Mwanzo 3:21 “BWANA Mungu
akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.”
Mwanamke wa Kikristo Nchini Syria akiwa Katika mavazi nadhifu kwa mujibu ta tamaduni zao
Utangulizi:
Moja ya mada ambazo zinalitesa sana kanisa
kwa miaka mingi ni pamoja na swala zima la Mavazi, swala hili limeleta mijadala
mikubwa mno na hata kulifanya kanisa ama watu wa Mungu wakose nini cha
kusimamia linapokuja swala la uvaaji, Kuna maswala mengi sana ya kujiuliza
katika swala zima la uvaaji, Mwenendo wako na mavazi yako ni swala linalopaswa
kujadiliwa kwa kina huku tukiliangalia neno la Mungu linasema nini?
Mwenendo wangu ni upi linapokuja swala la
mavazi, nina mawazo gani linapokuja swala la mavazi, Je ninakubaliana na
Maelekezo ya kibiblia linapokuja swala la Mavazi, Je Mungu hivi kweli anajali
namna ninavyovaa? Je ninatoa nafasi ya kutosha kwa uongozi wa Mungu katika kuvaa
kwangu? Maswali kama haya yakipata majibu yanayojitosheleza ndipo tunapoweza
kuona na kujua kuwa swala la mavazi kwa mtu wa Mungu ni swala nyeti sana, wengi
tunapenda kuhitimisha kwa kusema tu aaaha swala la mavazi ni swala la fashion
na kwa hiyo itategemea na mtindo na dhamiri aliyonayo mtu!
Ilivyo ni kwamba Biblia ina namana ambavyo
inaeleza kwa kina na mapana na marefu namna tunavyoweza kumpendeza Mungu katika
mwenendo wetu wote, Neno la Mungu lina muongozo wa kutosha kwa wanadamu namna
na jinsi wanavyopaswa kuenenda, swala la mwenendo wetu na kuvaa kwetu
hakuhusiani tu na wanawake peke yao, kuna husiana na kila mmoja wetu, kwa sababu
mstari wetu wa Msingi unaonyesha kuwa Mungu aliwafanyia mavazi ya Ngozi ADAMU
na MKEWE na akawavika.
Kusudi kubwa la somo hili ni kuchunguza kwa
umakini Mafundisho ya kibiblia kuhusiana na mavazi, kwa ujumla kwa wanawake na
wanaume na kwa watu maalumu, yaani kwa wanaume na pia kwa wanawake ili tufahamu
ni yapi yaliyo mapenzi ya Mungu juu ya mwenendo wetu na kuvaa kwetu, ili kwamba
tuishi sawa na mpango ambao Mungu ameukusudia kwetu tukimpendeza Yeye na
wanadamu. 2Wakoritho 8:20-21 “Tukijiepusha na neno hili, mtu asije akatulaumu kwa habari ya
karama hii tunayoitumikia; tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana
tu, ila na mbele ya wanadamu.” Linapokuja swala la mwenendo wetu ni
lazima tufikiri yaliyo mema sio mbele za Bwana tu ila na mbele za wanadamu,
kila mtu aliyeokoka anapaswa kuhakikisha kuwa hana lawama katika mwenendo wake
wote, kwa msingi huo ni muhimu kuhakikisha kuwa mwenendo wetu pia unaendana na
kuvaa kwetu sawa na Mungu anavyotarajia mtu wake avae!.
Viwango vya
Mungu katika mwenendo wa kuvaa kwetu!
1Timotheo
4:12 “Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe
kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na
usafi.”
Neno la Mungu linaonyesha kuwa kuna kiwango
cha mwenendo ambao Mungu ameukusudia, ili kwamba wakristo tuweze kutembea
katika mwenendo huo. Kwa msingi huo basi ni wazi kuwa kila kitu katika maisha
yetu kuna namna ambavyo Mungu anakusudia tuishi kwa kusudi la Kumpendeza yeye,
Biblia ina kitu cha kutuambia kuhusiana na mwenendo mzima tunaopaswa kuenenda,
Biblia ina majibu ya maswali yote magumu na mepesi ambayo ni muongozo mwema
katika maisha yetu na mwenendo wetu, Mungu anayo majibu vilevile namna
tunavyoweza kuenenda katika tabia na mavazi yetu.
Swali la Msingi je Mungu ana viwango katika
mwenendo wa kuvaa kwetu? Wengi wetu tunaweza kuwa na imani kuwa Mungu hana wala
hajaweka msingi wa mwenendo wa namna ya kuvaa kwetu, au watu wake wavae vipi,
tunaweza kufikiri tu kuwa ni vema kuvaa kwa heshima kulinga ana fasheni
zilizoko, au tunaweza kusema wako watu hawavai kwa heshima kulinga na hali ya
utandawazi na hivyo twaweza kudhani kuwa swala la mavazi ni swala huru hivyo
kila mmoja anaweza kujivalia kama anavyotaka tu. Hivyo swala la mavazi ni swala
la mtu binafsi na mazingira yake tu na kila mtu na ahukumu moyoni mwake namna
impasavyo kuvaa!
Swala lingine la kujiuliza Je wadhani Mungu
mwenye haki hakuwa na ujuzi kuwa kutakuwa na mavazi?, Yeye ambaye ni
mwanzilishi wa mavazi; wadhani ya kuwa hakuelewa kuwa utafika wakati tutakutana
na changamoto hizi tunazokutana nazo? Inawezekanaje Mungu mwenye haki akataka
sisi tuwe watakatifu katika mwenendo wetu wote alafu kisha akaacha tujivalie
kama tupendavyo? Angalia andiko hili 1Petro
1:15-16 “bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu,
ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa,
Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.” Kwa msingi wa andiko
hili utaweza kugundua kuwa Mungu anataka tuwe watakatifu katika mwenendo wetu
wote yaani ikiwa ni pamoja na namna tunavyovaa! Haiwezekani uwe msomi wa
maandiko kisha useme ahaaaa Mavazi sio ya kuyazungumzia! Ahaaa ni watu
waliofilisika kiinjili tu ndio wanaoweza kuzungumzia mavazi, ahaaaa ni makanisa
yaliyojaa sheria yanayobania watu uhuru ndio ambayo yanaweza kuzungumzia
mavazi! Ahhaaaa ni wachungaji
wasiotembea ndio ambao wanaweza kuzungumzia mavazi, aaah ni watumishi washamba
tu ndio wanaoweza kuzungumzia swala la mavazi, kama kuna theolojia ya maombi,
kuna theolojia ya kuabudu, basi ni lazima tukubaliane wazi kuwa kuna theolojia
ya mavazi na kama ulikuwa hujawahi kupitia darasa hilo basi ni vema sasa ukawa
mpole ili wote kwa pamoja tuiangalie Biblia inasema nini juu ya mwenendo wetu
na kuvaa kwetu. Ni lazima tukubali kuelewa kuwa Mungu ameweka viwango vya namna
na jinsi inavyotupasa kuenenda! Kwa nini na ni viwango gani? Ikiwepo pamoja na
kuvaa kwetu.
1. Mwili ni hekalu la Mungu!
Mwili wa Mtu
aliyeokoka ni hekalu la Mungu, ni hekalu la Roho Mtakatifu, kwa msingi huo ni
lazima ujue wazi kuwa mwili wa mtu asiyeokoka ni hekalu la shetani na mapepo,
kwa hiyo kuna tofauti kubwa kati ya mwili wa Mtu aliyeokoka na mwili wa mtu
asiyeokoka sisi tunatajwa kuwa ni hekalu la Mungu yaani Mungu anakaa ndani
yetu! 1Wakoritho 3:16 -17 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho
wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu
atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.”
Sio hivyo tu Yesu mwenyewe alisema mtu akimpenda atayashika maneno yake na
Baba atampenda na kuja kukaa ndani yake Yohana 14:23 “Yesu
akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu
atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.” Unaweza
kuona sasa kuwa ni wazi kabisa mtu aliyeokoka mwili wake ni Hekalu la Mungu, ni
mahali akaapo Mungu, Hekalu lilijengwa vipi maeneo yote nyeti katika hekalu la
Mungu yalifunikwa kwa mapazia maalumu, hii ilikuwa ni muonekano wa nje wa
hekalu, kutunza sehemu yenye uwepo wa Mungu. Wewe sio mtu baradhuli wewe sio wa
hovyohovyo mwili wako ni makazi ya Mungu wewe ni ikulu, ikulu haiwezi kuwa
mahali pa hovyo hovyo! Wewe kama ni
hekalu la Mungu basi hekalu haliwezi kuwa mahali pa hovyo hovyo, wewe ni makazi
ya Mungu Baba na Mungu mwana na makazi ya Roho Mtakatifu Mungu yu atembea ndani
yako je ni sawa ukakaa uchi? Ili hali ndani yako uko uwepo wa Mungu? Unaweza
kuona! Kwa vyovyote vile hatuwezi kuachilia miili yetu hovyo!.
2. Ole wake yeye asababishaye Makwazo!
Linapokuja
swala la uhusiano wako na Mungu, wewe pekee ambaye ndio hekalu la Mungu kisha
ukawa uchi, au unaoga, au ukawa unashiriki ngono na mumeo au mkeo au umelala
uchi Mungu hana neno na wewe, yeye bado yuko pamoja nawe, uhusiano wake na
Adamu katika Bustani ya Adeni haukujali hali ya Adamu kuwa uchi, yeye ndiye
aliyetuumba, ni baba yetu mikononi mwake sisi ni tupu tu, japo kama unapiga
magoti kuomba ni vema ukavaa nguo au ukajifunika Mungu ni baba yetu lazima
tumuheshimu kupitia miili yetu. Nakazia tena unaweza kuvaa nguo au kujifunika
iwapo umekusudia kupiga magoti na kusali.
Sasa ingawa
Mungu hakuna la kumkwaza lakini katika neno lake ameonya kuwa ni ole wake yeye
asababishaye makwazo! Hapa ni lazima tutangulie kufikiri yaliyo mema mbele za
Mungu na wanadamu, Kwa mtu aliyeokoka ni lazima afahamu kuwa kuvaa kwetu
kunamuwakilisha Yesu Kristo, watu waliomwamini Yesu wanaitwa wakristo kwa
msingi huo maisha yetu ni lazima yamwakilishe Yesu Kristo, na kwa sababu hiyo
tunapaswa kuwafikiri sana wanadamu tunapovaa ili kwamba tusiwakwaze na
kuwafungia mlango au kuwatoa nje ya Mpango wa Mungu kupitia mwenendo wetu na
kuvaa kwetu, Kama kuvaa kwetu kutasababisha makwazo kwa wengine ni lazima tujue
kuwa tutakuwa na hatia kwa kukwaza wengine!
Marko 9:42 “Na
ye yote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe
jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini.”
Hayo
yalikuwa maneno ya Yesu mwenyewe kuhusu kuharibu mioyo ya wengine! Je Mafundisho
ya mitume yanasemaje juu ya kukwaza wengine? Paulo anasema hivii!
1Wakoritho 8:13 “Kwa hiyo, chakula
kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza
ndugu yangu.” Ahaaaa unaweza kuona kumbe basi kama mavazi haya yanamkwaza ndugu
yangu je?. Sitayavaa hata milele nisije nikamkwaza
Ndugu yangu. Mkristo wa kweli wakati wote hatafikiri mambo yake tu atafikiri na
mambo ya wengine, hatupaswi kuwakwaza wengine katika jambo lolote na kwa msingi
huo Mkristo ambaye amekomaa kiroho na anaweka upendo wa Mungu mbele hatakubali
kuvaaa katika namna ambayo itawakwaza watu wengine na hivyo kufungiwa jiwe
kubwa shingoni na kutupwa kilindini hakutamuhusu!
Tunaweza
kudai kuwa katika Kristo tuko huru na tunaweza kujifanyia lolote tulipendalo
lakini biblia inaonya kuwa uhuru wetu usiwe kikwazo kwa wale wenye imani dhaifu 1Wakoritho 8:9
“Lakini angalieni
huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu.” Biblia ya
kiingereza ya New Living Translation inasema “But you must be careful so that your freedom does not cause others with
a weaker conscience to stumble” na biblia ya kiingereza ya NKJV inasema “But beware that lest somehow this liberty of yours become a
stumbling block to those who are weak.”
Uhuru
au haki tuliyo nayo katika Kristo haipaswi kutumiwa kijinga bali kwa tahadhari
ili tusiwakwaze wengine. Kanuni hii inahusiano na mambo yote kukiwemo kuvaa
kwetu.
3. Wala msiifuatishe namna ya Dunia hii.
Warumi 12: 2 “Wala msiifuatishe namna ya
dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi
ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” Andiko hili
linaweza kuunganishwa na lile la 1Yohana
2:15 “Msiipende
dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba
hakumo ndani yake.”
Neno la Mungu lnasema “Wala msiifuatishe namna ya Dunia hii” kwa
lugha ya kiingereza tunaweza kusema “And be not conformed to this world”
tafasiri halisi ya neno comformed ambalo limetumika katika Biblia ya kiingereza
ni “Be similar in form or type or agree
or behave according to socially acceptance convention acceptable or standards”
Hapa Neno la Mungu lina maanisha wala msiifuatishe
namna ya dunia hii yaani kwanza kabisa wakristo wasiishi sawa na watu walio
chini ya sheria ya Musa, wala tusiwe kama wayahudi ambao waliishi chini ya
sheria za kidini, lakini kwa nia njema sisi tusifanane nao, wala tusiishi sawa
na kiwango chao, ambacho ni cha chini, wala tusiwafanye wao kuwa mfano wala
kuwa na tabia kama zao au za jamii yao, lakini vile vile wakristo hawapaswi
kuwa kama mataifa yale yasiyomjua Mungu wala tusifanane nao, wala kuishi kwa
kiwango chao au kuwa na tabia kama zao, wala muonekano kama wao, hii maana yake
ni kuwa Mungu anatutarajia sisi kuwa tofauti na Wayahudi walioshi chini ya
sheria za Mungu lakini vile vile tuwe tofauti na mataifa yasiyomjua Mungu, Kwa
msingi huo Basi Mungu anamtarajia Mkristo kuwa na kiwango cha juu cha kuigwa na
watu wote, Kuanzia mtazamo wetu akili zetu, uwezo wetu na muonekano wetu, Mungu
hakutokumboa katika sheria ya Musa ili tuishi kama Mataifa hapana, Mungu
alitukomboa katika sheria ya Musa ili sisi tuwe kielelelezo kwa Wayahudi na
Wayunani pia, sisi tuwe na mfumo mpya na mwenendo mpya ambao kila mtu
atakayeuona atasema kweli hawa ni wanafunzi wa Yesu, Mwanafunzi wa Yesu ana
mfumo mpya wa kuigwa na sio kuigiza
1Petro
3:1-5 “Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu;
kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo
lile Neno; wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. Kujipamba kwenu, kusiwe
kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho
ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo
walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii
waume zao.”
Neno la
Mungu linatutaka tuwe kielelezo kiasi ya kwamba wasioamini waweze kuvutiwa kuwa
haya ndio maisha! Kanisa linapaswa kuelewa hili, haiwezekani sisi ndio tuwe
tunavutiwa na dunia, Dunia inapaswa kuvutiwa na sisi hasa kwa kuonyesha
mwenendo wetu ulio safi, swala hili ni katika kila eneo la Maisha yetu, Petro
anakazia kuwa wanawake waliookoka wanaweza kuwavuta waume zao kupitia mwenendo
wao mwema! Sasa kama mtu aliyeokoka ataendenda katika kuvaa kwake sawa na watu
waliochoka wa dunia hii mbovu wale wanaoutazama mwenendo wetu watavutwaje kuja
kwa Yesu?
Endapo sasa
tutavaa na kuenenda kama watu wa ulimwengu huu ni wazi kuwa tunaupenda
ulimwengu na ni wazi kuwa tunaifuatisha namna ya dunia hii na kwa sababu hiyo
kumpenda Mungu hakumo ndani yetu, Kumbuka kuwa Kanisa ni chumvi ya ulimwengu
tunapochanganyika na watu wa Dunia na kuwa kama wao tunapoteza ladha na ubora
wa Ukristo wetu utakuwa wapi?
Mathayo 5:13 “Ninyi ni chumvi ya dunia;
lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa,
ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.”
Kanisa lina wajibu wa kuwatunza Wayahudi na Mataifa
mengine, lina wajibu wa kuwa kielelezo kama tukishindwa tutatupiliwa mbali kama
walivyotupwa wayahudi, sisi ni kielelezo sisi ndio mfano wa kuigwa sisi
ndio Mungu anataka wale walio gizani
watufate watuone
Mathayo 5:14-16 “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa
juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya
kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo
yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni”
unaona Yesu anazungumza maneno mazito sana kwa Kanisa
kwamba sisi ndio kielelezo sisi ndio mfano tunapaswa kuishi katika viwango vya
juu mno kiasi ambacho watu watamtukuza Mungu kwa kwa kuyaona Matendo yetu ni
ujinga na upuuzi wa hali ya juu kuvaa katika kiwango ambacho kila mtu atapata
maswali kuhusu Mungu wako ni aibu kwamba duniani watu wanatembea uchi na
kuutukuza uchi kisha sisi tukawa tunaunga mkono swala hili huku tukidai kuwa
sisi ni wanafunzi wa Yesu, kuna wakati huitaji kutambua kuwa huyu ni
mwanajeshi, au Polisi au Muuguzi kwa sababu mavazi yao yanawatambulisha sisi
hatuwezi kuwa na uniform kama wao lakini tunaweza kuwa na mwenendo wetu na
uvaaji wetu nadhifu utakaomfanya mtu asiyeokoka aweze kutufuata!, wakati dunia
ikitusukuma kuliachia wazi Hekalu la Mungu na kufunua mapazia yake waziwazi
sisi tunapaswa kuionyesha dunia kuwa Hatuwezi kuacha maumbile yetu nyeti
yakaonekana hovyo, ni muhimu kanisa kuelewa kuwa Shetani ana mitindo yake ya
Mavazi anayo ndio anayo, na wakristo wanapaswa kulitambua hili, ni lazima
ufikie wakati tunaponunua nguo au kuijaribu tujiulize inamwakilisha nani, Je
hufahamu kuwa nguo nyingi zina alama za kishetani, ama alama zinaashiria
kuabudiwa kwa shetani lakini wakristo wa nyakati za leo wanavaa tu? Je unapovaa
alama zinazoashiria kumtukuza shetani je hujafanyika sehemu ya muhubiri wa
kishetani? Kwa sababu unapotembea unasaidia kutambulisha uwepo wake kwa sababu
hiyo ni lazima tuwe kielelelzo wala msiifuatishe namna ya dunia hii!.. sisemi
kuwa tusinunue nguo kutoka kwao viwanda ni vilevile lakini ni lazima tukangalia
kama kuna maandishi maandishi hayo yanamaanisha nini na je yanaleta utukufu kwa
Mungu au hapana na kama hapana ni kwa nini ninunue sasa?
4.
Mavazi ni ya
kuficha uchi!
Mwanzo 3:9-10, 21 “BWANA Mungu akamwita
Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa
kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha., BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe
mavazi ya ngozi, akawavika.” Msingi mwingine wa kibiblia kuhusu mwenendo
wetu na kuvaa kwetu unaweza kuonekana katika maandiko haya, swala hili linaweza
kutafasiriwa kimwili na kiroho vilevile, kama vile lilivyo neno la Mungu kuwa
siku mtakayokula matunda ya mti huu hakika mtakufa, baada ya kula matunda Adamu
na Hawa walikufa kiroho na baadaye kifo cha kimwili, pia kiroho walikuwa uchi
na waliona aibu kwa vile dhambi ni aibu, hata hivyo ilikuwa wazi kimwili kuwa
walikuwa uchi na hawakuona haya walipoumbwa, sasa walikuwa uchi na waliona haya,
Kimsingi Hapa tunaona wazi kuwa Mungu ndiye mwanzilishi wa mavazi na kusudi
lake kuu la kuwavika ilikuwa ni kuwaponya kimwili na kiroho, Damu ya mnyama
ilifunika dhambi zao kiroho lakini kimwili ngozi ya mnyama ilifunika uchi wao,
hivyo kusudi kuu la mavazi ni kufunika uchi!
Uchi ni nini ?
Uchi au kuwa
uchi ni hali yoyote ya kutokuvaa nguo au kutokufunikwa kwa nguo maeneo yoyote
yenye asili ya usiri. Hali hii ndio inayomtofautisha mwanadamu na mnyama,
Mwanadamu ana akili lakini mnyama hana akili hivyo mwanadamu anaweza
kujihifadhi lakini wanyama hawawezi, kwa msingi huo sasa uchi ni
Ni maeneo
yote ambayo kihalali yanapaswa kuonwa na mumeo au mkeo tu kwa wanandoa na
hayapaswi kuwekwa hadharani, mfano yafuatayo ni maeneo ambayo hayapaswi kuwa
wazi kwa mwanamke
1. Kifua (Maziwa au chuchu) Katika ufalme wa Mungu na katika ukristo kifua
cha mwanamke na maeneo yake yote ni uchi na ni sehemu ya siri, hivyo inapaswa
kuwa shemu ya siri na kufunikwa na Nguo Mithali 5;16-17 “Je chemichemi zako zitawanyike mbali, Na mito
ya maji katika njia kuu? Yawe yako mwenyewe peke yako wala si ya wageni pamoja
nawe” Neno la Mungu hapa linazungumza kwa hekima ya hali ya juu,
kwamba uwazi wa mkeo au mumeo ni mali yako mwenyewe wala si wa wageni, sehemu
za siri za mumeo au mkeo zinapaswa kuwa zako wewe mwenyewe na sio kila mtu
ajichotee na kujionea, Je na kwanini uonyeshe Maziwa yako? Je unataka wanaume
wote wayaone? Kisha … …unafanya dhambi
2. Mapaja – Mapaja ya mwanamke ni siri yake na inapaswa kuwa sehemu yake ya
siri, mapaja huanzia sehemu ya juu ya magoti kuelekea juu mpaka kwenye
mazingira ya kiuno au kitovu, kwa msingi huo wanawake wanapaswa kuyahifadhi
maeneno hayo, wanawake wa Kikristo ni wazi kuwa hawapaswi kuvaa mavazi
yanayoishia juu ya goti na kuacha wazi maeneo hayo isipokuwa kwa mumeo unaweza
kuacha maeneo hayo ni vema maeneo yote nyeti yakawa yanaonekana kwa mumeo tu na
sio vinginevyo, lakini unawezaje kuyaacha maeneo hayo yenye kuvutia kwa kweli
yakaonekana na watu wa mtaani lazima kuna kitu utakikaribisha.
3.
Kiuno – Mwanawake wa
Kikristo ni muhimu kufunika kiuno chake, kiuno chako ni uchi na ni siri hivyo
ni vema kikibakia kuwa siri
4. Makalio au Nyuma kwako – Ni vema ukajisitiri vema nyuma kwako, sio
vema kila mtu akaona zaidi ya mumeo, muonyeshe yeye kwaajili yan utoshelevu wa
kingono na sio wengine, kwa ujumla haya ni maeneo yenye kuwavutia sana wanaume
na kuwaletea fadhaa kubwa sana unapoachia Tako lako na umbile lake likaonekana
je wadhani Mungu atasifiwa tu kwaa uumbaji wake? Ndio atasifiwa lakini
utatamaniwa, utachochea hisia za kingono mno
5. Nguo za Ndani – Hizi ni nguo zote za ndani ikiwa na maana ya
chupi, sidiria, na kadhalika nguo hizi ni nguo za siri na hazipaswi kuonekana
kwa namna yoyote na ndio maana zikaitwa nguo za ndani au nguo za siri.
Kwa upande
wa wanaume vilevile ni muhimu kufahamu kuwa kisaikolojia wanadamu wote
wanafanana, wanawake pia kuna maeneo wakiyaona kwa wanaume wanavutiwa kama
ilivyo tu kwa wanaume wakiona baadhi ya maeneo ya wanawake wanavyovutiwa, hili
ni swala la asili ya uumbwaji tu kwa hiyo wanaume pia yako maeneo ambayo kwa
wanawake ni uchi, wote tuna paswa kulindana kwa kutokuyaonyesha maeneo hayo,
najua wako watu wanaweza kuwa na hoja kwamba kama mimi nimevaa hivi yeye
inamuhusu nini si tamaa zake mwenyewe? Jambo hili halipaswi kuwa hivi ytunao wajibu
wa kulindana na kujiepusha kusababbisha makwazo!
Jinsi gani mwanaume Mkrito anapaswa kujihifadhi?
1. Tunza kifua chako! – fiua chako hakipaswi kuonekana kwa
wanawake ni kifua cha mke wako tu uliyepewa na Mungu hivyo si vema mwanaume
akaonyesha kifua chake, wanawake wanavutiwa sana na mwanaume aliyejengaka vema
katika mazingira ya kifua kwa msingi huo kwa mwanaume Mkristo ni muhimu
kuyahifadhi mazingira hayo
2. Misuli ya Mikono yako – Misuli ya mikono yetu na ukakamavu tulio
nao kwenye mikono ukionekana na wanawake unaamsha hisia za kingono kwa hiyo ni
muhimu kwetu kuhakikisha pia tunayahifadhi maeneo hayo kwaajili ya wake zetu tu,
wanawake kwa haraka sana huangalia misuli ya mikono yetu na wanapoona mishipa
ya damu namna na jinsi iliyojengeka katika mikono yetu mawazo yao yanapaa, kwa
hiyo ni vema ukajihifadhi.
3. Nguo za Ndani – Nguo za ndani pia za mwanaume hazipaswi kuonekana wazi kwa
Mwanamke asiye mke wako, ni vema kujihifadhi na wale wanaovaa mlegezo ni muhimu
wakajua kuwa hii ni tabia mbaya sana, utafiti unaonyesha kuwa tabia ya kuvaa
mlegezo ni tabia ya kishoga na sio vema kwa mtu mwanamume aliyeokoka kuachilia
chupi yako ikaonekana je inapoonekana ni kwa utukufu wa nani?
Miili yetu haikuumbwa kwaajili ya kila mtu tu, mwili wa mwana mume
umeumbwa kwaajili ya mke wake tu na mwili wa mwanamke umeumbwa kwaajili ya mume
wake tu, hivyo wengine hawapaswi kuona kwa sababu zozote zile.
1Wakoritho
7:3-4
“Mume na ampe
mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu
ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali
mkewe.” Neno la Mungu
linadhihirisha wazi kuwa mwili wa mwanammme unamuhusu mkewe na mwili wa
mwanamke unamuhusu mumewe na hakuna amri, wao wanapaswa kuachiana na kupeana
miili yao na kutokuificha wanapokuwa faragha, huu ndio msimamo wa kimaandiko,
mbele ya uwepo wa mkeo au umeo unaruhusiwa kuvaa vyovyote utakavyo hata kama ni
kukaa uchi, kwa kusudi la kumfurahisha mwenzi wako na kutimiza hivyo mahitaji
ya kingono ya mwenzi wako, vaeni vyovyote mpendavyo mbele ya kila mmoja wenu muwapo
faraghani hapo sio tatizo.
Lakini nje yenu, hadharani mbele ya wazazi, kaka zako na dada
zako, mashemeji na kadhalika lazima uvae kwa heshima, na kujifunika maeneo yote
yenye kutafasirika kama uchi kwa jamii yako lazima yafunikwe.
Roho
ya kutokujali kuwa itakuwaje kwa wengine kaka au dada zangu wakiingia
majaribuni kwaajili yako haitokanani na Mungu, Mkristo wa kweli lazima ajali
kwamba nisije ni kasababisha makwazo na kuangusha dhambini wengine, Uhuru wako
usiwe sababu ya kusumbua wengine na kuwaingiza dhambini angalia 1Wakoritho 8:9 “Lakini
angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu.” Toleo
lingine la maandiko haya linasomeka Lakini angalieni huu uhuru wenu usije
ukawakwaza wale walio dhaifu. Mkristo
wa kweli ataishi sawa na viwango anavyovitaka Mungu, ataenenda kwa uadilifu na
kuvaa kwa uadilifu akijali uwepo wa Mungu na sio dunia itakavyo.
Je ni halali kukaa uchi Hadharani?
Kama kuwa
uchi hadharani ndio maendeleo na fasheni au ndio mtindo wa kisasa, na Mkristo
akaamua kuwa kama watu wa dunia hii inavyotaka ukweli ni kuwa unatenda dhambi
1Yohana 2:6 “Yeye asemaye ya kuwa anakaa
ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.”
Wakrito ni
wale wanaomfuata Yesu maana yake ni wale wanaoenedna kama yeye mwenyewe
alivyoenenda kwa msingi huo lolote lile ambalo tutalifanya ikiwemo kupiga picha
ambazo hazina uadilifu kama wa Kristo na kuzitupia katika mitandao ya kijamii
kama facebook, twitter, Instagram, google plus, whatssapp na kadhalika na
zikaonekana hadharani ukweli ni kumvunjia Mungu heshima si jambo jema kabisa
kwa Mkristo kueneza picha za utupu ama za kwakwe au za mtu mwingine, utupua ua
uchi umekuwa ndio mvuto mkubwa sana wa aina binadamu na kuwafanya wengi kuzama
katika mwenendo wa kishetani sisi sio wa ulimwengu huu na kama tutakubaliana na
kila kitu cha ulimwengu huu nazungumzia mfumo wa utendaji wa ibilisi, maana
yake kumpenda baba hakumo ndani yetu.
1Yohana 2;15 “Msiipende dunia, wala mambo
yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.”
Picha za
wanaume au wanawake walioko uchi na nyinginezo zinawakilisha wazi kazi za
ufalme wa shetani, ni kupitia picha hizi shetani na majeshi yake yaani mapepo
wanafanya kazi ya kuwavuta watu katika tamaa na kuinua hisia za kingono zisizo
halali, kwa hiyo ukiacha kuvaa tu ni vema na uadilifu kabisa kwa wakristo pia
kuacha mara moja kusambaza picha zenye kuonyesha utupu wa wanadamu, au
kuzitazama uchi ulileta laana kwa kizazi cha kanaani
Mwanzo 9:20-27 “Nuhu akaanza kuwa mkulima,
akapanda mizabibu; akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. Hamu,
baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili
waliokuwa nje. Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote
wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao
zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao. Nuhu akalevuka katika ulevi
wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea. Akasema, Na alaaniwe Kaanani;
Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake. Akasema, Na atukuzwe BWANA, Mungu wa
Shemu; Na Kaanani awe mtumwa wake. Mungu
akamnafisishe Yafethi, Na akae katika hema za Shemu; Na Kaanani awe mtumwa wake.”
5. Wengine watatamani tu bila kujali umevaa nini?
Yakobo 1:14-15 “Lakini kila mmoja
hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile
tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa
mauti”.
Ni muhimu
kufahamu na ikaeleweka wazi kuwa ni kweli wako watu ambao wanateswa na tamaa tu
bila kujali umevaaje watu wanateswa na roho ya tamaa wapo, watakutamani au
watatamani bila kujali mtu amevaa nini, lakini ni muhimu vilevile ikaeleweka
wazi na hata watu wa dunia hii wanajua wazi kuwa kuna muuunganiko wa kile mtu
amekivaa na tamaa, na hili linaweza kuchangiwa na jinsi wanaume na wanawake
wanavyovaa hasa katika mitindo ya kisasa.
Na ndio
maana matangazo mengi ya bidhaa hapa duniani hayawezi kutangazika bila kuweko
mwanamke mrembo au mwanaume mrembo wenye aina fulani ya mtindo wa kisasa
wakihusishwa na kutangaza matangazo hayo, kwa nini kwa sababu Dunia inajua kuwa
ukitaka mtu aangalie kitu au bidhaa au akitamani huna budi kuweka picha za aina
hiyo ya watu sasa swali je na Wakristo tunapaswa kufanya hivyo? Hatupaswi
kuichochea tamaa hata kama wako watu wenye tamaa, na tunapaswa kukumbuka kuwa
tamaa huzaa dhambi na kisha huleta mauti hivyo ni vema tukaidhibiti, ndani yetu
au sisi kuwa sababu ya watu wengine kutamani. Kila mtu anawajibika au
atawajibika kwa tamaa aliyo nayo
Mathayo 5:27-30 “Mmesikia kwamba imenenwa,
Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani,
amekwisha kuzini naye moyoni mwake. Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe
ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili
wako mzima usitupwe katika jehanum. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate
uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili
wako mzima usitupwe katika jehanum.”
Mungu anamtaka kila mmoja awajibike kudhibiti tamaa ndani
yake bila kujali kuwa mtu mwingine anavaaje
2Wakoritho 10;3-6 “Maana
ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali
zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu
kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira
ipate kumtii Kristo; tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu
kutakapotimia.”
Ni lazima tuhakikishe kuwa fikra zetu zinamtii Kristo,
mapambano ya kuushinda ulimwengu yako katika ufahamu wa mwanadamu, Hivyo kila
mwanadamu anapaswa kupambana na tamaa itendayo kazi ndani yake bila kusahahu
kuwa shetani hutumia watu katika kutekeleza majukumu yake
Mathayo 16:21-23. “Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya
kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa
makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Petro akamchukua,
akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. Akageuka,
akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi
yaliyo ya Mungu, Bali ya wanadamu.”
Unaweza kuona kwa msingi huo basi ni ujinga kufikiri kuwa
huwezi kujihifhadhi katika kiwango
ambacho kitamfanya mtu mwingine asitamani eti kwa sababu wako watu
wanatamaa hapana ni muhimu kufahamu kuwa neno la Mungu halitaki sisi tuwe
kikwazo kwa wengine na hivyo ni muhimu kujihifadhi, Warumi 14 inafundisha namna
na jinsi tunavyopaswa kuepuka kuwa kikwazo kwa wengine, ni ujinga kufikiri kuwa
unaweza kufanya mambo kuwa rahisi au magumu kutokana na kuvaa kwako la msingi
usiwe sababu ya mwakwazo kwa wengine warumi 14 iko wazi kuhusu hilo.
Wanawake wa
Kikristo Nchini Syria wakiwa katika ibada
6.
Kila mtu aliyeokolewa ni Balozi wa Mungu.
2Wakoritho
5:20 “Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba
Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe
na Mungu.” Neno hili la muhimu katika lugha ya kiingereza linasomeka “Now then we are ambassadors
for Christ” Neno hili linatumika kwa sifa sawa na Waefeso 6:20 “ambayo kwa
ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri katika huyo
kunena jinsi inipasavyo kunena.” Neno hilo mjumbe maana yake ni balozi “I
am an ambassador in bonds”Kwa asilineno hilo limetokana na neno la Kilatini
“Ambasciator” na likapata umaarufu katika lugha ya kirumi na ufaransa na
uingereza, Likimaanisha mjumbe au balozi ambalo kwa lugha nzuri na nyepezi
nimwalikishi, kila mtu aliyeokoka ni mwakilishi wa Yesu Kristo, balozi ni mtu
anayewakilisha badala ya hivyo sisis tunamuwakilisha Kristo ni mabalozi wa Yesu
Kristo ni mabalozi wa serikali ya Mungu, ni mabalozi wa ufalme wa Mungu, vile
alivyo balozi na heshima aliyo nayo ndivyo ilivyo na serikali anayoiwakilisha,
Miaka kadhaa iliyopita uingereza ilitaka kuleta balozi shoga hapa Tanzania na
Rais aliyekuweko madarakani alikataa, tulikataa kumpokea, kwa sababu kwetu
hatujahalalisha na kukubaliana na tabia hizo, awaye yote anayemwakilisha Kristo
anapaswa kuenenda kama Kristo mwenyewe alivyo, muonekano wako na mtazamo wako
unamwakilisha Kristo na hivyo ni muhimu kwako kujihoji na kujiuliza kuwa namna
unavyovaa je inaaakisi maana nzima ya kuwa wewe ni balozi wa masihi? Je
unamwakilisha vipi Yesu katika muonekano wako, Kama ilivyo ni kweli Yesu ni
mfalme wa wafalme katika Serikali yake je angekuchagua uwe balozi wake je
angechagua mtu wa namna gani? Na kama Yesu anaweza kumchagua kila mtu kwa kuwa
ni Mungu je wewe kwa Heshima aliyonayo Yesu Kristo ungeamua kumuwakilisha namna
gani? Kule kuvaa kwako, mwenendo wako na muonekano wako unapeleka ujumbe kuwa unatokea serikali ya namna gani je
unamwakilisha Mungu au unamwakilisha shetani?
7. Mavazi yako ni utambulisho wako.
2Wafalme
1:7-8
“Akawaambia, Je!
Mtu yule aliyetokea, akaonana nanyi, akawaambia maneno hayo, alikuwa mtu wa
namna gani? Wakamwambia, Alikuwa amevaa vazi la manyoya, tena amejifunga shuka
ya ngozi kiunoni mwake. Naye akasema, Ndiye yule Eliya Mtishbi.”
Nabii Eliya nyakati za agano la kale alitambulika kwa namna na
jinsi alivyokua anavaa, mavazi yana sehemu kubwa sana ya kukutambulisha,
Tunaona katika maandiko wakati Musa alipokuwa amekimbia Misri kuelekea Midian
wale walimuona kwa vile alikuwa amekulia kwa Farao walimtambua kama Mmisri kutokana
na uvaaji wake angalia Kutoka 3:16-19 “Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja
wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao.
Wachungaji wakaja wakawafukuza; lakini Musa akasimama, akawasaidia, akalinywesha
kundi lao. Walipofika kwa Reueli baba yao, akasema, Imekuwaje hata mkarejea
mapema leo? Wakasema, Mmisri mmoja alituokoa katika mikono ya wachungaji, tena
zaidi ya hayo, akatutekea maji, akalinywesha kundi.”
Kutokana na kukulia katika mazingira ya nyumba ya Farao na
utamaduniwa Misri Japo Musa alikuwa Muebrania alionekana kama Mmisri, Sababu
kubwa ilikuwa ni Mavazi yake kumbe mavazi yana uwezo mkuwa sana wa
kumtambulisha mtu, aina yake haiba yake tabia yake na mwenendo wake lakini hata
utaifa wake na wakati mwingine kazi yake, kwa msingi huo hata wale wanaojiuza
au makahaba utambulika kirahisi kuwa makahaba kutokana na mavazi yao na
ukatongozwa, wakati Fulami mwanamke mmoja aliyeitwa Tamari alivaa mavazi ya
kikahaba na Yuda mwana wa Israel alimtongoza na kuingia kwake kwa kudhani kuwa
alikuwa kahaba na kumbe alikuwa mkwewe ona katika
Mwanzo 38:15
“ Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji,
akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna.
Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, wala hakuozwa awe mkewe. Yuda
alipomwona alimdhania kuwa ni kahaba, maana amejifunika uso.”
Kuvaa kwetu kunaweza kuonyesha wazi kama sisi ni watu wa Mungu au
wasiomjua Mungu, watu wema au waovu, lazima ujihoji na kujiuliza kuwa unapovaa
unamuwakilisha nani na unapeleka ujumbe gani?!Ikiwa yako mavazi ambayo yanaweza
kueplekea wewe kutafasirika kama kitu kingine ni muhimu kwetu tukazingatia aina
ya ujumbe tunaoupeleka.
8. Ukristo ni kiasi
Tito 2:11-12 “Maana neema ya
Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na
tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu
huu wa sasa;”
Biblia
inakazia kuwa wakristo ni watu wanaopaswa kuishi kwa kiasi neno kiasi , haki na
utauwa katika biblia ya kiingereza yanasomeka hivi we should live soberly,
righteously, and godly, soberly maana
yake kwa Hekima, na nidhamu, tukijidhibiti wenyewe self control na kwa haki maana yake kwa heshima
tukizingatia sana namna wenzetu wanavyotufikiria na kwa utawauwa godly kama
vile tuko ndani ya uzima wa milele au tuko mbinguni au tuko na Mungu au kwa
utukufu wa Mungu, hii ina maana vyovyote vile tunavyofikiri ni muhimu kwetu
wakristo kuvaa kwa nidhamu tukimfikiri Mungu na majirani zetu walio nje hii ni
kanuni muhimu sana katika maisha yetu ya ukristo chochote kikizidi ni mno,
wakristo wanapaswa kulikumbuka hili siku zote za maisha yao.
Kanuni saba
za Mavazi ya Mkristo:-
1.
Yamwakilishe Yesu kuwa ameniokoa na kunibadilisha na kuwa sasa ninaishi maisha matakatifu ya
kumpendeza Yeye Warumi 12:1, “Wala
msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate
kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” Tito 2:11-12, “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi,
na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;” 1Timotheo 2;9-10, Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri,
pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu
na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo
wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.”
2.
Kuvaa vema huwa haimaanishi kuwa mtu huyu ndio yuko sawa na Mungu
lakini Mungu huangalia moyo na mwili pia. Kwamba nimechagua nguo yangu kwaajili
ya utukufu wa Mungu ama kwa sababu ya kuiangalia dunia ISamuel
16:7” Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake,
wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama
binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana
huutazama moyo.” Mithali 31:30 “Upendeleo
hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye
atakayesifiwa.”
3.
Ninachagua mavazi yangu kama mtu mwenye badiliko aliyebadilishwa
na Mungu, Warumi 6:12-13, “Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na
mauti, hata mkazitii tamaa zake; wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha
za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya
kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.” Waefeso 2;10, “Maana
tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea
awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.” Tito
2;14 “ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili
atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale
walio na juhudi katika matendo mema.”
4.
Je ninaishi kwa kuridhika na kwa kiasi Mathayo 6:28-30 “Na mavazi, ya nini
kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala
hayasokoti nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote
hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani
ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika
ninyi, enyi wa imani haba?” – Mungu
atakutana na mahitaji yetu na sio yote tuyatakayo, kama tutachukuliwa na mfumo
wa kujijali tunaweza kusahahu kuwajali wengine
5.
Je ninafuata muongozo wa Mungu ninapovaa na je ninafuata matakwa ya wazazi ninapovaa je
ninavaa kwa kuzingatia unyenyekevu? 1Petro5:5b “Vivyo
hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu,
mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa
wanyenyekevu neema.” kuvaa vema haimaanishi
kuwa kinyume na mitindo, maana yake kubwa ni kuvaa kwa makusudi ya kumpendeza
Mungu 1Timotheo 2:8 “Mkumbuke
Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daudi kama inenavyo injili
yangu.”
waamini ni lazima wajiweke katika nafasi iliyo njema na ya kuvutia watu kwa
Mungu wanapovaa na sio kuvaa kama
makahaba Mithali 7:10 “Na
tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;“
6.
Zingatia utamaduni wako, Paulo mtume alipozungumzia mavazi
alizungumza kwa mujibu wa tamaduni za warumi za wakti ule na alipokuwa
akiwataka wakristo wasiifuatishe mana ya dunia hii ilikuwa dunia ya wakati ule
hii ina maana gani? Yaani tuhakikishe kuwa kwanza hatuko kinyume na
utamaduni na mazingira yanayotuzunguka,
lakini vilevile tusivae sawa na jambo au namna inayooenakana katika jamii yako
kuwa sio sawa.
7.
Je unavaa kwa Heshima Na Uchaji wa Mungu? Mithali 31:25 “Nguvu na hadhi ndiyo mavazi
yake; Anaucheka wakati ujao.” Maisha yetu ni lazima yajawe na
kumuheshimu Mungu, lakini vilevile yajenge heshima yetu, ni lazima tujihoji
kama hiki tunachikivaa kina mpa Mungu utukufu 1Wakoritho 6:19-20, 19. “Au hamjui ya kuwa
mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu?
Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi,
mtukuzeni Mungu katika miili yenu.” 10:31,“Basi, mlapo, au
mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.” sisi sio
mali yetu wenyewe ni mali ya Mungu., lazima tulizingatie hili na kulikumbuka!
Hitimisho!
Kwa ujumla Biblia iko wazi sana kuhusu swala
la mavazi, ni swala la utamaduni na mkao wa Moyo lakini kwa makusudi muhimu
yaliyotajwa hapo juu, Kwa mfano Biblia inatambua tofauti iliyoko kwa kimaumbile
Mwanzo 1:27 “Mungu
akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke
aliwaumba.”, na inataka
kila mmoja avae kwa mujibu wa maumbile yake yaani mwanaume mavazi ya kiume na
mwanamke mavazi ya kike Kumbukumbu la
torati 22:5 “Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala
mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni
machukizo kwa Bwana, Mungu wako”. baadhi ya wanatheolojia wanaamini kuwa neno
hili lilihusu jamii ya watu waliokuwa wanavaa kama wanawake kwa kusudi la
kujificha na kushiriki zinaa kwa hiyo kwa makusudi ya kuepusha zinaa andiko
hili liliandikwa, swala hili limeinua mijadala mingi sana ya kitheolojia sasa
watu wavaeje lazima pia dhamiri ikishuhudie sawa na Neema ya Mungu iliyoko juu
yako namna unavyopaswa kuvaa Warumi
14:23, “Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana
hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni
dhambi.”
Wagalatia 2:20 “Nimesulibiwa
pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani
yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa
Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.“
Ni muhimu kufahamu kuwa kuna baadhi ya vitu
vilikatazwa katika Agano la kale kutokana na tamaduni zao kwa mfano wayahudi
walikatazwa kuvaa nguo mchanganyiko kwa wakati mmoja Kumbukumbu 22:11” Usivae nguo iliyochanganyikana sufu na kitani pamoja.” hata hivyo wataalamu wanakubali kuwa andiko
hili lilimaanisha katika halia ya kiroho kutokumshirikisha Mungu na miungu au
kuwa mshirikina ingawa hakuna anayejua kwa hakika maana ya andiko hili
Jambo moja lilillo wazi ni kuwa agano la kale
limekamilishwa na agano jipya na kuwa wakristo wako huru mbali na sheria ya
Musa iliyotolewa kwa wayahudi Warumi
8:1-2 “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao
walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika
Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.” na Wagalatia 5:13-14 “Maana
ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata
mwili, bali tumikianeni kwa upendo. Maana torati yote imetimilika katika neno
moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.” Paulo
anatoa ushauri huu kwa wanawake akimsihi Timotheo kuwaelekeza 1Timotheo 2:9-10, “Vivyo
hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na
moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za
thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa
Mungu. Petro pia anatoa hoja mfano wa hiyo katika” 1Petro 3:2-5 “wakiutazama
mwenendo wenu safi, na wa hofu. Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje,
yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa
moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na
utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba
wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao”.
Ukiangalia kwa makini aya hizo ni kama vile
mitume walikuwa wanakwepa swala zima la kuzungumzia mavazi huku wakisisitiza
utu wa ndani ambao kwa kawaida ukiwa safi na mtu nje yake atakuwa safi tu, hali
ya kimavazi kwa kweli inabadilika miaka na miaka huku kanisa nyakati zote
likipambana kupata uhakika kuwa ni mfumo gani wa kuvaa unapaswa kufuatwa, Mungu
ataokoa watu kutoka katika mkila taifa na jamii na utamaduni kwa hivyo ni
vigumu kulinganisha viwango gani kanisa limnapaswa kusimamia zaidi ya
kuzingatia isingi na dhamira ya kibiblia iliyoainishwa hapo juu, Mungu
amelikusudia kanisa lake liwe na umoja 1Wakoritho
11:20-22, 20. “Basi mkutanikapo pamoja haiwezekani
kula chakula cha Bwana; kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake
katika kule kula; hata huyu ana njaa, na huyu amelewa. Je! Hamna nyumba za
kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio
na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.” Wagalatia
3:28 “Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala
huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika
Kristo Yesu.”
Biblia imeonya kuwa tuache kuwahukumu watu,
au kuwapendelea watu fulani na kuwadharau wa aina fulani kutokana na kuvaa kwao
Yakobo 2:1-9 “Ndugu
zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa
kupendelea watu. Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu
na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; nanyi
mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali
pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu, je!
Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu? Ndugu
zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe
matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao? Bali ninyi
mmemvunjia heshima maskini. Je! Matajiri hawawaonei ninyi na kuwavuta mbele ya
viti vya hukumu? Hawalitukani jina lile zuri mliloitwa? Lakini mkiitimiza ile
sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako,
mwatenda vema. Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria
kuwa wakosaji.”
Jambo kubwa la msingi kila Mkristo anapaswa
kujifunza tu na kujiuliza swali kunbwa la msingi ni kitu gani ninataka kukisema
na ujumbe gani ninataka kuupeleka kwa kile ninachochagua kuvaa
Dua
Baba Mungu mpendwa katika jina la Yesu,
umeniumba kwa sura na mfano wako, nataka nikuheshimu wewe kwa kila kitu
ikiwemomwenendo wangu na kuvaa kwangu, tafadhali nipe hekima na ufahamu nauwezo
wa kuopambanua moyoni mwangu ili kwamba maisha yangu yakupendeze wewe na kuwa
ushuhuda na yenye kuwavutia walimwengu watakaonitazama Duniani amen!
Mwenendo wangu na Mavazi yangu kwa mujibu wa
Quran
Kwa vile inawezekana kuwa ngumu kujifunza na
kuelewa kutoka kwa Biblia kutokana na tafasiri tofauti za namna ya kuvaa ni
muhimu kufuatana nami kama mkuu wa wajenzi na kujifunza somo hili kwa upande wa
pili yaani wana wa Ishmael wao wanaesemaje kuhusu mwenedno wetu na kuvaa kwetu
kwa mujibu wa Quran fuatana nami
Mwenendo wangu na kuvaa Kwangu
“2”
Mstari wa Msingi: Surat Al- Ahzaab 33: 35 “Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake na waumini
wanaume na waumini wanawake na watiifu wanaume na watiifu wanawake na wasemao
kweli wanaume na wanawake na
wanaosubiriwanaume na wanawake na wanaofunga wanaume na wanawake na watoao
sadaka wanaume na wanawake na na WANAOJIHIFADHI TUPU ZAO wanaume na wanawake
wanao Mdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi wanaume na wanawake Mwenyezi Mungu
amewaandalia Msamaha na ujira mkubwa”
Utangulizi:
Ni
muhimu kufahamu kuwa Quran inazungumza kwa uwazi na upana sana kuhusu tabia na
mwenendo ambao watu wa Mungu wanapaswa kuuenenda, na ahadi kubwa ya Mwenyezi
Mungu kwa wale watakaoenenda sawa na
njia za mwenyezi Mungu au wenye kujitia nia katika kutenda matendo mema na
mojawapo la Msingi ikiwa ni pamoja na WANAOJIHIFADHI TUPU ZAO yaani wanawake
kwa wanaume wanaojihifadhi wanaovaa kwa nidhamu hawa wana ahadi ya msamaha na
thawabu kubwa sana kwa Mungu.
Maandiko
yanamtaka kila mtu Mcha Mungu kutilia maanani swala zima la mavazi, usafi na
nidhamu wakati wote tunapijihusisha na watu wengine na pia wakati wa ibada
Quran inasema katika Surat Al-‘Araaf
7:31 “Enyi wana wa Adamu Chukueni pambo lenu kwenye
kila pahala wakati wa ibada , na kueleni na kunyweni na wala msifanye
ubadhirifu kwa hakika yeye hapendi wanaofanya israfu”
Mungu
anataka watu wavae vizuri kwa heshima na nidhamu tena wavae mavazi nadhifu
yanayowapendeza na yenye muonekano mzuri kwa kufanya hivi waamini watakuwa
wanampendeza mwenyezi Mungu na kutii neno lake Surat Al-‘Araaf 7:32 “ Sema Ni nani
aliyeharimisha PAMBO la mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo
vizuri katika riziki, Sema hivyo ni kwa walio amini katika uhai wa duniani na
siku ya kiyama vitakuwa vyao wao tu,. Namna hivi tunazieleza Ishara kwa watu
wanaojua.”
Kwa
lugha Nyepesi qurani inazungumza katika eneo hili kuwa ni nani amewakataza
PAMBO yaani nguo nzuri nadhifu ambazo Mungu amewabarikia watu wake au vitu
vilivyo vizuri katika riziki yaani chakula, ni wale wanaoamini kuwa wataendelea
kuwepo duniani hata baada ya siku yamwisho ili vitu hivyo view vyao. Mungu
anataka kama una mavazi mazuri yaliyo nadhifu uyatumie sasa na katika ibada na
zaidi sana kama kuna chakula kizuri ukitumie sasa hii ndio ishara nya watu
wanaojua yaani watu wanaojua kuwa duniani tuko leo na kesho hatuko
Kwa
nini maneno ya Mwenyezi mungu yanasisitiza kuvaa kwa unadhifu tena kuvaa vizuri
na tena kwamba kuna dhawabu kubwa kwa watu wanaojihifadhi yaani wanaovaa kwa
kuzingatia kuficha tupu zao jambo ambalo lilianzishwa na mwenyezi Mungu. Ilivyo
ni kwamba kuna faidha kadhaa ambazo muumini anafaidika nazo kwa kuvaa kwa
nidhamu na unadhifi
Makusudi ya kuvaa kwa
nidhamu:-
1.
Mavazi
ni kwa kusudi la kujihifadhi hasa unapokuwa hadharani, Maandiko yanaeleza wazi
kuwa Mungu ndiye anayetupa mavazi na anatupa kwa sababu anataka tujihifadhi
angalia tena Surat Al-‘Araaf 7:26 “Enyi wanadamu
tumekuteremshieni nguo za kuficha tupu zenu na nguo za Pambo na nguo za uchaMungu
ndio Bora , Hayo ni katika ishara za mwenyezi Mungu mpate kukumbuka”
Unaona maandiko yanaoinyesha ya kuwa Nguo zinatoka kwa Mungu ni Mungu ndiye
aliyetupa mavazi kama vile alivyompa Adamu na Hawa walipokuwa wakali uchi,
Mungu anatuvika, na anatuvika kwa kusudi la kuficha uchi na kwa kusudi la
kumuabudu yeye hivyo mavazi ni ibada.
2.
Mwenyezi
Mungu pia ametupa mavazi kwa kusudi la kuupa mwili joto na kujikinga na madhara
ya baridi, wote tunafahamu kuwa joto na baridi ni hali zinzoweza kuleta madhara
kwa binadamu, hivyo Mwenyezi Mungu pia ametupa mavazi kwa kusudi la kudhibiti
hali hizo za hewa angalia Surat An-
Nahl,16:81 “Na mwenyezi Mungu amekufanyieni vivuli
katika vitu alivyoviumba na amekufanyieni Maskani milimali na amekufanyieni
Nguo za kukukingeni na joto na nguo za kukukingeni katika vita vyenu, Ndio
atakutimizieni neema zake ili mpate kutii” Kumbe ni dhahiri na ni
wazi kuwa mavazi ni thawabu inayotoka kwa mwenyezi Mungu na iko pale kwaajili
ya kutukinga na joto au baridi
Linapokuja
swala la Mavazi ni dhahiri kuwa watu wengine wanapinga sana na wanapingana mno
kwa sababu Mwenyezi Mungu hakuzungumzia mavazi katika njia ya uwazi sana kama
ilivyo katika Tourat na injili kama anavyozungumzia katikia Quran
Ni
qurani pekee yenye nguvu na utukufu mkubwa ambayo imesisitiza kwa namna ya
uwazi na bayana swala la mavazi kuliko katika imani za dini nyingine, Mwenyezi
Mungu ameweka sheria na utaratibu ulio wazi kabisa na ulioonyooka na wenye
sababu zinazokubalika wazi kwa nini watu wavae kwa nidhamu na uadilifu.
Sheria na kanuni
zinzooongoza katika mwenendo wetu na kuvaa kwetu.
Ni
muhimu kufahamu kuwa katika imani ya kiislamu sheria ya jumla kuhusu mavazi
inaruhusu mtu kuvaa chochote akitakacho, na wala sheria ya jumla haimkatazi
muumini wa kiislamu kuvaa ajisikiavyo nguo za aina zote ni halali isipokuwa tu
kama hazikiuki makusudi yanayohitajika ya mwenendo wa kuvaa kwetu, sheria
inakataza aina yoyote ya mavazi yatakayovaliwa yakazidi vile viwango na mipaka
ya uislamu na kuuvunjia heshima.
Mitume
walivaa mavazi yaleyale ambayo waliikuta jamii yao inavaa na wala hawajawahi
kuwapangia namna na jinsi ya kuvaa, lakini walitoa maonyo na muongozo wa namna
na jinsi inavyowapasa waamini wao kuvaa
Kanuni
ya uvaaji katika uislamu inamtaka kila mmoja avae vyovyote apendavyo endapo tu
ziko sababu za msingi za kumfanya avae hivyo, hii maana yake ni kwamba hakuna
kinachodhaniwa kuwa ni haramu katika kuvaa endapo tu kutakuwa na sababu
zilizowazi zinazopelekea mvaaji akavaa alivyovaa hii ina maana gani kama uko
chumbani vaa mavazi ya huko chumbani au jiachie wewe na mumeo au wewe na mkeo,
au kama mko ndani basi hakuna sababu ya kuficha tena yale maungo ambayo
mwanamke au mwanamme anayafunika kwaajili ya kuonyesha heshima kwa mwenza wake
anapokuwa nje, lakini wawapo faragha hakuwa cha kuwazuia na mavazi au ukaaji wa
hasara baina yenu wana ndoa sio haramu!
Qurana
pamoja na sunnah zinasema Sunan
An-Nasaa’ee 2559 “kuleni,Kunyweni, Vaeni na fanyeni ukarimu bila kubughudhi
watu wala kufanya Majivuni” hii maana yake nje ya nyumba yako kama utavaa
kikahaba au bila kujali uislamu ama dini ya haki ya mwenyezi Mungu basi
utawabughudi watu na ucha Mungu wako utaingia dosari kubwa na Mwenyezi Mungu
atakukataa.
Kwa
msingi huo Muumini wa Mwenyezi Mungu anaweza kuvaa nguo zilezile wanazovaa katika
inchi aliyojaaliwa kuwepo kwa kuzingatia mwenendo na kuvaa sawa na sheria za
kiislamu zinavyotaka au kupendekeza
Kanuni za mwenendo wa
mavazi katika uislamu.
1.
Usivae
mavazi yanayoonyesha utupu hii ni kwa
wote wanaume na wanawake Surat Al-Arraf
1:26. “Enyi wanadamu! Tumekuteremshieni nguo za
kuficha tupu zenu, na nguo zap ambo, na nguo za uchamungu ndio bora , Hayo ni
katika ishara za mwenyezi Mungu mpate kukumbuka” Nguo za kumcha Mungu
ndio bora zaidi
2.
Vaa
kulingana na aina yako ya jinsia, Katika uislam ni mauruku kama wewe mwanaume
kuvaa mavazi ya kike na kama wewe ni mwanamke kuvaa mavazi ya kiume hata kwa
kuigiza hairuhusiwi soma khadithi 4098
ya sunan Abu Daawood wamelaani wa wanaume wanaojifanya wanawake kwa kuvaa
kama wao na wanawake wanaojifanya wanaume kwa kuvaa kama wao’ pia Khadithi 5546 Saheeh Al- Bukharee
inawaelekeza wanawake kuvaa swwa na jinsia zao, Uislamu unawataka watu kuvaa
kulinga ana jinsia zao ili kukidhi haja ya uhalisia wa uumbaji wa Mungu kulinga
na jinsia zao.
3.
Hiruhusiwi
kuvaa mavazi yanavyovaliwa na wasiokuwa waislamu kwa mfano hairuhusiwi kuvaa
kama Mapadre, au makuhani wa kiyahudi, au kuvaa msalaba au mavazi yoyote
yanayoashiria utamaduni wa dini nyingine isiyokuwa islam. Sawa na khadithi ya
Sunan Abu-Daawood 4031
4.
Mavazi yanayovaliwa kwaa ujeuri inaelezwa
katika khadithi Saheeh Muslim 91 kwamba hakuna mtu mwenye kiburi moyoni mwake
atakayeingia peponi kwa maana hiyo muislamu hapaswi kuvaa kwa kiburi mwenyezi
Mungu sio tu hatawaruhusu nkuingia peponi lakini hatawaangalia kabisa katika
siki ya kiyama wanaovaa mavazi kwa misingi ya kiburi utasoma katika Saheeh Al-Bukhaare 3465 na Saheeh Muslim 2085
5.
Usilamu
pia umeonya kufaa mavazi yoyote yale yenye kuvutia hisia za watu yanaitwa kwa
kiarabu Libaas ash – shuhrah yaani mavazi yatakayofanya uonekane wa tofauti au
kila mtu akuangalie wewe mavazi yanayochota hisia za watu yaani lolote lile
litakalokufanya unateka hisia za watu Muhamad anasema awaye yote anayevaa SHUHRAH katika ulimwengu huu Mungu
atamvika mavazi ya aibu na kumnynyekesha mno wakatai wa kiyama siku ya hukumu
soma Musnad Ahmad 5664 na Sunan ibn Maajah 3607
6.
Mavazi
ya thamani kubwa mno ya kupita kawaida
yanayozidi kipato cha kawaida cha mtu hayo pia yameharimishwa, Mavazi
yakichanganywa na dhahabu na vito vya thamani kubwa na urembo urembo haya
yameruhusiwa kwa wanawake na yamakatwazwa kwa wanaume Sunan
ibin Majaa 3595 na Sunan Abu Daawood
4057
Kuleni na vaeni na toeni
kwa ukarimu na kila mmoja ajihadhari ni kiburi na majivuno na kamwe katika hayo
yote msichanganye na kiburi na majivuno Sunan An- Nasaa’ee 2559 kwa mba mpango
mzima wa kuvaa kwa mtu unategemeana na kipato chake, uchumi wake anavyowajali
masikini akiwa mbali na kiburi na majivuno bila kujali utajiri wake wala
kuwadharau masikini
Hii
ndio misingi ya mwenendo wetu na kuvaa kwetu katika uislamu
Sasa
kwanini nimeliweka somo hili? Uili kwamba usipoelewa misingi ya kuvaa kibiblia
basi uelewe misingi ya kuvaa kwa mujibu wa uislamu na usipoelewa misingi ya
kuvaa katika uislamu basi uelewe missing ya kuvaa katika Ukristo
Duah
Baba Mungu mpendwa katika jina la Yesu,
umeniumba kwa sura na mfano wako, nataka nikuheshimu wewe kwa kila kitu
ikiwemomwenendo wangu na kuvaa kwangu, tafadhali nipe hekima na ufahamu nauwezo
wa kuopambanua moyoni mwangu ili kwamba maisha yangu yakupendeze wewe na kuwa
ushuhuda na yenye kuwavutia walimwengu watakaonitazama Duniani amen!
Na
Rev. Innocent Kamote
Mkuu
wa wajenzi Mwenye Hekima!0718990796
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni