Jumatatu, 27 Septemba 2021

Hekima yao ikapate kuwa ubatili na maarifa yao yawe ujinga!



2Samuel 15:30-31 “Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akilia alipokuwa akipanda; naye alikuwa amejifunika kichwa chake, akaenda hana viatu; na watu wote waliokuwa pamoja naye wakajifunika vichwa vyao, kila mmoja wao, wakapanda juu, wakilia walipopanda. Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee Bwana, nakusihi, uligeuze shauri la Ahithofeli liwe ubatili


Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa unapokuwa kiongozi wa ngazi yoyote ile, iwe kisiasa au kiimani, huwezi kupendwa na kila mtu, sio viongozi tu lakini hata katika maisha haya ya kawaida, wanakuwepo watu wanaotukubali sana na vilevile wako watu ambao hawawezi kutukubali, hili ni jambo la kawaida sana, hatuwezi kuwapendeza watu wote, sisi sio wema sana kama Masihi Yesu Kristo yeye alikuwa mwema mno kuliko mtu awaye yote lakini watu walimchukia na kufikia ngazi ya kumsulubisha Luka 15:18-20 “Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu.” Unaona Yesu hapa alikuwa anawafundisha viongozi, yaani hawa ni wale wanafunzi 12 wa Yesu ambao walikuwa kimsingi wanaandaliwa kuwa viongozi wa kanisa, si unakumbuka Yesu alikuwa na wanafunzi wengi? Ila wachache waliandaliwa kuwa viongozi, sasa kaka kiongozi kama Yesu aliongoza vizuri na wakamfanyia mabaya wakamuasi ni wazi kuwa sisi tutafanyiwa mabaya makubwa zaidi Luka 23:31 “Kwa kuwa kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?kulijua jambo hili mapema ni muhimu kwa sababu biblia inatufundisha vilevile namna ya kukabiliana na changamoto za aina hii na namna tunavyoweza kumuomba Mungu yanapotokea maswala magumu katika maisha yetu!, Leo tunachukua muda tena kujifunza kwa undani kuhusiana na jinsi Mungu alivyomtetea mtumishi wake Daudi alipokuwa kiongozi na alipokuwa akitimiza majukumu yake kwa Mungu! Namna na jinsi alivyomuomba Mungu kwa hekima na Mungu akamsikia.

 

2Samuel 15:30-31 “Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akilia alipokuwa akipanda; naye alikuwa amejifunika kichwa chake, akaenda hana viatu; na watu wote waliokuwa pamoja naye wakajifunika vichwa vyao, kila mmoja wao, wakapanda juu, wakilia walipopanda. Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee Bwana, nakusihi, uligeuze shauri la Ahithofeli liwe ubatili

Katika mstari wetu wa msingi leo, tunajifunza mojawapo ya tukio gumu sana lililopata kumtokea Mfalme Daudi akiwa madarakani, Daudi alipata jaribu la kupinduliwa madarakani na kijana wake wa kumzaa aliyeitwa Absalom, hata hivyo uasi wake haukuwa na nguvu sana mpaka pale mtu mmoja muhimu mno katika utawala wa Daudi aliyeitwa Ahithofeli, alipoungana na upande wa uasi, Mtu huyu alikuwa ndiye mshauri mkuu wa Mfalme Daudi na alikuwa na sifa kubwa muhimu mno Maandiko yanasema uwezo wake wa kushauri ulikuwa sawasawa na Mtu anapouliza kwa Mungu ona.

2Samuel 16:23 “Na shauri lake Ahithofeli, alilokuwa akilitoa siku zile, lilikuwa kama mtu aulizapo kwa neno la Mungu; ndivyo yalivyokuwa mashauri yote ya Ahithofeli, kwa Daudi, na kwa Absalomu.”  

Unaweza kuona kwamba mtu huyu alikuwa na nafasi muhimu sana kwa mfalme na nafasi yake kama mshauri wa mfalme ilikuwa nafasi muhimu sana, Licha ya kuna na nafasi hii inasemekana pia Ahithopheli alikuwa na kijana wake ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa maakida yaani makomandoo  au mashujaa wanaotajwa kuwa waliokuwa mstari wa mbele katika majeshi ya Daudi Mfalme ona

2Samuel 23:34 “na Elifeleti, mwana wa Ahasbai, na Heferi, Mmaakathi, na Eliamu, mwana wa Ahithofeli, Mgiloni;

Unaona huyo Eliamu alikuwa ni kijana wa Ahithofeli kwa msingi hio kwa vyovyote vile lazima ieleweke wazi kuwa Ahithofeli alikuwa mtu muhimu na hakuwa mtu wa kawaida na katika mashauri na hekima alikuwa mtu muhimu kwa mfalme kwa miaka Mingi.

Hekima ya Ahithofeli

Wengi tunajiuliza ni nini kilimpata Ahithofeli kwanini alimchagua Absalom aliyeasi badala ya Daudi? Kwanini mtu huyu aliyekuwa na ujuzi wa kushauri na hekima ambayo inatajwa kuwa alikuwa akishauri, ushauri wake ulikuwa sawa na mtu kutafuta ushauri kwa Mungu? Nini kilimpa sifa kuwa anavyoshauri ni kama mtu akiuliza kutoka kwa Mungu? Watu wengi wanasema kuwa huenda ushauri wake kumwambia Absalom azini na wake za baba yake ulikuwa ushauri mbaya na usio wa kiungu, Binafsi ninakataa ushauri wake Ahithofeli ni kweli kabisa ulikuwa kama ushauri utokao kwa Mungu, Mapema sana Daudi alipofanya dhambi na kumtwaa mke wa Uria na kisha kufanya njama za kumuua Uria, Nabii Nathan alitumwa na Mungu kuja kumuonya Daudi dhidi ya dhambi zake na adhabu ambazo angepewa ona

2Samuel 12:1-13Ndipo Bwana akamtuma Nathani aende kwa Daudi. Naye akamwendea, akamwambia, Palikuwa na watu wawili katika mji mmoja; mmoja wao alikuwa tajiri, wa pili maskini. Yule tajiri alikuwa na kondoo na ng'ombe wengi sana; bali yule maskini hakuwa na kitu, ila mwana kondoo mmoja, mdogo, ambaye amemnunua na kumlea; naye akakua pamoja naye, na pamoja na wanawe; hula sehemu ya posho lake, na kukinywea kikombe chake, na kulala kifuani mwake, akawa kwake kama binti. Hata msafiri mmoja akamfikilia yule tajiri, naye akaacha kutwaa mmoja wa kondoo zake mwenyewe au mmoja wa ng'ombe zake mwenyewe, ili kumwandalia yule msafiri aliyemfikilia, bali alimnyang'anya yule maskini mwana-kondoo wake, akamwandalia yule mtu aliyemfikilia. Ndipo hasira ya Daudi ikawaka sana juu ya mtu yule; akamwambia Nathani, Aishivyo Bwana, mtu huyo aliyetenda jambo hili, hakika yake astahili kufa; naye atamrudishia yule mwana-kondoo mara nne, kwa sababu ametenda neno hili, na kwa sababu hakuwa na huruma. Basi Nathani akamwambia Daudi, Wewe ndiwe mtu huyo. Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nalikutia mafuta, uwe mfalme juu ya Israeli, nikakuokoa na mkono wa Sauli; nami nikakupa nyumba ya bwana wako, na wake za bwana wako kifuani mwako; nikakupa nyumba ya Israeli na ya Yuda; na kama hayo yangalikuwa machache, ningalikuongezea mambo kadha wa kadha. Kwa nini umelidharau neno la Bwana, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa wana wa Amoni. Basi, sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau, ukamtwaa mkewe Uria, Mhiti, kuwa mke wako. Bwana asema hivi, Angalia, nitakuondokeshea uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako mbele ya jua hili. Maana wewe ulifanya jambo lile kwa siri; bali mimi nitalifanya jambo hili mbele ya Israeli wote na mbele ya jua. Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia Bwana dhambi. Nathani akamwambia Daudi, Bwana naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa.”

Uko uwezekano ulio wazi kabisa kwamba maelekezo haya yaliyotolewa na Nabii Nathani ambayo yalikuwa yanatoka kwa Mungu wakati yanatolewa Ahithofeli hakuwepo kabisa na mwandishi wa Kitabu anamuona Ahithofeli kama mshauri ambaye ushauri wake anapoutoa ni kama mtu anayeuliza kutoka kwa Mungu, kwanini kwa sababu ukiiangalia adhabu hii ambayo Mungu alikuwa ameitangaza Nathan Nabii kwa Daudi na ushauri aliokuwa anautoa Ahithofeli ilikuwa ni kama mtu anayetaka kulitimiza neno lililotoka kinywani mwa Bwana kupitia nabii wake

2Samuel 16:20-23 “Kisha Absalomu akamwambia Ahithofeli, Haya, toa shauri lako, tufanyeje. Naye Ahithofeli akamwambia Absalomu, Ingia wewe kwa masuria ya baba yako, hao aliowaacha ili kutunza nyumba; na Israeli wote watasikia ya kuwa umechukizwa kabisa na baba yako; ndipo itatiwa nguvu mikono yao wote walio pamoja nawe. Basi wakamtandikia Absalomu hema juu ya nyumba darini; naye Absalomu akaingia kwa masuria ya babaye machoni pa Israeli wote. Na shauri lake Ahithofeli, alilokuwa akilitoa siku zile, lilikuwa kama mtu aulizapo kwa neno la Mungu; ndivyo yalivyokuwa mashauri yote ya Ahithofeli, kwa Daudi, na kwa Absalomu.”

Unaweza kuona namna na jinsi Ahithofeli alivyokuwa na Hekima ya ajabu, na uwezo mkubwa wa kushauri sawa na mapenzi ya Mungu, Ahithofeli alikuwa na hekima na busara kubwa na alijua namna ya kuishawishi jamii, kitendo cha kumshauri Absalom alale na masuria wa baba yake hadharani kiliifanya kambi ya Absalom kupata nguvu kwani kiliwaaminisha kuwa ni ukweli ulio wazi kuwa kijana amemchukia baba yake waziwazi hivyo waliweza kuiteka mioyo ya watu, kiuadilifu ushuri huu haukuwa mwema lakini kinabii Ahithofeli alisaidia kutimia kwa unabii wa Nathan na ahadi ya Mungu ya kumuadhibu Daudi, na ndio maana mapema sana Absalom alipoasi alimuhitaji mtu huyu aliyekuwa Mshauri hodari, mwenye hekima na sio tu kuwa alikuwa mwenye hekima lakini vilevile alikuwa shujaa yaani alikuwa na ujuzi wa kivita kwa hivyo uasi wa Absalom ulipata nguvu kubwa sana alipompata Aithofeli, vita hiii ilikuwa moja ya vita ngumu sana kwa Daudi na uwezekano wa kushinda ulikuwa ni mdogo kama sio rehema za Mungu ona 

2Samuel 15:10-13. “Lakini Absalomu akapeleka wapelelezi katika kabila zote za Israeli kusema, Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta, ndipo mtakaposema Absalomu anamiliki huko Hebroni. Na watu mia mbili walioalikwa wakatoka Yerusalemu pamoja na Absalomu, wakaenda katika ujinga wao wasijue neno lo lote. Absalomu naye akatuma kumwita Ahithofeli Mgiloni, mshauri wake Daudi, kutoka katika mji wake, yaani, Gilo, alipokuwa akitoa dhabihu. Fitina yao ikawa na nguvu; maana watu waliokuwa pamoja na Absalomu wakazidi kuwa wengi. Mjumbe akamfikilia Daudi, akasema, Mioyo ya watu wa Israeli inashikamana na Absalomu.”

Kwa namna na jinsi Daudi alivyofahamu uwezo wa Ahithofeli alijua wazi kabisa kuwa vita imekwisha kuwa kali sana na kutoboa kwake kuko katika mazingira magumu mno, Daudi alitoroka ikulu akiwa miguu peku na akajitanda nguo kichwani akiwa analia kwani alihitaji rehema za Mungu tu, kumuokoa katika vita ile kali

2Samuel 15:30 “Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akilia alipokuwa akipanda; naye alikuwa amejifunika kichwa chake, akaenda hana viatu; na watu wote waliokuwa pamoja naye wakajifunika vichwa vyao, kila mmoja wao, wakapanda juu, wakilia walipopanda.”

Swali kubwa la kujiuliza ni kwanini Ahithofeli aliyekuwa na hekima namna hii, Hekima yake haikumuongoza kuungana na Daudi? Kulikuwa na dhida katika maisha ya Ahithofeli, Hekima yake ilimezwa na uchungu na moyo wake wa kutokusamehe na kuachilia! Na roho mbaya      

Hekima imemezwa kwa uchungu!

Ahithofeli Pamoja na kuwa alikuwa mtu muhimu na kuwa yeye na mwanaye wote kwa Pamoja walimtumikia Daudi katika kulitimiza shauri la Mungu, Na kuwa mtu mwenye hekima ya kupita kawaida tunaposoma maandiko mwanaye anatajwa kuwa ni Eliam

2Samuel 23:34 “na Elifeleti, mwana wa Ahasbai, na Heferi, Mmaakathi, na Eliamu, mwana wa Ahithofeli, Mgiloni;”

unapofanya uchunguzi wa kimaandiko inaonekana kuwa binti wa Eliam kijana wa Aithofeli ndiye Bathsheba ona vizuri katika maandiko haya

2Samuel 11:2-3Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?

kwa maana hiyo sasa Ahithofeli alikuwa ni babu wa Bath-sheba, binti wa kijana wake Eliamu, kwa msingi huo basi Ahithofeli alitunza uchungu moyoni kwa kitendo alichofanyiwa mjukuu wake aliutunza uchungu huo kwa miaka mingi, hivyo alikuwa akimtumikia mfalme kwa unafiki, hivyo ndivyo uchungu ulivyoharibu maisha ya mtu mwenye hekima ya ajabu, uchungu uliweza kuharibu sio hekima yake tu hata maisha yake baadaye, uchungu huu ulifunuliwa sio tu kwa kuungana na Absalom lakini inaonekana katika ushauri wake alikuwa na nia ya dhati ya kumshambulia Daudi, sio tu akitumia Hekima yake lakini alikuwa tayari hata kumshambulia kwa mikono yake  na kumuua ona  shina la uchungu linapunguza neema ya Mungu kwetu na kutufanya tufanye mambo ya hovyo,

Waebrania 12: 14-15 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.”

Kutokana na kutunza uchungu kwa Muda mrefu Aithofeli sasa anapanga kumuua Daudi kwa mikono yake mwenyewe, anajiamini kuwa hakuna sababu ya kusumbua watu wala kumwaga damu ya watu wengi hapa ni kummaliza Daudi pekee na kazi imekwisha,

2Samuel17: 1-4 “Zaidi ya hayo Ahithofeli akamwambia Absalomu, Niache nichague watu kumi na mbili elfu, nami nitaondoka na kumfuatia Daudi usiku huu; nami nitamshambulia wakati atakaokuwa amechoka, na mikono yake imekuwa dhaifu, nami nitamtia hofu; na watu wote walio pamoja naye watakimbia; nami nitampiga mfalme peke yake; na hao watu wote nitawarejeza kwako; mtu yule umtafutaye ni kana kwamba wamerudi wote; na hivyo watu wote watakuwa katika amani. Shauri hili likawa jema machoni pa Absalomu, na machoni pa wazee wote wa Israeli.”

Unaweza kuona Ahithofeli alikuwa anajiamini sana hii ni wazi kuwa mtu huyu licha ya kuwa Mshauri na mtu mwenye hekima vilevile alikuwa anajua kupigana, kama kijana wake Eliamu alikuwa moja ya mashujaa wakubwa katika makomandoo wa Daudi ni wazi kuwa Ahithofeli alikuwa na uwezo mkubwa na mbinu kali za kivita alihitaji watu 12 elfu tu na angemuua Daudi tu na kazi ingekuwa imekwisha, ni wazi kabisa kumbe uchungu unapotunzwa moyoni watu wanatunza mauti,

Mathayo 5:21-22 “Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.”  

Ni wazi kuwa uchungu na kisasi kinaweza kuharibu Hekima ile Mungu anayoikusudia kwetu maisha ya Aithofeli na maneno yake na mpango wake ulionyesha wazi kuwa ana uchungu mkubwa na Daudi na, Daudi ni kweli alikuwa amefanya dhambi na alikuwa kweli amejutia dhambi yake alitubu mbele ya Nathani Nabii na alikuwa ametamkiwa msamaha na kukubali adhabu zote ambazo Mungu alikuwa amezikusudia, hata hivyo kwa upande wa Pili Ahithofeli alikuwa hazijui njia za Mungu yeye aliendelea kuitegemea akili yake mwenyewe na kusahahu kuwa ziko njia za kiungu

Mithali 3:5-8 “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu. Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako.

Unaona Ahithofeli alikuwa ameacha kumtegemea Mungu wala hakumtumaini kwa lolote alizitegemea akili zake alikuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe, alichukulia poa kile kitendo cha kukubalika katika Israel na kusifiwa na wazee, hakumcha Mungu na kwa sababu hiyo hakujua kuwa uovu ulikuwa unammendea, uchungu ukamuharibu mtu mwenye hekima moyo wake ukajaa kulipiza kisasi na kutaka kuua mtu asiye na hatia kwa Mungu, Daudi alitambua njia za Mungu, alifahamu kuwa Mungu atamhurumia na kumpa rehema alimuomba Mungu na kumtegemea yeye, hata kabla ya kupanga vita na kupigana yeye alimuomba Mungu, Daudi alikuwa tayari hata kuwasamehe watu waliomtukana

2Samuel 16:5-12Basi mfalme Daudi alipofika Bahurimu, tazama, kulitoka huko mtu wa jamaa ya nyumba ya Sauli, jina lake akiitwa Shimei, mwana wa Gera; alitoka, akalaani alipokuwa akienda. Tena akamtupia Daudi mawe, na watumishi wote wa mfalme Daudi; na watu wote na mashujaa wote walikuwako mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto. Na Shimei alipolaani, alisema hivi, Nenda zako! Nenda zako! Ewe mtu wa damu! Ewe mtu usiyefaa! Bwana amerudisha juu yako damu yote ya nyumba ya Sauli ambaye umetawala badala yake; naye Bwana ametia ufalme katika mkono wa Absalomu mwanao; kisha, angalia, wewe umetwaliwa katika uovu wako mwenyewe, kwa sababu umekuwa mtu wa damu. Ndipo Abishai mwana wa Seruya, akamwambia mfalme, Mbona mbwa mfu huyu amlaani mfalme bwana wangu? Na nivuke, nakusihi, nikaondoe kichwa chake. Mfalme akasema, Nina nini na ninyi, enyi wana wa Seruya? Kwa sababu yeye analaani, na kwa sababu Bwana amemwambia, Mlaani Daudi, basi, ni nani atakayesema, Mbona umetenda haya? Daudi akamwambia Abishai, na watumishi wake wote, Angalieni, huyu mwanangu, aliyetoka viunoni mwangu, anautafuta uhai wangu; si zaidi Mbenyamini huyu sasa? Mwacheni alaani, kwa sababu Bwana ndiye aliyemwagiza. Labda Bwana atayaangalia mabaya yaliyonipata, naye Bwana atanilipa mema kwa sababu ya kunilaani kwake leo.” Daudi alizifahamu njia za Mungu, alisamehe hata waliomlaani, akijua wazi kuwa Mungu atazigeuza laana zao kuwa Baraka!, Daudi alimtegemea Mungu kwa asilimia 100 na hakuzitegemea akili zake tu, Daudi alimlilia Mungu!

Ee Bwana, nakusihi, uligeuze shauri la Ahithofeli liwe ubatili   

Daudi alitumia njia ya kiungu, Yeye mwenyewe alikuwa shujaa wa vita, lakini alikuwa na uzoefu kuwa hakuna vita ambayo alipigana peke yake, alijua kuwa siri kubwa ya ushindi wa vita yake ni Bwana, tangu ujana wake alipompiga Goliathi alimpiga kwa jina la Bwana wa majeshi ya Israel, na kila wakati alihitahi fadhili za Mungu ziweze kumpigania na alihitaji kujua kuwa bwana yuko upande gani, kumbuka Daudi alikimbia ikulu akiwa analia alipaza Sauti yake juu akilia kwa uchungu na kurusha mavumbi juu alikuwa akimlilia Mungu aweze kuingilia kati

2Samuel 15:30 “Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akilia alipokuwa akipanda; naye alikuwa amejifunika kichwa chake, akaenda hana viatu; na watu wote waliokuwa pamoja naye wakajifunika vichwa vyao, kila mmoja wao, wakapanda juu, wakilia walipopanda.”

 Akiwa katika hali hii ya kuomba Daudi alielezwa kuwa Mshauri wake muhimu sana wa kutegemewa alikuwa amejiunga na uasi wa Absalom, huyu ndiye Ahithofeli alikuwa sasa amemsaliti alikuwa ni mtu wa karibu sana kwa Daudi lakini amemgeuka,Huenda hii ndio sababu ya Daudi kuimba zaburi hii

Zaburi 41:9 “Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake.”

Pamoja na mambo mengine Daudi alimuomba Mungu dua muhimu sana iliyoleta ushindi katika maisha yake Daudi alisema maneno haya

2Samuel 15:30-31 “Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akilia alipokuwa akipanda; naye alikuwa amejifunika kichwa chake, akaenda hana viatu; na watu wote waliokuwa pamoja naye wakajifunika vichwa vyao, kila mmoja wao, wakapanda juu, wakilia walipopanda. Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, EE BWANA, NAKUSIHI, ULIGEUZE SHAURI LA AHITHOFELI LIWE UBATILI

Daudi aliyalaani maarifa na hekima ya Ahithofeli tangu wakati ule iwe ubatili, aliibatilisha hekima yake haithofeli ikapate kuwa ubatili, na Maarifa yake yawe ujinga, hii ilikuwa duwa Muhimu sana inayoweza kutupa ushuindi katika maisha yetu hata katika wakati huu tulio nao, tunapokuwa na vita zozote za kiroho, tunapokabiliwa na majanga mazito na maadui wanaotafuta kutuua au kutuangamiza au kutuumiza au kutujeruhi, maombi pekee tunayoweza kumuomba Mungu ni kuifanya hekima yao maadui zetu kuwa ubatili ma maarifa yaio kuwa ujinga Daudi alikuwa anajua kuwa Mungu wa Mbinguni ana uwezo wa kutangua mashaurui ya watu wabaya, anauwezo wa kuharibu mikono ya watu waovu isitimize makudui yao na kuzinasaa hekima zao kuwa hila na mashauri yao kuharibika kwa haraka

Ayubu 5:12-13 “Yeye huyatangua mashauri ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao. Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe; Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka.”

 Ni tabia ya Mungu kugeuza mashauri ya wanaojidhani kuwa wana hekima, au maarifa ni kazi yake kuwatia wazimu, kuwarudisha nyuma na kuyafanya maarifa yao kuwa ujinga

Isaya 44:24-25. “Bwana, mkombozi wako, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni Bwana, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami? Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga;”

Watu wasiotembea katika njia za Mungu wamejaa chuki, hawana upendo, wamejaa kisasi, kila wakati wanatafuta mabaya watu hao hawatoboi, Mungu anaigeuza Hekima yao kuwa upumbavu

Warumi 1:21-22. “kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;”

Mungu yuko tayari kuiharibu hekima ya watu wenye hila hekima ya dunia hii na amaeahidi katika neno lake kuwa ataiharibu hekima yao wanaojidhani kuwa wana hekima na atazikataa akili zao wanaojidhania kuwa wana akili na hekima ya kidunia itafanywa kuwa upumbavu

1Wakoritho 1:19-20. “Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa. Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu?

Aithofeli alikuwa amemezwa na uchungu, hivyo Hekima na akili yake ilikuwa sio ya kungu bali ilikuwa ya dunia hii hekima iliyojaa ugomvi na kuondoa amani hii ndiyo Mungu anaibatilisha

Yakobo 3:14-18. “Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli. Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.”

