1Timotheo 4:7-8 “Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe
ujizoeze kupata utauwa. Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa
kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa
sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.”
Utangulizi:
Ni muhimu kufahamu kuwa kufanya
mazoezi ni moja ya sehemu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu, Mazoezi yana
faida kubwa sana katika maisha haya, Mazoezi yana faida kubwa sana kwa afya
zetu, Nyakati za Kanisa la kwanza wakati wa utawala wa kirumi jamii ya watu wa
dunia ya wakati ule walifanya sana mazoezi, Michezo ya tamaduni za kiyunani
Olympics ilikuwa imeshika kasi sana kwa hivyo watu wengi walifanya mazoezi ya
aina mbalimbali, kwa sababu mbalimbali na walikuwa na afya njema, Nyakati za
leo wakristo wamepuuzia sana mazoezi, aidha kwa sababu wanafikiri kuwa Biblia
haizungumzii mazoezi, ama kwa sababu ya tafasiri mbaya ya Mstari wa msingi
niliounukuu hapo juu! Lakini kula utakavyokula, zingatia maelekezo ya aina
yoyote ile ya kiafya kama utaweka mazoezi pembeni hutaweza kuwa na afya njema,
magonjwa mengi sana yameikumba dunia na watu wengi sana hata wakristo wanaumwa
magonjwa ya iana mbalimbali, lakini mengine yanaweza kuepukika, kupunguzwa au
hata kujikinga kama kanisa litaelewa umuhimu wa mazoezi, miili yetu ni Hekalu
la Roho Mtakatifu, na kwa sababu hiyo Maandiko yanatuagiza kuitunza na namna
mojawapo ambayo tunaweza kulitunza hekalu la Roho wa Mungu ni pamoja na kufanya
mazoezi kama nitakavyofafanua kwa kina ona 1Wakoritho
6:19 “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la
Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu
wenyewe;”
Kujizoeza kupata
nguvu za mwili kwafaa kidogo!
Kama nilivyogusia awali katika
utangulizi, kwamba kumekuwa na tatizo kubwa sana la kiafya katika nyakati za
leo hata kwa wateule, nchini Marekani kwa mfano watu wamekuwa na tatizo kubwa
la uzito unaopitiliza, ulaji wa hovyo, usio wa kiasi na uliokosa nidhamu ikiwa
ni mojawapo ya sababu zinazopelekea watu kuwa mabonge na hatimaye baadaye
kumlaumu Mungu kana kwamba ndiye aliyewashikia kijiko wale Maandiko yanatuonya
dhidi ya ulafi na kututaka tuwe na kiasi wakati wa kula Mithali
23:2 “ Tena ujitie kisu kooni, Kama ukiwa mlafi ”
sio hivyo tu lakini ili tuweze kuwa na afya imara, na kuwa wakakamavu kama
askari wema wa Yesu Kristo hatuna budi kuwa na wakati wa kufanya mazoezi,
Mazoezi yana uwezo mkubwa sana wa kutuimarisha, na kutulinda na magonjwa, yako
magonjwa mengi sana ambayo yanaweza kuepukika endapo tutakuwa na tabia ya
kufanya mazoezi, magonjwa kama Kisukari, Kansa, Moyo, presha na hata kuondoa
mawazo kunaweza kuwa mbali nasi kama tutajali afya zetu na kujihusisha kufanya
mazoezi.
Kujizoeza
kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo!
Kuna shida fulani katika tafasiri ya maandiko ya mstari huu 1Timotheo
4:7-8 “Bali
hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa.
Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa
kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo
baadaye.” Watafasiri wengi wa maandiko wamefikiri kwamba labda
huenda Paulo mtume amekataza mazoezi, au ameyapuuza mazoezi HAPANA Maandiko
haya hayakatazi watu kufanya mazoezi, isipokuwa Paulo mtume anataka kuonyesha
kuwa kujitia nidhamu katika kuishi maisha matakatifu kunafaa zaidi kwa maisha
haya nay ale ya uzima wa milele! Ilivyo ni kuwa nyakati za Kanisa la kwanza
utamaduni wa Kigiriki (Wayunani) ulikuwa umeitawala sana Dunia na kuiathiri
hata wakati wa utawala wa kirumi, watu walishika lugha na tamaduni za kigiriki
ikiwa ni pamoja na tamaduni za michezo ya aina mbalimbali, zingatia kuwa
Michezo ya Olympics ilikuwa imeshika chati ya dunia ya wakati ule, hivyo watu
walishiriki michezo ya aina mbali mbali lugha kubwa ya wakati ule ilikuwa ni
michezo na hata mifano ya wahubiri wa wakati huo ilitoka kwa wanamichezo ona
mfano 1Wakoritho 9:24-27 “Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio,
hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili
mpate. Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao
hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji
isiyoharibika. Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana
ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; bali nautesa mwili wangu na
kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa
kukataliwa.” Unaona Paulo mtume anatumia mifano ya wanamichezo na
nidhamu kubwa waliyo nayo wanamichezo na kuifananisha na namna watu wa Mungu
wanavyopaswa kujitia nidhamu ili waweze kupata taji isiyioharibika, Kwa hiyo
ulikuwa ni ulimwengu uliotawalaiwa na michezo na lugha nyingi sana zilikuwa za
kimichezo ikiwepo mifano hii aliyoitioa Paulo Mtume.
Kwa msingi huo ni wazi kuwa wat
wa jamii ya wakati ule walikuwa
wamehamasika sana katika kujishughulisha na michezo au hata mazoezi na wengine
wakijitia nidhamu kwaajili ya mazoezi, Mazoezi yalipewa kipaumbele na umuhimu
sawa na kuwekwa katika kiwango kimoja na maswala kadhaa yafuatayo
1. Kujiwekea
akiba Mathayo 6:19-21 “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na
wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa
nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo,
ndipo utakapokuwapo na moyo wako.”
2. Kutulia
na kutafakari Luka 10:41-42 “Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na
kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na
Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.”
3. Kujinyima
au kujizuia 1Timotheo 5:6 “Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai.”
4. Kufanya
kazi Yohana 6:27 “Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula
kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo
ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.”
5. Kujipamba
kwa wanawake 1Petro 3:3-6 “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka
nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni
usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu,
iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake
watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. Kama vile Sara
alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala
hamkutishwa kwa hofu yo yote.”
6. Kufanya
Mazoezi 1Timotheo 4:7-8 “Bali hadithi za
kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa. Kwa maana
kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo
yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.”
Unapotafakari Mistari hiyo hapo
juu inayokazia mambo yaliyopewa kipaumbele nyakati za Biblia utaweza kuona kuwa
wahudumu wa agano jipya waliyatumia mambo yaliyokuwa yamewekewa mkazo na jamii
kama somo la kuwekea mkazo jambo lililo la muhimu zaidi kwaajili ya Mungu au
kwaajili ya uzima wa milele, Mfano kujiwekea akiba wote tu nafahamu umuhimu
wake lakini kujiandaa kwaajili ya maisha milele ni kwa muhimu zaidi kuliko
akiba ya kawaida ya dunia hii ambayo ni ya kitambi tu hivyo maandiko
hayajakataza kuweka akiba, kutulia miguuni pa Yesu na kumsikiliza au kutafakari
ni fungu jema zaidi, kuliko kujitaabisha kwaajili yake, Yesu hakumkataza Martha
kufanya kazi, lakini alifurahishwa na kusikilizwa zaidi, kuliko kutumikiwa,
kujinyima kuishi maisha ya UTAWA, kutokuoa au kuolewa ni kuzuri, nidhamu wakati
wa michezo kampi na kadhalika, kujinyima vyakula Fulani na kujizuai kwa aina
yoyote ni kwa muhimu kama mtu anataka lakini kujizuia nafsi ni kwa muhimu
zaidi, Kufanya kazi kwaajili ya kupata ridhiki au chakula ni kwa Muhimu na Yesu
hazuii hali hiyo lakini kufanyia kazi uzima wa milele ni kwa Munhimu zaidi,
kujipamba kwa kusuka nywele na vito vya thamani ni kwa muhimu lakini, kujipamba
kwa tabia njema na kujiheshimu ni kwa muhimu zaidi kuliko mapambo
yanayoharibika, kufanya mazoezi kwaajili ya afya ni kwa muhimu sana lakini
kujizoeza kuishi maisha matakatifu ni kwa muhimu zaidi., kwa msingi huo Lugha
ile ya kibiblia hakimumaanisha kuwa mazoezi hayafai, yanafaa kidogo, kidogo hii
na maana gani yataimarisha afya zetu, tutakuwa imara, kutakuwa na afya njema
lakini mazoezi haya hayazuii mtu kutwaliwa na bwana, wala hayaongezi muda wa
maisha yetu duniani, kwa hiyo Lugha inayotumika hapo ni sawa na ile tu kama
watu wanatoa kipaumbele kujiwekea akiba Hazina duniani basin a watoe kipaumbele
kikubwa kijiwekea akiba au hazina mbinguni, andiko linamaana ya wazi kwamba
lolote linalopewa kipaumbele zaidi kuliko mambo ya Mungu, iwe ni TV, iwe ni
mpira, Gemu, na vikachukua nafasi ya
Mungu kwa kukosa kiasi hilo haliwezi kuwa jambo jema hata kidogo, Maandiko
yanachokitaka hata kama kitu sio dhambi ni muhimu kisipewe kipaumbele kuliko maswala
ya ufalme wa Mungu ambayo ndio kwa mujibu wa maandiko ni Muhimu zaidi Mathayo 6:33 “Bali
utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”
Unaona ndio maana Paulo akasema yanafaa kidogo, kama michezo na mazoezi ynapewa
muda mwingi na mkubwa zaidi kuliko kujisomea neno, kuomba au kushuhudia,
kutembelea wagonjwa, kuhudhuria ibada, hilo ndio tatizo, kuna faida gani ya
kuwa na nguvu na uimara wa kimwili kama roho zetu ni legevu? Kwa hiyo kimsingi Paulo hajaondoa umuhimu wa
Mazoezi, wala mazoezi sio dhambi na yana umuhimu mkubwa sana yatatuweka sawa
kiakili, kisaikolojia, kutulinda na magonjwa na kutupa nafasi ya kumtumikia
Mungu tukiwa na afya njema lakini yasichukue nafasi kubwa ya kupuuzia mambo ya
Mungu, Hilo tu!
Umuhimu wa Mazoezi katika mwili wa mwanadamu:
Kuna faida kubwa nyingi sana za
kufanya mazoezi, tafasiri mbaya za kimaandiko, zimewanyima sana wakristo tabia
ya kufanya mazoezi kiasi ambacho sasa makanisani kuna magonjwa ambayo yangeweza
kudhibitiwa tu na tabia ya kufanya mazoezi, badala ya kufanyiwa maombezi,
wakati mwingine Mungu anaweza kutushangaa kwamba unamuombea mtu tatizo ambalo
labda amefanya tu uzembe na angeweza kulitunza hekalu la Mungu kwa mazoezi, wakati
mwingine mtu anaweza kunenepa sana kumbe sababu yake ni stresses tu, mtu akifanya mazoezi pia anaongeza uwezo wa
kujiamini, Neema na iongezewe kwako unapozingatia
umuhimu wa mazoezi:
a. Mazoezi
yanasaidia kudhibiti uzito usiokuwa wa kawaia
b. Mazoezi
yanasaidia kutukinga na magonjwa ya aina mbalimbali
Mfano:
o
Kupooza au kiharusi
o
Shinikizo la damu
o
Aina zote za kisukari
o
Kupunguza stresses yaani mgandamizo wa mawazo
o
Kutulidha dhidi ya Kansa
o
Kuimarisha misuli ya mwili na kuimarisha viungo
vya uzazi
o
Kuuzuia mwili kuchoka haraka uzee
c. Mazoezi
yanasaidia kuongeza nguvu na usambaaji mzuri wa hewa ya oxygen kwenye viungo
vya mwili kuweka muonekano mzuri na kuumudu mwili wako vema
d. Mazoezi
yanasaidia kukupa usingizi mzuri
e. Mazoezi
yanasaidia na kuimarisha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa ubora.
Kwa msingi huo watu wa Mungu,
tusipouuzie mazoezi, na kufikiri kuwa wale wanaofanya mazoezi wako wmilini sana
na wasiofanya ndio wako kiroho, kumbuka tu kuwa mazoezi yanapaswa kuwa na
kiasi, lakini vilevile nia ya kufanya mazoezi kwa mkristo isiwe kubadilisha
muonekano wa maumbile yetu bali iwe ni kwaajili ya utukufu wa Mungu, pichani ni
mazoezi yanayoitwa squatting ni zoezi zuri kwa wanaume na wanawake, linaweza
kufanyika hata ndani, sio lazima uende kiwanjani, linaimarisha miguu, linajenga
shepu nzuri, linaimarisha via vya uzani, linakata tumbo, linajenga hips nzuri
na kukutioa jasho pamoja na faida kadhaa nilizozianisha hapo juu, Mtangulize
Mungu, Muombe Roho Mtakatifu, mwambie hili ni hekalu lako nataka kulitunza na
sasa ninapochukua mazoezi nisaidie kufanya haya kwa utukufu wako! Kisha fanya
mazoezi.
·
Na Rev.
Innocent Kamote
·
Mkuu wa
wajenzi mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni