Kiini: Umuhimu wa Kumuachia Roho wa Mungu atawale
Andiko la
Msingi: Zekaria 4:6-10
“.6. Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa
Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu,
asema Bwana wa majeshi. 7.Nani
wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye
atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema,
neema, ilikalie. 8. Tena neno la Bwana likanijia, kusema, 9. Mikono yake
Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza;
nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu. 10. Maana ni nani
aliyeidharau siku ya mambo madogo? Kwa kuwa watafurahi, nao wataiona timazi
katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi saba ndizo macho ya Bwana; yapiga mbio
huko na huko duniani mwote. ”
Utangulizi:
Zerubabel
alikuwa ni Liwali wa Jiji la Yerusalem baada ya Wayahudi kurudi kutoka
Uhamishoni, Jina Zerubabel ni muungano wa Maneno mawili ya Kiibrania Zeri na
Babilon ambalo maana yake ni Mzizi au Chipukizi kutoka Babeli, aliteuliwa kuwa
liwali wa Yuda na Mfalme Artashasta, liwali huyu alikuwa anakabiliwa na kazi
ngumu ya Ujenzi wa Hekalu, Kazi hii ilikuwa ni Mapenzi ya Mungu kabisa na Mungu
alikuwa ameweka moyoni mwake Mzigo wa
kulijenga Hekalu, wakati huu kazi ya Ujenzi ilikuwa ngumu sana kuliko wakati wa
Suleimani ni muhimu kufahamu kuwa ni kazi rahisi sana kujenga kitu mara moja
lakini ni kazi ngumu sana kukirudia, Kazi ilikuwa ngumu na yenye upinzani
mwingi sana, Kama ilivyokuwa kwa Nehemia Mungu alipoweka Moyoni mwake kuujenga
ukuta wa Yerusalem kulikuwa na upinzani mkubwa sana, Zerubabel hali kadhalika
alikutana na upinzani mkali wakati wa kulijenga Hekalu.
Hali
halisi ya upinzani ilikuwa Hivi:-
1. Watu waliokuwa wakiuzunguka mji
walijaribu kuwakatisha tamaa, waliwatisha, waliiba baadhi ya vifaa vya ujenzi,
2. Kila mara tunapojihusisha na kazi
yoyote ya Mungu ni lazima shetani atatumia kila mbinu na hila kuharibu kabisa
mikakati na mipango ya kimungu na kutukatisha tamaa.
3. Shetani anaelewa wazi nini kinatokea
watu wanapokuwa wamekata tamaa na kujichokea
4. Watu wanapokata tamaa kumuamini
Mungu kunapungua, Mambo yoyote yale yakifanyika katika hali ya hofu na
kutokumcha Mungu mafanikio huwa ni madogo sana, Biblia inasema Mungu hakutupa
Roho ya woga “2Timoth 1:7” watu waliokata tamaa hudumaa, hawawezi kufanya
jambo lolote lile Duniani, ukiwa na jeshi la wanajeshi waliokata tamaa hata uwe
na vifaa vya kisasa vya aina yoyoteile ushindi unaweza kuwa ni hadithi ya
kusikiliza tu
5. Shetani licha ya kututishia bali
pia atashambulia na kuiba furaha tuliyonayo
6. Watu walimuacha Zerubabeli peke
yake na kila mtu akaanza kuangalia mambo yake na kujenga nyumba yeke mwenyewe
na unjezi wa hekalu ukawa umesimama watu walikufa moyo “Mathayo 6:33” Kumbuka
jinsi Israel walivyokufa moyo baada ya wapelelezi kuleta habari mbaya ya
kuvunja Moyo, walisahahu kabisa kuwa Mungu yuko Pamoja nao, walianza kutumia
akili
7. Zerubabel alikata tamaa kwa sababu
alikuwa haoni njia tena maono yake yalianza kufifia na moyo wake ulianza
kupoteza matumaini jaribu lilionekana ni kubwa na tayari ujenzi wa Hekalu
ulionekana kuwa mzigo na mlima mkubwa ambao sio rahisi kuusawazisha
Ndipo
Mungu alipomuinua Nabii Zekaria kwaajili ya kumtia moyo Zerubabel Na nabii Hagai kwaajili ya kuwatia Moyo
wayahudi, Nabii Zekaria alimueleza wazi Zerubabel ujumbe kutoka kwa Mungu
kwamba si kwa nguvu si kwa uweza Bali kwa Roho yangu asema Bwana, Mungu aliukemea
mlima uliokuwa unamkabili Zerubabel na kuutabiria kuwa utakuwa Tambarare Mungu
alimuahidi kuwa macho yake yanazunguka kuangalia duniani kote ni nani
anamtumaini yeye na kila anayemtumaini yeye hatata tahayarika
Inawezekana
hali kama ya Zerubabel inajitokeza katika Maisha yako, umeanza kukata tamaa,umeshambuliwa
na kukosa msaada umeanza kutumia akili zako katikakutatua majaribio yako lakini
wiki hii ninazo habari njema kwako kuwa Bwana amenituma nikuambie umtegemee
yeye Machjo yake yanaangalia ni nani anamtegemea naye atamruhusu Roho wake
mtakatifu kukutia nguvu na kukuwezesha atalikemea kila tatizo linaloonekana
kuwa gumu katika maisha yako na litakuwa tambarare, Bwana akubariki na
kukuongeza kwa utukufu wake katika Jina la Yesu amen
Ujumbe Na
mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev.
Innocent Kamote.