Andiko
la Msingi: Yohana 17:21 “Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani
yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki
ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.”
Umoja
ni hali ya kuungana kushikamana na kushirikiana au kufanya mambo kwa nia moja
hata kuwa kitu kimoja, kadiri watu wanavyokuwa na umoja wanakuwa na mwanya
mkubwa sana wa kufanikiwa katika kila jambo wanalolifanya na kulikusudia hakuna
cha kuwazuia kwa kufahamu umuhimu wa Umoja Yesu aliwaombea wanafunzi wake wawe
na umoja.
Ujumbe.
Wakati
fulani kulikuwa na Mzee mmoja aliyeishi na vijana wake watatu huko kijijini,
vijana hao walikuwa ni wachapa kazi hodari, hata hivyo walikuwa na tabia ya
kugombana sana kila wakati, Mzee wao alijaribu kufanya kila njia ili
kuwapatanisha lakini ilishindikana. Ingawa wanakijiji walishukuru na kufurahia
utendaji wao wa kazi na bidii waliyokuwa nayo, lakini waliwatania kutokana na
ugomvi wao.
Miezi
ilipita ikatokea kuwa yule mzee alianza kuugua, aliwaita vijana wake na
kuwataka wawe na umoja , lakini hawakusikiliza, aliamua kuwafundisha kivitendo,
ili kwamba wasahau tofauti zao na kuungana
Mzee
aliwaita vijana na kuwaambia “Nitawapa fimbo nyingi sana na kuzigawanya kwa
kila mmoja nataka avunje fimbo hiyo mara mbili, yeye atakayevunja fimbo kwa
haraka atapata zawadi”.
Vijana
wakakubali.
Mzee
aliwapa kundi la fimbo kumikumi kila mmoja na aliwaambia wazivunje vipande
vipande, vija na walifanya hivyo kwa dakika chahe sana na kisha wakaanza
kugombana kuwa ni nani amekuwa wakwanza
Mzee
aliwaambia “wanangu wapendwa kazi bado, Sasa nitawapa kundi moja moja lenye
fimbo kumikumi zilizofungwa pamoja na sasa utatakiwa kuvunja kundi zima la
fimbo bila kuzitenganisha”
Vijana
walikubali na kuanza kutaka kuvunja kundi la fimbo kumikumi kila mmoja na lake,
kila mmoja alijaribu kufanya kila aliwezalo ili wazivunje lakini ilishindikana,
kisha walitoa taarifa kwa baba yao.
Mzee wao aliwaambia wanangu angalia
jinsi mlivyoweza kuvunja fimbo moja moja zilizokuwa peke yake kila moja kwa urahisi sana, lakini hamkuweza kuzivunja
fimbo za aina hiyohiyo zililipokuwa pamoja, kama mtakuwa mnagombana kila wakati
na kutengana ni rahisi kwenu kushindwa , Lakini kama mtaungana na kuwa kitu
kimoja hakuna atakayewaweza tafadhali sana nawaomba make pamoja
Vijana walielewa nguvu ya umoja na
wakamuahidi mzee wao kuwa watakaa pamoja kwa gharama yoyote!.
Kuna nguvu ya mafanikio makubwa
katika umoja, kuna siri katika umoja, Kanisa likikaa kwa umoja, ndugu wakikaa
kwa umoja, wanandoa wakikaa kwa umoja, familia zikikaa kwa umoja kwaya zikikaa
kwa umoja bendi zikikaa kwa umoja, wafanya kazi wakikaa kwa umoja, na taifa
letu tukiungana na kuwa kitu kimoja hakuna jambo litaweza kuzuiliwa kwetu
Mwanzo 11:1-7
“Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.
Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi
ya Shinari; wakakaa huko.Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome
moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Wakasema,
Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie
jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. BWANA akashuka ili auone mji
na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni
taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa
hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Haya, na tushuke huko, tuwachafulie
usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.”
“Ni wazi kuwa Mungu mwenyewe
anatambua Nguvu ya umoja anasema wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia
kulifanya” kumbe watu wakiwa na umoja kuna kuwa na nguvu kubwa ya mafanikio na
ndio maana shetani hupenda kupanda mbegu ya mafarakano ili yasiwepo mafanikio.
Umoja unaleta upako wa kiroho kama upako wa Haruni, Zaburi 133:1-3 “Tazama, jinsi ilivyo vema,
na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja.Ni kama mafuta mazuri kichwani,
Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake. Kama
umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko Bwana alikoamuru
baraka, Naam, uzima hata milele”.
Unaona kuna Baraka katika kukaa kwa
umoja kinyume chake kuna laana katika mafarakano kaangalie nyumba na familia na
ndoa ambazo hawaishi kugombana uone kama kuna maendeleo, angalia pia mataifa
wanaopigana wenyewe kwa wenyewe, tukikaa kwa umoja Upako utatiririka kutoka kwa
kuhani mkuu Yesu Kristo na kutuletea Baraka wote
Walawi 26:8
“Na watu watano wa kwenu watawafukuza watu mia, na
watu mia wa kwenu watawafukuza watu elfu kumi; na adui zenu wataanguka mbele
yenu kwa upanga.
Na Kumbukumbu la torati 32:3 inasema “Mmoja
angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi….”
Umoja unaleta ushindi wa kiroho,
kupitia umoja kunakuwa na nguvu kubwa ya kumshinda shetani, umoja unazalisha
nguvu iitwayo “Mastermind” ambayo ni kama nguvu ya nyuklia inayosababisha
kusudi lake liweze kutimia, hakuna kitakachozuiliwa kama watu watakuwa na umoja
katika lile wanalokusudia kulifanya.
Na Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni