ONYO! “Kama hauna akili ujumbe huu haukufai, Usisome ujumbe huu kama hauna akili hutaelewa”acha!
1Wakoritho 1:26-31 Biblia inasema hivi:-
“26. Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya
kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye
cheo walioitwa; 27. bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe
wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe
vyenye nguvu; 28. tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na
vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; 29.
mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. 30. Bali kwa yeye ninyi
mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na
haki, na utakatifu, na ukombozi; 31. kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye
fahari na aone fahari juu ya Bwana.”
Ndugu zangu unapoyatafakari
maisha kwa undani sana na hasa maisha ya kiroho unaweza kuchanganyikiwa na
ukagundua kuwa kitu au jambo linaitwa neema ya Mungu ni gumu kupokelewa kuliko
unavyofikiri, ni rahisi kutafakari mambo juujuu na ukasema ni kwa neema ya
Mungu lakini neema sio jambo jepesi kama unavyofikiri, leo sitaki kabisa
kufafanua nini maana ya neema kwa vile nafikiri tutazunguka tu lakini natka
kukazia kuwa Neema ya Mungu haitendi Haki! Najua kuwa hii ndio lugha nyepesi
itakayokusaidia leo kuelewa ninapotaka kuizungumzia neema ya Mungu.
Neema ya Mungu haitendi haki
swala hili kwa asili sio sahihii lakini ndio litakalotusaidia leo kuelewa maana
ya neema ya Mungu tukinena kiwazimu, kichwa hiki kinatusaidia kujua kuwa wewe
na mimi sio Mungu na Mungu sio mimi na wewe, wakale walisema “ Mungu sio
Athumani” hebu tufafanue kwa kina zaidi
Tunapoisoma biblia neno la Mungu
mara nyingi tunasoma katika mtazamo wetu our own perspective, Hata ingawa
tunafahamu kuwa hili ni neno la Mungu na kuwa njia zake sio njia zetu wala
mawazo yake sio mawazo yetu, angalia tunapokosea akili zetu hutuambia kuwa
tunahitaji kuadhibiwa kwa sababu ya makosa yetu ndio nah ii ndio Haki kabisa,
tunajisikia kuwa tumemkosea Mungu na ni lazima tuadhibiwe ndio hiyo ndio haki,
sio hivyo tu wanaotuzunguka wanaweza kuona kwamba tumemkosema Mungu na ni vema
tukiadhibiwa na ni haki kabisa si tumekosea si amekosea ni haki akaadhibiwa ni
haki tukasimamia aadhibiwe ni haki akione cha mtemakuni ni haki akome
afundishwe asirudie tena ajutie kosa lake aipate fresh, ashughulikiwe na ndio usahii wa mambo kwa mawazo yetu ya
kibinadamu, Lakini shida au Tatizo la Mungu haangalii mambo kama tunavyoangalia
sisi, sisis tunataka haki, tunatadhamia thawabu kwa mtu aliyetenda vizuri na
mabaya kwa aliyefanya vibaya Mungu ni tofauti, haangalii kama tunavyoangalia
sisi mtazamo wake sio sawa na wa kibinadamu “your perception is not always Gods
reality” Mtazamo wako sio ukweli kuhusu Mungu wakati wote. Mungu aliweka
mipango kabla sisi hatujazaliwa alijua kipi kitakuwa sahii na kipi hakitakuwa
sahii katika maisha alijua wapi utakaa vema na wapi utakosea alijua kabla
hajakuumba, na wakati wote huo mpango wake ni kutufanikisha, kuanguka kwetu sio
jambo la kushangaza kwa Mungu sio habari hata its not a news yeye anaendelea na
mpango wake wa kutufanikisha tu yuko busy kutufanikisha, sio lazima afungwe na haki, anaangalia mpango wake yuko kwenye
kutii mapenzi yake na makusudi aliyotuumba kwayo
Angalia kifungu cha maandiko
tulichokisoma pale juu, ni mfano ulio wazi kuhusu neema, kama Paulo angesema
Mungu anachagua watu maalumu, wenye akili, wenye cheo, wenye uwezo,
waliowakamilifu, watenda mema anawatafuta watu wa aina hii duniani awabariki na
kuwatumia kwa utukufu wake, hii ingekuwa ni sawa na inakubalika katika akili ya
kawaida Logical na lingekuwa ni jambo jema na wote tungejitahidi sana kuwa
wazuri kiasi ambacho Mungu angeshawishika kutuchagua, kama Mungu angekuwa
anaagalia watu wa aina hiyo wachapa kazi, wenye bidiii, wasio na maswalimaswali
hata katika maswala ya uadilifu, waungwana
kwa akili zetu za kawaida tusingeweza kulaumu chochote maana ni haki tu.
Paulo Mtume alichaguliwa na Mungu
na kutumiwa kuandika karibu nusu na zaidi ya agano jipya, kamakuchaguliwa kwake
kulitokana na kushinda mashindano ya mitume walio bora tusingelikuwa na maswali
maana ni haki, amewashinda mitume wengine, lakini la kushangaza ni kuwa Mtume
huyu hakuwa hata katika orodha ya mitume wale 12, wakati Yesu anapaa ndo kwanza
huyu alikuwa upande wa pili akiwapiga vita wakristo na kuwatesa vibaya na
kusimamia mauaji yao, aliomba hata kibali
cha kuwatesa na kuwaburuza wakristo kila waliko, cha kushangaza sasa Yesu
anamchagua huyu na kumtumia kwa kiwango kikubwa kuliko mitume wote, hii
inachanganya akili zetu za kawaida hii sio haki, huyu hafai, muuaji mtesi wa
kanisa alitakiwa afe, hii ndio ilikuwa haki yake lakini anachaguliwa kuwa mtume
hii sio haki kabisa hii ndio NEEMA YA
MUNGU!
Sasa tunajifunza nini hapa?
1. Neema
ya Mungu haitendi haki. Unapofundishwa kwa kutishiwa kuwa kila upandacho
utavuna au kuna kuvuna kile ulichopanda inakubalika akilini kuwa ni sawa
logically unakubali na kuelewa kuwa utakachopanda utavuna, ni rahisi kuelewa
kuwa apandacho mtu ndicho atakachovuna hii ni sawa hii ni haki, ni haki mtu
mbaya kupatwa na mabaya na mtu mwema kupata mema ni sawa tunavuna kila
tunachokistahili, lakini kama tunastahili mema kwa kutenda mema na mabaya kwa
kutenda ubaya sasa hapo ni malipo na sio neema tena. Mungu hatendi haki hata
kidogo Mungu hufanya mambo kwa sababu anatupenda, anakupenda na ananipenda
2. Usijaribu
kupigana na neema ya Mungu kwa akili za kibinadamu, wakati mwingine ni vigumu
kuelewa kwa nini Mungu anafanya kitu Fulani kwako au kwangu, ni muhimu tu
kukubali kuwa ni upendo wa Mungu na kupokea kila jambo kwa upendo, upendo wake
ndio unaomshukuma afanye kitu katika maisha yetu, Mungu anaposema kuwa anataka
kukubariki na kukutumia sana na akili yako inapopambana na kusema mbona
sistahili unapigana na neema, Mungu anapombariki mwingine huku unafahamu kabisa
udhaifu wake ukaanza kushangaa nankushutumu unapigana na neema ni lazima
tukubali kuelemewa na Neema ya Mungu acha kupigana na neema acha
3.
Luka 15: 11- 32 Biblia inasema hivi “11. Akasema, Mtu
mmoja alikuwa na wana wawili; 12. yule
mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia. Akawagawia
vitu vyake. 13. Hata baada ya siku
si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali;
akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati. 14. Alipokuwa amekwisha
tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji. 15.
Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani
kwake kulisha nguruwe. 16. Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula
nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu. 17. Alipozingatia moyoni mwake,
alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na
mimi hapa ninakufa kwa njaa. 18. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na
kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; 19. sistahili kuitwa
mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako. 20.Akaondoka,akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali
mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia
shingoni, akambusu sana. 21. Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya
mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena. 22. Lakini baba
aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na
pete kidoleni, na viatu miguuni; 23. mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje;
nasi tule na kufurahi; 24. kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye
amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia. 25. Basi,
yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba,
alisikia sauti ya nyimbo na machezo. 26.
Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini? 27. Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba
yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima. 28.
Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi. 29.
Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala
sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye
furaha na rafiki zangu; 30. lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu
vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona. 31. Akamwambia,
Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako. 32.
Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa
amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.” Yesu
alitoa ujumbe huu hapo juu kwa sababu ya watu waliokuwa wkipigana na NEEMA YA
MUNGU utawezaje kujua kuwa Yesu aliwaonya watu hao ili wasiingilie Kazi
anazozifanya Mungu kwa kutumia akili zao logic angalia mistari hii ya awali
katika Luka 15:1-2 Biblia inasema hivi “1. Basi watoza
ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize. 2. Mafarisayo na
waandishi wakanung'unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena
hula nao” Angalia maneno ya aya hizi kwa umakini na Mungu akusaidie
Yesu alikuwa anajiwa na watu ambao kwa akili za kawaida walikuwa wabaya,
waliitwa wenye dhambi, wahalifu kwa hiyo wale watakatifu wenye haki walinung’unika
kwa nini mwokozi anatenda jambo kama hili, kwa akili za kawaida ilikuwa ni
haki, Yesu ni Mungu na Mungu ni mwenye haki, rafiki zake ni wenye haki,
anapaswa kuwahudumia na kuwajali na kukaa nao na kuwatendea mema., Mfano wa
Yesu alioutoa kufuatia manung’uniko hayo unaonyesha tena Neema ya Mungu haitendi
haki, kwa vipi?
Mwana mpotevu
alikuwa tayari amepewa sehemu ya urithi wake na mali yake, alitaka kuishi mbali
na baba alitaka kuwa huru, amelelewa vizuri hakuna alichokikosa kwa baba yake
sasa anataka kuchukua kilicho chake akaishi maisha ya uhuru, Baba yake
alimruhusu, alimuachia alimpa alichokiomba na kukidai, aliondoka na kila
kilichochake, alivitumia kwa anasa na maisha ya ukahaba, Hakuna alichobakiza
nyumbani. Alichezea mali yake na uhuru wake, alifanya anayoyataka , mwisho
yakamkuta mabaya aliishiwa na kupigika sana, hakuna alichobakiza alipoteza
uhuru wake akawa kibarua akawal mlisha nguruwe, kwa mtazamo wa kawaida mtoto
huyu kibinadamu ungemfanya nini? Alistahili malipo yake angeachwa akione cha
mtema kuni angetaharizwa kipi kinakurudisha nyumbani umesahau nini? Umebakiza nini
hii ndio haki aliyopaswa kufanyiwa kibinadamu alitakiwa kufukuzwa, angeachwa
aonje joto ya jiwe akione cha mtema kuni!
Kutokana na
taabu aliyokutana nayo aliamua kurudi kwa baba, Jambo la kushangaza ni kile
baba alimfanyia
“Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio
akamwangukia shingoni, akambusu sana. 21. Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa
juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena. 22. Lakini baba
aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na
pete kidoleni, na viatu miguuni; 23. mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje;
nasi tule na kufurahi; 24. kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye
amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia.”
Hiki ndicho alichokifanya baba yake alimuonea huruma
maana yake Rehema za baba yake na neema ya baba yake ilimsukuma kumtendea
mwanawe sherehe kubwa na kumfanya mfalme Prince na watu wote wa nyumbani kwa
babaye walifurahi, Baba alijua kuwa mwanaye sasa anaweza kutofautisha maisha ya
uhuru na usalama aliokuwa ameupata kwa baba yake, ni mwanaye ulitegemea
atamfanya nini? Mwenyewe alielewa wazi kuwa anapaswa kuwa mtumwa tu, baba
akamfanya Prince kijana wa kifalme, tunapokosea sisi na wanaotuzunguka
tunategemea kuwa Mungu hawezi kutukubali tena wala kutufanyia mema haya ni
mawazo mabaya kwa Mungu wetu ni kuushushia hadhi upendo wake kumbuka kuwa mfano
huu na fundisho hili halitii moyo hata kidogo kuishi maisha ya dhambi lakini
pia halikubaliani hata kidogo na fikra za majivuno na kiburi cha kujifikiri
kuwa wewe unastahili kwa vile ni mwema kuliko Fulani, kipimo cha wema anacho
Mungu na kwa rehema zake na neema yake ana haki ya kumuona mmoja kuwa sawa na
wewe au kumuona mmoja kuwa bora kuliko wewe hata kama kwa vipimo vyako wajiona
kuwa uko sahii, hakuna kiburi kikubwa na kibaya duniani kama kujiona unastahili
nje ya neema ya Mungu, kama utakuwa na mawazo hayo utaiona Neema ya Mungu kuwa
Haikutendei haki.
Hukumu na aibu
ilimkuta ndugu mkubwa badala ya furaha kwake ilikuwa huzuni majuto na mkususa
na kukasirika na ilikuwa siku yake ya kuhubiriwa kwamba kwanini afurahii Baba
kumpata mwanaye, kwa nini hafurahii baba kumfanyia hserehe mwanaye ni wazi kuwa
kwa akili za kawaida kaka mkubwa alijiona ni mwenye haki na mwenye kustahili,
lakini lisahau kuwa amejikweza kwa matedno yake ya haki, aka kiburi Mungu
huwapinga wenye kiburi bali huwapa wanyenyekevu neema. Haya ndio yaliyomkuta
“Basi, yule mwanawe
mkubwa alikuwako shamba na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti
ya nyimbo na machezo. 26. Akaita
mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini? 27. Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba
yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima. 28.
Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi. 29.
Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala
sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye
furaha na rafiki zangu; 30. lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu
vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona. 31. Akamwambia,
Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako. 32.
Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa
amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.”
Kama kazi ya baba huyu ingekuwa ni
kuhukumu na kutokuhurumia kuacha kuutumia ukarimu wake basi angekuwa ametenda
haki, kama baba angemfanyi sherehe mwana wake mkubwa na kumpongeza kwa kuwa mtoto
mwaminifu angekuwa ametenda haki na wote tungekuwa na ujuzi na watu wote
wangeelewa kuwa Baba ni mtenda haki amemlipa kila mmoja sawa na kutenda kwake
sasa tatizo ni Moja Mungu ni wa rehema na neema hapa anaonyesha Upendo, rehema
na neema na ndipo linapokuja swala lililowazi linaloacha vinywa vyetu wazi kuwa
Neema ya Mungu Haitendi haki kwa nini haitendi haki ili ibaki kuwa Neema, Bila
shaka nikisema ni kwa neema sasa kila mmoja atakuwa anaelewa maana ya neema.
Unataka haki unataka Neema? Mimi nachagua
Neema ya Mungu.
Sala ya kuomba neema:-
Baba ninakushukuru sana nakushukuru
kwa Neema yako, kadiri ninavyojifunza kuhusu neema nagundua mambo ya kushangaza
sana, Unajua vema kuliko ninavyojua, na ninavyojijua, unajua mara ngapi
nimekosa na mara ngapi nimekulazimisha uingie name hukumuni uniadhibu, na
wakati mwingine nimejiadhibu na hata kuadhibiwa na wengine kwa makosa yangu,
lakini nashukuru kwa Upendo wako na kwa msamaha wako, umeniita hata hivyo,
unanitumia hata hivyo pamoja na kunijua nilivyo, sio kwa sababu ya akili nyingi
sana, sio kwa sababu ya kutoka katika familia ya wenye hekima, wenye vyeo,
watawala, si kwasababu nimestahili, bali ni kwa neema yako, Kwa neema yako
tunawashangaza wengi, kwa neema yako nitakuabudu na kukusifu siku zote za
maisha yangu, kwa neema yako Maadui zangu wataisoma namba, kwa neema yako
wanaoniwazia mabaya watatahayari, kwa neema yako umewatetemesha na kuwaziba
vinywa watesi,kwa neema yako umenipa mema ya umande wan chi, kwa neema yako
mdogo atakuwa elfu, kwa neema yako, Kaka zangu na Ndugu zangu wataniinamia,
hawataponyoka kamwe katika kongwa langu,kwa neema yako umenibariki, kwa neema
yako umeniinua, kwa neema yako kila kinywa kitakachoinuka kinyuma name kitahukumiwa,
kwa neema yako utabatilisha kila shauri lisiolo haki dhidi yangu, kwa neema
yako, kwa neema yako kila dua mbaya itageuzwa kuwa Baraka kubwa sana kwangu,
kwa neema yako utanyamazisha woote walioona hududa dhidi yangu, kwa neema yako
kila silaha itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa, nipe kuhubiri, kwa neema,
nipe kuimba kwa neema, nitumia kwa neema, weka moyoni mwangu jumbe mbalimbali
kwa neema, Neema neema neema
Wimbo kuhusu Neema
Wimbo:
Mungu amenihurumia
1. Mungu ametuhurumia, tendo hili
kubwa sana,
sikustahili jambo hili, nimelipata bure tu!
sasa najua hayo yote, sasa najua hayo yote,
nasifu rehema zake, nasifu rehema zake
sikustahili jambo hili, nimelipata bure tu!
sasa najua hayo yote, sasa najua hayo yote,
nasifu rehema zake, nasifu rehema zake
2. Nalistahili kupotea, lakini
nahurumiwa,
Mungu amenipatanisha na yeye kwa Yesu Kristo,
sababu hii namtumikia, sababu hii namtumikia,
nasifu huruma yake.
Mungu amenipatanisha na yeye kwa Yesu Kristo,
sababu hii namtumikia, sababu hii namtumikia,
nasifu huruma yake.
3. Mungu mwenye huruma nyingi,
usininyime huruma,
naitafuta siku zote nikiulizwa na watu,
hivi vyote vyatoka wapi? hivi vyote vyatoka wapi?
Nasema ni huruma tu!
naitafuta siku zote nikiulizwa na watu,
hivi vyote vyatoka wapi? hivi vyote vyatoka wapi?
Nasema ni huruma tu!
Ubarikiwe!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni