni jambo la
kushangaza kwani wachungaji wengi hawajujui kuwa wao ni viongozi wa ibada na
hivyo wanashindwa kuwa na Muda wa kupanga namna ya kuendesha ibada wanachukua Muda mwingi kujiandaa kwa ajili ya
jumbe lakini hawachukui muda kuandaa mpangilio mzima wa ibada
Viongozi wa ibada ni makuhani na ni
manabii huiandaa mioyo ya watu na kuhakikisha kuwa inapatana na Mungu lakini
pia husema kwa niaba ya Mungu ujumbe wake kwa watu wake
SURA YA KUMI NA TATU VIZUIZI VYA KUABUDU
Wakati bwana Yesu alipokuwa akiwafundisha
wanafunzi wake kusali alisema Bali wewe usalipo ingia katika chumba chako cha
ndani na ukiisha kufunga mlango usali mbele za Baba yako aliye sirini na baba
yako aonaye sirini atakujazi Mathayo 6;6, Mungu hapendezwi na unafiki anataka
watu wamuabudu kwelikweli lakini kuna uwezekano wakati mwingine pasipo kuelewa
tukajikuta katika ibada za aina hiyo kwa sababu ya vizuizi mbalimbali vya
kuabudi miongoni mwa vizuizi hivyo ni pamoja na
1.
Kusudi
la shetani
Mpango mkuu wa shetani ni kuharibu kabisa makusudi ya Mungu na
kwa namna Fulani huweza kuwatumia hata wakristo wenyewe kuytimiza mpango wake
,Paulo mtume alitahadharisha kuwa shetani angejaribu kuwaharibu washirika wa
Koritho kwa namna ya kuwadanganya , mpango wake ni kuhakikisha kuwa ana harivbu
kabisa makusudi ya ibada yenye kumuelekea Mungu 2Koritho 11;3 “Lakini nachelea kama Yule nyoka
alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha
unyofu na usafi wa Kristo” Moja ya njia ambayo shetani huitumia katika
kuharibu mpango wa Mungu ni kuleta mafarakano na kuleta hali ya kuchanganya
shetani alifanikiwa kumtia hawa mashaka kwa kumfanya aamini katika uongo wake
uliokuwa unaonekana kama kweli kisha kuanza kuwekea mashaka kweli ya Neno la
Mungu akili zetu ndio uwanja wa vita kati yetu na ibilisi tukianza kumsikiliza
yeye badala ya Mungu basi taratibi tunaanza kuingia katika mtego Mwanzo 3;1-13.
Shetani atatupinga kwa kutumia tama zetu na kwa sababu hiyo itatupasa kumpinga
1Petro 5;8-9, atatumia hisia zetu hali za kujiona kuwa hatufai, wivu, faraka ,
masengenyo, na kutukatisha tama ili yamkini kwamba tuweze kuondoa mawazo yetu
katika Mungu,atatumia hali zetu za kuchoka na kutusumbua kwa shida ambazo
tutaanza kuziangalia hizo na kuacha kumuangalia Mungu atatumia watu wanaopagawa
na pepo kuharibu hali ya kuabudu na watu wanaochelewa ibada ambao watatliza
viatu vyao ili kutoa usikivu wa watu kutoka katika kuabudu na kumwangalia
aliyechelewa, hata hivyo tiukumbuke kuwa nguvu zake zina mipaka na kuwa
tukimuomba Mungu tunaweza kumshinda
2.
Kuipenda
Dunia
Ni muhimu kufahamu kuwa shetani anaweza kutumua pia hali za
kukuvuta kimawazo kutoka katika kufikiri maswala ya ibada na kuanza kufikiri
maswala ya kidunia hili si jambo la ajabiu si unakumbuka mkewe Lutu hata akatika
hali ya ibada ya kuokolewa na kuhukumiwa kwa sodoma yeye bado alikuwa akiipenda
Sodoma na hakuweko na tendo la kuokolewa kwawe halikuwa na maana, wakati wa
ibada sio wakati wa kufikiri watoto watakula nini, wapi utafanya shoping au
mkeo yukoje au kuruhusu mawazo ya kidunia tama na uasherti kutembea katika
akili zetu 1Timotheo 5;8, ni kweli Mungu ametutaka tuzijali familia zetu lakini
kuwaza wapi utapata fedha na kuitunza familia yako wakati wa ibada sio sahii
1Timotheo 6;10 utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na mengine yote
mtazidishiwa1Yohana 2;15-17
3.
