Jumatano, 16 Novemba 2022

Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu!


Luka 16: 9 - 12Nami nawaambia, Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele. Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe? Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.


Utangulizi:

Mojawapo ya kifungu kigumu katika tafasiri za mafundisho ya Yesu ni pamoja na maneno haya ambayo Yesu aliyasema kama sehemu ya Hitimisho ya mfano tajiri na wakili wake, katika Luka 16:1-8 ambako kimsingi Yesu Kristo alikuwa anatufundisha wazi namna ya kutumia fedha na mali tulizopewa na Mungu na ujuzi ya kuwa hatuna tunachomiliki duniani, na kuwa tunwajibika namna tunavyotumia mali na fedha na kwamba tutatoa hesabu ya kila alichotupa Mungu. Baada ya fundisho hilo Muhimu ndipo sa Yesu alianza kuweka mikazo ya maneno haya tunayojifunza leo JIFANYIENI RAFIKI KWA MALI YA UDHALIMU! Kimsingi Yesu alikuwa anafundisha namna ya kujipatia utajiri wa kweli. Yesu qanawataka wanafunzi wake kutumia fedha na mali za ulimwengu huu walizonazo kujipatia thawabu za kudumu katika ufalme wa Mungu. Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo:-

Ø  Tafasiri ya Mali, fedha, Utajiri na udhalimu wakati wa Yesu Mst9-11

Ø  Jifanyieni rafiki kwa mali ya Udhalimu Msta 9-12

Ø  Jinsi ya kumtumikia Mungu na Mali Mst 13

Tafasiri ya Mali, fedha, Utajiri na udhalimu wakati wa Yesu (Mst9)

Luka 16:9-11 “Nami nawaambia, Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele.  Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.  Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli?”

Ni muhimu kufahamu kuwa wakati wa Yesu Kristo katika mwili Duniani falsafa kuhusu Mali utajiri na fedha ilikuwa na mitazamo mikubwa mwiwili, hasa katika jamii ya mafarisayo na watu wa ulimwengu wa wakati ule Katika mtazamo wa kwanza wa Mafarisayo hasa katika lugha ya KIARAMU, kuwa na Mali, fedha na utajiri kulihusishwa moja kwa moja na dhuluma (UDHALIMU). Kwa kiyunani ni “ADIKOS”- Wicked, treacherous, unjust au unrighteousness,  Matajiri walikuwa wanafikiriwa kuwa ni watu dhalimu na kuwa walivyonavyo wamevipata kwa kudhulumu au kwa njia zisizofaa kwa hiyo walivipata kwa kufanya dhambi, kwa njia za uovu, kudhulumu watu  kwa hila, au isivyo sawasawa na pia walivitumia kwa anasa na ubinafsi mkubwa ona 

Yakobo 5:1-6 “Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia. Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo. Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho. Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi. Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo. Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi.”

Kwa hiyo fedha na mali na utajiri ulifikiriwa na kuhusishwa na choyo na dhambi katika mtazamo wa kwanza, lakini vilevile katika mtazamo mwingine au falsafa ya pili fedha ilifikiriwa kuwa ni Baraka kutoka kwa Mungu kama mmiliki alikuwa amezipata kwa haki huku akiwa anamcha Mungu,

Marko 10:17-23 “Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu. Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako. Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu. Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate. Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi. Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!

Hata hivyo Matajiri wote wale waliofikiriwa ni wadhuluma na wale wa haki wote walikuwa na matatizo wote walikuwa wanakabiliwa na choyo na ubinafsi, na hivyo Yesu yeye alizuiona fedha mali na utajiri wa dunia hii kama havitatumika kwa usahihi madamu ni mali za duniani zote aliziita mali za udhalimu, kwa nini kwa sababu haziwezi kuwapa wanadamu manufaa ya kudumu katika ulimwengu wa ufalme wa Mungu.

Jifanyieni rafiki kwa mali ya Udhalimu Msta 9-12

Kama tulivyojifunza hapo awali ya kuwa Yesu aliona matumizi yote ya fedha kwa watu wa dunia hii bila kujali mali zao wamezipataje mali zao zingeliweza kuwapa manufaa ya kudumu kama watakosa akili na ufahamu wa kutosa katika kuzitumia, akiendelea kukazia mfano wa wakili dhalimu alioutoa katika Luka 16:1-8 Kwamba pamoja na kuwa wakili yule alikuwa afukuzwe kazi, alikumbuka kuwa kuna maisha baaya ya kufukuzwa kazi na hivyo alikumbuka kujiandalia marafiki kwa mali yake ya udhalimu ilia je kunufaika baadaye, aidha matajiri wa dunia hii vilevile  wakati ule waliweza kutumia fedha kujipatia marafiki na hata kujiongezea umaarufu duniani na ilikuwa rahisi kukubalika kwa sababu ya uwezo mkubwa wa kifedha waliokua nao

Mfano hata leo kama utahitaji kugombea ubunge na vyeo vinginevyo vya kikampeni, utaweza kuona kwamba ni lazima uwe na fedha za kutosha kuweza kuongeza ushawishi kujipatia nafasi uitakayo wazo hili hili alilokuwa nalowakili dhalimu kuhusu kesho yake lingeweza vilevile kutumiwa na wanafunzi wa Yesu kuwa na ujuzi na hekima na akili ya kujitengenezea maisha ya baadaye kwa kuwekeza katika Mungu, tunaweza kutumia fedha mali na utajiri  kwa makusudi mema, tunaweza kuzitumia mali fedha  na utajiri wao (Kwa Mtazamo wa Kiaramu Mali ya Udhalimu) kwa lengo zuri la kuujenga ufalme wa Mungu, badala ya kutumia fedha na mali na utajiri wetu kujifurahisha, kwa choyo na ubinafsi, tunaweza kuitumia kujijengea jina kwa kuwekeza kwa Mungu na kuwatendea mema wengine jambo litakalotufanya tuwe matajiri katika kazi njema kwa msingi huo   Agizo hili la Kristo linaweza kutafasiriwa sambamba na,

1Timotheo 6:17-18 “Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha. Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo;”  

kwa hiyo kama hatutakuwa waaminifu kuitumia mali, fedha na utajiri huu wa duniani (Wa Kidhalimu) kwa Mungu wetu, Mungu naye hatatatutumia au kutuamini katika mambo Halisi ya kweli ya ufalme wa Mbinguni, huko tutakuwa na hazina isiyoharibika,  Kimsingi Yesu hakuwa anamaanisha kuwa na fedha ni jambo baya wala hakuwa anatia moyo kuwa watu wajitafutie fedha kwa nia mbaya au kwa njia zisizofaa, lakini kama waili yule muovu alikuwa na uwezo wa kufikiri kuhusu maswala yajayo kwanini matajiri wa kawaida wawe wachoyo  na kushindwa kuutumia utajiri wao ambao kimsingi utawanufaisha tu hapa duniani kisha wasahau kujiwekeza katika ufalme wa Mbinguni. Aidha tunaweza kuzitumia fedha zetu sio kwaajili ya kutafuta umaarufu lakini kuwasaidia wengine wenye uhitaji jambo ambalo pia linatupa thawabu Mbinguni, Mungu anapotumilikisha fedha mali na utajiri maana yake ametuamini kuwa tunaweza kutunza kwaajili ya wote na sio kwaajili yetu, hivuo kila Mkristo anapaswa kuwa mwaminifu katika kutumia rasilimali ambazo Mungu ametupa kwa faida ya ufalme wake!

“Luka 6:11 Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu (mali fedha na utajiri wa Duniani), ni nani atakayewapa amana mali ya kweli (ya ufalme wa Mungu, na umilele)”?

Jinsi ya kumtumikia Mungu na Mali Mst 13

Kimsingi Bwana wetu Yesu Kristo anauona mlango ni mdogo sana kwa wenye utajiri kuingia katika ufalme wa Mungu kwa sababu ya ubinafsi na choyo, Wakristo ni lazima waende mbele zaidi na kujifunza kumpa Mungu kipaumbele kikubwa zaidi na jamii,  Mungu anapokuwa ametubarikia wingi wa mali, fedha na utajiri vilevile anataka tuvutumie kwa utkufu wake na kumuabudu yeye 

Kutoka 10:8-11 “Musa na Haruni wakaletwa tena kwa Farao; naye akawaambia, Nendeni, mkamtumikie BWANA, Mungu wenu; lakini ni kina nani watakaokwenda? Musa akamjibu, Tutakwenda na vijana wetu na wazee wetu, na wana wetu, na binti zetu, tutakwenda na kondoo zetu na ng'ombe zetu; kwa kuwa inatupasa kumfanyia BWANA sikukuu. Lakini akawaambia, Ehe, BWANA na awe pamoja nanyi, kama nitakavyowapa ruhusa kwenda zenu pamoja na watoto wenu; angalieni, kwa kuwa pana uovu huko mbele yenu. Sivyo; endeni ninyi mlio watu wazima, mkamtumikie BWANA; kwa kuwa ndilo jambo mtakalo. Nao walifukuzwa usoni pa Farao.”

Mungu anapotuita Kumuabudu yeye na kumfanyia ibada hatuiti nusu  nusu anakuwa ametuita sisi  na kila tulichonacho, kama sisis ni watumishi wake basi kila tunachomiliki ni kwaajili ya utumishi ulioko mbele yetu, sisis ni mawakili tu ambao tumeaminiwa na Mungu,  na tunawezaje kuonyesha imani yetu kwa Mungu ni pamoja na kumuabudu Mungu na kila tunachokitaka! Tunaweza kuonyesha imani yetu kwa Kristo kwa kumtumikia pamoja na mali zetu, katika kila jambo lazima tumpe Mungu kipaumbele na kuonyesha ya kuwa ni yeye anayetawala na wala sio mali zinazotutawala, kutawaliwa na fedha kuliko kutawaliwa na Mungu ni kosa la kiufundi katika maswala ya kiroho, lazima Bwana awe juu ya kila kitu na kila kitu kitiishwe chini yake

Luka 16:13 “Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali

1Timotheo 6:10 “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.”

Unaona kila mmoja wetu anapaswa kujiuliza kuwa je ni

1.       Mungu anayemiliki kila kitu katika maisha yake?

2.       Je una moyo wa ukarimu au kuna hali ya choyo katika maisha yako?

3.       Je unatenga fungu la kumtolea Mungu katika maisha yako?

4.       Je unahofu ya kuwa utapungukiwa?

Mafarisayo ambao kwa kweli walikuwa wamekwisha zama katika mtego wa kupenda fedha walijikwaa kwa mafundisho ya Kirsto na kumpuuzia kwa sababu choyo kilikuwa ikmetawala nia zao na mioyo yao ili hali wakati huo huo wakijikinai kuwa ni watumishi wa Haki. ona

Luka 16:14 -15 “Basi Mafarisayo, ambao wenyewe ni wapenda fedha, waliyasikia hayo yote, wakamdhihaki. Akawaambia, Ninyi ndinyi mnaojidai haki mbele ya wanadamu, lakini Mungu awajua mioyo yenu; kwa kuwa lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu.”

Na Rev. Innocent Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!



Akikulazimisha maili moja nenda naye mbili !


Mathayo 5:39-41Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili.”


Utangulizi:

Mathayo 5:38-42 ni  mojawapo ya sehemu muhimu sana katika hotuba ya Yesu Kristo ya Mlimani ambapo Yesu anafundisha namna ya kuonyesha muitikio wakati mtu anapokudhalilisha au kukutesa, wakati kanuni za msingi wa agano la kale zilikuwa zinakazia usawa na malipo ya jino kwa jino au jicho kwa jicho zikimaanisha kwamba mtu akikufanyia kosa Fulani alipaswa kulipizwa sawasawa na ukubwa wa kosa hilo, yaani kimahakama mtu apewe adhabu inayolingana na makosa yake, Lakini Kristo anakuja na mtazamo tofauti mno wakati mtu anapotendewa mambo yasiyo ya haki, Yesu anawataka wakristo kuonyesha uvumilivu mkubwa sana bila kulipiza kisasi, badala yake kuwapenda maadui na  hata kuwatendea mema yaliyopitiliza!

Akikulazimisha maili moja nenda naye mbili !

Nyakati za Biblia wakati wa Yesu Kristo, Israel pamoja na mataifa mengine yalikuwa chini ya utawala wa kikoloni wa warumi, Wakoloni wa kirumi hata hivyo kuna wakati hawakuweza kuwatendea haki raia wa kawaida na hasa raia wa kiyahudi, waliwaburuza barabarani na pia kuwalazimisha kubeba mizigo mizito kama watumwa  hali hii ilipelekea wakati mwingine kuamsha gahadhabu na kuchochea watu kutaka kujilipizia kisasi, kitamaduni ilikuwa inawasukuma sana wayahudi kutaka kujilipizia kisasi na kujitangazia uhuru na utawala

Baadhi ya wale waliokuwa wakimfuata Yesu, kwa kuwa walitambua kuwa ndiye Masihi walikuwa na fikra kuwa ataushimamisha ufalme wa Mungu kwa kuuondoa utawala wa Warumi hata hivyo amri ya Yesu Kristo na fundisho lake lilikuwa kinyume na matarajio yao na liliwashangaza sana  yeye aliwafundisha kuwa wakubaliane na mateso yale hata ikiwezekana zaidi ya kile walichokuwa wakifanyiwa, Yesu alisisitiza kuwa wakilazimishwa maili moja na waende nao mbili.

Kimsingi Yesu hakuwa anafundisha wanafunzi wake kuwa dhaifu kama wengi wanavyoweza kudhani, badala yake Yesu alikuwa anamaanisha kuwa hakuna mtu dhaifu duniani, Yesu alikuwa anatufundisha kuwa watu Hodari na wavumilivu kiasi cha kuweza kuvumilia watu waovu na kuwapa maadui zaidi ya kile wanachokitarajia, Kristo hakutaka wakristo washindwe na ubaya badala yake alikuwa akitutaka tuushinde uovu kwa wema

Warumi 12:19-21 “Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.”  

Yesu anawataka wafuasi wake watoe zaidi ya kile ambacho ulimwengu unaweza kutoa, Yesu hataki tuwe dhaifu lakini anataka tuwe wavumilivu kwa wanadamu ambao ni wadhaifu sana, wakristo wanapaswa kuwa hodari na wenye nguvu kiasi cha kuzalisha mambo bora wakati wengine wakizalisha uovu, hatuwezi kuwa sawa na wana wa ibilisi, sisi ji lazima mtuwe wakamilifu kama baba yetu wa Mbinguni alivyo mkamilifu,  Ubaya wa watu waovu kamwe haupaswi kuwa sababu ya kuvunjika moyo kwa wakristo na badala yake lazima sisi tuzalishe jamno lililobora ili kuonyesha kuwa wao ni wapuuzi.

Maandiko yanamsifia mtu anayejitawala kuwa bora kuliko shujaa, mtu anayeweza kujizuia nafi yake asikasirike ni mwema sana kuliko hata mtu mwenye uwezo wa kuteka mji, Wakristo waliokomaa kiroho hawasukumwi kamwe na misukumo ya kihisia bali wanakuwa wenye nguvu ndani kwa kuonyesha kuwa wanaweza kujizuia hata pale mtu anapotaka wakasirike

Mithali 16:32 “Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.”

Mtu mwenye ukomavu wa hali ya juu ni yule ambaye anaweza kuwasamehe adui zake na kuwapenda, Daudi ni moja ya Mfano wa watu waliokuwa wanaweza kuushinda ubaya kwa wema hakuwahi kufurahia hata kufa kwa adui zake kabisa   

2Wafalme 19:4-6 “Mfalme akajifunika uso; na mfalme akalia kwa sauti kuu, Mwanangu Absalomu, Absalomu, mwanangu, mwanangu! Basi Yoabu akaingia nyumbani kwa mfalme, akasema, Wewe leo umefedhehesha nyuso za watumishi wako wote, waliokuokoa leo roho yako, na roho za wanao, na za binti zako, na roho za wakezo, na roho za masuria wako; kwa kuwa unawapenda wakuchukiao, na unawachukia wakupendao. Maana umetangaza leo ya kuwa wakuu na watumishi wako si kitu kwako; maana leo nimetambua hivi; kama Absalomu angaliishi, na sisi sote tungalikufa leo, ingalikuwa vyema machoni pako.”

Luka 6:27-30 “Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi. Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang'anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu. Mpe kila akuombaye, na akunyang'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie.”

Mitume wa Bwana adiha walisisitiza pia fundisho hili la bwana na kuwataka wakristo kutokuwa watu wa kulipa baya kwa baya, wala laumu kwa laumu na wanatakiwa kubariki hata watu wanaowafanyia  maovu kwa kufanya hivi inaashirikia ukomavu mkubwa na unaonyesha kuwa sisi kweli tumekuwa wanafunzi wa Yesu kweli kweli jambo hili linapaleka habari njema kwa maadui wa Ukristo na kuwafanya wamkubali Kristo!

1Petro 3:9 “Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.”

Hitimisho:

Aina hii ya muiikio ndio utakaosababisha watu wauone uzuri wa Mungu hata katika maisha ya wale wanaowashutumu, kuwaonea na kuwatesa, aidha hii itamfanya mtu muovu akome kuutumia uovu wake kukomoa wakristo, kwa hiyo mateso na nia ovu za watu wabaya hazitakuja zishinde nguvu ya Mungu na uwepo wa utendaji nwa Kristo katika maisha yetu siku zote za maisha yetu. Nabii Elisha aliwahi kuitumia njia hii na washamu wakaacha kuwafuatia Israel kwa muda mrefu ona

2 Wafalme 6:19-23 “Elisha akawaambia, Njia hii siyo, na mji huu sio, nifuateni mimi, nami nitawapeleka kwa mtu yule mnayemtafuta. Akawapeleka Samaria. Hata walipokwisha kuingia Samaria, Elisha akasema, Bwana wafumbue macho watu hawa, wapate kuona. Bwana akawafumbua macho wakaona; kumbe! Walikuwa katikati ya Samaria. Naye mfalme wa Israeli alipowaona, akamwambia Elisha, Ee baba yangu, niwapige? Niwapige? Akamjibu, Usiwapige; je! Ungetaka kuwapiga watu ambao umewatwaa mateka kwa upanga wako na uta wako? Weka chakula na maji mbele yao, wapate kula na kunywa, na kwenda kwa bwana wao. Basi akawaandalia chakula tele; nao walipokwisha kula na kunywa, akawaacha, wakaenda zao kwa bwana wao. Na vikosi vya Shamu havikuja tena katika nchi ya Israeli.

Na Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia

 

Mathayo 23:23-28. “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia. Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi. Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi.”



Utangulizi:

Katika Mathayo 23:13-36, kuna mahubiri makali ya maonyo kutoka kwa Yesu Kristo kuelekea kwa mafarisayo na viongozi wa dini waliokuweko katia nyakati hizo, Neno ole ni sawa na onyo la kulaani au kuonya juu ya hukumu kubwa ya Mungu kwa watu ambao maonyo hayo yanaelekezwa kwao,Krito alikemea vikali kwa maneno mazito hata wakati mwingine akitumia neno vipofu na wanafaiki, Sababu kubwa ni kuwa watu hawa walikuwa wakiwashawishi watu wafuate imani zao na matiokeo yake ilikuwa ni kama kuwapeleka Jehanamu, wakikazia katika mafundisho yao maswala yasiyo ya msingi wa Neno la Mungu na kuwaelekeza katika mapokeo ya kibinadamu zaidi, huku wakipuuzia msingi wa sharia ya Mungu ambayo ni ADILI, REHEMA na IMANI

Kwa maana nyingine Kristo alikasirishwa na Jinsi ambavyo viongozi wa kidini walishindwa kuwatafasiria watu kile ambacho sheria ya Mungu inakipa kipaumbele na badala yake wakaanza kukazia sharia za kidini zinazotokana na mapokeo, mikazo hiyo haikuwa dhambi hata hivyo lakini ilikuwa si Muhimu, tabia mbaya waliyokuwa nayo Mafarisayo ilikuwa ni mkazo wa utoaji wa zaka hususani kutoka katika mazao ambao kimsingi ulikuwa ni urithi wa watumishi wa Mungu yaani walawi kwa wakati ule

Hesabu 18:20-24 “ Kisha Bwana akamwambia Haruni, Wewe hutakuwa na urithi katika nchi yao, wala hutakuwa na fungu lo lote kati yao; mimi ni fungu lako, na urithi wako, katika wana wa Israeli. Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania.  Mwanzo wa sasa wana wa Israeli wasikaribie hema ya kukutania, wasije wakachukua dhambi, nao wakafa. Lakini Walawi watatumika utumishi wa hema ya kukutania, nao watauchukua uovu wao; hii itakuwa amri ya milele katika vizazi vyenu vyote, na kati ya wana wa Israeli hawatakuwa na urithi. Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote.”

Kumbukumbu la torati 14:24-29 “Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako; ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako; na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako; na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe. Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako; na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.”                       

Unaweza kuona Mafarisayo na viongozi wa dini walikazia sana kuhusiana na vifungu vinavyokazia kuhusu utoaji wa zaka na kwa kweli kutokana na uroho walikazia utoaji wa zaka mpaka ya mnanaa, Bizari na jira kwa faida zao, Mnanaa ni mmea wenye majani madogo madogo ya kijani kwa kiingereza unaitwa Mint mmea huu unatumika kutibu magonjwa mbalimbali kama Aleji, kuvimbiwa, maumivu ya tumbo na kutibu magonjwa mengine kama kisonono, bawasiri na maumivu katika njia ya mkojo, mmea huu ulitumika kama tiba kwa miaka elfu nyingi sana duniani,

Bizari kwa kiingereza Dill ni kiungo cha manjano BINZARI ambacho tutumika kuweka rangi ya mchuzi na kuifanya iwe wa manjano au mwekundu na shughuli nyinmginezo za kimapishi na ladha au harufu nzuri kwenye chakula pia hutumika kama tiba ya magonjwa

Jira kwa kiingereza cummin ni vijijani vyenye vitunda vidogo vidogo sana vya kijana ambavyo vikianikwa huwa na rangi ya kijivu hivi ni viungo ambavyo huchanganywa na viungo vingine na kuleta ladha maalumu katika kama pilau na mchuzi na kadhalika, jira ina uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali ikiwepo, kusaidia kupunguza uzito, kuondoa msongo wa mawazo, kuyeyusha mafuta hatarishi mwilini, kisukari, na magonjwa mengineyo. Kwa ujumla vitu hivi vilikuwa vinahusiana na UPONYAJI, UZURI NA UNONO. Mafarisayo walisisitiza sana utoaji wa zaka hata wa vimimea hivi vidogo vidogo kwa mkazo mkubwa sana kwa makusudi tu wakuu wa dini wanufaike na utamu wa vyakula vyao na afya nzuri, Yesu hakuhukumu utoaji wala utoaji wa zaka lakini kuna kitu nyuma ya mkazo wa viongozi wa dini ambacho Kristo alikuwa anakikemea huku akiwakemea kwa kuacha kusisitiza maswala ya msingi na ya muhimu

Mafarisayo waliacha kuweka mkazo katika maswala makubwa ya msingi ya kiroho ambayo yangekuwa na faida kubwa kwa watu kuliko yale ambayo yangekuwa na faida kubwa kwao  waliacha maswala ya ADILI – Maswala ya kuhukumu kwa haki linapokuja swala la Mtu Fulani amekosea, REHEMA – Kushindwa kuwahurumia watu waliokosea na wale wanaohitaji msaada wa kibinadamu au walio kwenye mateso, IMANI -  Biblia ya kiingereza inatumia neno FAITHFULNESS ambalo linahusiana na UAMINIFU

Kuchuja mbu na kumeza ngamia

Wakati mwingine unaweza kudhani kuwa shida hii ilikuwa ya mafarisayo pekee wakati wa Yesu Kristo la hasha hata sasa ziko tabia Fulani zinazoweza kukemewa katika mtindo kama huu wa Masihi, Leo hii pia wako watu wameacha mambo ya msingi na kukazia mambio ya siyio ya msingi, kwa mfano sio vipaya kuhubiri uponyaji na mafanikio kwa vile ni wazi kuwa watu wanahitaji mafanikio na uponyaji na hakuna jambo baya kama umasikini, lakini ni ukweli ulio wazi kuwa injili inahitaji balansi, lazima wahubiri wasisahau kuwa tunapaswa kuhubiri injili kamili, mara kadhaa unaweza kukuta wahubiri wansisitiza juu ya utoaji lakini sababu kubwa ni kwaajili ya mahitaji makubwa waliyo nayo,  na wakati mwingine kwaajili ya ubinafsi na kujinufaisha, tunaweza kuhubiri kuhusu uponyaji lakini tusisahahu kuwa watu wanapaswa pia kuishi maisha matakatifu na kukumbushwa kuhusu toba na kusamehewa dhambi na sio uponyaji pake yake

Zaburi 103:3 “Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,” unaona wakati tunasisitiza kuhusu Uponyaji ni lazima vile vile tukumbuke kusisitiza toba na msamaha wa dhambi, itajkuwa ni hasara kubwa sana kama mtu ataponywa magonjwa yake yote lakini hajawahi kuambia atubu dhambi au aishi maisha matakatifu, na sio sahihi vilevile kuhubiri mafanikio na afya njema bila kusahau kuwa afya halisi inapaswa kuanzia rohoni

3Yohana 1:3 “Mpenzi naomba ufanikiåe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo

lakini vilevile inaweza kuwa makosa sana kuwahukumu watu kutokana na muonekano wao, au hali yao ya kifedha au cheo chao na kuacha kuweka uthamani wa mtu katika mizani ya kiroho, aidha kumekuweko na upendeleo katika utoaji wa haki, wako watu kwa sababu ya utajiri wao wanaweza kupewa heshima Fulani na hata wakifanya dhambi wanaweza kuhifadhiwa lakini wewe ambaye huna kitu ukadhalilishwa

Yakobo 2:1-5 “Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu. Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu, je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu? Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?

 Unaona watu hawajali umuhimu thamani ya nasfi na roho ambayo ni moja bali wanaangalia muonekano, wako watu ambao wanaweza kuhukumu mambo pia kwa sababu tu wamesikia umbeya na uongo bila hata kujithibitishia uhalisia wa mambo,  Pamoja na mahitaji ya watu wenye njaa, wenye uhitaji lazima tuonyeshe rahema kwa watu kwa kuwasaidia kukutana na mahitaji yao. Mtu anaweza akaonekana anahudhuria ibada na kutii kila kinachoamuriwa kanisani lakini maisha yake binafsi yakawa na uchafu wa kila aina, je tunaishi vipi na waume, zetu, wake zetu, watoto wetu, na je akilini tunawaza nini?  Wako watu wanahukumu wengine lakini akilini mwao ni waongo,  wana hasira, wachonganishi wamejaa fitina majungu na uzushi, kutaka sifa na kujitwalia utukufu, Yesu anachokitaka ni tuwe wakamilifu pande zote hatupaswi kuchagua kipi cha kutii na kipi sio cha kutii

Mathayo 23:23-24 “Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia.”

Yesu anacho kitaka wetu ni kuwa pamoja na mambo mengine tusiache kukazia maswala ya muhimu na kuyapa kipaumbele, kama tunahubiri injili na kuichukia dhambi basi tuhakikishe kuwa tunapambana na kile kitu, ukikataza ulevi kataza na tamaa, ukikataza uzinzi kataza na hasira, haki haki, rehema rehema na adili ni adili, hatuwezi kuhubiri uaminifu katika eneo Fulani na wakati huo huo eneo lingine tukawa tumelilegezea, huko ni kuchuja mbu na kumeza ngamia, nusu utii ni sawa na kutokutii haya ni machukizo sawa na namna Mungu alivyochukizwa na Sauli alipomwambia aangamize kila kitu cha amaleki yeye akabakiza  nab ado akawa anasisitiza kuwa ametii

1Samuel 15:1-23Wakati huo Samweli akamwambia Sauli, Bwana alinipeleka nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na maneno ya Bwana. Bwana wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda. Ndipo Sauli akawaita watu, akawahesabu huko Telemu, askari waliopanda farasi mia mbili elfu, na watu wa Yuda kumi elfu. Sauli akaufikilia mji wa Amaleki, akauvizia bondeni. Sauli akawaambia Wakeni, Haya! Enendeni zenu, mkashuke ili kujitenga na Waamaleki, nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao; maana mliwatendea wana wa Israeli mema, walipopanda kutoka Misri. Basi hao Wakeni wakaondoka, wakajitenga na Waamaleki. Sauli akawapiga Waamaleki, toka Havila uendapo Shuri, unaokabili Misri. Akamkamata Agagi, mfalme wa Waamaleki, yu hai, akawaangamiza hao watu wote kwa upanga. Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa. Ndipo neno la Bwana likamjia Samweli, kusema, Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia Bwana usiku kucha. Samweli akaondoka asubuhi na mapema ili aonane na Sauli; Samweli akaambiwa ya kwamba, Sauli alifika Karmeli, na tazama, akajisimamishia ukumbusho, akageuka, akapita, akatelemkia Gilgali. Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na Bwana, nimeitimiza amri ya Bwana. Samweli akasema, Maana yake nini, basi, hiki kilio cha kondoo masikioni mwangu, na huu mlio wa ng'ombe ninaousikia? Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng'ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa. Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami nitakuambia neno aliloniambia Bwana usiku huu. Naye akamwambia, Haya, sema. Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha kabila za Israeli? Naye Bwana akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli. Kisha Bwana akakutuma safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hata watakapoangamia. Mbona, basi, hukuitii sauti ya Bwana, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana? Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya Bwana, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa. Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng'ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, huko Gilgali. Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.”

Ukiyajua hayo heri wewe ukiyatenda!

Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Jumanne, 8 Novemba 2022

Kufa afavyo Mpumbavu!


2Samuel 3:33-34Ndipo mfalme akamwomboleza Abneri, akasema, Ilimpasaje Abneri kufa afavyo mpumbavu? Mikono yako haikufungwa, Wala miguu yako haikutiwa pingu; Aangukavyo mtu mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka. Na watu wote wakaongeza kumlilia.” 



Utangulizi:

Abner alikuwa ni binamu na mkuu wa majeshi ya ulinzi wa Jeshi la Mfalme Sauli, Jina lake limejitokeza katika maandiko vilevile kama Abner mwana wa Ner jina lake maana yake baba yangu ni Ner  na neno Ner maana yake ni Mwanga au Nuru!, Mkuu huyu wa majeshi alitumika na Sauli na Jonathan na hata baada ya kifo chake alikuwa mwaminifu kwa Mtoto wa Sauli aliyeitwa Ishboshethi hivyo tunapata picha ya kuwa wakati wote wa vita vya Sauli na Daudi Abner ndiye aliyekuwa akiongoza mapambano hayo lakini kwa neema ya Mungu siku hadi siku Nyumba ya Sauli ilizidi kudhoofika dhidi ya Nyumba ya Daudi kama yanenavyo maandiko.

2Wafalme 3:1 “Basi kulikuwa na vita siku nyingi kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi; Daudi akaendelea akasitawi, lakini nyumba ya Sauli ikaendelea kudhoofika.”

Hata hivyo kutokana na kutambua mapenzi ya Mungu, Abner alitambua wazi kuwa Mungu alikuwa amekusudia Daudi awe mfalme tangu miaka mingi alipopakwa mafuta na Samuel Nabii, lakini kibishibishi upande wa Sauli walikuwa wanachelewesha au kushindana na makusudi ya Mungu, hatimaye Abner aliamua kuwa atasaidia kumkabidhi Daudi ufalme baada ya kugombea mwanamke kati yake na Ishboshethi mwana wa Sauli.

2Wafalme 3:6-9 “Ikawa, wakati vilipokuwapo vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi, Abneri akajipatia nguvu nyumbani kwa Sauli. Basi Sauli alikuwa na suria, jina lake akiitwa Rispa, binti Aya; Ishboshethi akamwuliza Abneri, Kwa nini umeingia kwa suria ya babangu? Basi Abneri akakasirika kwa maneno ya Ishboshethi, akasema, Je! Mimi ni kichwa cha mbwa, aliye wa Yuda? Hata leo hivi nawafanyia fadhili nyumba ya Sauli babako, na ndugu zake, na rafiki zake, nisikutie wewe mkononi mwa Daudi; nawe hata hivyo wanitia hatiani leo kwa mwanamke huyu. Mungu amfanyie Abneri vivyo, na kuzidi, nisipomtendea Daudi kama vile Bwana alivyomwapia;”

Kwa hiyo unaweza kupata picha kuwa kwa kiwango fulani kikubwa Abner alikuwa ni kikwazo kikubwa kwa mapenzi ya Mungu kwa Daudi kutimia akitetea upande wa Sauli na watoto wake na pia kumbe alijua mapenzi ya Mungu kuwa Mungu alimuapia Daudi Ufalme lakini kwa makusudi alikuwa akipingana na mapenzi ya Mungu na kuchelewesha kusudi la Mungu juu ya Daudi ashukuriwe Mungu kuwa makusudi yake hayawezi kuzuilika, Mungu aliutumia ugomvi wao na Ishbotheth kutimiza Mpango wake na Abner sasa alikuwa katika njia ya Mungu akijua wazi kuwa anatimiza mapenzi ya Mungu.

Abner na mapenzi ya Mungu.

Abner alifahamu kuwa kama amekosana na Ishbotheth mwana wa Sauli na kujipa nguvu yeye mwenyewe kwa vyovyote vile atakayepambana na Daudi angekuwa yeye, uso kwa uso, kwa ujumla Jemedari huyu alikuwa na tatizo la kiburi moyoni mwake maandiko yanaposema alijipatia nguvu katika nyumba ya Sauli maana yake alijiinua yeye mwenyewe

2Wafalme 3:6-7 “Ikawa, wakati vilipokuwapo vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi, Abneri akajipatia nguvu nyumbani kwa Sauli. Basi Sauli alikuwa na suria, jina lake akiitwa Rispa, binti Aya; Ishboshethi akamwuliza Abneri, Kwa nini umeingia kwa suria ya babangu?

Unaona akajipatia nguvu nyumbani mwa Sauli hii maana yake kibiblia alianza kujiinua alianza kuwa na kiburi, kuchukua mke au suria katika mila za kifalme kulikuwa hakuna tofauti na kujifanya mfalme au kutaka ufalme ona, 1Wafalme 2:13-23 “Ndipo Adonia mwana wa Hagithi akaja kwa Bath-sheba mamaye Sulemani. Naye akasema, Je! Umekuja kwa amani? Naye akajibu, Kwa amani. Tena akasema, Nina shauri ninalotaka kukuambia. Naye akamwambia, Sema. Basi akasema, Wajua ya kwamba ufalme ulikuwa wangu, na Israeli wote wakaniwekea nyuso zao ili nimiliki mimi; walakini sasa ufalme umegeuka kuwa wake ndugu yangu; kwa maana ulikuwa wake kutoka kwa Bwana. Basi sasa nina haja moja ninayokuomba, usinikataze hiyo. Naye akamwambia, Sema. Akasema, Nena, nakusihi, na Sulemani, mfalme, (kwa kuwa hawezi kukukataza neno), kwamba anioze Abishagi, Mshunami. Naye Bath-sheba akasema, Vema; nitasema na mfalme kwa ajili yako. Basi Bath-sheba akaingia kwa mfalme Sulemani, aseme naye kwa ajili ya Adonia. Naye mfalme akainuka kwenda kumlaki, akamwinamia, akaketi katika kiti chake cha enzi; kisha akaagiza awekewe kiti cha enzi mamaye mfalme; naye akaketi mkono wake wa kuume. Ndipo akasema, Haja moja ndogo nakuomba; usinikataze. Mfalme akamwambia, Omba, mama; kwa kuwa siwezi kukukataza neno. Naye akasema, Nataka Adonia, ndugu yako, aozwe Abishagi, Mshunami. Akajibu mfalme Sulemani akamwambia mamaye, Na mbona wamtakia Adonia Abishagi, Mshunami? Umtakie na ufalme pia; kwa kuwa yeye ni ndugu yangu mkubwa; naam, umtakie yeye, na Abiathari kuhani, na Yoabu mwana wa Seruya. Ndipo mfalme Sulemani akaapa kwa Bwana, akasema, Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, isipokuwa Adonia amenena neno hili juu ya uhai wake mwenyewe.” hivyo ili Daudi atawale ilikuwa lazima Abner ashughulikiwe, naye akijua yatakayompata baada ya kuasi nyumba ya Sauli sasa anakuja na mpango wa kukabidhi mamlaka ya kifalme kwa Daudi, lilikuwa wazo jema na mapenzi ya Mungu, lakini ni yeye ndiye aliyekuwa anachelewesha kusudi la Mungu, sasa anataka kurudisha mamlaka kwa Daudi.

2Wafalme 3:9-10 “Mungu amfanyie Abneri vivyo, na kuzidi, nisipomtendea Daudi kama vile Bwana alivyomwapia; kuupitisha ufalme toka nyumba ya Sauli, na kukisimamisha kiti cha Daudi juu ya Israeli, na juu ya Yuda, toka Dani mpaka Beer-sheba.”

Abner alikuwa mtu mwenye kujiamini kupita kawaida yeye alijifanya kuwa ni Mungu, pamoja na kuwa aliapa kwa Mungu lakini anapotumia neno KUUPITISHA UFALME TOKA NYUMBA YA SAULI NA KUKISIMAMISHA KITI CHA DAUDI JUU YA ISRAEL NA JUU YA YUDA hii ilikuwa ni kazi ambayo haifanyiki kibinadamu neno kupitisha Katika kiingereza linasomeka kama “To translate” ambalo katika kiebrania maana yake ni Abar likisomeka kama AW-BAR ambalo maana yake ni ni sawa na kutenga au kusababisha au kuweka wakfu au kuhamisha kimsingi hayo yanaweza kufanywa na Mungu tu ona Wakolosai 1:13 “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;”  unaweza kuona Lugha hiyo pia katika Waebrania 11:5 “Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.” Kwa hiyo kumamisha au kupitisha ni kumtoa mtu katika hali moja na kumpeleka katika hali nyingine hii ni kazi ya Mungu na sio ya Mwanadamu. Ni wazi kuwa kamanda huyu alikuwa na kiburi.

Abner vilevile alikuwa ni mtu hatia ya damu ya shujaa anayeitwa Asahel, Huyu alikuwa moja ya watu mashujaa aliyekuwa na mbio za kufukuzia maadui kama mbio za kulungu, katika mashujaa watatu waliotoka kwa Seruya waliojulikana kama wana wa Seruya Asahel alikuwa ni hodari lakini zaidi sana aliyekuwa na uwezo wa kukimbiza adui, Asahel alikuwa akimkimbiza Abner na kwaajili ya kujihami Abneri alimshihi sana aache kumfuatilia lakini Asahel alikaza na kwa sababu hiyo yeye alimuua ona

2Samuel 18-28 Na wana watatu wa Seruya walikuwako huko, Yoabu, na Abishai, na Asaheli; na Asaheli alikuwa mwepesi wa miguu kama kulungu. Naye Asaheli akamfuatia Abneri; na katika kwenda kwake hakugeuka kwenda mkono wa kuume wala mkono wa kushoto katika kumfuatia Abneri. Basi Abneri akatazama nyuma yake, akasema, Ni wewe, Asaheli? Akajibu, Ni mimi. Basi Abneri akamwambia, Geuka mkono wa kuume au mkono wa kushoto, ukamshike mmoja wa vijana, ukazitwae silaha zake. Lakini Asaheli hakukubali kugeuka na kuacha kumfuata. Abneri akamwambia Asaheli mara ya pili, Geuka, acha kunifuatia mimi; kwa nini nikupige hata chini? Hapo ningewezaje kuinua uso wangu mbele ya Yoabu, ndugu yako? Lakini akakataa kugeuka; kwa hiyo Abneri akampiga tumboni kwa ncha ya nyuma ya mkuki wake, ule mkuki ukamtoka kwa nyuma; naye akaanguka hapo, akafa papo hapo; ikawa, watu wote waliofika hapo, alipoanguka Asaheli na kufa, wakasimama. Ila Yoabu na Abishai wakamfuatia Abneri; na jua likachwa hapo walipoufikilia mlima wa Ama, uelekeao Gia, katika njia ya nyika ya Gibeoni. Nao wana wa Benyamini wakakusanyika pamoja nyuma ya Abneri, wakawa kikosi kimoja, wakasimama juu ya mlima. Ndipo huyo Abneri akamwita Yoabu, akasema, Je! Upanga uwale watu sikuzote? Je! Hujui ya kwamba utakuwa uchungu mwisho wake? Basi itakuwa hata lini usijewaamuru watu warudi na kuacha kuwafuatia ndugu zao? Naye Yoabu akasema, Aishivyo Mungu, usingalinena, basi asubuhi wangalikwenda zao, wasiwafuatie kila mtu ndugu yake. Basi Yoabu akapiga tarumbeta, na watu wote wakasimama, wasiwafuatie Israeli tena, wala hawakupigana tena.” Mtu aliyeua mtu mwingine alipaswa kusalimisha maisha yake katika mojawapo ya miji sita ya makimbilio ili mwenye kujilipiza kisasi kwaajili ya nduguye aije akamuua, Hata hivyo Abneri hakuweza kujali maelekezo hayo ya torati kwa vile alikuwa akijiamini kutokana na umahiri wake katika vita

Agano la Abner na Daudi.

Pamoja na madhaifu makubwa aliyokuwa nayo Abner, huyu pia alikuwa ni jemadari wa vita, alikuwa ni mzoefu wa vita shujaa na kamanda mwenye nguvu sana lakini pia alikuwa mpenda amani na mwangalifu mno, katika uwezo wa kujihami,  ulifika wakati akaona pia kuwa sasa Israel wanahitaji amani.

2Samuel 3:12-16 “Basi Abneri akatuma wajumbe kwa Daudi mahali alipokuwapo, akisema, Nchi hii ni ya nani? Fanya agano nami, na tazama, mkono wangu utakuwa pamoja nawe, ili kuwaleta Israeli wote kwako. Daudi akasema, Vema, nitafanya agano nawe, lakini nina sharti moja nitakalo kwako, nalo ni hili; Hutaniona uso wangu, isipokuwa uniletee Mikali, binti Sauli, hapo ujapo kuniona uso wangu. Basi Daudi akatuma wajumbe kwa Ishboshethi, mwana wa Sauli, kusema, Nipe mke wangu Mikali, niliyemposa kwa govi mia za Wafilisti. Basi Ishboshethi akatuma watu, akamnyang'anya Paltieli, mwana wa Laishi, mumewe, mwanamke huyo. Huyo mumewe akafuatana naye, akiendelea na kulia, akamfuata mpaka Bahurimu. Ndipo Abneri akamwambia, Haya, rudi. Naye akarudi.”

Kwa kuwa ilikuwa ni desturi ya Israel mtu anapofanya agano lazima wawekeana masharti Daudi aliitumia nafasi hiyo kumdai Abner ili aweze kumona uso wake amletee mke wa ujana wake aliyemuoa kwa gharama ya givi za wafilisti 100 lakini yeye aliua 200 ambaye alikuwa ni mikali Binti wa Sauli jambo ambalo Abner alilitii,  hii ilikuwa picha halisi ya kuwa Abner kweli alikuwa anataka amani Jambo hili lilimpendeza Daudi, hata hivyo Daudi hakuwa anahitaji sana Nguvu ya Abner kwani vijana wa Daudi walikuwa wameshaonyesha uwezo mkubwa sana kivita kumzidi yeye ona

2Samuel2:14-17 “Abneri akamwambia Yoabu, Tafadhali vijana hawa na waondoke na kucheza mbele yetu. Yoabu akasema, Haya! Na waondoke. Basi wakaondoka, wakaenda upande wa pili kwa hesabu yao watu kumi na wawili wa Benyamini, na wa Ishboshethi, mwana wa Sauli na watu kumi na wawili wa watumishi wa Daudi. Wakakamatana, kila mtu akimshika mwenziwe kichwa chake, na kutia upanga wake katika ubavu wa mwenzake; wakaanguka pamoja; hata mahali pale pakaitwa Helkath-hasurimu, napo ni katika Gibeoni. Vita vile vilikuwa vikali sana siku ile; naye Abneri akashindwa, na watu wa Israeli, mbele ya watumishi wa Daudi.”

Hata hivyo swala la kuwa na amani ya pamoja lilikuwa ni wazo zuri na mapenzi ya Mungu hivyo Daudi alilikubali na alimkubali Abneri kama mtu mwenye akili na mwema na aliyekubali kushindwa na kukubali mpango wa Mungu.    

Kufa afavyo Mpumbavu!

Abneri alikuja Hebron ili aweze kuonana na Daudi na kufanya patano naye 2 Samuel 3:20-23 “Basi Abneri akamwendea Daudi huko Hebroni, na watu ishirini pamoja naye. Daudi akamfanyia karamu Abneri, na watu wote waliokuwa pamoja naye. Kisha Abneri akamwambia Daudi, Nitaondoka, niende zangu; nami nitamkusanyia bwana wangu mfalme Israeli wote, ili wafanye agano nawe, ukamiliki juu ya wote inaowatamani roho yako. Basi Daudi akamruhusu Abneri; naye akaenda zake kwa amani. Na tazama, watumishi wa Daudi pamoja na Yoabu walitoka jeshini, wakaleta mateka mengi pamoja nao; lakini Abneri hakuwako Hebroni kwa Daudi; maana alikuwa amemruhusu, naye amekwisha kwenda zake kwa amani. Hata Yoabu, na jeshi lote waliokuwa pamoja naye, walipofika, watu wakamwambia Yoabu, wakisema, Abneri, mwana wa Neri, alikuja kwa mfalme, naye amemruhusu, naye amekwenda zake kwa amani.”

Daudi aliamini kuwa yalikuwa ni mapatano ya kweli na kuwa Abneri sasa anakwenda kuwakusanya watu kwaajili ya Daudi ili wafanye patano naye na kumfanya mfalme kwa njia ya amani, Hata hivyo Kamanda mkuu wa majeshi ya Daudi alikuwa hayuko wakati hilo likifanyika na kwa medani za kivita Yoabu hakuamini kuwa Abneri alikuwa na nia ya dhati ya kufanya hivyo yeye alikumbuka kuwa huyu ndiye alikuwa mpinzani mkubwa wa kuzuia kusudi la Mungu na iweje leo aweze kuwa mwema aidha Yoabu alikuwa na ufahamu kuwa Abneri pia alikuwa na kisasi cha damu ya kumuua Asaheli Ndugu yake, Yoabu alisikitika kuwa ni kwanini Abneri amekuja na Daudi anamuachia aende zake kwa amani inawezekanaje mtu mwenye nia ovu kesho akawa na nia njema? Hivyo Yoabu aliagiza kuwa Abneri arudi akidhani ya kuwa ameitwa tena na Daudi kumbe Yoabu alitaka kujilipizia kisasi kwaajili ya Ndugu yake ona

2Samuel 3:24-27 “Basi Yoabu akamwendea mfalme, akasema, Umefanyaje? Tazama, Abneri amekuja kwako; mbona umemruhusu, naye amekwisha kwenda zake?  Wewe wamjua Abneri, mwana wa Neri, ya kuwa alikuja ili kukudanganya, apate kujua kutoka kwako, na kuingia kwako, akajue yote uyatendayo. Naye Yoabu alipotoka kwa Daudi, akapeleka wajumbe kumfuata Abneri, wakamrudisha kutoka kisima cha Sira; lakini Daudi alikuwa hana habari. Basi Abneri alipokuwa amerudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando hata katikati ya lango, ili aseme naye kwa faragha; akampiga mkuki wa tumbo huko, hata akafa; kwa ajili ya damu ya Asaheli, ndugu yake.”

Tukio hili lilimsikitisha sana Daudi, kwani lingeweza kuhesabika ya kuwa amechukua ufalme kwa upanga, hata hivyo Daudi alifahamu kuwa Abneri hakuwa na nia ya uovu, hivyo alilaani vikali tukio la Yoabu. Na kumlaani Yoabu pamona na nyumba yake kwa kumuua mtu ambaye alikuwa anataka amani, Daudi aliitisha mbiu ya maombolezo lilikuwa ni tukio la kusikitisha sana Hata hivyo katika maombolezo hayo Daudi hakumlaumu yeyote bali alimlaumu Abneri mwenyewe kwa kufa kipumbavu ona

2Samuel 3:28-34 “Hata baadaye Daudi aliposikia, akasema, Mimi na ufalme wangu hatuna hatia milele mbele za Bwana, kwa sababu ya damu ya Abneri, mwana wa Neri; na imwangukie Yoabu kichwani pake, na nyumba yote ya babaye, tena hiyo nyumba ya Yoabu isikose kuwa na mtu mwenye kutoka damu, au aliye na ukoma, au mwenye kutegemea fimbo, au mwenye kuanguka kwa upanga au mwenye kuhitaji chakula. Basi Yoabu, na Abishai nduguye, walimwua Abneri, kwa sababu yeye alimwua ndugu yao Asaheli katika vita huko Gibeoni. Kisha Daudi alimwambia Yoabu, na watu wote waliokuwa pamoja naye, Rarueni nguo zenu, mkajivike nguo za magunia, mkamlilie Abneri. Naye mfalme Daudi akaifuata jeneza. Wakamzika Abneri katika Hebroni; naye mfalme akapaza sauti yake, akalia kaburini kwa Abneri, nao watu wote wakalia. Ndipo mfalme akamwomboleza Abneri, akasema, Ilimpasaje Abneri kufa afavyo mpumbavu? Mikono yako haikufungwa, Wala miguu yako haikutiwa pingu; Aangukavyo mtu mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka. Na watu wote wakaongeza kumlilia.”

Kwa nini Daudi amsikitikie Abneri kuwa amekufa kipumbavu?  Hii ni kwa sababu Abneri aliuawa pembeni kidogo tu ya lango la mji wa Hebroni, Mji wa  Hebroni ulikuwa ni mji wa makimbilio, miji ya makimbilio ilikuwa ni miji maalumu iliyotengwa kwaajili ya kutunza uhai wa mtu aliyeua kwa bahati mbaya, Abneri alikuwa amemuua Asaheli hivyo ilikuwa rahisi kwa mtu mwenye kutaka kisasi cha damu ya ndugu yake kumuua na mahali sahihi na salama ni kwenye moja ya miji ya makimbilio na Hebron ulikuwa ni mojawapo ya miji hiyo, hii ni miji ambayo muuaji angekimbilia humo angekula angevaa na kuishi salama miji hii iliwekwa na Mungu kwa sababu hiyo!

Hesabu 35:9-16 “Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani, Ndipo mtajiwekea miji iwe miji ya makimbilio kwa ajili yenu; ili kwamba mwenye kumwua mtu, pasipo kukusudia kumwua, apate kukimbilia huko. Na hiyo miji itakuwa kwenu kuwa makimbilio, kumkimbia mwenye kutwaa kisasi, ili asiuawe mwenye kumwua mtu, hata atakaposimama mbele ya mkutano ahukumiwe. Na hiyo miji mtakayowapa itakuwa kwenu ni miji sita ya makimbilio. Mtawapa miji mitatu ng'ambo ya pili ya Yordani, na miji mitatu mtawapa katika nchi ya Kanaani; miji hiyo itakuwa ni miji ya makimbilio. Miji hiyo sita itakuwa miji ya makimbilio kwa ajili ya wana wa Israeli, na kwa ajili ya mgeni, na kwa ajili ya huyo aketiye kati yao hali ya ugeni; ili kila amwuaye mtu, naye hakukusudia kumwua, apate kukimbilia huko. Lakini kama alimpiga kwa chombo cha chuma, akafa, ni mwuaji huyo; mwuaji hakika yake atauawa.”

·         Ni miji iliyowekwa na Mungu kwaajili ya usalama wa kila mtu.

·         Ni miji iliyowekwa na Mungu kwaajili ya kupate neema ya kutokuuawa

·         Ni miji iliyowekwa na Mungu ikiwa na mamlaka ya kuokoa

·         Ni miji iliyowekwa na Mungu kwa makusudi ya kutunza uhai

·         Ni miji Iliyokuwa maarufu na iliyojulikana sana na kila mtu aliijua

·         Ni miji iliyowekwa na Mungu kutoa mahitaji ya kutosha kwa kila anayekimbilia

·         Ni miji iliyokuwa imeandaliwa kwa maelekezo ya Mungu

·         Ni miji ambayo njia zake hazikufungwa

·         Miji hii ilikuwa sita tu katika nchi nzima ya Israel

 

1.       Kadesh – maana yake Haki

2.       Shekemu – mabega maana yake nguvu za Mungu

3.       Hebron -  maana yake Ushirika

4.       Bezeri – maana yake Ngome

5.       Ramoth – maana yake juu

6.       Na Golan – Maana yake Furaha

Kwa hiyo ilihitajika hatua moja tu kujikinga ndani ya mji wa Hebron, kwa mtu aliyekuwa shujaa, aliyepigana vita vingi sana, jemadari, anakujaje kufa wakati wa amani tena hatua chache tu kutoka lango la mji unaoweza kuokoa, tena akiwa na silaha zake, tena akiwa hajatiwa pingu, tena akiwa hajafungwa miguu wala mikono, tena akiwa hajachukua tahadhari ya aina yoyote,  Komandoo anawezaje kufa kirahisi namna ile, kimsingi yako mambo ambayo yako katika uwezo wetu ambayo tulitakiwa kuchukua hatua moja tu na hiyo ingetuweka mahali salama, Mungu ametupa Mwokozi, ametupa Yesu Kristo aliye haki yetu, aliye na nguvu za kiungu za kutusaidia ambaye anahitaji ushirika na kila mtu, ambaye ni ngome imara, ambaye yuko mkono wa kuume wa Mungu mbinguni ambaye ni furaha yetu, yuko tayari kutoa neema kwa kila mtu, yuko tayari kuokoa, yuko tayari kutuhifadhi na kutunza uhai wetu, anatoa kila kitu ni msaada ulio karibu, yuko tayari kumsaidia kila mtu hata bila kujali umefanya dhambi kiasi gani yuko tayari kusamehe na kukuhifadhi ni kifo cha kujitakia kufa bila kumpokea Yesu, ni aibu kukaa karibu na injili na kushindwa kuchukua hatua moja tu itakayostawisha usalama wako milele, ndani ya mji yuko mfalme ambaye anataka amani na wewe anakuamini hata kama watu hawakuamini, iweje leo ushindwe kuchukua hatua, ndugu yangu ni aibu ni kufa kipumbavu kama tutashindwa kumtumia Yesu aliyetupa kila kitu katika maisha yetu, ni hatua moja tu ya maombi, ni hatua moja tu ya kufunga, ni hatua moja tu ya kukumbuka kuwa liko lango la Hebron ni kuingia tu hakuna wa kukuzuia hupaswi kufa kipumbavu!  Na huwezi kuwa salama nje ya mji wa makimbilio! Kamanda mwenye akili na mwenye kujua mapenzi ya Mungu na mtu ambaye aklikuwa na nguvu na mzoezu wa vita ilikuwaje akafa kipumbavu, leo hii yako magonjwa mengine kama yakituua ni kwa sababu tumejitakia, maandiko yanasema kila atakayeliitia jina la Bwana ataokoka, tena yanasema nimekukimbilia wewe bwana nisiabike milele, mtu mweye akili na hekima kama wewe huwezi kuangamia ilihali unajua ya kuwa Yesu ni kimbilio na msaada wetu, heri leo kama utayatoa maisha yako kwake na kukubali msaada mkubwa utokao kwake !

Na Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima!

Heri wenye Upole !


Mathayo 5:1-5 “Naye alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia; akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema, Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.”


Utangulizi.

Nimekuwa kiongozi na Mchunjaji kwa Muda mrefu sana nimemtumikia Mungu kwa karibu robo tatu ya maisha yangu yote sasa, nimekutana na changamoto nyingi na za aijna mbalimbali, Pia nimewahi kupigana vita za aina mbalimbali za kiroho na naweza kukiri wazi kuwa hakuna vita nimewahi kushindwa kwa sababu wakati wote nilipopigana nalimtafuta Bwana ili awe upande wangu kwanza kwa hiyo ushindi wangu umetokana na Bwana mwenyewe kunipigania!, Moja ya changamoto kubwa kutoka kwa watu wanaonipiga vita katika uongozi wangu ni pamoja na kunishutumu kuwa mimi sifai kwa sababu ni MPOLE sikuhuzunika lakini hili lilinipa kutafakari kwani Upole ni sifa mbaya kwa mwanadamu? Au ni sifa Njema? Hili lilinifanya nianze kurejea katika maandiko na kuanza kujifunza kwa kina na mapana na marefu ili nipate kujua kuhusiana na UPOLE. Viongozi wakubwa sana katika maandiko wanaelezwa kuwa walikuwa wapole akiwemo Musa ona katika Hesabu 12:3 “Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.” Unaona lakini sio hivyo tu Yesu akitoa mwaliko wa watu wenye kuelemewa na changamoto mbalimbali anajitaja mwenyewe kuwa ni mpole na mnyenyekevu wa Moyo unaweza kuona katika Mathayo 11:28-29 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; Upole ni nini hasa je ni sababu ya kulaumiwa? Ni sifa mbaya? Ama ni sifa njema? Hili swala litupa nafasi ya kutafakari kwa kina na mapana na marefu katika somo hili katika jina la Yesu Kristo amen!

Maana ya Upole!

Katika hutuba maarufu sana ya Yesu Kristo inayojulikana kama Hutuba ya Mlimani, Yesu alifundisha pamoja na mafundisho mengine mafundisho ya HERI kama nane hivi ambazo kwa kiingereza zinaitwa Beatitudes ambalo maana yake ni “Supreme Blessedness” yaani mtu aliyebarikiwa sana sasa katika moja ya sifa hizo za watu waliobarikiwa sana mojawapo ni UPOLE kwa hiyo Mathayo 5:5 “Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.” Maana yake wamebarikiwa sana wenye upole maana hao watairithi nchi kwa hiyo UPOLE ni Baraka UPOLE ni neema ya Mungu ya ngazi ya juu sana, lakini ni lazima nan i muhimu kuelewa maana na neno hilo UPOLE

Neno upole linalotumika katika Kiswahili kwenye Biblia ya kiingereza linasomeka kama MEEK ambalo kwa ujumla linabeba maana tajiri sana ambazo kimsingi zinaweza kukomba matunda yote ya roho yanayotajwa katika maandiko MEEK - MILD, SUBMISSIVE, MODERATE, QUITE, GENTLE, LONG-SUFFERING, PATIENT. Maneno hayo yote yanayozingumzia upole kama MEEK katika unyambulisho wake yanatupa picha pana sana kuwa mtu mwenye upole kwa vyovyote vile ni mtu mkamilivu na momavu na katika maswala ya kiroho ni mtu wa ngazi ya juu sana kwani ameweza kubeba matunda mengi ya rohoni ona maana hizo kwanza 

MILD – MTARATIBU, SUBMISSIVE – MTIIFU, MNYENYEKEVU, MODERATE – MTU WA WASTANI (KIASI), ULINGANIFU USAWA, QUITE MKAMILIFU, GENTLE – MUUNGWANA, LONG-SUFFERING – MVUMILIFU, ASIYEKASIRIKA KWA HARAKA, PATIENCE – ALIYE NA SUBIRA.

Unaona kwa hiyo tunaposoma katika kitabu cha Wagalatia 5:22-23 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

Aina hii ya upole Yakobo aliita Upole wa hekima Yakobo 3: 13 “N'nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima”.

Aidha neno hili katika Biblia ya kiyunani linatumika kama neno PRAUS au PRAEIS ambalo tafasiri yake ni MILD  ikimaanisha mtu mwenye uwezo wa kujishusha kwa Mungu na wanadamu, au mtu mwenye uwezo wa kutumia nguvu na mamlaka lakini akawa na subira kwa faida ya wengine, Kimsingi hii ilikuwa sifa kubwa sana ya viongozi wa kibiblia na hata mfalme Daudi alikuwa miongoni mwa watu wa namna  hata alipotafuta kuuawa na Sauli aliyekuwa anamchukia sana yeye hakufanya haraka kumdhuru waola kujitakia kisasi hata pale ambapo Mungu alimwambia kufanya hivyo yeye alisubiri wakati muafaka wa Mungu hii ona

Zaburi 37:10-13 “Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo. Bali wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani. Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki, Na kumsagia meno yake. Bwana atamcheka, Maana ameona kwamba siku yake inakuja.”

Unaona kwa msingi huo ni vema ikaeleweka wazi kuwa Upole sio udhaifu bali Nguvu za Mtu mwenye uwezo  chini ya udhibiti wa Nguvu za Mungu, kwa hiyo mtu Mpole ni mtu anayeachia mambo chini ya udhibiti wa Mungu, ili Mungu mwenyewe achukue hatua za haki, ni mtu ambaye hajifikiri kuwa bora nje ya neema ya Mungu, upole ni hali ya kufikiri kuwa nguvu zetu na mamlaka yetu ina mipaka ya kufikiri katika Mungu kwa nia njema kuliko kuitikia haraka kwa hasira za kibinadamu Yakobo 1:20 “kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendi haki ya Mungu.” Mtu mwenye upole hutembea katika neema ya Mungu na hanaga mpango wa kunia makuu kuliko impasavyo kunia.

Warumi 12:3 “Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.”

Heri wenye upole!

Maana yake kuna amebarikiwa sana Mtu mwenye upole hii maana yake ni kuwa kuna faida kubwa sana za upole kama ifuata vyo:-

ü  Watu wenye upole ni watu waliobarikiwa kwa kiwango kikubwa Mathayo 5:5 “Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.” Hii maana yake ni nini maana yake ni kuwa na uhusiano na Muumba wa mbingu na Nchi, urithi mtu huupata kutokwa kwa yule eliyemzaa au aliyekuandikisha uupate kwa sababu ya wema wake mtu akiwa mpole maana yake anafanana na Mungu ni mwana wa Mungu hivyo anastahili urithi, Ni Mungu ndiye aliyeumba mbingu nan chi na hivyo kuwa mwanae kwa sababu ya upole kwa msingi huo lazima tutarajie Baraka za Mungu hata pale atakapoiumba mbingu mpya nan chi mpya Mungu atawarithisha watoto wake

 

ü  Watu wenye upole hutetewa na Mungu Hesabu 12:1-9 “Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi. Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao. Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi. Bwana akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje. Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili. Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, Bwana, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa? Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake.”

 

ü  Watu wenye upole hudumu muda mrefu katika nafasi zao na katika maisha Zaburi 37:10-13 “Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo. Bali wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani. Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki, Na kumsagia meno yake. Bwana atamcheka, Maana ameona kwamba siku yake inakuja.” Unaona kama unataka kudumu Muda mrefu uwe mwenye haki, kama watu wapole kuna stori moja ya kuchekesha kuhusu Meno na Ulimi, siku moja ulimi ulimwambia Mungu kuwa tafadhali umeniweka mimi katika wito wangu pamoja na meno na meno ni mgumu kuliko mimi kwa hiyo mara kwa mara katika kutimiza wajibu wetu meno amekuwa akinumiza na kuniacha na majeraha nikipona tena baada ya Muda meno hufanya hivyo hivyo ndipo Mungu akamjibu meno kazi yenu ni ya muda tu lakini wewe ulimi ni wa muda mrefu zaidi kuliko meno hivyo ni lazima ujifunze kuvumilia, baada ya miaka 70 au 80 hivi ya maisha yenu uje unipe majibu, baada ya muda huo kupita kumbe meno mengi yalioza na kung’oka lakini ulimi ulibaki, ni wazi kabisa kama maandiko yasemavyo aggressive people shall not live longer but Mild people will live more than normal ,  watu wakali hawadumu lakini watu wapole hudumu, in the workplace the arrogant and powerful seems to win but in the end they  lose alisema mtu mmoja kazini watu jeusi na wanaojiinua huonekana kama washindi lakini mwishoni wanyenyekevu ndio wanaoshinda, Ni changamoto kubwa sana kuachia mamlaka zetu na nguvu zetu katika mikono ya Mungu na kujinyenyekesha, tunaweza kuona raja kwa kitambo kutumia mamlaka zetu, kufukuza watu, kumarisha watu lakini ni ukweli ulio wazi kuwa hatima yake ni huzuni, hawafanikiwi katika lolote watu jeuri hawana marafiki wala hata wakipata fedha hawatosheki, wanaweza kudhani kuwa wanaumiliki ulimwengu lakini ni ukweli kuwa ulimwengu unawamiliki, Mwanamke na mwanaume wanaojikweza na kutaka kuonyesha nguvu zao huishia katika aibu na upweke hakuna mtu anaweza kuwa na urafiki na mtu jeuri!, wanawake huvutiwa sana na mwanaume mpole. Mwaname mkali hawezi kufaidi lolote hata katika ndoa yake! Mithali 22:24-25 “Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego.”

 

ü  Upole unakaribisha uwepo wa Mungu Isaya 66:1-2 “Bwana asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzikia ni mahali gani? Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.” Uwepo wa Mungu unakaa na watu wanyenyekevu wanyonge na wapole bila upole nafsi ya mwanadamu inakuwa katika mgogoro wa ndani, inasababisha hasira, kuchanganyikiwa, uchungu, na kukosa utulivu,  Upole unaweka mambo sawa na kupunguza mawimbi, unaleta utaratibu wakati wa machafuko unaponya nafsi na kutiisha mawimbi, Lazima mwanadamu akumbuke kuwa yeye ni mavumbi, ukikumbuka kuwa wewe ni udongo itakusaidia, Upole unaleta furaha na amani ya kweli, kama Mungu akiwa na ghadhabu na hasira kama tulizonazo sisi kwa wengine tungekuwa wapi leo? Watu wengine hata wakisikia masengenyo tu  mahali wanakurupuka na kufanya maamuzi hata bila kufanya uchunguzi wa kina na wa kutosha  je Mungu anekuwa mwepesi wa hasira kama wewe na mimi ingekuwaje ?

 

ü  Upole ni alama ya ukomavu wa kiroho Wagalatia 5:22-23 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.” Hakuna jambo linachosha duniani kama kuchunga wakristo wa Mwilini yaani wakristo ambao hawajakomaa kiroho au waliodumaa, Paulo mtume alisikitishwa sana na Kanisa lililodumaa na la wakristo wa mwilini kwani jamii hii ya wakristo wana taabu sana kuliko hata wapagani kutokana na kufarakana na kugombana na kufanya mambo ya ajabu yanayotukanisha ukristo 1Wakorintho 3:1-3 “Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?  unaona watu waliokomaa kiroho hawana muda wa majungu, fitina na husuda na maswala mengine, UPOLE ni alama muhimu sana kwa mtu aliyekomaa kiroho, lakini mtu wa tabia ya mwilini asiyekomaa kiroho hawezi kuwa na utulivu, kwa sababu hana matunda ya rohoni!

 

Hitimisho:

Ni mmuhimu kuelewa kuwa tunaweza kumuomba Mungu atupe upole kama jinsi ambavyo tunaomba Mambo mengine Yakobo 1:5 “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.” Ingawa Yakobo hapo  anaelezea swala la kuomba Hekima ni muhimu pia kujua kuwa Upole ni Hekima kwa hiyo tunapoomba Hekima tunaweza kupokea na upokle ndani yake hekima ya kiungu ikoje? Yakobo 3:17-18 “Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.” Kumbe tunaweza kuiomba Hekima hii iliyojaaa amani, rehema, matendo mema na iko tayari kusikiliza kwa hiyo ni lazima tumuombe Mungu atupe upole. Martin Luther King Alipingana na ubaguzi uliokuwepo Marekani, alitaka watu wote wahesabike kuwa sana alifanya maandamano ya amani hakuwahi kufanya vurugu wala kuruhusu wafuasi wake kufanya fujo akitumia falsafa ya Mahatma Ghandi ya non-violence resistance, kupinga maswala yasiyo haki bila kumwaga Damu, hii maana yake ni kuwa alikuwa Mpole Bwana na ampe neema kila mmoja wetu kuwa mpole katika jina la Yesu Kristo, kwa hiyo ieleweke wazi kuwa Upole sio udhaifu upole ni sifa kubwa na ya kipekee sana katika uhusiano wetu na Mungu, hivyo wale wanaonishutumu kuwa mimi ni Mpole sasa nimewaelewa vema asanteni!

 

Na Rev. Innocent Samuel Kamote

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima