Leo ni sikukuu ya CHRISTIMAS Wakristo wote Nchini tunajiunga na wakristo wengine Duniani katika kuadhimisha siku kuu hii ya Kuzaliwa kwa Mwokozi, Zaidi ya miaka 2000 iliyopita huko Bethelehemu, Katika siku hii muhimu namna hii ni muhimu sana kwetu pia kujifunza na kutafakari kwa pamoja kuhusu kuzaliwa kwa Yesu Kristo, Ingawa kiini kikuu ni kuzaliwa kwa Yesu Kristo eneo kubwa tunatafakari mioyo mioyo ya watu kadhaa wakati wa kuzaliwa kwa Masihi, tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele viwili vifuatavyo:
Wise man means a man versed in magic, witchcraft, or astrology
(Mamajusi maana yake ni mtu anayejishughulisha na Uganga, Uchawi na Unajimu)
·
Maana ya CHRISTIMAS
·
Kuzaliwa kwa Masihi na mioyo ya watu
Maana ya CHRISTIMAS
Neno CHRISTMAS ni muungnaniko wa
Maneno mawili ya KILATINI CHRIST na MASS ambapo maana zake ni kama ifuatavyo
Christ maana yake KRISTO au MASIHI
Mass Maana yake ni Jumuiya au
mjumuiko au Ibada misa au Kuadhimisha
Kwa hiyo neno Christ na Mass
yanapounganishwa tunapata neno CHRISTMAS ambalo maana yake ni Kumuadhimisha
Kristo, au kumuabudu Kristo au jumuiya ya Kristo, maana muhimu zaidi ni
KUMUABUDU KRISTO.
Kuzaliwa kwa mashi na mioyo ya watu.
Ni muhimu kufahamu kuwa leo
tunapoadhimisha kuzaliwa kwa Masihi Biblia inatufunulia kuwa wakati Yesu
anazaliwa huko Bathelehemu. Mioyo ya watu iligawanyika katika makundi kadhaa
ambayo huenda hata leo makundi hayo yakawepo na huenda hata Yesu Kristo
atakaporudi tena mara ya pili atayakuta
1.
Mioyo
ya walimwengu
Yohana 1:10-11 Biblia inasema hivi “Alikuwako
ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu
haukumtambua. Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.” Biblia
inapozungumzia ulimwengu inazungumzia mfumo wa kawaida wa uharibifu wa Dunia
kiyunani Cosmos ni njamii inayojiendesha bila kujali uwepo wa Mungu, Neno lake
wala utawala wake, Ulimwengu siku zote ni mpinzani mkubwa sana wa Historia ya
wokovu, kuifuata dunia hii au mfumo wa ulimwengu huu ni kujifanya adui wa Mungu
Yakobo 4:4 Biblia inasema hivi “Enyi wazinzi,
hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye
kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.” Biblia inamuagiza
kila mtu anayemfuata Yesu Kristo kutokuifuatisha namna ya dunia hii Warumi 12:2 “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali
mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo
mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” Awaye yote ambaye anaifuatisha
namna ya dunia hii yaani mfumo wa ulimwengu huu au kawaida ya ulimwengu huu au
kufanya urafiki na dunia au kuipenda ni wazi kuwa mtu huyo yuko nje na kusudi
na mpango wa Mungu wa kuokoa, Yesu ni mwokozi na alikuja Duniani ili awaokoe
wanadamu lakini awaye yote ambaye hamuanimi ama amesikia habari za Yesu lakini
bado anaupenda ulimwengu huu, huyo amemkataa Yesu, 1Yohana 2:15 “ Msiipende dunia wala mambo yaliyomo katika dunia Mtu
akiipenda Dunia , kumpenda Baba hakumo ndani yake” Unaona! Kumbe watu
wanaofuata kawaida za ulimwengu huu ni raia wa ulimwengu huu wale wanaomfuata
Yesu sio raia wa ulimwengu huu kufuata kawaida ya ulimwengu huu ni dhambi Yesu
alipozaliwa alikuta mioyo ya watu ikiwa iko katika kawaida zao za kila siku za
kijamii na kisiasa na hakukuwa na mtu aliyeonyesha kujali kama Yesu amezaliwa Luka 2:1-7 Biblia inasema “Siku zile amri
ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa
ulimwengu. Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa
liwali wa Shamu. Watu wote wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao. Yusufu naye
aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa
Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi; ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye
amemposa, naye ana mimba. Ikawa, katika
kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo
za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi
katika nyumba ya wageni.” Wakati
Yesu anazaliwa watu wa ulimwengu walikuwa katika sense na agizo la kifalme ili
kuandikishwa hakuna mtu aliyekuwa na wazo la kufikiri kuhusu kuzaliwa kwa
masihi. Watu wengi leo wamekuwa busy na shughuli zao za kila siku za biashara,
kazi kilimo na shughuli nyingine za utafutaji jambo ambalo si baya lakini
hawatoi nafasi ya mioyo yao kufatakari mambo ya Mungu au hata kuhudhuria Ibada
jambo kama hili lilipelekea Yesu kuzaliwa katika hori ya kulishia Ng’ombe kwani
alikosa nafasi kwa walimwengu.
2.
Mioyo
ya wanasiasa.
Kundi hili la
pili ni kundi la wanasiasa kundi hili nalo wakati Yesu alipokuwa anazaliwa
lilishindwa kumpokea, kundi hili katika biblia linawakilishwa na mfalme Herode Mathayo 2:1-7, 12-16 1. “Yesu alipozaliwa
katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa
mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, 2. Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme
wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
3. Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja
naye. 4. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari
kwao, Kristo azaliwa wapi? 5. Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi;
kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, 6. Nawe Bethlehemu, katika nchi ya
Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala
Atakayewachunga watu wangu Israeli. 7. Kisha Herode akawaita wale mamajusi
faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota.”
“12. Nao wakiisha
kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia
nyingine. 13. Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana
alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake,
ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta
mtoto amwangamize. 14. Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda
zake Misri;”
unamuona Herode?
Huyu alikuwa ni mtu wa namna gani
- Alikuwa mtu wa Idumeya na Hakuwa Myhahudi Idumeya ni eneo la Edom watu wa Esau
- Alikuwa Mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa, warumi walimfanya awe kiongozi kibaraka wa Kaisari na mfalme wa jimbo la Galilaya na Uyahudi au Yuda
- Alioa mtoto wa kuhami mkuu
- Na ili aweze kukubalika na wayahudi alijenga Hekalu, Hili ndilo Hekalu ambalo yesu alilitumia alipokuwa duniani
Pamoja na hayo
yote kama tulivyosoma maadniko na sifa za Herode mwanasiasa huyu hakufurahi
aliposikia Yesu amezaliwa, aidha alikusudia kumuua Yesu ingawa ilionekana kama
anampenda Mungu wa wayahudi kwa kuwajengea hekalu, lakini moyo wake
haukumfurahia Mungu hii ndio tabia ya wanasiasa wanaweza kujenga nyumba za
ibada kwa kusudi tu la kuiteka mioyo ya watu kisiasa lakini mioyo yao haiku tayari
kumkaribia Mungu wanaweza kuonekana kama wema wanaposalimia salama za kidini
lakini wanachokitaka sio Mungu sio Yesu bali wanataka mioyo ya kuwapigia kura
kutokana na hali hii neema ya Mungu ilikuwa mbali nah erode na akafa bila
kumshuhudia Masihi, aidha alikuwa tayari kumiza na kuua watoto wengi sana
kwaajili ya kulinda cheo chake na faida yake ni mara ngapi tumeshuhudia, utu
ukitoweka karibu na uchaguzi watu wenye ualbino wakiuawa kama hapa Tanzania kwa
kusudi la watu wajinga na washirikiana kujipatia kibali cha kisiasa Bwana
aliangalie hili na kulikemea!
3.
Mioyo
ya Viongozi wa Kidini
Mathayo 2:1-6 Biblia inasema “1.Yesu alipozaliwa
katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa
mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, 2. Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme
wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
3. Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja
naye. 4. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari
kwao, Kristo azaliwa wapi? 5. Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi;
kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, 6. Nawe Bethlehemu, katika nchi ya
Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala
Atakayewachunga watu wangu Israeli.”
Biblia inaeleza
kuwa Herode aliposikia habari ya kuzaliwa kwa Masihi kutoka kwa Mamajusi
alikusanya Makuhani pamoja na waandishi akatafuta habari kwao Kristo azaliwa
wapi, Makuhani ni viongozi wa dini na waandishi walikuwa ni walimu wa torati
hawa walikuwa ni watu wenye ujuzi sana kuhusu neno la Mungu na unabii lilikuwa
ni kundi la watumishi wa Mungu Mungu anirehemu hapa maana na mimi pia ni
kiongozi wa kidini kundi hili linanihusu na maonyo yake pia yananihusu, Kundi
hili walipouliszwa swali kuwa Masihi azaliwa wapi ilikuwa rahisi kwao kujibu
kutokana na ujuzi wao katika maandiko walitafuta na walimjulisha mfalme kuwa
Masihi anazaliwa bethelehemu kama anenavyo nabii bila shaka walinukuu unabii
katika Mika 5:2 “Bali wewe,
Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako
wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake
yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.” Unaona watu hawa wa
Mungu yaani watumishi walikuwa na ujuzi mkubwa sana kuhusu maandiko, walijua
kuwa masihi ni kiongozi mkubwa ambaye matokeo yake yaani asili yake ni tangu
milele walitambua kuwa kiongozi huyu mkubwa sana na wa kuheshimika sana Duniani
anazaliwa Bethelehemu lakini jambo la kusikitisha viongozi hao wa dini pia
mioyo yao ilikuwa mbali na Mungu, hakuna hata mmoja aliyeonyesha shauku ya
kutaka kumuona Masihi ambaye walikuwa na taarifa zake kuwa ameshazaliwa na
walijua wapi anazaliwa
Ni dhahiri kuwa
kuwa na ujuzi wa maandiko hakuwezi kutupa nafasi ya kuwa na uhusiano wa kweli
na Yesu Kristo, aidha kuwaelekeza wengine neno hakumaanishi kuwa ndio nafasi ya
sisi kukubaliwa na Mungu, kama kwa matendo yetu tutamuabudu Mungu na
kumuadhimisha lakini mioyo yetu iko mbali naye tutakataliwa katika ufalme wa
Mungu Mathayo 15:7-9 “Enyi wanafiki ni
vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu akisema watu hawa huniheshimu kwa
midomo Ila mioyo yao iko mbali nami, Nao waniabudu Bure wakifundisha mafundisho
yakiyo maagizo ya wanadamu” Paulo mtume alikuwa muhubiri wa ngazi yajuu
sana lakini alijionya Ole wangu mimi nisije nikawahubiri wengine kisha mimi
nikawa mtu wa kukataliwa 1Wakoritho 9: 26-27 “26. Hata mimi
napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama
apigaye hewa;27. bali
nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine,
mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.” Kumbe uko uwezekano wa wahubiri
wengi kukataliwa katika ufalme wa Mungu kutokana na mkao wa mioyo yetu, leo hii
wako watumishi wa Mungu wana kesi ziko mahakamani wameshitakiana wakidaiana
mali na hawataki kusameheana, yako matumizi mabaya ya sadaka, uzinifu,
Mafarakano, choyo uadui ugomvi kusemana vibaya na maswala kedekede ni muhimu
kujikumbusha kuwa kuwa na Elimu kubwa za kidini, kutumiwa na Mungu kwa karama mbalimbali
kutoa Pepo na na kufanya unabii kamwe sio tiketi ya kutufanya tuingie katika
ufalme wa Mungu ni jambo la kustaabisha kuwa viongozi wa dini ndio waliokuwa
mstari wa mbele katika kumpinga Yesu Kristo na hata kutafuta namna ya kumuua
Mungu unikumbuke na kunisamehe na kamwe usinipite na kuniacha
4.
Mioyo
ywa watu Masikini na waliokata tamaa
Ni jambo la
Kushangaza kuwa Mungu anawaangalia sana wanyonge masikini na waliokata tamaa
wakati dunia haijali na mfumo wa dunia hauwajali watu masikini Mungu aliwapa
neema watu duni, walikuwa hawana ujuzi wa maandiko wala hawako karibu na ikulu,
na huenda walikuwa wamejikatia tamaa Mungu aliwatuma malaika zake kutoa habari
maalumu kwa kundi hili kuwa masihi amezaliwa
Luka 2:8-20 Biblia inasema hivi “8. Na katika nchi
ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu
usiku. 9. Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria
pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. 10. Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa
mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; 11.
maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo
Bwana. 12. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za
kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe. 13. Mara walikuwapo pamoja na
huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema, 14.
Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. 15.
Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana,
Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika,
alilotujulisha Bwana. 16. Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na
yule mtoto mchanga amelala horini. 17. Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa
juu ya huyo mtoto. 18. Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na
wachungaji. 19.Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni
mwake. 20. Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa
mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa”. Ni jambo la
kushangaza kabisa kuwa malaika aliwaambia wachungaji hao kuwa Leo hii katika
mji wa Daudi amezaliwa kwaajili yenu Mwokozi ndiye Kristo Bwana natamani kabisa
Mungu angenifanya maalumu kama wachungaji hawa ni watu wanyenyekevu wenye mioyo
iliyopondeka hawakuwa na ujuzi wa neno hawakuwa wanasiasa lakini Mungu
hakuwanyima vyote aliwapa habari njema na hili likawa kundi la kwanza kwenda Bethelehemu
na kujionea kundi hili likatoa habari ya kuzaliwa kwake Yesu kristo na
kushangaza watu, hii ndio ilikuwa iwe kazi ya makuhani lakini mioyo yao
iliwanyima kumjua masihi mioyo iliyopondeka aidha hawa waliishuhudia kundi la
malaika wakiimba kwa furaha na kumtukuza Mungu kuhusu kuzaliwa kwa masihi mwe
Mungu ni Mungu wa waliotupwa wanyonge na waliohesabika kuwa si kitu, Mungu
huwapinga wajikwezao bali huwapa neema wanyenyekevu.
5.
Mioyo
ya watu wenye subira.
Kundi hili
linawakilishwa na Simeon na Anna Binti Fanuel Simeon alikuwa mtu Mcha Mungu na
nabii alikuwa mwenye haki na alikuwa akisubiri kwa shauku kuzaliwa kwa masihi
alikuwa ni mzee mmno lakini Roho Mtakatifu alikuwa amemwambia kuwa hatakufa
mpaka amemwona masihi, huyu alikuwa mtu mvumilivu umri wake ulikuwa umekwenda
lakini bado alikuwa akiutazamia ukombozi, alipomuona masihi Roho Mtakatifu
alimuonyesha wazi habari za Mtoto huyo kule hekaluni na sasa alifurahi na kutoa
unabii kuhusu Mateso ya Yesu lakini sasa alikuwa tayari kufa kwa amani kwa vile
Mungu alikuwa amemtimizia ahadi, Anna binti Fanuel mjane alikaa ujane miaka 84
aliishi na mume miaka 7 tu alidumu katika maombi mwanamke huyu pia alikuwa
nabii yeye naye aliwaeleza wazi wote waliokuwa wakisubiria habari zake na
kuwathibitishia kuwa huyu ni masihi
Luka 2 25-38 “ 25.
Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu
mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu
alikuwa juu yake. 26. Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona
mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27. Basi akaja hekaluni ameongozwa na
Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama
ilivyokuwa desturi ya sheria, 28. yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake,
akamshukuru Mungu, akisema, 29. Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa
amani, kama ulivyosema; 30. Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako, 31.
Uliouweka tayari machoni pa watu wote; 32. Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na
kuwa utukufu wa watu wako Israeli. 33. Na babaye na mamaye walikuwa
wakiyastaajabia hayo yaliyonenwa juu yake. 34. Simeoni akawabariki, akamwambia
Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio
katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. 35. Nawe mwenyewe, upanga
utaingia moyoni mwako, ili yafunuliwe mawazo ya mioyo mingi. 36. Palikuwa na
nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake
ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. 37.
Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu
usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. 38. Huyu alitokea saa ile ile
akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu
akawatolea habari zake.” Ni
muhimu kwa kila mmoja wetu kuwa mtu mwenye subira na mwenye uvumilivu huku
tukimtazamia masihi bila shaka hatuataibika atakapofunuliwa Bwana wakati wa
kuja kwake mara ya pili, watu wa rohoni kama ilivyo kwa Simeon na Anna
wataelewa wazi Kristo atakapokuja na halitakuwa fumbo kwao hawa walikuwana
mioyo yenye kusubiri
6.
Mioyo
ya watu wasiotegemewa.
Kundi hili
linawakilishwa na jamii ya Mamajusi hili nimeliita kundi la watu wasiotegemewa
kwa vile hawakuwa wanamjua Mungu kabisa, hawakuwa na ujuzi wa neno la Mungu,
walitokea nchi ya mbali sana na ndio watu wa kwanza kugundua kuwa Kuna Mfalme
mkubwa sana wa Wayahudi amezaliwa na kwa vile wafalme huzaliwa ikulu walisafiri
kutoka Ukaldayo au mashariki ya mbali yaani Iraq kwa kuchunguza nyota mpaka
wakagundua kuwa masihi amezaliwa,\
Ni muhimu
kufahamu kuwa watu hawa walijulikana kama watu wenye Hekima na walikuwa ni watu
wenye ujuzi na maswala ya nyota yaani wanajimu walihusika na maswala ya uchawi
pia Daniel 2: 2 huko ukaldayo kulipotokea jambo gumu sana wao zamani walikuwa
ni watu waliotegemewa kutoa majibu Daniel
2: 2 inasema hivi “Ndipo mfalme akatoa amri kuwaita waganga, na wachawi, na
wasihiri, na Wakaldayo, wapate kumweleza mfalme ndoto zake. Basi wakaingia,
wakasimama mbele ya mfalme.” Wakristo wengi na wataalamu wa maandiko
hufikiri nkuwa Mamajusi walikuwa watu wazuri na watakatifu Hapana lilikuwa ni
kundi la Waganga, wachawi na wasihiri yaani wapiga lamri hawa sasa walikuwa
wanajimu kama ilivyokuwa kwa Marehemu Yahaya Husein kwa hapa Afrika mashariki ndio
maana hili ni kundi la watu wasiotegemewa Mungu aliruhusu katika ufahamu wao na
unajimu wao kuona Nyota iliyomuhusu Masihi na kwa moyo waliokuwa nao walijua
kuwa wanapaswa kumsujudia na kumuabudu na cha kushangaza zaidi ni kuwa Mungu
alisema nao na kuwaonya wasiende kwa Herode maana anataka kumuua mtoto nao
wakarudi kwao kwa njia nyingine
Mathayo
2:10-12 “10.
Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno. 11. Wakaingia nyumbani,
wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao
walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na
manemane. 12. Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode,
wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.”
Ni wazi kuwa
kundi hili linawakilisha watu watakaoingia katika Ufalme wa Mungu bila sisi
kuwatarajia, Mungu haukumu wala hatazami kama wanadamu watazamavyo, sikun ya
hukumu na katika ufalme wa Mungu tunaweza kabisa kushangaa wale tunaowadhani
ndio wakawa sio na wale tunawadhani sio wakawa ndiyo, Mioyo iliyopondeka Mungu
huiangalia sana , unyonge na kutokujihesabia haki ni wazi kuwa kama mioyo yetu itafanana na makundi makuu matatu
ya awali tunaweza tukajikuta tumekataliwa katika ufalme wa Mungu, ni jukumu letu
kuangalia na kujiangalia na kujipima namna tunavyoeneda ni mioyo ya makundi
matatuya mwisho ndio ambao waliweza kupata nafasi ya kumuadudu Yesu yani
kusheherekea CHRISTMAS jihoji je wewe utaweza kuisherekea siku hii na
unaisheherekea katika mkao upi wa Moyo?
Ujumbe. Na Mkuu
wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent
Kamote.