Tabia
mbaya sizizofaa.
Hali yoyote ya maisha ya dhambi za mtu binafsi, kutokuomba na
tabia zisizofaa ni kizuizi kikubwa kwa ibada ni muhimu kufahamu kuwa Paulo
mtume aliwataka waamini kuwekqa mbali kabisa matendo ya mwili Warumi 7-8,
1Koritho 3;1-4 aina zozote za matengano na faraka na kutokuelewana ni kizuizi
kwa ibada , mtu awaye yote akitaka kumfuata Yesu anatakiwa kujikana nafsi na
kumfuata Mathayo 16;24,Marko 8;34 na Luka9;23, aidha matendo yoyote
yasiyotokana na utii husababisha kikwazo kwa ibada sauli alishindwa kutii na alijikuta
anakataliwa 1samuel 13;11-14 dhambi na mambo mengineyo mengi huweza kuwa
kizuizi cha ibada
4.
Mtazamo
mbaya
Wako watu ambao mtazamo wao sio mzuri sana katika maswala ya
kuabudu wana hali ya kukosoa kila kitu, wana uchungu na hawataki kusamehe, na
huwa na kiburi, hali kama hizo ni kizuizi kwa ibada soma Yakobo 3; 9-12 inasema
hivi
“Kwa huo twamuhimidi Mungu baba yetu na kwa
huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu katika kinywa kilekile
kwatoka Baraka na laana …..” watu ambao wanaebdekeza ukosoaji na kupingana
na neno la Mungu tayari aikili zao ziko mbali na Mungu aidha awaye yote ambaye
anakuja mbele za Mungu huku anajifikiri kuwa ni bora kuliko wengine hawezi
kujipatia kibali kwa Mungu Mungu nhuwapinga wenye kiburi bali huwapa neema
wanyenyekevu Yakobo 3;2 sisi sote runajikwaa katika mambo mengi na hivyo hakuna
mtu mkamilifu hatupaswi kuwa wahukumu wa wengine na kujifikiri kuwa sisi ni
bora kuliko wao eti kwa sababu wana udhaifu huu ama ule na sisi kujiona kuwa wenye
haki ibada ya kweli lazima isimamie msingi wa kuwa na upendo kwa wengine Mtume
Yohana anakazia kuwa huwezi kuwa na madai kuwa unampenda Mungu huku unachukia
wengine 1Yohana 3;10, 4;20
5.
Hali ya
kutokusamehe
Yesu alifahamu kuwa roho ya kutokusamehe ni
kizuizi kikubwa sana cha ibada na kwa sababu hiyo alitoa mafundisho yafuatayo;-
“Mathayo 5; 22-24 bali mimi nawaambia kila mtu amwoneaye ndugu yake
Hasira itampasa hukumu,…..Basi ukileta sadaka yako madhabahuni na huku
ukikumbuka ya kuwa ndugu yakko ana neno juu yako iache sadaka yako mbele ya
madhabahu uende zako upatane kwanza na ndugu yako…”ukweli ni kwamba hakuna
ibada bila kusamehe wala hakuna maombi bila kusamehe wala hakuna toba
kusamehewa bila kusamahe wengine kwanza mathayo 6; 12,14-15. Efeso 4;32 Biblia
ina sisitiza kusameheana kwanza kama Kristo alivyotusamahe
6.
Uchungu
Hata pale inapotokea kuwa wengine wanaweza
kutusababishia machungu ni muhimu kufahamu kuwa uchungu huo utaathiri ibada
zetu waandishi wa agano jipya wanaonya habari ya kuwa katika uchungu kuwa si
njema Matendo 8;23,Warumi 3;14,Efeso 4;30-31,Waebrania 12;15,Yakobo,3;14
7.
Kiburi
Hali ya kutokusamehe , kuwa na uchungu na
roho ya kukosoa kila jambo jema zinatupelekea kupeleka mawazo yetu kwa watu
zaidi kuliko kwa Mungu na pia hali ya kujiona kuwa sisi tulistahili jambo
Fulani na kwa msingi hio basi inajenga kiburi na kutuondoa katika mpango wa
Mungu Yakobo 4;6 “Mungu huwapinga wenye kiburi bali huwapa neema wanyenyekevu”
kama wakristo watakuwa na upendo wa kweli basi hali ya kujiona kuwa unafaa
itaondoka na tutawapenda wengine upendo haujivuni kiburi sio mfano wa
Kristo ni muhimu kukumbuka kuwa yeye
alikuwa yuna namna ya Mungu lakini alikuwa mnyenyekevu sana na mtii Wafilipi
2;5-8 mambo ya aina hii yote huiharibu ibada na kama tutaklazimisha kuabudu
huku hatukubali kuyaweka kando mambo hayo ibada hizo zitakuwa hazina faida na
tutatimiza mathayo 15; 7-9 unaosema “Enyi
wanafiki ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu akisema watu hawa
huniheshimu kwa midomo ila mioyo yao iko mbali name nao waniabudu Bure
wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu” unaona kumbe kuna
uwezekano wa watu kuabudu Bure tu yaani kuabudu pasipo faida mpendwa endapo
maswala hayo hapo juu yataonekana katika maisha yetu na tukayakubali kututawala
basi shetani atakuwa ametushindwa kwa kuwa tumekosa kuzitambua fikra zake
SURA YA KUMI NA NNE NAMNA YA KUWASILISHA IBADA
Ninapotaka kuzungumzia swala la
uwasilishaji ibada nataka nikuonyeshe kwanza stori ya mtumishi mmoja wa Mungu
ambaye alikuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa yaan Birthday mtumishi huyu
alikuwa na watoto wanne wote walikuja kumpongeza baba yao na kumpa zawadi wa
kwanza ambaye alikuwa na miaka 26 wa kike, alimpa zawadi ya Fedha baba yake kwa
ajili ya kutembea kokote atakako kisha akambusu baba yake na kumwangalia kwa
upendo, wa pili ambaye alikuwa na miaka 23
wa kike Yeye alichora picha nzuri sana na alimkabidhi baba yake kisha
akambusu na kumkumbatia na kumnong’oneza kwa sauti ndogo nakupenda baba, kisha
mtoto wa tatu mwenye miaka 21 wa kiume yeye alileta shati zuri kisha
akamvalisha baba yake mabegani na kumwambia wewe ni baba wa pekee duniani na wa
mwisho mwenye miaka 16 wa kiume alimpa baba yake saa aliyokuwa amenunua
safarini na kisha akamwambia Baba yake najivunia kuwa na baba kama wewe bila shaka
utaipenda zawadi hii.
Unajifunza nini katika mfano huu? Kila mtoto anayo namna yake ya
kuonyesha upendo na shukurani kwa baba yake na kama ambavyo kila zawadi ilikuwa
tofauti hali kadhalika namna walivyoonyesha upendo na maneno waliyoyatoa yalikuwa
tofauti je unafikiri kuna aliyempendeza baba yake zaidi kuliko mwingine? Bila
shaka hapana wote walimpendeza hivyo ndivyo Mungu anavyopendezwa na kila mtu
anayeonyesha upendo wake kwake na kwa msingi huo basi ni muhimu kufahamu kuwa
kila ibada kama imeelekezwa kwa Mungu katika hali ya kumpenda basi hata kama ni
tofauti na ile uliyoizoea Mungu anapendezwa nayo Najua wako watu wanaweza
kufikiri kuwa Ibada zao ni bora kuliko za wengine sikiliza mpendwa kila mtu
anayo namna yake ya kuonyesha kuwa anampenda Mungu hivyo basi kama utaishi
ulimwenguni humu na kutaka aina Fulani ya ibada uliyoizoea wewe na kufikia ngazi ya kudharau za wengine
tayari umejivuna na unamuhitaji Kristo je hujawahi kuona wakristo wakiruka
baadhi ya makanisa ambayo wangeweza kabisa kuabudu hapo labda yako karibu nao
kuliko kule wanakoelekea kuabudu lakini kwa sababu ya mazoea utawasikia aha!
Ibada za pale sijui zikoje mi sijazizoea haya si mazoea mazuri. Mungu
hupendezwa na kila ibada inayotolewa katika misingi ya uwazi, na wepesi, isiyohusisha
kujiangalia, yenye kanuni ya upendo, inayotoka moyoni na isiyo ya kinafiki
ibada inapozingatia hayo inakuwa imewasilishwa katika njia inayoweza kabisa
kumpendeza Mungu na haya ndio tunayoyaangalia hapa tunapozungumzia namna ya
kuwasilisha ibada.
1.
Lazima
iwe yenye msingi wa uwazi na rahisi.
Mara nyingi
kibinadamu huwa tunaogopa kuona wenzetu watatuonaje na hivyo tunashindwa
kujifunua uhalisia wetu kwamba sisi tukoje, Tunahofia kwamba labda wakijua
jinsi tulivyo wanaweza kutudharau au kupoteza heshima yetu,na ndipo unapokuta
kuwa tunajaribu kuficha hisia zetu, kila binadamu anapenda kukubalika kwa
wengine na ndio maana hali hii huathiri hisia zetu waklati tunapokuwa mbele za
Mungu katika kuabudu tunajarinbu kubania hisia zetu mtu anaweza kuwa anajisikia
kulia lakini akaogopa watu watamuonaje hii inatunyima uhuru na uwazi wa
kumuabudu Mungu kwa urahisi , Bila shaka unakumbuka mfano wa mama Yule
aliyekuwa akitokwa na Damu kwa muda wa miaka kumi na miwili kwa kuogopa
makutano aliamua kwenda kwa siri ili kugusa upindo wa vazi la Yesu na kupokea
uponyaji wake Luka 8;47-48 Mtu huyu alimgusa sana Bwana Yesu na Yesu alipohoji
kuwa ni nani aliyenigusa kila mtu alijaribu kukanusha lakini Yesu alimwambia
imani yako imekuponya tunao watu wengi wa jinsi hii ambao hurudi toka Ibadani
wakiwa bado hawajaguswa hisia zao kwa sababu hawako wazi kwa ajili ya
kuhudumiwa na Mungu
Tusikubali
kudanganyika kwani kuna wakati itatupasa kuwa wajinga ili tuwe wenye hekima
Paulo alitoa ushauri huu 1Koritho 3; 18, 21, 23. Wakati wa kuabudu acha
kujibana mwaga hisia zako zote kwa Mungu kwa uwazi na Mungu atakusaidia
Wakati wa kuabudu
kubali kukutana na uso wa Mungu, Yesu alipojifunua kwa Simeon Petro baada ya
kufanya muujiza Petro alijiona kuwa mwenye dhambi na kumwambia Ondoka kwangu ee
bwana mimi ni mwenye dhambi Luka 5; 8 lakini ujuzi wake kuhusu Mungu ulivyokua
unaendelea kukua hatimaye aliendelea kuambatana na bwana Yesu na alikuwa huru
na hakujikakamua kuubania kuonyesha utu wake bali hata kuonyesha udhaifu wake
kwa Yesu na Mungu hakumfukuza!
Mwanamke aliyekuwa
kahaba alikwenda kumgusa Bwana Yesu Lakini farisayao alikasirishwa na kufikiri
kama huyu angekuwa nabii yaani Yesu angejua kuwa mwanamke anayemgusa ni kahaba
jinsi gani.Lakini Yesu aliwajua wote yeye alijua mpaka mioyo yao alitambua kuwa
mwanamke huyu ni wa namna gani na kuwa mguso wake unahitaji msamaha wa dhambi
lakini farisayo hakuwa tayari kufunua hisia zake akijifikiri kuwa yeye ni
mwenye haki na huku akiwa hana habari kuwa anatawaliwa na kiburi, Ndugu yangu
sikiliza hatuwezi kamwe kumdanganya Mungu kuhusu jinsi tulivyo yeye anatujua na kumuabudu kwetu kwa namna ya kinafiki
kunatupelekea kutokumgusa lazima tutubu dhambi zetu na kukubali kuachilia wazi
hisia zetu kwa uwazi kwa Mungu na kwa urahisi
2.
Lazima
iwe isiyohusisha kujiangalia yaani kujiachia uwe huru
Tumeona mara kadhaa watu wakimjia Mungu kwa sababu ya shida za
ndani kabisa sifikiri kama kuna ubaya kwa hilo hata pale moyo wako unapokuwa
umeumizwa bado unaweza kuja kwa Mungu na kumueleza hisia zako majaribu yetu
hutuleta karibu na Mungu na wakati mwingine hutusaidia kutufanya tukomae kiroho
Yakobo 1;2-4 zaburi nyingi zinaonyesha hisia za watu waliopitia mateso ya aina
mbalimbali lakini yaliwaleta karibu na Mungu,Jambo la msingi ni kukubali
kujiachia na kutokujiangalia tunapokuja kwa Mungu katika ibada tuwe huru kuweka wazi hisia zetu na kujisahau
tukiabudu na kumsifu na kumtukuza kwa moyo
3.
Lazima
kuwe kwa kanuni ya Upendo
Mathayo 22;27-29 Amri kuu ni Upendo
kumpenda Mungu na kuwapenda jirani zetu, Tunamuabudu Mungu kwa sababu
tunampenda tunaimba nyimbo kwa sababu tunampenda tunapokuwa na wenzetu katika
makundi tunarudia tena na tena kuonyesha kuwa tunampenda Mungu, zaidi ya yote tunapoishi
maisha yenye kuonyesha kumpendeza Mungu au maisha ambayo Mungu anakusudia
tuyaishi ni kuonyesha wazi kivitendo namna tunavyompenda Mungu na lolote tulifanyalo
tunalifanya kwa sababu tunampenda Mungu namna hii ibada inakuwa katika kanuni
ya kufanya kila kitu kwa upendo na sio sheria, Hata hivyo kumpenda kwetu Mungu
hakuwezi kuwa kamili kama tutakuwa hatuwapendi ndugu 1Yohana 3;14 upendo wetu
kwa wengine unafunuliwa kama vile tuwapendavyo wana familia zetu,jambo hilin
litatufanya tumuhudumie kila mtu na kuwatumikia wote na kuwalinda wasikwazike
au kuumizwa moyo na kuwasaidia wote katika ukuaji wa Kiroho Mathayo
25;34-46.Paulo alimuamuru Filemoni kuonyesha pendo kama hili kwa Onesmo Filimon
4-7. Upendo unapokuwa ndio kanuni ya ibada uhusiano na Mungu utakuwa wenye
kudumu katika kusanyiko la ibada hivyo ni muhimu kukazia kanuni ya upendo
katika kusanyiko lolote lile ambalo linakusudia kumpendeza Mungu na kutaka
kuutunza uhusiano wao na Mungu Uwepo wa Mungu leo unaondoka makanisani au haupo
kabisa kwa sababu nyingi lakini mojawapo ni hii ya kupuuzia upendo makanisani
sasa kuna chuki,migawanyiko, kukosekana kwa amani upendeleo na hata ile tabia
ya samaki mkubwa kumeza mdogo,tajiri kuendelea kuwa tajiri na masikini kuwa
maiskini hizi ni hali halisi kwa makanisa yaliyofanikiwa kifedha huko mjini
kuyasahau makanisa masikini ya vijijini bila shaka hilo nalo ni neno kivitendo!
Ndani ya washirika na watumishi leo hakuna kuvumiliana, kuna kuchukuliana hatua
kwa haraka, kuna wivu, kuna tabia mbaya zisizo za kimaadili, hakuna utu wema, hakuna
uaminifu,hakuna kulindana, kila mtu anaonyesha umwamba, hakuna kusaidiana,
hakuna huduma ya kurejeshana, watu wana hasira za haraka, watu wanahukumiana,
wala hawajali na hawataki kukiri kuwa wamekosea, wanteteana kukandamiza
wanyonge, wanaiba sadaka n.k hii yote ni kwa sababu upedno wa kweli umetoweka
leo mahali pa jinsi hiyo ibada haiwezi kuwasilishwa vema
4.
Lazima
iwasilishwe pasipo unafiki
Yesu
alikuwa akifundisha juu ya ibada ya kweli na ibada ya kinafiki alitoa mfano huo
kuonyesha ni ainagani ya ibada inakubalika kwa Mungu Luka 18;10-14 Biblia
mahali hapo inasema
“Watu
wawili walipanda kwenda hekaluni kusali,mmoja farisayo,wa pili mtoza ushuru
,Yule Farisayo akasimama akiomba hivi
moyoni mwake Ee;Mungu nakushukuru kwakuwa mimi si kama watu wengin ,
wanyang’anyi,wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru, Mimim nafunga
mara mbili kwa juma,hutoa zaka katika mapato yangu yote.Lakini Yule mtosha
ushuru alisimama mbali wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali
alijipiga piga kifua akisema Ee;Mungu
uniwie radhi mimi mwenye dhambi”
Farisayo
alifanya kosa kubwa sana hakua anaabudu kabisa ibada ya kweli, wala hakumpa Mungu
utukufu na badala yake alikuwa akijitukuza mwenyewe alikuwa amejaa kiburi na
majivuno eti kwa sababu hakuwa mwenye kudhulumu wala mnyang’anyi, mzinzi au
mtoza ushuru, alijivunia swala la kufunga na kutoa zaka, kama kweli haya
aliyoyasema farisayo ni kweli na kuwa alikuwa akiyyafanya vyovyote iwavyo Ibada
yake ilikataliwa wala haikukubalika haya hayakuwa maombi bali yalikuwa ni
majivuna hii haikuwa ibada je hujawahi kuona wewe wahubiri wakijua wazi kanbisa
mahubiri ni sehemu ya ibada lakini wakiyatumia kuponda wengine na kujisifu
wakieleza mafanikio waliyo nayo na wake wazuri waliopewa na kuwaponda wale
wanaowaita kuwa wanajidai huku hawana kitu chochote cha ziada au kufumbia watu
mafumbo na mahubiri yamekuwa kama mipasho ya taarabu hayana hata chembe ya
utukufu kwa Mungu? Muda usingeliweza kutosha kukukonyesha jinsi waimbaji
wanaoitwa wa injili wakiimba katika nyimbo zao kama watu ambao nyimbo zao
hazimpi Mungu utukufu na badala yake zinajibizana na hali halisi ya habari zao
katika magazeti au kuwasema watu wa mahali Fulani , waiume zao, wanamuziki
wenzao, na hakuna tofauti na ile mipasho ya taarabu, fuatilia hata mahubiri
katika televisheni leo utaweza tu kujua kuwa wahubiri hao wanapondana na
wameacha kusudi la kuwafikia watu na kuwakutanisha na Mungu sasa wanasagiana Je
haya ndio makusudi ya kuhubiri katika vyombo vya habari, fuatilia katika
magazetiya Kikristo leo je yanatoa
mafundisho au yamejaa sera za kujipigia debe ili waendelee kuchaguliwa kwa mara
ya kadhaa kuwa viongozi wakubwa wa makanisa yao hayo yote yanatukumbusha kila
alichokifanya Yule farisayo ibada yake ilikataliwa
Ni muhimu ikumbukwe kuwa Yesu alitoa mfano
huu kutukumbusha juu ya watu ambao wanafikiri kuwa wana uhakika na yale
wanayoyafanya kama kwamba ni mapenzi ya Mungu hawa ni watu waliojikinai wenye
kujihesabia haki Luka 18;9, Isaya 64;6 Biblia inasema hivi katika Isaya 64;6 “Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye
mchafu,na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi,sisi
sote twanyauka kama jani na maovu
yetu yatuondoa kama upepo uondoavyo”Hakuna
hata mtu mmoja awezaye kusimama mbele za Mungu akiwa salama au anastahili je
wewe unastahili mbele za Mungu? Kumbuka ni kwa neema yake tu tunaweza
kumkaribia wala si kwa haki zetuTito 3;4-5 inasema hivi Lakini wema wake
Mwokozi wetuMungu na upendo wake kwa wanadamu ulipofunuliwa alituokoa si kwa
sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi bali kwa rehema yake kwa kuoshwa
kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu unaona! Kumbe wokovu
ni kazi ya Mungu, kukubalika kwetu kwake ni kazi yake hatuna cha kujisifia
Hubiri kwa unyenyekevu,imba kwa unyenyekevu abudu kwa unyenyekevu fanya kwa
moyo mkunjufu nauliopondeka na kwa upendo ndugu hakikisha ibada yako inapata
kibali mbele za Mungu kuabudu katika Roho na kweli ni rahisi lakini sio rahisi
kwa watu wanaojifikiri kuwa bora kuliko wengine. Endapo eneo hili limekugusa
ndugu msomaji wangu shirikiana name katika sala hii
“Mungu mwema ni wewe
ninayetaka kukutukuza, wala sio wengine wala sio mimi mwenyewe, wewe pekee
ndiye unayestahili sifa zangu, ninapokuja kwako kumwaga hisia zangu nisaidie
kujisahau na kukuangalia wewe ili kwamba matatizo yangu na mizigo yangu
isinizuie kukuona,Nifanye kuwa huru na kukupenda na Roho wa Mungu anisaidie
kuwa huru na kuniongoza ili nikuabudu kwa furaha,Nifanye kuwa mtumwa wa wengine
ninapokuabudu,lifanye pedno kuwa kanuni yangu ya ibada nikupende wewe na watu
wotena nikuabudu wewe kwa unyenyekevu na kuvunjika nisihukumu wengine bali
nikuletee wewe heshima na utukufu kwa ajili ya jina lako takatifu amen!
SURA YA KUMI NA TANO: KUABUDU HUKO MBINGUNI
Ibada iliyokamilika
Hakuna ibada iliyokamilika kwa sababu wanaoabudu pia hawajakamilika ni
huko mbinguni ndiko kutakuwa na ibada iliyokamilika kabisa, moja ya mambo
yanayotufanya tuwe na ibada isiyo kamilika ni kwasababu hatuwezi kuyafahamu
mambo ya Rohoni mpaka Roho wa Mungu aweze kutufunulia na ingawaje anaiganya
kazi ya kutufunulia lakini ni kwa sehemu, Mungu yuko katika ngazi ya juu sana
kuliko tulivyo wanadamu sisi tuna mipaka karibu katika kila eneo la maisha
lakini kule mbinguni ufahamu wetu utaongezeka na tutafahamu kwa ukubwa zaidi
machoyetu na fahamu zetu zitafunguliwa kwa upana zaidi na maswala ya kiroho
yatakuwa dhahiri kuliko sasa ambao tunaona kwa jinsi ya fumbo na kufahamu kwa
sehemu Biblia inasema hivi katika 1Koritho 13;9-12
“ Kwa
maana tunafahamu kwa sehemu na tunafanya unabii kwa sehemu lakini ijapo ile
kamili iliyo kwa sehemu itabatilika, Nilipokuwa mtoto mchanga nalifikiri kama
mtoto mchanga,tokea hapo nilipokuwa mtu mzima nimeyabatilisha mambo ya
kitoto,Maana wakati wasasa tunaona kwa kiookwa jinsi ya fumbo wakati ule
nitajua sana kama na mimi ninavyojuliwa sana”
Paulo hapa
anazungumzia jinsi atakavyokuwa huko mbinguni hii ndio hali halisi huko
tutamwona mwokozi usokwa uso na ufahamu wetu kuhusu Mungu utakamilika huko, sio
tu ujuzi kuhusu Mungu lakini hata na sisi wenyewe tutajitambua kwa ukamilifu
kwa kuwa kazi njema aliyoianza katika mioyo yetu ataikamilisha Wafilipi 1;6,
lini itakuwa hivyo tusubiri maana kwa sasa hakuna ajuaye
Nani wataabudu
Ni wale washindao tu ndio watakaomwabudu
Mungu huko mbinguni mkazo wa ushindi unaonekana zaidi katika nyaraka ndani ya
kitabu cha ufunuo kwa makanisa yale saba
1.
Ufunuo 2;7 Yeye ashindaye nitampa kula matunda
uya mti wa uzima ulio katika biustani ya Mungu
2.
Ufunuo 2;11 Yeye ashindaye hatapatikana na
madhara ya mauti ya pili
3.
Ufunuo 2;17 Yeye ashindaye nitampa baafdhi ya ile mana iliyofichwa name
nitampa jiwe jeupe na juu ya jiwe hilo
limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea
4.
Ufunuo 2; 26-28 Yeye ashindaye nitampa mamlaka
juu ya mataifa,name nitampa ile nyota ya asubuhi
5.
Ufunuo 3;4-5Yeye ashindaye atavikwa mavazi meupe
wala sitalifuta jina lake katika kitabu cha uzima
6.
Ufunuo 3;12 Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu
wangu
7.
Ufunuo 3;21 Yeye ashindaye nitampa kuketi pamoja
nani katika kiti change cha enzi.
Ni furaha ya ajabu kwani hawa washindao
Yohana anafunua katika sura ya 7 kuwa ni wengi sana
Ndugu
yangu mpendwa zingatia basi maswala ya ibada na uishi maisha ya ushindi ilei
wewe na mimi kwa neema ya Mungu tuweze kufikia hatua ya ushindi na kumuabudu
Mungu wetu katika kweli iliyokamilika mbingunii Ubarikiwe na Bwana !.
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!