Alhamisi, 6 Oktoba 2016

Nabii Yona



A.      UTANGULIZI.



Ø  Je umewahi kusikia habari za Mwinjilisti ambaye amekasirika kwa sababu wenye dhambi aliowahubiri wametubu na kuokolewa? Yona ni miongoni mwao
Ø  Yeye anaitwa Nabii  asiyetii au Mmishionari Mzalendo yeye alikuwa na uchungu dhidi ya watu ambao Mungu alikuwa amemtuma akawahudumie, alikuwa mbishi muasi na mwenye ubinafsi wa hali ya juu alikosa upendo na huruma na kama ungekuwa wewe na mimi Tusingelimtuma Yona kuwa Nabii
Ø  Jina lake Yona ni la kiibrania ambalo maana yake ni “Njiwa” Ni mwana wa Amittai  ambaye maana yake ni kweli ya Mungu kutoka Gath-Hepher ambayo ni kana ya wakati wa Agano jipya  na ilikuwa karibu na Nazareth mahali alipokulia Bwana Yesu
Ø  Kitabu kinahusu kufanya umisheni katika nchi ngeni na Mungu anamtumia Nabii asiyependa kufanya umisheni wa kigeni kukiandika, Kitabu kinatufundisha jinsi Mungu anavyojihusisha na mataifa mengine pia na kuwa hana upendeleo.

B.      MWANDISHI 
Ø  Wanatheolojia wengi wanaamini kuwa huenda kitabu kiliandikwa kati ya 780- 753 K.K  mapema wakati wa utawala wa Yeroboamu wa pili 
Ø  Kuna uwezekano kuwa alianza huduma yake wakati wa Nabii Elisha mwishoni kwani kulingana na Tamaduni za Israel inasemekana kuwa ndiye mtoto wa mwanamke mjane wa Sarepter ambaye Eliya alimfufua kutoka kwa wafu tarahe kamili inakisiwa ya uandishi kuwa 780 K.K.
Ø  Yesu alinukuu Matukio ya Yona katika Mathayo 12; 39-41 Jambo linalothibitisha kuwa kitabu chake kimevuviwa na sio hadithi tu kama watu wengine wanavyofikiri Yona pia anatajwa katika 2Falme 14;23-25 kama mtu anayetambuliwa kuwa alikuwa Nabii katika ufalme wa kaskazini wakati wa Yeroboamu wa pili mwaka 792-753 K.K.

C.      HISTORIA YA WAASHURU WALENGWA.
Ø  Watu wa Ashuru walijulikana sana kwa ukatili wao baadhi ya watu waliochukuliwa mateka na wafalme wa kiashuru waliwekwa katika visanduku vidogo vya chuma na misumari  na kupelekwa nje ya mji wa Ninawi mji wao mkuu
Ø  Visanduku hivyo vilikuwa vidogo kiasi ambacho mtu hakuweza kukaa wala kusimamia waashuru waliwaua wafungwa wengi kwa kuwakata miguu kila siku mguu moja na siku nyingine mguu mmoja ili kuwafanya wasikie maumivu makali
Ø  Wengine walilazimishwa kuwachinja rafiki zao waliowafahamu zamani watu wengi waliona ni afadhali kujiua kuliko kuwa kwenye mikono ya waninawi Nahumu 3;19
Ø  Wanawake waja wazito waliwapasua tumboni ili kuona ni jinsi gani kitoto kinakaa ndani ya tumbo la mama zao.
Ø  Inawezekana hii ndio ilikuwa sababu iliyomfanya Yona kuchagua kufa kuliko kuwahubuiri watu hawa katili aliokuwa amesikia habari zao na huenda pia Yona alifahamu kuwa wangetumiwa na Mungu kuwaadhibu wa Israel. kwani mnamo mwaka wa 722 K.K. yaani miaka 38 baada ya mahubiri ya Yona Waashuru waliivamia Israel na kuwachukua mateka huko Ashuru

D.      UPEKEE WA KITABU CHA YONA
Ø  Kitabu cha Yona ni Tofauti na Vitabu vingine vya kinabii kwa sababu ya maswala ya msingi yafuatayo;-
1.       Kimeandikwa katika mtindo wa kihistoria kuliko Vitabu vingine vya kinabii ingawa kina kweli nyingi ambazo zinaweza kuwa ni changamoto kubwa na kweli kuu ambazo zaweza kufanya kazi katika maisha yetu leo.
2.       Matendo ya Mungu kwa asili katika kitabu hiki kina kweli kuu kuhusu Mungu kwa asili hii inafundisha wazi kabisa kuwa Mungu yuko kila mahali na ni vigumu kukimbia au kujificha mbali na uso wake Zaburi 139;7-12, kinafundisha pia kuwa Mungu ni Bwana wa Historia, mataifa na Viumbe vyote na kuwa anahukumu kila jamii inapokosea na anaweza kutumia asili kwa mfano alimtumia upepo, samaki mkubwa mmea wa mtango, mnyoo Jua n.k. katika kukamilisha mpango wake kwa Yona kwenda ninawi.
3.       Kitabu hiki kipekee sana kinasisistiza Umisheni  na kufunua Upendo wa Mungu na mpango wa Mungu wa wokovu sio kwa wayahudi pekee bali kwa watu wote wa mataifa Yoote Matendo 10;34-35
4.       Unabii unaotegemea Conditional natural Prophecy Yona alitangaza kuwa Ninawi utaharibiwa katika siku arobaini lakini haukuharibiwa mji kwa sababu watu walitubu Yeremia 18;7-10
E.       MGAWANYO

Ø  Yona kimegawanyika katika maeneo makuu mawili
1.       Wito wa kwanza na upinzani wa Nabii sura ya 1-2
2.       Wito wa mara ya pili na Manung’uniko ya Nabii 3-4

F.       MSTARI MKUU AU MISTARI YA MSINGI

Ø  2;9 Wokovu unatoka kwa Bwana
Ø  3;9 Nani ajuaye ya kuwa Mungu ataghairi na kusamehe
Ø  4;2 Najua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma si mwepesi wa hasira u mwingi wa rehema  nawe wagahiri mabaya.

G.       MCHANGANUO WA KITABU CHA YONA 

Kukimbia wito wa Mungu sura ya 1-2.
Ø  Yona hakuwa na mshaka kuhusu nini Mungu alikuwa anataka kukifanyaalipokea ujumbe kwa Mungu kabla na hivyo alifahamu sauti ya Mungu lakni kile ambacho mungu alikuwa amemtuma kilikuwa kimemshagaza kumbuka wakati Mungu alipomwambia Petro aende kwa Kornelio Matendo 10;1-29
Ø  Ninawi ulikuwa mji wa kipagani na mji mkuu wa Ashuru Utawala ambao ulikuwa ni adui mkubwa wa Israel kwa miaka  Mungu alisema uovu wao umepanda juu mbele zangu Mwanzo 18;25 Kwa hivyo yona aliitwa kwenda kuhubiri dhidi ya Ninawi lakini yona hakutaka kulitimiza Jukumu hilo hivyo alikimbia kwenda mbali ingawa alijua wazi kuwa Mungu yuko mahali kote 
Ø  Kumbuka Ninawi ilikuwa karibu kuluiko alikokuwa anakimbilia yaani Trshishi ambayo inaaminika kuwa ni sehemu za Hispania ya leo  Mbali sana kutoka Yaffa
Ø  Kilichofuata ni adhabu kwa ajili ya kutokutii kwa Yona lakini kwa upande mwinginie ni Rehema za Mungu ni upendo wake kumrejeza Yona katika hali ya utii Waebrania 2;10-11.Mungu alituma upepo mkali na mabaharia walifikiri kuwa meli ingevunjika.
Ø  Katika hali hizo zote za dhuruba Yona alikuwa amelala usingizi na hakuwa anajua nini kinaendelea 1;6 matoleo mengine ya Biblia kama Septuagint inasema alikuwa anakoroma
Ø  Yona alipoamsahwa alitoa ushuhuda wa ajabu kuwa anamwabudu “Mungu wa mbingu aliyeumba bahari na nchi kavu …. Na ya kuwa ninakimbia mbele zake” jambo la kushangaza ni kuwa zaidi ya kuasi kwake Yona alikuwa anashuhudia kuhusu Mungu wa kweli na kabla ya kutupwa watu hao waliomba sasa si kwa miungu yao bali kwa Mungu wa Yona 1;14 walitoa sadaka na kuweka nadhiri kwa Mungu huyo huenda waliahidi kumtumikia Ushuhuda wa Yona ulileta matokeo na watu walitubu ingawaje yeye alikuwa akielezea kukimbia kwake
Ø  Yona aliyatoa maisha yake kwa hiyari yake mwenyewe ili wale walikuwa kwenye meli waweze kuokolewa 1;12
Ø  Huenda Yona alijua wazi kuwa kama Ninawi watatubu Mungu atawasamehe na kuwaokoa lakini la kushangaza Yona mwenyewe hakuwa tayari kutubu na badala yake alikuwa tayari kufa kuliko kwenda Ninawi hii inaonyesha jinsi ambavyo kuna hatari katika kuasi mapenzi ya Mungu na na jinsi chuki dhidi ya wengine inavyoweza kutenda kazi ndani ya mtu.

H.      KUHIFADHIWA NA KUOKOLEWA.
Ø  Mungu hakuwa amemsahau mtumishi wake na bado alikuwa na mpango naye na huduma yake kwa ajili ya watu wa Ninawi aliandaa samaki mkubwa Nyangumi na kummeza Yona baadhi ya matoleo ya Biblia yanasema Mungu akaandaa au akachagua samaki mkubwa hii inaonyesha uweza wa Mungu dhidi ya mambo ya asili kuwa Mungu aweza kuyatumia mazingira au Viumbe katika kutimiza mpango wake,wengine wana fikiri kuwa labda swala la kumezwa na nyangumi ni hadithi lakini kumbuka kuwa ni mpango wa Mungu, Mungu aliandaa samaki mkubwa hii imerudiwa mara nne katika kitabu cha Yona

Ø  MAOMBI KWA AJILI YA WOKOVU.
Yona alifanya maombi na kujiuhukumu mwenyewe ndani ya samaki, lakini Mungu kwa huruma yake na Neema wakati mwingine anaruhusu sisi kupitia hukumu zake ili kwamba tumlilie yeye na kumtegemea yeye na kwa wakati huu sasa Yona alikuwa tayari kwenda Ninawi na kumtii Bwana  alithibitisha kujitoa kwake kwa Mungu na  Furaha ikaujaza moyo wake.

I.         KUTII WITO WA MUNGU MARA YA PILI.
-          Hakuna ajuaye ya kuwa Samaki alimpeleka wapi Yona huenda alimtapika huko Ninawi hata hivyo hili si la muhimu hapa la muhimu ni kuwa Yona alikubali wito wakati, Mungu alipomtuma mara ya pili.
-          Watu wengine hukataa wito wa Mungu na hawapati nafasi ya pili ya kumtumikia Mungu wengine hufikiri ya kuwa huenda Mungu hata watumia tena,Yona alitii neno la Bwana lilipomjia mara ya pili na alikwenda Ninawi
-          Inakisiwa watu wapatao 600,000. Waliishi Ninawi na vitongoji vyake ilimgharimu siku tatu Yona kuihubiri Ninawi ingawa alipewa siku 39. Ujumbe wake ulikuwa katika siku tatu ninawi utaangamia, kwa mujibu wa Luka 11;30  tunajua kuwa huenda Yona alimtumia uzoefu wake wa kumkimbia Mungu na kuokolewa na hii ilikuwa ishara kwa watu wa ninawi kutubu mji mzima na kumrudia Mungu

J.       KUMFAHAMU MUNGU NA MTAZAMO WAKE SURA YA NNE
-          Mwinjilisti anakasirika kwa sababu wenye dhambi wametubu  hiki nacho ni kioja ni wazi kuwa alijua kuwa Mungu ni mwingi wa Rehema na ya kuwa atawasamehe waninawi na ndio maana alikimbia wala hakutaka waninawi waokolewe
-          Wakati waninawi wanatubu kwa kufunga, Yona alikuwa anajijengea kibanda cha mapumziko kwa ajili yake nje ya mji akisubiri kwa tumaini kuwa Mungu atawaangamiza na siku arobaini zikapita patupu!
-          Yona alikasirika alikuwa na tatizo Kiburi,Ubinafsi na kukosa upendo alijihusisha sana na heshima yake kama Nabii ametabiri na Mungu ataitimiza unabii wake alikuwa tayari kufa kuliko kurudi Israel na kusimulia kuwa mahubiri yake yamewafanya Waninawi watubu na kuokolewa
-          Mungu ana namna yake anavyoweza kuyaangalia mambo na kutuonyesha makosa yetu na kutufundisha mtazamo wake aliandaa mtango kumpa Yona kivuli  na Nabii wake mwenye hasira akapumzika kisha akaandaa mnyoo upepo na jua kali vikaharibu kile kivuli Yona akakasirika zaidi
-          Kumbuka kuwa mungu alimuuliza yona unaona vema kukasirika hatupaswi kulaumu kile mungu anachokifanya Yona alijibu kuwa anafanya vema kukasirika hata kufa Hasira husumbua watu wengi na husababisha kifo au kupooza Srtokes
-          Mungu alikuwa akimfundisha Yona na sisi kuwa Yeye ni mwingi wa Rehema  Yona alifurahia faraja zake na starehe zake  kuliko maisha ya watu 120,000 watoto wachanga na wanyonyao Mungu aliwajali wao kwani anaupenda ulimwengu mzima Yohana 3;16.

Nabii Yoel



A.     MWANDISHI WA KITABU CHA YOELI

Ø  Mwandishi ni Yoel baadhi ya wasomi wanaamini alikuwa mwana wa Samuel (Samuel 8;1-2.) lakini Maandiko yanamtaja kama mwana wa Pethuel yaani uaminifu wa Mungu ingawa hatuna taarifa alizaliwa wapi na historia yake si kubwa sana ingawa inaonekana ya kuwa alikuwa kuhani Yoel 1;13-14,2;1 na 14-17.
Ø  Jina lake maana yake ni Yehova ni Mungu wasomi wengi wanaamini kuwa alikuwa kuhani hii labda huenda inatokana na kujishughulisha kwake zaidi na maswala ya hekalu na kushughulikia na majukumu ya kikuhani  1;13-14, 2;1, 14-17.Na mkazo wake katika kitabu chake chote unawafanya wasomi kuamini hivyo.
Ø  Inaonekana pia kuwa alikuwa anaishi Yudea na ni maarufu sana kama Nabii wa Pentekoste.Kwa sababu ya kuzungumzia swala la ujio wa Roho Mtakatifu katika Yoel 2; 28.


B.     TAREHE YA UANDISHI.

Ø  Tarehe ya uandishi wa kitabu cha Yoel Haijulikani hasa ni lini Baadhi wanaamini kuwa huenda kiliandikwa wakati wa baada ya Uhamisho wa Babel kwa sababu Yoel hajawataja waashuru wala wakaldayo wala maswala ya kuabudu sanamu.
Ø  Ingawaje baadhi ya wasomi wanaamini kuwa uchanganuzi wa wadudu kama tunutu, Madumadu n.k ni Lugha ya mafumbo inayohusiana na uvamizi wa majeshi ya kigeni hivyo kama hivyo ndivyo Basi tarehe ya uandishi inaweza kuwa ni kabla ya utumwa na moja ya jambo linalothibitisha kuwa hakikuandikwa wakati wa utumwa ni kwa sababu kinagusia maswala ya ukuhani na hekalu hivyo kunauwezekano kikawa kimeandikwa 830 k.k. kwani hekalu liliharibiwa mwaka wa 586 k.k.

C.      HISTORIA YA MATUKIO KATIKA KITABU CHA YOEL 2Falme 11; 1-12;3.

Ø  Ukweli kuwa Yoeli anashughulika na makuhani zaidi na sio wafalme unashuhudia ya kuwa kitabu huenda kiliandikwa wakati wa Yehoiada kuhani mkuu ambaye ni mtu mkubwa aliyechaguliwa kusimamia maongozi kwa sababu mfalme alikuwa mtoto hivyo Yoel hajazungumzia maswala ya mfalme katika kitabu chake.
Ø  Malkia wa Yuda Athalia alikuwa amewaongoza watu katika kuabudu mabaali. Lakini Yehoiada aliwaongoza kurudi kwa Mungu Na huduma ya Nabii Yoel ilichangia kuwarudisha watu kwa Mungu
Ø  Athalia alikuwa mtoto wa mchawi malikia Yezebeli aliyeolewa na Ahabu na aliolewa na Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda. Athalia aliwaongoza Yehoramu na Yuda kuenda mbali na Mungu kuabudu baali na kufanya dhambi nyingine Yehoramu aliwaua nduguze 6 ili kujihakikishia anabaki kwenye kiti cha kifalme na alipokufa mwanae Ahazia akawa Mfalme Badala yake, Athalia alimchochea Ahazia katika kuabudu miungu na baada ya mwaka mmoja aliuawa na Athalia alitawala na kutoa amri kuuawa kwa watoto woote wa Ahazia yaani wajukuu wake na warithi wa kiti cha ufalme.
Ø  Dada wa Ahazia alikuwa ni mke wa kuhani mkuu Yehoiada na kwa neema ya Mungu aliweza kumuokoa moja ya wana wadogo aliyeitwa  Yoashi na kwa kuwa alikuwa na umri mdogo  miaka 7 Yehoiada aliongoza makuhani na wazee wa Yuda kisiasa kufanya mapinduzi na kumfanya Yoashi kuwa mfalme na Athalia akauawa.
Ø  Yehoiada aliendelea kusaidia kuongoza mpaka Yoashi alipofikia Umri wa kuweza kutawala.

D.     UPEKEE WA KITABU CHA YOEL NA UJUMBE WAKE

a.       Yoeli alisisitiza kuhusu Siku ya Bwana, majukumu ya makuhani ambao ni muhimili wa dini na kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, Pamoja na mapigo yanayohusiana na nzige ni vitu maalumu sana katika kitabu hiki.
b.       Kitabu chote kialenga katika siku ya Bwana, huku Yoeli akitumia mifano ya Nzige kuwaonya dhidi ya hukumu ya Mungu itakavyokua isipokuwa kama watatubu. Jambo hili ingawaje linaenda zaidi ya hali halisi ya siku hizo kwani pia inazungumzia juu ya dhiki ile kuu siku za mwisho ambapo hasira ya Mungu itashuka ulimwenguni.
                


Nzige (Locust) Moja ya wadudu waharibifu wakubwa wa mazao kwa mujibu wa Yoel ni miongoni mwa Majeshi ambayo Mungu angeyatumia kuwashambulia watu wasipotubu uovu wao Picha na Maelezo kwa Hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote.

E.     MSTARI WA MSINGI AU MISTARI YA MUHIMU

Yoeli 2;1   - Siku ya Bwana inakuja
Yoel 2;13. -  Rarueni mioyo yenu
Yoel 2;28  - Nami nitawamwagia watu wangu Roho yangu
Yoel 3;10  - Yeye aliye dhaifu na aseme mimi ni Hodari

F.      MGAWANYO WA KITABU

Kitabu cha Yoeli kimegawanyika katika maeneo makuu mawili
a.       Nabii anazungumza 1;2-2;17
b.       Mungu anazungumza 2;18-3;21

G.    MCHANGANUO WA KITABU CHA YOELI

·         Hukumu na toba Yoel 1;1-2;27
Yoeli anatoa kwanza sababu za ujumbe 1;1, Neno la Bwana lilimjia, mara nyingi kile ambacho Bwana aliwapa Manabii walitakiwa kuwaambia watu na Mungu alizungumza wazi kulingana na mazingira yao nini cha kukifanya  ili waepuke hukumu zake na kufurahia Baraka zake zaidi
·         Mapigo ya Nzige 1;2-0
Mapigo ya nzige kulikuwa kitu cha kawaida katika mazingira yale lakini nzige hawa anaozungumza Yoel ni wa Tofauti na hawajawahi kuonekana mstari 2-3 ilikuwa ni kitu ambacho wazazi wangewasimulia kizazi kijacho cha watoto wao, kule kuonyesha kuwa wazazi hawatasahahu ni wazi kuwa watu wanapomuacha Mungu kwa hakika hukumu ya Mungu huwa inakuja juu yao bila mzaha, 2-4, Mstari wanne unaashiria labda vipindi vinne vya uvamizi wa nzige au hatua zao za kukua
·         Baadhi ya wanatheolojia wanaamini kuwa adhabu ya aina hii ya nzige inawakilisha falme nne zilizoigandamiza Yuda na Israel kwa miaka mingi
Ø  Tunutu – wanawakilisha Babeli
Ø  Nzige – wanawakilisha Waajemi na Waamedi
Ø  Parare - wanawakilisha Wayunani
Ø  Madumadu -   wanawakilisha Warumi.
Hata hivyo baadhi ya wanatheolojia wanasema hawa walikuwa ni wadudu halisi na hawakuwakilisha falme yoyote I; 4 na 2;25-26

H.    WITO WA KUTUBU 1;2-2;17

Ø  Yoeli aliwaita watu woote kutubu kuanzia na Viongozi 1;2,3,14, 2;15-16 na wote walioishi juu ya nchi 1;2,3,14, Watoto wachanga na wanyonyao 2;16, Walevi 1;5 wakulima na watunzaji wa mizabibu 1;11 makuhani 1;13,14,2;15,2;1,15,17.bwana harusi na bibi harusi 2;16,8 walitakiwa kuomboleza kama mwanamke aliyefiwa na mume wa ujana wake, walitakiwa kufunga na kuomba na kuitakasa siku ya bwana  hili lilikuwa linadhihirisha nini watu wanatakiwa kukifanya ili kuepuka hukumu ya Mungu
Ø  Yoeli aliwahakikishia watu kuwa Mungu ni mwingi wa Rehema na huruma na neema na si mwepesi wa hasira  na  kuwa hughairi mabaya
Ø  Uamsho lazima uanze na Viongozi wa kidini  hivyo makuhani waliagizwa kuomboleza kati ya patakatifu na madhabahu

I.       KUREJESHWA KWA BARAKA ZA MUNGU 2;18-27

Ø  Yoeli 2;18-27 Inatoa majibu ya Mungu kwa maombi ya Nabii, makuhani na watu wote, toba ya kweli inapofanyika Mungu Huiheshimu na kuikubali, hivyo Mungu alihaidi kuwaondolea Mbali nzige na kuwa angerejesha mazao na mavuno yangepatikana, miti ya matunda ingezaa na mashamba yangezalisha mavuno mengi
Ø  Baadhi ya wasomi wanatafasiri kuwa Yoel 2;20  jeshi la kaskazini kuwa kama ni Ashuru lakini mstari wa 25 unaweka wazi kuwa Mungu anamaanisha ni nzige halisi
Ø  Ingawaje namna atakavyo wafukuza nzige hao kungewatia moyo  watu wake kumuamini kwa wokovu dhidi ya majeshi ya wageni
Ø  Yoeli 2;21-27 inakazia maswala ya kiroho na Baraka ambazo zingewajilia watu wa Mungu,Baraka hizo za kimwili na kiroho zingeipata Yuda kama wataamua kumgeukia Mungu na hii pia iliwakilisha Baraka ambazo zingewapata kwa kumuamini Yesu wakati wa miaka 1000 ya Utawala wake duniani.

J.      SIKU ZA MWISHO 2;28-3;21

Ø  Kwa Maneno Hata itakuwa baada ya hayo 2;28 Nabii alimaanisha kuhusu wakati ujao mbali kutakuwa na utembeleo maalumu na hukumu
A.      Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu 2;28-29
Ø  Watu woote wa Mungu wangejazwa Roho Mtakatifu na kuna makundi sita yanatajwa kama ambao wangetembelewa na Roho Mtakatifu Wana wenu, binti zenu, vijana, wazee wanaume na wanawake.
Ø  Hiki alicho kitabiri Yoeli kilitimia kuanzia siku ya Pentecost Matendo 2;17-18 Petro aliitumia tafasiri ya siku za mwisho na kuendelea kwa kawaida siku za mwisho zilianza na Kuzaliwa kwa kanisa  siku ya Pentecost na kuendelea katika kipindi chote cha kanisa, Mungu aliwajaza watu wa chache Roho wake kwa kusudi maalumu lakini sasa anasema kwa watu woote kila mtu atakuwa na sehemu katika utumishi wa kazi yake Sehemu hii pia ya unabii wa Yoeli unaeleza nini kitatokea kutokana na kumwagwa huko kwa Roho wa Mungu, watu watatabiri, wataota ndoto, na kuona maono
Ø  Ishara hizi zoote zinafunua ushahidi wa Agano la kale  Mungu angaeendelea katika namna kama hiyo iliyokuwa wazi wakati wa Agano la kale  kujifunua mwenyewe lakini kwa upana zaidi katika Agano jipya
B.      Dhiki kuu 2;30-32.
Ø  Ishara na maajabu yanayotajwa katika mstari wa 30-32 yatatukia mwisho wa  kipindi  cha kanisa, Danieli alisema kutakuwa na kipindi cha dhiki ambayo haijawahi kuweko tangu kuumbwa kwa ulimwengu  lakini katika wakati huo watu wako kila atakayeonekana jina lake limeandikwa katika kitabu cha uzima wataokolewa Daniel 12;1, Tunaona katika Ufunuo 6;12-14 kile ambacho Yoel alitabiri lakini kwa undani zaidi
Ø  Tetemeko kuu jua kutiwa Giza na kuwa jeusi mwezi kuwa mwekundu kama damu lakini wale watakaoliitia jina la Bwana wataokolewa.
C.      Hukumu ya Mataifa 3;1-16 Isaya 2.
Ø  Mwishoni mwa dhiki ile kuu kutakuwa na hukumu kubwa kwa kuanziwa na vita vya Armageddon watu wa Mungu watakapokuwa wamepatwa na maangamizo makubwa mwishoni wataliitia jina la Bwana kwa wokovu 5;15
Ø  Maombi ya Israel wakati huu yatakuwa  watelemshe mashujaa wako ee Bwana Yoel 3;11 na Isaya 64;1
Ø  Yesu atakuja na watakatifu wake na jeshi la malaika  na atamshughulikia mpinga Kristo na Israel watakapomuona watatubu na kumtambua kama Bwana na mwokozi wao, Kisha hukumu ya mataifa itachukua nafasi yake na mataifa yoote yatahukumiwa katika msingi wa namna wanavyoshughulika na Israel na kanisa.
D.      Utawala wa Yesu Kristo wa Miaka 1000. 3;17-21 Isaya 35
Ø  Ujumbe wa Yoeli unamalizikia na Baraka kubwa iliyohaidiwa kwa watu wa Mungu
o   Bwana atakuwa kimbilio lao na Ngome yao kuu sana 3;16
o   Bwana atakaa katika Sayuni 17,21
o   Yerusalemu watakuwa watakatifu na haitovamiwa tena mstari wa 17
o   Israel itapata chemuchemu za maji na nchi itakuwa yenye kuzalisha sana mstari wa 18 na Yuda itadumu milele mstari wa 20. Mungu atawasamehe Israel Mstari wa 21.