Mungu aliishikia Maombi ya Daudi

Katika namna ya kushangaza sana Daudi alimtuma mshauri wake mwingine rafiki yake wa karibu aliyeitwa Hushai kwamba aende kwenye kambi ya maadui, awe miongoni mwa washauri wa Absalom na atumike kutangua ushauri wa Aithofeli, kwa kuwa tayari Ahithofeli alikuwa amejawa na uchungu na moyo wa kisasi na kutokusamehe, lakini zaidi sana kuwa na chuki dhidi ya mpakwa mafuta wa Bwana na hata kukusudia kumuua , Mungu aliutumia ushauri wa Hushai na kwa mara ya kwanza ushauri wa Aithofeli ulikataliwa na hapo ndipo mtu huyu mwenye kiburi alipokimbia nyumbani na kwenda kujiua mwenyewe

2Samuel 17:1-14 .”Zaidi ya hayo Ahithofeli akamwambia Absalomu, Niache nichague watu kumi na mbili elfu, nami nitaondoka na kumfuatia Daudi usiku huu; nami nitamshambulia wakati atakaokuwa amechoka, na mikono yake imekuwa dhaifu, nami nitamtia hofu; na watu wote walio pamoja naye watakimbia; nami nitampiga mfalme peke yake; na hao watu wote nitawarejeza kwako; mtu yule umtafutaye ni kana kwamba wamerudi wote; na hivyo watu wote watakuwa katika amani. Shauri hili likawa jema machoni pa Absalomu, na machoni pa wazee wote wa Israeli. Ndipo Absalomu akasema, Basi, mwiteni Hushai, Mwarki, naye, tukasikie atakayosema yeye pia. Basi Hushai alipofika kwa Absalomu, Absalomu akamwambia, akasema, Ahithofeli amesema hivi; je! Tufanye kama alivyosema? Kama sivyo, sema maneno yako. Hushai akamwambia Absalomu, Shauri hili alilolitoa Ahithofeli si jema wakati huu.Hushai akafuliza kusema, Wamjua baba yako na watu wake, ya kuwa ni watu mashujaa hawa, nao wana uchungu katika mioyo yao, kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake nyikani; tena baba yako ni mtu wa vita, hatalala pamoja na watu wake.Angalia, amefichwa sasa katika shimo, au penginepo; kisha itakuwa, watakapoanguka baadhi yao mwanzo, kila mtu atakayesikia, atasema, Kuna machinjo katika watu wanaofuatana na Absalomu. Basi hata yeye aliye shujaa, mwenye moyo kama moyo wa simba, atayeyuka kabisa; maana Israeli wote wanajua ya kuwa baba yako ni shujaa, na ya kuwa watu wale walio pamoja naye ni mashujaa. Kwa hiyo shauri langu ni hili, Waisraeli wote toka Dani mpaka Beer-sheba wakusanyike kwako, kama mchanga wa bahari kwa wingi; na wewe uende vitani mwenyewe. Hivyo tutamfikia mahali po pote atakapoonekana, na kumwangukia kama vile umande uangukavyo juu ya nchi; wala hatutaacha hata mmoja wao, yeye na watu wote walio pamoja naye. Tena, ikiwa amejitia katika mji uwao wote, basi Israeli wote wataleta kamba, na kuuendea mji ule, nasi tutaukokota mpaka mtoni, wala halitaonekana huko hata jiwe dogo moja la mawe yake. Naye Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, Shauri la Hushai, Mwarki, ni jema kuliko shauri la Ahithofeli. Kwa maana Bwana alikuwa amekusudia kulivunja shauri jema la Ahithofeli, ili Bwana alete mabaya juu ya Absalomu.” Unaona hivi ndivyo Mungu alivyomtetea Mtumishi wake Daudi na kubatilisha shauri la Aithofeli hebu na tuone yaliyomkuta sasa

2Samuel 17:23Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa shauri lake halikufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajisonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.”

Ahithofeli anamwakilisha Yuda, kama jinsi ambavyo Yuda alimsaliti Yesu na kisha alipopata uchungu alikwenda akajiua yeye mwenyewe, Hekima yake ya kumuza Yesu iliishia kuwa mauti, hatuna budi kuhakikisha kuwa wakati wote tunafanya mambo katika hekima ya kiungu, tunapamba kwa kutumia hekima ya Mungu na tujue namna ya kumuo,ba Mungu katika maisha yetu abatilishe kila makusudi mabaya ya adui zetu ama wale wanaotutakia mabaya na wale wenye hekima za dunia hii zilizojaa hila na uchungu tujifunze kumtegemea Mungu katika mambo yote wala tusizitumainie akili zetu wenyewe, Bwana atupe neema yake ili tuweze kuzijua njia zake na Mungu wangu na bwana wangu na aifanye hekima ya adui zetu kuwa ubatili na maarifa yao kuwa upumbavu katika jina la yesu Kristo Amen

Rev. Innocent Samuel Kamote


Mkuu wa wajenzi mwenye hekima!

#0718990796#




Alhamisi, 16 Septemba 2021

Bwana hatamtupa mtu hata milele!


Maombolezo 3:31-33 “Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.


Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu kama baba yetu, ana njia zake za anazozitumia katika kutujenga, kutufunza, kutubadilisha na kutuonya, katika wakati huo Mungu hutumia njia mbalimbali hata mateso, vita na hata matishio ya hapa na pale, ili Hatimaye aweze kutuleta katika toba tumgeukie yeye na kushikamana naye na kumfanya yeye kuwa tegemeo letu

2Petro 3:9 “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.”

Kusudi kubwa la Mungu ni kutuleta katika toba, toba maana yake ni mabadiliko, Neno toba katika lugha ya kiyunani (Greek) ni METANOIA Ambalo maana yake ni badiliko kubwa la moyo, au kugeuka na kuacha njia isiyofaa na kuendea njia inayofaa, kwa hivyi Mungu hutumia huzuni kama baba wa kiroho kutuleta katika makusudi yale yaliyo mema ona

 Waebrania 12:5-11 “tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye; Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.”

Mungu katika hekima yake anapotaka kutonya, kuturekebisha, kutufundisha anaruhusu mateso, lakini sio kwa kusudi la kututesa bali kwa kusudi la kutuleta katika toba yaani mabadiliko makubwa ili hatimaye, tuweze kujenga uhusiano imara na yeye na hatimaye tuweze kuwa na ukomavu wa kiroho na kumuua yeye na njia zake jambo ambalo litaleta furaha milele katika maisha yetu, sawa na baba anavyomuonya mwanae kwa makusudi yale yale ya kumzoeza mtoto kuzaa matunda ya haki na amani.

Bwana hatamtupa mtu hata milele!

Ni ukweli usiopingika kuwa Mungu hakutufanya sisi kuwa kama mashetani, ambao walipoasi aliwakataa milele, sisi ametupa nafasi ambayo kwayo tunaweza kurejesha uhusiano wetu na yeye, Wana wa Israel katika ufalme wa Yuda walikuwa wameacha kumtegemea Mungu na wakawa wakitegema mafanikio yao, akili zao na mambo mengine Mungu akiwaonya kwa vinywa vya manabii huwa angeakatilia mbali kutoka katika nchi njema aliyokuwa amewapa, na anageruhusu waende utumwani

Yeremia 27:6 -8 “Na sasa nimetia nchi hizi zote katika mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu; na wanyama wa mwituni pia nimempa wamtumikie. Na mataifa yote watamtumikia yeye, na mwanawe, na mwana wa mwanawe, hata utakapowadia wakati wa nchi yake mwenyewe, ndipo mataifa mengi na wafalme wakuu watamtumikisha yeye. Na itakuwa, taifa lile na mfalme yule asiyetaka kumtumikia Nebukadreza, huyo mfalme wa Babeli, na kutia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, mimi nitaliadhibu taifa lile kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, asema Bwana, hata nitakapokuwa nimewaangamiza kwa mkono wake.”

Kwa msingi huo Yeremia alitumiwa na Mungu mara kadhaa kuwaonya wana wa Israel na kuwataka wakubali kumtumiakia mfalme huyu wa Babeli kama adhabu  kwao ili baadaye akawabadilishe, Hata hivyo wana wa Yuda hawakutubu wala kuamini kile alichokionya Nebukadreza, hivyo walichukuliwa utumwani na hekalu lao lilibomeolewa na kuchomwa moto kila kitu cha kifahari kiliharibiwa vibaya watu walipitia mateso na walilia na kusaga meno huku Yeremia nabii akiona kila kilichokuwa kinaendelea  jambo lililomfanya ateseke mno kwani aliona mateso ambayo hajawahi kuyaona japo yeye akuuawa lakini ndugu zake na jamaa zake walipata taabu sana  ndipo Yeremuia anaeleza katika maombolezo yake 

Maombolezo 3:1-18 “Mimi ni mtu aliyeona mateso Kwa fimbo ya ghadhabu yake. Ameniongoza na kuniendesha katika giza Wala si katika nuru. Hakika juu yangu augeuza mkono wake Mara kwa mara mchana wote. Amechakaza nyama yangu na ngozi yangu; Ameivunja mifupa yangu.  Amejenga boma juu yangu, Na kunizungusha uchungu na uchovu.  Amenikalisha penye giza, Kama watu waliokufa zamani. Amenizinga pande zote hata siwezi kutoka; Ameufanya mnyororo wangu mzito. Naam, nikilia na kuomba msaada, Huyapinga maombi yangu. Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa; Ameyapotosha mapito yangu. Alivyo kwangu ni kama dubu aoteaye, Kama simba aliye mafichoni. Amezigeuza njia zangu, na kunirarua-rarua; Amenifanya ukiwa. Ameupinda upinde wake, Na kunifanya niwe shabaha kwa mshale. Amenichoma viuno Kwa mishale ya podo lake. Nimekuwa dhihaka kwa watu wangu wote; Wimbo wao mchana kutwa.  Amenijaza uchungu, Amenikinaisha kwa pakanga. Amenivunja meno kwa changarawe; Amenifunika majivu. Umeniweka nafsi yangu mbali na amani; Nikasahau kufanikiwa. Nikasema, Nguvu zangu zimepotea, Na tumaini langu kwa Bwana.”

Mfalme huyu katili alifanya unyama wa ajabu sana ona mukhtasari wa unyama wake:-

1.       Aliuzingira Yerusalem kwa muda wa miaka miwili na kuhakikisha kuwa wanateseka kwa njaaa

2.       Aliwavamia na kuwapiga na kuwachukua mateka vijana wenye nguvu

3.       Alilibiomoa hekalu na kulichoma moto kwa kuliteketeza

4.       Aliwaongoza njiani wayahudi huku akiwaachia wengine waliwe na simba

5.       Alihakikisha kuwa wanapelekwa utumwani Babeli moja kwa moja bila kupumzika ili kuwanyima wayahudi nafasi ya toba, na maombi ili Mungu wao asije akawaokoa

6.       Akiwaasi vijana wenye hekima na wazuri wasizae tena, na kuwageuza matowashi katika nyumba yake

Katika historia ya Israel wanamkumbuka Mfalme huyu kama mfalme katili zaidi kupata kutokea katika ulimwengu, dikteta asiye na huruma ambaye ataendelea kukumbukwa kwa miaka Mingi kama anavyokumbukwa “Adolf Hitler” aliyeua wayahudi wapatao milioni sita, watu wale walioona mateso haya walihuzunishwa sana na hiki kilichotokea, ilikuwa ni taabu mno na wengi wakasema Mungu ametutupa, ni ukweli uliokuwa wazi kwamba hata adui za Israel waliita Sayuni mji uliotupwa, Na ndipo Yeremia alipotoa unabii kuwa Mungu ataujenga tena Sayuni 

Yeremia 30:17-19 “Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye. Bwana asema hivi, Tazama, nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyokuwa desturi yake. Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge.”

Mungu ametuahidi kuwa hatatutupa kamwe !

Ni ahadi ya Mungu kuwa hatatutupa milele, Yesu alisema kila ajae kwangu sitamtupa nje kamwe Yohana 6:37-39 “Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka. Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho.”

  Ni wajibu wetu kufahamu kuwa tunaweza kupita katika giza, tunaweza kupitia mateso na huzuni nzito, mashaka na woga, mashutumu na masengenyo, giza na kutokufanikiwa, mashambulizi ya adui pande zote, kizibiwa niia, kama milango imefunga kila mahali lakini hatuna budi kukumbuka neno la Mungu na Bwana wetu Yesu ametuahidi kuwa hatatuacha milele, wala hatatutupa kamwe, wanadamu wanaweza kututupa, wanaweza kutudharau, wanaweza kutuweka pembeni, wanaweza kutozomea lakini Mungu hawezi kamwe kuwatupa watu wake, tunapohisi kuwa tunapita katiika huzuni na mateso kumbuka kuwa hatujaweka tumaini letu kwa mwanadamu wala kwa miungu tutaendelea kuliitia jina la bwana Mungu wetu mpaka kielelweke

a.       Endelea kuliitia jina la Bwana na kumpazia sauti  Zaburi 77:7 – 1-2, “Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam, nimpazie Mungu, naye atanisikia. Siku ya taabu yangu nalimtafuta Bwana; Mkono wangu ulinyoshwa usiku, haukulegea; Nafsi yangu ilikataa kufarijika.” 7-9 “Je! Bwana atatupa milele na milele? Hatatenda fadhili tena kabisa? Rehema zake zimekoma hata milele? Ahadi yake imekwisha hata vizazi vyote? Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake?

               

b.      Kumbuka wewe ndio urithi wa Bwana na hakuna mwingine  Zaburi 94:14 “Kwa kuwa Bwana hatawatupa watu wake, Wala hutauacha urithi wake,”

 

c.       Kumbuka tunalibeba jina lake kuu na Bwana amekusudia kutufanya kuwa watu wake 1Samuel 12:20-22 “Samweli akawaambia, Msiogope; ni kweli mmeutenda uovu huu wote; lakini msigeuke na kuacha kumfuata Bwana, bali mtumikieni Bwana kwa mioyo yenu yote. Wala msigeuke upande, maana, kufuata vitu vya ubatili, visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana Bwana hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza Bwana kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe.”

 

d.      Kumbuka kuwa mapito yako ni ya kitambo tu na kuwa Bwana hatamtupa mtu hata milele! Maombolezo 3:31-33 “Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.


Wewe ni Mungu mpasua bahari, haufananishwi na kitu kingine, haulinganishwi. na kitu kingine unafanya mambo ambayo mwanadamu hawezi kufanya, unatoa faraja ambayo mwanadamu hawezi kutoa haulinganishi na kitu kingine.

Na Rev. Innocent Samuel Jumaa Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye hekima!

Jumanne, 31 Agosti 2021

Kwa maana yupo Mkuu Pamoja nasi !


2Nyakati 32:7-8 “Iweni hodari, na wa moyo mkuu, msiogope, wala msifadhaike kwa sababu ya mfalme wa Ashuru, wala kwa majeshi yote walio pamoja naye; kwa maana yupo mkuu pamoja nasi kuliko aliye pamoja naye; kwake upo mkono wa mwili; ila kwetu yupo Bwana, Mungu wetu, kutusaidia, na kutupigania mapigano yetu. Na watu wakayategemea maneno ya Hezekia, mfalme wa Yuda.”              

Utangulizi:

Kwa maana yuko Mkuu pamoja nasi! Ni maneno ya kutia moyo katika wakati Mgumu, wakati ambapo Mfalme senekarebu wa Ashuru, alipokuja kuizingira Yerusalem ili auangamize, Mfalme huyu alikuwa anapata ushindi kila alikokwenda, na kwa sababu alikuwa akiabudu miungu aliamini ushindi wake umetokana na Mungu aliyemuamini, Yeye alikuwa ameshinda vita zote za kaskazini wakati wa kampeni yake ikiwemo ufalme wa Israel ya kaskazini maarufu kama samaria, Ushindi wake dhidi ya mataifa mengine na hata Israel ya kusini ulimpa kiburi na kujiona kuwa yeye sasa ni super power kingdom na kuwa ana uwezo wa kumshinda yeyoye, kwani hata hao waliodai kutegemea miungu ya aina mbalimbali pia aliwashughulikia ona maneno yake

 2Nyakati 32:9-19 “Na baada ya hayo Senakeribu mfalme wa Ashuru, akatuma watumishi wake waende Yerusalemu, (naye alikuwapo mbele ya Lakishi, na uwezo wake wote pamoja naye,) kwa Hezekia, mfalme wa Yuda, na kwa Yuda wote waliokuwako Yerusalemu, kusema, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, asema hivi, Mwatumainia nini hata mkae mkihusuriwa katika Yerusalemu? Siye Hezekia anayewashawishi, mtolewe kufa kwa njaa na kwa kiu, akisema, Bwana, Mungu wetu, atatuokoa na mkono wa mfalme wa Ashuru? Si yeye Hezekia huyo aliyeondoa mahali pake pa juu, na madhabahu zake, akawaamuru Yuda na Yerusalemu, akisema, Abuduni mbele ya madhabahu moja, na juu yake mtafukiza uvumba? Je! Ninyi hamjui mimi na baba zangu tuliyowafanyia watu wote wa nchi? Je! Miungu ya mataifa wa nchi iliweza kuokoa kwa lo lote nchi zao na mkono wangu? Ni yupi miongoni mwa miungu ya mataifa wale walioharibiwa kabisa na baba zangu, aliyeweza kuwaokoa watu wake na mkono wangu, hata Mungu wenu aweze kuwaokoa ninyi na mkono wangu? Basi sasa asiwadanganye Hezekia, wala asiwashawishi kwa hayo, wala msimwamini; kwa kuwa hapana mungu wa taifa lo lote, wala wa ufalme wo wote, aliyeweza kuwaokoa watu wake na mkono wangu, au na mkono wa baba zangu; sembuse Mungu wenu atawaokoaje ninyi na mkono wangu? Na watumishi wake wakazidi kusema juu ya Bwana Mungu, na juu ya Hezekia, mtumishi wake. Tena akaandika waraka, kumtukana Bwana, Mungu wa Israeli, na kumwambia, akisema, Kama vile miungu ya mataifa wa nchi isivyowaokoa watu wao na mkono wangu, vivyo hivyo Mungu wa Hezekia hatawaokoa watu wake na mkono wangu. Wakawalilia kwa sauti kuu, kwa lugha ya Kiyahudi, watu wa Yerusalemu waliokuwako ukutani ili kuwaogofisha, na kuwafadhaisha; hata wapate kuutwaa mji. Wakamnenea Mungu wa Yerusalemu, kana kwamba kuitaja miungu ya mataifa wa nchi, iliyo kazi ya mikono ya watu.”


Ushindi wake dhidi ya mataifa mengine na Israel ya Kaskazini ulimfanya Senekarebu ajivune na kufikiri kuwa hakuna Mungu mwingine anayeweza kumshughulikia, Hili lilikuwa tishio kubwa sana kwa Hezekia kwani senekarebu alichiokuwa anakisema ni kweli, na alikuwa ameshinda vita zote na sasa anaikabili Yuda na anaukabili mji wa Yerusalem, na alikuwa na kombaini kubwa sana ya majeshi, Yeye ndio alikuwa taifa kubwa Duniani kwa wakti ule na hakuna taifa lolote lililoweza kusimama mbele yake kwa miaka Mingi, Senekarebu alikuwa amejiimarisha vya kutosha akiwa na jeshi lenye nguvu kweli kweli na alikuwa tayari anaumiliki ulimwengu wa wakati ule na tayari hata taifa ndugu la Israel lilikuwa limesalimu amri, na kama ilivyokuwa desturi ya vita hapa senekarebu anapeleka vitisho na athari za kisaikolojia kwa utawala wa kiyahudi!


Mfalme Hezekia akiwa na ujuzi mkubwa wa siri ya ushindi, alimuomba Mungu lakini vilevile alitumia Hekima na akili ya kujilinda  Yeye Pamoja na nabii Isaya walimuomba Mungu na kumlilia kwa nguvu hata mbinguni ona 2Nyakati 32:20 “Na kwa ajili ya hayo Hezekia mfalme, na Isaya nabii, mwana wa Amozi, wakaomba, wakalia hata mbinguni.” Hezekia aidha alihakikisha kuwa maji hayatiririki kuwafikia maadui, hivyo yeye na watu wake waliwakati amaji kwa kuifunga mifereji ya kupeleka maji ili majeshi ya maadui wapatwe na kiu ona , Lakini pia alijenga ukuta wa Yerusalemu uliokuwa umeanguka, na kufanya maandalizi ya kivita kwa kutengeneza silaha na kuandaa maakida au makamanda aidha yeye mwenyewe alitoa speech ya kuwatia moto na kuwafurahisha watu ambayo ilikuja kuwa tumaini kubwa kwa watu na kuleta utayari wa vita ona 


2Nyakati 32:2-6. “Basi Hezekia, alipoona ya kuwa Senakeribu amekuja, na kuazimia kupigana na Yerusalemu, akafanya shauri na wakuu wake, na mashujaa wake, kuzuia maji ya chemchemi zilizokuwa nje ya mji; nao wakamsaidia. Wakakusanyika watu wengi, wakazizuia chemchemi zote, na kijito kilichopita kati ya nchi, wakisema, Kwa nini, wakifika wafalme wa Ashuru, waone maji mengi? Akapiga moyo konde, akaujenga ukuta wote uliobomoka, akauinua sawa na minara, na ukuta wa pili nje, akaongeza nguvu ya Milo, katika mji wa Daudi, akafanya silaha na ngao tele. Akaweka maakida wa vita juu ya watu, akawakusanya kwake uwandani penye lango la mji, akawafurahisha mioyo; akisema


Hezekia alikuwa na ufahamu kuwa Israel haiku yenyewe hivyo pamoja na maandalizi ya vita , na maombi yeye alikumbuka wazi kama nabii Elisha aliyemtia moyo mtumishi wake kuelewa kuwa katika ulimwengu war oho watu wamuaminio Mungu hawako pake yao hatuko peke yetu ona 

2Wafalme 6:15-16 “Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje? Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.”    

        

Hezekia alikuwa na ufahamu huo aliliamini neno la Mungu, alikuwa amejifunza kuwa watu wanaomuamini Mungu hawako peke yao, aliamini kuwa kuna zaidi ya majeshi ya kimwili yanayoonekana, na kuna majemadari zaidi ya majemadari wa kimwili wanaoonekana Hauijalishi kuwa senekarebu ana nguvu kiasi gani, ana historia ya ushindi na uonevu kiasi gani yeye hakuwa anatoa propaganda za kawaida za kijeshi yeye alikuwa anazungumza ukweli ulio wazi kwamba  yupo Mkuu Pamoja nasi !, na kuwa mfalme Senekarebu na majeshi yake yote hayana kitu kwa huyu Mungu wa wayahudi, na kwa kuwa mfaklme huyu alitoa maneno ya kejeli na kumtukana Mungu wa Israel Mungyu alileta ushindi wa ajabu sana safari hii Mungu alituma malaika mmoja tu na akadhalilisha jeshi zima la waashuru ona


2Nyakati 32:21-22 “Naye Bwana akatuma malaika aliyewakatia mbali mashujaa wote, na majemadari, na maakida, matuoni mwa mfalme wa Ashuru. Basi akarudia nchi yake mwenye haya ya uso. Naye alipoingia nyumbani mwa mungu wake, wale waliotoka viunoni mwake mwenyewe wakamwangamiza humo kwa upanga. Ndivyo Bwana alivyomwokoa Hezekia, na wenyeji wa Yerusalemu, na mkono wa Senakeribu, mfalme wa Ashuru, na mikononi mwa wote, akawaongoza pande zote.”  


Nisikilize sio kila wakati Mungu atawatawanya maadui zako wasikuzingire, Mungu atawaacha wakufkie wakutishe, lakini ukisimama imara na ukawa na uelewa kuwa Mungu anafanya kasi namna gani wataaibika na kufedheheka wanaokutafuta nafi yako kumbuka maandiko yanasemaWaandaa meza mbele yangu machioni pa watesi wangu” Zaburi 23;5. Tunaye Mungu ambaye wakati wote anawajali watu wamuaminio na kumtumaini yeye atwaacha adui zetu waingine kwenye 18 zake kisha atawateketeza, aliwaacha wamisri waingie kwenye bahari ya shamu na kisha akawafytilia mbali, alimuacha Senekarebu afike na kuizunguka Yerusalem lakini alimfutilia mbali


Siku zote nasema tukimtumaini Bwana na kumtegemea yeye tutakuwa salama, jambo kubwa la msingi la kuelewa ni kuwa Yule mkuu aliye pamoja nasi, ndio Emmanuel Mungu pamoja nasi, kila aina ya adui zako watapotea na Mungu atawaaibisha senekarebu alirudi kwa aibu kwao na kupinduliwa na watoto wake mwenyewe kupigo alichokipata kilikuwa kipigo cha kushangaza, hakupigwa na wingi wa majeshi alishughulikiwa na Askari mmoja tu kutoka Mbinguni, Bwana ni Mungu nwa Majeshi na atatupigania dhidi ya adui zetu na wale wanaotuandama na kututisha bila kujali historia zao kuwa wana nguvu kliasi gani, wana fedha kiasi gani ni maarufu kiasi gani Yuko mkuu pamoja nasi, yuko mkuu pamoja name, Yuko mkuu pamoja nawe, yuko mkuu ni Mungu pamoja nasi anatosha peke yake kusambaratisha maadui na ikuwarudisha nyumbani kwao kwa aibu wakafie mbele

 

Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima !

Jumatatu, 30 Agosti 2021

Si kumwamini tu ila na kuteswa kwaajili yake!


Wafilipi 1:29 “Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake;”


Utangulizi:

Ni muhimu kufahamu kuwa mojawapo ya masomo ya msingi sana mara baada ya mtu kumuamini Yesu, ni pamoja na uelewa mpana ya kwamba kumfuata Yesu sio jambo jepesi kama wengi wanavyokudhani, Lakini kumuamini Yesu, vilevile kutaambatana na changamoto kadhaa ikiwemo mateso, Wahubiri wengi wa nyakati za leo wameacha kuwakumbusha watu wa Mungu kwamba mateso, dhiki na udhia ni sehemu ya injili, kuhubiri upande mmoja tu wa mafanikio bila kuisema kweli hii ni sawa na kuhubiri injili ya mafanikio “Prosperity Gospel” kufanya hivyo ni kushindwa kutoa mlo kamili (The balance diet) wakati wa kuwapikia watu neno la Mungu, Lakini kutokuwatahadharisha watu ya kuwa kuna dhiki na udhia na mateso na hata kuuawa kwaajili ya injili ni kuwa kinyume na mafundisho ya Yesu na Mitume pia ambao wao kwa uwazi walikaza kuwa ni lazima watu wanaomuamini wajikane nafsi na kuwa imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nayingi na hivyo wasine kuwa ni ajabu wanapopita katika majaribu ya aina mbalimbali ona   

Mathayo 16:24-25 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.

Unaona? Kwa bahati mbaya nyakati za leo wahubiri wengi wa kisasa wanashindwa kuweka uwiano wa kuwaelezea watu ukweli huu kuwa kumfuata Yesu sio lele mama, kwa kadiri tunaposonga mbele katika imani utagundua wazi kuwa wokovu sio kitu chepesi na wala sio lele mama, tunahitaji sio tu kujikana nafsi lakini na neema izidiyo ili tuweze kustahimili, Nyakati za kanisa la kwanza somo kuhusu Mateso lilikuwa ni moja ya somo la kwanza la muhimu katika kuwaimarisha wanafunzi wa Yesu ona

Matendo 14:21-22 “Hata walipokwisha kuihubiri Injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia, wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.”        

Kumfuata Yesu kuna mchanganyiko wa mambo mazuri, furaha na amani, na mafanikio mengi sana  lakini vilevile kuna udhia yaani iko dhiki ambayo waliomuamini Yesu watakumbana nayo, Yesu aliweka wazi swala hili mapema wakati Petro alipouliza swali kuwa sisi tumeacha vyote tutapata nini kwa kufuata wewe? ona

Marko 10:28-30. “Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.”

Kwa msingi huo ni lazima ieleweke wazi kwamba kila mtu anayemuamini Yesu, sio tu kuwa kumuamini Yesu kutatufanya tusijaribiwe na au kupitia dhiki za namna mbalimbali hapana tutapitia dhiki na mateso ya aina mbalimbali Petro aliwaambia wakristo wa nyakati za kanisa la kwanza kuwa imani yao itajaribiwa kama dhahabu inapopitishwa katika moto

1Petro 1:6-7 “Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.”

1Petro 4:12 “Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho.   

Unaona kupitia mateso, au misiba kwa mtu aliyemuamini Yesu halipaswi kuonekana kuwa ni jambo geni, maana yake ni jambo la kawaida kwa sababu nasi tunashiriki mateso pamoja na Bwana wetu Yesu Kristo kwa msingi huo ni kawaida na tunapaswa kuwa na subira katika mapito haya, na kwa kadiri mtu anavyopenda kuishi maisha ya utauwa yaani maisha matakatifu ya kumpendeza Mungu ndio anaudhiwa zaidi ona:-

2Timotheo 3:12 “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.”

Kwa msingi huo kuna  muhimu kuwaelimisha watu wa Mungu mapema wakaelewa kuwa kuwa kuwa katika mpango wa Mungu hakukufanyi wakati wote uwe na raha tu, Yesu alisema ulimwenguni mnayo dhiki lakini jipeni moyo mimi nimeushinda ulimwengu, watu wengi sana hudhani pia labda mtu unapopitia changamoto za aina mbalimbali labda uko nje ya mapenzi  ya Mungu, au hauko sehemu sahihi hapana uko sehemu sahihi na Yesu yuko pamoja nawe lakini hii haimaanishi kuwa dhoruba utazikwepa kwa msingi huo ni lazima upambane na kuendelea kumtegemea Yesu kwani hako mbali atashughulika na changamoto yako ona jinsi Yesu alivyowafundisha jambo hili wanafunzi wake kwa maneno na kwa vitendo:-

Marko 4:35-41 “Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo. Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye. Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia? Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.  Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?  Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?

Ilikuwa ni jambo la kushangaza kuwa ni Bwana mwenye aliyewaahidi wanafunzi wake wavuke ng’ambo, na Yeye mwenyewe alikuwemo chomboni, lakini ni jambo lenye kushangaza kuwa dhoruba kubwa ilitokea na kuwatisha sana wanafunzi wake hata wakashangaa kwanini Yesu amerelax na kulala usingizi wala hana hofu wakati wao wanakaribia kuangamia, lakini kwa wakati wake walipomwamsha akaukemea upepo, na kuwakemea na wao kwa kuwa hawakuwa na imani kwamba Mungu yuko Pamoja nao,

Jambo kubwa la msingi na la kulielewa ni kuwa majaribu hayo na mateso hayo hayatakumaliza, Mungu hajamaanisha katika neno lake kuwa hatutapitia changamoto bali anataka tuendelee kutambua hata ndani ya changamoto hizo yeye yupo na analo kusudi ndani yake kwa msingi huo hatuna budi kutamka maneno ya ushindi kwamba hata kupitia changamoto za aina gani yeye yuko pamoja nasi na ametushika kwa mkono wake hakuna changamoto itakayokumeza hususani pale Yesu anapokuwa ametuahidi kuwa atakuwa pamoja nasi, na kama ametukomboa na ametuelekeza lolote katika neno lake basi hatupaswimkuogopa na kudhani au kufikiri kuwa tutazama, Muujiza huu alioufanya Yesu una mafundishi wazi kuwa tunaweza kuwa katika mapenzi ya Mungu na tunaweza kuwa na Mungu mwenyewe na wakati huohuo dhuruba zikatupata hii haina maana ya kuwa neno la Mungu sio kweli, wala haina maana kuwa uwepoo wake umepungua hapana, Yuko pamoja nasi, anatupenda na ahadi zake kwetu ni ndio na kweli na tutapitia changamoto kadhaa lakini hiyo haimaanishi kuwa Mungu ametuacha yeye hatimaye ataikemea ile hali somo kama hili lilikuwa wazi pia hata kwa nyakati za watakatifu wa agano la kale ona :-

 Isaya 43:1-2 “ Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. ”   

Ni  imani yangu kwamba safari ya imani ina mawimbi, ina hofu,ina huzuni, ina mateso, lakini Kristo Yesu atatufikisha ng’ambo salama, Mashaka na hofu zinazotusonga  na dhoruba zitatusumbua lakini kama Yesu atakuwa pamoja nasi ni yeye aliyetuita kwa neno lake kwa hiyo hatupaswi kuogopa  tunapozidiwa kumbuka kuomba au kuimba kama Marehemu Fanuel Sedekia aliyeimba Nishike mkono na Bwana  naye Mungu Yule tunayemtegemea atakushika Mkono na hatatuacha tuzame na atatukomboa:-

Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima  

Nishike Mkono

Fanuel Sedekia

Safari ya imani, nakutazama Yesu
Nataka nifike ng'ambo salama
Lakini njiani mawimbi ni mengi
Mashaka yanisonga kuniangamiza

Oh, oh, oh, nishike mkono nisizame
Mawimbi ni mengi, niokoe
Oh, oh, oh, nishike mkono nisizame
Mawimbi ni mengi, niokoe

Mawimbi ni makali nahitaji msaada
Nishike Mwokozi niwe salama
Wewe ulieniita nakuja kwa neno lako
Napata kutembea kwa neno lako

Oh, oh, oh, nishike mkono nisizame
Mawimbi ni mengi, niokoe
Oh, oh, oh, nishike mkono nisizame
Mawimbi ni mengi, niokoe

Safari ya imani, natembea kwa imani
Zambi isinishinde, nisaidie
Katika majaribu makali kama moto
Najua nitatoka kama dhahabu

Oh, oh, oh, nishike mkono nisizame
Mawimbi ni mengi, niokoe
Oh, oh, oh, nishike mkono nisizame
Mawimbi ni mengi, niokoe

Oh, oh, oh, nishike mkono nisizame
Mawimbi ni mengi, niokoe
Nishike mkono nisizame
Mawimbi ni mengi, niokoe

Nishike mkono nisizame
Mawimbi ni mengi, niokoe
Nishike mkono nisizame
Mawimbi ni mengi, niokoe

Jumatatu, 23 Agosti 2021

Kumuweka Bwana mbele Daima


Andiko la Msingi: Zaburi 16:8 “Nimemweka Bwana mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.”


Utangulizi:

Zaburi hii ni zaburi iliyotungwa na kuimbwa na Daudi, Ni zaburi ya kimasihi hasa kutokana na unabii unaomuhusu Yesu Kristo moja kwa moja, hata hivyo kupitia zaburi hii bado kuna mambo ya muhimu ya kujifunza kutokana na maisha ya Daudi, na uwezo wake aliokuwa nao katika kumtegemea Mungu na faida zake, Daudi anatufunulia siri mojawapo kubwa ya ushindi na mafanikio yake katika kudumisha uhusiano na Mungu, katika mstari huu wa nane kuna maswala ya msingi matatu ya kujifunza kama ifuatavyo:-


·         Kumuweka Bwana mbele Daima

·         Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu

·         Sitaondoshwa!


Kumuweka Mungu mbele Daima.

Moja ya siri kubwa ya ushindi katika maisha ya Daudi ilikuwa ni pamoja na kumuweka Mungu mbele, Katika biblia ya kiingereza neno kumuweka Mungu mbele linasomeka hivi “I have set the Lord always before meNeno “SET” la kiingereza linalotumika hapo liko sawa na neno la kiebrabia “SAWA” kwa msingi huo tafasiri rahisi ya mstari wa aya hiyo katika kiingereza inaweza kusemeka hivi “I have equally set” ambalo katika Kiswahili tunaweza kutumia neno Nimekwenda sambamba na Mungu, au nimetembea sawasawa na Mungu, au kwenda pamoja na Mungu, au kuendenda kwa jinsi ya Mungu lugha hii ya kibiblia ndiyo ambayo imetumika katika Mwanzo 5:22,24Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa” .ikionyesha jinsi “Henoko akaenda pamoja na Mungu” kwa hiyo duniani kuna aina tatu za mwenendo, kwa jinsi ya Mungu, kwa jinsi ya kishetani na kwa jinsi ya kibinadamu.

1Wakoritho 3:3 “Kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini, maana ikiwa kwenu kuna husuda, na fitina Je si watu wa tabia ya mwilini; tena mnaendenda kwa jinsi ya kibinadamu

Daudi alidhamiria katika maisha yeke kuenenda kwa jinsi ya Mungu siku zake zote. Hakutaka kuenenda kwa jinsi nya mwili wala ya kishetani aliamua maisha yake yote kumuweka Mungu mbele hii ilikuwa siri ya maisha ya ushindi kwa Daudi siku zote za maisha yake.

Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu.

Mkono wa kuume yaani mkono wa kulia kama unavyojulikana sana kwa lugha ya Kiswahili ni kuwekwa mahali pa Heshima kubwa sana, ni sawa na kutawala pamoja, au kukaa katika meza ya kifalme, kuamua pamoja naye, kula pamoja naye kushauriana na kufanya maamuzi ya pamoja, hivyo mtu alipomuweka mtu mkono wake wa kuume maana yake kumuweka mahali pa heshima kubwa unaweza kuona mfano:-

 2Samuel 9:1-9, “1. Kisha Daudi akasema, Je! Amesalia mtu mmoja katika nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema kwa ajili ya Yonathani? 2. Palikuwa na mtumishi mmoja wa nyumba ya Sauli, jina lake Siba, basi wakamwita aende kwa Daudi; na mfalme akamwuliza, Wewe ndiwe Siba? Naye akasema Mimi, mtumwa wako ndiye. 3. Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu ye yote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu. 4. Mfalme akamwambia, Yuko wapi? Siba akamwambia mfalme, Tazama, yumo katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari. 5. Basi mfalme Daudi akatuma watu, akamwondoa katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari. 6. Basi Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli akaenda kwa Daudi, akaanguka kifudifudi, akasujudu. Daudi akasema, Mefiboshethi! Naye akaitika, Mimi hapa, mtumwa wako! 7. Daudi akamwambia, Usiogope, maana bila shaka nitakutendea mema; kwa ajili ya Yonathani, baba yako, nami nitakurudishia mashamba yote ya Sauli, baba yako; nawe utakula chakula mezani pangu daima. 8. Akasujudu, akasema, Mimi mtumwa wako ni nini, hata ukamwangalia mbwa mfu kama mimi? 9. Ndipo mfalme akamwita Siba, mtumwa wa Sauli, akamwambia, Mali yote yaliyokuwa ya Sauli na ya nyumba yake nimempa mwana wa bwana wako. 10. Nawe utamlimia nchi hiyo, wewe, na wanao, na watumwa wako; nawe utamletea mwana wa bwana wako matunda yake, apate chakula ale; lakini Mefiboshethi, mwana wa bwana wako, atakula chakula mezani pangu sikuzote. Basi huyo Siba alikuwa na wana kumi na watano na watumwa ishirini. 11. Ndipo Siba akamwambia mfalme, Mimi, mtumwa wako, nitatenda hayo yote kama bwana wangu, mfalme, alivyoniamuru. Na kwa habari za Mefiboshethi, mfalme alisema, Atakula mezani pangu, kama mmojawapo wa wana wa mfalme. 12. Huyo Mefiboshethi alikuwa na mwana mdogo, jina lake akiitwa Mika. Na watu wote waliokaa nyumbani mwa Siba walikuwa watumwa wa Mefiboshethi. 13. Basi Mefiboshethi akakaa Yerusalemu; maana alikuwa akila chakula sikuzote mezani pa mfalme; naye alikuwa na kilema cha miguu yote miwili.

Watu wa nyakati za agano jipya walifahamu vizuri umuhimu wa swala hili, swala la kumuweka mtu mkono wa kuume lilimaanisha kumuheshimu mtu huyo kwa kiwango kikubwa na cha hali ya juu, katika serikali kumuweka mtu mkono wa kuume ni sawa na kumfanya kuwa makamu wa rais, wana wa  Zebedayo kupitia mama yao waliwahi kumuomba Yesu wapewe nafasi hii lilikuwa ni ombi la ajabu sana ambalo gharama yake ilikuwa ni kupitia mateso na aibu ileile aliyoipitia Yesu Kristo  Biblia inasema hivi:-

Mathayo 20:20-23 “Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno. Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako. Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza. Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.

 Aidha kumuweka mtu mkono wa kuume maana yake ni kumfanya kuwa msaada wako, na ngao yako au mlinzi wako au mtetezi wako, mtu anayeketi mkono wako wa kuume ni msaada mkubwa ni mwenzako ni  wakaribu ni mwanachama mwenzako COMRADE

Daudi kutokana na kumtegemea kwake Mungu na kutembea naye alikuwa na uhakika kuwa Mungu yuko mkono wake wa kuume ndiye anayemshauri, ndiye anayemlinda na ndiye anayemtegemea na kwa sababu hiyo alikuwa na uhakika kuwa hatoondoshwa!

Sitaondoshwa!

Kutokuondoshwa kunakotajwa mahali hapo, maana yake ni kuwa salama, kutokusumbuliwa na maadui, kutokuogopa, kutokutikiswa, kulindwa dhidi ya maadui, kuokuingia matatani, kutokuwamo taabuni Zaburi 10:6Asema moyoni mwake, Sitaondoshwa, Kizazi baada ya kizazi sitakuwamo taabuni.”, kudumu milele Zaburi 15:5 “Hakutoa fedha yake apate kula riba, Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele.”, kutokutetemeshwa Zaburi 46:5 “Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema.”, Hutotikisika

Kwa ufupi Daudi anatufundisha

1.       Kumuweka Mungu mbele siku zote za maisha yetu

2.       Kumfanya kuwa ngao yetu

3.       Kumfanya kuwa kinga yetu

4.       Kumfanya kuwa tegemeo letu

5.       Kumfanya kuwa mwangalizi wetu

6.       Kumueshimu na kutembea naye

7.       Kumtii yeye na kutafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na mengine tutazidishiwa

Na tukiyafanya hayo

1.       Tutakuwa na furaha

2.       Hatutatikisika milele

3.       Mungu atakuwa tegemeo letu na ngao yetu, na mshauri wetu, na tutayafanya mapenzi yake

Taifa lolote, chama chochote, mtu yeyote na taasisi yoyote kama tumedhamiria kumuweka Mungu mbele katika maisha yetu mafanikio ni lazima, furaha ya Bwana ndio nguvu zetu, amani ya Mungu ndio nguvu yetu kubwa sana, kama ukimuweka Mungu mbele, katika mitihani, katika maisha ya kila siku, katika kazi zetu, katika ndoa zetu, katika dua zetu na ibada na maombi yetu kila kitu mfanye Mungu kuwa mkono wako wa kuume na utakuwa msindi na zaidi ya kushinda.

Rev. Innocent Kamote

“Mkuu wa Wajenzi mwenye hekima”