Jumatatu, 18 Aprili 2016

Jionyeshe kuwa Mwanamume!



1 Wafalme 2:1-3 Basi siku ya kufa kwake Daudi ikakaribia, akamwusia Sulemani mwanawe akasema, Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujionyeshe kuwa mwanamume, Uyashike mausia ya Bwana Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheroia zake na amri zake na hukumu zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ulifanyalo na kila utazamako;”

Ni muhimu kujiuliza maswali kadhaa hasa kama wewe ni mwanamume kisha Baba yako akakuusia au kukuambia Mwanangu “JIONYESHE KUWA MWANAMUME” hii ina maana gani?

Katika jamii mbalimbali ikiwemo jamii zetu za kiafrika na Kiswahili tunazo namna nyingi sana za kutiana moyo, na maneno yoyote ya kutiana moyo mengineyo ni pamoja na kumwambie mtu Simama kiume, na kadhalika, katika jamii ya kimasai kuonyesha uanamume ni pamoja na kutokulia na kuvumilia uchungu na ugumu wakati wa kutahiriwa, Ngariba wa kimasai huwatairi vijana Morani bila ganzi na kila kijana anapaswa kuonyesha ujasiri wa kuvumilia bila kulia akionyesha uanaume, aidha kuua samba ilikuwa ni namna nyingine ya zamani sana katika jamii ya kimasai yenye kudhihirisha uanaume.

 Mfalme Sulemani:

Daudi anakaribia kufa na mwanaye Sulemani anapaswa kuchukua uongozi, uongozi ni kazi ngumu sio kazi nyepesi inahitaji hekima, ujasiri na kumtanguliza Mungu mbele lakini kubwa zaidi kusimama katika haki na kuonyesha uhodari na ushujaa Daudi anamwambia Sulemani asimame kiume, aonyeshe uanaume, ajionyeshe kuwa mwanamume, Kwa lugha na tamaduni za Kiyahudi au kiebrania nao walikuwana maana zaidi ya kawaida walipoambiana onyesha uanaume!

Neno hilo Jionyeshe kuwa Mwanamume Kwa kiebrania Husomeka kama IYSH na kwa Kiyunani Husomeka kama ANDRIZOMAI ambayo maana yake.

Mtu anayeweza kupambana wakati watu wengine wotewameshindwa! Mtu wa mwisho mwenye kuleta ufumbuzi au ukombozi wakati mji unapovamiwa na kutekwa na kila mtu anapoonyesha kushindwa, unapojitokeza kuleta suluhu wakati watu wengine wote wamepoteza tumaini hapo ndipo mtu anapoitwa ameonyesha Uanamume  

Kwa nini Daudi alimuagiza  Sulemani kusimama kiume?

1.      Daudi mwenyewe alikuwa mtu shujaa, alionyesha uanaume wakati Israel wote walipokuwa wakiogopa kumkabili Goliath yeye alijitokeza kutoa suluhu, sulemani angeelewa vema kila ambacho baba yake alikuwa akimuagiza
2.      Daudi mwenyewe alimpendeza Mungu na kuhakikisha kuwa Mungu yuko upande wake wakati wote hata alipokosea alitubu na kubadilika kwa haraka ili Mungu awe naye hakukubali kupoteza uwepo wa Roho Mtakatifu, alishika sheria za Mungu, alijua kuwa ili Sulemani aweze kufanikiwa hana budi kuishika Sheria ya Mungu
3.      Daudi alikuwa na uzoefu wa kupambana na changamoto mbalimbali na alikuwa na ujuzi wa kuizima mishale ya adui, alijua namna ya kuwashughulikia adui zake, kuwalipa mema walio wema na kuwashughulikia waovu au mafisadi na kutokuwaonea haya wenye kudhulumu Mstari wa 4-9 unasema hivi

 “ili Bwana afanye imara neno lake alilonena kwa habari yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa mtu katika kiti cha enzi cha Israeli. Na zaidi ya hayo, umejua alivyonitenda Yoabu, mwana wa Seruya, yaani, alivyowatenda majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri, mwana wa Neri, na Amasa, mwana wa Yetheri, ambao aliwaua, na kuimwaga damu ya vita wakati wa amani, akautia damu ya vita mshipi uliokuwa viunoni mwake, na viatu vilivyokuwa miguuni mwake. Kwa hiyo ufanye kama ilivyo hekima yako, wala usimwachie mvi zake kushukia Ahera kwa amani.  Lakini uwafanyie mema wana wa Barzilai Mgileadi, wawe miongoni mwao walao mezani pako; kwa jinsi walivyonijilia nilipokuwa nimekimbia mbele ya Absalomu, ndugu yako. Hata, angalia, yuko pamoja nawe Shimei, mwana wa Gera, Mbenyamini, wa Bahurimu, ndiye aliyenilaani kwa laana kuu siku ile nilipokwenda Mahanaimu; lakini akashuka kunilaki kule Yordani, nami nikamwapia kwa Bwana, nikamwambia, Mimi sitakuua kwa upanga.  Basi kwa hiyo usimwachilie, kwa kuwa wewe u mtu wa akili; nawe utajua ikupasayo umtendee, na mvi zake utazishusha Ahera pamoja na damu.”

Kuonyesha uanaume kibiblia kuna maana ya kusimama katika uhodari wa kuliangalia Neno la Mungu na kulishika, kuziangalia njia za Bwana kwa moyo wako wote na kuhakikisha kuwa wale waliokutendea wema au waliowatendea wema baba zako wanalipwa mema na wale waliotendea uovu baba zako wanashughulikiwa, tafasiri hii katika mtazamo wa agano jipya yaweza kuwa sio sahii, kwa sababu hatupaswi kulipa baya kwa baya au kuwatendea wema adui zetu. Lakini kisiasa ni tafasiri sahii kwa vile kitabu cha wafalme ni kitabu cha viongozi, Kiongozi wa kisiasa katika taifa letu na taifa lolote ni lazima amtangulize Mungu mbele, lakini pia waliohusika na ufisadi nilazima ahakikishe kuwa wanashughulikiwa ipaswavyo ili taifa liwezekuwa na amani.
Ahabu alikuweko katika serikali ya Daudi lakini aliuwa watu wawili wasiokuwa na hatia, alikuwa ni shujaa lakini hangefaa kuwa kiongozi wakati wa Sulemani angeleta laana kwa taifa kwa vile ana ufisadi moyoni mwake alitakiwa ashughulikiwe, Shimei alimtukana Daudi, hata ingawa Daudi alikuwa amemsamehe, Utawala wa Sulemani haungeweza kuwa wa amani kuendelea kupokea ushauri au kumfanyoia mema mtu ambaye alimtukana baba yako aliyeweka misigingi ya kitaifa, ilikuwa lazima shimei auawe halikadhalika alikuwa amemtukana masihi wa Bwana, huwezi kumtukana masihi wa Bwana kisha ukawa salama hata kidogo ilikuwa lazima ashughughulikiwe!

Katika kuyashughulikia haya yote kulihitaji Ushujaa, kulihitaji mtu asimame kiume, na kutokukubali kuyumbishwa ili amani ipatikane. Bwana angeufanya utawala wa Sulemani kuwa imara kama angeweza kuyashughulikia maagizo hayo muhimu, Ni maombi yangu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa John Pombe Magufuli atasimama kiume na kuhakikisha kuwa anaiangalia katiba na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na utawala bora akimtanguliza Mungu na kuwashughulikia mafisadi bila kuwaonea haya akifanya haya Mungu atauimarisha utawala wake na sifa ambazo zimeanza kuenea Duniani kwaajili yake zitazidi mara elfu. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

Ujumbe na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Jumanne, 22 Machi 2016

Ujumbe: Neema ya Mungu Haitendi Haki !


ONYO! “Kama hauna akili ujumbe huu haukufai, Usisome ujumbe huu kama hauna akili hutaelewa”acha!


1Wakoritho 1:26-31 Biblia inasema hivi:-
“26. Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; 27. bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; 28. tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; 29. mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. 30. Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; 31. kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.”

Ndugu zangu unapoyatafakari maisha kwa undani sana na hasa maisha ya kiroho unaweza kuchanganyikiwa na ukagundua kuwa kitu au jambo linaitwa neema ya Mungu ni gumu kupokelewa kuliko unavyofikiri, ni rahisi kutafakari mambo juujuu na ukasema ni kwa neema ya Mungu lakini neema sio jambo jepesi kama unavyofikiri, leo sitaki kabisa kufafanua nini maana ya neema kwa vile nafikiri tutazunguka tu lakini natka kukazia kuwa Neema ya Mungu haitendi Haki! Najua kuwa hii ndio lugha nyepesi itakayokusaidia leo kuelewa ninapotaka kuizungumzia neema ya Mungu.
Neema ya Mungu haitendi haki swala hili kwa asili sio sahihii lakini ndio litakalotusaidia leo kuelewa maana ya neema ya Mungu tukinena kiwazimu, kichwa hiki kinatusaidia kujua kuwa wewe na mimi sio Mungu na Mungu sio mimi na wewe, wakale walisema “ Mungu sio Athumani” hebu tufafanue kwa kina zaidi

Tunapoisoma biblia neno la Mungu mara nyingi tunasoma katika mtazamo wetu our own perspective, Hata ingawa tunafahamu kuwa hili ni neno la Mungu na kuwa njia zake sio njia zetu wala mawazo yake sio mawazo yetu, angalia tunapokosea akili zetu hutuambia kuwa tunahitaji kuadhibiwa kwa sababu ya makosa yetu ndio nah ii ndio Haki kabisa, tunajisikia kuwa tumemkosea Mungu na ni lazima tuadhibiwe ndio hiyo ndio haki, sio hivyo tu wanaotuzunguka wanaweza kuona kwamba tumemkosema Mungu na ni vema tukiadhibiwa na ni haki kabisa si tumekosea si amekosea ni haki akaadhibiwa ni haki tukasimamia aadhibiwe ni haki akione cha mtemakuni ni haki akome afundishwe asirudie tena ajutie kosa lake aipate fresh, ashughulikiwe  na ndio usahii wa mambo kwa mawazo yetu ya kibinadamu, Lakini shida au Tatizo la Mungu haangalii mambo kama tunavyoangalia sisi, sisis tunataka haki, tunatadhamia thawabu kwa mtu aliyetenda vizuri na mabaya kwa aliyefanya vibaya Mungu ni tofauti, haangalii kama tunavyoangalia sisi mtazamo wake sio sawa na wa kibinadamu “your perception is not always Gods reality” Mtazamo wako sio ukweli kuhusu Mungu wakati wote. Mungu aliweka mipango kabla sisi hatujazaliwa alijua kipi kitakuwa sahii na kipi hakitakuwa sahii katika maisha alijua wapi utakaa vema na wapi utakosea alijua kabla hajakuumba, na wakati wote huo mpango wake ni kutufanikisha, kuanguka kwetu sio jambo la kushangaza kwa Mungu sio habari hata its not a news yeye anaendelea na mpango wake wa kutufanikisha tu yuko busy kutufanikisha, sio lazima afungwe  na haki, anaangalia mpango wake yuko kwenye kutii mapenzi yake na makusudi aliyotuumba kwayo

Angalia kifungu cha maandiko tulichokisoma pale juu, ni mfano ulio wazi kuhusu neema, kama Paulo angesema Mungu anachagua watu maalumu, wenye akili, wenye cheo, wenye uwezo, waliowakamilifu, watenda mema anawatafuta watu wa aina hii duniani awabariki na kuwatumia kwa utukufu wake, hii ingekuwa ni sawa na inakubalika katika akili ya kawaida Logical na lingekuwa ni jambo jema na wote tungejitahidi sana kuwa wazuri kiasi ambacho Mungu angeshawishika kutuchagua, kama Mungu angekuwa anaagalia watu wa aina hiyo wachapa kazi, wenye bidiii, wasio na maswalimaswali hata katika maswala ya uadilifu, waungwana  kwa akili zetu za kawaida tusingeweza kulaumu chochote maana ni haki tu.

Paulo Mtume alichaguliwa na Mungu na kutumiwa kuandika karibu nusu na zaidi ya agano jipya, kamakuchaguliwa kwake kulitokana na kushinda mashindano ya mitume walio bora tusingelikuwa na maswali maana ni haki, amewashinda mitume wengine, lakini la kushangaza ni kuwa Mtume huyu hakuwa hata katika orodha ya mitume wale 12, wakati Yesu anapaa ndo kwanza huyu alikuwa upande wa pili akiwapiga vita wakristo na kuwatesa vibaya na kusimamia  mauaji yao, aliomba hata kibali cha kuwatesa na kuwaburuza wakristo kila waliko, cha kushangaza sasa Yesu anamchagua huyu na kumtumia kwa kiwango kikubwa kuliko mitume wote, hii inachanganya akili zetu za kawaida hii sio haki, huyu hafai, muuaji mtesi wa kanisa alitakiwa afe, hii ndio ilikuwa haki yake lakini anachaguliwa kuwa mtume hii sio haki kabisa hii ndio NEEMA YA MUNGU!

Sasa tunajifunza nini hapa?
1.       Neema ya Mungu haitendi haki. Unapofundishwa kwa kutishiwa kuwa kila upandacho utavuna au kuna kuvuna kile ulichopanda inakubalika akilini kuwa ni sawa logically unakubali na kuelewa kuwa utakachopanda utavuna, ni rahisi kuelewa kuwa apandacho mtu ndicho atakachovuna hii ni sawa hii ni haki, ni haki mtu mbaya kupatwa na mabaya na mtu mwema kupata mema ni sawa tunavuna kila tunachokistahili, lakini kama tunastahili mema kwa kutenda mema na mabaya kwa kutenda ubaya sasa hapo ni malipo na sio neema tena. Mungu hatendi haki hata kidogo Mungu hufanya mambo kwa sababu anatupenda, anakupenda na ananipenda

2.       Usijaribu kupigana na neema ya Mungu kwa akili za kibinadamu, wakati mwingine ni vigumu kuelewa kwa nini Mungu anafanya kitu Fulani kwako au kwangu, ni muhimu tu kukubali kuwa ni upendo wa Mungu na kupokea kila jambo kwa upendo, upendo wake ndio unaomshukuma afanye kitu katika maisha yetu, Mungu anaposema kuwa anataka kukubariki na kukutumia sana na akili yako inapopambana na kusema mbona sistahili unapigana na neema, Mungu anapombariki mwingine huku unafahamu kabisa udhaifu wake ukaanza kushangaa nankushutumu unapigana na neema ni lazima tukubali kuelemewa na Neema ya Mungu acha kupigana na neema acha




3.       Luka 15: 11- 32 Biblia inasema hivi “11. Akasema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili;   12. yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia. Akawagawia vitu vyake.        13. Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati. 14. Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji. 15. Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. 16. Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu. 17. Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. 18. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; 19. sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.                 20.Akaondoka,akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana. 21. Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena. 22. Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni; 23. mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi; 24. kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia. 25. Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo.  26. Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini?  27. Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima. 28. Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi. 29. Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu; 30. lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona. 31. Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako. 32. Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.” Yesu alitoa ujumbe huu hapo juu kwa sababu ya watu waliokuwa wkipigana na NEEMA YA MUNGU utawezaje kujua kuwa Yesu aliwaonya watu hao ili wasiingilie Kazi anazozifanya Mungu kwa kutumia akili zao logic angalia mistari hii ya awali katika Luka 15:1-2 Biblia inasema hivi  1. Basi watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize. 2. Mafarisayo na waandishi wakanung'unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula naoAngalia maneno ya aya hizi kwa umakini na Mungu akusaidie Yesu alikuwa anajiwa na watu ambao kwa akili za kawaida walikuwa wabaya, waliitwa wenye dhambi, wahalifu kwa hiyo wale watakatifu wenye haki walinung’unika kwa nini mwokozi anatenda jambo kama hili, kwa akili za kawaida ilikuwa ni haki, Yesu ni Mungu na Mungu ni mwenye haki, rafiki zake ni wenye haki, anapaswa kuwahudumia na kuwajali na kukaa nao na kuwatendea mema., Mfano wa Yesu alioutoa kufuatia manung’uniko hayo unaonyesha tena Neema ya Mungu haitendi haki, kwa vipi?

Mwana mpotevu alikuwa tayari amepewa sehemu ya urithi wake na mali yake, alitaka kuishi mbali na baba alitaka kuwa huru, amelelewa vizuri hakuna alichokikosa kwa baba yake sasa anataka kuchukua kilicho chake akaishi maisha ya uhuru, Baba yake alimruhusu, alimuachia alimpa alichokiomba na kukidai, aliondoka na kila kilichochake, alivitumia kwa anasa na maisha ya ukahaba, Hakuna alichobakiza nyumbani. Alichezea mali yake na uhuru wake, alifanya anayoyataka , mwisho yakamkuta mabaya aliishiwa na kupigika sana, hakuna alichobakiza alipoteza uhuru wake akawa kibarua akawal mlisha nguruwe, kwa mtazamo wa kawaida mtoto huyu kibinadamu ungemfanya nini? Alistahili malipo yake angeachwa akione cha mtema kuni angetaharizwa kipi kinakurudisha nyumbani umesahau nini? Umebakiza nini hii ndio haki aliyopaswa kufanyiwa kibinadamu alitakiwa kufukuzwa, angeachwa aonje joto ya jiwe akione cha mtema kuni!
Kutokana na taabu aliyokutana nayo aliamua kurudi kwa baba, Jambo la kushangaza ni kile baba alimfanyia

 “Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana. 21. Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena. 22. Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni; 23. mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi; 24. kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia.” 

 Hiki ndicho alichokifanya baba yake alimuonea huruma maana yake Rehema za baba yake na neema ya baba yake ilimsukuma kumtendea mwanawe sherehe kubwa na kumfanya mfalme Prince na watu wote wa nyumbani kwa babaye walifurahi, Baba alijua kuwa mwanaye sasa anaweza kutofautisha maisha ya uhuru na usalama aliokuwa ameupata kwa baba yake, ni mwanaye ulitegemea atamfanya nini? Mwenyewe alielewa wazi kuwa anapaswa kuwa mtumwa tu, baba akamfanya Prince kijana wa kifalme, tunapokosea sisi na wanaotuzunguka tunategemea kuwa Mungu hawezi kutukubali tena wala kutufanyia mema haya ni mawazo mabaya kwa Mungu wetu ni kuushushia hadhi upendo wake kumbuka kuwa mfano huu na fundisho hili halitii moyo hata kidogo kuishi maisha ya dhambi lakini pia halikubaliani hata kidogo na fikra za majivuno na kiburi cha kujifikiri kuwa wewe unastahili kwa vile ni mwema kuliko Fulani, kipimo cha wema anacho Mungu na kwa rehema zake na neema yake ana haki ya kumuona mmoja kuwa sawa na wewe au kumuona mmoja kuwa bora kuliko wewe hata kama kwa vipimo vyako wajiona kuwa uko sahii, hakuna kiburi kikubwa na kibaya duniani kama kujiona unastahili nje ya neema ya Mungu, kama utakuwa na mawazo hayo utaiona Neema ya Mungu kuwa Haikutendei haki.
Hukumu na aibu ilimkuta ndugu mkubwa badala ya furaha kwake ilikuwa huzuni majuto na mkususa na kukasirika na ilikuwa siku yake ya kuhubiriwa kwamba kwanini afurahii Baba kumpata mwanaye, kwa nini hafurahii baba kumfanyia hserehe mwanaye ni wazi kuwa kwa akili za kawaida kaka mkubwa alijiona ni mwenye haki na mwenye kustahili, lakini lisahau kuwa amejikweza kwa matedno yake ya haki, aka kiburi Mungu huwapinga wenye kiburi bali huwapa wanyenyekevu neema. Haya ndio yaliyomkuta 

“Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo.  26. Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini?  27. Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima. 28. Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi. 29. Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu; 30. lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona. 31. Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako. 32. Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.”

Kama kazi ya baba huyu ingekuwa ni kuhukumu na kutokuhurumia kuacha kuutumia ukarimu wake basi angekuwa ametenda haki, kama baba angemfanyi sherehe mwana wake mkubwa na kumpongeza kwa kuwa mtoto mwaminifu angekuwa ametenda haki na wote tungekuwa na ujuzi na watu wote wangeelewa kuwa Baba ni mtenda haki amemlipa kila mmoja sawa na kutenda kwake sasa tatizo ni Moja Mungu ni wa rehema na neema hapa anaonyesha Upendo, rehema na neema na ndipo linapokuja swala lililowazi linaloacha vinywa vyetu wazi kuwa Neema ya Mungu Haitendi haki kwa nini haitendi haki ili ibaki kuwa Neema, Bila shaka nikisema ni kwa neema sasa kila mmoja atakuwa anaelewa maana ya neema.

Unataka haki unataka Neema? Mimi nachagua Neema ya Mungu.

Sala ya kuomba neema:-

Baba ninakushukuru sana nakushukuru kwa Neema yako, kadiri ninavyojifunza kuhusu neema nagundua mambo ya kushangaza sana, Unajua vema kuliko ninavyojua, na ninavyojijua, unajua mara ngapi nimekosa na mara ngapi nimekulazimisha uingie name hukumuni uniadhibu, na wakati mwingine nimejiadhibu na hata kuadhibiwa na wengine kwa makosa yangu, lakini nashukuru kwa Upendo wako na kwa msamaha wako, umeniita hata hivyo, unanitumia hata hivyo pamoja na kunijua nilivyo, sio kwa sababu ya akili nyingi sana, sio kwa sababu ya kutoka katika familia ya wenye hekima, wenye vyeo, watawala, si kwasababu nimestahili, bali ni kwa neema yako, Kwa neema yako tunawashangaza wengi, kwa neema yako nitakuabudu na kukusifu siku zote za maisha yangu, kwa neema yako Maadui zangu wataisoma namba, kwa neema yako wanaoniwazia mabaya watatahayari, kwa neema yako umewatetemesha na kuwaziba vinywa watesi,kwa neema yako umenipa mema ya umande wan chi, kwa neema yako mdogo atakuwa elfu, kwa neema yako, Kaka zangu na Ndugu zangu wataniinamia, hawataponyoka kamwe katika kongwa langu,kwa neema yako umenibariki, kwa neema yako umeniinua, kwa neema yako kila kinywa kitakachoinuka kinyuma name kitahukumiwa, kwa neema yako utabatilisha kila shauri lisiolo haki dhidi yangu, kwa neema yako, kwa neema yako kila dua mbaya itageuzwa kuwa Baraka kubwa sana kwangu, kwa neema yako utanyamazisha woote walioona hududa dhidi yangu, kwa neema yako kila silaha itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa, nipe kuhubiri, kwa neema, nipe kuimba kwa neema, nitumia kwa neema, weka moyoni mwangu jumbe mbalimbali kwa neema, Neema neema neema

Wimbo kuhusu Neema
Wimbo: Mungu amenihurumia

1. Mungu ametuhurumia, tendo hili kubwa sana,
sikustahili jambo hili, nimelipata bure tu!
sasa najua hayo yote, sasa najua hayo yote,
nasifu rehema zake, nasifu rehema zake

2. Nalistahili kupotea, lakini nahurumiwa,
Mungu amenipatanisha na yeye kwa Yesu Kristo,
sababu hii namtumikia, sababu hii namtumikia,
nasifu huruma yake.

3. Mungu mwenye huruma nyingi, usininyime huruma,
naitafuta siku zote nikiulizwa na watu,
hivi vyote vyatoka wapi? hivi vyote vyatoka wapi?
Nasema ni huruma tu!
Ubarikiwe!

Mungu na wakimbizi:


Ni muhimu kufahamu kuwa kuwahudumia wakimbizi ni mpango wa Mungu!, Leo tutachukua Muda wa kutosha kwa kina na upana na urefu kuangalia huduma muhimu kwaajili ya wakimbizi Duniani, Mwaka 2004 pekee karibia watu milioni tatu na nusu walikuwa ni wakimbizi barani Afrika pekee, ambao walikimbia na kuishi nje ya nchi zao, na wengine zaidi ya milioni kumi walikuwa ni wakimbizi ndani ya nchi zao, wengi walikuwa hawakimbii tumatukio ya majanga ya kiasili nlakini walikuwa wanakimbia matatizo ya kisiasa, ugomvi wa kimadaraka, matatizo ya kidini, ukabila na maswala mengineyo je neno la Mungu linasema nini kuhusu wakimbizi, kanisa limewahi kutafakari nini kuhusu wakimbizi? Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:- 

 Kundi kubwa la wakimbizi wakiondoka Syria, wakimbizi nao ni watu


·         Neno la Mungu na wakimbizi
·         Mungu anawajali wakimbizi
·         Wakimbizi na mafundisho ya agano jipya

Neno la Mungu na wakimbizi:

Biblia inatambua kuweko kwa watu ambao wamewahi kukimbia huko na huko mbali na Nchi zao, kaini alikuwa mtu wa kwanza kufahamu madhara ya ukimbizi Mwanzo 4:12,”Utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake, utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao Duniani” Neno utakuwa mtoro ni sawa na utakuwa mkimbizi. Yakobo na Familia yake waliishimaisha ya ukimbizi kutokana na majanga ya njaa nchini kwao Mwanzo 47:3-4, “Farao akawauliza hao nduguze Kazi yenu ni nini? Wakamwambia Farao, Tumekuja kukaa ugenini katika nchi hii, kwa sababu wanyama wa watumwa wako hawana malisho, maana njaa ni nzito sana katika nchi ya kanaani, Basi twakusihi uturuhusu sisi watumwa wako tukae katika nchi ya gosheni” Yesu pia alikuwa mkimbizi huko Misri kwaajili ya kuokoa Maisha yake yaliyokuwa yakitafuta na mfalme Herode Mathayo 2:13-14. “Na hao walipokwisha kwenda zao tazama malaika wa Bwana alimtokea yusufu katika ndoto, akasema  Ondoka umchukue mtoto na mama yake , ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie kwa maana Herode anataka amwangamize, Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku akaenda zake Misri” ziko sababu mbalimbali na mazingira ya aina mbalimbali yanayoweza kusababisha kila mmoja wetu kuwa mkimbizi kwa namna moja ama nyingine.

Mungu anawajali wakimbizi

Biblia iko wazi kuwa Mungu anawajali wakimbizi, alionyesha kujalia sana maisha ya Kaini hata pamoja na kuwa ukimbizi wake ulisababishwa na makosa yake mwenyewe Mwanzo 4:15. Mungu alimwambia Musa katika Torati kuandaa miji ya makimbilio kwaajili ya wakimbizi watakaokimbilia kutokana na sababu mbalimbali ama ambao watu wangelikuwa wanatafuta kuwaua, Kutoka  21:12-14, Hesabu 35:9-34, Kumbukumbu 4:41-43, 19:3-13, Nyakati 6:42-55. Mungu aliagiza pia kuwa wageni walioambatana na Israel pia wanahitaji kuheshimiwa kimsingi tunapaswa kuwajali aina zote za wakimbizi waliokimbia nchi zao kwa sababu zozote zile ziwe za kisiasa, vita uchumi njaa  na ugumu mwingine wote wanapaswa kuheshimiwa kuhifadhiwa kutunzwa vizuri, kupendwa na kuhifadhiwa,kwa heshima na usawa sawa na raia wengine tukiwahesabu kuwa ni ndugu na jamaa zetu Walawi 25, Isaya 16:1-4, Ezekiel 47:21-23 Lawi 19:33-34.

Wakimbizi na mafundisho ya agano jipya

Agano jipya linasisitiza sana kuwahudumia wageni kuwapenda na kuwajali wenye mateso na masikini Mathayo 25:31-40, tofauti ya ndugu na wakimbizi iliondolewa kabisa katika agano jipya Yohana 13:34 kutokana na umoja wa waamini Yohana 17:20-23 na kutokana na udugu na wote kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo.
Hivyo ni muhimu kwa kanisa kujihusisha na kuwahudumia wakimbizi punde linapotokea swala la wakimbizi na kukutana na mahitaji yao ya muhimu haraka , kama usalama, upendo, chakula mavazi, malazi, maji safi,madawa, Kumbuka kuwa Yesu atakuja kubagua Kondoo na mbuzi kwa misingi ya namna tunavyowajudumia wengine au wenye uhitaji Mathayo 25:31-46, bila huduma hizi ni vigumu kwa wakimbizi kuikubali injili, wanyarwanda wana usemi usemao “Inda irimo ubusa ntigira amatwi” yaani tumbo tupu halina masikio, Ni muhimu kanisa likakumbuka hilo likakumbuka kuwahubiri injili lakini pia kusikiliza injili kutoka kwao ikiwa wanauwezo wa kuhudumu ili kuwalea na kukuza huduma zao punde warudipo au kuwa wamisionari katika taifa letu, hivi ndivyo nyakati za kanisa la kwanza walivyofanya pia Matendo 8;1-4, 18:1-2, Hali hii itainua heshima yao na kuwatia moyo, kanisa pia linapaswa kufanya kitu cha ziada sio tu kuwaletea maji katika birika bali kuwaelekeza namna wanavyoweza kuchimba visima wenyewe ili kujipatia maji, kanisa linapaswa pia kujihusisha katika swala zima la kuangalia chanzo cha ukimbizi na kukishughulikia hii ina maana kuwa kanisa linapaswa kujishughulisha na swala la kufanya upatanisho na kutafuta majibu ya matatizo ili kuyatatua na watu waweze kurejea katika nchi zao kwa amani badala ya kuiacha kazi hiiikafanywa na serikali zaidi, Kanisa ni lazima lisimamie demokrasia, Haki, upatanisho na mswala ya uongozi kwa ujumla, unaweza kufikiri kuwa kazi hii ni ya kiserikali zaidi nay a kijamii zaidi kuliko ya kiroho, lakini nataka nikuambie kuwa ni ya Kiroho zaidi na inapaswa kanisa kuwa sambamba na mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na huduma kwa wakimbizi

Ni muhimu kuwahudumia vema wakimbizi wao pia ni binadamu, kuna historia za kutisha kuwa sehemu nyingine wakimbizi wanabakwa, wanakataliwa, wanawekewa uzio, au wanafanyiwa hila wafe,n.k. hivi karibuni katika nchi ya Syria kutokana na vita kumekuwa na wakimbizi wengi wanaokimbilia ulaya na wengine wanapitia Libiya lakini wengi wamefanyiwa hila wakikimbia kuokoa maisha yao wengine wameuawa na mataifa mengine yameingia hofu ya kuwapokea Mungu isaidie Dunia kuwa mahali panapofaa kukaa ni wajibu wetu kupiga vita kila kinachosababisha watu kukimbia nchi zao na kujaribu kutatua migogoro iliyoko Duniani ili kila Nchi ipate Ustawi unaokusudiwa na Mungu.

Yeye aliye na sikio na alisikie neno hili ambalo Roho aliambia kanisa.