Mathayo
5:8 “Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu”
Injili
maalumu kwa watoto: “Waacheni watoto wadogo waje kwangu msiwazuie maana watoto
kama hawa ufalme wa Mungu ni wao”
Siku
moja katikati ya umati mkubwa sana wa watu kijana mmoja alisimama na akapiga
kelele akisema Jamani niangalieni mimi kwakweli nina moyo Mzuri kuliko watu
wote Duniani
Watu
wote walishituka na kumwangalia na kweli walishangaa kuona kwamba ana moyo
mzuri sana na ulikuwa mkamilifu katika umbile lake na haukuwa na mikwaruzo ya
aina yoyote, wote walishangazwa na uzuri wa moyo wake na walimsifu sana.
Hata
hivyo baada ya muda kidogo mzee mmoja alisimama na kumwambia kijana Hapana
mwanangu mimi nina moyo safi na mzuri zaidi kuliko wa kwako na nina moyo mzuri
zaidi kuliko wote duniani
Kijana
akamwambia nionyeshe moyo wako! Tuuone
Mzee
yule alionyesha Moyo wake, kwa kweli ulikuwa mbaya hauna sura nzuri una
majeraha na makovu makubwa ulikuwa umeharibika kiasi ambacho hata ile sura ya
moyo haikueleweka vizuri, ulikuwa kama vipande vipande vilivyoungwa.
Kijana
alimcheka sana na kumwambia Babu yangu umechanganyikiwa angalia moyo wangu
jinsi ulivyo mzuri kweli unaweza kufananisha na wako? Moyo wangu hauna hata
mkwaruzo ni mkamilifu katika kila eneo, unaweza kulinganisha na wa kwako kweli?
Una majeraha mengi umeungwaungwa umepoteza sura yake kabisa unawezaje kusema
kuwa una moyo mzuri kuliko wote Duniani?
Mwanangu
moyo wangu ni mzuri kuliko wa kwako alisema mzee yule, umeona majeraha? Umeona makovu,
umeona ulivyoungwaungwa?umeona ulivyopoteza sura? Nilinyofoa nyofoa moyo wangu
kwa kuwasaidia wengine, nilionyesha matendo ya huruma na upendo kwa watu
mbalimbali, lakini wengine hawakunirudishia, niliwatendea watu mema lakini
wengine walinirudishia mabaya, kwa hiyo nilitafuta vipande vya nyama nyingine
na kuziba sehemu za moyo wangu nilizowapa wengine,
Kijana
alishangaa!
Nisikilize
kijana wangu moyo wangu ni mzuri kama wa kwako tu unaona makovu haya? Kila kovu
linawakilisha sehemu ya moyo wangu nilioutoa kwa wengine, wakati mwingine
nilitoa kipande cha moyo kilichokuwa kikubwa zaidi, lakini sikurudishiwa! Kwa sababu
niliowapenda wengine walinilipa mabaya, wengine hawakunirudishia, wengine
waliuumiza moyo wangu zaidi wengine waliuchoma kwa mkuki na kuufanyia moyo
wangu kila walichokitaka,Sehemu nyingine nilitoa moyo wangu wote na
wakanirudishia kidogo au wasirudishe kabisa, sehemu nyingine niliwakopesha
sehemu ya moyo wangu hawakurudisha aidha wengine niliwapa wakauchezea,
nililazimika kuachilia kusamehe na kusahau na kuushona moyo wangu na
kuuungauunga na kuutibu ndio maana moyo wangu una majeraha na makovu makubwa,
na hauna sura nzuri ya kupendeza kama wako, Moyo wako wewe unaonekana kuwa
mzuri kwa sababu hujawahi kutoa hata kipande ukawapa wengine je hili sio kweli?
Kijana
alitulia kimyaa na akaishiwa maneno, alianza kutokwa na machozi, alimkumbatia
mzee yule na kuuchana moyo wake na kumpa mzee yule kipande.
ISamuel 16:7
“Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake,
wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama
binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana
huutazama moyo.”
Watu
wengi sana huangalia watu kwa umbile la nje na kuwasifu watu kwa umbile la nje lakini
Mungu huangalia moyo, umeutumiaje moyo wako kwa wengine moyo wako umejaa nini utu
wa mtu utapimwa kulingana na kile anachokitoa kutoka moyoni mwake je wewe
unatoa nini kwa watu Mungu huitazama mioyo Marko
7: 15-23 “Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho
kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo
unajisi yule mtu.Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie.] Hata alipoingia
nyumbani, ameuacha mkutano, wanafunzi wake wakamwuliza habari za ule mfano. Akawaambia,
Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu,
kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; kwa sababu hakimwingii moyoni, ila
tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula
vyote. Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya
mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa
mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.Haya yote
yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.”
Na mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni