Jumapili, 13 Machi 2016

Laiti ningekunywa maji ya kisima cha Bethelehemu !



  1Nyakati 11:17.
1Nyakati 11:10 – 19
Ni muhimu kwetu kufahamu kuwa hakuna kitu au jambo linatokea tu hivihivi duniani, bila baadhi ya watu, kuhatarisha Maisha yao, ili kwamba wengine waweze kufikia Ndoto zao, Ndoto za kila mmoja wetu haziwezi kufikiwa ikiwa kwa msaada wake peke yake, ni lazima wengine wahusike, katika kuzifanikisha ndoto hizo!.

 Kisima cha Daudi Mjini Bethelehemu

Unapoona mataifa Mengi yako huru leo ni lazima ufahamu kuwa uhuru huo, haukupatikana kirahisi, wako walioupigania, unapoona kuna haki zimepatikana mahali Fulani ambako hakukuwa na haki, ni lazima ujue kuwa, kuna watu waliopigania haki hizo hata zikapatikana na wakati mwingine iligharimu maisha yao na hata kufa!, Uhai, Elimu na mafanikio yamtu moja moja pia yatategemea kwa namna moja ama nyingine kujitoa kwa watu wengine ili kutimiza azima ya mafanikio yetu na kuishi kwetu.

Askari mmoja Nchini Marekani wakati wa kimbunga kikali sana kijulikanacho kama Hurricane Sandy alijitosa katika mafuriko na kuokoa watu wazima sita na mjomba wake mdogo sana na baada ya kufika Ng’ambo aligundua kuwa Baba yake hakuweko, hivyo alirudi tena ili amuokoe Baba yake aliporejea, hakufanikiwa kumuona na baba yake kwa bahati njema alikuwa ameokolewa kwa njia nyingine na kufika n’gambo lakini baadaye ilibainika kuwa Artur Kasprizak alikuwa amefariki dunia alipokuwa akijaribu kumtafuta baba yake.

Mtakatifu Maximilian Kolbe wakati wa vita vya wanazi WANAZI wa Hitler waliamua kujaribu kuuwa waqtu kumi kwa njaa ili waona itakavyokuwa, wafungwa hawa kila mmoja alikuwa akiogopa , Wanazi walichagua mtu mmoja mfungwa aanze zoezi la kufa na Njaa na mtu huyu alilia sana akiitaja Familia yake Ndipo Maximilian Kolbe aliamua kujitoa yeye ili achukue nafasi ya mfungwa huyo, na akaanza zoezi la kushinda na njaa, Kolbe aliimba na kuomba kwa sauti kwa wiki tatu ili kuokoa roho za wengine lakini wanazi walidhihaki na wakaamua kumchoma sindano ya sumu akafa na baadaye Kanisa Katoliki lilimtangaza kuwa Mtakatifu.

 Mtakatifu Maximilian Kolbe

Mwaka 1984 mwezi kama wa tano na wa sita hivi mwaka huo nikiwa kijana mdogo sana niliugua sana, wakati huo tulisafiri na baba kutoka Lindi mjini tulipanda Ndege na kuja Dar es Salaam, kisha tulipanda basi kuja hapa Muheza kumpa Pole shangazi kwani alikuwa amefiwa na Mumewe, kwa bahati mbaya nilianza kuugua njiani huku nikiishiwa na nguvu na nilumwa sana sana, hali yangu ilikuwa ngumu kiasi ambacho Madaktari walikata tamaa na kusema labda tukajaribu maswala ya nyumbani, mama alikuwa amebaki Lindi na kaka na mdogo wangu mdogo sana aliyekuwa na miaka mitatu tu, Shangazi aliyekuwa amefiwa na ndio tumekuja kumpa pole alilazwa name katika Hospitali ya teule hapa Muheza, likizo yote iliishia hospital mama yangu alipoambiwa kuwa ninaumwa sana alipiga magoti na kumuomba Mungu sana, aliambiwa kuwa wakati wowote lolote lingeweza kutokea, “Mama yangu aliomba Ee Mungu tafadhali unichukue mimi badala ya Mwanangu!” Nilipona kwa njia ambazo Mungu alikuwa anajua na tulifanikiwa kurudi Lindi nikiwa salama lakini nilikuwa Nimekonda sana mama alifurahi kuniona lakini kabla ya mwezi kumalizika July 19 Alhamis 1984, Mama yangu alifariki baada ya Operesheni ya kidole tumbo kushindikana

Maisha yalianza kuwa tofauti, tulianza kuishi katika mikono ya watu wasio na Huruma, na wakatutenda kila walichojisikia, Nafahamu wazi kuwa Maisha yangu yaligharimiwa na watu Hata sasa sifahamu kuwa nitampata wapi Mama japo nilipe fadhila, ama nifanye nini ili niweze kuifurahisha roho yake, 

Katika Maandiko wote tunafahamu kuwa Daudi alikuwa ni shujaa na ni mtu wa Vita, alimpiga Goliath, aliuwa wafilisti wapatao Miambili alipoagizwa na Sauli kuwa anataka Govi za wafilist mia moja ili amuoze Binti yake.

Lakini hata hivyo Ushujaa wa Daudi hauwezi kukamilishwa na Daudi peke yake, huwezi kuamilisha Jambo lolote mwenyewe, wala kwa kudharau wengine wanaokuzunguka, mafanikio yako hayatokani na wewe mwenyewe na akili zako na nguvu zako bali pamoja na wale Mungu anaokupa kukuzunguka, wako wanaokuombea, wako wanaochukuliana nawe, wako waliokusamehe, wako wanaokutia moyo, wako waliokuelekeza wako wanaokutetea, na mengineyo.

Daudi aliweza kutiwa Moyo na makamanda ambao walikuwa wapiganaji Hodari sana kupita kawaida licha ya kupigana kwaajili yake pia walimlinda na Mungu alimpa Ushindi ushindi Daudi kupitia wao.

1.       Yashobeamu mhakmoni 1Nyakati 11:10-11
2.       Eleazar mwana wa Dodai 1Nyakati 11:12
3.       Mwingine aliitwa Abishai 1Nyakati 11:20 

Majemadari hao ndio waliosababisha Ufalme wa Daudi kuwa Imara
Siku Moja Daudi alifanya jambo la kipumbavu sana hatujui ilikuwa ni kwa sababu Gani, lakini alitamani kunywa maji ya Kisima cha Bethelehemu, Daudi alizaliwa Bethelehemu, alikulia hapo alitumia maji ya kisima kile huenda yalikuwa matamu au aliyazoea na hivyo aliyakumbuka
Hata hivyo wakati huu alipokuwa akiyadai, hali ilikuwa ni Mbaya kulikuwa na Vita kali sana kati yao na Wafilisti na kisima kile pale kilipokuweko ndiko kulikokuwa na Ngome ya Wafilisti yaani maadui wa Israel lakini wakati huohuo Ndio Daudi anatamani maji ya kisima kile tena anayadai kwa Nguvu kubwa LAITI NINGEKUNYWA MAJI YA KISIMA CHA BETHELEHEMU ! 

Majemadari wake Daudi waliposikia kauli ya mfalme wao, bila kujalia kuwa wanajidhihirisha kwa maadui zao na kuhatarisha Maisha yao, tena bila ya kuuliza haya maji yana tofauti gani na mengine? Mfalme leo ana wazimu au inakuwaje anataka maji ya Bethelehemu ni Udhaifu wa namna gani huu? Hawakuwa na maswala dhidi ya kutii, walisema liwalo na liwe wakapenya ngome ya Wafilisti safari hii sio kuokoa taifa au kuokoa mtu aliyetekwa hapana ni kuleta maji kwa mfalme mwenye kiu ya kijinga tu!

Daudi alipogundua kuwa amefanya Ujinga wa kipuuzi, aliamua naye kujitesa aliyapokea maji yale na kuyatoa dhabihu kwa Bwana, Hakukubali kuyanywa akasema MUNGU wangu apishie Mbali, nisifanye Hivi je “NINYWE DAMU YA WATU WALIOHATARISHA MAISHA YAO”,  hatuwezi kumpuuzia bwana wetu Yesu alikufa Msalabani akamwaga Damu yake, tunatumia jina lake, kupata ushindi na mafanikio mbalimbali ni muhimu kumuenzi Bwana wetu, Tukumbuke wote waliotusaidia kufikia hapo tulipofikia, tuache kupuuza maswala na michango ya watu wengine, wako watu wenye dharau Duniani ambao hawaoni michango ya watu wengine katika jamii, wanatamani hata kufuta Historia zao, hawataki kuona hata picha za waasisi na waliopoteza maisha kwaajili yao, Kusoma kwetu na kulipiwa kwetu Ada kuna michango ya watu mbalimbali ambao wanataka kufurahia ndoto zako kufikiwa wanataka kuhakikisha kuwa kiu yako inatimilizwa na wako tayari wao wafe ili wewe uisho usihesabu mchango wao kuwa ni Upuuzi.

Ujumbe na Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima.

Jumatano, 9 Machi 2016

Upigane nao Wanaopigana nami!



UJUMBE:  UPIGANE NAO WANAOPIGANA NAMI!

Zaburi 35:1-38

     Zaburi ni mojawapo ya vitabu vya kipekee sana katika Biblia ni moja ya kitabu maarufu kilichoko katika kundi la vitabu viitwavyo vitabu vya mashairi ya kiebrania na ndicho kitabu kirefu kuliko vyote katika Biblia kwani kina sura karibu 150 zilizogawanywa katika vitabu vitano, inaaminika kuwa ndicho kitabu kinachosomwa zaidi na kuhubiriwa zaidi kuliko vyote katika agano la kale, aidha waimbaji wengi sana  na watunzi wa nyimbo hutoa nyimbo zao katika zaburi, sababu moja kuu inayovutia wengi katika zaburi ni kwa sababu zinagusa hisia za watu 



·         Zaburi ziliandikwa kwa sababu mbalimbali za kihisia kama vile watu walipokuwa na furaha, huzuni, nk, Mfano mwandishi wa wimbo nionapo amani kama shwari kwa hiyo kuna sababu nyingi zilizopelekea zaburi kuandikwa kati ya hizo ni pamoja na
1.      Zaburi kwa ajili ya hekima na maadili mfano zaburi ya 1
2.      Zaburi kwa ajili ya shukurani nyingi huanza kwa kusema mshukuruni Bwana!
3.      Zaburi za kujitia moyo mfano zaburi ya 27
4.      Zaburi za kifalme au za kimasihi
5.      Zaburi za kihistoria au za kukumbuka matukio maalumu
6.      Zaburi za kusifu au “Halel Psalms” ambazo huanza na neno Haleluya
7.      Zaburi za maombolezo
8.      Zaburi za dua na maombi pamoja na kulaani Mfano Zaburi ya 35 : 1-8

Leo nataka tuchukue Muda kuitafakari zaburi hii ambayo huangukia katika kundi la zaburi za kulaani, au zaburi za maombi lakini wakati huu mwandishi wa zaburi hii anaomba mabaya au hukumu ndhidi nya adui zake! Ni zaburi ngumu wakati mwingine kuitafasiri ukilinganisha na Mafundisho nya Bwana Yesu kuwa tusiwalaani maadui zetu bali tuwaombee mema hata wale wanaotuudhi! Luka 23:34 na Mathayo 5:39,44. Hata hivyo ni muhimu kujiuliza Kwanini Roho Mtakatifu ameruhusu Zaburi hii kuweko!

1.      Kila mtu aliyeokoka anayo haki ya kudai ulinzi wa Mungu dhidi ya watu waovu na wanaotuonea, Mungu hakutuita duniani tu ili tutukanwe na kudhulumiwa na kusemwa vibaya na kuteswa na kuonewa na kuuawa na kuchukuliwa wake zetu, waume zetu, kujaziwa mimba watoto wetu, kusemwa vibaya kukandamizwa kuzibwa vinywa eti kwa vile sisi ni walokole Hapana! Simama na kuitetea haki yako!

2.      Mwandishi wa zaburi hii hatufundishi kujichukulia sheria mkononi na kujilipia Kisasi lakini anatufundisha Kumtegemea na Kumsihi Mungu awaadhibu waovu kulingana na uovu wao anayeteta name Bwana atete naye!, anayepigana nani Bwana apigane naye! Hatuwezi kama wakristo kukaa kimya pale uonevu unapofanyika kisha Mbingi ziko kimya na serikali iko kimya Biblia inatufundisha kuidai haki, naweza kushindwa kuandamana, kubeba silaha, kujitetea mwenyewe, kwenda mahakamani n.k lakini siwezi kushindwa kuingia Magotini na kuidai haki yangu Mungu ni Lazima anilipie Zaburi 28:4 Unasema Hivi “ Uwape sawasawa na Vitendo vyao Na kwa kadiri ya Ubaya wa kufanya kwao, Uwape sawa sawa na Kazi za mikono yao Uwalipe stailizao”

3.      Biblia kupitia Zaburi hii inatufundisha kuwa kiko kiwango cha uvumilivu lakini kama uovu utaendelea kupita kiasi na kufikia kilele Ni lazima Kumkumbusha Mungu katika Haki yake kutoa haki na hukumu, ni lazima tusimame kuhakikisha kuwa Uonevu na ukatili vinakomeshwa na kuharibiwa Yesu Mwenyewe alifundisha Mfano wa Mwanamke mjane Katika Luka 18:3 aliendelea kuomba bila kukata tama mpaka haki yake ikapatikana tena Kristo alihahidi kuwa Mungu hataacha kuwapatia haki wateule wake wanaomlilia Mchana na Usiku Luka 18:7

4.      Zaburi hii inatufundisha kuwa ingawa tunatamani kuona watu wanamgeukia Mungu na kuja kwake kupitia Upole wetu, upendo na Unyenyekevu, Lakini pia tutamani kuona Uovu ukiharibiwa na watu wakatili wakishughulikiwa, Nimlazima tumuombe Mungu ashughulikie adui zetu ndio adui yetu mkuu ni shetani lakini na wale anaowatumia kutuonea na kutubughudhi na kutukerehesha ni muhimu kumsihi Mungu ashughulike navyo ni lazima tumuulize Mungu Maswali ambayo hata Daudi na upendo wake na huruma na rehema alimhoji Mungu!

Mbona Mataifa wamefanya ghasia
Na kabila za watu wametafakari Ubatili?
Wafalme wa Dunia wamejipanga
Na wakuu wamefanya shauri pamoja
Juu ya Bwana na juu ya Mpakwa mafuta wake.

Ni wakati wa kusimama na kudai haki yako dhidi ya Udhalimu wa kila aina, lazima umwambie Bwana ashughulike na kila kinachokukosesha raha na amani hapa duniani, kama ni magonjwa, Mapepo, Mateso, Ugaidi, Uonevu, Dhuluma, Kunyanyaswa n.k. Usikubali ukaonelewa Yuko awezaye Kupambana navyo mweleze ashughulike navyo!

Ujumbe:
Na Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.

Jumanne, 8 Machi 2016

Kwanini Waislamu Humchukia Paulo Mtume?



     Paulo Mtume ni moja ya nguzo muhimu sana Katika Ukristo na ulimwengu kwa ujumla kuliko hata Muhamad,Waislam wanaamini kuwa kila jamii ina mtume wake na kuwa Muhamad ndilo jibu la Matumaini ya umma wa Kiarabu, na mataifa mengine, Lakini ilivyo ni kwamba Matumaini ya mtume anayefiti anayestahiki kwa ulimwengu Mzima yanajibika kibiblia kuwa Paulo mtume ndiye Jibu hilo na ndio maana waislamu wanamchukia, ni wazi kuwa kama jinsi ambavyo ni kufuru kumlinganisha Muhamad na Yesu kristo kwani Ni Mungu, lakini ni kumvunjia Kristo heshima kwa kumlinganisha Paulo na Muhamad.

 Paulo Mtume ni Mkuu Kuliko Muhamad mwanzilishi wa dini ya Kiisalamu

    Paulo ni Mtume wa Mataifa. Kama Waislam walikuwa wanaona kuna hitaji kwa kila taifa kuwa na Mtume wake ni Muhimu kwao kufahamu kuwa Mpango wa Mungu tangu mwanzo haukuwa kuwapendelea wayahudi tu, yeye tangu mwanzo alimkusudia Ibrahimu kuwa Baraka kwa jamaa zote za dunia (Mwanzo 12;1-3),Baraka hii ilitimizwa kupitia Yesu kristo ambaye alitolewa kwa kusudi lileliel la kiulimwengu (Yohana 3;16),Katika mpango huu mzima wa kuwafikia Mataifa yoote Masihi aliwaagiza wanafunzi wake kuihubiri injili kwa kila taifa (Mathayo 28;19) inashangaza sana kufikiri kuwa Manabii waliotumwa Pamoja na Ujio wa Kristo duniani uliihusu Israel tu au wayahudi tu na ndio maana hata ile siku ya Pentekoste Roho mtakatifu alipo washukia wanafunzi wa Yesu waliwezeshwa kuzungumza lugha mbalimbali ikiwemo kiarabu soma (Matendo 2;1-12).Hii maana yake ni kuwa Mungu alitaka kuufikia Ulimwengu mzima kupitia Taifa teule alilolitenga la Kiyahudi maana huko ndiko wokovu unakotokea(Yohana 4;22), na mwokozi wa ulimwengu ni mmoja tu (Yohana 4;39-42).

  Ni katika kusudi zima la kuufikia ulimwengu Mungu alimchagua Paulo mtume aifanye kazi hii (Matendo 9;1-15). Ni dhahiri kuwa hata Roho Mtakatifu alithibitisha kuwa amemuita Paulo kwa kazi hii maalum (Mdo 13;1-3).Jambo hili lilikuwa bayana hata kwa Paulo mwenyewe kuwa neema na utume alioitiwa ulikuwa maalum kwa mataifa (Warumi 1;5, Wagalatia 2;7-8,9-9).Mungu bado hata sasa aweza kutumia watu mbalimbali na wakawa ni viongozi Maarufu sana duniani toka jamii ya mataifa lakini woote watakuwa na kazi moja tu kumhubiri Yesu Kristo, Hivyo kama ilikuweko haja ya mtume kwa waarabu angeinuliwa na angemhubiri kristo na sivinginevyo,Kinyume chake basin a waafrika tutahitaji nabii wetu, Wahindi nao, wazungu, nao nk. Kilichokuwa kinahitajika ni mtume na sio injili Nyingnie  kwani yeye aliyeleta injili nyingine amelaaniwa!(Galatia 1;6-9).

Paulo alipewa mafunuo Makubwa sana kuliko Muhamad.
     Woote tunajua kuwa Paulo Mtume alipewa mafunuo makubwa sana kuliko aliyopewa muhamad,Injili aliyoihubiri si ya namna ya kibina damu kwani aliipokea na kufundishwa kwa ufunuo wa Kristo Yesu mwenyewe aliyemuita (Wagalatia 1;10-12),Paulo alinyakuliwa mpaka peponi na kufika mbingu ya tatu kwa ajili ya maono na mafunuo ya Bwana (yaani Yesu) soma (2Koritho12;1-7),Mungu alimtumia Paulo mtume kwa namna ya kupita kawaida Biblia inasema (Matendo 19;11) “Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida;” Neema ya Mungu iliyokuwa juu yake hailinganishwi kamwe na utume wa Muhammad kwanini waislamu wasione wivu zaidi ya yoote tunaweza kuseama mambo ya msingi yafuatayo kumhusu Paulo.
Paulo ni Mtetezi Mkuu wa Ukristo na Mafundisho yahusuyo kuhesabiwa haki kwa imani.Paulo alizungumza, kufundisha, Kufafanua na kutetea  mafundisho yahusuyo haki inayotokana na Imani mafundisho yanayooonekana kuwa Mwiba na tishio kwa waislamu ambao hufundisha kuwa haki inapatikana kwa matendo, Kwa waislamu matendo mema yanahesabiwa kuwa thawabu na yanampa mwislamu nafasi ya kuingia Paradiso, Hiki ambacho waislamu wanafundisha ni matendo ya sheria kuwa mtu anaokolewa kwa matendo, na bidii ya kibinadamu nakwa kufuata matendo ya sheria na Sikukuu zao,Paulo anafanyika mwiba wa mafundisho hayo na ndio maana wanamchukia.(Galatia 2;15-16,3;10 Kolosai 2;16-22).

Paulo alikuwa na bidii na kuusambaza Ukristo duniani.(Mdo 13;46-48).
     Paulo alifanikiwa kuipeleka injili nje ya mipaka ya Israel na mipaka ya iliyokuwa himaya ya Rumikutoka huko injili ilifika hata ulaya na hatimaye ulimwengu mzima wa wakati ule, Waislamu wanaona kuwa Paulo hakufanya sahihi alifanya makosa kwa kuipeleka injili nje ya mipaka ya Wayahudi, Ukristo kwa waislamu wanaamini kwamba uliwahusu wayahudi tu wanaamini ukristo ulikuja kwa ajili ya kuwakosoa wayahudi,kuwarekebisha na kuwaongoza wao, Kwa kuupeleka kwa Mataifa Paulo ameharibu ukristo halisi, na hivyo ameufanya Ukristo kuenea dunia nzima hili linawaudhi sana waislamu na ndio maana Humpinga.

    Wakolosai 1;3-6, Leo injili imezaa matunda na kusambaa ulimwengu mzima kutokana na kazi aliyoifanya Paulo Mtume Unadhani shetani atampenda? Sisi kama wasomi wa Biblia tunakubaliana kuwa Paulo anamchango mkubwa sana usiopingika katika kusambaza nuru ulimwenguni hivyo kumchikia yeye ni kuichukia nuru, aliisambaza injili kwa mafanikio kwa amani wala hakutumia upanga kama Muhamad.Paulo mtume alikuwa na neema kuu sana ambayo Muhamad hawezi kuifikia hata leo.

Uhusiano wa Quran na Ugaidi !



UHUSIANO WA QURAN NA UGAIDI  
    Mara nyingi tumeona  katika television,kusikia katika maredio na kusoma katika magazeti na hata kuona matukio ya ugaidi yanayotajwa  katika vyombo mbalimbali vya habari,tumesikia habari za watu wanaovaa mabomu na kujilipua miongoni mwa watu na kuuwa watu wengi sana hata watoto wadogo, walengwa wengi wakiwa ni wayahudi au wakristo au watu na mataifa yanayofikiriwa kuwa ni makafiri Dunia imeshuhudia kulipuliwa kwa balozi za Marekani jijini Dar es salaam,Tanzania na Nairobi nchini Kenya na hoteli ya Paradise inayomlikiwa na wayahudi mjini Mombasa na tukio la kihistoria la kuuawa kwa watu wengi  baada ya ndege kutumiwa kama silaha huko Marekani mnamo 11 september 2001, na matukio mengine mengi Yesu kristo alitabiri katika (Yohana 16;1-3),Matukio haya yana uhusiano mkubwa na Mafundisho ya Quran na imani ya kiislamu hasa wale wanaoifuata qurani sawasawa(Surat at tawba 9;29)

     Mwanzoni Muhamad katika quran aliagiza mtu asilazimishwe kuingia katika Uislamu (surat al baqara 2;256)Lakini upinzani zaidi wa ujumbe wake ulipozidi pale makka na alipopata nguvu aliongeza chuki na uchungu na kuamuru yafuatayo(surat tawba “toba” 9;5,123,surat al maida “meza5;33).Muhamad amewafundisha Waislamu kuwachukia kabisa, wayahudi na wakristo na kutofanya urafiki nao (surat al maida 5;51) Aidha qurani inawataka waislamu wanapokuwa vitani kuwapiga makafiri shingoni ili wafe haraka kama unabisha soma (Muhamad 47;4-6)

   Tukio la ugaidi la September 11 2001,lililofanywa na kundi la al-qaeda la Osama bin Laden lilifanyika kutekeleza aya ya quran ya Surat at tawba 9;110-111 katika juzuu ya 11 na ndio maana liliungwa mkono na wanaharakati woote wa kiislamu kama nitakavyoonyesha tukio hili katika kielelezo ukurasa ujao, uislamu hauna huruma na mzaha na Dini nyingine wao ni jino kwa jino anakiri hivyo Farsiy katika kitabu maisha ya nabii Muhamad uk 48 sura ya 9 kifungu cha pili kutoka mwisho anasema nanukuu “…Kweli haiwezi kukatalika kuwa Uislamu haufuati kawaida “akikupiga shavu la kushoto mgeuzie la kulia” kwa mazungumzo hayo hapo juu sheikh amekanusha aliyokuwa akiyatetea juu kuwa uislamu haukuenezwa kwa upanga maana hapo anakiri na sheikh Baghoza katika kitabu chake JIHAD je inaendelea au imekufa anahamasisha Shehk huyu kurudi kwenye amri za allah yaani jihad kwani hii ni njia fupi ya kuingia peponi kwa waislamu ni kama nguzo ya sita katika uislamu



 Kulia kiongozi wa ugaidi Osama bin Laden na Mwana mapambano dhidi ya ugaidi raisi wa zamani wa Marekani George .W.Bush. Ugaidi asili yake ni Quran.

 Kielelezo namna tukio la ugaidi la September 9 mwaka 2001 September(mwezi wa 9) ni sura ya tisa at tawba Mwezi wa kumi na moja 11 ni juzuu  ya 11. Mwaka 2001 ni mjumuisho wa aya ya 110-111 na tukio lililoko hapo ni kuvunjwa kwa jengo.

Juzuu 11                                                                             at-tawba 9                                                                 yaatadhirun.
………………………………………………………………………………………….……………………………………………………………….Ayaya110-111 ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..
Kielelezo juu jinsi quran livyo katika muundo na mtazamo wa kigaidi wa tukio la September 11 2001

Ahadi za Malipo ya Ugaidi
   Kwa Mujibu wa qurani kuna thawabu kubwa sana mtu anapojihusisha na ugaidi (jihad)na ahadi hizi ndizo zinazo hamasisha sana waislamu kujituma katika kujilipua mabomu,njia nyingine ni ngumu mtu kuingia peponi hasa kwa sababu unaweza kukosa swala au kushindwa kufunga swaumu hivyo jihad ndio njia ya mkato ya kuingia peponi na yenye uhakika na ahadi kemkem toka kwa allah
  • Kufutiwa dhambi (surat as saff 61;9-12)kuua kwa ajili ya dini ya mwenyezi mungu au kuuawa ni biashara yenye faida.
  • Kulipwa mambo mazuri (surat saafat 37;40-49) kupewa wanawake wenye macho kama mayai ya Mbuni
  • Kupewa wanawake wazuri wenye macho kama vikombe(surat tur 52:19-20)
  • Kufanya ngono saa 24 soma (sunnan ibn majah vol 4 uk 540 khadhithi namba 2481)  …. “Dhakari hazitasinyaa watapewa wanawake 70 kila mmoja atakuwa bikira na wana makalio kama masanduku.
  • Kupigana jihadi ni kufuzu kuliko kukubwa (at tawba 9:111)
  • Mkimsaidia Allah nae atawasaidia (Muhamad 47;7)
  • Kuna daraja saba walizoandaliwa Mujahidini,pia ziko daraja mia moja “Pepo ina daraja miamoja ambazo allah amewaandalia wale wanaopigana kwa ajili yake…..”(vol 4-H;448) Abu Huraira.
  • Ahadi saba  za watakaojitoa Muhanga  ni pamoja na  1. Roho za waliokufa kwa kujitoa muhanga zimo ndani ya ndege wa kijani wanaoishi peponi2.Madhambi na makosa yao yoote yatafutwa 3.mujahidin anayo haki ya kuwaombea radhi kwa allah watu wake 70 4.Ataokoka na Mateso na usumbufu wa mauti 5. ataokoka na Vitisho vyoote vya siku ya kiama 6. Hataogopa kitu siku ya hesabu (hukumu) 7.Hatohisi machungu ya kifo illa ni kama mfinyo mdogo tu. Hizo ndio daraja walizopewa Mujahidin soma uk 11-12 wa kitabu JIHAD cha Abdullah said Baghoza.
  • Ni wazi kabisa Quran inafundisha na kukazia swala la kuua au kuawa kwa kujitoa muhanga kwaajili ya Mungu Allah au kwa ajili ya uislamu  kuwa ni swala muhimu na la lazima na kuwa lina thawabu kubwa sana kwa mola  ni muhimu msomaji wangu ukachukua mUda kutafakari kama Mungu alivyojifunua kupitia Kristo na mafundisho yake yaliyojaa upendo katika ulimwengu huu tulio nao je mafundisho ya namna hii yanaweza kukubalika ulimwenguni na sisi tukae kimya? Katika sura inayokuja tutawachambua kwa undani Osama kuwa ni nani na al-qaeda ni nani?: