Mambo
ya walawi 24:2-4 “ Waagize wana wa Israeli kwamba wakuletee mafuta ya
zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya ile nuru, ili hiyo taa iwake daima. Hapo
nje ya pazia la ushahidi, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeza tangu
jioni hata asubuhi mbele za BWANA daima; ni amri ya milele katika vizazi
vyenu. Atazitengeza hizo taa katika kile
kinara kilicho safi mbele za BWANA daima.”
Kutoka
27:20-21 “Nawe
waamuru wana wa Israeli wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili
ya nuru, ili kufanya ile taa kuwaka daima. Ndani ya ile hema ya kukutania, nje
ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeza
tangu jioni hata asubuhi mbele ya BWANA; itakuwa ni amri ya milele katika
vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israeli.”
Utangulizi:
Moja ya fanicha muhimu sana ambazo
ziliwekwa katika Hema ya kukutania na baadaye katika hekalu lililokuwako
Yerusalem, ni pamoja na taa ya dhahabu yenye vinara saba,taa hii ilitengenezwa
wakati wa Torati kwa maelekezo ya Mungu mwenyewe kwa mtumishi wake Musa huko jangwani,
Taa hii ambayo ilipaswa kuwaka kwa kutumia mafuta ya zeituni ilipaswa kuwaka
daima, Waebrania wanaiita taa hii yenye vinara saba Menorah, Ni moja ya alama muhimu sana kwa watu wote wanaoamini
maandiko lakini ni ya muhimu zaidi kwa wayahudi na wakristo, Taa hii imekuwa ni
alama muhimu ya Kiyahudi na ndio nembo ya taifa la Israel kwa sasa.
Hema ya kukutania pamoja na hekalu
lililokuwako Yerusalem ilikuwa ni ishara ya mpango wa Mungu kukaa katikati ya
wanadamu na kushirikiana nao, Hema ile ya kukutania pamoja na Hekalu lilikuwa
limegawanyika katika maeneo makuu matatu:-
1. Ua wa nje
ambao ulikuwa umetengenezwa kwa Mapazia maalumu na kulikuwa na Madhababu ya
shaba kwa sadaka za kuteketezwa na Bakuli la shaba la kutawadhia, ua wa nje
ulikuwa ni maalumu kwa watu kufika na kufanya ibada na kutoa kafara za wanyama
kwa mujibu wa maelekezo ya Torati. Nuru iliyoangaza mahali hapa ilikuwa nuru ya
asili ya mwanga wa jua tu.
2. Mahali
patakatifu, kutoka uwa wa nje mtu angeingia ndani ambapo pamefunikwa na mapazia
maalumu, mahali hapa waliingia makuhani tu, hapa palikuwa na Meza ya mikate ya
wonyesho, Madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba na taa ya dhahabu yenye
vinara saba, ni makuhani tu walioruhusiwa kuingia hapa tena wakiwa wamejitakasa
kwa maelekezo maalumu, Nuru iliyotakiwa kuangaza mahali hapa ilikuwa ni ile taa
yenye vinara saba.
3. Patakatifu
pa patakatifu, hapa ni chumba cha ndani zaidi, ni eneo ambalo lilikuwa
limetengana na patakatifu, palitengwa na pazia maalumu, ndani yake kulikuwa na
lile sanduku la agano lililotengenezwa kwa dhahabu na Makerubi waliofunikia
kiti cha rehema kwa mbawa zao Nuru iliyoangaza mahali hapa ilikuwa ni nguzo ya
wingu la utukufu wa Mungu mwenyewe
Ile
taa
Kwa mujibu wa maelekezo ya Mungu
kupitia mtumishi wake Musa, waliagizwa watu watengeneze mafuta ya mzeituni na
kisha wayapeleke hekaluni kwaajili ya taa hii ya dhahabu yenye vinara saba na
kwamba wahakikishe kuwa taa hii inawaka daima, ingawa ni kuhani tu aliyepaswa
kuingia hemani, na kuhakikisha kuwa taa inawaka lakini kumbuka watu walishiriki
kwa kuchangia mafuta kwa msingi huo kila mtu alishiriki. Walawi 24:1-4 “Kisha BWANA akanena na Musa,
na kumwambia, Waagize wana wa Israeli kwamba wakuletee mafuta ya zeituni safi
ya kupondwa kwa ajili ya ile nuru, ili hiyo taa iwake daima. Hapo nje ya pazia
la ushahidi, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeza tangu jioni hata
asubuhi mbele za BWANA daima; ni amri ya milele katika vizazi vyenu. Atazitengeza hizo taa katika kile kinara
kilicho safi mbele za BWANA daima.”
Umuhimu mkubwa sana wa ile taa yenye
vinara saba ni kutoa huduma, yenye kusababisha makuhani waweze kufanya wajibu
wao wa kufanya mamombi kwaajili ya watu na kuwapatanisha na Mungu, kumbuka eneo
hili lilikuwa limefunikwa kwa mapazia mazito ya ngozi, na kwa sababu hiyo kwa
vyovyote vile mahali hapo palikuwa pana giza, kwa hiyo ingekuwa ni vigumu kwa
viongozi wa kiroho kuendelea kuutafuta usio wa Bwana kwaajili ya watu wake kama
taa hii muhimu yenye vinara sana haingelikuwepo, kwa hiyo taa hii ilikuwa
muhimu kwaajili ya kuwawezesha makuhani kufanya wajibu wao, na taa ingeweza
kuwaangazia waone madhabahu ua dhahabu ya kufukizia uvumba ba maombi, na pia
waweze kuiona meza ya mikate ya wonyesho na kuwawezesha hivyo makuhani kuwa na
ushirika na Mungu na kuwaiombea watu wa Mungu kwa niaba yao!
Maana
ya ile taa yenye vinara saba!
Ni muhimu kufahamu kuwa taa hii ya
dhahabu yenye vinara saba imekuwa ikileta utata sana miongoni mwa wana
theolojia kutokana na kuwa na mitazamo mbalimbali hasa inayosababishwa na uwepo
wa vinara sana, kwa hiyo imeleta changamoto kwa wayahudi na wakristo katika
kufikiri namna halisi ya kutafasiri taa hii, yako majibu na mitazamo mbalimbali
kuhusiana na taa hii
·
Wengine hufikiri kuwa taa hii inazungumzia
siku sita za uumbaji wa Mungu na siku ya saba ya mapumziko ya kisabato kwa taa
ile ya kati kati ya saba
·
Wengine hufikiri kuwa labda taa hii
inawakilisha wazo la Hekima na uahamu wote unaokusudiwa na Mungu kama
utakavyokuwa juu ya masihi Isaya 11:2-3 “Na
roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na
uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana;
na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa
kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa
masikio yake;”
·
Wengine hufikiria kuwa taa yenye vinara saba
kwa wayahudi inahusishwa na kusheherekea sikukuu ya Hanukkah ambayo maana yake
ni sikukuu ya Nuru kwa hivyo moja kwa moja wanachukua maana ya neno Menorah
jina la ile taa ambalo maana yake kuangaza kwa hiyo ni kama taa hii ina ujumbe
wa amka uangaze.
·
Wengine huzungumzia kuwa taa yenye vinara saba
huwakilisha uwepo wa kuhani mkuu Yesu Kristo ambaye ndie asili ya nguvu ya
kanisa hasa kutokana na maono ya kitabu cha ufunuo katika Ufunuo 1;12-13 “Nikageuka niione ile sauti
iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu; na
katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika
miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini”.
·
Na wengine kutokana na asili hii ya kitabu cha
ufunuo wannamuona Yesu ambaye ndie mmiliki wa kanisa katika nyakati zote hivyo
wanahusisha na Historia ya Kanisa tangu ufunuo mpaka kurudi tena kwa Yesu kwa
hiyo wao huzungumzia nyakati saba za kanisa ona yaani Makanisa yale saba katika kitabu cha ufunuo pia huwakilisha
nyakati saba za kihistoria katika kanisa tangu wakati wa kanisal la kwanza
siku ya pentekoste hata wakati wa kuja kwa Bwana, haya pia yanaweza kuwa
makanisa au madhehebu ambayo yana mapungufu mbalimbali na baraka mbalimbali
sambamba na hali ya yale makanisa saba, makanisa hayo pia yanawakilisha Roho za
kinabii Ufunuo 19;10.
o Apostolic
Church 33-100 Kanisa la wakati wa
Mitume kanisa lenye shughuli.
o Persecuted
Church 100-113 kanisa la Karne ya
kwanza lililoteseka
o Imperial
Church 313- 476 Kanisa la kpindi cha
lililopata ushindi na kanisa lililokosea
o Medieval
Church 476-1453 kanisa lililopoa kipindi cha giza kanisa lenye tatizo
o Reformed
Church 1453-1648 kanisa la kimapinduzi
kanisa lililotazama nyuma
o Morden
church 1648-1970 kanisa la leo kanisa la kiinjilisti
o
Morden charismatic church
1970 mpaka leo. Kanisa lenye mafanikio
§ Fanya ile taa iwake Daima!
Tumeona
kuwa kuna dhana tofauti tofauti kuhusiana na mafundisho yaliyoko katika taa
yenye vinara saba vyovyote vile watu wanavyofikiri Mungu Roho Mtakatifu
alinirudisha mimi kujiuliza kwanini Mungu akazie kuwa taa ile iwake fanya taa
iwake daima hii maana yake ni kuwa kama taa ile ingezimika makuhani
wasingeliweza kuona, wasingeliweza kufanya majukumu yao ya kila siku,
wasingeliweza kupatanisha watu na Mungu kwani sehemu ya huduma ya upatanisho
ingekuwa iko giza, Taanyenye vinara saba ninatufundishan kuhakikisha kuwa
uhusiano wetu na Mungu unadumu kila siku na kuwa tunakuwa karibu naye kila
siku, tyunapodumisha uhusiano wetu na Mungu tunapewa nafasi ya kuona na
kufikiri na kutambua mambo kama Mungu anavyoona, kuna matokeo makubwa sana kwa
kanisa kuhakikisha kuwa tunadumisha uhusiano na Mungu, kuhakikisha kuwa taa
inawaka daima ni sawa na kuhakikisha kuwa hatuvunji uhusiano wetu na Mungu, sio
makuhani tu watru wote wanapaswa kushiriki katika kuhakikisha kuwa wote kwa
pamoja na kanisa kwa pamoja na Israel kwa pamoja wanadumisha uhusiano wao na
Mungu, kukua kwetu kiroho na kuona Mungu akijishughuklisha na maisha yetu
kutakuwa dhahiri endapo imani yetu na upendo wetu utaendelea kuwa pamoja na
Yesu daima, Mungu hana mpango wa kutuacha yeye ameahidi kuwa atakuwa pamoja
nasi ni sisi ndio twenye wajibu wa kubaki ndani yake lakini yeye ameahidi kuwa
hatatuacha wala hatatutupa nje kamwe ona
Yoahana 6:37 “Wote
anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe”.
Isaya 41:10 “usiogope,
kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako;
nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa
haki yangu.”
Mika 7:8 “Usifurahi
juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, Bwana
atakuwa nuru kwangu.”
Torati 31:6-8 “Iweni
hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana, Mungu
wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha. Musa
akamwita Yoshua, akamwambia machoni pa Israeli wote, Uwe hodari na moyo wa
ushujaa, maana utakwenda pamoja na watu hawa hata nchi Bwana aliyowaapia baba
zao, ya kwamba atawapa; nawe utawarithisha. Naye Bwana, yeye ndiye
atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope
wala usifadhaike.”
Usalama
wetu uko ndani ya kudumisha mahusiano yetu na Mungu, taa ile ilitakiwa kuwaka
daima ili makuhani waendelee kutoa huduma za kiungu kwa watu, tunapodumisha
uhusiano wetu na Mungu ndipo tunapokuwa salama na ndipo tunapoweza kusema kwa
ujasirimkuwa Bwana ni Nuru yangu na wokovu wangu nimuogope nani
Zaburi 27:1-3 “ Bwana ni nuru
yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu
nani? Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui
zangu, Walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu
hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini.”
Mtu wa
Mungu kama unataka kufanikiwa usiharibu wala usiruhusu uhusiano wako na Mungu
ukavunjika unao wajibu wa kuleta mafuta na kuhakikisha kuwa taa ile haizimiki,
fanya ile taa iwake daima Mungu alimuita Samuel na kusema naye wakati ambapo
taa ile haijazimika 1Samuel 3:1-3 “Basi, mtoto Samweli akamtumikia Bwana mbele ya Eli. Na
neno la Bwana lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri. Ikawa
wakati huo, Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa
yameanza kupofuka, hata asiweze kuona), na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika
bado, na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la Bwana, palipokuwa na sanduku
la Mungu; ” uhusiano wetu na
Mungu, kujibiwa maombi, kuisikia sauti ya mungu, kukuia kwetu kiroho, kupata
ufunuo mpya, maelekezo maono, nuru, kujua siri za Mungu, kuwa na karama na
vipawa, ujuzi na taarifa za kiungu kutakuwa hai katika maisha yetu kama taa ya
Mungu haijazimika ile taa tukiiacha ikazima tumekwisha ! twende kwa nani Bwana
wewe unayo maneno ya uzima wa milele!
Na Rev.
Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa
wajenzi mwenye hekima !
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni