Jumanne, 26 Januari 2016

MFULULIZO WA MASOMO YAHUSUYO UTETEZI WA IMANI (APOLOGETICS) 5



MLIPUKO WA MAPINDUZI YA KIPROTESTANT.
Mnamo karne ya 16th c  kulitokea mlipuko wa kimapinduzi huko Ujerumani ambao ulilitikisa kanisa la Rumi na kutoka katika mapinduzi hayo kulitokea migawanyiko mikubwa  ya kanisa na sura ya kanisa ilijiunda katika namna ambayo haitakuja irekebishike tana na kuwa kama wakati ule kanisa lilipozaliwa na kutoka katika shinikizo hilo ulikuja kuzaliwa msukumo wa kipentekoste unaoendela hata leo.

Mapinduzi.

1.       Mwanzilishi wa Mapinduzi
-          Alikuwa ni Martin Luther aliyezaliwa November 10th 1483 akiwa msomi na mwalimu wa theolojia alianza kuhoji uhalali wa baadhi ya mafundisho ya Kanisa  hususani sheria na mapokeo ya kikanisa akisisitiza kuwa ni Biblia pekee iliyo mamlka ya mwisho
-          Alivutiwa kwa kiwango kikubwa na Warumi 1;17 inayosema “Mwenye haki ataishi kwa imani” alishawishika na fundisho hilo kuwa ni Imani katika Kristo tu ndiyo inayoweza kumfanya mwanadamu kuhesabiwa hali mbele za Mungu
-          Na Tangu wakati huo kuhesabiwa haki kwa imani na Mamlaka ya maandiko yakawa ndio Fundisho lake kuu.
Martin Luther mwanatheolojia wa Kijerumani na kiongozi mkubwa wa kidini. Luther alishiriki kuleta mapinduzi ya kiprotestant kwa matangazo yake aliyobadika mwaka 1517 akikosoa kwa maswala 95 tisini na Matano akikosoa maswala ya kuuzwa kwa vyeti vya msamaha na maswala kadhaa ya kanisa la Roman Catholics Luther alisisitiza kuwa umuhimu wa Ukristo hautegemeani na namna ya uongozi wa kanisa na shirika linaloongozwa na Papa lakini na namna kila mmoja anavyoweza kumfikia Mungu. Mapinduzi haya ya Luthetr yalifungua kwa kiwango kikubwa sana  mlipuko wa jamii kubwa kujitenga na kanisa la Roma na kuanza kwa msukumo mkubwa wa kiprotestan ukiwemo ule wa Calvinism na Presbyterianism.

 
     


Martin Luther.


2.       SABABU ZA KIMAPINDUZI

-          Kuna sababu kadhaa zilizopelekea kuweko kwa mapinduzi ya kiprotestant  na kumfanya Luther na wengineo kulipinga Kanisa Katholic
§  Uozo katika Kanisa.
Akiwa anasoma Martin alitumwa kwenda Rome na wakubwa wake  alipowasili alihitushwa na  Utajiri mkubwa sana wa kanisa Maisha yao ya zamani kabla ya kuokoka, ufisadi na rushwa  maisha ya anasa ya viongozi na makasisi wa Kirumi yakiwa ni maswala ya kawaida

§  Kuuzwa kwa vyeti vya Msamaha Jambo hili lilianzishwa na Papa Leo wa X mwaka wa 1517 alipotoa mpango wa kuuzwa kwa vyeti hivyo ili kukusanya fedha kwaajili ya kanisa na mnunuzi angelisamehewa dhambi

§  Mamlaka ya Pope wa Rumi Luther ambaye alifunua maswala mengi yasiyo ya kimaandiko ya kansia la Rumi, aliweka bayana kuwa Kanisa hilo lilikuwa limepitisha kuwa ni Pope pekee mwenye uwezo wa Kutafasiri Biblia  na si vinginevyo pia ndiye mwenye mamlaka ya mwisho ya kuitisha  mikutano

§  Mfumo wa Sacrament  wakatoliki walifundisha kuwa Sacrament ndio njia ya pekee ya kupokea neema , Luther alisisitiza kuwa Sacrament ziko mbili tu yaani Meza ya Bwana na Ubatizo hata hivyo alisisitiza kuwa kuna ugeuko wa kweli  wa mwili wa Kristo na uwepo wa kweli wa Yesu ingawa mkate na kinywaji hakionekani kubadilika katika meza ya bwana jambo lililokuja kupingwa  na Zwingli aliyefundisha kuwa Meza ya bwana ni kumbukumbu tu ya ufa na kufufuka kwa Bwana Yesu

§  Ukuhani wa Mwamini.
Luther aliandika pamfelti linaloonyesha kuhusu ukuhani wa mwamini kwa ushahidi wa kimaandiko

Aliwataka watawa kuacha Nadhiri zao na kuoa na kuolewa katika mkutano wa maalumu wa  speier mwaka 1529 ilitangazwa kuwa Imani ya Kanisa la Roman ndio pekee imani ya kweli na sahii, Luther alisimama kama mtetezi wa imani  na mwanzilishi wa Protestant Movement alisimama kutetea kanuni za Ukristo na kuanzia wakati huo  madhehebu mengi ya Kiprotestant yaliinuka na  kuzaliwa kama Lutheran, Anglican, Presbyterian, Methodist, Baptist na mpaka karne ya 19th  na 20th  mfumuko wa makanisa yanayoamini wokovu na Ubatizo wa Roho Mtakatifu “Pentekoste”

MAPAMBANO YA KUJARIBU KUUDHIBITI UPROTESTANT

§  Kanisa Katoliki liliunda mbinu mbalimbali kwaajili ya kujilinda na kuulinda mfumo wake hivyo mambo kadhaa yalifanyika
1.       Kuwajibishwa huko Hispania (Spanish Inquisition)
Huko Hispania na Rumi mamia ya watu waliopinga waliitwa kujieleza na kulazimishwa kukubaliana na ukatoliki kwa ukatili mkubwa na nguvu wengi waliuawa wakti huu
2.       Shirika la Jesuit (Jesuit Society)
Shirika lilianzishwa kwa makusudi ya kutafuta waamini na kuwaleta R.C.pia kurejesha utaratibu wa kidini shirika hili llianzishwa na Mtakatifu Ignatius wa Loyola mwaka 1534 na kuthibitishwa na Papa Paulo wa III mwaka 150 usemi wao mkubwa ulikuwa Ad majorem Dei gloriam Neno la kilatini lenye maana ya “Kwenye utukufu mkubwa wa Mungu” na jukumu kubwa lilikuwa ni kusambaza kanisa na mafundisho na kutimiza jukumu lolote la muhimu lililohitaji kushughulikiwa na kanisa wakati ule, Elimu ilikuwa nmdio jukumu kubwa na walijulikana kama wenye mchango mkubwa wa utoaji elimu ya theolojia na elimu ya kawaida.


Mtakatifu Ignatius wa Loyola
3.       Kuitishwa kwa mkutano wa Trent 1545-1563.
Wakatoliki waliitisha mkutano huo walipitia kwa upya fundisho la kuuzwa kwa vyeti vya msamaha na mamlaka ya Papa ,walijadili kuhusu fundisho la kiprotestan kuhusu dhambi na Neema na Biblia  na walifanya mabadiliko kuhusu ukuhani wa kila muuamini ingawa walilaani kuvunjiwa heshima kwa Papa

4.       Wakatoliki walijifanyia tathimini na kujigundua kuwa wameiacha imani ambayo ilitolewa kwa watakatifu kwa njia nyingi.


MASWALA YA MSINGI YA KUZINGATIA.
-          Kuna wakristo wengi ndani ya Kanisa Katoliki walio wakweli na wanyenyekevu ambao wanampenda Mungu na bwana wetu Yesu ni muhimu kukumbuka kuwa tunawaangalia hao kama ndugu na dada katika Kristo
-          Katika miaka ya 1900 kumekuwa na utembeleo mkubwa wa Roho Mtakatifu (Charismatic Movements) ambao umelikumba kanisa ikiwemo Katholiki na wengi wameanza kumuabudu Mungu katika Roho na Kweli ingawa kuna maswala kadhaa kidini yasiyo sahii kwa mafano
*      Wana madai kuwa wao ndio kanisa la kwanza na Halisi kabisa
*      Wana amini kuwa kanisa linazungumza kama wawakilishi wa Mungu  kwa wakati huu wa leo  kwa hiyo kile inachoamua Basi Mungu ameamua
*      Wana madai kuwa Pope anapozungumza  ni kitakatifu “Ex- Cathedra”
Biblia ya Roman Catholic
-          Wakatoliki waliitangaza Biblia yao iliyochapwa mwaka 1610 kuwa imevuviwa na ni neno la Mungu Biblia hiyo inajumuisha vitabu ambavyo vilikataliwa katika kanuni ya kupima maandiko Apocrifa kuwa havina uvuvio
-          Walikazia kuwa hakuna mwenye mamlaka ya kulitafasiri neno la Mungu isipokuwa Papa pekee
-          Mwanzoni wakatoliki walitafasiri Mathayo 16;18,19 kuwa unalihusu kanisa katoliki kwa hiyo hilo ndilo kanisa la kweli
-          Waliamini kuwa Petro ndiye aliyeachiwa funguo za kanisa  wanasema Yesu alimuita Petro mwamba  kwa hiyo kanisa limejengwa juu ya Petro, Petro ndiye aliyekuwa Akofui wa kwanza wa kanisa la Rumi Na kuwa aliachia funguo hizo kwa warithi wake kwa kanisa baadaye  na hivyo kanisa la Rumi ndio kanisa la kweli.
Petro akipewa funguo.
Picha hii ya fresco iliyochorwa na Perugino huko Vatican Sistine Chapel inaonyesha Yesu akimpa Patro Funguo za Ufalme wa Mbinguni kwa mujibu wa mafundisho ya kikatoliki wanaamini kuwa Petro ndiye aliyechaguliwa kuwa Papa wa kwanza na Yesuna hivyo kuwa na nafasi sawa naya Yesu ,Papa anakuwa ndiye mrithi wa Mitume na hivyo yeyote anayekuwa papa ndiye mtume kwa kanisa.
Ukweli kuhusu Petro kibiblia.
-          Kanisa ni waamini waliomkubali Yesu kama bwana na mwokozi kwa mioyo yao na kwa kukiri Warumi 10;9-10,Yohana 16;16-18 Yesu analijenga kanisa kupitia ukiri kuwa Wewe Yesu Umwana wa Mungu aliye hai huo ndio mwamba
-          Tukiwa tunaendelea kujifunza kwa undani zaidi kuhusu kanisa ni muhimu tena tukayaangalia maneno ya Bwana Yesu katika Mathayo 16;13-18 Maneno haya kwa muda wa karne kadhaayamekuwa yakieleweka vibaya na wasomi wa Biblia wakiwemo wanatheolojia wa kikatoliki wanaodhani ya kuwa kanisa limejengwa juu ya Mwamba ambaye ni Petro ni muhimu kufahamu kuwa Yesu alizungumzia maneno haya akiwa pale Kaisaria – Filipi mji huu ulikuwa kaskazini kabisa mwa Israel ambapo Yesu alitembelea, mji huu ulikuwa karibu na chemichemi ya mto wa Yordani na ulipewa jina kaisaria kwa heshima  ya kaisari wa Rumi na  na jina la pili Filipi kwa heshima ya Herode Filipo mtawala wa Galilaya, mji huu ulikuwa ni kitovu cha maovu na dhambi za kila aina kiasi kilichopelekea watu kuuita mji huu lango la kuzimu, ni mahali hapa ndipo Yesu  alitamka maneno haya Kuwa atalijenga kanisa lake juu ya mwamba na kuwa malango ya kuzimu hayataliweza. Kimsingi Yesu alisema kuwa atalijenga kanisa lake juu ya ukiri huu “wewe ndiwe Kristo mwana wa Mungu aliye hai  Maneno hayo ndio msingi au ndio mwamba wa kanisa mtu awaye yote akiamini na kukiri kama alivyokiri Petro maneno hayo anakuwa kanisa na neema ya kuushinda uovu wa aina yoyote inakuwa juu yake  hivyo mtu akimkriri Yesu anakuwa sehemu ya kanisa na sio Petro Yesu hapa alitumia mchezo wa maneno katika lugha ya asili iliyoleta agano jipya kwetu usemi huo hapo juu unaitwa “Petra” ambalo maana yake ni Mwamba mkubwa au jiwe kubwa ambaye ndiye Yesu  na Petro au Kefa ni jiwe dogo kutoka katika mwamba yaani kipande cha jiwe, Hapa linatumika neno “Petros” jiwe dogo kutoka katika mwamba hivyo kanisa limejengwa juu ya msingi ambao ndio Kristo mwana wa Mungu aliye hai na sio Petro mtume 1Korotho 3;11 na Waefeso 2;20-21. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii  naye Kristo ndiye jiwe kuu la Pembeni, au Maana msingi mwingine hakuna awezaye kuuweka isipokuwa ni ule uliokwisha wekwa yaani Yesu Kristo, Maandiko yako wazi kuwa Yesu ndie Msingi ndiye mwamba sasa inakuwaje Petro awe ndiye mwamba au msingi Je hii inapanda kichwani Msingi ni Yesu Kristo.
 

                                                                   Petra -Mwamba Ukiri wa Petro Yesu ni mwana wa Mungu aliye Hai
 

                                                                   PetrosJiwe dogo au kipande cha mwamba maana ya jina Petro


Hiki ndicho kilimaanishwa na Bwana Yesu na sio kuwa kanisa limejengwa juu ya Petro bali ju ya Mwamba yaani ukiri ule kuwa Yesu ni mwana wa Mungu aliye hai.
 

                                                                 Petra - Jiwe la Msingi au jiwe kuu la Pembeni Yesu kristo                
                                                                 Petros   -            Kefa Petro jiwe dogo Tofali   ndiye Petro                                               
 

 Kwa hivyo Yesu analijenga kanisa Tangu wakati huo kupitia ukiri huo Kanisa ambalo waamini ndio wanachama wake na Kanisa, Yesu analipenda kanisa na kanisa huitwa mwili wake  ingawaje kuna kusudi linguine zaidi ya kuwa wana wa Mungu kwani aliyeamini kutoka dhambini bado hajakamilika  anahesabiwa kuwa na haki  na Mungu kwa sababu ya imani ingawa alikuwa mbali na haki  hiki ndicho tunakiita Neema Kwamaana tumeokolewa kwa neema kwa njia ya imani  wala si kwa sababu yetu ni kipawa cha Mungu Waefeso 2;8  Kwa ajili ya utukufu wake Waefeso 1;11-12
Biblia haina maandiko yoyote yenye kuthibitisha kuwa Yesu alimpa Petro Funguo wala kuonyesha Petro akienda Rumi naya kuwa alikuwa askofu wa kwanza wa Rumi wazo hilo linawezekana kuwa linatoka katika mawazo ya kale ya Kirumi na pia hangeweza kuwa na sifa za kuwa Papa wa kwanza kwa kuwa Petro alikuwa ameona alikuwa na mke Mathayo 8;14-15
Petro hakupewa pia mamlaka juu ya wanafunzi wengine wa Yesu na kule Yerusalem kwenye mkutano mkuu wa kwanza wa kanisa Yakobo mtume ndiye alikuwa kama mwenyekiti na sio Petro, hata mtume Paulo hakumpa Petro kipaumbele kama ndiye kiongozi wa juu wa kanisa zaidi sana alimkwemea Wagalatia 2;11.

Ukuhani wa Mwamini.
-          Kanisa katoliki lina idadi kubwa sana ya Mapadre, Maaskofu na makadinari ambao wanapewa nafasi kubwa na mamlaka kubwa ya kuwa waombezi kati ya Mungu na wale wanaoungama , Lakini kwa mujibu wa Biblia kila muumini ni kuhani kwa Mungu na anaweza kujipatanisha na Mungu bila mtu mwingine kuingilia kati
*      Ufunuo Yohana 1;6 Ametufanya kuwa wafalme na Makuhani kwa Mungu na Baba
*      1Petro 2;5,2;9 Bali ninyi ni mzao mteule Ukuhani wa kifalme taifa takatiu,watu wa miliki yake Mungu, Mpate kuzitangaza Fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani….
Ibada za Sanamu
-          Kosa lingine la Wakatoliki  ni kujumuisha Sanamu na Picha za Watakatifu  katika Maswala yao ya Ibada Pamoja na madai yao yanayoonekana kuwa Mazuri kuwa hawaziabudu, Lakini hii haikuwa tamaduni ya Kanisa la kwanza , swala la ibada za Sanamu lilianza mnamo Karne ya 11th C A.D. na hazikuwa zinatofautiana na zile za Wapagani swala ambalo Biblia ik kinume nalo
*      Kutoka 20;3
*      Luka 4;8
*      Yohana 4;24

Ibada zinazomuhusu Mariamu (Mariology)
-          Wanaamini kuwa Mariam ni Mama wa Mungu na hivyo ni Mungu
-          Wakatoliki waliamua kuwa kama ilivyokuwa kwa Yesu Mariamu pia alizaliwa Pasipokuwa na Dhambi (The Immaculate Conception) na kuwa pia alitwaliwa Mbinguni kwa kupaa ambako huku hufanya kazi ya kutuombea pamoja na Yesu kwa hiyo wengi huambiwa kuwa waombe kwake ili aweze kuwaombea Biblia inasema Muombezi na Mpatanishi ni Kristo tu 1Tim 2;5.

Kwa habari ya Dhambi na Wokovu
-          Wakatoliki wanaamini kuwa kazi njema zinaweza kusaidia katika kuleta wokovu
-          Wanaongezea maswala ya utendaji wa aina za sala kama zinazoweza kuangazia na kupunguza adabu ya dhambi
*      Kusali Rozari
*      Kuomba katika maeneo makuu saba ya Kanisa
*      Kutembelea Makaburi Matakatifu
-          Martin Luther alilaumu  na kukataa kutambua shughuli hizo na kuwa Haziwezi kusaidia kupata wokovu
*      Efeso 2;8 - Tumeokolewa kwa Neema wala si kwa matendo
*      Yohana 1;12 - Wote waliompokea aliwapa uwezo kuwa wanae
*      Yohana 3; 36 – Kila amwaminie mwana anao uzima wa Milele
Kwa habari ya Maisha baada ya kufa na hukumu.
-          Biblia haikubaliani na wazo la Pugatory au toharan (limbo) Kwani nafasi ya Pekee ya kutubu dhambi ni wakati tuwapo hai hapa duniani  Wazo hili lilipandikizwa kuwapa watu tumaini Potofu la uongo kuhusu kifo kwa kuwaeleza watu kuwa kuna nafasi nyingine huko purgatory hii ni dhana inayopingana na Maandiko matakatifu
*      Warumi 6;23 – Mshahara wa dhambi ni mauti
*      Waebrania 9;27 – Baada ya kufa ni hukumu
*      2Thesalonike1;7-8  - Kuna malipo kwa kila jambo.
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
 

Hakuna maoni: