Alhamisi, 5 Agosti 2021

Fanya ile taa iwake Daima!


Mambo ya walawi 24:2-4Waagize wana wa Israeli kwamba wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya ile nuru, ili hiyo taa iwake daima. Hapo nje ya pazia la ushahidi, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeza tangu jioni hata asubuhi mbele za BWANA daima; ni amri ya milele katika vizazi vyenu.  Atazitengeza hizo taa katika kile kinara kilicho safi mbele za BWANA daima.”

Kutoka 27:20-21Nawe waamuru wana wa Israeli wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya nuru, ili kufanya ile taa kuwaka daima. Ndani ya ile hema ya kukutania, nje ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeza tangu jioni hata asubuhi mbele ya BWANA; itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israeli.”

 


Utangulizi:

Moja ya fanicha muhimu sana ambazo ziliwekwa katika Hema ya kukutania na baadaye katika hekalu lililokuwako Yerusalem, ni pamoja na taa ya dhahabu yenye vinara saba,taa hii ilitengenezwa wakati wa Torati kwa maelekezo ya Mungu mwenyewe kwa mtumishi wake Musa huko jangwani, Taa hii ambayo ilipaswa kuwaka kwa kutumia mafuta ya zeituni ilipaswa kuwaka daima, Waebrania wanaiita taa hii yenye vinara saba Menorah, Ni moja ya alama muhimu sana kwa watu wote wanaoamini maandiko lakini ni ya muhimu zaidi kwa wayahudi na wakristo, Taa hii imekuwa ni alama muhimu ya Kiyahudi na ndio nembo ya taifa la Israel kwa sasa.

Hema ya kukutania pamoja na hekalu lililokuwako Yerusalem ilikuwa ni ishara ya mpango wa Mungu kukaa katikati ya wanadamu na kushirikiana nao, Hema ile ya kukutania pamoja na Hekalu lilikuwa limegawanyika katika maeneo makuu matatu:-

1.       Ua wa nje ambao ulikuwa umetengenezwa kwa Mapazia maalumu na kulikuwa na Madhababu ya shaba kwa sadaka za kuteketezwa na Bakuli la shaba la kutawadhia, ua wa nje ulikuwa ni maalumu kwa watu kufika na kufanya ibada na kutoa kafara za wanyama kwa mujibu wa maelekezo ya Torati. Nuru iliyoangaza mahali hapa ilikuwa nuru ya asili ya mwanga wa jua tu.

 

2.       Mahali patakatifu, kutoka uwa wa nje mtu angeingia ndani ambapo pamefunikwa na mapazia maalumu, mahali hapa waliingia makuhani tu, hapa palikuwa na Meza ya mikate ya wonyesho, Madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba na taa ya dhahabu yenye vinara saba, ni makuhani tu walioruhusiwa kuingia hapa tena wakiwa wamejitakasa kwa maelekezo maalumu, Nuru iliyotakiwa kuangaza mahali hapa ilikuwa ni ile taa yenye vinara saba.

 

 

3.       Patakatifu pa patakatifu, hapa ni chumba cha ndani zaidi, ni eneo ambalo lilikuwa limetengana na patakatifu, palitengwa na pazia maalumu, ndani yake kulikuwa na lile sanduku la agano lililotengenezwa kwa dhahabu na Makerubi waliofunikia kiti cha rehema kwa mbawa zao Nuru iliyoangaza mahali hapa ilikuwa ni nguzo ya wingu la utukufu wa Mungu mwenyewe

Ile taa

Kwa mujibu wa maelekezo ya Mungu kupitia mtumishi wake Musa, waliagizwa watu watengeneze mafuta ya mzeituni na kisha wayapeleke hekaluni kwaajili ya taa hii ya dhahabu yenye vinara saba na kwamba wahakikishe kuwa taa hii inawaka daima, ingawa ni kuhani tu aliyepaswa kuingia hemani, na kuhakikisha kuwa taa inawaka lakini kumbuka watu walishiriki kwa kuchangia mafuta kwa msingi huo kila mtu alishiriki. Walawi 24:1-4 “Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Waagize wana wa Israeli kwamba wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya ile nuru, ili hiyo taa iwake daima. Hapo nje ya pazia la ushahidi, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeza tangu jioni hata asubuhi mbele za BWANA daima; ni amri ya milele katika vizazi vyenu.  Atazitengeza hizo taa katika kile kinara kilicho safi mbele za BWANA daima.”

Umuhimu mkubwa sana wa ile taa yenye vinara saba ni kutoa huduma, yenye kusababisha makuhani waweze kufanya wajibu wao wa kufanya mamombi kwaajili ya watu na kuwapatanisha na Mungu, kumbuka eneo hili lilikuwa limefunikwa kwa mapazia mazito ya ngozi, na kwa sababu hiyo kwa vyovyote vile mahali hapo palikuwa pana giza, kwa hiyo ingekuwa ni vigumu kwa viongozi wa kiroho kuendelea kuutafuta usio wa Bwana kwaajili ya watu wake kama taa hii muhimu yenye vinara sana haingelikuwepo, kwa hiyo taa hii ilikuwa muhimu kwaajili ya kuwawezesha makuhani kufanya wajibu wao, na taa ingeweza kuwaangazia waone madhabahu ua dhahabu ya kufukizia uvumba ba maombi, na pia waweze kuiona meza ya mikate ya wonyesho na kuwawezesha hivyo makuhani kuwa na ushirika na Mungu na kuwaiombea watu wa Mungu kwa niaba yao!

Maana ya ile taa yenye vinara saba!

Ni muhimu kufahamu kuwa taa hii ya dhahabu yenye vinara saba imekuwa ikileta utata sana miongoni mwa wana theolojia kutokana na kuwa na mitazamo mbalimbali hasa inayosababishwa na uwepo wa vinara sana, kwa hiyo imeleta changamoto kwa wayahudi na wakristo katika kufikiri namna halisi ya kutafasiri taa hii, yako majibu na mitazamo mbalimbali kuhusiana na taa hii

·         Wengine hufikiri kuwa taa hii inazungumzia siku sita za uumbaji wa Mungu na siku ya saba ya mapumziko ya kisabato kwa taa ile ya kati kati ya saba

 

·         Wengine hufikiri kuwa labda taa hii inawakilisha wazo la Hekima na uahamu wote unaokusudiwa na Mungu kama utakavyokuwa juu ya masihi  Isaya 11:2-3 “Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana;  na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;”

 

·         Wengine hufikiria kuwa taa yenye vinara saba kwa wayahudi inahusishwa na kusheherekea sikukuu ya Hanukkah ambayo maana yake ni sikukuu ya Nuru kwa hivyo moja kwa moja wanachukua maana ya neno Menorah jina la ile taa ambalo maana yake kuangaza kwa hiyo ni kama taa hii ina ujumbe wa amka uangaze.

 

 

·         Wengine huzungumzia kuwa taa yenye vinara saba huwakilisha uwepo wa kuhani mkuu Yesu Kristo ambaye ndie asili ya nguvu ya kanisa hasa kutokana na maono ya kitabu cha ufunuo katika Ufunuo 1;12-13 “Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu; na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini”.

 

·         Na wengine kutokana na asili hii ya kitabu cha ufunuo wannamuona Yesu ambaye ndie mmiliki wa kanisa katika nyakati zote hivyo wanahusisha na Historia ya Kanisa tangu ufunuo mpaka kurudi tena kwa Yesu kwa hiyo wao huzungumzia nyakati saba za kanisa ona yaani Makanisa yale saba katika kitabu cha ufunuo pia huwakilisha nyakati saba za kihistoria katika kanisa tangu wakati wa kanisal  la kwanza  siku ya pentekoste hata wakati wa kuja kwa Bwana, haya pia yanaweza kuwa makanisa au madhehebu ambayo yana mapungufu mbalimbali na baraka mbalimbali sambamba na hali ya yale makanisa saba, makanisa hayo pia yanawakilisha Roho za kinabii Ufunuo 19;10.

 

o   Apostolic Church 33-100 Kanisa la wakati wa Mitume kanisa lenye shughuli.

o   Persecuted Church 100-113 kanisa la Karne ya kwanza lililoteseka

o   Imperial Church 313- 476 Kanisa la kpindi cha lililopata ushindi na kanisa lililokosea

o   Medieval Church 476-1453 kanisa lililopoa kipindi cha giza kanisa lenye tatizo

o   Reformed Church 1453-1648 kanisa la kimapinduzi kanisa lililotazama nyuma

o   Morden church 1648-1970 kanisa la leo kanisa la kiinjilisti

o   Morden charismatic church 1970 mpaka leo. Kanisa lenye mafanikio

 

§  Fanya ile taa iwake Daima!

 

Tumeona kuwa kuna dhana tofauti tofauti kuhusiana na mafundisho yaliyoko katika taa yenye vinara saba vyovyote vile watu wanavyofikiri Mungu Roho Mtakatifu alinirudisha mimi kujiuliza kwanini Mungu akazie kuwa taa ile iwake fanya taa iwake daima hii maana yake ni kuwa kama taa ile ingezimika makuhani wasingeliweza kuona, wasingeliweza kufanya majukumu yao ya kila siku, wasingeliweza kupatanisha watu na Mungu kwani sehemu ya huduma ya upatanisho ingekuwa iko giza, Taanyenye vinara saba ninatufundishan kuhakikisha kuwa uhusiano wetu na Mungu unadumu kila siku na kuwa tunakuwa karibu naye kila siku, tyunapodumisha uhusiano wetu na Mungu tunapewa nafasi ya kuona na kufikiri na kutambua mambo kama Mungu anavyoona, kuna matokeo makubwa sana kwa kanisa kuhakikisha kuwa tunadumisha uhusiano na Mungu, kuhakikisha kuwa taa inawaka daima ni sawa na kuhakikisha kuwa hatuvunji uhusiano wetu na Mungu, sio makuhani tu watru wote wanapaswa kushiriki katika kuhakikisha kuwa wote kwa pamoja na kanisa kwa pamoja na Israel kwa pamoja wanadumisha uhusiano wao na Mungu, kukua kwetu kiroho na kuona Mungu akijishughuklisha na maisha yetu kutakuwa dhahiri endapo imani yetu na upendo wetu utaendelea kuwa pamoja na Yesu daima, Mungu hana mpango wa kutuacha yeye ameahidi kuwa atakuwa pamoja nasi ni sisi ndio twenye wajibu wa kubaki ndani yake lakini yeye ameahidi kuwa hatatuacha wala hatatutupa nje kamwe ona

Yoahana 6:37 “Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe”.

Isaya 41:10 “usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.”

Mika 7:8 “Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, Bwana atakuwa nuru kwangu.”           

Torati 31:6-8 “Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha. Musa akamwita Yoshua, akamwambia machoni pa Israeli wote, Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana utakwenda pamoja na watu hawa hata nchi Bwana aliyowaapia baba zao, ya kwamba atawapa; nawe utawarithisha. Naye Bwana, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike.

Usalama wetu uko ndani ya kudumisha mahusiano yetu na Mungu, taa ile ilitakiwa kuwaka daima ili makuhani waendelee kutoa huduma za kiungu kwa watu, tunapodumisha uhusiano wetu na Mungu ndipo tunapokuwa salama na ndipo tunapoweza kusema kwa ujasirimkuwa Bwana ni Nuru yangu na wokovu wangu nimuogope nani

 

Zaburi 27:1-3 “   Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini.”

 

Mtu wa Mungu kama unataka kufanikiwa usiharibu wala usiruhusu uhusiano wako na Mungu ukavunjika unao wajibu wa kuleta mafuta na kuhakikisha kuwa taa ile haizimiki, fanya ile taa iwake daima Mungu alimuita Samuel na kusema naye wakati ambapo taa ile haijazimika 1Samuel 3:1-3 “Basi, mtoto Samweli akamtumikia Bwana mbele ya Eli. Na neno la Bwana lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri. Ikawa wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona), na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku la Mungu;   uhusiano wetu na Mungu, kujibiwa maombi, kuisikia sauti ya mungu, kukuia kwetu kiroho, kupata ufunuo mpya, maelekezo maono, nuru, kujua siri za Mungu, kuwa na karama na vipawa, ujuzi na taarifa za kiungu kutakuwa hai katika maisha yetu kama taa ya Mungu haijazimika ile taa tukiiacha ikazima tumekwisha ! twende kwa nani Bwana wewe unayo maneno ya uzima wa milele!

 

Na Rev. Innocent Samuel Kamote

 

Mkuu wa wajenzi mwenye hekima !

Kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo!


1Timotheo 4:7-8Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa. Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.”


Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa kufanya mazoezi ni moja ya sehemu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu, Mazoezi yana faida kubwa sana katika maisha haya, Mazoezi yana faida kubwa sana kwa afya zetu, Nyakati za Kanisa la kwanza wakati wa utawala wa kirumi jamii ya watu wa dunia ya wakati ule walifanya sana mazoezi, Michezo ya tamaduni za kiyunani Olympics ilikuwa imeshika kasi sana kwa hivyo watu wengi walifanya mazoezi ya aina mbalimbali, kwa sababu mbalimbali na walikuwa na afya njema, Nyakati za leo wakristo wamepuuzia sana mazoezi, aidha kwa sababu wanafikiri kuwa Biblia haizungumzii mazoezi, ama kwa sababu ya tafasiri mbaya ya Mstari wa msingi niliounukuu hapo juu! Lakini kula utakavyokula, zingatia maelekezo ya aina yoyote ile ya kiafya kama utaweka mazoezi pembeni hutaweza kuwa na afya njema, magonjwa mengi sana yameikumba dunia na watu wengi sana hata wakristo wanaumwa magonjwa ya iana mbalimbali, lakini mengine yanaweza kuepukika, kupunguzwa au hata kujikinga kama kanisa litaelewa umuhimu wa mazoezi, miili yetu ni Hekalu la Roho Mtakatifu, na kwa sababu hiyo Maandiko yanatuagiza kuitunza na namna mojawapo ambayo tunaweza kulitunza hekalu la Roho wa Mungu ni pamoja na kufanya mazoezi kama nitakavyofafanua kwa kina ona 1Wakoritho 6:19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;

Kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo!

Kama nilivyogusia awali katika utangulizi, kwamba kumekuwa na tatizo kubwa sana la kiafya katika nyakati za leo hata kwa wateule, nchini Marekani kwa mfano watu wamekuwa na tatizo kubwa la uzito unaopitiliza, ulaji wa hovyo, usio wa kiasi na uliokosa nidhamu ikiwa ni mojawapo ya sababu zinazopelekea watu kuwa mabonge na hatimaye baadaye kumlaumu Mungu kana kwamba ndiye aliyewashikia kijiko wale Maandiko yanatuonya dhidi ya ulafi na kututaka tuwe na kiasi wakati wa kula  Mithali 23:2 “ Tena ujitie kisu kooni, Kama ukiwa mlafi sio hivyo tu lakini ili tuweze kuwa na afya imara, na kuwa wakakamavu kama askari wema wa Yesu Kristo hatuna budi kuwa na wakati wa kufanya mazoezi, Mazoezi yana uwezo mkubwa sana wa kutuimarisha, na kutulinda na magonjwa, yako magonjwa mengi sana ambayo yanaweza kuepukika endapo tutakuwa na tabia ya kufanya mazoezi, magonjwa kama Kisukari, Kansa, Moyo, presha na hata kuondoa mawazo kunaweza kuwa mbali nasi kama tutajali afya zetu na kujihusisha kufanya mazoezi.

 Kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo!

Kuna shida fulani katika tafasiri ya maandiko ya mstari huu 1Timotheo 4:7-8Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa. Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.” Watafasiri wengi wa maandiko wamefikiri kwamba labda huenda Paulo mtume amekataza mazoezi, au ameyapuuza mazoezi HAPANA Maandiko haya hayakatazi watu kufanya mazoezi, isipokuwa Paulo mtume anataka kuonyesha kuwa kujitia nidhamu katika kuishi maisha matakatifu kunafaa zaidi kwa maisha haya nay ale ya uzima wa milele! Ilivyo ni kuwa nyakati za Kanisa la kwanza utamaduni wa Kigiriki (Wayunani) ulikuwa umeitawala sana Dunia na kuiathiri hata wakati wa utawala wa kirumi, watu walishika lugha na tamaduni za kigiriki ikiwa ni pamoja na tamaduni za michezo ya aina mbalimbali, zingatia kuwa Michezo ya Olympics ilikuwa imeshika chati ya dunia ya wakati ule, hivyo watu walishiriki michezo ya aina mbali mbali lugha kubwa ya wakati ule ilikuwa ni michezo na hata mifano ya wahubiri wa wakati huo ilitoka kwa wanamichezo ona mfano 1Wakoritho 9:24-27 “Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate. Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika. Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.” Unaona Paulo mtume anatumia mifano ya wanamichezo na nidhamu kubwa waliyo nayo wanamichezo na kuifananisha na namna watu wa Mungu wanavyopaswa kujitia nidhamu ili waweze kupata taji isiyioharibika, Kwa hiyo ulikuwa ni ulimwengu uliotawalaiwa na michezo na lugha nyingi sana zilikuwa za kimichezo ikiwepo mifano hii aliyoitioa Paulo Mtume.

Kwa msingi huo ni wazi kuwa wat wa jamii ya wakati ule  walikuwa wamehamasika sana katika kujishughulisha na michezo au hata mazoezi na wengine wakijitia nidhamu kwaajili ya mazoezi, Mazoezi yalipewa kipaumbele na umuhimu sawa na kuwekwa katika kiwango kimoja na maswala kadhaa yafuatayo

1.       Kujiwekea akiba Mathayo 6:19-21 “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.”

 

2.       Kutulia na kutafakari Luka 10:41-42 “Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.”

3.       Kujinyima au kujizuia 1Timotheo 5:6 “Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai.”

 

4.       Kufanya kazi Yohana 6:27 “Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.”

 

 

5.       Kujipamba kwa wanawake 1Petro 3:3-6 “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote.”

 

6.       Kufanya Mazoezi 1Timotheo 4:7-8Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa. Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.”         

Unapotafakari Mistari hiyo hapo juu inayokazia mambo yaliyopewa kipaumbele nyakati za Biblia utaweza kuona kuwa wahudumu wa agano jipya waliyatumia mambo yaliyokuwa yamewekewa mkazo na jamii kama somo la kuwekea mkazo jambo lililo la muhimu zaidi kwaajili ya Mungu au kwaajili ya uzima wa milele, Mfano kujiwekea akiba wote tu nafahamu umuhimu wake lakini kujiandaa kwaajili ya maisha milele ni kwa muhimu zaidi kuliko akiba ya kawaida ya dunia hii ambayo ni ya kitambi tu hivyo maandiko hayajakataza kuweka akiba, kutulia miguuni pa Yesu na kumsikiliza au kutafakari ni fungu jema zaidi, kuliko kujitaabisha kwaajili yake, Yesu hakumkataza Martha kufanya kazi, lakini alifurahishwa na kusikilizwa zaidi, kuliko kutumikiwa, kujinyima kuishi maisha ya UTAWA, kutokuoa au kuolewa ni kuzuri, nidhamu wakati wa michezo kampi na kadhalika, kujinyima vyakula Fulani na kujizuai kwa aina yoyote ni kwa muhimu kama mtu anataka lakini kujizuia nafsi ni kwa muhimu zaidi, Kufanya kazi kwaajili ya kupata ridhiki au chakula ni kwa Muhimu na Yesu hazuii hali hiyo lakini kufanyia kazi uzima wa milele ni kwa Munhimu zaidi, kujipamba kwa kusuka nywele na vito vya thamani ni kwa muhimu lakini, kujipamba kwa tabia njema na kujiheshimu ni kwa muhimu zaidi kuliko mapambo yanayoharibika, kufanya mazoezi kwaajili ya afya ni kwa muhimu sana lakini kujizoeza kuishi maisha matakatifu ni kwa muhimu zaidi., kwa msingi huo Lugha ile ya kibiblia hakimumaanisha kuwa mazoezi hayafai, yanafaa kidogo, kidogo hii na maana gani yataimarisha afya zetu, tutakuwa imara, kutakuwa na afya njema lakini mazoezi haya hayazuii mtu kutwaliwa na bwana, wala hayaongezi muda wa maisha yetu duniani, kwa hiyo Lugha inayotumika hapo ni sawa na ile tu kama watu wanatoa kipaumbele kujiwekea akiba Hazina duniani basin a watoe kipaumbele kikubwa kijiwekea akiba au hazina mbinguni, andiko linamaana ya wazi kwamba lolote linalopewa kipaumbele zaidi kuliko mambo ya Mungu, iwe ni TV, iwe ni mpira, Gemu,  na vikachukua nafasi ya Mungu kwa kukosa kiasi hilo haliwezi kuwa jambo jema hata kidogo, Maandiko yanachokitaka hata kama kitu sio dhambi ni muhimu kisipewe kipaumbele kuliko maswala ya ufalme wa Mungu ambayo ndio kwa mujibu wa maandiko ni Muhimu zaidi Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Unaona ndio maana Paulo akasema yanafaa kidogo, kama michezo na mazoezi ynapewa muda mwingi na mkubwa zaidi kuliko kujisomea neno, kuomba au kushuhudia, kutembelea wagonjwa, kuhudhuria ibada, hilo ndio tatizo, kuna faida gani ya kuwa na nguvu na uimara wa kimwili kama roho zetu ni legevu?  Kwa hiyo kimsingi Paulo hajaondoa umuhimu wa Mazoezi, wala mazoezi sio dhambi na yana umuhimu mkubwa sana yatatuweka sawa kiakili, kisaikolojia, kutulinda na magonjwa na kutupa nafasi ya kumtumikia Mungu tukiwa na afya njema lakini yasichukue nafasi kubwa ya kupuuzia mambo ya Mungu, Hilo tu!

Umuhimu wa Mazoezi katika mwili wa mwanadamu:

Kuna faida kubwa nyingi sana za kufanya mazoezi, tafasiri mbaya za kimaandiko, zimewanyima sana wakristo tabia ya kufanya mazoezi kiasi ambacho sasa makanisani kuna magonjwa ambayo yangeweza kudhibitiwa tu na tabia ya kufanya mazoezi, badala ya kufanyiwa maombezi, wakati mwingine Mungu anaweza kutushangaa kwamba unamuombea mtu tatizo ambalo labda amefanya tu uzembe na angeweza kulitunza hekalu la Mungu kwa mazoezi, wakati mwingine mtu anaweza kunenepa sana kumbe sababu yake ni stresses tu,  mtu akifanya mazoezi pia anaongeza uwezo wa kujiamini,  Neema na iongezewe kwako unapozingatia umuhimu wa mazoezi:

a.       Mazoezi yanasaidia kudhibiti uzito usiokuwa wa kawaia

b.      Mazoezi yanasaidia kutukinga na magonjwa ya aina mbalimbali

Mfano:

o   Kupooza au kiharusi

o   Shinikizo la damu

o   Aina zote za kisukari

o   Kupunguza stresses yaani mgandamizo wa mawazo

o   Kutulidha dhidi ya Kansa

o   Kuimarisha misuli ya mwili na kuimarisha viungo vya uzazi

o   Kuuzuia mwili kuchoka haraka uzee 

 

c.       Mazoezi yanasaidia kuongeza nguvu na usambaaji mzuri wa hewa ya oxygen kwenye viungo vya mwili kuweka muonekano mzuri na kuumudu mwili wako vema

d.      Mazoezi yanasaidia kukupa usingizi mzuri

e.      Mazoezi yanasaidia na kuimarisha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa ubora.

Kwa msingi huo watu wa Mungu, tusipouuzie mazoezi, na kufikiri kuwa wale wanaofanya mazoezi wako wmilini sana na wasiofanya ndio wako kiroho, kumbuka tu kuwa mazoezi yanapaswa kuwa na kiasi, lakini vilevile nia ya kufanya mazoezi kwa mkristo isiwe kubadilisha muonekano wa maumbile yetu bali iwe ni kwaajili ya utukufu wa Mungu, pichani ni mazoezi yanayoitwa squatting ni zoezi zuri kwa wanaume na wanawake, linaweza kufanyika hata ndani, sio lazima uende kiwanjani, linaimarisha miguu, linajenga shepu nzuri, linaimarisha via vya uzani, linakata tumbo, linajenga hips nzuri na kukutioa jasho pamoja na faida kadhaa nilizozianisha hapo juu, Mtangulize Mungu, Muombe Roho Mtakatifu, mwambie hili ni hekalu lako nataka kulitunza na sasa ninapochukua mazoezi nisaidie kufanya haya kwa utukufu wako! Kisha fanya mazoezi.

·         Na Rev. Innocent Kamote

·         Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima


·         0718990796




Imani ya Nikea!


Yuda 1:3-4 “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.”

Mji wa Nicaea wa kale unavyoonekana leo, katika Nchi ya Uturuki zamani ilikuwa ni sehemu ya Ugiriki


Utangulizi:

Nicaea au Nicea Ni moja ya mji wa kale zaidi katika nchi ya Ugiriki kaskazini-mashariki ya mji wa Anatolia, ambao kimsingi unajulikana kama eneo ambalo Mkutano mkuu wa kwanza na wa pili wa kanisa ulifanyika kwa mujibu wa Historia ya kanisa na ndio chimbuko la Msingi wa imani ya Kikristo ambayo inajulikana kama Imani ya Nikea!

Mnamo mwanzoni mwa Karne ya Nne moja ya fundisho muhimu sana liliinuka na kuleta Utata miongoni mwa Kanisa, mijadala iliinuka kupitia wanatheolojia  wakubwa na wenye nguvu, pia kukiwa na utetezi wenye nguvu na mawazo mbalimbali yaliyopelekea kuitishwa kwa mkutano wa uliofanyiika katika mji huo wa Nicea ili kupata msimamo wa kweli wa kikanisa kuhusiana na imani yetu.

Yuda 1:3-4Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.

Neno la Mungu linatuagiza kwamba tunao wajibu wa kuilinda imani yetu, na vilevile neno la Mungu linatutaka kujilinda na upotofu! Kama watu watakuwa wanaipotosha imani yetu nasi tukanyamaza kimya swala hilo linaweza kusababisha wakristo wakapotea na kujitenga na imani iliyo hai ona Waebrania 3;12 Biblia inasema “Ndugu zangu, angalieni, asiwepo miongoni mwenu mtu mwenye moyo mwovu usioamini, unaojitenga na Mungu aliye hai.

Nyakati za Kanisa la Kwanza mitume walikuwa na tabia ya kukutana pamoja kwa kusudi la kujadili mafundisho yasiyo sahihi katika imani yetu na kisha kutoa matamko ambayo yangeweza kurekebisha na kuweka wazi msimamo wa Imani yetu angalia kwa mfano Matendo ya Mitume 15:1-2 “Wakashuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka. Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee kwa habari ya swali hilo.”  

Unaona nyakati za mitume walikuweko walimu ambao walifundisha watu mafundisho yasiyo sahihi, fundisho lao ni kuwa “mtu asipotahiriwa hawezi kuokoka” fundishi hili lilikuwa haliko sawa na injili ya Yesu na ile iliyohubiriwa na Mitume kwamba Yesu anaokoa watu wa mataifa yote na wa desturi zote kwa imani bila masharti ya sheria ya Musa, ili kupata muafaka wa kipi kiwe fundisho sahihi la Injili Paulo na Barnabas walikwenda Yerusalem na kukusanyika na mitume na kupata tamko la pamoja  kama tunavyoweza kuliona katika

Matendo ya mitume 15:7-20 “Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba Mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini. Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi; wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani. Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua. Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao. Basi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paulo wakiwapasha habari za ishara na maajabu, ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika Mataifa. Na hao walipokwisha kunyamaza Yakobo akajibu, akisema, Ndugu zangu, nisikilizeni. Simeoni ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza alivyowaangalia Mataifa ili achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake. Na maneno ya manabii yapatana na hayo, kama ilivyoandikwa, Baada ya mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena nyumba ya Daudi iliyoanguka. Nitajenga tena maanguko yake, Nami nitaisimamisha; Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana, Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao;  Asema Bwana, ajulishaye hayo tangu milele. Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi; Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa; bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu.”

Hivi ndivyo namna na jinsi nyakati za kanisa la kwanza walifanya kwa kusudi la kuitetea imani, na kuilinda, kuitetea dhidi ya mafundisho yasiyo sahihi kutokana na walimu wa uongo na vilevile kutoa matamko yenye kuweka misingi ya kweli ya injili. Hata hivyo kama tumeiona kuwa nyakati za kanisa la kwanza waliwategemea Mitume kutoa muongozo wa kweli za kiungu, kwa kuwa wao walipewa neno, mtume wa mwisho kabisa kufa alikuwa Yohana mwandishi wa kitabu cha ufunuo ambaye alikuwa mwaka wa 100 Baada ya kristo.

Karne mbili baadaye mafundisho mengi ya uongo yalitokea au wakati mwingine mabishano ya kitheolojia kutoka miongoni mwa viongozi wa Kanisa, Kwa desturi kama ile ya mitume mababa wa kanisa walikusanyika NICEA kwa kusudi la kujadili na kupata kweli zinazoweza kuwaongoza vema bila kuchukuliwa na mafundisho yasiyo sahihi ya kibiblia. Mkutano huo uliitishwa kwa mamlaka ya Mfalme Contantine aliyetawala RUMI kati ya 306-337 BK.

Katika mkutano wao wa Kwanza  mjadala ulikuwa kuhusu Mafundisho ya Arius na Athanasius ambao walikuwa na mitazamo ifuatayo

 

a.       Arius wa Alexandria  256-336 BK

Alikuwa ni kiongozi mkubwa wa imani ya Kikristo na mwanzilishi wa imani ya Arianism moja ya imani potofu iliyokuwa inapinga uungu wa Yesu Kristo, Arius alikuwa mwana theolojia aliyesomea huko Antiokia (Antakya ya Leo huko Uturuki) alijifunza theolojia chini ya Msomi aliyejulikana sana aliyeitwa Lucian na huenda ndiko alikotoka na fundisho hilo alijulikana kwa kusisitiza maswala ya kihistoria na njia zanye kujenga na kuzalisha za kidini pamoja na maswala ya utafiti kuhusu umoja wa Mungu na Utatu Mtakatifu shule yake ilijulikana pia kama shule iliyokuwa ikimuona Kristo kama  yuko chini ya Mungu Baba,.

Arius alizaliwa Afrika na alikuwa mwangalizi wa Kanisa la Alexandria nchini Misri, alikataa kuweko kwa ushirika wa milele kati ya Yesu na Mungu usemi wake maarufu unasema “kuna wakati ambapo Yesu Hakuweko”na kuwa Mungu alimpitisha Yesu kuwa mwana wake baada ya ufufuo wake na kumpa baadhi ya majukumu ya uungu, alisema Yesu alikuwa na mwili wa kibinadamu lakini hakuwa na Nafsi ya Kibinadamu na hivyo hakuwa Mungu wala hakuwa mwanadamu wa kawaida Yuko mahali Fulani hapo katikati. Arianism wanaamini Yesu alimumbwa kwa tafasiri ya andiko hili Ufunuo 3:14c unaosema “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, MWANZO WA KUUMBA KWA MUNGU      

 

b.      Athanasius 293-373 B.K.

Mtakatifu Athanasius aliishi kati ya mwaka wa 293-373 B.K. Ni mwanatheolojia mkubwa wa Kikristo na Doctor wa Kanisa Pia alikuwa Askofu ni miongoni mwa watu walioshindana na kusababisha kuundwa kwa kanisa la Orthodox katika karne ya 4 akishindania imani dhidi ya Arianism alisimikwa kuwa shemasi akiwa kijana, akitumika kama Katibu wa askofu wa Alexandria na ndipo alipopata nafasi muhimu ya kitheolojia ya kuongoza mapambano dhidi ya fundisho la Arius ambalo lilijadiliwa katika mkutano wa Nicea mwaka wa 325 na kwa ujumla alikuwa na nguvu ya ziada ya kupambana na imani hiyo na aliweza kueleza sawia kuwa mwana wa Mungu Yesu Kristo ni sawa na Mungu Baba  ingawa Arius aliendelea kudai kuwa sio sawa kwani Yesu ni kiumbe tu aliye mkamilifu kuliko viumbe wengine na kuwa alitumiwa na Mungu katika uumbaji na kazi nyingine za uumbaji baada ya kuumbwa kwanza.

Mijadala hii ilipelekea kuzuka kwa mjadala mkubwa kuhusu Utatu wa Mungu mjadala huu ulikuwa umekita miguu yake katka kutaka kujua kuhusu Uungu wa Yesu kwamba je Yesu ni Mungu? Na kuna uhusiano gani kati ya Roho na Mwili wa Yesu Je Mungu ni Watatu au mmoja? Na wana uhusiano wa aina gani?

Arius alikuwa ameshindwa kutafasiri andiko la Ufunuo 3:14 na kuelewa vema neno MWANZO WA KUUMBA KWA MUNGU katika Biblia ya kiyunani linatumika neno “PROTOTOCOS” ambalo ni sawa na neno Protocol la kiingereza, Neno hilo Prototocos kwa kiyunani maana yake ni WAKWANZA KATIKA CHEO, kwa kiebrania maana yake Mzaliwa wa Kwanza, Uzaliwa wa kwanza katika kiyunani na kiebrania ulikuwa na maana ya cheo na hivyo kingeweza kuhama kwa yeyote Mungu aliyemchagua mfano Esau kwenda kwa Yakobo, au Manase kwenda kwa Efraimu, Hivyo linapotumika katika Biblia linamaanisha Yesu ndiye mwenye cheo cha juu zaidi kuliko chochote duniani au mbinguni  katika kiingereza maandiko hay ohayo yanasomeka hivi ona :-

Biblia ya Kiingereza ya King James Version inasomeka hivi;-

       Revelation 3:14c And unto the angel of the church of the Laodiceans write; These things saith the Amen, the faithful and true witness, THE BEGINNING OF THE CREATION OF GODKJV

 

Na biblia ya kiingereza the Amplified Bible inasomeka hivi;-

 

       Revelation 3:14 To the angel of the Church in Laodicea write: These are the words of the Amen, the faithful and true witness, “THE RULER OF GODS’ CREATION

 

Kwa kuwa Biblia ya Kiswahili SUV. Swahili union Versio imetafasiriwa moja kwa moja tioka KJV inasomeka MWANZO WA KUUMBA KWA MUNGU, tafasiri halisi ilipaswa kuwa Mtawala wa uumbaji wa Mungu unaona.

 

Chanzo cha tatizo:

Kwa nini imani Potofu zilitokea ziko sababu kadhaa za msingi;-

Mabadiliko makuu matatu katika kanisa.

 

-          Kanisa katika hatua za mwanzoni lilikuwa ni kanisa kama shirika lisilo na sheria au kanuni au makusudi ya kimaadili au kimuuundo

 

-          Hakukuweko na Muundo maalumu wa kimaongozo wala wa kitaratibu na baadaye lilikumbwa na mabadiliko hususani katika karne ya pili ambapo waamini walianza kufikiri kuhusu ushirika na kuweka viwango vya kimaadili na mafundisho, aidha agano jipya yaani maandiko ya agano jipya na mitume yalikuwa hayajafanyika neno kamili la Mungu yaani kukusanywa maktaba na kupata Agano jipya. Kwa hiyo kanisa lilikuwa na mabadiliko kwa sababu za msingi zifuatazo:-

a.       Kufa kwa Mitume wa Bwana.

Mwishoni mwa Karne ya kwanza Mitume wote wa Bwana walikuwa wamekwisha kufa wao walikuwa ni kama Mamlaka ya juu kabisa ya Kanisa na kila kulipotokea tatizo walikuwa wakitoa suluhisho je nani atakuwa mwenye mamlaka kama ile?

 

Je kanisa lingewezaje kutunza umoja wake wa imani bila kuweko kwa Mitume? Ilikuwa ni lazima na muhimu jibu lipatikane na zaidi sana Mchanganuo wa majibu ya Misingi ya Imani ilikuwa lazima Isitawishwe.

 

b.      Mateso dhidi ya Kanisa.

 

Wafalme wengi wa Kirumi makaisari walitaka kuabudiwa wao kama miungu, aidha wayahudi walianza kuwaona wakristo kama dhehebu lililo kinyume na sheria ya Musa na kuwa ni imani pinzani au tishio kwao Kanisa lingeweza kukabili vipi dharula hizo zilizojitokeza ndipo ilipoonekana haja ya kuwepo na Ushirika thabiti pamoja na sauti kamili ya kimafundisho au mafundisho sahii ambayo ungekuwa ndio msingi wa Imani ya wakristo wote.

 

c.       Kuweko kwa mafundisho ya uongo.

 

Mafundisho ya Mitume yalikuwa yanakubalika na kuheshimika kama Mamlaka ya mwisho hususani walipokuwa wakiwa hai, Lakini baada ya wao kufariki waalimu wa uongo wengi walitokea, je ni nani angesimama na kuzungumzia maswala ya imani na misingi ya mafundisho ya kweli ya kanisa? Hapa ndipo tunapoona umuhimu wa kuwa na Msimamo mmoja wa kiimani na sasa  Tatizo lilikuwa kubwa zaidi wakati jamii ya wakristo wa Mataifa walipoamini na kuingia kanisani kulizuka mawazo tofauti falsafa tofauti na migogoro iliinuka hapa na pale.

 

Namna ya kupata muafaka.

 

Waefeso 2:20 “Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.”

 

Katika kufikia muafaka Mkutano mkuu wa Nicea ambao pia ni maarufu kwa jina la Nicaeno-Contantinopolitan Creed mababa wa kanisa waliadhimia kwa pamoja kutengeneza ukiri wa imani ambayo ni mukhtasari wa mafundisho ya Msingi yaliyosadikiwa na Mitume na kufundishwa na mitume kwa kuzudi la kuzuia uzushi ukiwemo wa Arianism na aina nyingine za uzushi ambazo zilisumbua kanisa kwa karne nne, kwa msingi huo kanisa la Mashariki na Magharibi waliamua kwa pamoja kuwa na ukiri, ambao huo ndio utakuwa msingi wa kanisa la kweli kokote duniani, na kwa msingi huo kanisa au dhehebu lolote linalofundisha kinyume na misingi hii ya imani ndio inaitwa imani potofu, ni kutokana na mkutano huo uliofanyika Nicea ndio tunapata msingi wa Imani uliokuwa unafundishwa na mitume, na kwa heshima ndio misingi hiyo ikaitwa Imani ya Nikea, imani hiyo ilikuwa na maneno yafuatayo;-

Twaamwamini Mungu mungu mmoja, Baba mwenyezi, Muumba wa mbingu na Nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.” 

Na Yesu Kristo mwana wake wa pekee Bwana wetu, Atokaye kwa Baba kabla ya ulimwengu kuwako, Mungu kutoka kwa Mungu, Nuru kutoka katika Nuru, Mungu kweli kutoka katika Mungu kweli mwana wa azali asiyeumbwa, Mwenye uungu mmoja na Baba, ambaye kwa yeye vitu vyote viliumbwa, kwaajili yatu na kwa wokovu wetu, aliyeshuka kutoka Mbinguni, aliyechukuliwa mimba, kwa uweza wa Roho Mtakatifu akazaliwa na  bikira Mariam, akawa mwanadamu, zamani za Pontious Pilato aliteswa, akasulubiwa akafa akazikwa, siku ya tatu akafufuka kama yanenavyo maandiko matakatifu akapaa mbinguni ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba, toka huko atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu watu walio hai na wafu na ufalme wake hauna mwisho,

Twamwamini Roho Mtakatifu Bwana mtoa uzima atokaye katika Baba na Mwana, anayeabudiwa na kutukuzwa Pamoja na Baba na mwana aliyenenwa kwa vinywa vya manabii,

 

Twamini Kanisa takatifu Catholic na apostolic, ushirika mtakatifu, twakiri ubatizo mmoja wa kuondolewa dhambi, Twatazamia kufufuliwa kwa wafu na uzima wa ulimwengu ujao Amen.”

 

 

Huo ndio Ukiri wa Imani yetu, kila kanisa na kila dhehebu, maswala yote wanayohubiri na mafundisho yote yanayofundishwa hutokana na msingi wa imani hii waliyokuwa wakiiamini Mitume na kuifundisha, kanisa lolote dhehebu lolote au fundisho lolote lililo kinyume na misingi hii linakuwa limetoka nje ya njia, kwa hiyo ukifuatilia kwa makini utaona hiki Mafundisho yote ya kweli yanasimama katika fundisho hili, Mtu akisema Yesu sio Mungu, au akisema hakuna Roho Mtakatifu, au akisema wafu hawafufuliwi, au akisema Yesu hajasulubiwa msalabani basi hayo ni mafundisho potofu, Hivyo imani ya nikea ni mukhtasari wa misingi ya imani yetu ya kweli, Kanisa linapewa wito wa kujsomea maandiko na kujifunza kweli tunapoikumbuka imani ya NIcea ambayo ndio ilikuwa misingi ya kweli ya mafundisho ya Mitume.

Uongezewe neema!

Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima

Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka.

1Timotheo 5:17-18Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.”



Utangulizi:

Usimfunge ng’ombe kinywa apurapo nafaka! Ni moja ya agizo tata la kibiblia ambalo neno la Mungu limeamuru kanisa kulifanyia kazi ili Baraka za Mungu ziweze kumiminika kwetu hususani katika nyakati hizo za agano jipya!. Tuusome tena mstari huu kwa makini na kisha tuanze kuuchambua na kuufanyika kazi ili tuweze kupata uelewa unaokusudiwa!

 1Timotheo 5:17-18Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.”

Katika mukhtadha wa mstari huu kwanza tunaona Paulo mtume akitoa maagizo ya namna mbalimbali, katika kuwahudumia wajane walio wajane kweli kweli, kisha anazungumzia Kustahili heshima maradufu kwa wazee wanaotawala vema yaani wale watu wanaojitaabisha katika kuhubiri na kufundisha neno la Mungu. Ni muhimu kuchambua maswala kadhaa ya kuyatilia maanani kabla ya kuingia katika kiini cha somo letu! Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-

·         Wazee watawalao vema

·         Wahesabiwe kustahili heshima maradufu

·         Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka.


Wazee watawalao vema.

Wazee watawalao vema ni akina nani!

Neno wazee linalotumika hapo katika maandiko ya kiyunani linasomeka kama “PROESTOTES” Kwa kiingereza Presbyter ambalo maana yeke ni yeye mwenye kuongoza serikali ya kikanisa ecclesiastical Government au kwa lugha rahisi mwangalizi wa Kanisa, Mchungaji  wa kanisa au askofu  watu wenye sifa kama zile zilizoainishwa katika 


1Timotheo 3:1-7 “Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?) Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.” 

Kwa hiyo maandiko yanawazungumzia watu wenye huduma ya kichungaji, wanaotoa huduma za kiroho kwa kuwahudumia watu kwa neno la Mungu kwa kuhutubu yaani kuhubiri na kufundisha maandiko yanataka watu hawa waheshimiwe sana, yaani wanastahili heshima maradufu! Kwa msingi huo Biblia inatoa heshima kubwa sana na kuamuru kuheshimika kwa watu wanaofanya kazi ya kuhubiri na kufundisha, kwa bahati mbaya sana watu wengi na makanisa mengi na hata taasisi, wameifanya kazi hii au kuidhania kazi hii kuwa ni kazi duni naya kiwango cha chini nani ya kujitolea kiasi ambacho watu wanaohudumu hawapewi chochote na huishia kudharauliwa kama watu wasiotaabika kwa kazi hiyo ngumu! Biblia inaonyesha kuwa kazi hii sio nyepesi na kuwa wahubiri kama zilivyo kazi nyingine wanajitaabisha kwaajili ya maisha ya watu kiroho na kimwili pia. Kwa msingi huo maandiko ni kama yanaagiza kuwa watu hawa walipwe, angalia maneno yale mtenda kazi anastahili ujira wake! 1Timotheo 5:18 “Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.”

Wahesabiwe kustahili heshima maradufu.

Kwa msingi huo maandiko yanaamuru kuwa watu wafanyao kazi hii ya kichungaji wanastahili kulipwa, neon heshima maradufu maana yake wasihesabiwe kama watu wanaojitolea tu, watu watoe sadaka na sadaka itumike kuwalipa maandiko hayaichukulii kazi ya kuchunga kuhubiri na kufundisha kama kazi ya chini duni na ya kipuuzi hapana hii ni kazi iliyoko chini ya utawala na serikali ya Mungu hivyo watu hawa wasiachwe wakaishi maisha duni nay a mateso na kudhalilika kama kanisa litajua umuhimu wa kuwatia nguvu wahubiri na wachungaji na kutoa kile wanachobarikiwa na kuwasaidia watumishi hao wa Mungu wanatkuwa na uwezo mkubwa sana wa kuacha kujitafutia vipato vyao na familia zao na badala yake watajitoa zaidi na kutoa kipaumbele katika kulihudumia neno ona

Matendo 6:1-7 “Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung'uniko ya Wayahudi wa Kiyunani juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya kila siku. Wale Thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani. Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili; na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno. Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia; ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao. Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.”

Petro alikuwa anaonyesha wazi kuwa kulihudumia neno la Mungu sio kazi ya kukurupuka tu, inahitaji kujitoa kwenye kiwabngo kikubwa sana kunakoitwa kulihudumia neno, yaani hii hujumuisha kuomba na kufanya maandalizi ya neno la Mungu kwaajili ya watu wake na kufanya huduma za kichungaji, kazi hii hata ukiacha kuwa maandiko yamesema watu hawa walipwe lakini pia Mungu amekusudia kuwapa taji ya utukufu huko mbinguni baada ya kuja kwake Bwana  ona

1Petro 5:1-4 “Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye; lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi. Na Mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka.”

Utaratibu wa kuhakikisha kuwa watumishi wa Mungu wanapata posho yao kutokana na kuhudumu madhabahuni haukuanza tu katika nyakati za agano jipya lakini umeendelezwa kutoka katika agano la kale, tangu mwanzo Mungu akliandaa mazingira yaliyokuwa wazi kwa manabii wa kale zaidi na hata kwa jamii ya makuhani walawi kuwa waishi kutokana na madhabahu, huduma ya kichungaji haiitaji mtu adhurule inahitaji mtu awe na muda wa kuutafuta uso wa Mungu na kuyajua mapenzi yake ili awajulishe watu wake na kuwaonyesha njia pia kuomba kwaajili ya wenye mahitaji mbalimbali, hivyo tangu enzi za agano la kale walielewa kuwa huwezi kumwendea mtumishi wa Mungu mikono mitupu!, sio hivyo tu lakini hata watu waendao kwa waganga wa kienyeji pia huwa hawaendi mikono mitupu 

1Samuel 9:5-8 “Hata walipofika nchi ya Sufu, Sauli akamwambia yule mtumishi aliyefuatana naye, Haya, na turudi, baba yangu asije akaacha kufikiri habari za punda akatufikiri sisi. Naye akamwambia, Tazama, katika mji huu mna mtu wa Mungu, naye ni mtu mwenye kuheshimiwa; yote asemayo hutukia kweli kweli; basi, twende huko; labda yeye aweza kutuambia habari ya safari yetu tunayoiendea. Ndipo Sauli akamwambia mtumishi wake, Lakini angalia, kama tukienda, tumpelekee mtu huyo kitu gani? Maana chakula kimekwisha vyomboni mwetu, wala hapana zawadi ya kumpelekea mtu wa Mungu; tuna nini sisi? Yule mtumishi akamjibu Sauli, akasema, Tazama, mkononi mwangu nina robo ya shekeli ya fedha; nitampa huyo mtu wa Mungu fedha hiyo, atuambie njia yetu.Unaona katika hali ya kawaida Sauli aliweza kufikiri na kuelewa kuwa ni mapenzi ya Mungu kumuendea Mtu wa Mungu Nabii au Mchungaji kwa wakati huo ukiwa na zawadi, kwa sababu yeye anashughulika kuyatafuta mapenzi ya Mungu kwaajili yatu/yenu/yao Mungu analitambua hilo vema.

Watumishi wa Mungu pia ni watu waliko mstari wa mbele katika vita ya kupamba na shetani na kuipeleka injili kwa msingi huo wao huitwa askari ona 2Timotheo 2:3 “Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu kuwaacha watumishi wa Mungu bila msaada wetu ni sawa na kumuachia askari aende vitani kwa gharama zake mwenyewe jambo hili limekemewa vikali katika maandiko angalia mafundishi ya Paulo mtume kuhusu kazi hii ona

1Wakoritho 9: 7-14Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi? Je! Ninanena hayo kwa kibinadamu? Au torati nayo haisemi yayo hayo?  Kwa maana katika torati ya Musa imeandikwa, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Je! Hapo Mungu aangalia mambo ya ng'ombe?  Au yamkini anena hayo kwa ajili yetu? Naam, yaliandikwa kwa ajili yetu; kwa kuwa alimaye nafaka ni haki yake kulima kwa matumaini, naye apuraye nafaka ni haki yake kutumaini kupata sehemu yake. Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini? Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo. Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.” 


Unaweza kuona ni amri ya Mungu na ni mapenzi yake kuwa wote wanaomtumikia kwa njia mbalimbali wapate riziki yao kwa njia ileile wanayotumika, Mungu anatarajia kuwa utakuwepo utaratibu maalumu wa kuwapatia watumishi wake fedha kwaajili ya kujikimu, Kuwatumia watu wa Mungu bila kuwafikiria mahitaji yao ni dhambi? Hii ndio heshima maradufu wanayoweza kupewa wale wanaojitaabisha katika kazi ya Mungu kwa ujumla wake ikiwa ni pamoja kuhutubu na kufundisha angalia, Kanisa lazima ufikie wakati tuache uchoyo, uko wakati eti mtu anaumia kuona kuwa mchungaji analipwa, wako watu hawaoni raha hata kuona wachungaji wakifanikiwa kwa hiyo kwa miaka mingi sana kazi hii imefikiriwa kuwa duni, na kuwa ni ya kujitoa tu, matokeo yake tumeidhoofisha kazi ya kichungaji na kupoteza Baraka za Mungu kwa muda mrefu!

Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka.

1Timotheo 5:17-18Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.” Tunarejea sasa katika mstari wetu wa msingi ambao ndio una kiini cha somo letu!

Kimsingi andiko hili Paulo mtume amelinukuu kutoka katika agano la Kale hususani Kumbukumbu la torati 25:4 Biblia mahali hapo inasema “Ng'ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa.” Ingawa andiko hili lilitumika kwa lugha ya mficho lakini linafafanuliwa wazi katika mtazamo wa agano jipya na Paulo amelieleza kwa kina zaidi kama tulivyoona Katika 1Wakoritho 9:7-14, Kwamba hakuna askari aendaye vitani kwa gharama zake mwenyewe! Mafundisho kuwa mtenda kazi anastahili ujira wake yaani mshahara wake ni swala ambalo liko wazi kuanzia na Bwana Yesu mwenyewe katika mafundishi yake kwani aliligusia mara kadhaa! Katika Mathayo 10:10 na Luka 10:7 ambazo zinasema Mathayo 10:9-10Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu;  wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; MAANA MTENDA KAZI ASTAHILI POSHO LAKE.” Luka 10:7 “Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, MTENDA KAZI AMESTAHILI KUPEWA UJIRA WAKE. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii” Unaona maandiko hayo yote yanasisitiza kuwa Mtenda kazi anastahili ujira wake, Hakuna askari anayekwenda vitani kwa gharama yake mwenyewe hivyo watumishi wote wa Mungu ni lazima walipwe, ni lazima wafikiriwe namna ya kuishi, wamisionary, wachungaji, walimu, wainjilisti, manabii na mitume ni lazima waheshimike katika kanisa na kuepwa riziki yao, Kanisa ambalo haliwajali watumishi wa Mungu au haliwalipi watumishi japo hata posho ya utumishi wao ni kanisa linalolidharau neno la Mungu.

Kwa hiyo kwa Msingi huu ni halali kimaandiko kwa watumishi wa Mungu kutunzwa, Kanisa linapaswa kuandaa utaratibu maalumu wa kuwalipa na kuwalisha watumishi wa Mungu ili wasiwaze mambo mengine walitumikie kundi la Mungu kwa ufasaha, kumekuwapo na maneno ya kejeli mengi kuhusu watu wa Mungu, mara ooo wanakula sadaka zetu mara ooo wanatajirika kwa fedha zetu na kadhalika jambo la namna hii sio jema kwa watu wa Mungu, Hatuna budi kuhakikisha kuwa watumishi wa Mungu wanatunzwa sawasawa na kipato na mzunguko wa ugumu wa maisha ili waweze kukabiliana na changamoto za kimaisha zinazowazunguka lakini wakati huohuo wakitoa huduma bila manung’uniko. Kama liko kanisa linawatumiwa watumishi wake bila utaratibu wa kuwapatia posho basi kanisa hilo limelaaniwa, Laana hii inakuja kwa sababu gani? Mungu ameitoa sadaka iliwe itumiwe na watumishi wake Hesabu 18:24Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote. Mungu aliwapa zaka walawi kwa vile walikuwa wakitumika nyumbani mwa Mungu ili wapate chakula, au ili kiwemo chakula katika nyumba ya Mungu, kuwadharau watumishi wa Mungu na kutokutoa zaka, dhabihu na matoleo ili wao walipwe stahiki zao ni kudhoofisha kazi ya Mungu na hapa ndipo laana inapojitokeza na baraka kufungwa Malaki 3:7-12Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani? Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.” Unaona laana hii inatamkwa katika mazingira ambayo wana wa Israel walikuwa hawajali tena kuwepo kwa chakula katika nyumba ya Mungu yaani haki na posho ya walawi na hivyo walipigwa na ukwasi, mtu yeyote anayetakamkuwadhalilisha watumishi wa Mungu kwa kuwanyima Posho yao kwa makusudi hata kama zitatumika kwa nia njema amelaaniwa!. Kwa msingi huo kwa watumishi wa Mungu wote wakiwemo wale wenye huduma za kitume, kinabii, kiinjilist, kichungaji na hata walimu wa neno la Mungu wanastahili heshima hii, yaani kutunzwa kupitia kile wanachokifanya katika madhabau Mpaka hapo neno la Mungu liko sawa.

Kuwanyima posho watumishi wa Mungu kunafananishwa na kuwafunga kinywa ng’ombe wanyama kazi ambao ni wao wanaotaabiika kulima lakini mkulima anawafunga midomo yao eti wasipure nafaka,  ni tendo la ukatili wa hali ya juu kuzuia posho, ujira wa watumishi wa Mungu usiwafikie ni kuwavunjia Heshima na ni kumvunjia Mungu heshima ni kumdharau Mungu,  Mungu anawaona watumishi wake kama chanzo cha Baraka kwa watu wake, Mungu huwabariki watu wake kupitia matamko ya watumishi wake kwa hiyo kitendo cha kuwanyima mapato watumishi wa Mungu kiko sawa kabisa na kukosa ubinadamu kunakoweza kufanywa na mtu ambaye anawatumia ng’ombe nkulima ardhi kubebea mazao na mavuno lakini anamchapa fimbo nyingi sana ng’ombe huyo akila mazao bila kukumbuka kuwa ni ng’ombe huyo huyo ndiye aliyesababisha wao wawe salama, kwa hiyo ukiacha ya kuwa Mungu anataka tuwe na utu kwa wanyama ni zaidi sana anataka tuwe na utu uliotukuka kwa watumishi wanaohudumu Madhabahuni, ikiwa Mungu aliwafundisha Israel kuacha ukatili dhidi ya watu wanyama wake na watumwa ni zaidi sana mtu wa haki hataacha watumishi wa Mungu wateseke bali atawalisha kwanza!

Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima !