MLIPUKO
WA MFUMUKO WA MADHEHEBU (SECTARIAN MOVEMENTS)
Moja ya maswala ya
kuzingatia ni kukumbka kuwa kumekuwako na mlipuko wa Madhehebu mengi ya kiimani
katika Urkisto hata hivyo mengi ya madhehebu haya ni sect yaani madhehebu ya
Uongo lakini tunawezaje kwanza kujua kuwa dhehebu Fulani ni la Uongo ukweli ni
kuwa utagundua kuwa mengi ya hayo yanapotosha imani ya kweli iliyonyooka
Orthodox katika theolojia zao na ili kuweza kuzibaini vema ni wazi kuwa dhehebu
lolote la Kikristo lililo kinyume na Maswala Saba muhimu yafuatayo hilo liko
kinyume na imani iliyonyooka ya msingi Orthodox.
§
Yeyote anayepingana na Utatu
Isaya 48; 16, Mathayo 3; 17,28;19,1Timotheo
2;5
§ Yeyote anayepinga uungu wa Yesu Kristo
Yohana 1;1, 14, Isaya 7;14 Warumi
1;4
§ Yeyote anayepinga uungu wa Roho Mtakatifu.
Yohana 15;26, 16;8,13,14;17,Matendo
2;1-4
§ Yeyote anayekataa kuwa Dhambi ni hali halisi ya mwanadamu
Warumi 3; 10, 23. 14;23; 1Yohana
3;4,5;17
§ Yeyote anayekataa ukombozi kupitia Damu ya Yesu
Efeso 1;7, Wakolosai 1;20, Waebrania
10;12.
§ Yeyote anayekataa wokovu kuwa ni zawadi ya Neema ya Mungu
Efeso 2;8, Yohana 1;12,3;36
§ Yeyote anayekataa kuwa kuna hukumu baada ya kufa
Warumi 6; 23, Waebrania 9; 27,2Thesalonike 1;7,8.
SIFA ZA KAWAIDA ZA IMANI POTOFU CULTS.
Kwa kawaida yako maswala kadaa
ambayo yanasaidia kuzitambua imani Potofu zifuatazo ni Alama saba zenye
kuthibitisha au kutoa mwanga wa Imani potofu
1.
Maisha ya Mwanzilishi.
-
Je Ni mtu aliyejiweka mwenyewe Madarakani?
-
Je anatumia aina gani ya Jina lenye kujiinua sana Mtume? Nabii? Dr,
Mwalimu mkuu au Hata Mpakwa mafuta?
-
Je ni msiri? Ni mwenye kukiri kuwa anauwezo mkubwa na nguvu za kupita
kawaida au mwenyu kuona maono makubwa na ndoto au maswala Maruweruwe
-
Kama majibu ni ndivyo hiyo ni Dalili ya kuifahamu imani potofu
-
Imani nyingi potofu hudai kuwa kiongozi wao ni wa kimungu au yuko sawa
na Yesu au hupewa Heshima kubwa anazostahili Masihi Yesu.
2.
Ufahamu wake kuhusu Mungu.
-
Swala linine la kujiuliza kuhusu imani hizi potofu ni namna wanavyo kiri
ufahamu kuhusu Mungu je wanaaminikatika Utatu
-
Wengine humuona Mungu kama nguvu, au mtesaji au kuwa katili au ambaye
sio nafsi
-
Kunaweza kuweko kwa sanamu au alama ambazo zinapewa umuhimu na heshima
katika dini hiyo
-
Yesu anaweza kupewa heshima ya mwalimu tu au nabii au msemaji mzuri au
moja ya watakatifu tu
-
Roho Mtakatifu hapewi nafasi ya nafisi na huonekana kama Nguvu tu au
kuwa hayuko kabisa
3. Wanaweza kuwa na Maandiko yao au ya viongozi wana na hupewa nafasi kama maandiko
-
Cults mara nyingi zinakuwa na Maandiko yao au maandiko ya viongozi wao
ambayo huheshimiwa kama yako sawa na Biblia.
-
Wanaweza kuwa wanaamini kuwa kitabu chao hicho ni cha Muhimu na cha lazima katika kutafasiri Biblia
-
Wanaweza kudai kuwa wamepewa ufunuo mpya au kweli mpya maalumu kwa ajili
yao na huenda wengine hawana
-
Wanweza kusema jambo Fulani kutoka katika Biblia lakini mkazo mkubwa
unakluwa katika Vitabu vyao mfano ni
Imani ya Mormonism ambao wana biblia yao inayodaiwa kuwa ni ufunuo wa Joseph Smith ambaye alikuwa na madai kuwa anaweka sawa injili
iliyokuwa imefichwa
-
Wanaona kuwa chanzo cha maono yao ni cha kuaminiwa, ndoto na maono ni
moja ya chimbuko la imani zao
4. Wana madai kuwa wana kweli isiyopatikana popote.
-
Baadi ya imani potofu hudai kuwa wana kweli ambayo haipatikani sehemu
nyingine au wana viwango vya kiroho vya juu zaidi kuliko popote au wanamjua
Mungu vema zaidi kuliko wengine
-
Wanaweza pia kudai kuwa wengine wamechakachua kweli lakini wao wanayo
injili kamili
-
Wanaweza kudai kuwa nje ya wao wengine ni wazushi, hakuna uhuru, ni
giza ni utumwa
-
Wana weza kuchanganya maswala ya Ukristo na ya kidunia.
5.
Kuna maswala yenye kuleta maswali
-
Mara nyingi imani potofu zinakuwa
na aina za maswala yasiyo ya kikristo yenye kuleta Maswali, wanaweza kuwa na
aina Fulani ya mambo ya kuvutia sana au mapambo yenye kuvutia, au aina Fulani
ya mavazi ya kuvutia sana ya kidini, au kuwa na mtu maalumu anayewaombea nabii
muombezi au mtu maalumu sana
-
Wanaweza kuwa na hirizi au mapete makubwa maalumu,aina Fulani ya
uchezaji na ngoma au aina Fulani za maandishi ya kichawi katika ibada zao na
kwa siri maswala ya zinaa huweza kujumuishwa katika ibada
-
Wakati mwingine unaweza kuona Vongozi wao wakiwa na roho ya Uzinzi ya
kupita kawaida au kuoa wake wengi
6. Mkazo wa kutambulika kwa Dhehebu lao au kundi lao zaidi.
-
Imani potofu huwa na Tabia ya kujiona Bora au kuona dhehebu lao kuwa Bora zaidi ya
mengine
-
Wanaamuriwa kuwatii viongozi wao Bila maswalai na kutishiwa
kulaanika endapo watafanya hivyo pia
kuna kutishiwa endapo utaiacha imani hiyo unaweza kutishiwa hata kifo
-
Wanaonyesha uwezo mkubwa sana wa kuwasaidia na kuwapenda wale ambao ni wanachama wapya au
kuwaonyesha jinsi wao walivyo muhimu au kuwapa umuhimu Fulani
-
Wanajaribu kuthibiti kila swala la waamini wao ikiwemo ni kitu gani cha
kuvaa, nani wa kuoa, na wapi pa kufanya kazi.
-
Wanachkua Muda mwingi sana katika kushuhudia na kufuatilia na wako
vizuri katika eneo hilo
7.
Wokovu kwa kazi kubwa
-
Nyingi ya imani Potofu hufundisha wokovu kama unaopatikana kwa bidii za
kibinadamu au kwa kushika maswala Fulani ai sheria Fulani na kwa ujumla wazo
lao kuu ni wokovu kwa jitihada za kibinadamu
-
Kwa ujumla wanaweza kusema kitu Fulani hadharani lakini wanafanya
kingine sirini au wako tofauti na kile wanachokisema wengi kwa mfano hujiita
wakristo ingawa ukweli wanaishi tofauti na Ukristo.
KWANINI IMANI POTOFU HUFANIKIWA?
Ziko sababu kadhaa za
msingi kwanini imani potofu hufanikiwa na watu wengi hujiunga au kuzikimbilia
1. Wanatoa majibu ya mahitaji ya watu.
-
Imani nyingi potofu zinatoa majibu kwa ulimwengu huu ambao
hauna majibu ya uhakika katika maswala muhimu ya Maisha wanajibu maswali muhimu
mfano wewe ni nani na uko kwa sababu gani na wapi unakwenda
-
Kunapokuwa na maswali a kujiuliza kuhusu maisha wakati wote
imani potouf zinakuwa na majibu na kwa
ujumla wanajua ni nini cha kujibu wanatoa majibu mepesi na rahisi kwa mtu ambaye ulimwengu
haujamridhisha katika maswala yake
kulingana na hali halisi ya wakati ulioko lakini wakati mwingine majibu
yao hutokana na nguvu za giza.
2. Wanajali wanatoa wanatia moyo wanabidii
na wana mvuto wa hali ya juu
-
Wakristo wengi au Ukristo umeshindwa kuwa na hali za kujali,
kutia moyo, kuwa na bidii na hata kupoteza mvuto kwa ulimwengu jambo
linalopelekewa wengi kuvutiwa na imani hizi potofu zinazozukla
3. Imani potofu zina mkazo katika
Mafundisho na Semina za Neno la Mungu
-
Wanakazia kwa kiwangi kikubwa maswala ya Nidhamu kwa kila
mshirika kinyuma na inavyofanyika kwa
wakristo wa kweli
-
Wana uwezo wa kugundua kuwa wengine wamepungukiwa na nini na
kujaziliza ili kuwawinda wajinga pia wanaweza kusaidia katika maswala ya
kusomesha na hata kutopa elimu kubwa
4. Kujitoa na kuhusisha/kushirikisha
waamini
-
Kila muuumii hujumuishwa katika utumshi na
kushirikishwa kiasi cha kuwachukulia
muda na kuwatawala kimazingira, wanazamishwa
katika mfululizo wa matukio kiasi ambacho wanaweza kukosa muda wa
kujihoji kuhusu nini kinaendelea u[pande wa pili
-
Ukatili na hisia zavitisho hutumiwa kama silaha kwa wale
wanaoshindwa kujishughulisha vema katka wajibu wao mfano kushindwa kuchangia,
kushindwa kuleta washirika wapya, na wanakaziwa kimafundisho kiasi na kivitendo
kiasi cha kufikia hatua kuwa unaposhinsdwa kutimiza jambo Fulani unaweza
kudhani kuwa umefanya dhambi au unajisikia hatia.
5. Wana mkazo wa aina yake katika maswala
ya ufuatiliaji
-
Imani potofu zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwa eneo la
ufuatiliaji wa wale wanachama wapya, wengine wanaujuzi mkubwa sana wa kueneza
vijarida vyenye picha nzuri za kuvutia
ili kuweza kukunasa na kukuingizia mafundisho yao
-
Wana ujuzi mkubwa na wepesi wa kutumia vyombo vya habari
kama tv, Magazeti kaseti za mahubiri na redio na mengineyo kuliko imani zilizo
sahii
-
Wana mafundisho yenye maadili mema na wanaakazia na huweza
kunasa aina ku mbili za watu wale wanaoitafuta kweli na wale wanaikimbia kweli
mara nyingi hujikuta wamenaswa na imani potofu.
JINSI YA KUKABILIANA
NA IMANI POTOFU.
Ni muhimu kufahamu
kuwa tunapaswa kuzikabili imani potofu au watu wenye imani potofu katika namna
ambayo itawakomboa na kuwarejeza katika imani sahii na kuwafanya kufunguliwa
toka katika imani potofu 1Petro 3; 15 Yuda 1; 23. Njia kadhaa zaweza kutumiwa
katika kuhakikisha tunawarejeza
1. Kuwaonyesha upendo.
-
Ni muhimu kuwaonyesha upendo kivitendo kwa kufanya matendo
ya kikarimu dhidi yao kama kuwapa lifti, kuwatembelea, kuwasaidia swala hili
litawaondolea dhana potofu kuwa nje ya kundi lao hakuna upendo na endapo
itakupasa kumfuatilia mwenye jinsia tofauti ni muhimu kuwa makini muombe Mungu
na uwe mwangalifu ikiwezekana nenda na mtu zaidi hii ni kwa sababu wengi wa
imani potofu hawaongozwi na Roho Mtakatifu na weni hawajaokoka.
2. Usionyeshe kuwavutia katika kanisa
lako.
-
Ni muhimu kwanza kuonyesha kuvutiwa na mtu huyo na sio
mtazamo wake wala usiwe na haraka ya kuonyesha kumtaka ahamie kwenye imani
yako ni muhimu wakato wote kukubali
kuongozwa na Roho Mtakatifu
3. Uwe hodari katika maandiko.
-
Mtu awaye yote anayetaka kujishuhulisha na kuhudumia
waathirika wa imani potofu ni lazima awe hodari katika Maandiko ikiwa na maana
ya ujuzi halisi wa kuitafasiri Biblia na kujua kwa haraka ni wapi kuna mtego au
andiko limepindishwa ili aweze kusaidia
kuonyesha tafasiri iliyo sahii 2Timotheo 2;15.
4. Jihadhari na mabishano.
-
Lengo lako kuu ni liwe ni kumleta mtu kwa Yesu au katika
Fundisho lililo sahii ili kuokoa nafsi
na lisiwe mabishani ya kimaandiko au mijadala tu
5. Elewa mitego ya upotofu.
-
Ni muhimu kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu maandiko na
mitego inayotumiwa na imani potofu na namna wanavyoitafasiri Biblia na misamiati yake ili kuthibitisha fundisho
lao hii itakusaidia katika kuichanganua kweli
6. Uwe katika hali ya Maombi wakati wote.
-
Ni muhimu kuwa kaika hali ya kuomba wakai wote huku ukiwa unakemea na kuwafunga Pepo wa uongo
wanaokuwa wamehusika kuwafunga watu katika imani potofu wakati wote huo
unapaswa kumtegemea Roho Mtakatifu na kumuomba akuongoze ukiwafungua hao
waliofungwa
BAADHI YA IMANI AMBAZO ZINASADIKIWA
KUWA NI IMANI POTOFU
1.
IMANI POTOFU YA MORMONISM WATAKATIFU WA
SIKU ZA MWISHO.
-
Ni moja ya kanisa lenye bidii katika kufanya umisheni
Duniani na kama haki ingelikuwa inahesabiwa kwa kutuma wamishionari bsi wao
wangestahili haki hiyo wao wametuma zaidi ya wamishionari 18,000 duniani
-
Mwanzilishi wa imani hii aliitwa Joseph Smith Jr. ambaye
alizaliwa huko Sharon Vermont U.S.A. 23th December 1805, alikuwa kijana
asiyesoma aliyesumbuliwa sana na wingi wa makanisa na madhehebu na alihitimisha
kwa kusema hakuna hata moja kati ya hayo lililo sawa
-
Siku ya Tarehe 21 september 1823 alidai kuwa aliona malaika
aliyemtaja kwa jina la “Moron” Malaika huyo alimwambia na kumuonyesha mahali ambapo angeona Mbao za dhahabu za Neno la Mungu na historia ya kale ya Amerika alidai kuwa maandishi hayo yalikuwa katika
mfumo wa Kimisri ambayo aliyasoma kwa mawani za mawe alizoziita Urim na Thumim
na aliweza kusoma tafasiri ya maandishi hayo kwa msaada wa malaika huyo
aliyekuwa ametengwa naye kwa kioo
-
Alipokuwa na umri wa miaka 25 Smith alianzisha kanisa
aliloliita “The True church The restoration of the initiated by Jesus while he
was in the earth” yaani kanisa la kweli la urejesho wa kanilsa la kweli
lililoanzishwa na Yesu alipokuwa Duniani.
-
Katika jimbo la Illinois Smith alijaribu kuweka na kukusanya
mafundisho yake lakini pia alituhumiwa
kujihusisha na maswala yenye utata na
hivyo alikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa maswala ya ubadhirifu wa fedha na
kuoa wanawake wengi alikuwa na wanawake 48, baadaye vita ilitokea kati ya
wafuasi wake wa kimomon na wasio wa kimomon hivyo Smith na viongozi wengine
walikamatwa na watu wenye hasira walimpiga
kwa mawe na kuuawa na kaka yake Hyrum June 27 1844 hivyo wa Momon humuhesabia
kuwa mfia dini
-
Mrithi wa Smith aliitwa Brigham Young aliyeongozwa na Mungu
kuhamia Utah ambako alijenga mji na hekalu na kuishi huko mpaka wakati wa kufa
kwake 1877 wa mormon walifikia idadi ya 150,000
Brigham
Young
Kiongozi wa Pili wa
Kanisa la Kristo la watatkatifu wa siku za mwisho lijulikanalo pia kama
Mormonism Kiongozi huyu aliongoza wafuasi wake kuhama mwaka 1846-1847
kutoka katikati ya Jimbo la Illinois
mpaka mji wa ziwa la chumvi uitwao Utah wakiwa chini wa maingira mapya ya kiongozi
huyo kijana wakati huo Mormon walijiendeleza sana kwa kilimo na
umwagiliaji na ujenzi na kuanzisha kituo
cha vijana kilichoitwa Brigham Young Academy
kwa sasa ndio chuo kikuu cha Brigham Young University huko Provo Utah jamaa huyu alijulikana pia kwa
kuoa wanawake wengi alioa mara 27 na
inaaminka kuwa alikuwa na watoto 60
2.
Maandiko matakatifu ya Moromons
-
Kanisa la Mormon Linatambua Vitabu vikuu vine kuwa ndio
Vitabu vitakatifu
a. Kitabu cha Mormon
b. Kitabu kiitwacho The Peair of great
Price
c. Kitabu kiitwachi Docctrine and
Covenants
d. Na Biblia
-
Wanaamini kuwa Biblia ni neno la Mungu pale linapotafasiriwa
tu na wao Mormons
3.
Mafundisho potofu ya Mormons
a. Katika mafundisho yao kuhusu Mungu.
o
Kutokana na kitabu chao
cha mafundisho ya imani yao kiitwacho
the Pearl of Great Price Mormon wanatambua kuhusu Utatu wa Mungu lakini
wanaamini au wanakubali kuwa kuna miungu mingine, wanaamini pia kuwa kuna
wakati Mungu alikuwa mwanadamu na hivyo
kuna uwezekano wa mwanadamu wa kimormon kuja kuwa mungu
o Smith wakati Fulani alisema “Kama
mwanadamu alivyo ndivyo na Mungu alivyokua na kama Mungu alivyo mwanadamu
atakuwa”
Hekalu la Mormon Huko, Utah
Salt Lake City ndio makao makuu ya
Kanisa la Mormon au kanisa la watakatifu wa siku za mwisho hekalu hili
lilikamilika mwaka 1893 baada ya ujenzi uliochukua miaka 40 una minara ya
ghorofa zenye urefu wa mita 67 ambazo ni sawa na futi 220 kwenda juu.
b. Katika mafundisho yao kuhusu Yesu
Kristo.
o Wanaamini kuwa Yesu alikuwa Roho kabla
ya kuja kujitokeza ulimwenguni kama ilivyo kwetu pia lakini yeye amewekwa wakfu kuwa wa kwanza
kati ya wana wa kiroho wa Mungu
o Wanafundisha kuwa Yesu alioa wanawake
wawili Mary na Matha na inaaminika kuwa
ile Harusi ya kana ya Galilaya ilikuwa
ni harusi ya bwana Yesu mwenyewe
o Wanaamini kuwa Yesu na Shetani Lucifer
ni ndugu wote wanamuendea Mungu na
mipango yao ya wokovu na Lucifer alikusudia kuwafanya watu wamuabudu Mungu, Lakini Kristo
alikusudia kuonyesha watu namna ya
kumuabudu Mungu
o Mpango wa Lucifer ukakataliwa na Mungu
na mpango wa Yesu Kristo ukakubalika.
c. Katika mafundisho kuhusu wokovu.
o Ili mtu asamehewe dhambi anapaswa
kufanya kazi kubwa kwaajili ya wokovu
wake ikiwemo kufundisha,kushika mashariti na kufuata mfumo wa makanisa kama ya
kimormons
o Lazima kujifunza namna ya kuwa Mungu
wewe mwenyewe, wanaamini pia kuwa neema na shughuli vyote vinahitajika kwaajili
ya wokovu baadhi ya kazi hizo ni pamoja
na kutoa zaka , kushuhudia na kubatizwa
o Wanaamini pia kuwa mtu anaweza
kubatizwa kwa niaba ya ndugu zake waliokwisha kufa wanatumia andiko la 1Koritho
15; 29 wenye kubatizwa kwaajili ya wafu.
Kumbuka!
Neno hilo wenye kubatizwa kwaajili ya wafu linamaanisha wale
walioamini na kuwa wakristo na walikuwa wakibatizwa kwa sababu walitaka baadaye
watakapokufa kukusanywa pamoja na ndugu na marafiki zao waliokwisha kufa katika imani ya Kikristo
katika maisha yajayo kama hakuna ufufuo wa wad kufanya hivyo kungelikuwa ni
kazi Bure hiki ndicho Paul alichokuwa anamaanisha.
d. Katika mafundisho kuhusu Mbingu na
Jehanamu
o Kwa Mujibu wa mafundisho yao Mormons
wanaigawa mingi katika makundi makubwa matatu kwa madaraja matatu ya watu
tofauti
o Celestial – (Mbingu ya anga) hii ni
mbingu ya kwanza na ni maalumu kwa watu wa imani ya kimormon
o Terrestrial & Telestial –(Mbingu ya
ardhi) hii ni kwaa ajili yaw at wa madaraja mengine na jamii nyingine ya watu wanaobaki wataenda
kwenye giza
o Mormon wanaamini kuwa hakuna jehanamu
ya moto wa milele wala hukumu ya milele hili linawavutia sana watu wanaoogopa
hukumu.
IMANI
POTOFU YA WASABATO SEVENTH-DAY ADVENTISM.
1. Kuundwa
kwa dhehebu la S.D.A.
-
S.D.A. ni kanisa lililoundwa katika misingi ya
kurudi upesi kwa Bwana Yesu Kristo kiini
kikuu kikiwa ni unabii wa au huduma ya kinabii ya Bwana William Miller
(1782-1849) ambaye alikuwa muhudumu wa Kibaptist
-
Alikuwa amejifunza elimu ya theolojia kwa
kusikiliza tu lakini alikuwa mwanafunzi makini sana na hodari wa maandiko
akijenga msingi kupitia kitabu cha Daniel 8;14 alielewa kuwa jioni na asubuhi 2300
ni sawa na miaka 2300 na kutoka hapo alijaribu kuweka tarehe ya kuja kwa Masihi
-
Kutoka mwaka 457 B.K. nyakati ambazo Ezra
alikuwa akilijenga Hekalu na ujenzi wa
ukuta wa Yesrusalem aliongeza miaka 2300
na akajikuta anapata tarehe 21th March mwaka 1843 ambayo aliitangaza kuwa ndio tarehe ya kuja kwa masihi ingawa
haikutokea Bwana Miller alirudia tena kufanya mahesabu yake na kudai kuwa
alikosea na alipata tarehe nyingine 22th
October 1844 ambayo hata hivyo ilipita patupu tena
-
Kosa lake lilikuwa ni kujaribu kueleza Tarehe ya
kuja kwa Masihi jambo ambalo liko kinyume na Biblia inayosema kuwa kwa habari
ya siku ile hakuna mtu aijuaye Marko 13; 32.
-
Baada yake uongozi ulichukuliwa na Ellen White ambaye alisema kuwa ana madai kuwa amepewa
ufunuo kuwa bwana Miller hakuwa amekosea
kwa vyovyote kwani Kristo alikuwa
anaingia katika patakatifu pa kimbinguni
tarehe ile ya October 1844 alidai kuwa kuna hema halisi kabisa huko
mbinguni kama ilivyokuwa kwa Musa ambayo Kristo aliingia Patakatifu pa
Patakatifu na hivyo 1844 aliingia katika
mahali hapo na kuwa atakapomaliza kazi ya kuombea wenye dhambi kwa
sadaka yake ya Calvary atarudi tena duniani.
-
Mwaka 1860 ndipo imani hii ikajulikana kama
S.D.A. makao yake makuu yakiwa huko Washington D.C.
-
Leo hii kuna waamini zaidi ya milioni tatu
3 wa kisabato duniani, wanafanya
umisheni na waamini wake hujitoa sana ni maarufu kwa masomo ya afya na ulaji wa
mboga za majani na matunda huku
wakijiepusha na ulaji nyama pombe na chain a kahawa ambavyo huaminika kuharibu
afaya ya mwanadamu
2. Maandiko
maakatifu kwa wasabato
-
Wasabato wanaamini kuwa Biblia ndio mamlaka ya
mwisho na ndio neno la Mungu lakini kama ilivyo kwa madhehebu mengi ya imani
potofu ambao wanaamini kuwa maandiko yao ni ya muhimu sana katika kutafasiri
Biblia
-
Wanaamini katika kitabi kiitwacho “The Great
Controversy” (Bishano kuu) cha Bi Ellen White
kuwa kimevuviwa kama ilivyo kwa Biblia
3. Mchepuko
wa Mafundisho ya imani ya kisabato S.D.A.
-
Wasabato wanakataa kuwa kazi ya Kristo Msalabani
haikamilishi kabisa swala la upatanisho wa mwanadamu
-
Mrs White alisema Kuwa damu ya bwana Yesu ina
kazi ya kukutangazia na kukuombea msamaha kwa Mungu Baba lakini dhambi za mwanadamu hubaia bado katika
kitabu cha kumbukumbu swala ambalo ni
kinyume na maandiko Yohana 19;30,Waebrania 1;3,9;11-12.
-
Mrs white pia alidai kuwa na maono maalumu
ambapo katika maono hayo alidai kuwa
aliona Mbao mbili za sheria huku amri ya
nne ambayo inahusiana na maswal ya sabato ikiwa inazungukwa na mwanga na kutoka hapo sabato imekuwa ni moja yanguzo
ya imani ya muhimu sana kwa wa S.D.A.
-
Kushika sabato imekubalika kuwa ni moja ya njia
muhimu sana ya kazi zinazofanya Mungu akupe rehema na wokovu
-
Kumbuka!
Kushika sabato ni swala linalorudisha watu
katika utumwa ambao Kristo alikwisha kutuweka huru nao
Sabato ni agano la kudumu kati ya Israel na
Yehova
Sabato haiwezi kushikwa ulimwenguni kote kwani
ziko inchi kijiografia ambazo hazina jua kwa kipindi cha nyakati zote au
huliona jua kwa muda tu aidha ziko nchi nyingine ambao huliona jua mara moja tu
baada ya miezi sita na Biblia imeagiza kuwa moto usiwashe, wala taa wala
kupikwa siku ya sabato katika nchi ambazo ni za baridi moto ni wa lazima na
muhimu hivyo sabato ni kwa wayahudi tu
kwa wakati wake na kwa mpango wake
Soma Wakolosai 2;16,Warumi 6;14, 14;5-8
4. Kuhusu
Asili ya Kristo
-
Wasabato wanadai kuwa katika ubinadamu wake
Kristo alichukua asili ya dhambi kama waliyonayo wanadamu wengine kusudi
ajaribiwe kama tunavyojaribiwa sisi.
-
Kumbuka!
Kristo aliye na dhambi hangeweza kufaa kuwa
mwokozi hata kidogo
Musa alielekeza kutoa kondoo wa dhabihu aliye
mkamilifu
Je inawezekanaje kisicho kamili kuleta
ukamilifu?
Soma waebrania 4;15,9;14, 2Koritho 5;21,1Petro
1;19
5. Kuhusu
wakati ujao
-
Wasabato wanaamini kuwa nafsi inalala yaani
wanakuwa kama walio usingizini kati ya kifo na ufufuo
Kumbuka!
Ukweli ni kuwa mtu anapokufa roho yake huenda
kukaa na bwana lakini miili yao hulala
udongoni mpaka wakati wa ufufuo
Lakini nafsi ya mwanadamu hailali
Soma Wafilipi 1;21-23,Wakoritho 5;6-8 kumbuka
mfano wa Lazaro na yule Tajiri
6. Hatima
ya waovu
-
Wasabato wanaamini kuwa hatima ya waovu ni
kufutiliwa mbali milele na wanadai kuwa wazo la mateo ya milele halikubaliki na
kuwa liko kinyume na maandiko
-
Kumbuka!
Bilia inasema kutakuwa na hukumu ya milele na
moto wa milele na adhabu
Soma Mathayo 25;46, Marko 9;48,Thesalonike 1;7,9
Yuda 7.
IMANI
POTOFU YA MASHAHIDI WA YEHOVA JEHOVAS WITNESSES
1. Kuundwa
kwa Mashahidi wa Yehova.
-
Mashahidi
wa Yehova pia huitwa Russelism, au Mnara wa Mlinzi (Watch tower) au Millennial
Dawn.
-
Ni
dhehebu lililoanzishwa na Charles Taze Russell 1852-1916 huko Pennsylvania
U.S.A. akiwa kijana mnamo mwaka 1870 huku akiwa hana mafunzo ya kutosha kuhusu
theolojia alianzisha Darasa la Biblia
ambapo waamini wake walimfanya kuwa mchungaji, mwaka 1896 aliandka pamphlets
mbalimbali
-
Alikuwa
na woga mkubwa sana kuhusu Jehanamu ya moto
mpaka alipokutana na mafundisho a wasabato kuhusu kuja kwa Yesu Kristo
na akachukua baadhi ya mafundisho yao
-
Mwaka
1896 alianzisha Mnara wa mlinzi taasisi inayohusika na uandishi wa Tracts na
maandiko mengineyo aidha 1908 alihamishia makao yake makuu Brooklyn New York
-
Mengi
ya maandishi yake yalikusanywa katika makundi saba seven Volumes yaitwayo
Kusoma maandiko, alikubaliana na mafundisho ya kisabato kuwa Kristo aliwasili
Hekaluni 1914
-
Russel
alikuwa mtu mwenye majivuno makubwa sana akiyasifia maandiko yake kuwa ni ya
hali ya juu kama ilivyo kwa maandiko ya Paulo mtume, Martin Luther na Wycliffe
na kuna wakati alidai kuwa ni afadhali kuchagua maandiko yake kwanza kasha
Biblia baadaye
-
Mkewe
alimshutumu na kuomba talaka mwaka 1913 kwa sababu ya zinaa, kiburi na kupenda
kutawala alishutumiwa pia na magazeti kuwa ni mwenye hila aliwahi kuai
mahakamani kuwa anajua kiyunani na alipoombwa kutambua herufi alishindwa
-
Alifariki
mnamo mwaka 1916 akiwa ndani ya treni huko Texas
-
Mwaka
1917 mwanasheria na jaji msaidizi J.F. Rutherford 1870-1942 alikuwa mrithi na
kionozi wa kundi alijipa mamlaka kubwa sana kiasi cha kumfukuza yeyote ambaye
angehoji maswali kumuhusu na mnamo mwaka 1930 aliliita kundi lake Mahsahidi wa
Yehova kutokana na andiko la Isaya 43;10.
-
Rutherford
alikufa kwa ugonjwa wa kansa huko San Diego Califonia January 8th
1942 baada ya kifo chake waruth wao hawakuwa maarufu kwa jamii isipokuwa
maandiko yao yakawa maarufu na kusambazwa zaidi
-
Mashahidi
wa Yehova wanakataa dhana ya kupiga kura, kupiga saluti, kuheshimu bendera,
kuimba wimbo wa taifa, na kutumikia Jeshi pia hupinga swala la kuongezewa au
kuongeza mtu damu.
-
Mtazamo
wao kuhusu Kristo wanamuona kama kiumbe wa kwanza kuumbwa na Mungu ambaye
baadaye alishirikishwa na Yehova katika uumbaji na hivyo Yesu sio Mungu na kuwa
hakuna utatu, Roho Mtakatifu kwao ni nguvu za Mungu tu na sio nafsi
2. Imani
yao kuhusu maswala yajayo.
-
Walitabiri
kuwa ulimwengu ungefikia mwisho mnamo mwaka 1914,1918,1920,1925 na 1941 na pale
inapotokea kuwa mwisho haukufika walijaribu kuweka vema hesabu zao walijumuisha
miaka 6,000 ya uumbaji na kupata (4026.B.K.) na walitabiri kuwa Yesu atakuja
mara ya pili 1975 B.K.
-
Kwa
sasa wanaazamia vita vya Harmageddon na ufufuo wa watu 144,000 ambao ni
mahshidi waliotiwa muhuri huko mbinguni mwaka 1914 kama wafalme na makuhani
-
Kama
ilivyo kwa S.D.A. wanaamini kuwa nafsi inalala na wanakanusha kuweko kwa
jehanamu ya moto na kuwa hakuna hukumu ya waovu zaid ya kufa milele wanaona ni
jambo lisiloingia akilini kuwa Munu mwenye upendo kuruhusu wanadamu awapendao
kuingia katika moto wa milele.
3.
Kama ilivyo kwa imani nyingine potofu wao pia hutumia
maandiko mengi sana kama ushahidi wa mafundisho
yao.
-
Mashahidi wa Yehova
wanasahau kuwa ni upendo wa Mungu ulioruhusu Yesu kuteseka na kufa msalabani
-
No wazi pia kulingana
na haki ya Mungu wazo la Jehanamu ya moto halipingani na haki a Mungu,
-
Mungu amempa kila
mwanadamu utashi na anaweza kuchagua uzima wa milele au mauti ya milele
ingawaje uamuzi huo unaweza kufanyika katika wakati huu wa sasa tukiwa hai
Waebrania 9; 29.
-
Mashahidi wa Yehova
ni wainjilisti wa chini kwa chini hufanya kazi kwa kushuhudia nyumba kwa nyuba
ni ni Hodari sana katika maandiko mpaka kwenye miaka ya 1900 walikuwa na
waamini zaidi ya milioni tatu duniani.
4. Mafundisho
ya Mashahidi wa Yehova kinyume na Utatu wa Mungu
-
Mashahidi
wa Yehova wanapingana kabisa na fundisho kuwa kuna Mungu watatu katika
umoja yaani Mungu baba na Mwana na Roho Mtakatifu na kuwa wote watatu wana nguvu sawa umoja na
kuwa ni wa milele Katika kitabu chao kiitwacho Let God be true cha Brooklyn kinajenga hoja kali kuhusu utatu
kama ifuatavyo
-
Shetani
ndiye mwanzilishi wa fundiso la Utatu wanadai kuwa fundisho hilo halikuanzishwa
na Yesu wala wanafunzi wa Yesu wa mapema, huu ni mpango wa ibilisi ili kwamba
mtu akitaka kumjua Mungu wa kweli na kumtumikia aweze kujikuta ana wakati mgumu
wa kumpenda na kumuabudu Mungu ambaye ni mgumu kueleweka huu ni mkakati wa
shetani kutaka kuwapoteza watu wengi wenye mioyo ya kumcha Mungu kuwa na ukweli
halisi kuhusu Yehova Mungu na Mwana wake Yesu Kristo kwanini kwa sababu hakuna
utatu!
-
Jaribio
lolote la kujifunza kuhusu Utatu wa Mungu linaishia katika kuchanganya akili za
watu na kuharibun hata maana ya andiko la Yohana1;1-2 badala ya kurahisisha
uwazi wa andiko hili inapelekea kuwachanganya watu
-
Je
ni kweli kuna Utatu? Mungu Yehova ni utatu? Hapana Yehova Baba ni Mungu mmoja
wa pekee Yohana 17;3 Marko 12;29 Yesu ni mzaliwa wa kwanza na anatioishwa chini
ya Baba 1Koritho 11;3 Baba ni mkuu kuliko mwana Yohana 14;28
-
Roho
Mtakatifu (roho takatifu) sio nafsi ni Nguvu ya utendaji wa Mung Mwanzo 1;2, Matendo 2;18
-
Hakuna
kitabu chochote kati ya 39 vilivyokubalika katika agano la kale wala 27 vya
agano jipya vinavyounga mkono au kufundisha kwa uwazi kabisa fundisho la utatu
ni wazi kuwa kibiblia na kihistoria fundisho kuhusu utatu halikuweko wala
halikujulikana na hata kwa karne kadhaa baadaye.
5. Mafundisho
ya mashahidi wa Yehova kinyume na uungu wa Yesu Kristo.
-
Maandiko
yanamzungumzia mwana wa mungu Neno kama mungu (m ndogo) na sio (M kubwa)
Ni mungu mwenye nguvu lakini sio
Mungu mwenye nguvu zote katika kitabu chao kiitwacho The Truth Shall make You
Free cha Brooklyn kinafundisha hivyo kwa msisitizomkubwa
-
Kwa
maana nyingine wanamaanisha kuwa Yesu ndiye kiumbe pekee kilichoumbwa na Mungu moja
kwa moja Biblia inaonyesha kuwa yuko
Mungu mmoja na ni mkuu kuliko mwana
mwana yeye ni mzaliwa wa kwanza , ni mwana wa pekee na aliumbwa na Mungu
ana mwanzo na hoja ya kuwa Baba ni mkuu kuliko mwana iko wazi na ni rahisi
kueleweka na hiki ndicho Biblia
inachokifundisha
-
Uwazi
kuwa alikuja duniani akiwa ametumwa na Mungu ni uwazi ulio wazi kuwa hayuko swan a Mungu lakini ni mdogo na ndio maana
haishangazi kuona Yohana akisema Hapo mwanzo kulikuwako Neno naye neno alikuwa
kwa Mungu ingawa wakati huo huo huyo Neno ni mungu (m ndogo)
-
Ni
wazi kuwa Yesu alikuwa na Mungu huko mbinguni lakini hilo halimaanishi kuwa
alikuwa sawa na Mungu huko ni wazi kuwa Biblia inatoa picha kuwa Yesu aliumbwa
wakati Fulani akiwa kiumbe wa kiroho kama ilivyo kwa malaika wa Mungu kwa hiyo
sio Yesu au malaika ambao waliwahi kuweko kabla ya kuumbwa.
6. Mafundisho
ya mashahidi wa Yehova kinyume na uungu wa Roho Mtakatifu.
-
Roho
takatifu ni nguvu zisizoonekana za utendaji wa Mungu ambayo hutembea kwa
watumishi wake wanaotenda mapenzi yake
-
Kama
tulivyoona ni makosa kumfanya roho takatifu kuwa ni nafis wakati hiyo sio
nafsi hili ni jambo ambalo liko wazi
katika maandiko kuwa roho takatifu ni nguvu tu ya utendaji wa Mungu katika kukamilisha makusudi yake ni nguvu
inayodhibitiwa na ungu na huitumia kama apendavyo hii ni nguvu tu kama ulivo
umeme.
-
Nguvu
hiyo haiwezi kuwa Mungu wala kuwa sawa na Mungu.
IMANI POTOFU YA CHRISTIAN SCIENCE
Christian Science ni imani
inayoweka msingi wake wa maishja na mafundisho ya Yesu Kristo pamoja na maswala
ya uponyaji kama inavyoainishwa katika Agano jipya, kulingana na mwanzilishi wa
imani hiyo Mary Baker Eddy anasema Christian Science imetokana na usomaji wa
Biblia wa Muda mrefu , Eddy anaamini kuwa Mungu ni Mungu wa Upendo na ni mwenye nguvu zote na ni baba wa watu wote na hivyo swala hilo lilimpa maswali kuhusu
kuweko kwa maovu na uhalisia wake na
uhusiano ulioko katika maisha ya mwanadamu
Eddy alizaliwa huko Bow, New
Hampshire, mwaka 1821 wazazi wake
walikuwa watu walijitoa sana kwa Mungu. Alichangia kwa kiasi kikubwa kutoka
katika maumivu yake ya ghafla yaliyomtea sana mwaka 1866 aliandika kitabu
kiitwacho “glimpse of the great fact” Kweli kuu kwa Ufupi yaani kinachozungumzia maisha na Roho
(Mungu)aliamini kuwa maisha ya kiroho ndio msingi wa maisha halisi tunayoyaona Eddy alitumia miaka 45 ya maisha yake
yaliyosalia kufanya utafiti wa uhakika
wa ufahamu na matumizi yake ingawa wakati wote wa uatafiti wake aliamini kuwa
wokovu unajumuisha utiii kwa amri za Bwana Yesu hususani ya kuponywa wagonjwa
sio kwa muujiza wa kuingilia sheria ya asili bali kwa utendaji wa nguvu za
Mungu unaoonekana katika sheria ya asili ya Kiroho.
Mary Baker Eddy
Eddy alifundisha wanafunzi wake kuwa kupitia
maombi wanaweza kujiweka wenyewe katika ahsria ya kiroho na kuweza kuondoa
magonjwa na masumbufu yote ya aina binadamu na ndio maana watu wa imani hii
huomba zaidi kuliko kuliko kutegemea madawa katika uponyaji wa magonjwa. Na
inapotokea muamini wa imani hii anahitaji msaada maombi yao hugeukia kwa
muombaji maalumu ambaye amajisajili kuweko wakati wote akijishughulisha na
maombi kwaajili ya uponyaji baahi ya hao waombaji pia ni waalimu wenye mamlaka
katika kanisa wanaofundisha wanafunzi wao kanuni za sayansi ya Kikristo “Christian
Science”.
Mwaka 1875 Eddy alichapisha kitabu chake cha
kwanza kuhusu Sayansi na Afya na baadaye
toleo la Sayansi na Afya na ufunguo wa kimaandiko mwaka 1881, miaka miwili
baadaye baada ya kuanzisha kanisa
alikwenda Boston,Massachusetts. wanachama wa kanisa lake waliongezeka
kwa kasi na akakamilisha ujenzi wa
kanisa lake 1895 na majengo mengine makubwa yaliyokamilika 1906 mpaka Eddy
anafariki kulikuwa na makanisa 1190 ya jamii yake, Hata kufikia 1911 kanisa
lake lilienea sehemu za Marekani na ulimwenguni na katika inchi 72 za
kiprotestant.
Mwaka 1892, Eddy alitambua kanisa la Boston na kubakia hapo na
likatambuliwa kama kanisa mama la makanisa ya Christian Science kanisa hili
huongozwa na Bodi ya wakurugenzi wakiliangalia kanisa tokea hapo makao makuu na
makanisa mengine ya kawaida huhesabika kama matawi kila kanisa hujiongoza ingawa ni lazima
kufuata mfumo wa kanisa mama
Mafundisho na ibada zinafuata kanuni
zilizowekwa na mwanzilishi, kitabu cha msingi ni kile cha Sayansi na afya
kilichoandikwa mara kadhaa na Eddy
Mafundisho na imani ya Christian Science.
-
Wanaamini kuwa wazo la Mwanzo 2;7 kuwa ni la
uongo na ni la kibinadamu kwa kuwa mwanadamu hakuumbwa kwa mavumbi kwani udogo
ni kitu kisicho na uhai na mwanadamu ni kiumbe chenye uhai hivyo dhana hiyo sio
ya kweli
-
Wazo la utatu wa Mungu ni wazo la wanadamu
ambao hufikiri kuwa mwanadamu pia ni utau
-
Wakristo wanaoamini katika mari ya kwanza ni
wale wanaoamini katikia Mungu mmoja kama wayahudi na kuwa wanatambua pia kuwa
Yesu sio Mungu kama ilivyo kwa wayahudi
-
Wanaamini kuwa Yesu Kristo ni Muungano wa
nafsi mbili Yesu ni mwanadamu na Kristo ni Mungu
-
Mungu ni kila kitu na kila kitu ni Mungu,
Mungu ni kanuni, kweli, maisha, upendo, ufahamu. Maarifa, hekima, akili nafsi.
-
Hakuna dhambi ila kuna mawazo tu kuwa kuna
dhambi ni mawazo ya maruweruwe ni mawazo yasiyo sahiimbingu I utawala wa
maswala ya kiroho tu ni sayansi ya ujuzi wa kiungu
-
Mwanadamu alishaokoka tangu milele
-
Maombi hayawezi kumbadilisha Mungu, wala
kuumba kitu kipya,ila yanainua imani kwamba dhambi imeondolewa maombi yenye
kelele hayana msingi wowote lakini maombi ya kimyakimya ndio yenye matokeo.
-
Mwenye dhambi hujitengenezea jehanamu yake
mwenyewe kwa uovu wake na mwema hujitengenezea mbingu yake kwa wema wake
mwenyewe kwa hiyo maswala ya kuweko kwa jehanamu ni ya wale wanaofikiri kuweko
kwa mwili
-
Shetani maana yake ni makosa,uovu,kinyume cha
kweli, kuamini katika dhambi,magonjwa, kifo na tama za mwili
-
Wanaamini maswala Saba kuhusu Mungu.
Mungu anakumbuka
Mungu anasema
Mungu anasikia ,anaona na anaumba
Mungu anajua, ana akili
Mungu atahukumu ulimwengu
Mungu Roho.
Mungu ana utashi
-
Wanaamini kuwa wagonjwa hawaponywi kwa
kutamka kuwa hakuna magonjwa bali kwa kujua kuwa hakuna magonjwa Christian
science hawaamini katika miujiza kwani Eddy anaamini kuwa magonjwa,dhambi na
kifo sio vitu vya kweli mawazo tu ambao
watu wameingiziwa na kuamini kuwa viko lakini haviko
-
Mungu ni kanuni tu za kiroho
-
Yesu sio Mungu
-
Maandiko yanaweza kukosea
-
Mungu hana umbile lolote maalumu umbile alilo
nalo ni lile analopewa na wanadamuu tu kwa akili zao za kibinadamu
-
Sayansi ndiyo inayoleta kweli kwenye mwanga
.na amani katikam ulimwengu kwani pasipo watu wenye kufikiri na wenye akili huu
ulimwengu utakuja kuzimia.
IMANI
POTOFU YA JESUS ONLY
-
Mwanzilishi wa imani hii ni mwinjilisti William
Branham ni mwinjilisti aliyekuwa na upako
wa kupita kawaiada katika maswala ya uponyaji alikuwa ni mtu
aliyejiamini sana na alifikia hatua ya
kutokumuamini mtu zaidi ya Yeye mwenyewe
-
Alijikuta akiamini kuwa yeye pekee ndiye
aliyeangaziwa alipinga sana mafundisho
kuhusu Utatu jambo ambalo kanisa limeamini kwa zaidi ya miaka 1900 na alisema
awaye yote anayepingana naye amekosea
matokeo yake kulitokea faraka na kutokuelewana
-
Alidai kuwa anaufunuo kuwa watu walitakiwa
kulitumia jina la Yesu tu kana inavyoonekana kaika kitabu cha Matendo wakati wa
ubatizo
-
Alidai kuwa Yesu ndiye Mungu baba, Mwana na Roho
Mtakatifu, walidai kuwa wale wanaodai utatu wanaamini katika utamaduni wa
mapokeo kuhusu miungu mitatu
Kumbuka!
-
Mungu yu Utatu Baba, mwana na Roho Mtakatifu na
Baba sio mwana na mwana sio Roho Mtakatifu waebrania katika lugha ya asili
walipomtaja Mungu walitumia Neno Elohim ambalo kwa ujumla liko katika wingi
ingawa linatumika katika umoja.
-
Waamini wa imani hii wanakazia zaidi katika
kanuni ya ubatizo iliyoko katika matendo ambayo hukazia “wakabatizwa kwa jina
la Yesu” pia hukazia kuwa jina hilo ltamkwapo kwa mtu hata kama hajabatizwa au
kuokoka anakuwa mwamini
-
Kwa ujumla ni makosa sana kuamini hivi je namna
gani mtu kutamka jina la Yesu tu anakuwa amepokea wokovu? Pia ni muhimu kuahamu
kuwa hakuna wakati ambapo risto amekiri kuwa yeye ni baba na baba ni yeye au
Roho
-
Kama ilivyo kwa imani nyingine potofu Jesus Only
wana maandiko yao wanayoyatumia lakini ukiyachunguza kitaalamu yametafasiriwa
nje ya kanuni za Hermeneutics somo lihusulo kanuni za kutafasiri maandiko na
kuyatumia kwa halali
-
Uanzilishi wake pia ulikuwa katika misingi a
kugawanya wau na kuwapotosha na wanaamini kuwa badhi a mababa wa kanisa kuwa
ndio waanzilishi wa imani yao na mafundisho yao.