Andiko la Msingi: 2Wathesalonike 1:6 “Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso
wale wawatesao ninyi”
Musa akimuomba Mungu kwaajili ya kuwaangamiza Amaleki walioinuka kinyume na Israel
Ni muhimu kufahamu wazi kuwa
kuonewa kwa mtu wa Mungu, sio mpango wa Mungu, wala sio mapenzi yake, watu
wengu hususani wakristo kwa kutokuwa na ujuzi wa maandiko wamefikiri kuwa
kuonewa ni sehemu ya maisha ya ukristo dhana hii sio mpango kamili wa Mungu,
Biblia inatufundisha wazi kuwa Wakristo wanayo namna yao ya kulipiza kisasi, na
hata kudai au kujitakia kisasi kwa Bwana Mungu wetu pale tunapoonewa, Maandiko
yanayotumika vibaya na kupelekea wakristo wengi kuonewa na shetani kwa sababu
ya kutokuelewa ni kama “Mathayo 5: 38-39” “Mmesikia kwamba
imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, Msishindane
na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.” Ni kutokana na kuweko kwa andiko hili wengi
wamefikiri kuwa wakristo hawana namna yao ya kulipiza kisasi na kuwa wakionewa basi kila kitu kimeishia
hapo, hayo sio mapenzi ya Mungu kamwe.tutajifunza somo hili kwa kuzingatia
vipengele kadhaa vifuatovyo;-
·
Bwana Ndiye Mlipiza Kisasi
·
Jinsi ya kujitakia kisasi kwa Bwana!
·
Pale unapolazimika kujitakia kisasi!
·
Jinsi ya kuharibu Ngome za adui
Bwana Ndiye Mlipiza Kisasi.
Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu
wetu habadiliki Yeye ni Yeye Yule Jana Leo na hata milele, watu wengi sana
hususani Wakristo wameonewa na shetani pamoja na watumishi wake kwa sababu ya
kufikiri kuwa wakipigwa shavu la kuume wanapaswa kugeuza lile la pili, na kwa
sababu hii shetani amepata nafasi ya kutuibia haki yetu ya kujilipizia kisasi
dhidi ya wanaotuonea, wengne wameweza kupoteza haki zao na kutokuzidai kwa
namna yoyote ile kwa sababu ya dhana hii, Biblia inaonyesha jinsi ambavyo wakristo
wanavyoweza kulipa kisasi, au kujitakia kisasi kwa Bwana, haya ni mapenzi ya
Mungu kabisa, Biblia inaonyesha wazi ya kuwa tunaweza kumsihi Mungu ainuke na
kushughulika na adui zetu Zaburi 68:1-3
“Mungu
huondoka, adui zake wakatawanyika, Nao wamchukiao huukimbia uso wake. Kama moshi upeperushwavyo, Ndivyo
uwapeperushavyo wao; Kama nta iyeyukavyo mbele ya moto, Ndivyo waovu wapoteavyo
usoni pa Mungu. Bali wenye haki hufurahi, Na kuushangilia uso wa Mungu, Naam,
hupiga kelele kwa furaha.”
Ni muhimu kufahamu Biblia ya
Kiswahili hapo ilitafasiriwa kwa lugha yenye kupoteza maana kidogo andiko hilo
katika biblia ya kiingereza NIV linasomeka “May God arise, may his enemies be
scattered” ni kama ingesemwa “Mungu uinuke na watawanyike maadui zako” KJV
insomeaka hivi “Let God arise, let His enemies be scattered” ni kama ingekuwa
hivi “Acha Mungu ainuke adui zake watawanyike” andiko laonyesha wazi kuwa Mungu
yuko pamoja na wenye haki yaani watu wake na kuwa kila aliye adui wa mtu wa
Mungu pia ni adui wa Mungu, kuinuka kwa Mungu ni hatua ya Mungu kuwachukulia
hatua walio kinyume naye na walio kinyume na watu wake.
Yesu mwenyewe ametufundisha ni
namna gani tunaweza kujiombea au kujitakia, akimaanisha kuwa tunaweza kumlilia
Mungu atupatie haki yetu dhidi ya adui zetu haki hii ndio kujitakia kisasi kwa
Bwana angalia Luka 18:1-8a, “Akawaambia mfano,
ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa. Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani,
hamchi Mungu, wala hajali watu. Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane,
aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu. Naye kwa muda
alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,
lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha
kwa kunijia daima. Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu. Na
Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni
mvumilivu kwao? Nawaambia, atawapatia
haki upesi;” Hebu angalia kwa makini maandiko hayo Mungu
anatufundisha nini ? Yeye ndiye hakimu wetu yeye ndiye amabaye tunaweza
kumlilia na kuugua kwake mpaka haki ipatikane, kumbe basi Mkristo haitakiwi
ukidhulumiwa tu unakubali, ukionewa tu unakubali, ukitukanwa tu unakubali,
ukifukuzwa tu unakubali hapana haiwezekani wakupige tu haiwezekani usikae kimya
yuko hakimu mkuu yuko Jaji anza kumlilia yeye atakulipia kisasi, Mungu
akufungue uweze kuelewa maandiko haya inaweza kuwa vigumu kwako kwa sababu
ndivyo ulivyozoezwa kwa miaka mingi makanisani leo mBwana na akufunulie hili
ili uweze kupatiwa haki yako katika jina la Yesu.
Hakuna shaka kuwa Mathayo 5:38-39 imetafasiriwa
vibaya na watu wengi wakati wote na
umetumika vibaya , kwa mfano watu wametumia kifungu hiki kufikiri kuwa wakristo
wanapaswa kuwa wapumbavu na wajinga na kuwa mtu yeyote akitaka kuwadhulumu
wakristo atawadhulumu atakavyo, maandiko haya yametumika pia kama aya za
kupinga vita na kila aina ya uasi n.k, tafasiri za aina hiyo sio za
kimantikikatika eneo hili, Yesu aliweka wazi kuwa hakuja kuivunja torati bali
kuitimiza na kuwa hakuna hata nukta moja ya torati itakayoondolewa Mathayo 5:17-19,Hii ni sheria inayohusu
heshima, utii na kulinda haki za binadamu, sheria hii iliwekwa ili kuwalinda
watu wasijichukulie sheria mkononi na pia kulipana kisasi kwa kuvizia dhidi ya
maadui, lakini pia inazitaka mahakama kuhakikisha kuwa zinawatendea watu haki,
Hivyo kimsingi Yesu hakuondoa kisasi na badala yake alikuwa akitufundisha
wakristo kuwa iko namna yetu ya kujilipia kisasi, ambayo ni tofauti nay a watu
wa dunia hii waliopotea, Mungu ametupa njia ya kujitakia Kisasi ili kukomesha
uonevu kwa kumuachia yeye ashughulike na adui zetu, lakini hii haina maana kuwa
kisasi hakipo!
Angalia kwa makini Biblia yako Warumi 12:19-20 “Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana
imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui
yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo,
utampalia makaa ya moto kichwani pake.” Angalia kwa makini sana Biblia
inaposema Msijilipizie kisasi maana yake nini Msijichukulie sheria mkononi,
msjitafutie haki ninyi wenyewe, Biblia inasema ipisheni ghadhabu yaani achieni
Hasira ya Mungu iamue, kwa nini kwa sababu ameahidi katika neno lake kuwa
kisasi ni kazi yake na ni lazima atalipa, sisi tumeamuriwa kuwatendea mema adui
zetu na maana yake unap[omtendea mema nini kitatokea? UNAMPALIA MAKAA YA MOTO
KICHWANI PAKE, yaani ndio unaharibu na kuifanya hukumu ya Mungu dhidi ya adui
yako au zako izidi kuwa tamu, kama nitakavyokuelekeza baadaye.
Mungu ni Mungu wa Kisasi, mafuta
na upako wa Roho Mtakatifu hakuo kwaajili ya mema tu wala hakuo kwaajili ya
kutangaza habari njema tu, lakini upako wa Roho Mtakatifu uko pia kwaajili
Bwana kujilipizia kisasi angalia vizuri Isaya
61:1-2 “Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa
sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili
kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa
habari za kufunguliwa kwao. Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya
kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;” Umeona habari njema sio
kwa wajeuri na wenye kiburi habari njema ni kwa wanyenyekevu, wanaogangwa ni
wale waliovunjika moyo, wanaotangaziwa uhuru ni wale waliotekwa, wanaofunguliwa
ni wale waliofungwa na unapotangazwa mwaka wa Bwana wa jubilee pia Kisasi cha
Mungu wetu kwa wale wanaolia au walioonewa.
Unaona Mungu wetu ni Mungu wa
kisasi, Kisasi maana yake Ni kurejesha maumivu ya kujeruhiwa kwako kwa nguvu
kwa mtu aliyekudhulumu katika wakati ambao hangependa iwe hivyo, ni kurejeshewa
maumivu kutokana na kosa lililofanyika mwanzoni, ni kurejeshewa kwa mtu kwa
kutendea mabaya, Mungu emomba mwenyewe katika maandiko kwamba kazi hii iwe yake
yeye atalipa Warumi 12:19b Mizani na kipimo cha adhabu ya wema au ubaya anayo
yeye, yeye ndiye anayejua atapimaje kwa kupitia Hasira yake takatifu, Mungu
analipa kisasi na kuwaadhibu waovu kwa vipimo vya haki yake.
Mungu hatamuacha mdhalimu aende
zake kwa amani tu bila kumshughulikia Nahumu
1:3 “Bwana si mwepesi wa hasira, ana uweza
mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; Bwana ana njia yake
katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.” Kumbe
Mungu ana namna yake na ni lazima atashughulika na mtu muovu, yeye hataki sisi
tulipe katika hasira zetu, kumbuka kuwa yeye si mwepesi wa hasira ana uwezo
mwingi yaani ana nguvu zote atashughulika tu.
Na ndio maana anasema Kisasi ni
juu yake ameahidi kuwa atatupigania nasi tutanyamaza kimya Kutoka 14:14 wakati mwingine hatuwezi kuwa naamani mpaka tumekuwa
na vita , na ni muhimu kufahamu kuwa kazi ya adui ni kuhakikisha kuwa wakati
wote kunakuwa na machafuko tu, na muhimu zaidi kufahamu kuwa hatuwezi kuwa na
mpenyo ama amani ya kweli kama adui zetu hawatatokomezwa kabisa “Hawa wamisri
mnaowaona leo hamtawaona tena milele” ni lazima adui aondolewe, na ili uwe na
uhakika wa uhuru wako ni ni lazima aondolewe
milele.
Kutoka 22:18 Biblia inasema “Usimwache mwanamke mchawi kuishi.” Unajua
biblia inamaanisha nini usiruhusu shughuli za kichawi zikakuharibu, maana yake hakikisha hakuna shughuli za
kichawi wala mchawi mwenyewe, hii ina maana gani Ulinzi wa uhakika wakati
mwingine ni kumsambulia adui yako na kuimmaliza, iko kanuni isiyobadilika
inayosema hivi “Usipowamimamisha
watakusimamisha wewe” Unaona shughulika na adui zako katika
ulimwengu war oho kabla hawajainua hata silaha zao, Mungu tunayemtumikia ni
Mungu mwenye wivu, atatangaza siku ya kisasi kwa adui zako, shuhuda nyingi
namatukio mengi ya ushindi yanatokea Mungu anapokuwa ameingilia kati dhidi ya
adui zako.
Jinsi ya kujitakia kisasi kwa Bwana!
Tumekwisha kuona sasa kuwa kisasi
ni mapenzi ya Mungu lakini ni kuwa Mungu amejitwika yeye jukumu hilo na kuwa
atawalipia kisasi adui zetu, lakini sasa ni namna gani tunaweza kujitakia
kisasi kupitia Bwana Mungu wetu? Zifuatazo ni namna mbalimbali ambazo tunaweza
kujilipizia kisasi.
1.
Fungua
kesi ya uliyotendewa Mbinguni.
Mara moja
unapoumizwa au kuonewa sio vema kukaa kimya na kusema tu namwachia Mungu, ni
Muhimu kesi hiyo ikaripotiwa mbinguni haraka, Nyakati za kanisa la kwanza
hawakuwa wajinga walichukua hatua za haraka wakamwambia Bwana yaangalie matisho
ya watu hawa, walinukuu na vifungu jinsi masihi Yesu anavyofanyiwa ghasia kisha
iachie Mbingu itashughulikia kesi yako Matendo
4:23-31. “23.
Hata walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha habari ya mambo yote
waliyoambiwa na wakuu wa makuhani na wazee. Nao waliposikia, wakampazia Mungu
sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya
mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo; nawe ulinena kwa Roho
Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya
ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?
Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja Juu ya
Bwana na juu ya Kristo wake. Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na
Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako
mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta, ili wafanye yote ambayo mkono wako na
mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee. Basi sasa, Bwana, yaangalie
matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha
mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako
mtakatifu Yesu. Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika
pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.”
Unaona nyakati za kanisa la kwanza walijua nini walichotakiwa kukifanya walishitaki
kwa Mungu yale waliyotendewa, Sisi hapa Afrika na hapa Tanzania na hapa Tanga
na sehemu nyingine mbalimbali tunafahamu jinsi watu wachawi na wauaji wengine
wa kishirikina wanavyojua kushitaki kwa miungu yao na kujitakia kisasi,
Wakristo wamekuwa wajinga tu wananewa tu na kamwe awapeleki taarifa za uonevu
wao huko mbinguni,
Mwanaume mmoja
huko Muheza katika kijiji kimojawapo aliibiwa Nazi shambani kwake na alipokuta
kuwa ameibiwa nazi alisikitika sana, waliokuwa wamemuibia nazi walizifua na
kuacha maganda ya nazi shambani kwake, mwanaume huyo alipiga mbiu kuwa kila mtu
aliyehusika kuchukua nazi shambani kwake azirejeshe na alitahadharisha kuwa mtu
asinunue nazi hizo wala kuzitumia alitangaza kuwa siku saba tu itakuwa “grace
period” yaani siku za kujisalimisha na baada ya hapo mwanaume huyo alichukua
maganda ya nazi na kuyaweka juu ya kichuguu cha mchwa kisha akalia na kusema
maneno juu ya adui zake waliokuwa wameiba nazi zake, baada ya siku chache sana ndugu wengi sana wa
watu waliomuibia nazi walianza kupatwa na misiba mfululizo hali iliyopelekea
nyuma ile yote kuwa ukiwa kwa kufa.
Kwa nini
nimeweka stori hii hapa wana wa dunia hii wako siriasi sana wanapoonewa, wana
wa ufalme wanazubaa ni lazima ulie ni lazima uipeleke kesi kwa hakimu wetu
mbinguni ni lazima umtaarifu na kumueleza jinsi ulivyoumizwa na kile
anachokutendea au walichokutendea wadhalimu.
2.
Peleka
vitisho vyote mbele za Bwana
Ni muhimu
kumweleza Mungu kile ambacho adui amekutamkia, mweleze Mungu wamekuita jinga,
wamekudharau. Wamekutishiawamekuonyesha shuhuda zao kuwa wametesa wengi na kuwa
wewe sio lolote, sio chochote, wanaonyesha nguvu zao na uwezo wao katika
shuhuda zao ili kukuonyesha kuwa huwezi kufanya lolote inawezekana ikawa kweli
madai yao lakini Mungu ni mwenye nguvu peleka vitisho vcya adui zako kama
vilivyo, usipunguze wala usiongeze , angalia kwa mfano tishio la Senekarebu
2Wafalme 19: 10-13 “ Mwambieni Hezekia, mfalme wa
Yuda, maneno haya, mkisema, Asikudanganye Mungu wako unayemtumaini, akisema,
Yerusalemu hautatiwa katika mikono ya mfalme wa Ashuru. Tazama, umesikia ni
mambo gani wafalme wa Ashuru waliyozitenda nchi zote, kwa kuziangamiza kabisa;
je! Utaokoka wewe? Je! Miungu ya mataifa wale, ambao baba zangu waliwaangamiza,
imewaokoa? Yaani, Gozani, na Harani, na Resefu, na wana wa Adini waliokuwa
katika Telasari? Yuko wapi mfalme wa Hamathi, na mfalme wa Arpadi, na mfalme wa
mji wa Sefarvaimu, na wa Hena, na wa Iva? ” Unaona hapa Mfalme
Senekarebu alikuwa amepeleka habari za kutisha na kutaka kudhuru huku akiwa na
kiburi kwamba mfalme Hezekia asijidanyanye katika habari za Mungu wake kwa kuwa
yeye ana uzoefu wa ushindi na amepiga nchi ambazo pia zilikuwa na miungu,
alimpa na shuhuda waulize wenzio yuko wapi mungu wa Gozani na harani na Resefu
n.k unafanyaje unapopokea vitisho kutoka kwa mtu mwenye nguvu kukuzidi, ana
pesa kukuzidi, wewe sio tajiri kama yeye na anakunyanyasa na kukuambia kuwa
nenda kokote huwezi kunifanya lolote unamfanyaje?lazima umripoti kwa Mungu
mwenye nguvu hiki ndicho alichokifanya Hezekia 2Wafalme 19:14-20, “Basi Hezekia akaupokea waraka katika mikono ya wale
wajumbe, akausoma; kisha Hezekia akapanda, akaingia katika nyumba ya Bwana,
akaukunjua mbele za Bwana. Naye Hezekia akaomba mbele za Bwana, akasema, Ee
Bwana, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya makerubi, wewe, naam, wewe peke yako,
ndiwe Mungu wa falme zote za dunia; wewe ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi. Tega sikio lako, Ee Bwana, usikie; fumbua
macho yako, Ee Bwana, uone; uyasikie maneno ya Senakeribu, ambayo amemtuma mtu
aje nayo ili kumtukana Mungu aliye hai. Ni kweli, Bwana, wafalme wa Ashuru
wamewaharibu mataifa na nchi zao, na kuitupa miungu yao motoni; kwa maana
haikuwa miungu, bali ni kazi ya mikono ya wanadamu; ilikuwa miti na mawe tu,
ndiyo sababu wakaiharibu. Basi sasa, Ee Bwana, Mungu wetu, utuokoe na mkono
wake, nakusihi, ili kwamba falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe ndiwe
Bwana Mungu, wewe peke yako. Ndipo Isaya, mwana wa Amozi, akapeleka ujumbe kwa
Hezekia, akisema, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa kuwa umeniomba juu
ya Senakeribu, mfalme wa Ashuru, mimi nimekusikia.” Ikawaje wakati
huu Bwana alituma malaika na jeshi lake lote lilipigwa nay eye mwenyewe mwenye
jeuri aliuawa na watumishi wake soma Mstari
35-37 35. Ikawa usiku uo huo malaika wa Bwana
alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia na themanini na tano
elfu. Na watu walipoondoka asubuhi na mapema, kumbe! Hao walikuwa maiti wote
pia. Basi Senakeribu mfalme wa
Ashuru akaondoka, akaenda zake, akarudi akakaa Ninawi. Ikawa, alipokuwa
akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza wakampiga kwa
upanga; wakaikimbilia nchi ya Ararati. Na Esar-hadoni mwanawe akatawala mahali
pake. “ Unaona mtaarifu Mungu usiache adui yako akakutukana na kukufuru
hata kama ana nguvu kiasi gani ni lazima watambue kuwa tunaye Mungu mwenye
nguvu zaidi.
3.
Tangaza
vita dhidi ya adui zako.
Biblia
inatufundisha kwamba kunapotokea vita dhidi ya adui zetu wanaotuonea tupige
kelele ya kugutusha kwa tarumbeta na Bwana atatukumbuka Hesabu 10:9 “Tena hapo mtakapokwenda
kupiga vita katika nchi yenu, kupigana na adui awaoneaye ninyi, ndipo
mtakapopiga sauti ya kugutusha kwa tarumbeta; nanyi mtakumbukwa mbele za Bwana,
Mungu wenu, nanyi mtaokolewa na adui zenu.” Biblia inamaanisha nini hapa
Tangaza vita kwa kuabudu unakumbuka jinsi ukuta wa Yeriko ulivyoanguka tarumbeta
zilihusika yaani pembe za kondoo mume endapo unayo pembe halisi kutoka Israel
hapo ndipo mahali pake ipulize abudu lia mbele za bwana mwambie ninatangaza
vita na adui yangu na Mungu ayashikaye maagano atakukumbuka.
4.
Omba
kwamba Mungu aingilie kati.
Nimuhimu
kufahamu kuwa hatupaswi kukawia kumsihi Mungu aingilie kati mara moja adui zetu
wanapotushambulia Nehemia alikuwa kiongozi Hodari na alifanikiwa kuujenga ukuta
wa Yerusalem chini ya upinzani mkali, akielewa wazi kuwa ni mapenzi ya Mungu
ukuta na mji huo kujengwa tena hakuweza kupoteza muda pale adui walipomsumbua
aliomba dua awarudishie mashutumu adui zao Nehemia
4:1-5 “Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya
kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana,
akawadhihaki Wayahudi. Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria,
akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa
dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu
hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto? Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa
karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa
ukuta wao wa mawe. Sikia, Ee Mungu wetu; maana tunadharauliwa; ukawarudishie
mashutumu yao juu ya vichwa vyao, ukawatoe watekwe katika nchi ya uhamisho; wala usiusitiri uovu wao, wala isifutwe
dhambi yao, mbele zako; kwa maana wamekukasirisha mbele ya hao wanaojenga.”
Unaona mara moja Nehemia aliwasilisha shutuma na dharau kwa Mungu hakutaka
kujibu mashambulizi kimwili, alitaka kujibu kiroho, alitaka Mungu aingilie kati
mara moja, Usikawie kuingia katika uwanja wa mapambano mara moja Daniel 6: 8-10 “Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya,
yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika.
Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku. Hata Danieli,
alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani
mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili
Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za
Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo”. Unaona
Biblia inataka hatua za haraka zichukuliwe mara moja ni kama vile linapotupwa
Kombora kutoka katika jeshi la maadui, kutokuchukua hatua kwa haraka kunaweza
kumpa nafasi zaidi ya kuleta shambulio lingine jibu mashambulizi mara moja kwa
kumsihi Mungu aingilie kati haraka.
5.
Maombi
yako lazima yatoke Moyoni kwa uchungu
Unapoomba maombi
ya kujitakia kisasi kamwe haupaswi kuomba kwa kinywa chako tu, tunajua yako
maombi unaomba kwa kusema, yako maombi unatumia ulimi, yako maombi unatumia
akili kwa kutafakari, lakini maombi ya kujitakia kisasi ni lazima yatoke kwenye
kiini cha uchungu wa moyo wako omba kwa kulalama, kwa kulia kwa kuugua kwa
manung’uniko hii ndio inaitwa Dua, Kisasi kinaombwa kwa kilio na sauti kubwa Ufunuo 6:10 “Wakalia
kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini
kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?”
Unaona! Mlilie Mungu wakati wa shida zako atakusikia.
6.
Mwambie
Mungu yatosha sasa!
Ili Maombi ya
kisasi yawe na nguvu lazima uonyeshe kuwa umechoshwa na hali hiyo na kuwa hapo
ilipofikia adui amepitiliza mpaka, wakati mwingine uko uonevu ambao unaweza
kuvumilika katika hali ya kawaida ya kibinadamu na kuwa ukichanganya na imani
yetu kwa Mungu inakuwa ni rahisi kusamehe na hata kuchukuliana nalo, hata hivyo
uko uonevu mwingine ni udhalilishaji na haukubaliki ni lazima tukate rufaa kwa
Mungu na kumwambia Mungu hili limezidi angalia mfano huu 1Wafalme 20:1-6 Biblia inasema hivi “Basi,
Ben-hadadi mfalme wa Shamu akakusanya jeshi lake lote; nao walikuwapo wafalme
thelathini na wawili pamoja naye, na farasi, na magari: akakwea akauhusuru
Samaria, akaupiga vita. Akatuma wajumbe kwa Ahabu mfalme wa Israeli, mjini,
akamwambia, Ndivyo asemavyo Ben-hadadi. Fedha yako na dhahabu yako ni zangu
mimi; na wakezo na wanao, walio wema, ni wangu. Mfalme wa Israeli akajibu,
akasema, Ni kama ulivyosema, bwana wangu, mfalme; mimi ni wako, na vyote
nilivyo navyo. Wajumbe wakarudi tena, wakasema, Ndivyo asemavyo Ben-hadadi,
Hakika nimetuma kwako kusema, Fedha yako, na dhahabu yako, na wake zako, na
wanao, utanitolea mimi; lakini kesho kama wakati huu nitatuma kwako watumwa
wangu, ili watazame-tazame nyumba yako na nyumba za watumwa wako; na itakuwa
kila kipendezacho machoni pako watakitia mikononi mwao,na kukichukua”.
Hapa unaweza kuona Dhuluma inayofanywa na mfalme Ben-Hadadi alikuwa ni mfalme
mwenye nguvu na alipiga zaidi ya wafalme 30 hivyo alikuwa na uhakika wa kuwa
ataivuruga Israel ya kaskazini na mji wake mkuu wa Samaria, Ingawa Ahabu hakuwa
mfalme mwema lakini aliuliza ushauri kwa wazee nao walimwambia usikubali, ziko
aina za uonevu ambazo hupaswi kukubali na kwamba lazima upigane kulinda Heshima
yako, Lazima umwambie adui hapa imetosha sasa na umwambie Mungu aingilie Kati
na kujilipizia kisasi dhidi ya udhalimu wote.
7.
Omba
hukumu ya Mungu dhidi ya adui zako.
Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu
anapohukumu na kukulipia kisasi hali inakuwa si ya kawaida kwa vile ni hukumu
ya Mungu, Hapa muomba kisasi anapaswa kutamka namna ngumu ambayo anataka adui
yake afanyiwe na Mungu ni lazima utangaze hukumu yake Biblia imejaa mifano
mingi ya matamshi ya aina hii, ona Hesabu
16:1-4 “Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa
Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa
Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni; nao, pamoja na
watu kadha wa kadha wa wana wa Israeli, watu mia mbili na hamsini, Wakuu wa
mkutano, waliokuwa wateule wa mkutano, watu wenye sifa, wakainuka mbele ya
Musa; nao wakakusanyika kinyume
cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni
mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, Bwana naye yu kati yao; n'nini basi kujitukuza
juu ya mkutano wa Bwana? Musa aliposikia maneno haya, akapomoka kifudifudi;” Kifungu
hicho kinaonyesha wazi kuwa kundi kubwa la watu wenye sifa walikuwa wamemuasi
Musa huu ulikuwa umati mkubwa sana wa uasi kupata kutokea, walimkataa Musa na
Haruni, na sasa walikuwa hawako tayari kusikiliza Musa aliwaonea huruma kwa
uasi wao aliwaombea na alisema nao vizuri lakini hawakusikiliza Ndipo Musa
alikasirika na kuomba Dua ya kisasi hata hivyo hawakujali kwa Jeuri Hesabu 16:15-19 “Musa
akakasirika sana, akamwambia Bwana. Usiikubali sadaka yao; mimi sikutwaa hata
punda mmoja kwao, wala sikumwumiza hata mtu mmoja miongoni mwao. Kisha Musa
akamwambia Kora, Wewe na mkutano wako wote iweni hapa mbele ya Bwana kesho,
wewe, na wao, na Haruni; mkatwae kila mtu chetezo chake, na kutia uvumba juu
yake, mkavilete mbele za Bwana, vyetezo mia mbili na hamsini; wewe pia, na
Haruni, kila mtu na awe na chetezo chake. Basi wakavitwaa kila mtu chetezo
chake, wakatia na moto ndani yake, wakatia na uvumba juu ya moto, na kusimama
pale mlangoni pa hema ya kukutania, pamoja na Musa na Haruni. Kisha Kora
akakutanisha mkutano wote kinyume chao mlangoni pa hema ya kukutania; na
utukufu wa Bwana ukatokea mbele ya mkutano wote”. Kutokana na Ujeuri wa
Kora pamoja na Musa kuomba reheza za Mungu dhidi yao lakini waliendeleza uasi
Ndipo Musa akatangaza hukumu ya kupita kawaida Hesabu 16:28-32 “28. Musa akasema, Kwa
jambo hili mtajua ya kwamba Bwana amenituma, ili nifanye kazi hizi zote; kwa
kuwa mimi sikuzifanya kwa akili zangu mwenyewe. Kama watu hawa wakifa kifo cha
sikuzote, kama watu wote wafavyo, au kama wakipatilizwa kwa mapatilizo ya watu
wote; hapo basi Bwana hakunituma mimi. Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo
nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia
shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau Bwana, Basi
ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao
ikapasuka; nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na
wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote.” Unaona ! Musa
aliomba na kutangaza hukumu ya Mungu dhidi ya adui zake ilikuwa lazima kiwe
kitu cha tofauti ili watu wajue kuwa Musa ameitwa na Mungu, Unapoomba dhidi ya
adui zako Mungu akulipizie kisasi omba hukumu ya kupita kawaida, Hanna
aliyekuwa amenyanyaswa vya kutosha na Penina kwa sababu ya kukosa
Mtoto,alimlilia Mungu sana aweze kuzaa mtoto na kuweka nadhiri, hata hivyo
Mungu alipomjibu na kumsikiliza aliomba kwa uchungu Mungu afanye kitu, angalia 1Samuel 2:1-10 “Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia Bwana, Pembe yangu
imetukuka katika Bwana, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa
naufurahia wokovu wako; Hakuna aliye mtakatifu kama Bwana; Kwa maana hakuna ye
yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu. Msizidi kunena kwa
kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa
maarifa, Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani. Pinde zao mashujaa zimevunjika,
Na hao waliojikwaa wamefungiwa nguvu. Walioshiba wamejikodisha ili kupata
chakula, Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha. Naam, huyo aliyekua tasa
amezaa watoto saba, Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika. Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha
hata kuzimu, tena huleta juu. Bwana
hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu. Humwinua
mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe
pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za
dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake. Yeye atailinda miguu ya
watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna
atakayeshinda; Washindanao na Bwana watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye
atawapigia radi; Bwana ataihukumu miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake
nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake.” Unaona Musa aliomba aridhi
ifunue kinywa na kummeza wahusika, hana anaomba Bwana awapige radi, ili
ijulikane kuwa Mungu ameingilia kati haiwezekani adui ashughulikiwe katika
namna ya kawaida, adui atashughulikiwa kwa namna ambayo kila mtu natajua kuwa
Mungu ameshughulika naye tunaweza pia kuangalia mfano wa Eliya kwa wale askari
waliotumwa kumkamata ilikuwaje 2Wafalme
1: 9-15 “Ndipo mfalme akatuma akida wa askari
hamsini pamoja na hamsini wake, wamwendee Eliya. Akamwendea, na tazama, ameketi
juu ya kilima. Akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka. Eliya
akajibu, akamwambia yule akida wa hamsini, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na
ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto ukashuka,
ukamteketeza, yeye na hamsini wake. Akatuma tena akida wa hamsini mwingine
pamoja na hamsini wake, wamwendee. Akajibu, akamwambia, Ewe mtu wa Mungu,
mfalme asema, Shuka upesi. Eliya akajibu, akamwambia, Ikiwa mimi ni mtu wa
Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto
wa Mungu ukashuka kutoka mbinguni, ukamteketeza, yeye na hamsini wake. Tena
akatuma akida wa hamsini wa tatu, pamoja na hamsini wake. Yule akida wa hamsini
wa tatu akapanda, akaenda akapiga magoti mbele ya Eliya, akamsihi sana,
akamwambia, Ee mtu wa Mungu, nakusihi, roho yangu, na roho za watumishi wako
hawa hamsini, ziwe na thamani machoni pako. Tazama, moto ulishuka kutoka
mbinguni, ukawateketeza wale akida wa hamsini wawili wa kwanza pamoja na
hamsini wao; laiti sasa roho yangu na iwe na thamani machoni pako. Malaika wa
Bwana akamwambia Eliya, Shuka pamoja naye; usimwogope. Akaondoka, akashuka
pamoja naye hata kwa mfalme.” Hapa watu 102 wanakufa kwa neno la Eliya
anashusha moto kutoka mbinguni na kuwaunguza walikuwa wametumwa kumkamata,
wakati wote tunapoomba hukumu ya Mungu baadaya ya kuchoshwa na kuonewa na adui
zetu hatuna budi kujitakia jambo la kupita kawaida, Lazima tuombe Mungu afanye
kitun ambacho adui hata kisahau maishani mwake, unaposoma katika eneo hili
unaweza kudhani kuwa sasa mkuu wa wajenzi anafundisha nini ? jambo hili sio
jema labda huenda ni kinyume na injili jibu ni hapana Yesu mwenyewe alikuwa
akijitakia kisasi kwa vitu vyenye maudhi dhidi yake mfano Marko 11:12-14,20-21 biblia inasema hivi, “Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa. Akaona
kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na
alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini. Akajibu,
akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake
wakasikia., Na asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona ule mtini umenyauka toka
shinani. Petro akakumbuka
habari yake, akamwambia, Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka.” Hebu
tujiulize Yesu alikuwa anatufundisha nini kumbuka kuwa mtini huu haukuwa
umemkosea Yesu neno, Ni Yesu ndiye aliyekuwa na njaa na mwandishi anatuambia
wala haukuwa wakati wa tini unaona kunmbe hata wakati haukuwa wa tini Lakini
kitendo cha Yesu kukosa huduma kutoka katika mti huo aliusemea maneno na mtini
ulinyauka, Sio hivyo tu, Luka 23:27-31
“Mkutano mkubwa wa watu wakamfuata, na wanawake
waliokuwa wakijipiga vifua na kumwombolezea.Yesu akawageukia, akasema, Enyi
binti za Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto
wenu. Kwa maana tazama, siku zitakuja
watakaposema, Heri walio tasa, na matumbo yasiyozaa, na maziwa yasiyonyonyesha.
Ndipo watakapoanza kuiambia milima, Tuangukieni, na vilima, Tufunikeni. Kwa
kuwa kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?”
Unaona Yesu anatamka maneno kwaajili ya kizazi kile na mji wa Yerusalem
wanahistoria wote wanajua kuwa maneno haya ya Yesu yalitimizwa mwaka wa 70
baada yake kitendo cha Warumi kumsulubisha Yesu kilikuwa na maana ya wazi
kabisa kuwa kuwa hukumu kubwa ingekuja kutoka kwa warumi kuja kwa wayahudi
walioshuhudia kuwa Yesu asulubiwe ukweli maneno hayo yaliwadhuru hata leo, Je
hili sio agano jipya? Je Yesu hana uwezo wa Kusamehe? Anao lakini angalia
alimuonya hata Yuda kwa kitendo cha kumsaliti alisema ole wake mtu yule
atakayenisaliti ingekuwa heri kwake kama asingalizaliwa Mathayo 26:21-25 “Nao walipokuwa
wakila, alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu atanisaliti. Wakahuzunika sana,
wakaanza kumwuliza mmoja mmoja, Ni mimi, Bwana? Akajibu akasema, Yeye aliyetia
mkono wake pamoja nami katika kombe, ndiye atakayenisaliti. Mwana wa Adamu
aenda zake, kama alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana
wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa. Yuda, yule mwenye
kumsaliti, akajibu, akasema, Ni mimi, Rabi? Akamwambia, Wewe umesema.”
Angalia kwamba Yesu alitoa onyo kali kwa Yuda kutokana na Tendo la Kumsaliti
Yesu hakukuwa na msamaha kwake, najua unaweza kusema kuwa si ulikuwa mpango wa
Mungu? Tungewezaje kukombolewa ilikuwa ni muhimu Yuda atumike kumsaliti! Lakini
mtu ambaye angemsaliti Yesu alikuwa na laana kali sana ambayo ilikuwa imekwisha
andikwa katika zaburi hivyo kila mwanafunzi wa Yesu alikuwa na wajibu wa
kukwepa kutimiza andiko hilo baya dhidi yake, lakini kwa sababu ya tamaa Yuda
alipatwa na mabaya je Zaburi ilikuwa imetabiri nini dhidi ya mtu atakayemsaliti
Yesu ? Angalia Zaburi ya 69 : 1-20 “Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamazeKwa maana
wamenifumbulia kinywa; Kinywa cha mtu asiye haki, cha hila, Wamesema nami kwa
ulimi wa uongo.Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka, Wamepigana nami bure. Badala ya upendo wangu wao hunishitaki,
Ijapokuwa naliwaombea. Wamenichukuza mabaya badala ya mema, Na chuki badala ya
upendo wangu. Uweke mtu mkorofi juu yake, Mshitaki asimame mkono wake wa kuume.
Katika kuhukumiwa ataonekana hana haki, Na sala yake itadhaniwa kuwa ni dhambi.
Siku zake na ziwe chache, Usimamizi wake na atwae mtu mwingine. Wanawe na wawe
yatima, Na mkewe na awe mjane. Kutanga na watange wanawe na kuomba, Watafute
chakula mbali na mahame yao. Mdai na anase vitu vyote alivyo navyo, Wageni na
wateke mapato ya kazi yake. Asiwe na mtu wa kumfanyia fadhili, Wala mtu wa
kuwahurumia yatima wake. Wazao wake waangamizwe, Jina lao likafutwe katika
kizazi cha pili. Uovu wa baba zake ukumbukwe mbele za Bwana, Na dhambi ya
mamaye isifutwe. Ziwe mbele za Bwana daima, Aliondoe kumbukumbu lao duniani. Kwa
kuwa hakukumbuka kutenda fadhili, Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, Hata
akamfisha mtu aliyevunjika moyo, Naye alipenda kulaani, nako kukampata.
Hakupendezwa na kubariki, kukawa mbali naye, Alijivika laana kana kwamba ni
vazi lake. Ikamwingilia moyoni kama maji, Na kama mafuta mifupani mwake. Na iwe kwake kama vazi ajivikalo, Na kama
mshipi ajifungao daima. Ndiyo malipo ya washitaki wangu toka kwa Bwana, Na ya
hao wanaoisingizia nafsi yangu mabaya.” Unaweza kuona hii ilikuwa ni zaburi yenye laana yenye maombi ya
kisasi dhidi ya mtu atakaye msaliti Yesu Mtume Petro alinukuu katika Matendo ya Mitume 1:20 akionyesha kuwa
imeandikwa nafasi yake aitwae mtu mwingine, ilikuwa ni lazima kuepuka tendo la
kumsaliti Yesu kwani lilikuwa limetamkiwa mambi mabaya sana lakini kutokana na
kiburi na ukaidi ndanin ya Yuda laana hii ilimpata Yesu alitakiwa au huenda
aliiomba hii na ndio maana alionya mtu yuleatakayemsaliti, Ndugu Biblia imejaa
fundisho hili la kujitakia Kisasi kwa Bwana.
8. Tangaza
hukumu na kisasi dhidi ya adui zako.
Biblia imejaa mafundisho ya
kutosha namna ya kujitakia kisasi kwa Bwana sio tu kwamba utaomba kisasi dhidi ya adui zako
lakini pia unaweza kutangaza au kutabiri namna adui yako atakavyoshughulikiwa
matamshi haya yanafanyika kwa imani na uchungu na katika uwepo wa Roho
Mtakatifu angalia mfano wa uasi wa Abimeleki na jinsi Yonathan nduguye
alivyomtangazia hukumu yake Waamuzi
9:1-6 “Abimeleki, mwana wa Yerubaali, akaenda
Shekemu kwa ndugu za mama yake, akanena nao, na wote waliokuwa wa nyumba ya
baba ya mama yake, akasema, Haya, neneni tafadhali masikioni mwa waume wote wa
Shekemu, mkaulize, Je! Ni lipi lililo jema kwenu, kwamba hao wana wa Yerubaali
wote, ambao ni watu sabini, watawale juu yenu, au kwamba mtu mmoja atawale juu
yenu? Tena kumbukeni ya kwamba mimi ni mfupa na nyama yenu. Hao ndugu za mama
yake wakanena habari zake masikioni mwa hao watu wote wa Shekemu maneno hayo
yote; na mioyo yao ikaelekea kumwandama Abimeleki; kwa kuwa walisema, Huyu ni
ndugu yetu. Wakampa vipande vya fedha sabini vilivyotoka katika nyumba ya
Baal-berithi, na kwa fedha hizo Abimeleki akaajiri watu wapuuzi mabaradhuli,
wafuatane naye. Kisha akaenda nyumbani kwa babaye huko Ofra, akawaua nduguze,
hao wana wa Yerubaali, watu sabini, akawaua juu ya jiwe moja; lakini Yothamu,
mwana mdogo wa Yerubaali, alisalia; kwa maana alijificha. Kisha hao watu wote
wa Shekemu wakakusanyika pamoja, na jamaa yote ya Milo, wakaenda na kumtawaza
Abimeleki awe mfalme, karibu na huo mgandi ulio karibu na ngome iliyo katika
Shekemu.”
Unaweza kuona kitendo kiovu
kilichofanywa na Abimeleki aliwaua ndugu zake ili apate kutawala yeye nduguze
walikuwa wapata sabini aliwaua katika jiwe moja, Lakini nduguye mmoja Yothamu
aliokoka kwa kukimbia Yothamu alishuhudia nduguze wakiuawa na alielezwa hatuoni
kuwa Yothamu alikuwa nabii hapana lakini kwa vile kilichotendeka sio haki
alitabiri alitangaza kisasi cha Bwana dhidi ya Abimeleki na watu wa shekemu
angalia Waamuzi 9:7-21 “Kisha walipomwambia huyo Yothamu, yeye akaenda, akasimama
juu ya kilele cha kilima cha Gerizimu, akapaza sauti yake, akapiga kelele, na kuwaambia,
Nisikieni mimi, enyi watu wa Shekemu, ili kwamba Mungu naye apate kuwasikia
ninyi. Siku moja miti ilitoka ili kuutia mmoja mafuta uwe mfalme juu yao;
ikauambia mti mzeituni, Tawala wewe juu yetu. Lakini huo mzeituni ukaiambia,
Je! Niache mafuta yangu, ambayo kwangu mimi watu wamheshimu Mungu na wanadamu,
ili niende nikayonge-yonge juu ya miti?
Kisha miti ikauambia mtini, Njoo wewe, utawale juu yetu. Lakini huo
mtini ukaiambia, Je! Niuache utamu wangu, na matunda yangu mazuri, niende
nikayonge-yonge juu ya miti? Kisha miti ikauambia mzabibu, Njoo wewe, utawale
juu yetu. Huo mzabibu nao ukaiambia, Je! Niiache divai yangu, ambayo
humfurahisha Mungu na wanadamu, ili niende nikayonge-yonge juu ya miti? Ndipo
hiyo miti yote ikauambia mti wa miiba, Njoo wewe, utawale juu yetu. Huo mti wa
miiba ukaiambia miti, Kwamba ninyi mwanitia mafuta niwe mfalme juu yenu
kwelikweli, basi njoni mtumaini kivuli changu; na kwamba sivyo, na utoke moto
katika mti wa miiba na kuiteketeza mierezi ya Lebanoni. Basi sasa ikiwa
mmetenda kwa uaminifu na uelekevu, katika kumtawaza Abimeleki awe mfalme, na
ikiwa mmemtendea mema Yerubaali na nyumba yake, na kumtendea kama ilivyostahili
mikono yake; (kwa maana baba yangu aliwatetea ninyi, na kuhatirisha uhai wake,
na kuwaokoa na mikono ya Midiani; nanyi mmeinuka juu ya nyumba ya baba yangu
hivi leo nanyi mmewaua wanawe, watu sabini, juu ya jiwe moja, nanyi mmemtawaza
Abimeleki, mwana wa kijakazi chake, awe mfalme juu ya watu wa Shekemu kwa
sababu yeye ni ndugu yenu;) basi
ikiwa mmemtendea kwa uaminifu na uelekevu Yerubaali na nyumba yake hivi leo,
basi furahini ninyi katika huyo Abimeleki, yeye naye na afurahi kwenu ninyi; lakini kwamba sivyo hivyo, basi,
moto na utoke katika Abimeleki na kuwateketeza watu wa Shekemu, na jamaa ya Milo;
kisha moto na utoke katika hao watu wa Shekemu, na katika jamaa ya Milo, na
kumteketeza Abimeleki. Kisha
Yothamu akaenda zake na kukimbia, akaenda Beeri, na kukaa kuko, kwa kumwogopa
Abimeleki nduguye”. Unaweza kuona Yothamu alitangaza hukumu hii, hii ilikuwa
ni namna ya kutangaza kisasi au hukumu kwa tendo lisilo la haki na je tangazo
hili lilitimizwa? Angalia Biblia inasema
hivi Waamuzi 9:50-57 “ Ndipo Abimeleki alipokwenda Thebesi, akapanga kinyume cha
Thebesi na kuutwaa. Lakini ndani ya huo mji palikuwa na buruji yenye nguvu, na
watu wote waume na wake wakakimbilia huko, na watu wote wa mji, nao
wakajifungia ndani, wakapanda paa la buruji. Abimeleki akaiendea hiyo buruji na
kupigana nayo; naye akaukaribia mlango wa buruji ili auteketeze kwa moto. Na
mwanamke mmoja akabwaga jiwe la kusagia la juu, nalo likampiga Abimeleki
kichwani, na kulivunja fuvu la kichwa chake. Ndipo akamwita kwa haraka huyo kijana
aliyekuwa anamchukulia silaha zake, na kumwambia, Futa upanga wako, uniue, ili
watu wasiseme juu yangu Aliuawa na mwanamke. Basi huyo kijana wake akamchoma
upanga, naye akafa. Basi hapo watu wa
Israeli walipoona ya kuwa Abimeleki amekufa, wakaondoka wakaenda kila mtu
mahali pake. Basi hivyo Mungu akalipiza kisasi juu ya uovu wa Abimeleki
aliomtenda baba yake, katika kuwaua hao nduguze watu sabini; uovu wote wa watu
wa Shekemu Mungu alilipiza juu ya vichwa vyao; na hiyo laana ya Yothamu mwana
wa Yerubaali ikawajilia juu yao.”
Ni wazi kuwa Mungu ameweka nguvu ya ziada katika
kinywa chako unapotendewa jambo lisilo haki unaweza kutangaza namna Bwana
anavyoweza kukulipia kisasi au kushughulika na adui yako, ni vigumu kunukuu
kila andiko ili upate kusadiki lakini nitanukuu mfano wa Daudi kwa Goliath
ambao wote walitamka laana na kutangaziana hukumu kwa vinywa vyao na kila mtu
kwa jina la Mungu wake ni wazi kuwa Mungu wa Israel aliye hai alijilipizia
kisasi kwa vile mfilisti alikuwa amawatukana Israel nah ii ilikuwa ni sawa na
kumtukana Bwana, awaye yote anayekudharau na kukutukana na kukuonea na
kukulaani huku wewe unamtegemea Mungu aliye hai anajitafutia gharama za kulipa 1Samuel 17:43-47 “Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia
kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake. Mfilisti akamwambia Daudi,
Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni.
Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na
mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi
ya Israeli uliowatukana. Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami
nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na
wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya
kuwa yuko Mungu katika Israeli. Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba
Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia
ninyi mikononi mwetu.” Unaona ni mapenzi ya Mungu kumtangazia adui yako
namna atakavyomalizika ajijue wazi afahamu mwisho wake utakavyokuwa mtamkie kwa
uchungu na maumivu mengi na katika upako na wivu wa Mungu wetu naye Bwana
atalitimiza neno lako.
9. Mpe ishara ya kumtia Nidhamu!
Wakati mwingine ni vigumu watu
wakorofi na jeuri kukumbuka kwamba yanayowapata yametokana na adhabu maalumu
kutoka kwa Bwana kupitia wewe na hivyo kumtangazia hukumu ambayo yeye haijui,
hajaisikia na hana dalili kunaweza kuwa kwenye mafanikio madogo ya kujua kuwa
anatengenezwa kwa sababu ya ujeuri wake hivyo ni muhimu wakati mwingine
kutangaza wazi kuwa ishara hizi zitampata ili atambue kuwa wapi alikosea na
kwaajili ya nini anapatwa na yanayompata hata kama ni kutoka moyoni angalia
kwamfano Matendo ya Mitume 13: 6-12 “Walipokwisha
kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa
uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu; mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio
Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake,
akataka kulisikia neno la Mungu. Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri
ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile
imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia
macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa
haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa
Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi
kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na
kumwongoza. Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini,
akiyastaajabia mafundisho ya Bwana”. Ni wazi kuwa mchawi huyu alipata
adhabu ya kuwa kipofu kwa muda Paulo mtume alitumia mamlaka yake ya kitume ana
kitumishi kumshikisha adabu mtu ambaye alikuwa akizuia kwa uchawi mkuu wa mkoa
asiokoke kwa kuisikia injili, kumtia nidhamu huku kulifanya Liwali yaani mkuu
wa mkoa aokoke na wale waliolionatukio waliamini na kumpa Bwana utukufu.
10. Hakikisha unalia kwa Uchungu.
Maombi ya kujitakia kisasi ni
maombi yanayojumuisha uchungu na kulia au kulia kwa uchungu kisasi hakiombwi
kavukavu kinaombwa kwa kilio, Mungu huwajibika anaposikia kilio angalia kilio
cha Habili kwa nduguye aliyedhulumu uhai wake Kaini kilisababisha adhabu na
laana kubwa kwa Habili Mwanzo 4:8-12 “Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa
walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.BWANA
akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi
wa ndugu yangu? Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia
kutoka katika ardhi. Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua
kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; utakapoilima ardhi
haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.” Unaona kilio cha uchungu kina
maana kubwa sana Daudi alikuwa anaifahamu siri hii waziwazi hivyo mara kadhaa
katika Zaburi zake alikuwa akilia kwa uchungu mfano katika Zaburi 5:1-2 “Ee Bwana uayasikie
maneno yangu, Ukuangalie Kutafakari kwangu. Uisikie Sauti yangu ya kilio change,
Ee Mfalme wangu na Mungu wangu, Kwa maana wewe Ndiwe nikuombaye.” Mungu huyaangalia machozi na uchungu
kwani ni muhimu kuomba na kuonyesha hisia za kuumizwa kwetu na ndipohaki yetu
itapatikana, Kumbuka Yesu alisema
hivi katika Luka 18:7 “ Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake WANAOMLILIA
mchana na usiku,naye ni mvumilivu kwao?”
Unaona ni wazi Yesu anakubaliana nasi kuwa sio maombi ya kawaida
yanatumika pale unapotaka haki bali ni maombi ya kulia, ni kulia ndiko
kunakoweza kuleta mageuzi makubwa dhidi
ya mipango mibaya ya adui dhidi yetu.
11. Tumia silaha ya sifa!
Ni muhimu kufahamu kuwa kuna
siri ya ziada katika kumsifu Mungu, sifa zina tabia ya kuwasambaratisha maadui
zetu, ushahidi wa kibiblia, mara moja adui wanapokushambulia hakikisha kuwa unamwimbia
Mungu na kumtukuza na kumsifu hii ndio ilikuwa silaha kubwa ya Daudi, katika
agano jipya maandiko yanaonyesha Jinsi Paulo na Sila walivyoweza kufanikiwa
kuwasambaratisha maadui kwa kutumia sifa Matendo 16:22-26 “Makutano wote wakaondoka wakawaendea, makadhi wakawavua
nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora. Na walipokwisha kuwapiga
mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde
sana.Naye akiisha kupata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga
miguu kwa mkatale. Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa
wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa
wakiwasikiliza. Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza
ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.”
Aidha wote tuna kumbuka jinsi
Mji wa Yeriko ulivyoangushwa kupitia kumsifu Mungu, Yoshua 6:1-5, Israel walipiga kelele baada ya matarumbeta na
kupitia agizo hili kuta za mji wa Yeriko zilianguka na wakaweza kuteka mateka na kuwashambulia adui,
Njia hii ni ya kujipatia ushindi pia.
12. Tangaza laana kwa wanaokulaani
Tunayo ahadi ya kudumu kutoka
kwa baba yetu wa imani Abrahamu, Mungu Baba yetu alipomuita Ibrahimu baba
aliahidi kuwa ngao kwake na alimpa ahadi ya ulinzi na usalama na kwamba yeye
anauwezo wa kuwa chanzo cha Baraka lakini vilevile kusababisha laana kwa watakao
mlaani Mwanzo 12:1-3 “BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na
jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami
nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe
uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na
katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa”. Unaona ahadi hii
inatuhusu moja kwa moja inukuu na kumkumbusha Mungu na mara unapoanza kutamka
laana dhidi ya adui yako kupitia ahadi hii Mungu anaanza kulifanyia kazi kwa
kulipa kisasi.
13.
Omba kwa
kunena kwa Lugha kwa Muda mrefu.
Tuko vitani katika hali ya
kawaida vita za duniani majemadari huwa wanawasiliana kwa kutumia lugha za
mficho ili adui asije akagundua, ni muhimu kunena kwa lugha kwa muda mrefu sana
aidha pia unaweza kuitumia Damu ya Yesu na ushuhuda yaanineno lake na
kumkumbusha Mungu yalke ambayo amewahi kukutendea na jinsi alivyoweza kukupa
ushindi katika vita mbalimbali,Ufunuo
12:11 “Nao wakamshinda kwa damu ya
Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata
kufa.” Pia unaweza kutumia nadhiri na utoaji wa sadaka maalumu kwaajili
ya kuwashughulikia adui zako.
14. Fuata nyayo za Daudi
Daudi alikuwa ndio kiongozi Bora zaidi aliyekuwa
na mafanikio makubwa sana dhidi ya adui zake alifanikiwa katika kila vita na
hakuwahi kushindwa vita Yesu alitumia mamlaka ya daudi katika uanadamu wake Ufunuo 3:7 “Na
kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye
mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala
hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.” Daudi alikuwa mtu
aliyeupendeza Moyo wa Mungu, alikuwa na upako wa kinabii,upako wa kifalme na
upako wa kishujaa, alijaa sifa na ibada aliabudu kwa upako na uwepo, alikuwa
muombaji, alikuwa na upako wa kikuhani, alikuwa na upako wa kuokoa watu,
alikuwa na ujuzi wa vita, alimpiga Goliath, aliwapiga wafilisti mara
kadhaa,Hajawahi kushindwa vita, hivyo ni muhimu sana kujifunza utendaji wake na
maisha yake katika swala zima lamaombi ya kujilipia au kujitakia kisasi kutoka
kwa Bwana.
Pale unapolazimika kujitakia kisasi!
Ni nyakati gani
tunalazimika kujitakia kisasi? Ni pale tunapokutana na changamoto mbalimbalia
kama ilivyokuwa kwa muombaji maarufu wa kisasi yaani Daudi, utahitaji kujiombea
kisasi kwa Bwana katika sababu kadhaa zifuatazo.
Ø
Ni pale unapokuwa na adui mwenye kutisha kama
goliath, au unapokuwa na mtu mwenye nguvu anayekutafuta kama ilivyokuwa kwa
Sauli aliyekuwa akimtafuta Daudi apate kumuangamiza, Kama Daudi utaomba maombi
kama yake kwa vile u mfalme lakini bado unaishi kama mtumwa.
Ø
Utahitaji maombi ya kujitakia kisasi unapokuwa
wewe ndiye lengo la Adui au unapokuwa umezingirwa na mtandao wa wachawi au
unapokuwa umezingirwa na wimbi la majaribuna umezama katika dimbwi la taabu na
shida.
Ø
Unapotaka kurekebisha maisha yako ya baadaye,
unapozingirwa na hatari za kifo, unaposumbuliwa na magonjwa na kufanya kazi kwa
bidii bila kupata maendeleo, taabu mbalimbali zinapojitokeza na ukaanza aina
hizi za maombi taabu huanza kujitokeza katika kambi ya maadui zako, Maadui
wanaweza kuinuka na kuanza kupigana wenyewe kwa wenyewe, wakati wote kumbuka
kuwa kila unapotaka kujitakia kisasi kwa Bwana basi maombi ya Daudi katika
zaburi ni ya muhimu sana kuyatumia, unapoanza kuomba aina hii ya maombi adui
wanaanza kukosa amani.
Ø
Pale unapoomba njia yao iwe giza ukweli ni kuwa
wanaanza kuchanganyikiwa na kukosa namna ya kufanya na hatimaye wataangamia,
Mungu unapomuomba awapige kofi awavunje taya maana yake wataanza kukosa maneno
ya kusema na maneno yao wanayotamka juu yako yatashindikana kutimia, kuvunja
meno yao pia ina maana ya kuharibu kila aina ya silaha wanazozitumia, kwa hiyo
kila mara unapotaka kujitakia kisasi kwa Bwana omba kama mwandishi wa zaburi.
Jinsi ya Kuomba Maombi ya kujitakia kisasi kwa Bwana !
1. Lazima
wewe mwenyewe utubu
2. Acha
kuwa adui wa Mungu
3. Fanya
urafiki na Mungu mwenyezi
4. Jitenge
na ulimwengu wa dhambi, usifanye dhambi
5. Jiandae
kwa vita dhidi ya maadui zako wote
Mambo ya kuombea.
1. Ee
Bwana kilio changu kikufikie na unipe msaada wa malaika zako leo katika jina la
Yesu
2. Ee
Bwana nipe jina litakalokuwa Baraka kwangu leo katika jina la Yesu
3. Ee
Bwana kila vizuizi vya yule mwovu,na mipango yake yote kinyume name na malaika
wangu viunguzwekwa moto katika jina la Yesu
4. Ee
Bwana unilinde mimi mtumwa wako na mawe yote ya kishetani ninayotupiwa na
wanaonichukia katika jina la Yesu
5. Kila
aina ya uasi dhidi yangu ukaaibishwe katika jina la Yesu
6. Uniokoe
mimi na keleleza Shetani katika jina la Yesu
7. Uniokoe
na watu nwabaya na wenye nia mbaya katika jina la Yesu
8. Kila
mwenye kunikusudia mabaya atawanywe na kutupwa katika nchi ya upweke katika
jina la Yesu
9. Nakushukuru
kwa kunisikia maombi na dua yangu
Jinsi ya kuharibu Ngome za adui.
Ni muhimu kufahamu kwamba Biblia ni kitabu cha vita! ni kitabu cha
kijeshi, unapoifungua Biblia na kuanza kupitia ukurasa mmoja hadi ukurasa
mwingine hata mwisho utagundua kuwa imejaa misamiati ya kijeshi na vita
Katika 2Wakoritho 2:11
Biblia inasema “Shetani asije akapata kutushinda;
kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.” Neno Fikra katika
biblia ya kiingereza linatumika neno “Schemes”
ambalo maana yake ni Mipango au miakakati inayopangwa na adui kwa kusudi
lakukushinda katika vita kwa msingi huo
basi ni muhimu kwa kila mmoja anayataka kujilipizia kisasi kutoka kwa mBwana
kukumbuka kuwa tuko vitani na adui ana hila kwa msingi huo ni lazima tufahamu
kwanza lugha za kivita ili tunapoingia katika ulimwengu wa roho kutangaza
hukumu au kutamka kisasi dhidi ya adui na kujilipizia kisasi ni kwa sababu hii
biblia imetupalugha nyingi za kivita
Biblia
inatumia neno Kushindana mieleka (wrestle) hii ni kama inaashiria kuwa ziko
vita za ana kwa ana ni mapambano yenye kutumia nguvu na akili na ni lazima
umshinde adui yako, pia kuna neno kushambulia au kuvamia Smiting, kuna neno
kama kukatilia mbali Slaughter na kutokubali kupinga strife na kadhalika haya
yote yanazungumzia mapambano ya kivita, Biblia pia inazungumzia kuwashinda
maadui, kuvukuza, kuchukua mateka, kuzuia, kufukuza majeshi ya aduim
kuzima,kuepuka,kushambulia kumtupa chini adui n.k. hizi nilugha za kivita Waefeso 6:12-18 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama;
bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya
pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza
kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli
viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa
Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza
kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu,
na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila
wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea
watakatifu wote;”
Historia
ya mwanadamu imefunikwa na vita tu, Biblia inafunua kuwa hata malaika mbinguni
wamewahi kupigana vita, Katika ufunuo tunaambiwa kuwa Mikael na malaika zake
wakapigana na lile Joka na kumshinda,
kwa msingi huo unapozungumza kuhusu vita ni lazima waweko majemadari wa vita na
ndio wapiganaji, Vita sio kitu cha kimyakimya, unapoingia vitani kupambana
unashambulia ngome za maadui, unajishughulisha na ngome na ndio maana biblia
inatumia lugha za kivita katika kututia moyo kusonga mbele kwa gharama yoyote
Kama
shetani atamshambulia mwanadamu na kuweka vikwazo kiasi kwamba kikwazo hicho
kikamfana mwanadamu kushindwa kuendelea mbele hilo ni shambulizi na ni ngome
imewekwa dhidi yako, Shetani anapopanga mipango na ikawa inafanikiwa dhidi yetu
huo ni uvamizi,ni kikwazo tayari ni jambo ambalo litakuwa limewekwa na shetani
ili kutuzuia, Zaburi 124:6-8 inasema
“Na ahimidiwe Bwana; Asiyetutoa kuwa mawindo kwa
meno yao. Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego
umevunjika, nasi tumeokoka. Msaada wetu u katika jina la Bwana, Aliyezifanya
mbingu na nchi.” Mtego unaotajwa hapo ni hila na mipango ya shetani na maajenti wake kutuhusu sisi na hutokea
hasa tunapokuwa vitani, ni mpaka uwe na ujuzi wa kujitoa katika mipango hiyo
ndipo unapoweza kuwa huru
Ngoja nikuambie Ndugu kuna mikakati mingi ya shetani mibaya
kukuhusu katikamaisha yako lengo kuu likiwa ni kuharibu kabisa maisha yako
Kijana mmoja ambaye anatokea katika familia masikini sana, na ni
yeye tu aliyekuwa wa kwanza kufanikiwa kwenda Chuo kikuu katika Familia yao, alikuwa
na mtihani wa muhimu wa kumalizia mtihani huu ulikuwa ndio uamue hatima yake na
kuleta faida katika familia yao na mpenyo katika maisha yake,kijana alijisomea
kwa bidii sana wiki ile na wakati mwingine hakulala, siku moja ambayo kesho yake ilikuwa ndio ya mtihani
alijitahidi usiku kucha kwaajili ya kujiandaa na kisha asubuhi pia alijiandaa
dakika chache sana kabla ya mtihani alisoma kupitiliza mpaka akawa amechoka,
siku ile ya mtihani ikiwa imebaki saa moja tu kabla ya kuingia katika chumba
cha mtihani ambako angetembea kwa dakika tano tu kutoka chumbani kwake
alijisemea njoja apumzike kidogo kama dakika kumi na tano hivi, akiwaamepumzika
jambo laajabu alikuja kushituka usingizini mtihani aliokuwa amejiandaa ulikuwa
umeisha na hivyo alilazimika kurudia mwaka mzima kwaajili ya mitihani hiyo na
alipokuja kurudia mwakani alifeli na ndoto ya mafanikio yake na familia yake
ilikuwa imeishia hapo, Mambo kama haya ndugu ni mashambulizi ya kishetani.
Miaka kadhaa nyuma binti mwenye miaka 37 alipata Mchumba wa kumuoa
na uchumba ukaendelea ikiwa imebaki wiki moja tu waoane kijana akasema
hajisikii tena kumuoa mwanamke huyo kwa sababu ni mfupi na amesikia kuwa watu
wafupi ni wajeuri na wakorofi, alipofikisha miaka 39 alipata mtu mwingine
aliyekuwa anataka kumuoa maandalizi yaliendelea ikiwa imebaki wiki moja tu
kabla ya harusi yao kijana aligongwa na basi lililokuwa limeacha njia na kufa
papo hapo, alipofikisha miaka 41 alipata mchumba mwingine maandalizi yaliendelea
na siku ya harusi ilifanikiwa ikafika saa ya ibada wakati Mtumishi wa Mungu
anuliza nani mwenye kizuizi kwa watu hao wasioane alijitokeza mwanamke na
kujitambulisha kuwa anayeoa ni mume wake wa halali! Hiki ninini ?
Ni mashambulizi mkaubwa ya shetani kwa mwanamke huyu, Ndugu kuna
mapambano kwaajili ya maisha yako na mafanikio yako, kuna mikakati maalumu ya
kishetani inawekwa kwakko kukuumiza, kukufanya ukate tamaa, kukufanya uwe na
nuksi, kukufanya ukataliwe, kukufanya usizae, kukuharibia kazini, kukufanya
udhoofike, kuna mashambulizi ya kishetani, kuna mashambulizi ya kichawi hizi
zote ni ajenda za shetani kuharibu kabisa maisha yetu, kuna mambo ambayo sio ya
kawaida yanaendelea katika maisha yetu ambayo sio ya kawaida lazima tupambane
na kujitafutia kisasi kwa Bwana !
1. Kuna wala nyama na wanywa damu za watu wanaweza kuweka mikosi
katika maisha ya watu
2. Kuna nguvu za giza na kichawi
3. Kuna mizimu katika koo za watu mbalimbali zenye kuwadhuru
4. Kuna dini za kichawi
5. Kuna roho chafu majini na mapepo
6. Kuna roho chafu za umasikini na ukandamizaji wa kila aina
7. Kuna maswala ya kurithi yananayoweza kuathiri familia
8. Kuna majina uliyopewa ambayo yanaweza kubeba mkosi katika maisha
yakom Mfano mtu anayeitwa ayubu maana yake Achukiwe, Isabela maana yake chungu cha
uchawi cha porini, Rebecca maana yake ngombe mdogo,Yoel maana mbuzi wa mlimani
lazima ulipitie jina lako na kuliangalia kama linamchango gani katika maisha
yako, Kumbuka kama shetani atakupaka na nuksi hizo rafiki zako watakukimbia na
wale wote wanaotakiwa kutoa msaada wakati unashambuliwa na shetani wanakimbia
mbali au wanageuka kuwa maadui, Unaweza kuota ndoto mbaya, utasumbuka na
unashangaa hufanikiwi, utawaota hata waliokufa, unaweza kusikia sauti za ajabu
ajabu, ni kwa sababu hii ni lazima kufanya kila linalowezekana kuondoa uvamizi
huo wa ibilisi katika maisha yetu, Nuksi na mikosi ya kivamizi kutoka kwa
shetani inaposhughulikiwa vilivyo unaanza kuwa na shuhuda katima maisha yako,
utaanza kuona miujiza ya ajabu ikijitokeza katika maisha yako na mambo mazito
yataanza kuwapata waliokuwa wakikusakama katika maisha yako!
Jinsi ya kuharibu Ngome za
kivamizi za shetani
·
Yakabidhi maisha yako kwa Yesu
·
Tubu kila aina ya dhambi
unayoikumbuka na usiyoikumbuka katika maisha yako, dhambi ina tabia ya kumpa adui
nguvu za kukushambulia
·
Tambua kila aina ya uvamizi wa
kishetani katika maisha yako
·
Tangaza vita na kulia kwaajili
ya uvamizi dhidi yako.
Jinsi ya kuomba.
·
Mikosi kutoka kwa ukoo wa Baba
yangu na mama yangu dhidi yangu na dhidi ya maisha yangu nakuharibu katika jina
la Yesu
·
Malaika wa giza ambao mnazuia
maombi yangu, nawatawanya na kuwasambaratisha katika jina la Yesu
·
Nguvu za shetani zilizotumwa
kinyuime na nyota yangu, kuififisha, nakuua katika jina la Yesu
·
Kila aina ya mwizi, katika
maisha yangu, huna mamlaka dhidi ya maisha yangu nakuua katika jina la Yesu
·
Mapanya ya kishetani,
wanaokopera na kuniibia lisikie neno la Bwana muda wako umekwisha nakuua kabisa
katika jina la Yesu
·
Kila nguvu ambayo imetumwa
kwangu, kunipotezea muda na kunipotezea mavuno yangu nakumaliza katika jina la
Yesu
·
Ndege wachafu wanaoruka
kinyume name katika jina la Yesu kristo nakusambaratisha
·
Kisha chukua muda wa
kumshukuru Mungu kwa imani katika maombi
Jinsi ya kungoa Pando
asilolipanda Baba wa Mbinguni.
Mapando ya shetani yako kila mahali duniani, shetani amekusudia
kuharibu kila Nyanja ya maisha ya watu wa Mungu na kwa sababu hiyo unapaswa
kuwa na ujuzi huu ili utamke kisasi kwaajili ya kila eneo ambalo limepadwa
mbegu mbaya na kungoa mbegu hiyo mbaya katika jina la Yesu. Mathayo 13:24-30 “Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana
na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; lakini watu walipolala, akaja
adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.Baadaye majani ya
ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. Watumwa wa mwenye nyumba
wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata
wapi basi magugu? Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia,
Basi, wataka twende tukayakusanye? Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na
kuzing'oa ngano pamoja nayo. Viacheni
vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao,
Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano
ikusanyeni ghalani mwangu.” Unaona shetani anaweza
kupanda taabu katika kila eneo la maisha yako ni muhimu kutambua mambo ya
kawaida ya yasiyo ya kawaida tusimkubalie kabisa shetani kufanya anayotaka
kuyafanya katika maisha yetu katika Jina la Yesu.
Uwe na hasira takatifu!
Ni muhimu kufahamu kuwa ulimwengu unazidi kuwa na uovu siku hadi
siku,na ufalme wa giza unajipanga kuharibu maisha ya watu siku hadi siku, ni
lazima sasa kuwakabili manabii wa baali na majeshi yake yote bila huruma,
lazima kuitumia mamlaka yetu kwa viwango vya juu mpaka watuogope, Ni wakati wa
kukabilia na na kila aina ya vitisho vya ibilisi na kuwatamkia maneno magumu
yeye na watumishi wake au awaye yote ambaye wakati huo anatumika kama chombo
cha shetani ni wakati wa watu wa Mungu kujitokeza na kuutisha ufalme wa giza na
kuwanyamazisha na kuondoa maneno na matendo yao ya vitisho!
Ili tufikie ngazi ya kuyafanya hayo ni lazima kuwa na hasira
takatifu, uwe mgumu na ikiwezekana kuwa na vurugu za kiroho ili pale wanaposema
kuwa hakuna njia sisi ndio tunapita, pale wanapodhani kuwa hakuna ushindi sisi
tunakuwa nao, na nilazima tuwe washindi kwani Yesu mwenyewe ni mharibifu wa
Uovu Biblia inasema kwa maana “alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisi” 1Yohana 3:8 “…Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa,
ili azivunje kazi za Ibilisi”
Nguvu za Mungu hazina mipaka, Ni Mungu habadiliki ana nguvu zote
omnipotent hajawahi kushindwa na hatawahji kushindwa ni mkuu na matendo yake ni
makuu ni zaidi ya utoshelevu, nimkuu sana atafanya mambi makbwa ya kutisha na
kushangaza katika maisha yetu, Mungu alipomtuma Saul kuwauwa waamaleki
maelekezo yake yalikuwa wazi tu kuwa asibakize hata mmoja auwe hadi wanyama
Biblia inasema sasa shoka limewkisha kuwekwa tayari kila mti usiozaa matunda
utakatwa na kutupwa motoni.
Angamiza kabisa.!
Baada ya mti kukatwa kumbuka kuwa unaweza kutumika kwa
kutengenezea vifaa na fanicha za majumbani na kadhalika, pia inaweza kutumika
kama kuni na kupikia chakula agizo linataka kuteketeza kabisa kwa sababu hiyo
chochote kile ambacho kinaweza kuchangia haribiko lako kinafaa kuharibiwa
kabisa, chochote ambacho hakitaki wewe uwe na furaha maishani mwako na nguvu
yoyote inayotaka kukuletea mauti haistahili kuishi adhabu yake ni kuharibiwa
kabisa.
“Kumbukumbu la torati 13:
6-11 “Atakapokushawishi kwa siri ndugu
yako, mwana wa mamaako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako,
au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu
mingine usiyoijua wewe wala baba zako; katika miungu ya mataifa yaliyo kando-kando
yenu karibu nawe au mbali nawe, tokea ncha moja ya dunia hata ncha ya pili ya
dunia; usimkubalie wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala
usimwache, wala usimfiche; mwue kweli; mkono wako na uwe wa kwanza juu yake
katika kumwua, na baadaye mikono ya watu wote. Nawe mtupie mawe hata afe; kwa
kuwa alitaka kukupotoa na Bwana, Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri,
katika nyumba ya utumwa. Na Israeli wote
watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako.”
Mungu
anataka ufutilie mbali kila kinachosimama kinyume nawe, ukiue kabisa kila
kinachopingana nawe na kukifutilia mbali milele, yeyote anayetaka kukuua
hastahili kuishi pia Mungu anapokomesha adui humkomesha milele
Maandiko
yanarekodi habari za uadui wa kudumu kati ya Isarael na waamaleki, Mungu
aliamuru na kuelekeza Israel kuhakikisha kuwa wanawafutilia mbali waamaleki na
kuwaondoa kabisa juu ya uso wa dunia angalia Kutoka 17:8-13 Biblia inasema “Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli
huko Refidimu. Musa akamwambia Yoshua,
Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele
kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Basi Yoshua akafanya
kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri
wakapanda juu ya kile kilima. Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli
walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. Lakini mikono ya
Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia.
Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu;
mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. Yoshua akawaangamiza Amaleki na
watu wake kwa ukali wa upanga. BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika
kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta
ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu. Musa akajenga
madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi;akasema, BWANA ameapa; BWANA atakuwa
na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.” Unaweza kuona kuwa Bwana
aliapa kuwa atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi kwa nini
nitakueleza baadaye tuongeze maandiko mengine zaidi kuhusu Amaleki
1Samuel 15:2 Biblia inasema “Bwana wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu
mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo
walipopanda kutoka Misri. Basi
sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo,
wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye,
ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.” Unaweza kuona
kwa nini amri ya Mungu inakuwakali sana
kwa waamaleki na kwa nini Mungu anataka waangamizwe kabisa wao na kila kitu
walichokuwa nacho na mpaka mifugo yao? Kwa sababu waliwapinga wana wa Israel
njiani walipokuwa wakitoka Misri, tuone maandiko zaidi Kumbukumbu la Torati 25:17-19 Biblia inasema haya “Kumbuka
aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri; jinsi alivyokukuta
katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge
nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu. Basi itakuwa,
hapo atakapokwisha kukupumzisha Bwana, Mungu wako, katika adui zako wote walio
kando-kando, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo
uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau” Unaona Musa
naye anakazia kwamba Israel asisahau kuhusu Amaleki na matendo yasiyo ya Huruma
aliyoyafanya Israel wakati Israel wakiwa wamechoka wanatoka Misri, wakiwa na
kiu wakiwa wanyonge Amaleki walifanya jambo la kuhuzunisha hawakumuogopa Mungu
waliwapinga Israel Jangwani? Ni kwa sababu ya jambo hili Mungu aliweka kinyongo
na Ameleki aliweka Kisasi cha milele alisema ni lazima waharibiwe kila
walichonacho wasiachiwe uhai watokomezwe kabisa
Unyama
wa amaleki dhidi ya Israel ndio uliomfanya Mungu awakumbushe Israel kila wakati
kuhakikisha kuwa wanakifuta kizazi hiki duniani unaona ni mapenzi ya Mungu
kuwaangamiza adui zako kabisa bila kusaza, wakati mwingine wewe uko katika
dhiki,na safari ya Jangwani badala ya mtu kugeuka kuwa msaada mkubwa kwako
anakuwa adui kwako anakudhalilisha akipingana na Mungu. Na mapenzi ya Mungu
katika maisha yako Mungu anaamuru usibakize jina la amaleki juu ya uso wa dunia wafutwe kabisa
na hapo ndipo utakapokuwa huru kwelikweli usisahau! Mungu alionyesha msisitizo.
Maombi ya kusambaratisha
Vifungu
hapo juu vimetufundisha jinsi ya kushughulika na adui na uovu wake kama ilivyo
mbele za Mungu, kila mwenye kusikia na asikie kuna maombi ya kujenga lakini
vilevile kuna maombi ya kuharibu, kuna ya kupanda na kuna ya kung’oa, Mungu
alimwambia Yeremiah nimekuita Yeremia
1:8-10 “angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na
juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga
na kupanda” Unaona! Mwandishi
wa Zaburi anasema “Mara watakapoisikia sauti yangu watanitii, wageni
watainama wenyewe mbele zangu” unaweza kuona vilevile unapoisoma
biblia vema hususani kuhusu habari za Yesu utaweza kuona na kushangaa Yesu akizungumza na magonjwa
kama uziwi, ukoma, upofu, dhuruba, mti, magonjwa na maiti, maneno anayoyatumia
ni kama Funguka, Tulia, toka, inuka uende, na kadhalika kumbe basi Mungu
anataka kila kitu kitamkiwe kulingana na uharibifu kiliosababisha kila nguvu ya
uharibifu inahitaji maombi ya kuharibu na kusambaratisha, “Kwa maana mwana wa Mungu alidhihirishwa
ili azivunje kazi za ibilisi” Ni lazima tubadilishe mtazamo wa
maombi yetu na kuzungumza uharibifu kwa kila kinachotaka kutuharibu, umefika
wakati sasa watu wa Mungu kuachana na unyonge
na kusimama na kukabiliana na kila hali ya uovu, na unajua kuwa kuna
maeneo mengi sana shetani amefanikiwa kupanda kila mbegu ya uovu na hatuna budi
kuyango’a mapando hayo kwa mamlaka tuliyopewa na Mungu.
Sifa za maombi ya kusambaratisha kila
pando lililo ovu!
1. Lazima
kufanya maombi yenye usumbufu na magumu yasiyo ya huruma huruma
2. Maombi
yenye kuamuru na kudai haki
3. Maombi
yasiyo na mashaka
4. Maombi
ya kutamka laana za kiungu
5. Maombi
ya kinabii yenye matamsi ya kumshughulikia adui katika ulimwengu wa kiroho kama
daudi alivyomtamkia Goliath
6. Maombi
yenye kuhoji nani ewe mlima mkubwa na kuusambaratisha
7. Maombi
yenye kuzungumza na tatizo moja kwa moja na kulikemea
8. Maombi
yanye kutimiza makusudi ya Mungu
Kumbuka
unapokuwa umeanza aina hii ya maombi ya kusema na vitu au watu watu wanaweza
kufikiri kuna tatizo ndani yako, kuna shida unapotabiria vitu watu wanaweza
kudhani kuwa wewe ni kichaa, lakini usiwajali endelea unaweza kuwekea mikono
hata mashine na kuondoa roho mbaya ndani yake!
Maombi ya kungoa Pando asilolipanda baba
Ni
lazima uwe na maombi ya kungoa kila pando asilolipanda Baba katika maisha yako
kila siku, lakini ni lazima uwe umempokea Yesu, ni lazima uyachunguze maishga
yako na kuangalia kimwili na kiroho na usiruhusu lolote lisilo la kawaida liwe
la kawaida katika maisha yako, angalia kama ni kutokana na uasi na dhambi,
kisha yango’oe Biblia inasema kila pando asilolipanda baba yangu wa Mbinguni
litamgo’lewa. Utaanza kuona utamu wa kuwa na Mungu tangu sasa.
Mambo ya kuombea wakati wa kungo’a
1. Pando
lolote la giza katika maisha yako life katika jina la Yesu
2. Pando
lolote la mauti katika maisha na ukoo wangu life katika jina la Yesu
3. Pando
lolote na shambulizi lolote dhidi yangu life katika jina la Yesu
4. Narudisha
kule yalikotoka kila aina ya mashambulizi ya ibilisi
5. Mungu
wa kisasi kama Mungu wa Eliya jitokeze na ujidhihirishe katika jina la Yesu
6. Zika
dhambi zangu na maanguko yangu yote katika jina la Yesu
7. Kila
pando na nguvu zinazozuia nisiendelee life katika jina la Yesu
8. Mikono
yangu na iwe shoka la vita vya Bwana
katika jina la Yesu
9. Damu
ya Yesu ingoe’ kila muhuri niliogongwa nisiendelee katika maisha yangu katika
jina la Yesu
10. Mungu
usimame na kuwa aibisha adui zangu katika Jina la Yesu.
11. Asante
Bwana kwa kunijibu maombi yangu katika jina la Yesu.
Silaha
za mapambano.
Mapambano
katika maisha ni jambo lisiloepukika uwe unataka au hutaki, Adui yetu shetani
amejipanga kwa vita ana majeshi ya vita na silaha za vita, kwa msingi huo
tunahitaji silaha za nguvu kuweza kupambana naye silaha utakazojifunza hapa
zitakupa somo ambalo hutalisahau maishani mwako, Shetani anatumia silaha nzito
na mbaya za kutisha lakini tutazichambua na kuzibainisha na mara utakapokuwa
umezibaini utasimama kwa ushindi na kutangaza kuwa Hakuna kazi ya kufanya
1. Risasi
za rohoni: swala la mtu linapochukuliwa katika ulimwengu wa giza haraka nsana
wanatafutwa watu wa familia ya mtu yule wenye nguvu za giza, Kadiri kunavyokuwa
na watu wengi wenye nguvu za giza katika familia ya mtu ndivyo na shambulizi la
mtu huyo linakuwa baya zaidi, habari zote ambazo adui anazitaka zitakuwa
zinatolewa na wanafamilia, na hapo ndipo roho ya mtu huyo inapoweza
kushambuliwa na hata kumfanya mtu huyo asiamke tena, unaweza hata kuota
umepigwa risasi katika ndoto na ikaingia katika mwili wako, na hapo ndipo
magonjwa kama kansa huanza na safari ya kifo huanza taratibu, na kama risasi
itakuwa imeingia mguuni au mkononi au tumboni basi maeneo hayo ya mwili
yanaanza kutofautiana na sehemu nyingine za mwili
·
Kujitoa hapo unahitaji kufanyiwa upasuaji
wa kiroho na kuiondoa risasi uliyopigwa
·
Kisha irudishie kwa aliyeituma
2. Mshale
wa rohoni: iko mishale ya kiroho watu hushambuliana kwa njia mbalimbali inaweza
kutokea katika familia kwa mfano zenye wake wenza, kijana ambaye anaweza kuja
kuwa ndie kiongozi wa familia au mwenye akili za kupita kawaida au mzuri lakini
akatupiwa mishale tangu akiwa tumboni mwa mama yake na kama hilo linafanyika
mara nyingi ubongo ndio unakuwa sehemu ya kwanza kushambuliwa na hivyo anaweza
kupungukiwa na akili au akawa taahira
·
Kujitoa ni lazima kuuchomoa mshale wa kichawi
na kuurejesha kwa aliyeutuma
·
Jiombee uwe na ukuta wa ulinzi wa moto ili
mishale ya aina hii isikuweze
3. Kubadilishiwa
mwili: Kuna nguvu za kipepo za kubadilishiwa mwili, kama umebadilishiwa mwili
unaonekana kuwa mzee kuliko umri wako, unajisikia vibaya, hauna amani, uzito,
unakuwa mbaya, unajikunjakunja, hauelezeki na unachukiwa na ndoa yako inaweza
kusambaratika na matatizo mengine mengi, katika ndoa kama mwili wako
umebadilishwa unaweza kushangaa mumeo au mkeo anakuchukia kwa namna ambayo sio
ya kawaida kiasi ambacho inawezekana hata asitake kukuona hapo lazima utambue
kuwa kuna kitu kigeni kimetendeka katika ulimwengu war oho.
·
Hakikisha unaomba ili kwamba mwili wako wa
asili uweze kurejea, utakapokwisha kuomba utaweza kuona mabadiliko na utagundua
kuwa kweli kuna kitu kilikuwa kinaendelea
4. Kulishwa
vitu vichafu: ukiota ndoto unakula au umehudhuria pati ya kipepo na ukala vitu
humaanisha vitu vibaya na mara utaona mikosi inaanza kukuandama, hutakua kiroho
na magonjwa yatakuandama.
·
Hapo ni lazima maombi ya kufunguliwa na
ikiwezekana mpaka vitu ulivyolisha vitoke
5. Ndoa
za kipepo: Mtu anapooa au kuolewa katika
ulimwengu wa kipepo kwa kukusudia au kwa ndoto atakuwa na vita kali sana, ndoa
ya kiroho ni agano kamili kama lilivyo agano la ndoa, hivyo aliyeolewa au kuoa
pepo ni lazima atambue kuwa atapambana mpaka tone la mwisho la damu kuhakikisha
kuwa anatetea ndoa yake kama umeoa mwanadamu mwezako wa kawaida yule pepo
atahakikisha kuwa mnaachana, kutakuwa na chuki ya ajabu, ugomvi usiokuwa wa
kawaida, umasikini, kuporomoka kwa biashara,hali ya hatari nyumbani inakuwa
ngumu na kubwa mno,muingiliano wa kifamilia nao unakua wenye migogoro mikubwa,
na mpezni wa kiroho atahakikisha kuwa anamshambulia wa mwilini mpaka ashindwe.
·
Maombi ya kujikomboa
·
Maombi ya kuhakikisha kuwa mpenzi wako wa
kiroho anakufa na unabaki na yule ambaye Mungu amekupa uishi naye, shambulia
kila roho mbaya iliyopandikizwa dhidi yako, njia nzuri ya kujilinda sio
kujikinga katika damu ya Yesu bali ni kushambulia kubomoa kuharibu na kurudisha
mishale yote ya moto wa kichawi kwa adui ili asikushambulie milele.
·
2Thesalonike
1:6 “Kwa kuwa ni haki
mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi;” ni kwa sababu hii
ndio maana ukiwarudishia mishale yao wale waliokuonea inafanya kazi kwa sababu
ni mapenzi ya Mungu Zaburi 109:17 “Naye alipenda kulaani, nako kukampata. Hakupendezwa na
kubariki, kukawa mbali naye,”
·
Wakati watu waovu wanapofanya mashambulizi
yasiyo ya kimungu na kurushia mishale ya kichawi kwa watu wa Mungu ni lazima
wanyamazishwe na kurejeshewa wao wenyewe uovu wao na mishale yao, siri moja
wapo kubwa unayopaswa kuijua ni kuwa shetani na maajenti wake kama kuna jambo
wanaliogopa ni kurejeshewa mashambulizi waliyoyatuma wao wenyewe, na
usipowafanyia hivyo wakati mwingine hawatakoma, ndio maana biblia inasema waovu
ni lazima wainame kwa wenye haki
Mambo
ya kuombea
1. Jiwwekee
mikono na sema kuwa najilinda kwa damu ya Yesu
2. Taja
baadhiya uovu wa ibilisi na maajenti wake na yatume kwao mara saba kwa jina la
Yesu mfano
·
Ndoto mbaya
·
Ndoto za kukojoa kitandani
·
Nuksi
·
Hofu
·
Umasikini
·
Mishale ya adui
·
Matatizo katika damu
·
Maumivu ya kichwa
·
Maumivu ya tumbo
·
Mikosi toka katika mito
·
Mikosi kutoka baharini
·
Mikosi ya ndoa za mitala
·
Mikosi kutokana na tohara
·
Mikosi ya utasa na ugumba
·
Mikosi ya kipepo
·
Mapepo ya uadui
·
Mapepo ya kichawi
3. Silaha
za jadi za kishetani, ziniachilie na zirudi kwa aliyevituma katika jina la Yesu.
4. Weka
mkono wako kishwani na mwingine katika tumbo kemea mishale yote ya adui na
iamuru kurudi kwa wachawi na wanga na shetani katika jina la Yesu.
5. Mweleze
Bwana kila kitu kigeni na kila hali ngeni unayoipitia na ndoto ulizoziota kisha
ziamuru kurudi kwa waliozituma katika jina la Yesu.
6. Sema
kila silaha ya shetani ikoseshwe amani na kusambaratishwa katika jina la Yesu.
Songa mbele:
Ili
uendelee kujitakia kisasi cha bwana na kuendelea kuusumbua ulimwengu wa adui ni
lazima usonge mbele katika kutembea na bwana na Jeshi lake Biblia inasema
katika Yuda 1:3 “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia
habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili
niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.”
Ni muhimu kufahamu kuwa wakati wa uamsho
na wakati ambapo neno la Mungu
linashehimika kweli ye neno watu wanaitii na kiwango cha injili kinahubiriwa
katika viwango vyake na kiwango cha maadui na uchawi na upinzani vinapanda
Kutokutii
kunafananishwa na dhambi ya uchawi, 1Samuel
15:23 hivyo ili kusonga mbele katika mapambano haya, hatuna budi
kuhakikisha kuwa tunamtii Mungu kwa gharama yoyote unapoasi madhara makubwa
yanaweza nkukupata
1. Utapungukiwa
na uwepo wa Mungu
2.
Inawapa nguvu mapepo na shetani
kukushambulia
3.
Kutokutii ni roho
4.
Itakusababishia taabu
5.
Itakaribisha dhoruba kwenye maisha yako
6.
Itakuletea kutokupendelewa na Mungu
7.
Itakueletea usingizi
8.
Itakufanya uwe katika kundi la wana mbuzi
na sio Kondoo
9. Itakufanya
uwe unachukuliana na maswala ya dunia. Hakuna uovu mbaya kama kuchukuliana na
dunia ukinionyesha mtu aliyerudi nyuma nitakuonyesha mtu aliyechukuliana na
dunia kwa siku nyingi, hakuna anguko la ghafla lazima atakuwa amechukuliana na
dunia kidogokidogo na mwishoe anaangulka
kabisa, anaweza kuwa amehudhuria chuo cha Biblia na kumaliza masomo yake na
kusimikwa kuwa mtumishi na huku ni kutoa cheo cha kiroho bila kuthibitishwa na
Mungu.
Achana na Unafiki.
Ni roho ya kinafiki kukaa kimya mahali
unapotakiwa kuzungumza eti kwa sababu unaogopa kuwaumiza marafiki au kwa lengo
la kuwafurahisha marafiki ni roho ya kuvumilia uovu kwa sababu hutaki watu
wakufanye wewe kuwa adui yao, ni muhimu kujiuliza swali je uko unafiki wowote
ndani yangu?
Ni
muhimu kuomba kama mwandishi wa zaburi alivyoomba unichunguze uone kama iko
njia iletayo majuto ndani yangu Zaburi
139:23-24 inasikitisha kuwa wengi tunapenda kuabudu miungu iliyoko katika
ubongo wetu.
Injili ya Mchepuko
Inasikitisha
kuwa watu wengi leo wanaweza kuwa wanahubiri injili na isiyokazia kuhusu
utakatifu, na kutoonyesha kuwa wanachukia dhambi lakini sababu kuu ikiwa ni kwa
sababu wanataka kuwa na umati mkubwa wa watu au wanataka kufungua tawi,
wanaifanya injili kuwa laini badala ya kukemea dhambi, wanasengenya, wanatoa
mimba, wanatoka nje ya ndoa, mashoga wanawaita kaka poa, watu wengi leo
wanachukizwa na mafundish yanayohusu kujitoa, kufunga, utakatifu, na ntofauti
iliyoko kati ya watu hao na wa dunia ni kuwa wao wanabeba Biblia tu.
Achana na ukisasa
Ni
muhimu kutokusahau kuwa Mungu huyu aliyemtuma Yesu duniani kwa wokovu ndiye
yuleyule aliyewachoma moto watu wa sodoma na gomorah, wanasahau kuwa aliyemuita
Paulo kunwa mtume ndiye aliyemzamisha Farao kwenye maji, wanawaambia watu
wachague ni eneo gani la biblia wanataka kulisoma inasikitisha kwamba maovu
mengi ambayo yamefanywa na wazungu kwa jina la Ukristo kwa sasa yamechukuliwa
kama njia ya kuwatia moyo watu kurudi nyuma wazungu sasa wamefikia uovu hata wa
kuona kwa mapenzi ya jinsia moja na kuyaleta makanisani lazima tuukatae uovu.
Kuifuta namna ya Dunia hii
Biblia
inasema wala msiifuatisha nemna ya dunia hii,
namna ya dunia hii inataka Mungu aonekane kuwa mdogo kuliko mawazo yao,
inamfanya Mungu aonekane kuwa mwongo, wanafikiri kuwa Mungu anayepaswa kufuatwa
ni Mungu atakayewafanya wakati wote wajisikie vizuri, wanataka Mungu ambaye
hata ukifanya dhambi anakulipa mshahara, wanataka kuwapa watu wazo kuwa Mungu
ni Mungu wa Rehema na hahukumu kwa urahisi, wanataka Mungu akubaliane na kila
tunachikifanya na staili yetu ya maisha, wanafikiri kuwa Mungu ni kama
anahitaji mtazamo mdogo tu ambao tunaweza kumpa siku ya jumapili tu na kumtolea
sadaka, lugha zinabadilisha kuifanya dhambi ionekane kuwa kitu kidogo sana
kisicho na madhara, wanacheza aina za muziki unaocheza katika kumbi za disco,
muziki unaopigwa hauna tofauti sana na ule wa duniani, inahubiriwa injili
inayotoa msahama wa dhambi bila mtu kubadilika au kutubu,inayotia moyo kwenda
mbinguni bila kuonyesha kuwa kuna moto, Biblia inaonye katika 1Wakoritho 10:12 “Yeye ajidhaniaye kuwa amesimama na aangalie asianguke”
Maombi.
1. Naamuru
kuchanganyikiwa na fadhaa zilizoratibiwa na shetani Dhidi yangu katika jina la
Yesu
2. Kila
mpango mbaya wa ibilisi kinyume na maisha yangu katika jina la Yesu
3. Kila
ina ya laana na mapepo ambayo shetani ameyakusudia dhidi yangu nayadhoofisha
katika jina la Yesu
4. Kila
aina ya vita iliyokusudiwa kinyume na amani niliyo nayo naiharibu katika jina
la Yesu
5. Naamuru
kuchanganyikiwa kwa ibilisi katika kila mpango wake katika jina la Yesu
6. Kila
aina ya vita inayokusudiwa na kupangwa kinyume nami naiharibu katika jina la
Yesu
7. Kila
vita kinyume na amani niliyo nayo naiamuru kwa jina la Yesu
8. Kisha
anza kumshukuru Mungu kwa imani kwani ataanza kujibu maombi yako.
Na Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote
)718990796
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni