Mstari wa Msingi: Yohana 15:13 “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake”
Injli Maalumu kwa Watoto. Waacheni watoto wadogo waje kwangu msiwazuie kwa maana watoto kama hawa Ufalme wa Mungu ni wao!
Sungura mmoja mcheshi sana aliishi msituni, kutokana na ucheshi wake
aliweza kujipatia marafiki wengi sana wenye nguvu na maarufu sana
aliwapenda na kujivunia sana Marafiki zake
Siku moja sungura
Mcheshi alikumbana na kundi la mbwa mwitu wakali ambao walikusudia
kumla, Sungura mcheshi aliogopa sana na alikimbilia kwa moja ya marafiki
zake kwa kusudi la kutafuta msaada, haraka sana alikimbilia kwa swala
dume rafki yake wa karibu na kumwambia tafadhali rafiki yangu mpendwa
nisaidie kuna kundi la mbwa mwitu wakali wamekudia kunila nyama, najua
unaweza kuwafukuzia mbali kupitia pembe zako ndefu ulizo nazo.
Swala alijibu na kusema ni kweli nina pembe ndefu na ninaweza
kuwashambulia mbwa mwitu kwa pembe zangu lakini nina shughuli nyingi
sana tafadhali mwambie Dubu akusaidie.
Sungura mcheshi
alikimbilia kwa Dubu na kumwambia Tafadhali rafiki wewe una nguvu za
kutosha niokoe kutoka kwa mbwa mwitu hawa wakali tafadhali, wafukuze
tafadhali alimuomba Dubu
Dubu alimjibu, pole sana rafiki yangu
nina njaa na nimechoka sana nahitaji kutafuta namna ya kula tafadhali
muombe tumbili akusaidie.
Sungura mcheshi alimuendea tumbili, tembo, na nyati na rafiki zake wengine lakini hakuna aliyemsaidia
Alitambua kuwa anapaswa kutafuta namna ya kujitoa katika tatizo hilo
mwenyewe, aliamua kupambana na hali yake na kuliitia jina la Mungu
aliyemuumba, na kumwambia ee Mungu wagu je uliniumba ili nije kuwa
kitowewo cha wengine duniani? ndipo Mungu akamjibu na akamuelekeza
kuchimba shimo na kujificha kimyaa ikawa kila Sungura anapoona hali ya
Hatari hukimbilia shini ya shimo lile na kuwa salama na kuokoka, Ndipo
mbwa mwitu waliendelea kufukuza wanyama wengine na walimkosa Sungura,
aliyekuwa salama chini ya shimo!
Sungura alijifunza kumtegemea
aliyemuumba kwaajili ya kutunza uhai wake na sio kuwategemea rafiki
zake, sungura alitambua kuwa mwenye uchungu na yeye ni yule aliyemuumba
tu!
Yeremia 17:5 “Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule
amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni
mwake amemwacha Bwana. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona
yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya
chumvi isiyokaliwa na watu. Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana,
Ambaye Bwana ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya
maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari
ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa
uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.”
Tunajifunza: “Kumtegemea Mungu na kumfanya aliyetuumba kuwa rafiki yetu wa Kweli”
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote
Yesu kwetu ni rafiki,
Huambiwa haja pia,
Tukiomba kwa Babaye
Maombi asikia,
Lakini twajikosesha,
Twajitweka vibaya,
Kwamba tukimwomba Mungu,
Dua atasikia.
Huambiwa haja pia,
Tukiomba kwa Babaye
Maombi asikia,
Lakini twajikosesha,
Twajitweka vibaya,
Kwamba tukimwomba Mungu,
Dua atasikia.
Una dhiki na maonjo?
Una mashaka pia?
Haifai kufa moyo,
Dua atasikia.
Hakuna mwingine mwema
Wa kutuhurumia
Atujua tu dhaifu,
Maombi asikia.
Una mashaka pia?
Haifai kufa moyo,
Dua atasikia.
Hakuna mwingine mwema
Wa kutuhurumia
Atujua tu dhaifu,
Maombi asikia.
Je, hunazo hata nguvu,
Huwezi kwendelea?
Ujapodharauliwa,
Ujaporushwa pia,
Watu wangekudharau,
Wapendao dunia
Hukwambata mikononi,
Dua atasikia
Huwezi kwendelea?
Ujapodharauliwa,
Ujaporushwa pia,
Watu wangekudharau,
Wapendao dunia
Hukwambata mikononi,
Dua atasikia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni